Kazi na Kuingia (8)

Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, uwe umebadilishwa, hivyo kuokoa nafsi yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na uovu; ni kwa sababu ya kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu. Weka pembeni mazungumzo ya ni namna gani maisha na uzoefu wa mwanadamu ni ya kiburi au ya kina; mioyo ya watu itakapokuwa imeamshwa, wanapokuwa wameamshwa kutoka kwa ndoto zao na kujua kikamilifu madhara yaliyoletwa na joka kuu jekundu, kazi ya huduma ya Mungu itakuwa imekamilika. Siku ambayo kazi ya Mungu itakuwa imekamilika pia ni siku ambapo mwanadamu ataanza rasmi kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu. Wakati huu, huduma ya Mungu itakuwa imekamilika: Kazi ya Mungu katika mwili itakuwa imekamilika kabisa, na mwanadamu atakuwa ameanza rasmi kufanya kazi ambayo anapaswa kufanya—atatekeleza huduma yake. Hizi ni hatua za kazi ya Mungu. Hivyo mnapaswa kutafuta kwa kupapasa kuingia kwenu katika misingi ya kujua mambo haya. Haya yote ndiyo mnayopaswa kuyajua. Kuingia kwa mwanadamu kutaboreka tu pale ambapo mabadiliko yatatokea ndani kabisa ya moyo wake, maana kazi ya Mungu ni wokovu kamili wa mwanadamu—mwanadamu aliyekombolewa, ambaye bado anaishi chini ya nguvu za giza, na ambaye hajawahi kuzinduka kutoka katika eneo hili la kusanyiko la pepo; ili kwamba mwanadamu aweze kuwekwa huru dhidi ya milenia ya dhambi, na kuwa wapendwa wa Mungu, kumkanyaga kabisa joka kuu jekundu, kuanzisha ufalme wa Mungu, na kuupumzisha moyo wa Mungu mapema, ni kutoa mawazo bila woga, bila kubania, kwa chuki inayovimbisha kifua chenu, kuondoa kabisa vijidudu hivyo, kuwafanya muache maisha haya ambayo hayana tofauti na maisha ya ng’ombe au farasi, ili msiwe watumwa tena, ili msiweze kukanyagwa tena au kuamrishwa na joka kuu jekundu; hamtakuwa tena wa taifa hili lililoanguka, hamtakuwa tena wa joka kuu jekundu lenye chuki, hamtafungwa nalo tena. Kiota cha pepo hakika kitachanwachanwa na Mungu, na mtasimama kando ya Mungu—nyinyi ni wa Mungu, na sio wa milki hii ya watumwa. Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga mwovu huyu, joka wa zamani mwenye chuki, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote. Mungu hatamsamehe hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote,[1] Atamwangamiza kabisa.

Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanakimbia kila mahali, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi,[2] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida.[3] Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu bila hisia yoyote, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, wanaenda kinyume na dhamiri yote, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! Nani ambaye ameikumbatia kazi ya Mungu? Nani ametoa maisha yake au kumwaga damu kwa ajili ya kazi ya Mungu? Kwa kizazi baada ya kizazi, kutoka kwa wazazi hadi watoto, mwanadamu aliyepo katika utumwa bila heshima amemfanya Mungu mtumwa—hii inawezaje kukosa kuamsha hasira? Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo—inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake, usimwache kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani. Kwa nini uweke kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini utumie mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini utumie nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini usimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini umsumbue Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? Wema upo wapi miongoni mwa wanadamu? Ukarimu upo wapi miongoni mwa wanadamu? Kwa nini usababishe matamanio makubwa kiasi hicho kwa Mungu? Kwa nini umfanye Mungu kuita tena na tena? Kwa nini umlazimishe Mungu kuwa na wasiwasi kwa sababu ya Mwana Wake mpendwa? Katika jamii hii ya giza, kwa nini mbwa wao walinzi wasimruhusu Mungu kuja bila kizuizi na kuzunguka dunia ambayo Aliiumba? Kwa nini mwanadamu haelewi, mwanadamu anayeishi katika maumivu na mateso? Mungu amevumilia mateso makubwa kwa ajili yenu, kwa maumivu makubwa Amemtoa Mwanawe wa pekee, mwili wake na damu, kwa ajili yenu, sasa kwa nini bado mnakuwa vipofu? Katika mtazamo mzima wa kila mtu, mnakataa ujio wa Mungu, na mnakataa urafiki wa Mungu. Kwa nini mnakosa busara kiasi hicho? Mko tayari kuvumilia uonevu katika jamii ya giza kama hii? Kwa nini, badala ya kujaza tumbo lenu kwa milenia ya uadui, mnajidanganya wenyewe kwa “kinyesi” cha mfalme wa pepo?

Je, vikwazo kwa kazi ya Mungu ni vikubwa vipi? Je, kuna yeyote aliyewahi kujua? Watu wakiwa wamefungwa tunduni na rangi za ushirikina zenye nguvu, ni nani anayeweza kuujua uso wa kweli wa Mungu? Kwa ujuzi huu wa kitamaduni wenye maendeleo ya nyuma mno ulio wa juujuu na wa upuuzi, wangewezaje kuelewa kwa ukamilifu maneno yaliyosemwa na Mungu? Hata wakati wanapozungumziwa ana kwa ana, na kulishwa, mdomo kwa mdomo, wangewezaje kuelewa? Wakati mwingine ni kana kwamba maneno ya Mungu yamepuuzwa kabisa: Watu hawana mjibizo hata kidogo, wao hutikisa vichwa vyao na hawaelewi chochote. Je, hili lingekosaje kuwa lenye kutia wasiwasi? Hii “historia ya kitamaduni ya kale na maarifa ya kitamaduni ya mbali[4]” imekuza kikundi cha watu wasio na thamani hasa. Utamaduni huu wa kale—urithi wa thamani—ni rundo la takataka! Uligeuka kuwa aibu ya milele kitambo, na haustahili kutajwa! Umewafundisha watu hila na mbinu za kumpinga Mungu, na “mwongozo wa utaratibu, wa upole”[5] wa elimu ya kitaifa umewafanya watu kuwa wakaidi hata zaidi kwa Mungu. Kila sehemu ya kazi ya Mungu ni ngumu sana, na kila hatua ya kazi Yake duniani imekuwa ya kumhuzunisha Mungu. Jinsi kazi Yake duniani ilivyo ngumu! Hatua za kazi ya Mungu duniani zinahusisha shida kubwa: Kwa ajili ya udhaifu wa mwanadamu, upungufu, utoto, ujinga na kila kitu cha mwanadamu, Mungu hufanya mipango yenye uangalifu na hufikiria kwa makini. Mwanadamu ni kama duma wa kutisha ambaye mtu hathubutu kumtega au kumchokoza; anapoguswa tu anauma, au vinginevyo anaanguka chini na kupoteza mwelekeo wake, na ni kana kwamba, akipoteza umakini kidogo tu, anarudia uovu tena, au anampuuza Mungu, au anakimbia kwa wazazi wake walio kama nguruwe na mbwa kuendeleza mambo machafu ya miili yao. Ni kizuizi kikubwa kiasi gani! Katika kila hatua ya kazi Yake, Mungu anakabiliwa na ushawishi, na takribani katika kila hatua Mungu anakumbana na hatari kubwa. Maneno yake ni ya kweli na ya uaminifu, na bila uovu, lakini nani yupo tayari kuyakubali? Nani yupo tayari kutii kikamilifu? Inavunja moyo wa Mungu. Anafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya mwanadamu, Anasongwa na wasiwasi kuhusu maisha ya mwanadamu na Anauonea huruma udhaifu wa mwanadamu. Amevumilia shida nyingi katika kila hatua ya kazi Yake, kwa kila neno Analozungumza; Yupo katikati ya mwamba na sehemu ngumu, na kufikiria juu ya udhaifu wa mwanadamu, ukaidi, utoto, na vile alivyo hatarini wakati wote … tena na tena. Nani amewahi kulijua hili? Nani anaweza kuwa na imani? Nani anaweza kufahamu? Anachukia dhambi za wanadamu daima, na ukosefu wa uti wa mgongo, mwanadamu kutokuwa na uti wa mgongo, ndiko kunamfanya kuwa na hofu juu ya hatari aliyonayo mwanadamu, na kutafakari njia zilizopo mbele ya mwanadamu; siku zote, anapoangalia maneno na matendo ya mwanadamu, je, yanamjaza huruma, hasira, na siku zote vitu hivi vinamletea maumivu moyoni Mwake. Hata hivyo, wasio na hatia wamekuwa wenye ganzi; kwa nini ni lazima Mungu siku zote afanye vitu kuwa vigumu kwao? Mwanadamu dhaifu, ameondolewa kabisa uvumilivu; kwa nini Mungu awe na hasira isiyopungua kwa mwanadamu? Mwanadamu aliye dhaifu na asiye na nguvu hana tena uzima hata kidogo; kwa nini Mungu anamkaripia siku zote kwa ukaidi wake? Nani anayeweza kuhimili matishio ya Mungu mbinguni? Hata hivyo, mwanadamu ni dhaifu, na yupo katika dhiki sana, Mungu ameisukuma hasira Yake ndani kabisa moyoni Mwake, ili kwamba mwanadamu ajiakisi mwenyewe taratibu. Ilhali mwanadamu, aliyepo katika matatizo makubwa, hazingatii hata kidogo mapenzi ya Mungu; amedondoshwa miguuni na mfalme mzee wa pepo, na bado haelewi kabisa, siku zote anajiweka dhidi ya Mungu, au si moto wala baridi kwa Mungu. Mungu amezungumza maneno mengi sana, lakini nani ambaye ameyazingatia? Mwanadamu haelewi maneno ya Mungu, lakini bado hashtuki, bila kuwa na shauku, na hajawahi kuelewa kabisa hulka ya ibilisi wa kale. Watu wanaishi Kuzimu, lakini wanaamini wanaishi katika kasri la chini ya bahari; wanateswa na joka kuu jekundu, lakini bado wanadhani “wamependelewa”[6] na nchi; wanadhihakiwa na ibilisi lakini wanadhani wanafurahia ustadi wa hali ya juu wa mwili. Ni wachafu kiasi gani, ni mafidhuli kiasi gani! Mwanadamu amekutana na bahati mbaya, lakini haijui, na katika jamii hii ya giza anapatwa na ajali baada ya ajali,[7] lakini hajawahi kufahamu hili. Ni lini atakapoachana na wema wake wa kibinafsi na tabia ya mawazo ya kiutumwa? Kwa nini hajali moyo wa Mungu kiasi hicho? Je, anajifanya haoni ukandamizaji na shida hii? Je, hatamani kuwe na siku ambayo atabadilisha giza kuwa nuru? Je, hatamani zaidi kuponya uonevu dhidi ya haki na ukweli? Je, yupo tayari kutazama tu bila kufanya chochote watu wakitupilia mbali ukweli na kupindua ukweli? Je, anafurahia kuendelea kuvumilia matendo haya mabaya? Je, yupo radhi kuwa mtumwa? Je, yupo tayari kuangamia mkononi mwa Mungu pamoja na watumwa wa taifa hili lililoanguka? Azma yako ipo wapi? Malengo yako yapo wapi? Heshima yako ipo wapi? Maadili yako yapo wapi? Uhuru wako upo wapi? Je, uko tayari kutoa maisha yako yote[8] kwa ajili ya joka kuu jekundu, mfalme wa pepo? Je, unafurahi kumwacha akutese hadi kufa? Kina chake ni vurugu na giza, ilhali mtu wa kawaida, anayeteseka na mateso kama hayo, analalamika bila kupumzika. Ni lini mwanadamu ataweza kunyanyua kichwa chake juu? Mwanadamu amekuwa kimbaumbau na amekonda, anawezaje kuridhika na ibilisi huyu katili na dikteta? Kwa nini asiyatoe maisha yake kwa Mungu mapema awezavyo? Kwa nini bado anayumbayumba? Anaweza kumaliza kazi ya Mungu lini? Hivyo anaonewa na kunyanyaswa bila sababu yoyote, maisha yake yote hatimaye yatakuwa bure; kwa nini ana haraka hivyo ya kufika, na haraka hiyo ya kuondoka? Kwa nini hahifadhi kitu kizuri cha kumpa Mungu? Je, amesahau milenia ya chuki?

Labda, watu wengi huchukia sana baadhi ya maneno ya Mungu, au labda hawayachukii sana wala hawana shauku kwayo. Hata hivyo, ukweli hauwezi kugeuka kuwa kufikiri kwa upuuzi; hakuna anayeweza kusema maneno ambayo yanaupinga ukweli. Mungu amefanyika kuwa mwili wakati huu kufanya kazi hii, kukamilisha kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kuifunga enzi hii, kuihukumu enzi hii, kuwaokoa waliozama kabisa dhambini kutoka katika ulimwengu wa bahari ya mateso na kuwabadilisha kabisa. Wayahudi walimsulubisha Mungu msalabani, hivyo kuhitimisha safari za Mungu kwenda Uyahudi. Sio baada ya muda mrefu, Mungu mwenyewe Alikuja kwa wanadamu kwa mara nyingine tena, na kuwasili kimyakimya katika nchi ya joka kuu jekundu. Kimsingi, jumuiya ya kidini ya serikali ya Kiyahudi kwa muda mrefu ilikuwa imetundika picha ya Yesu katika kuta zao, na kwa vinywa vyao watu wakalia “Bwana Yesu Kristo.” Hawakujua kwamba Yesu alikubali zamani sana amri ya Baba Yake kurudi miongoni mwa wanadamu kukamilisha hatua ya pili ya kazi Yake ambayo haikuwa imekamilika bado. Na matokeo yake, watu walipigwa na butwaa walipomwangalia: Alikuwa Amezaliwa katika ulimwengu ambamo enzi nyingi zilikuwa zimepita, na Alionekana miongoni mwa wanadamu kwa umbo la yule ambaye ni wa kawaida kabisa. Kimsingi, kadri enzi zilivyopita, mavazi Yake na umbo lote vimembadilika, kana kwamba Amezaliwa upya. Watu wangewezaje kujua kuwa ni Bwana Yesu Kristo yule Aliyeshuka msalabani na Aliyefufuliwa? Hana hata chembe ya jeraha, kama ambavyo Yesu hakuwa Anafanana na Yehova. Yesu wa leo kwa muda mrefu hajakuwa na kuvumilia kwa nyakati zilizopita. Watu wangewezaje kumjua? Watu wenye mashaka kama “Tomaso” mnafiki siku zote anakuwa na mashaka kwamba ni Yesu aliyefufuka, na siku zote anataka kuona makovu ya misumari katika mikono ya Yesu kabla hajatuliza akili yake; bila kuyaona, siku zote anaweza kusimama katika wingu la mashaka, na anakuwa hana uwezo wa kusimama imara na kumfuata Yesu. Maskini “Tomaso”—angewezaje kujua kuwa Yesu amekuja kufanya kazi Aliyoamriwa na Mungu Baba? Kwa nini Yesu anataka kuchukua makovu ya msalaba? Je, makovu ya kusulubiwa ni alama za Yesu? Amekuja kufanya kazi kwa ajili ya mapenzi ya Baba Yake; kwa nini Aje Akiwa Amevaa na kupambika kama Myahudi wa miaka elfu kadhaa iliyopita? Je, umbo ambalo Mungu analichukua katika mwili linaweza kuzuia kazi ya Mungu? Je, hii ni nadharia ya nani? Kwa nini, Mungu anapofanya kazi, ni lazima iwe kulingana na mitazamo ya mwanadamu? Kitu cha pekee ambacho Mungu anazingatia ni katika kazi Yake ni ili kazi hiyo iwe na matokeo. Hafuati sheria, na hakuna kanuni katika kazi Yake—mwanadamu angewezaje kuielewa? Mwanadamu anawezaje kupenya kikamilifu kazi ya Mungu kwa kutegemea fikira na mawazo yake? Hivyo itakuwa heri kwenu kutulia vizuri: Msihangaike na mambo madogomadogo, na msichukulie kwa ukubwa mambo ambayo ni mapya kwenu—hii itakuzuia kujitania na watu kukucheka. Umemwamini Mungu kwa miaka yote hii lakini bado humjui Mungu; hatimaye unatumbukiza katika kuadibu, wewe, ambaye umewekwa katika “kiwango cha juu kabisa,”[9] umewekwa katika madaraja ya walioadibiwa. Ni bora zaidi usitumie mbinu zako za kijanja kuonyesha hila zako; je, mtazamo wako huo finyu unaweza kumwelewa Mungu, Anayefahamu kutoka milele hadi milele? Je, uzoefu wako wa juujuu unaweza kukuruhusu ubaini kabisa mapenzi ya Mungu? Usiwe na majivuno. Hata hivyo, Mungu sio wa dunia—kwa hiyo inawezekanaje kazi Yake iwe kama ulivyotarajia?

Tanbihi:

1. “Kiongozi wa uovu wote” inahusu ibilisi mkongwe. Kirai hiki kinaonyesha kutopenda kabisa.

2. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo ibilisi hutumia huwadhuru watu.

3. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo ibilisi hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.

4. “Ya mbali” inatumiwa kwa dhihaka.

5. “Mwongozo wa utaratibu, wa upole” imetumika kimzaha.

6. “Wamependelewa” inatumiwa kuwadhihaki watu wanaoonekana wagumu na hawajitambui.

7. “Anapatwa na ajali baada ya ajali” inaonyesha kuwa watu walizaliwa katika nchi ya joka kubwa jekundu, na hawawezi kuwa na ujasiri.

8. “Kutoa maisha yako yote” imetumika kwa namna ya kimatusi.

9. “Kiwango cha juu kabisa,” inatumiwa kuwadhihaki wale wanaomtafuta Mungu kwa bidii.

Iliyotangulia: Kazi na Kuingia (7)

Inayofuata: Kazi na Kuingia (9)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp