
Neno Laonekana katika Mwili Toleo La 5
Majukumu ya Viongozi na WafanyakaziMajukumu ya Viongozi na Wafanyakazi ni juzuu ya tano ya Neno Laonekana katika Mwili. Kitabu hiki kinajumuisha mahubiri na ushirika wa Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, kwa makanisa kuhusu mada hii. Mungu ameshiriki kwa uwazi kuhusu majukumu ya viongozi na wafanyakazi, na vile vile kanuni mahususi na njia za utendaji kwa vipengele mbalimbali vya kazi ya kanisa. Pia Amefichua kiini cha udhihirisho na matendo mbalimbali ya viongozi wa uongo. Hili lina msaada mkubwa sana kwa watu katika kujifunza kutambua viongozi wa uongo, kufanya kazi halisi, kufikia utii kwa Mungu na kustahili kutumiwa na Yeye. Lina manufaa makubwa kwa watu kuuelewa ukweli, kujijua wenyewe, na kutekeleza wajibu wao kulingana na kanuni.
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho
- Kipengele cha Sita: Kuendeleza na kukuza kila aina ya talanta inayostahili ili wote wanaofuatilia ukweli waweze kuwa na fursa ya kujifunza na kuingia katika uhalisi wa ukweli haraka iwezekanavyo
- Kipengele cha Kumi na Moja: Kuwachagua watu wanaotegemewa ambao ubinadamu wao unafikia kiwango kinachostahili kwa ajili ya kazi ya kusajili, kujumlisha na kulinda matoleo kwa utaratibu; kupitia mara kwa mara na kuangalia mapato na matumizi ili visa vya ubadhirifu au uharibifu, pamoja na matumizi yasiyo ya busara, viweze kutambuliwa mara moja—kukomesha mambo kama hayo na kudai fidia inayofaa; zaidi ya hayo, kuzuia, kwa njia yoyote ile, matoleo yanayoanguka mikononi mwa watu waovu na kumilikiwa na wao
- Kipengele cha Kumi na Tatu: Kuwalinda Watu Wateule wa MunguWasisumbuliwe, Kupotoshwa, Kudhibitiwa, na Kudhuriwa Vibaya Sana na Wapinga Kristo, na Kuwawezesha Watambue Wapinga Kristo na Kuwatelekeza Kutoka Mioyoni Mwao