Matamko ya Kristo Mwanzoni—Sura ya 3

Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Sayuni na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai ndani yake, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi. Kwa hakika Mungu atawahukumu hao, na kwa hakika Atakuwa mwenye hasira nao na mle uadhama wa Mungu utafichuliwa. Hukumu ya aina hiyo itakuwa papo hapo na kuwasilishwa bila kuchelewa. Moto wa ghadhabu ya Mungu utateketeza uhalifu wao mbaya na janga litawafikia wakati wowote; wao hawatajua njia ya kutoroka na hawatakuwa na mahali pa kujificha, wao watalia na kusaga meno yao, na watajiletea maangamizi.

Wana wapendwa wa Mungu wenye ushindi hakika watakaa katika Sayuni, kamwe hawataiacha. Umati utasikiliza sauti Yake kwa makini, watatilia maanani kwa uangalifu matendo Yake, na sauti zao za sifa Kwake kamwe hazitakoma. Mungu mmoja wa kweli Ameonekana! Tutakuwa na uhakika juu Yake katika roho na kumfuata kwa karibu na kukazana kusonga mbele bila kusita. Mwisho wa dunia unajitokeza mbele yetu; maisha sahihi ya kanisa pamoja na watu, shughuli, na mambo ambayo yanatuzunguka sasa hata yanayafanya mafunzo yetu yawe makali zaidi. Acha tufanye hima kurudisha mioyo yetu ambayo inapenda dunia sana! Acha tufanye hima kurudisha maono yetu ambayo yamefichwa sana! Hatutasonga mbele zaidi tusije tukazidi mipaka na tutashikilia ndimi zetu ili tuweze kuishi kwa kufuata neno la Mungu, na tena hatutazozana juu ya faida zetu wenyewe na hasara. Acha upendo wako wa dunia ya kawaida na utajiri! Ah, jiwekeni huru kutoka kwake—upendo wenu wa kuning’nia kwa waume zenu na mabinti na wana wenu! Acha maoni yako na upendeleo! Amka, kwa sababu muda ni mfupi! Iruhusu roho yako iangalie juu, angalia juu na umruhusu Mungu Achukue uongozi. Usijiruhusu kuwa kama mke wa Lutu. Kutelekezwa ni jambo la kusikitisha sana! Ni la kusikitisha kweli! Amka!

Iliyotangulia: Matamko ya Kristo Mwanzoni—Sura ya 2

Inayofuata: Matamko ya Kristo Mwanzoni—Sura ya 5

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp