Neno Laonekana katika Mwili

Neno Laonekana katika Mwili

Toleo La 1, Kuonekana na Kazi ya Mungu

Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, ambaye Ameonekana kufanya kazi Yake, anaonyesha ukweli wote ambao huwatakasa na kuwaokoa wanadamu, na wote umejumuishwa katika Neno Laonekana katika Mwili. Hili limetimiza kile kilichoandikwa katika Biblia: “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu(Yohana 1:1). Na kuhusu Neno Laonekana katika Mwili, hiyo pia ilikuwa mara ya kwanza Alipozungumza mengi hivyo, na kwa muda mrefu sana, kwa wanadamu wote. Ilikuwa ya kipekee kabisa. Na zaidi, matamshi haya yalikuwa maneno halisi ya kwanza yaliyoonyeshwa na Mungu miongoni mwa wanadamu ambapo Aliwafichua watu, akawaongoza, akawahukumu, na kuzungumza nao wazi wazi na kwa hiyo, pia, yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo kwayo Mungu aliwaruhusu watu wajue nyayo Zake, mahali Anapokaa, tabia ya Mungu, kile Mungu anacho na alicho, mawazo ya Mungu, na sikitiko Lake kwa wanadamu. Inaweza kusemwa kwamba haya yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo Mungu alikuwa amezungumza kwa wanadamu kutoka mbingu ya tatu tangu uumbaji, na mara ya kwanza ambapo Mungu alikuwa ametumia utambulisho Wake wa asili kuonekana na kuonyesha sauti Yake kwa wanadamu katikati ya maneno.
Neno Laonekana katika Mwili (linalofupishwa kama Neno), kilichoonenwa na Kristo wa Siku za Mwisho, Mwenyezi Mungu, kwa sasa kina buku sita: Buku la Kwanza, Kuonekana na Kazi ya Mungu; Buku la Pili, Kuhusu Kumjua Mungu; Buku la Tatu, Mihadhara ya Kristo wa Siku za Mwisho; Buku la Nne, Kuwafichua Wapinga Kristo; Buku la Tano, Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi; na Buku la Sita, Kuhusu Ufuatiliaji wa Ukweli.

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp