Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Chaguzi zilizo katika kitabu hiki zote ni maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, zilizochukuliwa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili. Ni ukweli ambao kila mtu anayetafuta na kuchunguza kazi ya Mungu katika siku za mwisho anahitaji haraka kupata, zilichaguliwa ili kuwawezesha wale wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu waisikie sauti Yake haraka iwezekanavyo. Maonyesho ya Mungu katika kitabu hiki ni yale ambayo Roho Mtakatifu anayanena kwa makanisa kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo. Maneno haya ya sasa ya Mungu ni ushuhuda bora wa kuonekana Kwake na kazi Yake, na vile vile ushuhuda bora wa ukweli kwamba Kristo ndiye njia, ukweli na uzima. Tunatumaini kwamba wote wanaosubiri kuja kwa Bwana na wanaotazamia kuonekana kwa Mungu na kazi Yake wataweza kusoma kitabu hiki.

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp