Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (5)

Katika mkutano uliopita, tulishiriki kuhusu kipengele cha tano cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Katika mchakato wa ushirika kuhusu kipengele cha tano, tulichanganua baadhi ya udhihirisho na matendo ya viongozi wa uongo, na tukamaliza kushiriki juu ya kipengele hiki. Sasa tutashiriki kuhusu vipengele vya sita na saba vya majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Je, maudhui maalum ya vipengele hivi viwili ni yapi? (Kipengele cha Sita: Kuendeleza na kukuza kila aina ya talanta inayostahili ili wote wanaofuatilia ukweli waweze kuwa na fursa ya kujifunza na kuingia katika uhalisi wa ukweli haraka iwezekanavyo. Kipengele cha Saba: Kuwatenga na kuwatumia watu wa aina tofauti kwa busara, kwa kuzingatia ubinadamu na nguvu zao, ili kila mmoja atumike kadiri ya ubora wake.) Hebu basi tuchanganue vitendo na maonyesho mbalimbali ya viongozi wa uongo kuhusu vipengele hivi viwili. Vipengele hivi viwili ni vya kundi moja, ambalo linahusu kanisa kuwakuza, kuwastawisha, na kuwatumia watu wa aina zote. Hebu kwanza tushiriki kuhusu kanuni za nyumba ya Mungu katika kukuza na kustawisha kila aina ya talanta zilizo na sifa hitajika. Kwa njia hiyo, je, basi kimsingi si mtaweza kuelewa baadhi ya kanuni ambazo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuzingatia wanapofanya kazi hii? Mnaweza kuwaza, “Kama viongozi na wafanyakazi, mara nyingi tunakutana na mambo haya, tayari tunaifahamu kazi hii na tuna uzoefu kiasi nayo, kwa hivyo hata Usiposema chochote zaidi kuihusu, tunaielewa, na Huhitaji kushiriki zaidi kuihusu.” Kwa hivyo, je, hakuna haja ya kushiriki kuihusu? (Tunahitaji ushirika Wako kuihusu. Bado hatuelewi kanuni katika suala hili, na kuna baadhi ya watu wenye talanta ambao bado hatujui jinsi ya kuwatambua.) Viongozi na wafanyakazi wengi bado wamechanganyikiwa sana kuhusu jinsi ya kufanya kazi hii, na wako katika mchakato wa kuielewa zaidi, na hawawezi kuelewa kanuni sahihi, kwa hivyo bado tunahitaji kushiriki kuhusu mambo ya ndani.

Kipengele cha Sita: Kuendeleza na kukuza kila aina ya talanta inayostahili ili wote wanaofuatilia ukweli waweze kuwa na fursa ya kujifunza na kuingia katika uhalisi wa ukweli haraka iwezekanavyo

Viongozi wa Uwongo Hawafanyi Kazi Halisi, Jambo Linalochelewesha Maendeleo ya Kazi

Kwa nini nyumba ya Mungu inakuza na kustawisha aina zote za watu wenye talanta? Je, inakuza na kustawisha aina zote za watu wenye talanta kwa ajili ya kujihusisha na sayansi, elimu, na fasihi? Watu wateule wa Mungu wanapaswa kujua tayari kwamba nyumba ya Mungu inapokuza na kustawisha aina mbalimbali za watu wenye talanta, hili halifanyiki ili kutengeneza aina fulani ya bidhaa ya teknolojia ya hali ya juu na kuunda muujiza au kufanya utafiti katika historia ya maendeleo ya mwanadamu, sembuse kupanga aina yoyote ya mipango kwa ajili ya mustakabali wa wanadamu. Kwa nini, basi, nyumba ya Mungu inakuza na kustawisha aina zote za watu wenye talanta? Je, mnaelewa hili au la? (Ili kueneza injili ya ufalme.) Ili kueneza injili ya ufalme—hii ni sababu moja. Kuna lipi lingine? (Kwa hivyo kila mtu anayefuatilia ukweli anaweza kupata fursa ya kufundisha.) Hiyo ni kweli, jibu hili lina mantiki kabisa na linagonga ndipo. Ni ili watu wengi zaidi wanaofuatilia ukweli waweze kupata fursa ya kufundisha, na kuingia katika uhalisi wa ukweli haraka iwezekanavyo. Majibu yote mawili ambayo ninyi mmeyatoa sasa hivi ni sahihi na sawa. Kuwakuza na kuwastawisha watu wenye talanta za kila aina na nyumba ya Mungu kwa upande mmoja kunahusiana na kueneza injili ya ufalme na kazi ya Mungu, na kwa upande mwingine, kunahusiana na shughuli za mtu binafsi na kuingia. Hivi ndivyo vipengele viwili vikuu. Kuzungumza kwa uhakika, umuhimu wa nyumba ya Mungu kukuza na kustawisha watu wenye talanta za kila aina ni upi? Hasa ni kazi gani inayofanywa kanisani na watu hawa wanaokuzwa na kustawishwa? Nyumba ya Mungu inapomkuza na kumstawisha mtu kuwa kiongozi wa timu, msimamizi, au kiongozi wa kanisa au mfanyakazi, je, anafanywa kuwa kiongozi? (Hapana.) Nyumba ya Mungu huwakuza na kuwastawisha watu ili waweze kuwajibika kwa miradi au kazi maalum ndani ya kazi mbalimbali za kanisa, kama vile kazi ya injili, kazi ya maandishi, kazi ya utengenezaji wa filamu, kazi ya unyunyizaji, pamoja na mambo mengine ya jumla, na kadhalika. Kwa hivyo, wanafanyaje kazi hizi maalum? Kwa kufanya kazi mbalimbali za kanisa kulingana na mahitaji ya Mungu, kanuni za ukweli za maneno ya Mungu, na mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu, na hivyo kufanya wajibu wao kulingana na mahitaji ya Mungu na kutenda kulingana na kanuni za ukweli. Kwa kuzingatia ukweli kwamba watu hawa wanakuzwa na kustawishwa ili watekeleze kazi, si kuwa na cheo au hadhi rasmi inayowawezesha kufanya kazi yao vizuri. Badala yake, lazima wawe na kiwango fulani ili waweze kufanya kazi maalum, yaani, kufanya kile ambacho Mungu amewaaminia kufanya, au kwa maneno mengine, wajibu na kazi iliyo na kujukumika. Huu ndio umuhimu na ufafanuzi maalum wa kukuza na kustawisha aina mbalimbali za watu wenye talanta kama ilivyotajwa katika kipengele cha sita cha majukumu ya viongozi na wafanyakazi. Kwa hivyo, katika kuwakuza na kuwastawisha watu, lengo la nyumba ya Mungu ni kukuza aina zote za watu wenye talanta ili kufanya kazi mbalimbali za kanisa vizuri kulingana na mahitaji ya Mungu na mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu; ni kuwawezesha watu hawa kufanya kazi mbalimbali maalum za kanisa. Wakati huo huo, nyumba ya Mungu huwalea na kuwafundisha watu hawa ili wajifunze jinsi ya kutafakari maneno ya Mungu, kushiriki katika ukweli, na kutenda kulingana na kanuni, ikiwaongoza kutenda ukweli na kuishi kwa maneno ya Mungu, na kuingia katika uhalisi wa ukweli, na kuwawezesha kuwa na uzoefu na ushuhuda wa kweli, baada ya hapo wanaweza kuwaongoza, kuwanywesha, na kuwapa wengine, na kufanya kazi nzuri ya vitu mbalimbali vya kanisa, na wakati huo huo, watu wateule wa Mungu wanaweza kuwezeshwa kujitiisha kwa Mungu, kumshuhudia Mungu, na kutimiza wajibu wa kuhubiri injili. Njia ya kutenda kwa ajili ya kukuza na kustawisha kila aina ya watu wenye talanta ni, kwa upande mmoja, kuwaongoza watu katika kutenda na kupitia maneno ya Mungu, kujijua wenyewe, kutupilia mbali tabia zao mbovu, na kuingia katika uhalisi wa ukweli; kwa upande mwingine, ni kwa viongozi na wafanyakazi kutumia uzoefu wao wa vitendo wa uaminifu na utii kuwaongoza na kuwalea watu katika kutimiza majukumu yao na kutoa ushuhuda mkubwa kwa Mungu. Hizi ndizo njia mbili kuu za kutenda kwa ajili ya kuwastawisha aina mbalimbali za watu wenye talanta. Hii ndiyo kazi mahususi inayohusika katika kukuza na kustawisha aina mbalimbali za watu wenye talanta, na pia ni umuhimu halisi wa kukuza na kustawisha.

Vigezo Vinavyohitajika kwa Aina Mbalimbali za Watu Wenye Talanta Ambao Nyumba ya Mungu Inakuza na Kustawisha

I. Vigezo Vinavyohitajika kwa Viongozi na Wafanyakazi na Wasimamizi wa Vipengele Mbalimbali vya Kazi

“Aina mbalimbali za watu wenye talanta wanaokuzwa na kustawishwa na kanisa” hurejelea akina nani? Hilo linajumuisha malengo gani? Kwanza ni aina ya watu ambao wanaweza kuwa wasimamizi wa vipengele mbalimbali vya kazi. Je, viwango vinavyohitajika kwa wasimamizi wa vipengele mbalimbali vya kazi ni vipi? Kuna viwango vitatu vikuu. Kwanza, lazima wawe na uwezo wa kuuelewa ukweli. Ni wale tu ambao wanaweza kuelewa ukweli bila upotoshaji na kupata hitimisho ndio watu wenye ubora mzuri wa tabia. Watu wenye ubora mzuri wa tabia lazima angalau wawe na uelewa wa kiroho na waweze kula na kunywa maneno ya Mungu kwa kujitegemea. Katika mchakato wa kula na kunywa maneno ya Mungu, lazima waweze kukubali kwa kujitegemea hukumu, kuadibu, na upogoaji wa maneno ya Mungu, na kutafuta ukweli ili kutatua dhana na mawazo yao wenyewe na kuchafuliwa kwa mapenzi yao wenyewe, pamoja na tabia zao potovu—wakifikia kiwango hiki inamaanisha wanajua jinsi ya kupitia kazi ya Mungu, na hii ni dhihirisho la kiwango kizuri. Pili, lazima wabebe mzigo kwa kazi ya kanisa. Watu wanaobeba mzigo kweli hawana shauku tu, wana uzoefu wa kweli wa maisha, wanaelewa ukweli fulani, na wanaweza kuona kupitia baadhi ya matatizo. Wanaona kwamba katika kazi ya kanisa na watu wateule wa Mungu kuna shida na matatizo mengi ambayo yanahitaji kutatuliwa. Wanaona hili kwa macho yao na kuwa na wasiwasi nalo mioyoni mwao—hii ndiyo maana ya kubeba mzigo kwa ajili ya kazi ya kanisa. Ikiwa mtu ni mwenye ubora mzuri wa tabia tu na ana uwezo wa kuelewa ukweli, lakini ni mvivu, anatamani starehe za mwili, hayuko tayari kufanya kazi halisi, na hufanya kazi kidogo tu wakati Aliye juu Anapompa muda wa mwisho wa kukamilika kwake, wakati hawezi kuepuka kutofanya hivyo, basi huyu ni mtu asiyebeba mzigo. Watu wasiobeba mzigo ni watu ambao hawafuatilii ukweli, watu wasio na hisia ya haki, na wazembe ambao hushinda siku nzima wakila tu, bila kufikiria chocote kwa uzito. Tatu, lazima wawe na uwezo wa kufanya kazi. “Uwezo wa kufanya kazi” unamaanisha nini? Kwa ufupi, inamaanisha kwamba sio tu kwamba wanaweza kugawa kazi na kuwapa watu maagizo, lakini pia wanaweza kutambua na kuyatatua matatizo—hii ndiyo maana ya kuwa na uwezo wa kufanya kazi. Zaidi ya hayo, wanahitaji pia ujuzi wa kupangilia. Watu wenye ujuzi wa kupanga wana ujuzi hasa wa kuwaleta watu pamoja, kupanga na kupanga kazi, na kutatua matatizo, na wanapopanga kazi na kutatua matatizo, wanaweza kuwashawishi watu kikamilifu na kuwafanya watii—hii ndiyo maana ya kuwa na ujuzi wa kupanga. Wale ambao kweli wana uwezo wa kufanya kazi wanaweza kutekeleza kazi maalum zilizopangwa na nyumba ya Mungu, na wanaweza kufanya hivyo haraka na kwa uamuzi bila uzembe wowote, na zaidi ya hayo wanaweza kufanya kazi mbalimbali vizuri. Hivi ndivyo viwango vitatu vya nyumba ya Mungu kwa ajili ya kuwakuza viongozi na wafanyakazi. Ikiwa mtu anafikia viwango hivi vitatu, ni mtu adimu, mwenye talanta na anapaswa kustawishwa, kukuzwa, na kufundishwa mara moja, na baada ya kufanya kutenda kwa muda, anaweza kuchukua kazi hiyo. Yeyote aliye na ubora mzuri wa tabia, anayebeba mzigo, na mwenye uwezo wa kufanya kazi hahitaji watu kuwa na wasiwasi kila wakati juu yake na kumsimamia na kumhimiza katika kazi yake. Yeye ni makini, anajua ni kazi zipi zinazopaswa kufanywa wakati gani, ni kazi zipi za kukagua na kusimamia, na ni kazi zipi zinazohitaji kuchunguzwa au kuangaliwa kwa karibu. Anafahamu vyema mambo haya. Watu kama hao ni wa kutegemewa na wa kuaminika kiasi katika kazi zao, na hakuna matatizo makubwa yatakayotokea. Hata kama matatizo yatatokea, yatakuwa masuala madogo ambayo hayaathiri kazi muhimu, na Mungu hawezi kuwa na wasiwasi kuhusu kazi ambayo watu hawa hufanya. Ni wale tu ambao wanaweza kujitegemea katika kazi zao ndio wenye uwezo wa kufanya kazi. Wale ambao hawawezi kujitegemea na kila mara wanawafanya wengine wawe na wasiwasi kuwahusu, wawaangalie, kuwasimamia, na hata kuwashika mkono na kuwafundisha cha kufanya ni aina ya watu ambao wana sifa duni sana. Matokeo ya kazi ambayo watu wenye ubora wa tabia wa kawaida hufanya ni ya kawaida kabisa, na watu hawa wanawahitaji wengine wawaangalie na kuwasimamia kabla hawajafanya chochote. Kwa upande mwingine, watu wenye ubora mzuri wa tabia wanaweza kujitegemea wenyewe baada ya kufundishwa kwa muda, na kila wakati Aliye juu Anapowapa maelekezo ya kazi na kujifunza kanuni fulani, wanaweza kuelewa kanuni, kutekeleza kazi kulingana nazo, na kimsingi kufuata njia sahihi bila kupotoka au kuwa na dosari kubwa sana, na kufikia matokeo wanayopaswa kupata—hii ndiyo maana ya kuwa na uwezo wa kufanya kazi. Kwa mfano, nyumba ya Mungu inahitaji kanisa lisafishwe, na wapinga Kristo na watu waovu watambuliwe na kutimuliwa kutoka kanisani, na aina ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi kimsingi hawapotoki wanapotekeleza kazi hii. Mara tu mpinga Kristo anapotokea, inachukua takriban nusu ya mwaka kwa wao kufunuliwa na kuondolewa. Wakati huu, wale walio na uwezo wa kufanya kazi wanaweza kuwatambua, kushiriki kuhusu ukweli ili kuchanganua udhihirisho wa mpinga Kristo, na kuwasaidia akina ndugu kupata utambuzi wao na wasipotoshwe, na hivyo kuwawezesha kuinuka ili kufichua na kumfukuza mpinga Kristo pamoja. Wapinga Kristo au watu waovu wanapoonekana katika mawanda ya kazi ya watu walio na uwezo wa kufanya kazi, kimsingi akina ndugu hawapotoshwi au kushawishiwa. Ni watu wachache tu wenye kuboronga na wale wenye ubora duni wa tabia ndio hupotoshwa, na hili ni jambo la kawaida. Watu wenye ubora mzuri wa tabia na walio na uwezo wa kufanya kazi wanaweza kufanikisha matokeo haya katika kazi yao, na watu kama hao wana uhalisi wa ukweli na wako katika kiwango cha juu kama viongozi na wafanyakazi.

Miongoni mwa aina mbalimbali za watu wenye talanta Niliowataja sasa hivi, aina ya kwanza ilikuwa wale ambao wanaweza kuwa wasimamizi wa kazi mbalimbali. Sharti la kwanza kwao ni kwamba wawe na uwezo na ubora mzuri wa tabia wa kuelewa ukweli. Hili ndilo sharti la msingi kabisa. Sharti la pili ni kwamba wabebe mzigo—hili ni muhimu sana. Baadhi ya watu huelewa ukweli haraka zaidi kuliko watu wa kawaida, wana uelewa wa kiroho, wana ubora mzuri wa tabia, wana uwezo wa kufanya kazi, na baada ya kutenda kwa muda, wanaweza kujitegemea wenyewe. Lakini kuna tatizo kubwa na watu hawa—hawabebi mzigo wowote. Wanapenda kula, kunywa, kufurahi, na kufanya kazi kwa bidii. Wanapendezwa sana na mambo haya, lakini wakiombwa kufanya kazi fulani maalum inayowahitaji wateseke na kulipa gharama, na kujizuia kidogo, wanakosa raha, na wao hudai kwamba wana ugonjwa au mateso fulani, na kwamba kila sehemu yao huhisi vibaya. Hawajizuii na hawana nidhamu, ni wa kawaida, wakaidi, na wapotovu. Wanakula, kulala, na kufurahia wakati wowote wanapotaka, na hufanya kazi fulani tu wakati hisia zinapowaelekeza. Kazi ikiwa ngumu kidogo au inayochosha, wanapoteza hamu na hawataki tena kufanya wajibu wao. Je, huku ni kubeba mzigo? (Hapana.) Watu ambao ni wavivu na wanaotamani starehe za mwili sio wale wanaopaswa kukuzwa na kustawishwa. Pia kuna watu ambao ubora wao wa tabia unatosha kwa kazi, lakini kwa bahati mbaya hawabebi mzigo, hawapendi kuchukua jukumu, hawapendi shida, na hawapendi kuwa na wasiwasi. Wao huifumbia macho kazi inayohitaji kufanywa, na hata kama wanaweza kuiona, hawataki kuishughulikia. Je, watu wa aina hii wanastahili kukuzwa na kustawishwa? Hapana; watu lazima wabebe mzigo ili waweze kukuzwa na kustawishwa. Kubeba mzigo pia kunaweza kuelezwa kama kuwa na hisia ya uwajibikaji. Kuwa na hisia ya uwajibikaji kunahusiana zaidi na ubinadamu; kubeba mzigo kunahusiana na mojawapo ya viwango ambavyo nyumba ya Mungu hutumia kuwapima watu. Wale wanaobeba mzigo huku wakiwa na vitu vingine viwili—uwezo na ubora wa tabia wa kuuelewa ukweli, na uwezo wa kufanya kazi—ndio aina ya watu ambao wanaweza kukuzwa na kustawishwa, na aina hii ya watu wanaweza kuwa wasimamizi wa vipengele mbalimbali vya kazi. Hivi ndivyo viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kuwakuza na kuwastawisha watu ili wawe aina mbalimbali za wasimamizi, na watu wanaofikia viwango hivi ndio wanaostahili kukuzwa na kustawishwa.

II. Vigezo Vinavyohitajika kwa Watu Wenye Talanta Katika Taaluma Mbalimbali Walio na Talanta au Vipawa Maalum

Mbali na aina ya watu ambao wanaweza kuwa wasimamizi wa kazi mbalimbali, aina nyingine ya watu ambao wanaweza kukuzwa na kustawishwa ni wale walio na talanta au vipawa maalum au wamebobea katika ujuzi fulani wa kitaaluma. Je, kiwango ambacho nyumba ya Mungu inahitaji kwa ajili ya kuwakuza watu kama hawa kuwa viongozi wa timu ni kipi? Kwanza angalia ubinadamu wao—mradi tu wanapenda mambo chanya na si watu wabaya, hiyo inatosha. Baadhi ya watu wanaweza kuuliza, “Kwa nini halazimiki kuwa mtu anayefuatilia ukweli?” Kwa sababu viongozi wa timu si viongozi wa kanisa au wafanyakazi, wala si wanyunyizaji, na kuwataka kufikia kiwango cha kufuatilia ukweli kungekuwa kutarajia mengi zaidi kutoka kwao, na wengi hawawezi kufikia haya. Hili halihitajiki kwa watu wanaofanya kazi ya mambo ya jumla au kazi maalum za kitaaluma; kama ingekuwa hivyo, ni wachache tu ambao wangekuwa wanastahili, kwa hivyo viwango vinapaswa kupunguzwa. Mradi tu watu wanaelewa taaluma yao na wana uwezo wa kuifanya kazi, na hawafanyi uovu au kusababisha usumbufu wowote, basi hiyo inatosha. Kwa watu hawa, ambao wana utaalamu katika ujuzi na taaluma fulani na wana nguvu fulani, ikiwa watafanya kazi inayohitaji ujuzi fulani na inayohusiana na taaluma zao katika nyumba ya Mungu, mradi tu wawe wakamilifu na wanyofu katika tabia zao, si waovu, hawajapotoka katika ufahamu wao, wanaweza kuvumilia magumu, na wako tayari kulipa gharama, basi hiyo inatosha. Kwa hivyo, sharti la kwanza la kuwakuza watu kama hao wawe viongozi wa timu ni kwamba lazima wapende vitu chanya kwa kiasi, na zaidi ya hayo, lazima waweze kuvumilia magumu na kulipa gharama. Kuna kipi kingine? (Lazima wawe na tabia nyofu, na wasiwe waovu, na wasiwe waliopotoka katika ufahamu wao.) Tabia zao lazima ziwe nyofu kiasi, lazima wasiwe watu waovu, na lazima wasiwe wamepotoka katika ufahamu wao. Baadhi ya watu wanaweza kuuliza, “Kwa hivyo uwezo wao wa kuelewa ukweli unaweza kuzingatiwa kuwa wa hali ya juu? Baada ya kusikia ukweli, je, wanaweza kuutambua uhalisi wa ukweli, na kuingia katika uhalisi wa ukweli?” Hakuna haja ya kuhitaji haya yote; inatosha kuhitaji kwamba watu kama hao wasipotoke katika ufahamu wao. Watu ambao hawajapotoka katika ufahamu wao wanapofanya kazi yao, moja ya faida ni kwamba hawawezi kusababisha usumbufu au kufanya jambo lolote la kipuuzi. Kwa mfano, nyumba ya Mungu imefanya ushirika mara kwa mara kuhusu kanuni za rangi ya mavazi ya waigizaji, ambayo yanapaswa kuwa ya hadhi na ya heshima, na yenye rangi za kupendeza badala ya kuwa ya kuchosha. Lakini bado kuna wale ambao hawawezi kuelewa wanachoambiwa, hawaelewi wanachosikia, hawawezi kuelewa, na hawawezi kutambua kanuni zilizo ndani ya mahitaji haya ya nyumba ya Mungu, na huishia kuchagua mavazi ambayo yote ni ya kijivu—je, huu si ufahamu uliopotoka? (Ndiyo.) Hivi ndivyo inavyomaanisha kuwa na ufahamu uliopotoka. Inamaanisha nini hasa kupenda vitu chanya kwa kiasi fulani? (Kuweza kukubali ukweli.) Hiyo ni kweli. Inamaanisha kuweza kukubali maneno na vitu vinavyopatana na ukweli, na kuweza kukubali na kutii maneno ya Mungu na vipengele vyote vya ukweli. Bila kujali kama watu kama hao wanaweza kuweka mambo haya katika vitendo, angalau, ndani kabisa hawapaswi kupinga au kuchukizwa nayo. Watu kama hao ni watu wazuri, na kwa lugha ya kawaida inaweza kusemwa kwamba wao ni watu wazuri. Je, sifa za watu wema ni zipi? Wanahisi maudhi, mkuruhu, na kuchukizwa na matendo maovu ambayo wasioamini hupenda kufanya, na pia mwelekeo mbaya ambao wasioamini hufuata. Kwa mfano, mitindo ya ulimwengu usioamini hutetea nguvu za uovu, na wanawake wengi hufuatilia kuolewa na mtu tajiri au kuwa mpeni wa siri wa mtu. Je, huu si uovu? Watu wanaopenda ukweli huona mambo haya kuwa ya kuchukiza sana na wengine husema, “Hata nisipoweza kupata mtu wa kuoa, hata kama ningekuwa nakufa kwa ajili ya umasikini, singewahi kutenda kama mmoja wa watu hao,” kwa maneno mengine, wanawadharau na kuwatweza watu kama hao. Sifa moja ya watu wema ni kwamba wanaona mitindo mibaya kuwa ya kuchukiza na ya kukirihi, na wanawadharau wale ambao wamenaswa na mitindo kama hiyo. Watu hawa ni waadilifu kiasi; kunapotajwa kumwamini Mungu na kuwa mtu mwema, kutembea katika njia sahihi, kumwabudu Mungu na kuepuka na uovu, kuepukana na mitindo mibaya, na kuepukana na tabia zote mbaya duniani, ndani kabisa wanahisi kwamba hili ni jambo jema. Iwe wanaweza kupiga hatua kufikia haya yote au la, na bila kujali jinsi azimio lao lilivyo kubwa la kumwamini Mungu na kutembea katika njia sahihi, baada ya yote, ndani kabisa wanatamani kuishi katika nuru na wanatamani kuwa mahali ambapo haki ina nguvu. Watu mashuhuri kama hawa ni aina ya watu wanaopenda mambo chanya. Wale ambao wanakuzwa na kustawishwa na nyumba ya Mungu lazima angalau wawe na tabia ya ubinadamu waadilifu na upendo wa mambo chanya. Hiki pia ni kiwango cha kwanza kinachohitajika kwa kukuza aina ya watu wenye talanta ambao wana ujuzi na nguvu za kitaaluma. Kiwango cha pili ni kwamba watu kama hao lazima waweze kupitia magumu na kulipa gharama. Hiyo ni, linapokuja suala la sababu au kazi ambayo wanaipenda, wanaweza kuweka kando matamanio yao wenyewe, kuweka kando raha za mwili au mtindo wa maisha wa starehe, na hata kuacha matarajio yao ya baadaye. Zaidi ya hayo, ugumu kidogo au kuhisi uchovu kidogo si jambo kubwa kwao; mradi tu wanafanya jambo lenye maana na ambalo wanaamini kuwa ni sahihi, basi kwa furaha wao huacha raha na manufaa ya kimwili—au, angalau, wana azimio na wanatamani kufanya hivyo. Baadhi ya watu husema, “Wakati mwingine mtu huyo bado anatamani starehe za mwili: Wakati mwingine anataka kulala, au kula chakula kizuri, na wakati mwingine anataka kwenda nje kuzurura au kutembeatembea—lakini mara nyingi anaweza kupitia shida na kulipa gharama; ni kwamba tu wakati mwingine hisia zao huwaongoza kwenye mawazo kama hayo. Je, hili linazweza kuchukuliwa kuwa tatizo?” Haliwezi. Itakuwa kutarajia makuu kudai kwamba waache kabisa raha za mwili, isipokuwa katika hali maalum. Kwa ujumla, unapowapa watu kama hao kazi ya kufanya, iwe ni kazi kubwa au la, na iwe ni kitu wanachopenda kufanya au la, na haijalishi kazi hiyo ni ngumu kiasi gani, au ugumu wanaopaswa kuvumilia ni mkubwa kiasi gani, au ni gharama gani wanayopaswa kulipa, mradi tu ukiwapa, wanahakikisha kuifanya kwa uwezo wao wote hata bila wewe kuhitaji kuwachunga au kuwasimamia. Watu kama hao wanaweza kupitia shida na kulipa gharama, na huu ni udhihirisho mwingine wa watu wema. Inamaanisha nini kuweza kupitia shida na kulipa gharama? Inamaanisha kuwa mkamilifu, kujitolea sana na kuwa makini, na kuwa tayari kupitia shida yoyote na kulipa gharama yoyote ili mambo yafanyike ipasavyo. Watu kama hao, linapokuja suala la kukamilisha mambo, hutimiza ahadi zao na ni wenye kutegemewa, tofauti na watu ambao ni walafi na wavivu, wanaopenda starehe na wanachukia kazi, na huweka faida mbele ya kila kitu. Watu hao hukosa kutimiza ahadi zao, husema maneno ya uongo kila mara ili kuwadanganya na kuwashawishi wengine, na hawasiti kusema uongo na kuapa viapo vya uongo ili kufikia malengo yao—Mungu hatawaokoa watu hao. Mungu anapenda watu waaminifu. Ni watu waaminifu pekee wanaotimiza ahadi zao na ni waaminifu kwa majukumu yao, na ni wale tu wanaoweza kupitia magumu na kulipa gharama ili kutimiza agizo la Mungu ndio wanaoweza kuokolewa na Mungu. Kuweza kupitia magumu na kulipa gharama ndiyo sifa na udhihirisho wa pili ambao mtu anapaswa kuwa nao ili kukuzwa na kustawishwa na nyumba ya Mungu. Kiwango cha tatu ni kutopotoshwa katika ufahamu wa mtu. Yaani, baada ya kusikiliza maneno ya Mungu, angalau anaweza kujua maneno yanamaanisha nini, anaweza kuelewa kile ambacho Mungu anasema, na ufahamu yeye si wa kupotoka au wa kipuuzi. Kwa mfano, ukizungumzia rangi ya samawati, hataielewa vibaya kama nyeusi, na ukizungumzia rangi ya kijivu, hataielewa vibaya kama ya zambarau. Hiki ndicho kiwango cha msingi. Hata kama wakati mwingine ufahamu wake umepotoka, wengine wanapotajaja hili analikubali, na akiona kwamba mtu mwingine ana ufahamu safi zaidi kuliko wake yeye, anaweza kuukubali kwa urahisi—mtu wa aina hii ana ufahamu safi. Nne, hapaswi kuwa mtu mwovu. Je, hili ni jambo rahisi kuelewa? Kutokuwa mtu mwovu kunamaanisha kulazimika kufanya jambo moja angalau, ambalo ni kwamba baada ya kushindwa kufanikisha kile alichoambiwa na nyumba ya Mungu, au kukiuka kanuni na kufanya jambo baya, watu kama hao lazima waweze kukubali na kunyenyekea wanapopogolewa, bila upinzani na bila kueneza mawazo hasi au dhana. Zaidi ya hayo, bila kujali wako katika kundi gani, wanaweza kuelewana na watu wengi na kushirikiana nao kwa amani. Hata mtu anapowaumiza kwa kusema jambo lisilopendeza, wanaweza kuvumilia bila kuweka kisasi, na mtu yeyote akiwanyanyasa, hawaadhibu uovu kwa uovu, lakini badala yake wanachukua njia za busara za kukaa mbali na kujiondoa katika nafasi ile. Ingawa watu kama hao wanashindwa kuwa watu waaminifu, angalau wao ni waadilifu na hawafanyi uovu, na mtu yeyote akiwakosea hawalipizi kisasi au kumtesa mtu huyo pia, wala kumkandamiza. Zaidi ya hayo, watu kama hao huwa hawajaribu kuanzisha falme zao huru, kutenda kinyume na nyumba ya Mungu, kueneza mawazo kumhusu Mungu, kujaribu kumhukumu, au kufanya chochote kinachovuruga au kusababisha usumbufu. Mambo manne yaliyotajwa hapo juu ni vigezo vya msingi vya kuwakuza na kuwastawisha watu wenye talanta ambao wana uwezo fulani na wanaoelewa ujuzi fulani wa kitaaluma. Mradi tu wanatimiza vigezo hivi vinne, kimsingi wanaweza kutekeleza majukumu fulani na kufanya kazi fulani kwa njia ipasayo.

Baadhi ya watu wanaweza kuuliza: “Inakuwaje kwamba vigezo ambavyo watu wenye talanta wanapaswa kufikia ili kukuzwa na kustawishwa havijumuishi kuelewa ukweli, kuwa na uhalisi wa ukweli, na kuwa na uwezo wa kumcha Mungu na kuepuka uovu? Inakuwaje kwamba havijumuishi kuweza kumjua Mungu, kuweza kumtii Mungu, kuwa mwaminifu kwa Mungu, na kuwa kiumbe aliyeumbwa ambaye anafikia viwango vinavyohitajika? Je, mambo haya yameachwa nyuma?” Hebu Niambie, iwapo mtu anaelewa ukweli na ameingia katika uhalisi wa ukweli, na anaweza kumtii Mungu, na ni mwaminifu kwa Mungu, na ana moyo wa kumcha Mungu, na zaidi ya hayo, anamjua Mungu, hatampinga, na ni kiumbe aliyeumbwa ambaye anafikia kiwango kinachohitajika, je, bado anahitaji kukuzwa? Iwapo wamefikia haya yote, je, si matokeo ya ukuzaji tayari yamefanikisha? (Ndiyo.) Kwa hivyo, mahitaji ya watu wenye talanta wanaopasa kukuzwa na kustawishwa hayajumuishi vigezo hivi. Kwa sababu wagombea wanastawishwa na kukuzwa kutoka miongoni mwa wanadamu ambao hawaelewi ukweli na waliojawa na tabia potovu, kwa hiyo haiwezekani kwa wagombea hawa wanastawishwa na kukuzwa tayari kuwa na uhalisi wa ukweli, au tayari kumtii Mungu kikamilifu, sembuse wao tayari kuwa waaminifu kabisa kwa Mungu, na kwa hakika bado wako mbali zaidi na kumjua Mungu na kuwa na moyo wa kumcha Mungu. Vigezo ambavyo kila aina ya watu wenye talanta wanapaswa kufikia zaidi ya yote ili waweze kukuzwa na kustawishwa ndivyo tulivyotaja hivi punde—hivi ndivyo vya uhalisi na mahususi. Baadhi ya viongozi wa uwongo husema, “Hatuna watu wenye talanta yoyote hapa ambao wanaweza kukuzwa na kustawishwa. Fulani haelewi ukweli, fulani hufanya mambo bila moyo wa kumcha Mungu, fulani hawezi kukubali kupogolewa, fulani hana uaminifu ...” na kadhalika, akichagua rundo zima la makosa. Je, viongozi hawa wa uongo wanamaanisha nini kwa kusema mambo haya? Ni kana kwamba watu hao hawawezi kukuzwa na kustawishwa kwa sababu hawaelewi ukweli, na hawapitii kazi ya Mungu, na bado hawana uhalisi wa ukweli, na kadhalika, ilhali viongozi wenyewe waliweza kuwa viongozi kwa sababu tayari wana uzoefu fulani wa vitendo na wana uhalisi wa ukweli. Je, si hivi ndivyo wanavyomaanisha viongozi hawa wa uongo? Machoni mwao, hakuna aliye mzuri kama wao, na hakuna mtu anayefaa kuwa kiongozi isipokuwa wao wenyewe. Hii ni tabia ya kiburi ya viongozi wa uongo; linapokuja suala la nyumba ya Mungu kukuza na kustawisha watu, wao wamejaa fikira na mawazo.

III. Vigezo Vinavyohitajika kwa Wafanyakazi wa Kazi ya Masuala ya Jumla

Nimetaja sasa hivi aina mbili za watu ambao nyumba ya Mungu inalenga kuwakuza. Aina moja ni watu wanaoweza kuwa viongozi na wafanyakazi, na aina nyingine ni watu wanaoweza kufanya kazi mbalimbali za kitaaluma. Pia kuna mtu wa aina nyingine. Hawezi kusemwa kuwa ana uwezo fulani au ujuzi wa kitaaluma; kazi yake haihusishi teknolojia yoyote ya hali ya juu, hiyo ni kusema, watu hawa hufanya kazi fulani ya mambo ya jumla katika kanisa, wanashughulikia mambo fulani yasiyo ya kawaida kwa kazi kuu ya kanisa. Ni aina ya watu wanaofanya kazi za jumla. Matakwa makuu ya nyumba ya Mungu kwa watu kama hao ni yapi? Takwa lililo muhimu zaidi ni kwamba waweze kutetea masilahi ya nyumba ya Mungu, wasiwasaidie watu wa nje kutumia rasilmali ya nyumba ya Mungu, na wasisaliti masilahi ya nyumba ya Mungu ili kujipendekeza kwa Shetani. Ni hayo tu. Bila kujali kama yeye ni mzungumzaji mwenye kipawa, mzuri sana katika jamii, au kuwa na talanta maalum, anapaswa kuweza kutetea masilahi ya nyumba ya Mungu anaposhughulikia mambo ya nje kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Masilahi ya nyumba ya Mungu yanajumuisha nini? Pesa, nyenzo, sifa za nyumba ya Mungu na kanisa, na usalama wa akina ndugu—kila mojawapo ya vipengele hivi ni muhimu sana. Yeyote anayeweza kutetea maslahi ya nyumba ya Mungu ana ubinadamu wa kawaida, na ana msimamo wa kutosha, na ni mtu ambaye yuko tayari kutenda ukweli. Baadhi ya watu hawana utambuzi, na husema, “Kuna mtu mwenye ubinadamu mwovu, lakini anaweza kuitetea kazi ya nyumba ya Mungu.” Je, hilo linawezekana? (Hapana, haliwezekani.) Watu waovu wanawezaje kuitetea kazi ya nyumba ya Mungu? Wanaweza tu kutetea maslahi yao wenyewe. Hivyo, ikiwa mtu anaweza kweli kutetea maslahi ya nyumba ya Mungu, hakika atakuwa na tabia njema na ubinadamu; hili haliwezi kuwa kosa. Mtu akiwasaidia watu wa nje kwa gharama ya nyumba ya Mungu anapofanya mambo kwa ajili ya nyumba ya Mungu, na kusaliti maslahi ya nyumba ya Mungu, na zaidi ya kusababisha hasara kubwa za kiuchumi na kimwili kwa nyumba ya Mungu, pia asababishe uharibifu mkubwa kwa sifa za nyumba ya Mungu na kanisa, je, yeye ni mtu mwema? Watu kama hao hakika si mambo mazuri. Hawajali jinsi nyumba ya Mungu inavyopata hasara kubwa ya kimwili na kifedha; jambo muhimu zaidi kwao ni kujinufaisha wenyewe na kujipendekeza kwa wasioamini; mbali na kuwatumia wasioamini zawadi, wao pia huwapa ridhaa kila mara wakati wa mazungumzo—hawajafikiria kupigania maslahi ya nyumba ya Mungu. Na bado, wanaidanganya nyumba ya Mungu, wakisema jinsi walivyokamilisha kazi, na kutetea maslahi ya nyumba ya Mungu—wakati kwa kweli, kazi ya kanisa tayari imepata hasara, na nyumba ya Mungu imetumiwa vibaya sana na wasioamini. Ikiwa, katika kila jambo, mtu anaweza kuyatetea maslahi ya nyumba ya Mungu anaposhughulikia masuala ya nje, je, mtu huyu ni mtu mzuri? (Ndiyo.) Na kwa hivyo ikiwa mtu wa aina hii hawezi kufanya kazi nyingine yoyote katika nyumba ya Mungu, na anafaa tu kwa aina hii ya kazi ya mambo ya jumla, je, anapaswa kustawishwa na nyumba ya Mungu? (Ndiyo.) Mbali na kuwa na uwezo wa kufanya kazi, na kuweza kutekeleza kazi yake kulingana na kanuni zinazohitajika na nyumba ya Mungu, pia anaweza kutetea maslahi ya nyumba ya Mungu, kwa hivyo anafikia kiwango kinachohitajika, na watu kama hao wanapaswa kustawishwa. Kwa upande mwingine, wale wanaosababisha madhara kwa maslahi ya nyumba ya Mungu kila mara, ambao huhatarisha usalama wa akina ndugu kila mara, na ambao husababisha athari na matokeo mabaya kila mara kwa sifa ya nyumba ya Mungu na kanisa—watu kama hao hawapaswi kustawishwa au kukuzwa; ikiwa watastawishwa na kutumiwa, lazima watimuliwe haraka. Pia kuna baadhi ya watu ambao hujikuta matatani kila wakati wakifanya kazi zao, kama vile kupata ajali wanapoendesha gari, kuharibu mambo wanayoshughulikia, au kuleta migogoro inayosababisha malalamiko ya mara kwa mara, na ikiwa kuna dosari zozote hawajui jinsi ya kuzirekebisha. Watu kama hao ni punguani, na pia wao na waletaji wa bahati mbaya, na ni wafujaji. Mtu wa aina hii akiwa kiongozi wa timu, msimamizi, kiongozi au mfanyakazi, mbali na kutimuliwa haraka, ni lazima pia afukuzwe kanisani. Hii ni kwa sababu mtu wa aina hii ni kichocheo cha maafa na mleta bahati mbaya. Mradi tu kuna mtu mmoja au wawili wa kama hawa kanisani, hakuwezi kuwa na amani kanisani. Watu kama hao wanaonekana kuwa na roho mbaya ndani yao, au kuwa na tauni. Yeyote anayekutana nao atapatwa na balaa, kwa hivyo mtu wa aina hii anapaswa kung’olewa bila kuchelewa. Hata sifa za nyuso za watu hawa wote huwa mbaya, zimejaa ujanja au sifa za kishetani au sura mbaya sana, na yeyote anayekutana nao atahisi kana kwamba kitu kibaya kiko karibu kutokea. Watu wa aina hii lazima watimuliwe na kufukuzwa, na hapo ndipo mambo yanapoiendea vizuri kanisa. Kuwakuza na kuwastawisha watu mbalimbali kanisani kunahitaji kufuata kanuni na utambuzi, ili kutenda kulingana na kanuni. Miongoni mwa aina mbalimbali za watu wanaostawishwa na kukuzwa, kuna wale wanaohudumu kama viongozi na wafanyakazi wa kanisa, wale wanaowajibika kwa taaluma mbalimbali kanisani, na pia wale wanaoshughulikia mambo ya jumla ya kanisa. Vigezo mbalimbali ambavyo aina hizi kadhaa za watu wenye talanta wanapaswa kufikia pia vimefanyiwa ushirika waziwazi. Unapokuwa wazi kuhusu kanuni za jinsi ya kuchagua viongozi na wafanyakazi na jinsi ya kuwastawisha na kuwakuza watu, basi kazi yote ya kanisa itaingia kwenye njia sahihi.

Watu wengine wanaweza kuuliza, “Kwa nini watu hawa wanaostawishwa na kukuzwa na nyumba ya Mungu wanaitwa wenye talanta?” Watu wenye talanta tunaowazungumzia hurejelea wagombeaji wa ustawishwaji na ukuzwaji. Kuna mahitaji tofauti kwa watu ambao wanaweza kufanya kazi tofauti, na kwa sababu wako katika mchakato wa kukuzwa na kustawishwa, kwa hiyo inatosha kabisa kwamba hawa wanaoitwa watu wenye talanta wanaweza kufikia vigezo hivyo tulivyotaja. Lingekuwa jambo lisilo la busara kutarajia watu hawa wawe wana uhalisi wa ukweli tayari, wawe tayari watiifu na waaminifu, na wawe tayari wanamcha Mungu. Kwa hivyo, watu wenye talanta tunaozungumza juu yao ni wale tu ambao wana baadhi ya sifa na uadilifu ambao watu wenye ubinadamu wa kawaida wanapaswa kuwa nao, na ubora wa tabi ya kuelewa ukweli—kwa hivyo wanachukuliwa kuwa walio na sifa. Haimaanishi kwamba tayari wameelewa ukweli na kuingia katika uhalisi wa ukweli, wala haimaanishi kwamba tayari wamefikia utii kamili kwa Mungu baada ya kukubali hukumu na kuadibu Kwake, na mambo kama haya. Bila shaka, neno “watu wenye talanta” halirejelei wale ambao wamehudhuria chuo kikuu au kufuatilia kuhitimu Ph.D., au watu walio na malezi bora ya familia au hali ya juu ya kijamii, au watu wenye uwezo au vipawa maalum—halirejelei watu hawa. Kwa kuwa wanapaswa kustawishwa na kukuzwa, baadhi ya watu wanaokwenda kufanya kazi za kitaalamu wanaweza kuwa hawajawahi kufanya kazi hiyo au kuisomea hapo awali, lakini Mradi wanafikia vigezo hivyo kadhaa vya kustawishwa na kukuzwa, na wako tayari kujifunza na ni wazuri wa kujifunza taaluma fulani, basi nyumba ya Mungu inaweza kuwastawisha na kuwakuza. Ninamaanisha nini kusema hili? Simaanishi kwamba mtu anaweza kustawishwa na kukuzwa ikiwa tu kwa kawaida anafanya vyema katika taaluma fulani. Badala yake, ni kwamba, ikiwa ana mwelekeo wa kujifunza na anayo masharti ya msingi, au hata ikiwa ana mambo fulani ya misingi katika taaluma hii, basi anaweza kukuzwa na kustawishwa—hii ndiyo kanuni. Huu ndio mwisho wa ushirika wetu juu ya vigezo vinavyopaswa kufikiwa na watu mbalimbali wenye talanta ambao nyumba ya Mungu inataka kukuza na kustawisha.

Malengo ya Nyumba ya Mungu katika Kukuza na Kustawisha Watu wa Kila Aina Wenye Talanta

Kisha tutashiriki kuhusu kwa nini nyumba ya Mungu inakuza na kustawisha kila aina ya watu wenye talanta. Baadhi ya watu hawaelewi hili kabisa, na huwaza, “Je, haitatosha tu kwa nyumba ya Mungu kuchukua hatua moja kwa moja na kuwakuza na kuwatumia watu mbalimbali wenye talanta? Kwa nini inahitaji kuwakuza na kuwafundisha kwa kipindi cha muda?” Je, mnaelewa hili au hamwelewi? Hebu kwanza tuzungumze kuhusu aina ya watu ambao wanakuwa viongozi na wafanyakazi. Kwa nini nyumba ya Mungu inawakuza na kusitawisha wale walio na uwezo wa ufahamu, wanaobeba mzigo kwa ajili ya kanisa, na ambao wana uwezo wa kufanya kazi? Ni kwa sababu ingawa wamehitimu kulingana na kiwango chao na kufikia vigezo, bado hawajapata uzoefu halisi na hawaelewi ukweli, sembuse kujua jinsi ya kutenda ukweli na kufanya mambo kulingana na kanuni. Ni lazima wafundishwe kwa muda na kupewa mwongozo, na ni pale tu wanapokuwa wamefahamu kanuni za kufanya wajibu wao na kuwa na uzoefu wa kweli ndipo wanaweza kutumika rasmi. Kama wangekuwa kama akina ndugu kanisani, wakila na kunywa maneno ya Mungu, wakisikiliza mahubiri, wakiishi maisha ya kanisa, na kufundishwa kufanya wajibu, na wangekuzwa na kustawishwa tu baada ya maisha yao kukua, basi maendeleo yao yangekuwa ya polepole sana. Katika hali hiyo, ingechukua miaka mingapi kwao kufaa kwa matumizi ya Mungu? Je, hii haitaathiri kazi ya kanisa? Kwa hivyo, mradi mtu ana uwezo wa kuelewa ukweli, ana uwezo wa kufanya kazi, na ana hisia ya kubeba mzigo, anapaswa kustawishwa na kukuzwa na kutakiwa kujifundisha katika kutekeleza wajibu wa kiongozi au mfanyakazi, na kupewa mzigo. Kwa upande mmoja, inawafanya watumie uwezo wao kikamilifu. Kwa upande mwingine, wanapokumbana na hali maalum, ni muhimu kushiriki nao juu ya ukweli ili kutatua matatizo yao. Wakati mwingine lazima pia wapogolewe, na ikilazimu, lazima pia waafundishwe nidhamu na wapitie majaribu mengi na usafishaji, na wastahimili mateso mengi. Ni kwa kupitia mafundisho hayo ya vitendo tu ndiyo wanaweza kufanya maendeleo ya kweli, na hatua kwa hatua waelewe ukweli na kushika kanuni, na kisha wajitwike kazi ya viongozi na wafanyakazi haraka iwezekanavyo. Kuwakuza na kuwafundisha viongozi na wafanyakazi kwa njia hii kutaleta matokeo bora na ukuaji wa haraka zaidi, jambo ambalo ni la manufaa zaidi kwa kazi ya nyumba ya Mungu na manufaa zaidi kwa kuingia katika uzima kwa watu wateule wa Mungu, kwa sababu viongozi na wafanyakazi wenye uzoefu wa vitendo wanaweza kuwanyunyizia na kuwakimu watu wateule wa Mungu moja kwa moja. Nyumba ya Mungu inapomkuza na kumsitawisha mtu kuwa kiongozi, inampa mzigo zaidi wa kumfundisha, kumfanya amtegemee Mungu, na kumfanya ajitahidi kuelekea ukweli; ni hapo tu ndipo kimo chake kitakua haraka iwezekanavyo. Kadiri mzigo unaowekwa juu yake unavyokuwa mkubwa, ndivyo anavyowekewa shinikizo zaidi, na ndivyo anavyolazimika kutafuta ukweli na kumtegemea Mungu zaidi. Hatimaye, ataweza kufanya kazi yake ipasavyo na kufuata mapenzi ya Mungu, na hivyo atakuwa ameanza kuitembea njia sahihi ya kuokolewa na kukamilishwa—haya ndiyo matokeo yanayopatikana wakati nyumba ya Mungu inapowakuza na kuwastawisha watu. Bila kufanya kazi hizi mahususi, hawangejua kile wanachopungukiwa nacho, hawangejua jinsi ya kufanya mambo kulingana na kanuni, na hawangejua maana ya kuwa na uhalisi wa ukweli. Kwa hiyo kufanya kazi maalum huwasaidia kugundua mapungufu yao na kuona kwamba, mbali na vipaji vyao, hawana uhalisi wa ukweli; inawasaidia kuhisi jinsi walivyo duni na wenye kusikitisha, na kuwafanya watambue kwamba wasipomtegemea Mungu na kutafuta ukweli, hawatakuwa na uwezo wa kufanya kazi yoyote; inawafanya wajijue wenyewe na kuona waziwazi kwamba ikiwa hawatafuatilia ukweli na mabadiliko ya tabia, haitawezekana kwao kufaa kwa matumizi ya Mungu. Haya yote ni matokeo yanayopaswa kupatikana wakati viongozi na wafanyakazi wanapostawishwa na kukuzwa. Ni kwa kuelewa vipengele hivi pekee ndiyo watu wanaweza kufuatilia ukweli wakiwa na uthabiti, kujiendesha kwa namna ambayo si ya kujionyesha, kuhakikishiwa kutojisifu tena wakati wa kufanya kazi yao, kumtukuza Mungu mfululizo na kushuhudia kwa Mungu katika kutekeleza wajibu wao, na kuingia hatua kwa hatua katika uhalisi wa ukweli. Wakati mtu anapostawishwa na kukuzwa kuwa kiongozi, anawezeshwa kujifunza jinsi ya kutambua hali za watu tofauti, kujifunza kutafuta ukweli ili kutatua matatizo ya watu mbalimbali, na kuwasaidia na kuwakimu watu wa aina tofauti, na kuwaongoza watu kuingia katika uhalisi wa ukweli. Wakati huo huo, lazima pia wajifundishe kutatua shida na matatizo mbalimbali yanayowakabili wakati wa kazi, na kujifundisha jinsi ya kutofautisha na kukabiliana na aina mbalimbali za wapinga Kristo, watu waovu, na wasioamini, na jinsi ya kufanya kazi ya kulitakasa kanisa. Kwa njia hii, ikilinganishwa na wengine, wanaweza kupitia watu, matukio, na mambo zaidi, na mazingira zaidi yaliyowekwa na Mungu, wanaweza kula na kunywa maneno ya Mungu zaidi na zaidi, na kuingia katika uhalisi zaidi wa ukweli. Hii ni fursa ya kujifunza, siyo? Kadiri fursa za mafunzo zinavyoongezeka, ndivyo uzoefu wa watu unavyokuwa mwingi zaidi, ndivyo ufahamu wao unavyoongezeka, na ndivyo watakavyokua haraka zaidi. Hata hivyo, watu wasipofanya kazi ya uongozi, kile wanachokutana nacho na kupitia kitakuwa tu sehemu ya maisha yao ya kibinafsi na uzoefu wao wa kibinafsi, na kile wanachotambua kitakuwa tu tabia zao potovu za kibinafsi na hali mbalimbali za kibinafsi—yote yanawahusu wao wenyewe tu. Mara tu wanapokuwa viongozi, wanakutana na watu wengi zaidi, matukio zaidi, na mazingira zaidi, ambayo yanawatia moyo mara nyingi kuja mbele za Mungu kutafuta kanuni za ukweli. Kwao, watu, matukio, na mambo haya yanajumuisha mzigo kwa njia isiyoonekana, na kwa kawaida pia huunda hali nzuri sana kwa kuingia kwao katika uhalisi wa ukweli, ambalo ni jambo zuri. Na kwa hivyo, mtu ambaye ana ubora wa tabia wa kawaida, anabeba mzigo, na ana uwezo wa kufanya kazi ataingia polepole kama muumini wa kawaida, na haraka kama kiongozi au mfanyakazi. Je, kwa watu, ni jambo zuri kuingia katika uhalisi wa ukweli haraka, au polepole? (Haraka.) Kwa hivyo, inapokuja kwa watu walio na ubora wa tabia, kubeba mzigo, na uwezo wa kufanya kazi, nyumba ya Mungu huacha ukawaida kwa kuwakuza watu kama hao, isipokuwa kama wao si watu wanaofuatilia ukweli na hawajitahidi kuelekea ukweli, na ikiwa hivyo, nyumba ya Mungu haitawalazimisha. Mradi mtu ana msingi wa imani katika Mungu, anafikia vigezo vya kuwa kiongozi au mfanyakazi, na yuko tayari kufuatilia ukweli na kutumiwa na Mungu, basi hakuna shaka kwamba nyumba ya Mungu itamkuza na kumstawisha, kumpa fursa ya kujifundisha kuwa kiongozi au mfanyakazi, na kumwezesha kujifundisha kufanya kazi ya kanisa, na kujifunza kuwatambua watu, na kujifunza kushughulikia matatizo yote mbalimbali kanisani, na kujifunza kutekeleza kazi mbalimbali kulingana na mipango ya kazi. Katika kipindi cha kufundishwa, ikiwa watu wanaweza kuukubali ukweli na kukubali kupogolewa, wanaweza kutii utaratibu na mipango ya Mungu, wanaweza kutafuta ukweli ili kutatua matatizo mbalimbali, na kujifunza kuwatendea watu wa kila aina na kutofautisha na kushughulika na kila aina ya watu kulingana na maneno ya Mungu, basi wanaweza kushika kanuni za ukweli husika, na kuja kuelewa ukweli na kuingia katika uhalisi—haya ni mbambo ambayo waumini wa kawaida hawawezi kupitia au kupata. Kwa hivyo kwa mtazamo huu, je, ni jambo jema au baya kwa nyumba ya Mungu kumkuza na kumstawisha mtu fulani? Je, ni lenye manufaa kwake, au ni taabu anayolazimishiwa? Ni lenye manufaa kwake. Bila shaka, wakati baadhi ya watu wamestawishwa, hawajui ni kazi gani wanayopaswa kufanya au jinsi ya kuifanya, na wanachanganyikiwa kidogo. Hii ni kawaida; ni nani aliyezaliwa na uwezo wa kufanya kila kitu? Ikiwa ungeweza kufanya kila kitu, bila shaka ungekuwa mtu mwenye kiburi na majivuno zaidi, na hungejishusha kwa mtu yeyote—ikiwa hivi, je, bado unaweza kukubali ukweli? Ungeweza kufanya kila kitu, je, bado ungemtegemea Mungu na kumtazamia Yeye? Je, bado ungetafuta ukweli ili kutatua matatizo ya upotovu wako mwenyewe? Hakika hungefanya. Kinyume chake, ungekuwa na kiburi na majivuno na kutembea katika njia ya wapinga Kristo, ungepigania mamlaka na hadhi na kutojishusha kwa yeyote, na ungewapotosha na kuwatega watu, na kuvuruga na kuisumbua kazi ya kanisa—na ikiwa hivi, je, bado ungeweza kutumiwa na nyumba ya Mungu? Ikiwa wewe unajua kwamba una mapungufu mengi, unapaswa kujifunza kutii na kunyenyekea, na kufanya kazi mbalimbali vyema kulingana na mahitaji ya nyumba ya Mungu; hatua kwa hatua hii itakuruhusu ufikie nafasi ambayo unaweza kufanya wajibu wako kwa njia ambayo ni ya kiwango kinachohitajika. Lakini watu wengi hawawezi kufanya jambo rahisi kama kutii na kunyenyekea, kwa hivyo hawapaswi kuilaumu nyumba ya Mungu kwa kutowakuza na kuwastawisha. Kwa kuwa huwezi kutii, kwa kuwa hata kutii ni kitu kinachokuzidi, je, nyumba ya Mungu ingethubutu kukustawisha na kukukuza? (Hapana.) Na kwa nini isiwe hivyo? Kukutumia itakuwa hatari sana, shida nyingi, wasiwasi mwingi! Kwa sababu ikiwa nyumba ya Mungu itawahi kukutumia, unaweza kuchukua udhibiti juu ya watu, na uwaongoza kwenye njia ya uovu—ndiyo maana ni hatari sana. Wewe ukitumiwa, unaweza kufanya maovu bila kujali na kuiweka kazi katika hali ya kuchanganyikiwa, na nyumba ya Mungu ingelazimika kukutimia na kukuondoa—ndiyo maana ni shida sana. Na kama ungetumiwa, hungejua jinsi ya kufanya kazi yoyote, na hungeleta matokeo yoyote katika suala la kazi yako; katika kazi zote unazofanya, ungepaswa kuhimizwa, kusimamiwa, na kufuatiliwa na Aliye juu, ambaye Angepaswa kuingilia kati katika masuala yote—kwa hivyo kwa nini wewe utumike? Unaleta wasiwasi mwingi sana! Mtu wa aina hii hawezi kabisa kutumika. Hata kama angestawishwa, isingekuwa na faida yoyote, na hata ingesababisha shida nyingi na pia kuleta athari katika ustawishaji wa wengine; faida si zingezidiwa na hasara? (Ndiyo.)

Watu wengine, kwa sababu hawajakuzwa au kutumiwa na nyumba ya Mungu, wanapata mawazo kichwani mwao na kusema, “Kwa nini Aliye juu hanitambui? Kwa nini nyumba ya Mungu hainistaiwishi na kunikuza? Hii si haki!” Naam, unapaswa kwanza kupima ikiwa unaweza kutii, na kama unaweza kutii mipango ya nyumba ya Mungu. Pili, unapaswa kupima ikiwa unatimiza vigezo vitatu vinavyohitajika ili nyumba ya Mungu iwakuze na kuwastawisha watu wawe viongozi na wafanyakazi—kuwa na uwezo wa kufahamu ukweli, kubeba mzigo, na kuwa na uwezo wa kufanya kazi. Ikiwa unafikia vigezo hivi, basi hivi karibuni utapata fursa ya kukuzwa, kustawishwa na kutumiwa. Ili nyumba ya Mungu ikukuze, kuna mambo ambayo yanahitajika kutoka kwako. Na mambo haya ni yapi? Wewe unatakiwa kutenda kulingana na kanuni na mahitaji ya nyumba ya Mungu; lazima ufanye yale yanayohitajika kutoka kwako, na kwa namna ambayo imehitajika, na hivyo kukusitawisha ili ujifunze kwanza kutenda kwa njia ya kanuni, na ujifunze kutafuta ukweli na kuutii ukweli, na kujifunza kushirikiana kwa upatanifu. Wakati ambapo unastawishwa, nyakati fulani nyumba ya Mungu itakupogoa; wakati mwingine itakukemea vikali; wakati mwingine itauliza kuhusu maendeleo ya kazi yako; wakati mwingine itakuuliza jinsi kazi inavyoendelea hasa, na itaangalia kazi yako; na wakati mwingine, itajaribu maoni yako kuhusu jambo fulani ni yapi. Lengo la majaribio haya si kufanya mambo yawe magumu kwako, lakini kukufanya uelewe, katika masuala haya, nia za Mungu ni ipi, na ni mtazamo na kanuni gani unazopaswa kuwa nazo. Nyumba ya Mungu hufanya hivi ili kukufundisha na kukufanya utende. Na lengo na dhumuni la kuwafundisha watu ni lipi? Ni kuwawezesha waelewe ukweli. Lengo la kuelewa ukweli ni kwa watu kuweza kutii ukweli na kutenda kulingana na kanuni, kuweka nafasi yao na kutimiza wajibu wao kwa uaminifu, na, katika mchakato wa kufanya wajibu wao, waingie katika uhalisi tofauti wa ukweli na kufikia mabadiliko katika tabia zao. Nyumba ya Mungu huwafundisha viongozi na wafanyakazi kwa njia hii. Mradi viongozi na wafanyakazi wanaelewa ukweli, kuna tumaini la wao kuwa na uwezo wa kuwaongoza watu wateule wa Mungu kuelewa ukweli. Licha ya ukweli mwingi ambao viongozi na wafanyikazi wanaelewa, hivyo ndivyo ukweli mwingi ambao watu wanaowaongoza wana matumaini ya kuelewa. Viongozi na wafanyakazi wanaposhika kanuni za ukweli katika kazi zao, wale wanaoongozwa nao wanaweza pia kufahamu kanuni na kuingia katika uhalisi wa ukweli katika kazi yao. Kwa hivyo, viongozi na wafanyikazi wanaopitia mafunzo lazima wawe na ubora mzuri wa tabia kuliko watu wengine. Wanawezeshwa kuelewa kanuni za ukweli kwanza na kuingia katika uhalisi wa ukweli kwanza, na kisha wanawaongoza watu zaidi katika kuingia uhalisi wa ukweli na kuelewa kanuni za ukweli. Mnaonaje kuhusu mbinu kama hiyo? (Ni nzuri.) Huenda watu kama hao wasiwe na elimu ya kutosha au wasiseme sana, au hawaelewi mengi kuhusu teknolojia au mambo ya sasa na siasa. Huenda hata wasiwe na ujuzi mwingi katika taaluma fulani. Lakini wanaweza kuelewa ukweli, na baada ya kusikia maneno ya Mungu, wanaweza kuyatenda na kuyapitia, na kuweza kupata kanuni za ukweli, na kuweza kuwaongoza watu wengi zaidi kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu na kutii kanuni za ukweli. Hawa ndio tunamaanisha tunapozungumzia aina ya watu wenye talanta wanastawishwa na kukuzwa ili kutumika kama viongozi. Je, hii ni dhahania? (Hapana, siyo.) Huenda baadhi ya watu wakauliza: “Unazungumza kuhusu watu wenye talanta, kwa hiyo wao ni watu bora katika jamii? Je, ni lazima wawe wameendesha aina fulani ya biashara, au wamekuwa wakurugenzi wa aina fulani au wajasiriamali katika jamii? Je, ni wakuu wa serikali walio na historia ya kisiasa, au talanta za biashara, au vipaji katika duru za kisanii na fasihi? Je, ni watu wenye talanta za kipekee?” Watu wenye talanta wanaozungumziwa katika nyumba ya Mungu ni tofauti na wale watu wenye talanta walioko ulimwenguni. Ni nini maana ya kauli hii “watu wenye talanta” tunayoizungumzia? Inamaanisha kuwa na uwezo wa kuelewa ukweli, na kuwa na uwezo wa kuwaongoza watu katika uhalisi wa ukweli, na kujua jinsi ya kutambua aina mbalimbali za watu, na jinsi ya kutatua hali mbalimbali na matatizo ambayo watu wanajikuta katika, na kuwa na maoni na mitazamo sahihi wanapokumbana na masuala, na kuwa na maoni na mitazamo ambayo watu wanaomwamini Mungu na kumfuata wanapaswa kuwa nayo. Hairejelei watu ambao hawana ufahamu wa kiroho, au kwa watu wanafiki, au watu wanaosema maneno ya juu na maneno matupu. Badala yake, inarejelea watu ambao wana uhalisi wa ukweli. Hii ndiyo maana ya “watu wenye talanta”. Je, huu ni uongo? (Hapana.) Je, si vigezo hivi ambavyo nyumba ya Mungu inahitaji kutoka kwa aina hii ya watu wenye talanta ambayo inawakuza na kuwastawisha ili wawe viongozi na wafanyakazi wa vitendo sana? (Ndiyo.) Ni vya vitendo sana! Wagombea kama hao hawahitajiki wawe na sifa za juu za kitaaluma, lakini lazima angalau wawe na ubora wa tabia ya kuelewa ukweli. Baadhi ya watu wanaweza kusema: “Ikiwa hawatakiwi kuwa na sifa za juu za kitaaluma, je, ni sawa kwao kutojua kusoma na kuandika?” Kusoma maneno ya Mungu haingewezekana bila elimu fulani. Wanahitaji kuelewa neno lililoandikwa, lakini hawahitaji sifa za juu za kitaaluma. Wale wanaostawishwa katika nyumba ya Mungu ni pamoja na wahitimu wa shule ya upili, wahitimu wa chuo kikuu, na wahitimu wa Ph.D., kwa hivyo hakuna mipaka katika suala la kiwango cha elimu. Kwa kuongeza, hakuna mipaka juu ya hali ya kijamii ya mtu pia. Kuanzia wakulima na wasomi, wafanyabiashara na akina mama wa nyumbani—watu wa kila aina wanakaribishwa. Kando na kutokuwa na vizuizi katika kiwango cha elimu na hadhi ya kijamii, vigezo vinavyohitajika ni vile kadhaa ambavyo nilizungumza. Je, hilo ni la busara? (Ndiyo.) Ni la busara sana! Sasa, je, mnaelewa kidogo zaidi Ninachomaanisha kwa kusema “watu wenye talanta ambao nyumba ya Mungu inawakuza na kuwastawisha”? (Ndiyo.) Watu wanaoridhisha vigezo hivi kadhaa vya kuweza kufahamu ukweli, kubeba mzigo, na kuwa na uwezo wa kufanya kazi ni wagombea wa kukuzwa na kustawishwa na nyumba ya Mungu. Ikiwa wanaridhisha vigezo hivi, wana sifa. Kuhusu mambo mengine kama vile elimu, maisha ya nyuma ya familia, hali ya kijamii, mwonekano wa mtu, na kadhalika, mahitaji si ya juu sana. Hili linahusu kuwakuza na kuwastawisha watu kuwa viongozi na wafanyikazi.

Tumeshiriki tu hivi punde juu ya vigezo kadhaa ambavyo watu wenye talanta walio na ujuzi au taaluma wanapaswa kutimiza ili waendelezwe na kukuzwa, ambavyo ni kwamba wanapaswa kupenda vitu chanya na kuweza kukubali ukweli, wasipotoke katika uelewa wao, waweze kutekeleza wajibu wao kwa uaminifu, wapitie ugumu na kulipa gharama bila kulalamika, na angalau wasitende maovu—vigezo hivi kadhaa ni muhimu kwa watu hawa. Basi lengo la kuwaendeleza na kuwakuza watu hawa ni lipi? Vivyo hivyo, ni ili watu hawa wanapokumbana na matatizo wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao na kufanya kazi maalum, waweze kutafuta ukweli ili kutatua matatizo hayo, na kutenda kulingana na kanuni. Katika mchakato wa kutenda uingiaji, wao hufunzwa na kudhibitiwa bila wao kujua, na hufanya mazoezi ya kuachilia nia zao wenyewe, wakirekebisha mitazamo yao isiyo sahihi na ya kipuuzi ya watu wa dunia, wakiachilia baadhi ya mawazo ya kitoto, na wakiachilia maoni ya upendeleo, mawazo, na dhana kuhusu imani katika Mungu, na mambo kama hayo. Bila shaka, bila kujali chochote, mchakato huu wa kufanya mazoezi unakusudiwa kuwawezesha watu kuelewa ukweli hatua kwa hatua, kujifunza kutii, na kujifunza kuingia katika uhalisi mbalimbali wa ukweli. Katika mchakato wa kujifunza, wao hushika kanuni za ukweli hatua kwa hatua, na kujua maana ya kumwamini Mungu, na maana ya kutenda ukweli, na maana ya kutekeleza wajibu wa mtu, na hatimaye, wao huelewa kile wanachopaswa kufanya hatua kwa hatua ili kutekeleza wajibu wao kwa njia inayofikia kiwango kinachostahili, jinsi wanavyopaswa kufanya mambo jinsi muumini anavyopaswa kufanya, na kadhalika—haya yote ni mambo ambayo watu huingia ndani yake hatua kwa hatua baada ya kuendelezwa na kukuzwa. Mchakato wa watu kuingia hatua kwa hatua ndio mchakato wa kukuzwa, na mchakato wa kukuzwa kwa kweli ndio mchakato wa watu kutenda kuingia katika uhalisi wa ukweli. Lakini kama hujaendelezwa na kukuzwa, na wewe unatenda tu kama muumini wa kawaida anayehudhuria mikutano, anayesoma maneno ya Mungu, anayeshiriki kuhusu ukweli, au anayejifunza nyimbo za sifa, kwa kumwamini Mungu kwa njia hii wewe hutimizi wajibu wako kweli kama kiumbe aliyeumbwa, kwa hivyo uko mbali sana na utekelezaji wa wajibu wako kwa njia inayofikia kiwango kinachostahili. Huelewi hata ni kanuni zipi unazopaswa kushika katika kutekeleza wajibu wako, na unaweza tu kusema mafundisho na kauli mbiu fulani; kwa hivyo, bado hujaingia katika uhalisi wa ukweli, na kuingia kwako katika uzima ni polepole. Vile vile, lengo na dhumuni la kuwaendeleza na kuwakuza watu hawa wanaojihusisha na kazi za kitaaluma ni ili waingie katika uhalisi wa ukweli haraka zaidi na wapate ufahamu bora na sahihi zaidi wa kanuni za ukweli. Wale wanaoweza kushika kanuni za ukweli na kuingia katika uhalisi wa ukweli—hawa ndio watu wenye talanta wanaoendelezwa na kukuzwa na nyumba ya Mungu. Kauli watu wa aina hii wenye talanta nini? Inamaanisha wale ambao—kwa msingi wa kupenda vitu chanya, na kuweza kuvumilia ugumu na kulipa gharama, na uelewa wao usiwe na potovu, na wasiwe watu waovu—wamefikia uelewa wa kanuni za ukweli na wameingia katika uhalisi wa ukweli, na wanaweza kumtii Mungu na mipango ya nyumba ya Mungu, na wana moyo umchao Mungu kiasi. Hii ndiyo aina ya pili ya watu wenye talanta Ninaowazungumzia. Mahitaji kwao pia ni ya vitendo, mahususi vya kutosha, na si ya kufikirika. Basi, je, watu wa aina hii wenye talanta wanahitajika kuwa watu bora katika jamii, na wenye uzoefu wa kijamii, na wawe na sifa fulani za kitaaluma, na hadhi fulani ya kijamii? (Hapana.) Nyumba ya Mungu kamwe haiwahitaji watu wawe na hadhi ya kijamii, umaarufu, sifa za kitaaluma au kiwango cha juu cha maarifa—mambo haya hayahitajiki kamwe. Inapowaendeleza na kuwakuza watu, nyumba ya Mungu haiangalii sura zao, yaani, jinsi walivyo wabaya au wanavyopedeza. Mbali na kutowaendeleza watu wa aina inayoonekana kama wasioamini, au walio na sura mbovu au waovu, vigezo vingine ni vile Nilivyotaja hivi punde—hivi ndivyo vya vitendo zaidi. Wasioamini wanapomwendeleza mtu, kwanza wao huangalia sura ya mtu huyo; wanaume wanapaswa kuwa wenye sura nzuri, kama maafisa, na wanawake wanapaswa kuwa wa kupendeza, kama malaika. Zaidi ya hayo, wao pia hulinganisha sifa za kitaaluma za watu, hadhi ya kijamii, asili ya familia, na hila. Ikiwa una sifa za juu za kitaaluma lakini huna ustadi, hilo halitafaa pia, hutaendelezwa kamwe na hakuna mtu atakayekuchukulia kwa heshima. Ikiwa una sifa za juu za kitaaluma na talanta halisi, lakini huna sura nzuri hasa, na wewe ni mfupi, na hujui jinsi ya kujipendekeza kwao au kuwakaribia wakuu wako, basi hutaendelezwa au kukuzwa kamwe maishani mwako, na hakuna mtu atakayekugundua. Kwa hivyo, wasioamini wana msemo huu unaosema, “Kuna farasi wengi wenye kasi, lakini kuna wachache wanaoweza kuwatambua.” Je, hili lina ukweli katika nyumba ya Mungu? (Hapana, halina.) Basi, je, usemi “Dhahabu ya kweli hatimaye itang’aa tu” una ukweli? Je, unafaa? (Hapana.) Watu wenye dharau na wasiokubali kushindwa na yeyote mara nyingi husema hivi. Kutaka kung’aa kila wakati—haya ni matamanio makuu ya binadamu. Aina mbalimbali za watu wenye talanta wanaoendelezwa na kukuzwa na nyumba ya Mungu si dhahabu, wao ni watu wa kawaida tu. Uendelezaji na ukuzaji tunaouzungumzia ni namna tu ya kusema; kwa kweli, hili hurejelea kuinuliwa na Mungu. Je, wewe, kiumbe aliyeumbwa, ni dhahabu mbele ya Muumba? Wewe ni vumbi tu, wewe si hata shaba au chuma. Kwa nini Ninasema kwamba wewe ni vumbi badala ya dhahabu? Hakuna kitu cha kusifiwa kuhusu watu. Wengine wanaweza kuuliza: “Je, kile Ulichosema si kinzani? Si Umesema hivi punde kwamba mtu anaweza kuendelezwa ikiwa anatimiza kigezo cha kupenda vitu chanya?” Kama mwanadamu, je, hupaswi kupenda vitu chanya? Ukipenda vitu vichache chanya, je, hilo linakufanya uwe dhahabu? Je, hilo linakufanya ung’ae? Ukipenda vitu vichache chanya, je, inamaanisha kwamba una ukweli? Ni kwa kuwa na ukweli tu ndiyo mtu hung’aa. Ikiwa huna ukweli, inawezaje kusemwa kwamba unang’aa? Ukweli ni kwamba kiumbe aliyeumbwa haelewi ukweli wowote. Kuwa na ubinadamu kiasi, na uwezo na ubora wa tabia kiasi wa kuelewa ukweli haimaanishi kwamba mtu anao ukweli kiasili. Watu hawana ukweli, na hata kama ubinadamu wao ni mnyofu au mwema, mambo haya si ukweli, ni sifa tu ambazo ubinadamu wa kawaida unapaswa kuwa nazo. Kwa hivyo, msizungumzie kung’aa. Basi, mtu anaweza kung’aa kidogo wakati gani? Wakati anapoweza kusema maneno ya Ayubu, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe” (Ayubu 1:21), hapo ndipo anaweza kusemwa kuwa anang’aa kidogo na anaishi katika nuru. Unapoweza kutumia uhalisi wa ukweli ulio nao na ukweli unaouelewa ili kuwapa riziki, kuwategemeza, na kuwaongoza wengine, kupitia katika haya wanaweza kuletwa mbele za Mungu na katika uhalisi wa ukweli, kumtii Mungu na kumwabudu Mungu, ni hapo tu ndipo unaweza kung’aa kidogo.

Aina mbalimbali za watu wenye talanta wanaokuzwa na nyumba ya Mungu hawana vipaji vya kimwujiza, wao ni watu wa kawaida tu, watu waliopotoka. Maadamu wanaweza kukubali ukweli, kutii na kujiweka chini, na wana ubora fulani wa tabia, basi nyumba ya Mungu itawapa fursa isiyo ya kawaida kwa kuwaendeleza na kuwakuza. Ninapozungumza kuhusu kutoa fursa isiyo ya kawaida ya kuwaendeleza na kuwakuza watu, huku ni kuinuliwa na Mungu, ni kuhusu kukupa fursa ya kuja mbele za Mungu na kukubali uongozi wa Mungu, na kukubali Mungu Akukuze na kukufundisha, ili kwamba katika kipindi hiki uweze kuingia katika uhalisi wa ukweli haraka iwezekanavyo na uweze kushika kanuni za ukweli kwa usahihi, kutekeleza wajibu wako kwa njia inayofikia kiwango kinachostahili, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu. Hii ndiyo maana ya kauli “watu wenye talanta” katika nyumba ya Mungu. Watu kama hao si wakuu na wa kuvutia hata kidogo, wanaelewa tu ukweli na wana uhalisi wa ukweli, na wanaweza kutekeleza wajibu wao kwa makini na kwa uwajibikaji, na wana unyoofu kiasi na wanaweza kulipa gharama kiasi, na hawatendi ovyoovyo kwa kuzingatia mawazo na dhana zao. Kwa kutoa fursa isiyo ya kawaida ya kuwaendeleza na kuwakuza watu wanaoweza kutimiza vigezo hivi, na kuwafundisha, je, inafaa kwa nyumba ya Mungu kufanya hivi? Je, kuna faida kwa watu? Kuna faida kubwa sana kwa watu! Kama tu waumini wengine, wale wanaoendelezwa na kukuzwa humwamini Mungu, na husoma maneno ya Mungu, na husikiliza mahubiri, na hutekeleza wajibu wao, lakini wakilinganishwa na waumini wengine, wao hukua haraka zaidi na kupata mengi zaidi. Je, ninyi mngependa kupata mengi zaidi, au kupata kidogo tu? (Kupata mengi zaidi.) Watu wengi wana hamu hii, jambo linalomaanisha kwamba wanapenda vitu chanya. Wakati mwingine Mimi hufanya ushirika na baadhi ya timu kuhusu kuingia katika uzima, na watu wengi hufuata kusikiliza, jambo linaloonyesha kwamba watu wengi wana shauku ya kutamani ukweli, na wako tayari kuelewa ukweli zaidi, na pia wako tayari kuingia katika uhalisi wa ukweli. Mwanzoni, Nilifanya ushirika na baadhi ya watu na walikuwa baridi kabisa. Nilizungumza kwa muda mrefu lakini hawakuitikia, au hata kuonyesha dalili ndogo kabisa ya tabasamu. Baada ya Mimi kuwa na mawasiliano nao kwa mwaka mmoja au miwili, wengi wao walikuwa wa asili zaidi katika sura zao na waliitikia, na baada ya muda mwitikio wao ukawa wa haraka kiasi. Yaani, waligeuka kutoka kwa watu waliokufa na kuwa watu walio hai, na roho zao zikaamka. Hili lilifikiwaje? Ikiwa watu hawaelewi ukweli, basi haijalishi wanapenda vitu chanya kiasi gani, au jinsi walivyo werevu au wenye akili, bado wao ni watu waliokufa. Watu wengine huanza wakiwa wajinga na wazembe, hakuna mtu duniani anayewaheshimu, na hawajasoma sana na uelewa wao si mpana sana. Lakini baada ya kuanza kumwamini Mungu, wanaweza kuelewa kweli nyingi na kuona mambo mengi waziwazi, na kisha kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu, na hivyo kuwa watu walio hai. “Watu walio hai” inamaanisha nini? Si kuhusu kama mwili wako uko hai au umekufa, au kama mwili wako unaweza kusonga au kupumua, bali ni kama roho yako ina ufahamu na ni sikivu kwa maneno ya Mungu na ukweli. Watu walio hai huitikia ukweli na maneno ya Mungu. Baada ya kusikia maneno ya Mungu, wanakuwa na ufahamu, njia, mpango, na lengo. Watu waliokufa hawana maonyesho haya. Kwa hivyo, ikiwa nyumba ya Mungu inamwendeleza na kumkuza mtu, mtu huyu atapata mengi zaidi kwa ulinganisho. Basi watu wasiotimiza vigezo hivi na wasioendelezwa au kukuzwa wanawezaje kupata vya kutosha? Wanawezaje kuingia haraka katika uhalisi wa ukweli? Ni lazima wajifunze kutenda na kupitia maneno ya Mungu, kufikia uelewa wa kweli nyingi, na pia waweze kutumia ukweli kuwatambua watu na kutatua matatizo—kisha wanaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli.

Watu wengine husema: “Kwa kuwa nyumba ya Mungu huwaendeleza na kuwakuza watu wenye talanta wa kila aina na kuwaruhusu waingie katika uhalisi wa ukweli haraka iwezekanavyo, je, hilo halimaanishi kwamba watu wasio na talanta hawawezi kuingia katika uhalisi wa ukweli?” Je, ni sahihi kusema hivyo? (La, si sahihi.) Basi, baada ya kushiriki juu ya mada hii, je, hilo limewafanya baadhi ya watu wasisimke huku likiwafanya wengine wakate tamaa na kuvunjika moyo? Jambo hili linapaswa kutazamwa hivi: Wale ambao wameendelezwa na kukuzwa hawapaswi kujivuna. Huna cha kujivunia, hii ni neema na baraka ya Mungu. Mungu anapokupa mengi zaidi, Yeye pia hukuomba ujitoe zaidi. Ikiwa nyumba ya Mungu inakupa fursa isiyo ya kawaida kwa kukuendeleza na kukukuza, inamaanisha kwamba unahitaji kulipa gharama kubwa zaidi. Kama unaweza kuvumilia ugumu huu, basi bila shaka utapata mengi zaidi. Ukisema, “Siko tayari kupitia ugumu huu,” basi hutapata ukweli, wala kupata baraka ya Mungu. Watu wengine husema, “Ninataka kupata vitu hivyo lakini sidhani ninaweza, kwa sababu nyumba ya Mungu haitanipa fursa isiyo ya kawaida kwa kuniendeleza na kunikuza. Sifikii vigezo vinavyohitajika.” Haijalishi kama hutimizi vigezo. Maadamu unafuatilia ukweli na kujitahidi sana kuuelekea, Mungu hatakutendea isivyo haki. Watu hawa wanaoendelezwa na kukuzwa wanaweza tu kuingia katika uhalisi wa ukweli mapema zaidi kwa sababu ya ubora wa tabia yao na kwa sababu ya hali zao mbalimbali. Hata hivyo, kuingia huku mapema hakumaanishi kwamba wao pekee ndio wanaoweza kuingia katika uhalisi wa ukweli. Inamaanisha tu kwamba wanaweza kupata mengi zaidi kiasi mapema, na wanaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli mapema kidogo. Wale ambao hawajaendelezwa watabaki nyuma yao kidogo, lakini hii haimaanishi kwamba hawawezi kuingia katika uhalisi wa ukweli. Kama mtu anaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli au la inategemea ufuatiliaji wao. Watu hawa wanaoendelezwa na kukuzwa wanaweza kushika kanuni za ukweli haraka zaidi na kuingia katika uhalisi wa ukweli haraka zaidi wakati wa mchakato wa ukuzaji, jambo ambalo linafaidi kazi ya nyumba ya Mungu. Kwa hivyo, ni sahihi kuwaendeleza na kuwakuza watu wanaopatikana kuwa na ubora mzuri wa tabia na wanaopenda ukweli. Ikiwa mtu anaweza kuwapata watu hawa na kuwaendeleza na kuwakuza bila kuwaonea wivu au kuwashusha, bali badala yake awape utunzaji, basi anaijali nia ya Mungu. Kinyume chake, ikiwa watu wengine wana wivu na wanahofia kwamba watu hawa ni bora kuwaliko wao na watawapita, kwa hivyo wanawatenga na kuwashusha, hili ni tendo ovu waziwazi na kitu ambacho wapinga Kristo hufanya mara nyingi. Ni watu waovu na wapinga Kristo tu wanaoweza kuwapinga na kuwatenga ndugu na dada.

Ufahamu na Mtazamo Ambao Mtu Anapaswa Kuwa Nao Kuhusiana na Ukuzaji na Ustawishaji wa Watu na Nyumba ya Mungu

Tulichoshiriki kuhusu hivi punde ni malengo ya nyumba ya Mungu katika kuwaendeleza na kuwakuza watu wenye talanta wa kila aina. Haijalishi ni kazi ya aina gani ambayo wale wanaochaguliwa kwa ajili ya kuendelezwa na kukuzwa hufanya—iwe ni kazi ya kiufundi, kazi ya kawaida, au shughuli za jumla za kanisa—kwa ufupi, yote ni kwa ajili ya kuwawezesha kuelewa kanuni za ukweli na kuingia katika uhalisi wa ukweli, na ili waweze kutekeleza wajibu wao kwa njia inayofikia kiwango kinachostahili haraka iwezekanavyo ili kuridhisha nia ya Mungu—hili ndilo hitaji la Mungu kwa watu, na bila shaka, ndilo pia linalohitajika kwa ajili ya kazi ya kanisa. Je, sasa mnaelewa umuhimu wa nyumba ya Mungu kuwaendeleza na kuwakuza watu wenye talanta wa kila aina? Je, bado kuna suitafahamu yoyote? (La.) Watu wengine husema, “Sasa kwa kuwa mtu huyu ameendelezwa kuwa kiongozi, na ana hadhi, yeye si mtu wa kawaida tena.” Je, ni sahihi au si sahihi kusema hivi? (Si sahihi.) Wengine wanaweza kusema: “Wale wanaokuwa viongozi wana hadhi, lakini ukiwa kileleni una upweke. Kadiri unavyopanda juu, ndivyo unavyoanguka kwa kishindo!” Je, ni sahihi au si sahihi kusema hivi? Bila shaka si sahihi. Msemo “Kadiri unavyopanda juu, ndivyo unavyoanguka kwa kishindo” unarejelea watu gani? Unarejelea watu wenye tamaa ya makuu na matamanio, unarejelea wapinga Kristo. Wale wanaofuatilia ukweli wanapokuwa viongozi, huko si kupanda juu—ni Mungu anayewapa fursa isiyo ya kawaida kwa kuwainua, na ni baraka ya Mungu inayoweka mzigo huu juu yao na kuwaruhusu wafanye kazi ya uongozi. “Kadiri unavyopanda juu, ndivyo unavyoanguka kwa kishindo” ni hitimisho linalotolewa na wasioamini, na linaeleza matokeo ya wasioamini wanaofuatilia taaluma katika uongozi serikalini. Wasioamini hao hawana utambuzi na hutumia msemo huu kwa watu chanya, jambo ambalo ni kosa kubwa. Wengine wanaweza kusema: “Alizaliwa katika eneo la mashambani, na sasa amekuwa kiongozi wa kanisa—ameinuka kutoka hali ya chini na kuwa mtu wa maana.” Je, ni sahihi au si sahihi kusema hivi? Haya ni maneno ya kishetani ya wasioamini na hayawezi kutumiwa kwa watu wateule wa Mungu. Katika nyumba ya Mungu, Mungu huwabariki wale wanaofuatilia ukweli, wale walio wanyofu, wale walio na moyo mwema, na wale wanaotetea kazi ya nyumba ya Mungu. Punde tu watu hawa wanapoelewa ukweli na kupata kimo kiasi, wataendelezwa kwa ajili ya ukuzaji na utendaji hivi karibuni, ili wachukue mahali pa wale walio viongozi wa uwongo na wapinga Kristo. Katika nyumba ya Mungu, watu chanya ambao wamepitia majaribu na majaribio mengi na ambao wameitetea kazi ya nyumba ya Mungu kila mara ni watu wanaopata idhini ya Mungu, na haingefaa kutumia maneno ya kishetani ya wasioamini kuwaeleza watu hawa. Kwa hivyo, wale ambao daima hutumia maneno ya kishetani ya wasioamini kueleza mambo katika nyumba ya Mungu na kueleza maoni yao wenyewe ni watu wasioelewa ukweli na walio na mitazamo ya kipuuzi kuhusu mambo. Mitazamo yao kuhusu mambo haijabadilika hata kidogo, na bado ni mitazamo ya wasioamini, na wamemwamini Mungu kwa miaka kadhaa na bado hawajapata ukweli wowote, na bado hawawezi kutazama mambo kulingana na maneno ya Mungu—hivyo basi, watu hawa ni wasioamini na watu wa mataifa. Mtu anapoendelezwa kutumika kama kiongozi au mfanyakazi, au anapokuzwa kuwa msimamizi wa aina fulani ya kazi ya kiufundi, hili si lolote ila ni nyumba ya Mungu inayomkabidhi mzigo. Ni agizo, jukumu, na bila shaka, pia ni wajibu maalum, fursa maalum, na ni kuinuliwa kusiko kwa kawaida—hakuna chochote cha kusifiwa kuwahusu. Mtu anapoendelezwa na kukuzwa na nyumba ya Mungu, haimaanishi ana cheo au hadhi maalum katika nyumba ya Mungu, ili aweze kufurahia huduma na upendeleo maalum. Badala yake, baada ya kuinuliwa kwa namna isiyo ya kawaida na nyumba ya Mungu, anapewa mazingira bora ya kupokea mafunzo kutoka kwa nyumba ya Mungu, kufanya mazoezi ya kufanya kazi fulani muhimu ya kanisa, na wakati huo huo nyumba ya Mungu itakuwa na viwango vya juu vinavyohitajika kwa mtu huyu, jambo ambalo lina manufaa sana kwa kuingia kwake katika uzima. Mtu anapoendelezwa na kukuzwa katika nyumba ya Mungu, inamaanisha atawekwa chini ya masharti makali na kusimamiwa kwa karibu. Nyumba ya Mungu itakagua, kusimamia, na kusukuma mbele kazi anayoifanya kwa ukali, na itaelewa na kutilia maanani kuingia kwake katika uzima. Kutokana na mitazamo hii, je, watu wanaoendelezwa na kukuzwa na nyumba ya Mungu hufurahia huduma maalum, hadhi maalum, na cheo maalum? La hasha, sembuse wao kufurahia hadhi yoyote maalum. Kwa watu ambao wameendelezwa na kukuzwa, wakihisi kwamba wana kitu cha kujivunia kwa sababu ya kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi kiasi, na hivyo wakadorora na kuacha kufuatilia ukweli, basi watakuwa hatarini wanapokumbana na majaribu na dhiki. Ikiwa kimo cha watu ni kidogo sana, kuna uwezekano watashindwa kusimama imara. Wengine husema, “Mtu akiendelezwa na kukuzwa kama kiongozi, basi ana hadhi. Hata kama yeye si mmoja wa wana wazaliwa wa kwanza, angalau ana tumaini la kuwa mmoja wa watu wa Mungu. Sijawahi kuendelezwa au kukuzwa, kwa hivyo, je, sina tumaini la kuwa mmoja wa watu wa Mungu?” Ni makosa kuwaza namna hii. Ili kuwa mmoja wa watu wa Mungu, ni lazima uwe na upitiaji wa maisha, na ni lazima uwe mtu anayemtii Mungu. Haijalishi kama wewe ni kiongozi, mfanyakazi, au mfuasi wa kawaida, yeyote aliye na uhalisi wa ukweli ni mmoja wa watu wa Mungu. Hata kama wewe ni kiongozi au mfanyakazi, ukikosa uhalisi wa ukweli, bado wewe ni mtendaji huduma. Kwa hakika, hakuna kitu maalum kuhusu watu wanaoendelezwa na kukuzwa. Kitu pekee kilicho tofauti na wengine ni kwamba wana mazingira yanayofaa zaidi, fursa zinazofaa zaidi, na hali bora za kufanya kazi maalum inayohusisha kanuni za ukweli. Hata kama kazi nyingi unazofanya zinahusisha taaluma fulani, ikiwa hakuna kanuni za ukweli za kuidhibiti na kuikagua, basi wajibu unaoutekeleza hautapatana na kanuni, na wewe unatumika tu, na hakika hutapata kibadli cha Mungu. Je, mahitaji ya nyumba ya Mungu kwa watu mbalimbali wenye talanta wanaoendelezwa na kukuzwa ni yapi? Ili kuendelezwa na kukuzwa na nyumba ya Mungu, angalau ni lazima wawe watu wenye dhamiri na busara, watu wanaoweza kukubali ukweli, watu wanaotekeleza wajibu wao kwa uaminifu, na watu wanaoweza kutii mipango na mipangilio ya Mungu, na angalau ni lazima waweze kukubali na kutii wanapokabiliwa na kupogolewa. Matokeo yanayopaswa kufikiwa na watu wanaopitia ukuzaji na mafunzo na nyumba ya Mungu si kwamba wanaweza kuwa maafisa au wakubwa, au kuongoza kundi, na si kwamba wanaweza kuwashauri watu kuhusu njia yao ya kufikiri, na bila shaka, hata kidogo si kwamba wana ujuzi bora wa kitaaluma au kiwango cha juu cha elimu, au sifa kubwa zaidi, au kwamba wanaweza kulinganishwa na wale walio mashuhuri duniani kwa ujuzi wao wa kitaaluma au mafanikio ya kisiasa. Badala yake, matokeo yanayopaswa kufikiwa ni kwamba wanaelewa ukweli na kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu, na kwamba wao ni watu wanaomwogopa Mungu na kuepuka maovu. Wanapokuwa wakijifundisha, wanaweza kuelewa ukweli na kushika kanuni za ukweli, na kujua vizuri zaidi hasa imani katika Mungu ni nini na jinsi ya kumfuata Mungu—hili lina manufaa makubwa kwa wale wanaofuatilia ukweli ili kufikia ukamilisho. Haya ndiyo matokeo na kiwango ambacho nyumba ya Mungu inataka kufikia katika kuwaendeleza na kuwakuza watu wenye talanta wa kila aina, na pia ndiyo mavuno makuu zaidi yanayopatikana na wale wanaoendelezwa na kutumiwa.

Watu wengine hutekeleza wajibu wao kwa uwajibikaji kiasi na wanakubaliwa na wateule wa Mungu, kwa hivyo wanakuzwa na kanisa ili wawe viongozi au wafanyakazi. Baada ya kupata hadhi, wao huanza kujiona kuwa bora kuliko wengine na huwaza, “Kwa nini nyumba ya Mungu imenichagua mimi? Je, si kwa sababu mimi ni bora kuliko ninyi nyote?” Je, haya hayasikiki kama maneno ya mtoto? Ni ya kitoto, ya kipuuzi, na ya kijinga. Kwa kweli, wewe si bora kuliko watu wengine hata kidogo. Ni kwamba tu unatimiza vigezo vya kukuzwa na nyumba ya Mungu. Iwapo unaweza kujitwika jukumu hili, kutekeleza wajibu huu vizuri au kukamilisha agizo hili ni jambo tofauti. Mtu anapochaguliwa kuwa kiongozi na ndugu na dada, au anaendelezwa na nyumba ya Mungu kufanya kazi fulani au kutekeleza wajibu fulani, hii haimaanishi kwamba ana hadhi au cheo maalum, au kwamba kweli anazozielewa ni za kina na nyingi zaidi kuliko za watu wengine—sembuse kwamba mtu huyu anaweza kumtii Mungu, na hatamsaliti Yeye. Bila shaka, haimaanishi pia kwamba anamjua Mungu, na ni mtu anayemwogopa Mungu. Hajafikia lolote kati ya haya, kwa kweli. Uendelezaji na ukuzaji ni uendelezaji na ukuzaji tu kwa maana ya moja kwa moja, na si sawa na wao kuwa wameamuriwa kimbele na kupatikana kuwa wanastahili na Mungu. Uendelezaji na ukuzaji wao unamaanisha tu wameendelezwa, na wanangoja kukuzwa. Na matokeo ya mwisho ya ukuzaji huu yanategemea iwapo mtu huyu anafuatilia ukweli, na iwapo ana uwezo wa kuchagua njia ya kufuatilia ukweli. Hivyo, mtu kanisani anapoendelezwa na kukuzwa kuwa kiongozi, anaendelezwa na kukuzwa tu kwa maana ya moja kwa moja; haimaanishi kwamba tayari anafikia kiwango kinachostahili na ana uwezo kama kiongozi, kwamba tayari ana uwezo wa kuchukua kazi ya uongozi, na anaweza kufanya kazi halisi—hivyo sivyo ilivyo. Watu wengi hawawezi kung’amua mambo haya, na kwa kuzingatia dhana zao wenyewe wanawaheshimu wale ambao wameendelezwa. Hili ni kosa. Haijalishi wamemwamini Mungu kwa miaka mingapi, je, wale wanaoendelezwa wana uhalisi wa ukweli kweli? Si lazima. Je, wanaweza kutekeleza mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu? Si lazima. Je, wana uwajibikaji? Je, wao ni waaminifu? Je, wanaweza kutii? Wanapokumbana na suala, je, wanaweza kutafuta ukweli? Haya yote hayajulikani. Je, watu hawa wana mioyo imwogopayo Mungu? Na mioyo yao imwogopayo Mungu ni mikubwa kiasi gani? Je, wanaweza kuepuka kufuata mapenzi yao wenyewe wanapofanya mambo? Je, wanaweza kumtafuta Mungu? Katika wakati ambapo wanatekeleza kazi ya uongozi, je, wanaweza kuja mbele za Mungu mara kwa mara kutafuta nia ya Mungu? Je, wanaweza kuwaongoza watu katika uhalisi wa ukweli? Hakika hawawezi kufanya mambo kama hayo. Hawajapokea mafunzo na hawajapitia vya kutosha, kwa hivyo hawawezi kufanya mambo haya. Hii ndiyo sababu kumwendeleza na kumkuza mtu haimaanishi kwamba tayari anaelewa ukweli, wala haisemi kwamba tayari ana uwezo wa kutekeleza wajibu wake kwa njia inayofikia kiwango kinachostahili. Basi lengo na umuhimu wa kumwendeleza na kumkuza mtu ni lipi? Ni kwamba mtu huyu anaendelezwa, kama mtu binafsi, ili aweze kutenda, na ili aweze kunyunyiziwa na kufunzwa kwa njia maalum, na hivyo kumwezesha kuelewa kanuni za ukweli, na kanuni, njia, na mbinu za kufanya mambo tofauti na kutatua matatizo mbalimbali, na pia jinsi ya kushughulikia na kukabiliana na mazingira na watu wa aina mbalimbali anaokutana nao kulingana na nia ya Mungu, na kwa njia inayolinda maslahi ya nyumba ya Mungu. Kwa kuhukumu kulingana na hoja hizi, je, watu wenye talanta wanaoendelezwa na kukuzwa na nyumba ya Mungu wana uwezo wa kutosha wa kuchukua kazi yao na kutekeleza wajibu wao vizuri wakati wa kipindi cha kuendelezwa na kukuzwa au kabla ya kuendelezwa na kukuzwa? Bila shaka haiwezekani. Hivyo, haiwezi kuepukika kwamba, wakati wa kipindi cha ukuzaji, watu hawa watapitia upogoaji, hukumu na kuadibu, kufichuliwa na hata kutimuliwa; hili ni jambo la kawaida, haya ni mafunzo na ukuzaji. Watu hawapaswi kuwa na matarajio yoyote ya juu au madai yasiyo ya kweli kwa wale wanaoendelezwa na kukuzwa; hilo halitakuwa jambo la busara, na si haki kwao. Ninyi mnaweza kusimamia kazi yao. Mkigundua matatizo au mambo yanayokiuka kanuni katika utendaji wa kazi yao, mnaweza kuibua suala hilo na kutafuta ukweli ili kutatua mambo haya. Kile msichopaswa kufanya ni kuwahukumu, kuwashutumu, kuwashambulia, au kuwatenga, kwa sababu wako tu katika kipindi cha ukuzaji, na hawapaswi kutazamwa kama watu ambao wamekamilishwa, sembuse kama watu wakamilifu, au kama watu walio na uhalisi wa ukweli. Kama vile mlivyo ninyi, wao wako tu katika kipindi cha mafunzo. Tofauti ni kwamba wanachukua kazi na majukumu mengi zaidi kuliko watu wa kawaida. Wana jukumu na wajibu wa kufanya kazi zaidi; ni lazima walipe gharama kubwa zaidi, wavumilie ugumu zaidi, watumie juhudi zaidi za kiakili, watatue matatizo zaidi, wavumilie lawama zaidi kutoka kwa watu, na bila shaka ni lazima pia wafanye juhudi kubwa zaidi, na—ikilinganishwa na watu wa kawaida wanaotekeleza wajibu wao—ni lazima wapate usingizi mdogo kiasi, wafurahie mambo mazuri kidogo kiasi, na wasijihusishe sana na udaku. Hiki ndicho kitu maalum kuwahusu; mbali na hili, wao ni sawa na mtu mwingine yeyote. Lengo la Mimi kusema hivi ni lipi? Ni kuwaacha kila mtu ajue kwamba ni lazima awakabili watu wenye talanta wa aina mbalimbali wanaoendelezwa na kukuzwa katika nyumba ya Mungu kwa usahihi, kwamba hawapaswi kuwa na madai makali kwa watu hawa, na, bila shaka, kwamba hawapaswi kuwa na maoni yasiyo ya kweli kuwahusu pia. Ni upumbavu kuwastaajabia na kuwaheshimu juu kupita kiasi; si ubinadamu na si jambo la kweli kuwa na madai makali kupita kiasi kwao. Basi njia ya busara zaidi ya kuwatendea ni ipi? Ni kuwaona kama watu wa kawaida na, unapohitaji kumtafuta mtu kuhusu tatizo, kufanya ushirika na wao na kujifunza kutoka kwa sifa nzuri za kila mmoja na kukamilishana. Zaidi ya hayo, ni jukumu la kila mtu kuwasimamia viongozi na wafanyakazi ili kuona kama wanafanya kazi halisi, kama wanaweza kutumia ukweli kutatua matatizo; hivi ndivyo viwango na kanuni za kupima iwapo kiongozi au mfanyakazi anafikia kiwango kinachostahili. Ikiwa kiongozi au mfanyakazi ana uwezo wa kushughulikia na kutatua matatizo ya jumla, basi anafaa. Lakini ikiwa hawezi hata kushughulikia na kurekebisha matatizo ya kawaida, hafai kuwa kiongozi au mfanyakazi, na ni lazima aondolewe haraka kutoka katika wadhifa wake. Mtu mwingine lazima achaguliwe, na kazi ya nyumba ya Mungu haipaswi kucheleweshwa. Kuichelewesha kazi ya nyumba ya Mungu ni kujiumiza mwenyewe na wengine pia, hakuna faida kwa yeyote.

Watu wengine hupandishwa vyeo na kusitawishwa na kanisa, wakipokea fursa nzuri ya kupata mafunzo. Hili ni jambo jema. Inaweza kusemwa wameinuliwa na kupewa neema na Mungu. Basi, wanapaswa kutekelezaje wajibu wao? Kanuni ya kwanza wanayopaswa kuzingatia ni kuelewa ukweli—wasipoelewa ukweli, ni lazima wautafute ukweli, na ikiwa bado hawaelewi baada ya kutafuta wenyewe, wanaweza kumtafuta mtu anayeelewa ukweli ili wafanye ushirika na kutafuta naye, jambo ambalo litafanya utatuzi wa tatizo uwe wa haraka na kwa wakati ufaao zaidi. Ikiwa unazingatia tu kutumia muda mwingi kusoma maneno ya Mungu peke yako, na kutumia muda mwingi kuyatafakari maneno haya, ili kufikia uelewa wa ukweli na kutatua tatizo, hili ni jambo la polepole mno; kama methali isemavyo, “tiba za polepole haziwezi kushughulikia mahitaji ya dharura.” Ikiwa, linapokuja suala la ukweli, unataka kupiga hatua haraka, basi ni lazima ujifunze jinsi ya kushirikiana na wengine kwa upatanifu, na kuuliza maswali zaidi na kutafuta zaidi. Ni hapo tu ndipo uzima wako utakua haraka, na utaweza kutatua matatizo mara moja, ili yote mawili yasichelewe. Kwa sababu umepandishwa cheo hivi punde na bado uko katika kipindi cha majaribio, na huelewi ukweli kwa hakika wala huna uhalisi wa ukweli—kwa sababu bado huna kimo hiki—usifikiri kwamba kupandishwa kwako cheo kunamaanisha kwamba una uhalisi wa ukweli; sivyo ilivyo. Ni kwa sababu tu una mzigo kwa ajili ya kazi na una ubora wa tabia wa kiongozi ndiyo maana umechaguliwa kupandishwa cheo na kusitawishwa. Unapaswa kuwa na busara hii. Ikiwa, baada ya kupandishwa cheo na kuwa kiongozi au mfanyakazi, unaanza kusisitiza hadhi yako, na kuamini kwamba wewe ni mtu anayefuatilia ukweli na kwamba una uhalisi wa ukweli—na ikiwa, bila kujali ni matatizo gani ambayo ndugu wanayo, unajifanya kuwa unaelewa, na kwamba wewe ni wa kiroho—basi hii ni njia ya kipumbavu, na ni sawa na Mafarisayo wanafiki. Ni lazima unene na utende kwa ukweli. Usipoelewa, unaweza kuwauliza wengine au kutafuta ushirika kutoka kwa Aliye juu—hakuna jambo la aibu katika haya yote. Hata usipouliza, Aliye juu bado atajua kimo chako cha kweli, na atajua kwamba huna uhalisi wa ukweli. Kutafuta na kufanya ushirika ndivyo unavyopaswa kufanya; hii ndiyo busara inayopaswa kupatikana katika ubinadamu wa kawaida, na kanuni ambayo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kuzingatia. Si jambo la kuaibikia. Ikiwa unafikiri kwamba pindi unapokuwa kiongozi kutoelewa kanuni, au kuwauliza watu wengine au Aliye juu maswali kila mara ni jambo la kuaibisha, na unaogopa kwamba wengine watakudharau, na kisha unaigiza, ukijifanya kuwa unaelewa kila kitu, kwamba unajua kila kitu, kwamba una uwezo wa kazi, kwamba unaweza kufanya kazi yoyote ya kanisa, na huhitaji mtu yeyote akukumbushe au afanye ushirika nawe, au mtu yeyote akukimu au kukuunga mkono, basi hili ni jambo la hatari, na wewe ni mwenye kiburi na wa kujihesabia haki mno, huna busara kabisa. Hujui hata kipimo chako mwenyewe—je, hili halikufanyi kuwa mtu aliyevurugika? Watu kama hao kwa kweli hawafikii vigezo vya kupandishwa vyeo na kusitawishwa na nyumba ya Mungu, na siku moja watatimuliwa na kuondoshwa. Na kwa hivyo, kila kiongozi au mfanyakazi ambaye amepandishwa cheo hivi punde anapaswa kuelewa wazi kwamba hana uhalisi wa ukweli, anapaswa kuwa na kujielewa kwa aina hii. Wewe sasa ni kiongozi au mfanyakazi si kwa sababu uliteuliwa na Mungu, bali kwa sababu ulipandishwa cheo na viongozi na wafanyakazi wengine, au ulichaguliwa na watu wateule wa Mungu; hili halimaanishi kwamba una uhalisi wa ukweli na kimo cha kweli. Unapoelewa hili, utakuwa na busara kiasi, ambayo ndiyo busara ambayo viongozi na wafanyakazi ni lazima wawe nayo. Je, mmeelewa sasa? (Ndiyo.) Basi, mnapaswa kufanyaje kazi hasa? Mnapaswa kutekelezaje ushirikiano wenye upatanifu? Mnapaswa kutafutaje ukweli ili kutatua matatizo kila mnapokumbana nayo? Mambo haya ni lazima yaeleweke. Tabia potovu zikifichuliwa, tafuteni ukweli na mzitatueni haraka iwezekanavyo. Zisipotatuliwa kwa wakati na ziathiri kazi yenu, hili ni tatizo. Ikiwa hamuifahamu taaluma fulani, mnapaswa pia kujifunza bila kuchelewa. Kwa sababu baadhi ya wajibu huhusisha maarifa ya kitaaluma, ikiwa mnaelewa ukweli tu bila kufahamu maarifa yoyote ya kitaaluma, itaathiri pia matokeo ya kazi yenu. Angalau, ni lazima mfahamu na muelewe maarifa ya msingi ya kitaaluma, ili muweze kuwa na ufanisi katika kufuatilia na kuelekeza kazi ya watu. Ikiwa ninyi ni wastadi tu katika taaluma lakini hamwelewi ukweli, vivyo hivyo kutakuwa na mapungufu katika kazi yenu, kwa hivyo mtahitaji pia kufuatilia ukweli na kushirikiana na watu wanaoelewa ukweli ili kutekeleza wajibu wenu ipasavyo. Kwa sababu tu una ustadi wa kitaaluma au katika fani fulani ya maarifa, haimaanishi kwamba unaweza kufanya mambo kulingana na kanuni, kwa hivyo ni muhimu kabisa kutafuta ushirika na watu wanaoelewa ukweli—hii ni kanuni ambayo ninyi mnapaswa kuzingatia. Chochote unachofanya, ni lazima usijifanye. Uko katika kipindi cha mafunzo na usitawishaji, na una tabia potovu, na huelewi ukweli hata kidogo. Niambieni, je, Mungu anajua kuhusu mambo haya? (Ndiyo.) Basi, si unaonekana mpumbavu ukijifanya? Je, ninyi mnataka kuwa watu wapumbavu? (La, hatutaki.) Ikiwa hamtaki kuwa watu wapumbavu, mnapaswa kuwa watu wa aina gani? Kuweni watu wenye busara, watu wanaoweza kutafuta ukweli kwa unyenyekevu na wanaoweza kuukubali ukweli. Msijifanye, msiwe Mafarisayo wanafiki. Kile unachojua ni maarifa fulani tu ya kitaaluma, si kanuni za ukweli. Ni lazima utafute njia ya kutumia ipasavyo nguvu zako za kitaaluma na kutumia maarifa na elimu uliyoipata kwa msingi wa kuelewa kanuni za ukweli. Je, hii si kanuni? Je, hii si njia ya utendaji? Pindi tu unapojifunza kufanya hivi, utakuwa na njia ya kufuata na utaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli. Chochote unachofanya, usiwe mkaidi, na usijifanye. Ukaidi na kujifanya si njia ya busara ya kufanya mambo. Badala yake, ni njia ya kipumbavu zaidi ya kufanya mambo. Watu wanaoishi kwa kufata tabia zao potovu ndio watu wapumbavu zaidi. Ni wale tu wanaotafuta ukweli na kushughulikia mambo kulingana na kanuni za ukweli ndio watu werevu zaidi.

Kupitia ushirika huu, je, sasa ninyi mna uelewa na mtazamo sahihi kuhusu kupandishwa vyeo na kusitawishwa kwa watu wenye talanta wa kila aina na nyumba ya Mungu? (Ndiyo.) Sasa kwa kuwa mna mtazamo sahihi kuhusu hili, je, mnaweza kuwachukulia watu hawa kwa njia sahihi? Ni lazima mvichukulie vipaji vyao kwa usahihi, na vile vile mapungufu na kasoro walizo nazo katika ubinadamu wao, kazi, taaluma, na nyanja nyingine mbalimbali—mambo haya yote ni lazima yachukuliwe kwa usahihi. Aidha, bila kujali kama mnapandishwa vyeo na kusitawishwa kuwa viongozi au wafanyakazi, au kama ninyi ni watu wenye talanta katika taaluma mbalimbali, ninyi nyote ni watu wa kawaida, ninyi nyote mmepotoshwa na Shetani, na hakuna yeyote kati yenu anayeelewa ukweli. Kwa hivyo, hakuna yeyote kati yenu anayepaswa kujificha wala kujifunika; badala yake mnapaswa kujifunza kujifungua katika ushirika. Ikiwa hamwelewi, basi kubalini kuwa hamwelewi. Ikiwa hamjui jinsi ya kufanya kitu, basi kubalini kuwa hamjui jinsi ya kukifanya. Bila kujali matatizo au ugumu unaotokea, kila mtu anapaswa kufanya ushirika na kutafuta ukweli kwa pamoja ili kupata suluhisho. Mbele ya ukweli kila mtu ni kama mtoto mchanga, kila mtu ni masikini na duni na hana kitu kabisa. Kile ambacho watu wanahitaji kufanya ni kuwa watiifu mbele ya ukweli, kuwa na moyo wa unyenyekevu na wenye shauku na kutafuta na kuukubali ukweli, na kisha kutenda ukweli na kufikia utii kwa Mungu. Kwa kufanya hivi watu wanaweza kuingia katika uhalisi wa ukweli wa maneno ya Mungu wanapotekeleza wajibu wao na katika maisha yao halisi. Kila mtu yuko sawa mbele ya ukweli. Wale wanaopandishwa vyeo na kusitawishwa si bora sana kuwaliko wengine. Kila mtu amepitia kazi ya Mungu kwa takribani muda sawa. Wale ambao hawajapandishwa vyeo au kusitawishwa wanapaswa pia kufuatilia ukweli wanapotekeleza wajibu wao. Hakuna mtu anayeweza kumnyima mwingine haki ya kufuatilia ukweli. Watu wengine wana shauku zaidi katika ufuatiliaji wao wa ukweli na wana ubora wa tabia kiasi, kwa hivyo wanapandishwa vyeo na kusitawishwa. Hii ni kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya nyumba ya Mungu. Basi kwa nini nyumba ya Mungu ina kanuni kama hizo za kuwapandisha vyeo na kuwatumia watu? Kwa sababu kuna tofauti katika ubora wa tabia na sifa za watu, na kila mtu huchagua njia tofauti, hili husababisha matokeo tofauti katika kumwamini Mungu. Wale wanaofuatilia ukweli wanaokolewa na kuwa watu wa ufalme, huku wale wasioukubali ukweli hata kidogo, ambao si waaminifu katika kutekeleza wajibu wao, wanaondoshwa. Nyumba ya Mungu huwasitawisha na kuwatumia watu kulingana na iwapo wanafuatilia ukweli, na iwapo ni waaminifu katika kutekeleza wajibu wao. Je, kuna tofauti katika madaraja ya watu mbalimbali katika nyumba ya Mungu? Kwa sasa, hakuna madaraja kwa upande wa nafasi, thamani, hadhi, au cheo cha watu mbalimbali. Angalau katika kipindi ambacho Mungu anafanya kazi ili kuwaokoa na kuwaongoza watu, hakuna tofauti kati ya vyeo, nafasi, thamani, au hadhi ya watu mbalimbali. Vitu pekee vilivyo tofauti ni katika mgawanyo wa kazi na katika majukumu ya wajibu yanayotekelezwa. Bila shaka, katika kipindi hiki, baadhi ya watu, isivyo kawaida, wanapandishwa vyeo na kusitawishwa kufanya kazi fulani maalum, huku baadhi ya watu hawapati fursa kama hizo kutokana na sababu mbalimbali kama vile matatizo ya ubora wa tabia zao au mazingira ya familia. Lakini, je, si Mungu huwaokoa wale ambao hawajapata fursa kama hizo? Sivyo ilivyo. Je, thamani na nafasi yao ni ya chini kuliko ya wengine? Hapana. Kila mtu yuko sawa mbele ya ukweli, kila mtu ana fursa ya kufuatilia na kupata ukweli, na Mungu humtendea kila mtu kwa haki na busara. Ni wakati gani ndipo kuna tofauti zinazoonekana katika nafasi, thamani, na hadhi za watu? Ni wakati watu wanapofika mwisho wa njia yao, na kazi ya Mungu imekwisha, na hitimisho hatimaye linafikiwa juu ya mitazamo na maoni ambayo kila mtu alionyesha katika mchakato wa kufuatilia wokovu na alipokuwa akitekeleza wajibu wake, na vile vile juu ya udhihirisho na mitazamo yao mbalimbali kwa Mungu—yaani, kunapokuwa na rekodi kamili katika daftari la Mungu—wakati huo, kwa sababu matokeo na hatima za watu zitakuwa tofauti, kutakuwa pia na tofauti katika thamani, nafasi, na hadhi zao. Ni hapo tu ndipo mambo haya yote yanaweza kuonekana na kuthibitishwa takribani, ilhali sasa kila mtu yuko sawa. Je, mmeelewa? Je, ninyi mnaingojea siku hiyo? Je, mnaitarajia na kuiogopa kwa wakati mmoja? Mnachotarajia ni kwamba siku hiyo hatimaye kutakuwa na matokeo, na mtakuwa mmefika siku hiyo hatimaye licha ya ugumu wote; na mnachoogopa ni kwamba hamtakuwa mmetembea katika njia hiyo ipasavyo, na kwamba mtaanguka njiani na kushindwa, na kwamba matokeo ya mwisho hayatakuwa ya kuridhisha, yatakuwa mabaya zaidi ya mnavyofikiria na kutarajia—jinsi itakavyokuwa huzuni, uchungu na kukatisha tamaa! Msifikirie mbali hivyo, si jambo la vitendo kufikiria mbali hivyo. Kwanza angalieni kile kilicho mbele ya macho yenu, tembeeni ipasavyo katika njia iliyo chini ya miguu yenu, fanyeni kazi iliyo mikononi mwenu vizuri, na timizeni wajibu na majukumu ambayo Mungu amewakabidhi. Hili ndilo jambo muhimu na la maana zaidi. Eleweni ukweli na kanuni za kutekeleza wajibu wenu ambazo mnapaswa kuzielewa sasa hivi, na mfanye ushirika juu ya vitu hivyo hadi viwe wazi kabisa—ili myaweke akilini mwenu, na mjue waziwazi na kwa usahihi kanuni ni zipi katika kila kitu mnachofanya—na mhakikishe hamkiuki kanuni, au kukengeuka kutoka kwazo, au kusababisha vurugu au usumbufu, au kufanya chochote kinachodhuru masilahi ya nyumba ya Mungu—haya yote ndiyo ambayo ninyi mnapaswa kuingia sasa hivi. Hakuna haja ya sisi kuzungumza juu ya jambo lolote la mbeleni zaidi, na wala hakuna haja ya ninyi kuuliza au kufikiria kulihusu. Haina maana kufikiria mbali hivyo—hicho si kile mnachopaswa kufikiria. Wengine wanaweza kuuliza: “Kwa nini tusifikirie kulihusu? Hali ya maafa imekuwa kubwa sana sasa, je, si sasa ndio wakati wa sisi kufikiria mambo kama hayo?” Je, huu ndio wakati wa kufanya hivyo? Je, ukweli kwamba maafa ni makubwa unaathiri kuingia kwenu katika ukweli? (La, hauathiri.) Hali ya maafa imekuwa kubwa sana, lakini ni lini Mimi hufanya mikutano au kutoa mahubiri mahususi kuhusu maafa? Mimi kamwe siangazii jambo la maafa, Mimi daima huzungumza tu juu ya ukweli, ili ninyi muweze kuelewa ukweli na kuelewa nia za Mungu, na ili ninyi muelewe jinsi ya kutekeleza wajibu wenu vizuri na jinsi ya kuingia katika uhalisi wa ukweli. Siku hizi, watu wengine hawaelewi hata uhalisi wa ukweli ni nini na mafundisho ni nini. Wao hurudia-rudia tu maneno na mafundisho yale yale machache na maneno matupu kila siku na bado wanahisi kwamba wameingia katika uhalisi wa ukweli. Mimi ninawahangaikia, lakini wao hawajihangaishi wenyewe. Bado wanafikiria juu ya mambo hayo ya mbali ya wakati ujao—kufikiria juu ya mambo hayo si jambo la vitendo.

Lengo la kuwapandisha vyeo na kuwasitawisha watu wenye talanta wa kila aina si kuwageuza kuwa watu wenye bidii, wala kupanga wawe nguzo kuu za aina fulani siku zijazo, bali ni kuwapa baadhi ya watu ambao, kwa kulinganisha, wanafuatilia ukweli zaidi na wanaofikia vigezo kwa ajili ya kupandishwa vyeo na kusitawishwa fursa ya kupata mafunzo katika mazingira yanayofaa na chini ya masharti mazuri zaidi. Jambo la muhimu zaidi ni kwamba wanaweza kuelewa maneno ya Mungu, kuelewa ukweli na kuingia katika uhalisi wa ukweli. Je, si hili ndilo ambalo watu wanapaswa kufikia kwa kumwamini Mungu? Je, si hili ndilo ambalo watu wanapaswa kupata kwa kumwamini Mungu? Ili kuingia katika uhalisi wa ukweli, ni jambo gani kuu ambalo ninyi mnapaswa kufuatilia sasa hivi? Je, mna mipango au hatua zozote za kulifanya? Nitawaambia njia ya mkato ambayo ni rahisi, nyepesi na ya haraka. Kwa maneno rahisi, kuingia katika uhalisi wa ukweli kwa kweli ni kutenda ukweli. Ili kutenda ukweli, ni muhimu kwanza kushughulikia tabia potovu za mtu. Mwanzo wa haraka zaidi wa kutatua tabia potovu za mtu ni upi? Kwa upande wenu, njia rahisi, ya haraka na isiyo na matatizo zaidi ni kutatua tatizo la kufanya wajibu wenu kwa kijuujuu tu kwanza, mkitatua tabia zenu potovu hatua kwa hatua. Inaweza kuwachukua muda gani kulitatueni? Je, mna mpango? Watu wengi hawana mpango, wao huendelea tu kulifanyia kazi akilini mwao, bila kujua ni lini wataanza rasmi. Ingawa wanajua kwamba wanafanya mambo kwa kijuujuu tu, hawajitahidi kulitatua na hawana suluhisho lolote mahususi. Kuwa mvivu katika kutekeleza wajibu wa mtu, na kutokuwa waangalifu na sahihi sana, kutokuwa makini, na kutowajibika—haya yote ni maonyesho ya kufanya mambo kwa kijuujuu tu. Hatua ya kwanza ni kutatua tatizo la kufanya mambo kwa kijuujuu tu. Hatua ya pili ni kutatua tatizo la kutenda kulingana na mapenzi ya kibinafsi. Kuhusu mambo mengine kama vile kunena kwa udanganyifu mara kwa mara, au kufunua tabia za udanganyifu au za kiburi, msijishughulishe na mambo hayo kwa sasa. Je, si jambo la vitendo na lenye ufanisi zaidi kwanza kushughulikia kufanya mambo kwa kijuujuu tu na kutenda kulingana na mapenzi ya mtu binafsi? Je, si masuala haya mawili ndiyo rahisi zaidi kuyaona? Je, si ni rahisi kuyatatua? (Ndiyo.) Je, unatambua unapofanya mambo kwa kijuujuu tu? Je, unatambua unapowazia kuwa mvivu? Je, unatambua unapofikiria kufanya hila au kuwa mjanja na kujihudumia kwa ujanja? (Ndiyo.) Ikiwa unatambua, basi ni rahisi kulitatua. Anza kwa kutatua matatizo ambayo unaweza kuyaona kwa urahisi na ambayo unatambua ndani yako. Kufanya wajibu wa mtu kwa kijuujuu tu ni tatizo dhahiri na la kawaida sana, lakini pia ni sugu sana ambalo ni gumu sana kulitatua. Mtu anapotekeleza wajibu, ni lazima ajifunze kuwa mwangalifu, mwenye nidhamu, makini, na mwenye kuwajibika, na kuufanya kwa njia thabiti, kwa kupiga hatua moja baada ya nyingine kwa uthabiti. Ni lazima atumie nguvu zake zote kutekeleza wajibu huo vizuri, hadi aridhike na jinsi alivyoutekeleza. Mtu asipoelewa ukweli, anapaswa kutafuta kanuni, na kutenda kulingana nazo na mahitaji ya Mungu; anapaswa kutia bidii zaidi kwa hiari ili kutekeleza wajibu wake vizuri, na kamwe asiufanye kwa kijuujuu tu. Ni kwa kutenda hivi tu ndiyo mtu anaweza kuhisi amani moyoni mwake, bila dhamiri yake kumlaumu. Je, kufanya mambo kwa kijuujuu tu ni jambo rahisi kutatua? Maadamu una dhamiri na busara, unaweza kulitatua. Kwanza, ni lazima umwombe Mungu: “Mungu, ninaanza wajibu wangu. Nikifanya kwa kijuujuu tu, ninakuomba Uniadhibu na kunikemea moyoni mwangu. Pia nakuomba Uniongoze nitekeleze wajibu wangu vizuri na nisifanye kwa kijuujuu tu.” Tenda kwa njia hii kila siku na uone itachukua muda gani kutatua tatizo lako la kufanya mambo kwa kijuujuu tu, ili hali zako za kufanya mambo kwa kijuujuu tu zipungue, uchafu katika wajibu wako uwe mchache, na matokeo yako halisi yaboreke na ufanisi wako uongezeke katika utendaji wa wajibu wako. Kutekeleza wajibu wako bila kufanya kwa kijuujuu tu—je, hili ni jambo unaloweza kufikia kwa kujitegemea? Unapofanya kwa kijuujuu tu, je, unaweza kulidhibiti? (Si rahisi.) Basi hilo ni jambo gumu. Ikiwa ni vigumu kweli kwako kulidhibiti hili, basi ninyi mna tatizo kubwa linalowakabili! Basi, ni mambo gani ambayo ninyi mnaweza kufanya bila kufanya kwa kijuujuu tu? Watu wengine wanajali sana kuhusu kile wanachokula; ikiwa mlo hauwapendezi, hawatakuwa na furaha siku nzima. Wanawake wengine wanapenda kujipamba na kujirembesha; hawatakosa kuushughulikia unywele hata mmoja. Watu wengine ni wazuri katika kufanya biashara; wao huhesabu kwa makini kila senti. Ikiwa ninyi mnatenda kwa mtazamo wa uangalifu wa aina hii, mnaweza kuepuka kufanya mambo kwa kijuujuu tu. Kwanza, tatueni tatizo la kufanya mambo kwa kijuujuu tu, kisha tatueni tatizo la kutenda kulingana na mapenzi yenu binafsi. Kutenda kulingana na mapenzi ya kibinafsi ni tatizo la kawaida, na ni lingine ambalo watu wanaweza kuligundua kwa urahisi ndani yao. Kwa kujitafakari kidogo, mtu anaweza kutambua kwamba anatenda kulingana na mapenzi yake ya kibinafsi, jambo ambalo halipatani na kanuni za ukweli. Matatizo ambayo watu wanaweza kuyatambua ni rahisi kuyatatua. Jipangeni kwanza kutatua masuala haya mawili, moja likiwa ni tatizo la kufanya mambo kwa kijuujuu tu na lingine likiwa kutenda kulingana na mapenzi yenu ya kibinafsi. Jitahidini, ndani ya mwaka mmoja au miwili kufikia matokeo, kutofanya mambo kwa kijuujuu tu, au kutenda kulingana na mapenzi yenu ya kibinafsi au pamoja na mchanganyiko wa mapenzi yenu katika chochote mnachofanya. Mara tu matatizo haya mawili yatakapotatuliwa, ninyi hamtakuwa mbali na kutekeleza wajibu wenu kwa njia inayofikia kiwango kinachostahili. Na ikiwa ninyi hamwezi hata kuyatatua, basi bado mko mbali na kumtii Mungu au kujali nia Zake—hamjaligusa hata kidogo.

Tumefanya ushirika hivi punde kuhusu vigezo na malengo ya kuwapandisha vyeo na kuwasitawisha watu wenye talanta wa kila aina walio na sifa, na vile vile kuhusu uelewa na mtazamo ambao mtu anapaswa kuwa nao kuhusu kupandishwa vyeo na kusitawishwa na nyumba ya Mungu kwa watu wenye talanta wa kila aina. Aidha, kipengele kingine ni mtazamo na jinsi ya kuwatendea watu wa aina mbalimbali wenye talanta wanaopandishwa vyeo na kusitawishwa. Haya ni baadhi ya masuala ambayo yanapaswa kufanyiwa ushirika katika kipengele cha sita. Hivyo basi, la kufuatia, tukilenga hasa kipengele cha sita, tutafichua na kuchanganua jinsi viongozi wa uwongo wanavyotekeleza kazi ya kuwapandisha vyeo na kuwasitawisha watu wenye talanta wa kila aina. Haya ndiyo maudhui makuu tutakayoyafanyia ushirika.

Mitazamo na Udhihirisho wa Viongozi wa Uwongo Kuhusiana na Kukuza na Kuwastawisha Watu wa Aina Zote Wenye Talanta

Viongozi wa uwongo hawaelewi ukweli na hawatafuti ukweli. Kwa hivyo, linapokuja suala la kazi muhimu ya kuwapandisha vyeo na kuwasitawisha watu wenye talanta wa kila aina walio na sifa katika nyumba ya Mungu, wao pia hulifanya ovyoovyo kabisa, na kuliharibu kabisa, na wao hushindwa kabisa kufikia mahitaji ya nyumba ya Mungu. Kwa sababu hawaelewi vigezo, sembuse nia za Mungu, kuhusu kupandishwa vyeo na kusitawishwa kwa watu wa aina mbalimbali wenye talanta walio na sifa, na wala hawaelewi umuhimu wa kuwapandisha vyeo na kuwasitawisha watu wa aina mbalimbali wenye talanta walio na sifa, ni vigumu sana kwao kufanya kazi hii kwa njia inayofikia kiwango kinachostahili na kulingana na kanuni. Watu wa aina mbalimbali “wenye talanta” ambao viongozi wa uwongo huwasitawisha wakati wa kufanya kazi yao ni mchanganyiko wa kila aina. Badala ya kuwapandisha vyeo na kuwasitawisha watu wenye talanta walio na sifa, viongozi wa uwongo huwapandisha vyeo watu ambao hawapaswi kamwe kupandishwa vyeo na kusitawishwa ili watumike kama viongozi au wafanyakazi, na kuwaruhusu watu hawa kulitegemea kanisa na kutapanya matoleo ya Mungu. Viongozi wote wa uwongo hufanya mambo kama haya, na kusababisha baadhi ya watu wanaofuatilia ukweli na walio na hisia ya haki kukanyagwa chini na wasipandishwe vyeo na kutumiwa. Badala yake, wale wasiofaa kitu huwa watu wanaoitwa wenye talanta machoni pa viongozi hawa wa uwongo, na hupandishwa vyeo na wao na kusitawishwa. Basi maonyesho ya viongozi wa uwongo wanapofanya kazi hii ni yapi? Tuchukulie, kwa mfano, kwamba kutokana na mahitaji ya kazi yake, nyumba ya Mungu ni lazima itafute watu fulani wa kushughulikia mambo ya nje. Basi, inapaswa kuwatafuta watu wa aina gani? Nimeorodhesha hivi punde vigezo kadhaa, ambavyo ni kuwa na uwezo wa kazi, kuweza kutekeleza wajibu wa mtu kulingana na kanuni zinazohitajika na nyumba ya Mungu, na kuweza kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu. Je, viongozi wa uwongo wanazijua kanuni hizi? Ni wazi kwamba hawazijui, kwa hivyo wanawatafutaje watu wa kushughulikia mambo ya nje? Wao hujiwazia: “Ni nani anayeweza kushughulikia mambo ya nje? Kuna dada mmoja ambaye ni mwenye akili nyingi na mwepesi wa kuitikia, ni mzungumzaji mzuri na anajua jinsi ya kuamiliana na watu. Macho yake huzunguka-zunguka kwa hila anapozungumza, na mtu wa kawaida hawezi kumsoma. Angekuwa hafai kiasi kama kiongozi wa kanisa, lakini angekuwa stadi katika kushughulikia mambo ya nje, kwa hivyo nitamchagua. Ila tu kiwango chake cha elimu kiko chini kidogo, nina wasiwasi kwamba wasioamini watamdharau, kwa hivyo nitamtafuta mhitimu wa chuo kikuu—ambaye alikuwa rais wa muungano wa wanafunzi—ili ashirikiane naye. Mtu huyu ni mwerevu kiasi lakini ana uzoefu mdogo kiasi katika jamii na ameona mambo machache kiasi duniani, kwa hivyo anaweza kujifunza kutoka kwa mwenzake. Kati ya watu hawa wawili, mmoja ana kiwango cha chini cha elimu na mwingine ana elimu ya juu, mmoja ana uzoefu katika jamii na mwingine hana—wanafaa kushirikiana, sivyo?” Mmoja ni mwenye ufasaha na msemaji hodari, mwenye akili nyingi, na mjanja hasa wa kijamii; kila anapotangamana na wasioamini, hawawezi kujua kwamba yeye ni muumini. Mwingine ana elimu ya juu na ana hadhi ya kijamii; kila anapotangamana na wasioamini, hawamdharau. Mnaonaje kuhusu kanuni hizi mbili ambazo viongozi wa uwongo hutumia kuwachagua watu? Viongozi wa uwongo huamini kwamba maadamu mtu ana kipawa cha kuongea, akili nyingi, na ni mwepesi wa kuitikia, anaweza kushughulikia mambo ya jumla kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Je, hii ni njia inayofaa ya kuwachagua watu? (Hapana.) Haifai vipi? (Watu kama hao mara nyingi huwa wajanja sana; ingawa wanaweza kutumia falsafa za shughuli za kidunia na wengine, na wanajua jinsi ya kuamiliana na watu, si lazima waweze kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu.) Hilo ni sahihi. Jambo la muhimu zaidi ni kwamba haijalishi ni mambo gani ambayo mtu anayashughulikia kwa ajili ya nyumba ya Mungu, angalau ni lazima awe mnyofu na aweze kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu. Je, kuwa na ufasaha wa maneno na kuweza kumfufua aliyekufa kwa maneno kunamaanisha kwamba anaweza kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu? Je, kuwa mwenye akili nyingi, mwenye ufasaha, na msemaji hodari kunamaanisha kwamba anaweza kulinda masilahi ya nyumba ya Mungu? (La, haimaanishi hivyo.) Hata akiapa, haina maana, na haina maana vile vile ukimwekea masharti—ni lazima awe na sifa hiyo. Lakini viongozi wa uwongo hawachunguzi mambo haya, wanatazama tu ni nani aliye na uzoefu katika jamii, nani ni mjanja, mwenye akili nyingi, mwenye ufasaha na msemaji hodari, anayejua jinsi ya kutenda kulingana na hali, na aliye kama kinyonga, na mjanja wa kijamii. Wao hufikiri kwamba watu kama hao wanaweza kushughulikia mambo ya jumla katika nyumba ya Mungu. Je, hili si kosa? Hili ni kosa kwa upande wa kanuni na viwango vya kuwachagua watu. Ukweli ni kwamba mtu wa aina hii ana ulimi mtamu kupita kiasi: Haijalishi anaamiliana na nani, kila kitu anachosema ni uwongo, na hawezi kubadilika bila kujali anakula viapo vingapi. Anapofanya mambo, analinda tu masilahi yake mwenyewe, na hasa anapokabiliwa na hatari, anajilinda mwenyewe kwanza kabisa, na hafikirii hata mara moja kuhusu masilahi ya nyumba ya Mungu. Maadamu ana uhusiano mzuri na wasioamini, hilo linamtosha; kuhusu iwapo masilahi ya nyumba ya Mungu yanadhurika au la, hajali hata kidogo. Usalama wa akina ndugu pia si jambo analolizingatia, wala hajali iwapo jina la Mungu linafedheheshwa; anajilinda mwenyewe tu. Viongozi wa uwongo hawawezi kumng’amua mtu wa aina hii na wanafikiri kwamba ndiye anayefaa zaidi kushughulikia mambo ya nje kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Je, huu si upumbavu? Wanayasaliti masilahi ya nyumba ya Mungu lakini viongozi wa uwongo hawajui hata hilo na bado wanawapa kazi muhimu, na kuwategemea kwa kila kitu. Je, hiki si kilele cha upumbavu? Je, watu wenye ufasaha, wasemaji hodari, na wenye akili nyingi ni watu wenye nia nyoofu? Ikiwa hamjaamiliana nao au kuwatazama kwa makini, hamtajua. Mnapoamiliana na kushughulikia mambo nao, oneni tu iwapo kile wanachosema kinapatana na kile wanachofanya. Hili linaweza kujaribiwa kupitia tukio moja. Tuseme, kwa mfano, ninyi mnahamisha vitu. Wanapoona hili, hawatawasaidia. Mtakapomaliza tu kazi ndipo watakuja na kusema, “Mnawezaje kufanya kazi ya kuchosha namna hii peke yenu? Ningewasaidia kama mngeuliza tu, haijalishi nilikuwa na shughuli kiasi gani. Mnaonekana mmechoka kabisa. Nitawapikia baadaye, hamna haja ya kufanya hivyo leo.” Baada ya kusema hivyo, wanatoweka. Mmechoka kabisa na bado inawabidi mpike. Kisha punde tu mnapomaliza kupika, wanakuja kula na hata kusema, “Kwa nini hamkuniita mlipokuwa karibu kuanza kupika? Mmechoka kabisa na bado mnanipikia chakula—hilo linawezaje kuwa sawa? Kwa kuwa tayari mmekitayarisha sasa, nitakila tu. Nitapika mlo unaofuata, na niiteni wakati wowote mtakapokuwa na kazi inayohitaji kufanywa siku zijazo.” Tukio hili moja linatosha kuwaona walivyo hasa. Wana ulimi laini sana, akili nyingi, na wanajua la kusema. Wanajua jinsi ya kutenda kulingana na hali, na wanachofanya tu ni kusema mambo mazuri ya kusikika, bila kamwe kufanya kazi yoyote halisi. Je, watu kama hao ni wa kutegemewa? Mkiwauliza washugulikie mambo ya jumla ya nyumba ya Mungu, je, wanaweza kulinda masilahi yake? Je, wanaweza kulinda sifa ya kanisa na kulinda usalama wa akina ndugu? (Hapana.) Je, mali ya nyumba ya Mungu na masilahi yake yote ni kipaumbele chao cha kwanza? La hasha. Macho na akili za viongozi wa uwongo ni vipofu kwa matatizo yanayoweza kugunduliwa kwa urahisi namna hii, hawawezi tu kuyaona. Badala yake, wanaweza tu kunena maneno na mafundisho. Ni nani anayependwa na Mungu na ni nani asiyependwa na Mungu, ni nani anayependa ukweli na nani asiyependa ukweli, inamaanisha nini kuwa na msingi katika imani ya mtu kwa Mungu na ni watu wa aina gani wasio na msingi, ni watu wa aina gani walio waaminifu katika kutekeleza wajibu wao na ni watu wa aina gani wasio waaminifu katika kutekeleza wajibu wao—wanazungumza kuhusu mambo haya kwa njia ya busara na kimantiki, na wanaonekana kuyaelewa kweli, lakini yote ni maneno matupu na mafundisho. Wakati wowote wanapoombwa kuwatambua watu, macho na akili zao huwa na upofu; hawajui tu jinsi ya kuwasoma watu. Haijalishi wanatangamana na watu wa aina hii kwa muda gani, bado hawawezi kuwang’amua, na hata wanawapa kazi muhimu.

Ni jambo la kuchukiza tayari kwa viongozi wa uwongo kuwatumia watu wasiofaa, lakini pia wanaongezea kosa hili kwa kufanya mambo ya kuchukiza hata zaidi. Tuseme, kwa mfano, kwamba kiongozi wa uwongo alimtumia mtu asiyefaa. Mtu huyu hafai kabisa kuwa msimamizi na hatimizi vigezo vya nyumba ya Mungu vya kupandishwa cheo na kusitawishwa. Lakini kiongozi wa uwongo bado anang’ang’ania kumtumia na kamwe hakagui kazi ya mtu huyu, akiamini, “Usimtilie shaka yule unayemtumia, wala usimtumie yule unayemtilia shaka. Kwa kuwa nimekuchagua na kukupandisha cheo, utaweza kufanya kazi hii vizuri, kwa hivyo endelea tu na ufanye kazi jinsi unavyoona inafaa. Nitakuunga mkono katika chochote unachofanya, na haina maana kwa yeyote kupinga hili!” Walimtumia mtu asiyefaa, na bado wakaacha kosa lao liendelee mpaka mwisho—hivi ndivyo wanavyojiamini. Viongozi wa uwongo wote ni vipofu. Hawawezi kuona matatizo yoyote, hawawezi kutambua ni watu gani walio waovu au wasioamini, na haijalishi ni nani anayevuruga na kusumbua kazi ya kanisa, hawana ufahamu wowote kuihusu, na hata huwapa kazi muhimu watu waliovurugika. Viongozi wa uwongo huwaamini sana yeyote wanayempandisha cheo, na kwa wepesi wa moyo wao huwakabidhi kazi muhimu. Matokeo yake, watu hao huivuruga kazi ya kanisa, wakiathiri vibaya kuenea kwa injili na kudhuru maslahi ya nyumba ya Mungu. Viongozi wa uwongo hata hujifanya kwamba hawajui chochote kuhusu hili. Aliye juu anawauliza, “Yule mtu uliyempandisha cheo anaendeleaje katika kazi yake? Je, anafaa kufanya kazi hii? Je, anatetea kazi ya kanisa na maslahi ya nyumba ya Mungu? Katika nyakati muhimu, atajilinda mwenyewe, au ataitetea kazi ya kanisa?” Viongozi hawa wa uwongo hujibu: “Aliapa kiapo cha kutetea kazi ya kanisa. Kando na hilo, amemwamini Mungu kwa miaka 20. Angewezaje kujilinda mwenyewe na kusaliti maslahi ya nyumba ya Mungu? Labda atatetea maslahi ya nyumba ya Mungu.” Aliye juu anajibu: “Je, unayoyasema ni sahihi? Je, umeikagua kazi yake?” Viongozi hawa wa uwongo hujibu, “Sijaikagua kazi yake, lakini nilimwambia asitetee maslahi yake mwenyewe, na kwamba ni lazima atetee kazi ya kanisa, na akaniahidi kwamba atafanya hivyo.” Ahadi yake kwako ilikuwa na faida gani? Hawezi hata kutimiza kiapo alichoapa mbele za Mungu. Je, unafikiri kwa sababu tu alikuahidi wewe, ahadi yake ni hakikisho? Je, anaweza hakika kufanya kile alichoahidi? Kwa kuwa hujaikagua kazi yake, unajuaje kama yeye ni mtu anayetetea maslahi ya nyumba ya Mungu? Inakuwaje unajiamini kiasi hicho? Je, viongozi wa uwongo kama hao si wahuni? Katika kumtumia mtu asiyefaa, tayari wamefanya kosa kubwa, na kisha wanaongezea kosa lao kwa kutowahi kuuliza, kuchunguza, au kukagua kazi ya mtu huyu, na kwa kutosimamia au kuitazama. Wanachofanya tu ni kuendelea kumvumilia mtu huyu akitenda kwa kutojali na kufanya maovu. Hivi ndivyo viongozi wa uwongo hufanya kazi. Wakati wowote kipengele cha kazi kinapokosa watu, viongozi wa uwongo kwa wa wepesi wa moyo hupanga mtu wa kukiwajibikia na hilo huwa ndio mwisho wake; kamwe hawakagui kazi, au kwenda mahali pa kazi ili kuwasiliana na mtu huyo, kumtazama, na kujaribu kujua zaidi kumhusu. Katika maeneo fulani mazingira hayafai kwa kukutana na kutumia muda na mtu huyo, lakini ni lazima uulize kuhusu kazi yake, na kuuliza maswali kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuhusu kile amekuwa akifanya, na jinsi amekuwa akikifanya—unaweza kuwauliza akina ndugu na dada, au mtu aliye karibu naye. Je, si hili linawezekana? Lakini viongozi wa uwongo hata hawasumbuki kuuliza maswali yoyote, hivyo ndivyo wanavyojiamini. Katika kazi yao, wao hufanya mikutano na kuhubiri mafundisho tu, na mikutano inapoisha na kazi imepangwa, hawafanyi kingine chochote; hawaendelei kufuatilia au kujua iwapo mtu waliyemchagua anaweza kufanya kazi ya utendaji. Mwanzoni, hukumwelewa mtu huyo, lakini kulingana na ubora wake wa tabia na dhihirisho zake za juu juu na shauku yake, ulihisi kwamba anafaa kwa kazi hii na hivyo ukamtumia—hakuna ubaya katika hili, kwa sababu hakuna anayejua jinsi watu watakavyokuwa baadaye. Lakini baada ya kumpandisha cheo, je, hupaswi kufuatilia na kuchunguza iwapo anafanya kazi ya utendaji, jinsi anavyofanya kazi, na iwapo amekuwa akifanya kazi kijuujuu, kwa ujanja, au kwa ulegevu? Hii hasa ndiyo kazi unayopaswa kuwa ukifanya, lakini huifanyi hata kidogo, huchukui jukumu lolote. Wewe ni kiongozi wa uwongo, na unapaswa kutimuliwa na kuondoshwa.

Viongozi wa uwongo hufanya kosa kubwa, ambalo ni kwamba baada ya kuwapandisha watu cheo, wao huwaelezea kazi, kisha wanaropoka mafundisho fulani, wao hutoa maneno machache ya himizo na kuishia hapo, bila kamwe kufuatilia au kushiriki katika kazi mahususi. Mkisema kwamba mna ubora duni wa tabia na mnakosa kuwang’amua watu, basi mnaweza kufuatilia na kujua jinsi kazi mahususi zinavyoendelea, na mnaweza kuielewa hali kikamilifu. Hata hivyo, viongozi wa uwongo hawafuatilii na kujua jinsi kazi inavyoendelea hata kidogo. Chukua uchapishaji wa vitabu, kwa mfano, ambayo ni kazi mahususi. Kiongozi wa uwongo alimpa mtu jukumu la kusimamia kazi hii, lakini hakumkagua hata mara moja katika nusu mwaka. Matokeo yake, baada ya miezi sita, vitabu vyote vilivyochapishwa vilikuwa na kasoro—hali ya shaghalabaghala iliyoje! Hivi ndivyo viongozi wa uwongo walivyo—hawafanyi kazi yoyote mahususi hata kidogo. Unapaswa kufanya nini ikiwa unapanga kuchapisha kitabu? Ni lazima kwanza umpe jukumu msimamizi anayefaa, na kisha usimamie na ukague jinsi anavyofanya kazi vizuri, na iwapo anaweza kuiharibu. Ni lazima usimamie na ufuatilie kazi, na utatue matatizo moja kwa moja ukigundua kwamba kuna yoyote—ni hili tu linaloweza kuhakikisha kwamba hakuna matatizo yanayotokea. Lakini viongozi wa uwongo hawafanyi hivi. Wanafikiri kwamba majukumu yao ni kuwaropokea tu watu mafundisho, na kuwafanya waelewe mafundisho, na kwamba mradi watu wanaelewa mafundisho, matatizo yanaweza kutatuliwa. Kwa hivyo, wanazingatia tu kuropoka mafundisho na kusema kauli mbiu, na hawashiriki katika kazi mahususi. Kwa maoni ya viongozi wa uwongo, wanafikiri kwamba si jukumu lao kushiriki katika kazi mahususi, na kwamba hili linapaswa kuwa jukumu la watu walio chini yao. Basi, wao wenyewe hufanya nini? Wao huamrisha hali yote wakiwa juu na kuwa warasimu. Haijalishi ni kazi gani, hawapo wala hawashiriki katika kazi hiyo. Baada ya kuwaambia watu kanuni, wakiulizwa kuhusu masuala ya kina au njia mahususi, watasema, “Kazi mahususi ni juu yenu, mimi sielewi mambo haya.” Kwa hivyo, hawajui jinsi wale walio chini yao wanavyoendelea na kazi. Kuhusu iwapo msimamizi ana uwezo na anaweza kuibeba kazi, au ubinadamu wake ukoje, au iwapo ni mtu anayefuatilia ukweli, au iwapo anawajibika katika kutekeleza wajibu wake, au iwapo anafanya kazi kijuujuu au anafanya mambo maovu bila kujizuia, au iwapo kuna ucheleweshaji wa kazi, na kadhalika—viongozi wa uwongo hawajui lolote kati ya haya, wanazurura tu kama warasimu wa dunia isiyoamini, wasiofanya kazi yoyote ya utendaji. Katika makanisa wanayofanyia kazi, viongozi wa uwongo hawajui wakati wasimamizi wengine wamesimamisha kazi, au wakati wasimamizi wengine wanaanzisha falme zao huru, au wakati wasimamizi wengine hawatimizi wajibu wao ipasavyo na badala yake wao hishinda siku nzima wakila, kunywa na kujifurahisha, na hata watafumbia macho wakati wasimamizi wengine wana ubora duni sana wa tabia, ufahamu uliopotoka, na hawawezi kufanya kazi hata kidogo. Viongozi wa uwongo kama hao ni maganda matupu tu, wao ni viongozi kwa jina tu, na hawafanyi kazi yoyote yenye kiini ya kiongozi. Kwa juujuu, viongozi hawa wa uwongo huonekana wenye tabia njema. Wao huwapa wasimamizi jukumu kwa kila kipengele cha kazi, wao huwaita watu hawa kwenye mkutano mara kwa mara, na hutumia muda wao uliosalia katika sehemu moja wakishiriki katika ibada za kiroho, wakiomba, wakisoma maneno ya Mungu, wakisikiliza mahubiri, wakijifunza nyimbo za sifa, na wakiandika mahubiri yao wenyewe. Kuna baadhi ya viongozi wa uwongo ambao hata hawatoki vyumbani mwao kwa wiki nzima. Pia kuna viongozi wa uwongo wasiofanya lolote ila kufanya mikutano ya mtandaoni, bila kwenda kamwe mahali pa kazi ili kuelewa hali. Ndugu na dada hawawaoni wao ana kwa ana kwa muda mrefu, na hawana habari kuhusu jinsi uzoefu wa maisha au kimo cha viongozi hao wa uwongo vilivyo. Wakati wa mikutano, viongozi wa uwongo hushughulikia tu baadhi ya mambo ya jumla, lakini kuhusu kile ambacho kila msimamizi anafanya, na iwapo watu waliowapandisha cheo na kuwasitawisha wanafaa kwa kazi waliyopewa, au jinsi mtazamo wa watu hawa ulivyo katika kutekeleza wajibu wao, au iwapo wako makini na wanachunguza kwa undani katika kazi yao, au kama wako hasi na wanafanya kazi kijuujuu, au iwapo watu hawa wanafuata njia sahihi, au iwapo ni watu wenye haki, viongozi wa uwongo hawajali au kuuliza kuhusu lolote kati ya masuala haya, na hawataki kuyajua pia. Je, si asili ya tatizo hili ni nzito? (Ndiyo.)

Nyumba ya Mungu inahitaji watu wenye talanta wanaoelewa fani fulani za kitaaluma na walio na ustadi fulani, na itawasitawisha watu hawa kujifunza taaluma hizo ili waweze kutekeleza wajibu katika nyumba ya Mungu. Je, mnadhani viongozi wa uwongo huwatafuta watu wa aina gani? Wao huwakusanya pamoja vijana wote ambao wameenda katika chuo kikuu na wamewafuata wazazi wao katika kumwamini Mungu, na wanaangalia ni nani msemaji hodari na nani anayependa kujionyesha, na kuwaambia, “Nyumba ya Mungu inataka kuwasitawisha ninyi; ninyi ni jeshi la akiba na nguvu mpya.” Kisha, wao huwapa watu hawa jukumu la kutekeleza wajibu. Kwa kweli, watu hawa hawajawahi kutekeleza wajibu, wanakosa uzoefu wa aina mbalimbali, na hawaelewi ukweli hata kidogo. Lakini viongozi wa uwongo huwapendelea na kuwapenda, kwa hivyo wanaanza kuwasitawisha. Wao huwapa watu hawa jukumu la kutekeleza wajibu kulingana na utaalamu unaowafaa kujifunza; wengine wanapewa kazi ya maandishi, wengine wanapewa kazi ya utengenezaji filamu, wengine wanapewa kazi ya kutengeneza video, na wengine wanapewa kazi ya kuwa waigizaji. Kwa viongozi wa uwongo, mradi watu hawa wana wajibu wa kutekeleza, inatosha. Viongozi wa uwongo hawachunguzi iwapo watu hawa wanapenda ukweli au iwapo wanaweza kukubali ukweli, wala hawachunguzi kile ambacho watu hawa wanafuatilia au ni malengo gani waliyo nayo. Mwishowe, ni nini hutokea? Baadhi ya watu hao huondoshwa. Hii ni kwa sababu wao ni wapotovu na wasiojizuia, na wanafuatilia mitindo ya kidunia, na wao hutumia siku zao wakijipamba na kuchumbiana ovyo na wengine, na hawaelewi sheria zozote au hawana adabu hata kidogo—ni dhahiri kwamba wao ni wasioamini na watu wa mataifa. Hawashughulikii kazi yao ipasavyo wanapotekeleza wajibu wao, na wanafanya kila kitu kwa njia ya kijuujuu, lakini viongozi wa uwongo hawawezi kuona hili hata kidogo. Je, si viongozi wa uwongo ni vipofu wa macho? (Ndiyo.) Ni nini husababisha upofu huu wa macho? Je, si ni kwa sababu viongozi wa uwongo ni vipofu wa moyo? Upofu wa macho na upofu wa moyo ni sifa mbili bainifu za viongozi wa uwongo. Ingawa macho yao yako wazi, viongozi wa uwongo hawawezi kuelewa chochote au kumng’amua mtu yeyote—yaani, macho yao yamepofuka. Katika mioyo yao, hawana upambanuzi au maoni juu ya mtu yeyote au kitu chochote, na haijalishi wanaona nini, hawana uwezo wa kutofautisha lililo sahihi na lisilo sahihi, na hawana mitazamo, maoni, wala maelezo—hii ni hali mbaya ya kuwa vipofu wa moyo. Viongozi wa uwongo wote ni watu ambao wamemwamini Mungu kwa miaka mingi na mara nyingi husikiliza mahubiri, kwa nini basi hawawezi kuwatambua wasioamini hao? Huu ni uthibitisho zaidi kwamba viongozi wa uwongo wana ubora duni sana wa tabia, kwamba hawawezi kuufahamu ukweli, na kwamba haijalishi wanasikia ukweli mwingi kiasi gani, haina faida, na hawauelewi. Wao ni vipofu wa macho na moyo, na hawawezi kabisa kuwatambua watu. Wangewezaje kufaa kuwa viongozi au wafanyakazi kanisani? Wanaamini kwamba wazungumzaji wazuri ni watu wenye talanta, na kwamba watu wanaoweza kuimba na kucheza densi pia ni watu wenye talanta; wanapoona watu wanaovaa miwani au watu ambao wameenda chuo kikuu, wanawachukulia kuwa watu wenye talanta, na wanapoona watu wenye hadhi katika jamii, watu walio matajiri, watu wanaojua kufanya biashara na kushiriki katika vitendo vya udanganyifu, na watu wanaofanya kazi za aina fulani muhimu katika jamii, viongozi wa uwongo wanafikiri kuwa wao ni watu wenye talanta. Wanaamini kwamba nyumba ya Mungu inapaswa kuwasitawisha watu wa aina hii. Hawaangalii sifa za watu hawa au iwapo imani yao katika Mungu ina msingi, na sembuse kuangalia mtazamo ambao watu humchukulia Mungu na ukweli. Wanaangalia tu hadhi ya kijamii ya watu na malezi yao. Je, si ni upuuzi kwa viongozi wa uwongo kuwaona watu na vitu kwa njia hii? Viongozi wa uwongo huwaona watu na vitu kwa njia sawa na wasioamini—mtazamo wao ni ule ambao wasioamini huwa nao kuelekea mambo. Hii inatosha kuthibitisha kwamba viongozi wa uwongo si watu wanaopenda na kuelewa ukweli, na kwamba wanakosa upambanuzi wowote. Je, si wao ni wa juu juu sana? Wao ni vipofu kweli—na sana!

Hapo zamani, nilikutana na kiongozi wa uwongo ambaye alizungumza na kucheka nilipokuwa nikizungumza naye, lakini punde tu nilipomwuliza kuhusu kazi, aliyakazia macho yake angani kwa njia ya ganzi na kijinga, na hakujibu lolote nililomwambia. Ubora wa tabia wa mtu huyu ni duni mno kiasi kwamba hawezi kutumika. Si ajabu kwamba hakuelewa lolote nililomwambia na hakuweza kulitekeleza. Chochote nilichozungumza naye, aliendelea kusema, “Nilifanya mkutano na niliikagua kazi siku chache zilizopita.” Nikasema, “Je, kweli huna kazi nyingine yoyote mbali na kufanya mikutano? Kuna kazi nyingi sana za kufanywa kanisani, kwa nini hutafuti kitu kingine cha kufanya?” Akasema: “Je, kuwa kiongozi au mfanyakazi si ni kufanya mikutano tu? Hakuna kingine cha kufanya isipokuwa kufanya mikutano, sijui jinsi ya kufanya kitu kingine chochote!” Hii inaonyesha kwamba alikuwa amekusudiwa kuwa kiongozi wa uwongo alipochukua wadhifa huo, na kwamba hawezi kufanya kazi yoyote ya utendaji, kwa sababu ubora wake wa tabia ni duni mno! Ubora duni sana wa tabia husababisha upofu wa macho na upofu wa moyo. Upofu wa macho unamaanisha nini? Unamaanisha kwamba haijalishi kile anachoona mtu, hawezi kugundua matatizo mahususi, na hivyo macho yake hayana faida yoyote. Upofu wa moyo unamaanisha nini? Unamaanisha kwamba haijalishi ni kitu gani kinachotokea, mtu hatambui na anashindwa kuelewa tatizo lililomo humo, na hawezi kuona kiini cha tatizo lenyewe—hii ndiyo maana ya kuwa mpofu wa moyo. Ikiwa mtu ni mpofu wa moyo, basi amekwisha kabisa. Viongozi wa uwongo ni vipofu wa macho na moyo kwa njia hii. Je, mnasema kwamba viongozi wa uwongo huhisi vibaya wanaposikia maneno haya? Wa huwaza, “Macho yangu ni makubwa, lakini Yeye anasema mimi ni mpofu wa macho; na nina nia njema moyoni, lakini Yeye anasema mimi ni mpofu wa moyo—ufafanuzi Wake si sahihi sana, au siyo? Kwa nini usiniite tu kiongozi wa uwongo? Kwa nini uongeze kwamba mimi pia ni mpofu wa macho na moyo?” Kama singeeleza kwa njia hiyo, kwa kuangalia ubora wa tabia wa viongozi wa uwongo, wangeweza kutambua kwamba wana ubora duni wa tabia? (Hapana, wasingeweza.) Je, kusema kwamba viongozi hawa wa uwongo ni vipofu wa macho na moyo hakuelezi jambo hili kikamilifu? Kwa mfano, tuseme kwamba mpinga Kristo anaanzisha ufalme wake huru kanisani. Lakini viongozi wa uwongo husema, “Mtu huyu ana uwezo mkubwa. Hapo awali alikuwa profesa wa chuo kikuu, na anazungumza kwa uwazi, kimantiki, na kwa njia iliyopangwa vizuri na fasaha. Isitoshe, haogopi hadhara, haijalishi ni hadhara kubwa kiasi gani.” Ni wazi kabisa kwamba mtu wanayemzungumzia ni Mfarisayo anayeanzisha ufalme wake huru, na bado viongozi wa uwongo wanampongeza. Je, huo si upofu wa macho? (Ndiyo.) Ikiwa mtu anaimba nje ya tuni na wewe husikii, je, hilo linaweza kuchukuliwa kuwa upofu wa macho? (Hapana.) Hilo ni suala la kitaaluma, wala si suala la ubora wa tabia. Lakini baada ya kusikiliza ukweli mwingi, viongozi wa uwongo hawawezi hata kuwatambua wapinga Kristo, na hawawezi kutambua iwapo ubinadamu wa mtu ni mzuri au mbaya, au iwapo mtu anafaa kupandishwa cheo na kusitawishwa na nyumba ya Mungu, au iwapo mtu ni asiyeamini au iwapo mtu huyo anamwamini Mungu kwa dhati, na hawawezi kutambua iwapo mtu ni mwaminifu katika kutekeleza wajibu wake—basi, wamepata nini kutokana na kusikiliza mahubiri kwa miaka hii yote? Hawajapata ukweli wowote, ambayo ina maana kwamba wao ni wajinga vipofu; hivi ndivyo viongozi wa uwongo walivyo vipofu. Wanaamini kwamba kazi kuu ya kiongozi ni kuweza kutoa mahubiri, na kuhubiri kwa masaa mawili au matatu, na kwamba mradi wanaweza kusema maneno na mafundisho, kusema kauli mbiu, na kuwatia watu moyo, wamefikia kiwango kinachohitajika kama viongozi, wanaweza kuibeba kazi, wana uhakika wa ukweli, na Mungu ameridhika nao. Haya ni mantiki ya aina gani? Kwa sababu viongozi wa uwongo hawaelewi ukweli na wana ubora duni sana wa tabia, na ni vipofu wa macho na moyo, hawana uwezo wowote wa kutambua aina mbalimbali za watu, na hawawezi kuwang’amua watu wa aina mbalimbali. Basi, je, wanaweza kuwatumia watu wa aina mbalimbali kwa njia ya busara? (Hapana.) Wana mkakati mmoja tu: Wale ambao hapo awali walikuwa walimu wanapewa jukumu la kutoa mahubiri, wale ambao wamehusika katika biashara ya nje wanapewa jukumu la kushughulikia mambo ya jumla, wale wanaoweza kuzungumza Kiingereza wanapewa jukumu la kuwa watafsiri, na yeyote aliye msemaji hodari na asiye na haya anapewa jukumu la kuhubiri injili; wale walio waoga wanapewa jukumu la kuandika makala za ushuhuda wa kupitia wakiwa nyumbani, wale walio jasiri na wanapenda kuigiza wanateuliwa kuwa waigizaji, na wale wanaotaka kuwa maafisa wanateuliwa kuwa viongozi au waelekezi. Hivi ndivyo viongozi wa uwongo huwatumia watu, bila kanuni zozote.

Ndani ya upeo wa kazi ambao viongozi wa uwongo wanawajibikia, mara nyingi kuna baadhi ya watu wanaofuatilia ukweli kwa dhati na kutimiza vigezo vya kupandishwa cheo na kusitawishwa ambao hupuuzwa. Baadhi ya watu hawa huhubiri injili, na wengine hupewa wajibu wa kuwa wenyeji. Ukweli ni kwamba wote wana ubora wa tabia, na wanaelewa ukweli fulani, na wanastahili kusitawishwa kama viongozi na wafanyakazi, ni kwamba tu hawapendi kujionyesha au kuvutia umakini wa watu wengine. Na bado, viongozi wa uwongo hawawatambui watu hawa hata kidogo. Hawashirikiani nao au kuuliza kuwahusu, na kamwe hawawasitawishi watu wenye talanta kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Wao huzingatia tu kuwanasa wale wanaojipendekeza kwao, ili kutosheleza tamaa zao za ubinafsi. Matokeo yake, watu hao wanaofuatilia ukweli kwa dhati hawapandishwi cheo na kusitawishwa, ilhali wale wanaopenda kujionyesha, walio wasemaji hodari, wanaojua kujipendekeza kwa watu, na wanaopenda umaarufu, faida, na hadhi—wote wanapandishwa cheo, na hata wale ambao wamekuwa maafisa, Maafisa Wakuu Watendaji wa kampuni, au ambao wamesomea usimamizi wa mashirika katika jamii wanapewa nyadhifa muhimu. Bila kujali iwapo watu hao ni waumini wa kweli au la, au iwapo ni watu wanaofuatilia ukweli au la, kwa vyovyote vile, hao ndio watu wanaopandishwa cheo na kutumika ndani ya upeo wa kazi ambao viongozi wa uwongo wanawajibikia. Je, huku ni kuwatumia watu kulingana na kanuni? Je, viongozi wa uwongo kuwapandisha cheo watu wa aina hii tu si ni sawa kabisa na jinsi jamii isiyoamini ilivyo? Katika kipindi ambacho viongozi wa uwongo wanafanya kazi, wale wanaoweza kufanya kazi ya utendaji wanapotekeleza wajibu wao, walio na hisia ya haki, na wanaopenda ukweli na vitu chanya—hawapandishwi cheo wala kusitawishwa, na ni vigumu kwao kupata fursa za mafunzo. Badala yake, ni wale walio wasemaji hodari, wanaopenda kujionyesha na wanaojua kujipendekeza kwa watu, na vilevile wale wanaopenda umaarufu, faida, na hadhi, ndio wanaopewa nyadhifa muhimu. Watu hao huonekana kuwa werevu kiasi, lakini kwa kweli hawana uwezo wa kufahamu, wana ubora mbaya sana wa tabia na ubinadamu duni, hawabebi mzigo halisi kwa ajili ya wajibu wao, na hawastahili kusitawishwa hata kidogo. Hata hivyo, ni wao ndio wanaoshikilia nyadhifa za viongozi na wafanyakazi kanisani. Matokeo yake ni kwamba kazi nyingi za kanisa haziwezi kuanzishwa vizuri kwa wakati unaofaa, au hupiga hatua polepole, na mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu huchukua muda mrefu sana kutekelezwa. Hizi ndizo athari na matokeo yanayosababishwa kwa kazi ya kanisa na viongozi wa uwongo kuwatumia watu isivyofaa.

Viongozi wengi wa uwongo wana ubora duni wa tabia. Ingawa wanaonekana kuwa wasemaji hodari, hawana uwezo wowote wa kuufahamu ukweli, kiasi kwamba hawana ufahamu wa kiroho. Wao ni vipofu wa macho na moyo, hawawezi kung’amua jambo lolote na hawaelewi ukweli hata kidogo, ambalo lenyewe ni tatizo la kuangamiza. Wana tatizo lingine, zito zaidi bado, ambalo ni kwamba wanapokuwa wameelewa na kuyashika maneno na mafundisho machache na wanaweza kusema kauli mbiu chache, wanafikiri kwamba wana uhalisi wa ukweli. Kwa hivyo kazi yoyote wanayofanya na yeyote wanayemchagua kumtumia, hawatafuti kanuni za ukweli, na hawashiriki na wengine, na sembuse kuzingatia mipango ya kazi na kanuni za nyumba ya Mungu. Wanajiamini sana, daima wanaamini kwamba mawazo yao ni sahihi na wao hufanya chochote wanachotaka. Matokeo yake, wanapokumbana na ugumu fulani au hali isiyo ya kawaida, wanachanganyikiwa. Isitoshe, mara nyingi wao huamini kimakosa kwamba, kwa kuwa wamefanya kazi kwa miaka mingi katika nyumba ya Mungu na wana uzoefu wa kutosha wa kutumikia kama viongozi humo, wanajua jinsi ya kuifanya kazi ya kanisa iendeshwe na kuendelezwa. Wanaonekana kuwa wameelewa mambo haya, lakini kwa kweli, hawajui kabisa jinsi ya kufanya kazi yoyote. Wanafanya kazi ya kanisa kwa njia yoyote wanayopenda, wakifuata mawazo na dhana zao wenyewe, uzoefu na mazoea yao, na kanuni zao. Hili husababisha fujo na mchafuko katika vipengele mbalimbali vya kazi ya kanisa, na kusababisha visitoe matokeo yoyote halisi. Ikiwa kuna watu wawili au watatu katika timu wanaouelewa ukweli na wanaoweza kufanya kazi kidogo ya utendaji, wanaweza kudumisha hali ya kawaida katika kazi ya timu hiyo. Hata hivyo, hili halihusiani kabisa na kiongozi wao wa uwongo. Sababu ya kazi kuweza kufanywa vizuri ni kwamba kuna watu wema wachache katika timu wanaoweza kufanya kazi kidogo ya utendaji na kuiweka kazi katika mkondo wake; haimaanishi kwamba kiongozi wao wa uwongo amefanya kazi ya utendaji. Hakuna kazi yoyote inayoweza kufanywa bila kuwa na watu wema wachache kama hawa wanaosimamia. Viongozi wa uwongo hawawezi kabisa kufanya kazi yao, na hawana dhima yoyote wanayoitimiza. Kwa nini viongozi wa uwongo huivuruga kazi ya kanisa? Sababu ya kwanza ni kwamba viongozi wa uwongo hawaelewi ukweli, hawawezi kushiriki kuhusu ukweli ili kutatua matatizo, na hawatafuti jinsi ya kutatua matatizo, na kusababisha matatizo kurundikana na kuikwamisha kazi ya kanisa. Ya pili ni kwamba viongozi wa uwongo ni vipofu, na hawawezi kuwatambua watu wenye talanta. Hawawezi kuwabadilisha wasimamizi wa timu ipasavyo, jambo ambalo husababisha baadhi ya kazi kutokuwa na mtu anayefaa wa kusimamia, na kuifanya ikwame. Ya tatu ni kwamba viongozi wa uwongo hutenda sana kama warasimu. Hawasimamii au kuelekeza kazi, na pale penye sehemu dhaifu katika kazi, hawashiriki kwa wao wenyewe kuchukua hatua au kutoa mwongozo katika mambo mahususi ya kazi. Tuseme, kwa mfano, kwamba katika kipengele fulani cha kazi, watu kadhaa wanaofanya kazi ni waumini wapya wasio na msingi imara, hawaelewi ukweli, hawaijui vizuri fani ya kazi, na hawajazielewa vizuri kanuni za kazi. Kiongozi wa uwongo, akiwa kipofu, hawezi kuona matatizo haya. Anaamini kwamba ni sawa mradi tu mtu fulani anafanya kazi; haijalishi kama inafanywa vizuri au vibaya. Hajui kwamba popote palipo na sehemu dhaifu katika kazi ya kanisa, anapaswa kuwa anaifuatilia, akifanya ukaguzi, na kutoa mwongozo, kwamba anapaswa kushiriki yeye mwenyewe katika kutatua matatizo na kuwaunga mkono wale wanaotekeleza wajibu wao hadi waelewe ukweli, waweze kutenda kulingana na kanuni, na kuingia katika mkondo sahihi. Ni katika hatua hii tu ndipo hawahitaji kuwa na wasiwasi sana. Viongozi wa uwongo hawafanyi kazi kwa njia hii. Wanapoona kuna mtu wa kufanya kazi, hawajali tena. Hawaulizi maswali, haijalishi kazi inaendeleaje. Pale penye sehemu dhaifu katika kazi, au msimamizi aliye na ubora duni wa tabia, hawatoi mwongozo wao binafsi kuhusu kazi, na hawashiriki katika kazi wao wenyewe. Na msimamizi anapoweza kuibeba kazi, viongozi wa uwongo hukagua mambo au kutoa mwongozo wao binafsi kwa kiasi kidogo zaidi; wanajistarehesha tu, na hata kama mtu ataripoti tatizo, hawaulizi kulihusu—wanafikiri hakuna haja. Viongozi wa uwongo hawafanyi yoyote kati ya kazi hii mahususi. Kwa muhtasari, viongozi wa uwongo ni wapotovu wasiofanya hata chembe ya kazi ya utendaji. Wanaamini kwamba kwa kazi yoyote, mradi tu mtu fulani anasimamia na wafanyakazi wote wako tayari kushika kazi, mambo huwa yamekwisha. Wanafikiri kwamba wanachopaswa kufanya tu ni kufanya mkutano mara kwa mara, na kuuliza maswali tatizo linapotokea. Huku wakifanya kazi kwa njia hii, viongozi wa uwongo bado wanaamini wanafanya kazi nzuri na wanajipongeza wenyewe. Wao huwaza, “Hakuna matatizo na kipengele chochote cha kazi. Wafanyakazi wote wamepangwa kikamilifu, na wasimamizi wako tayari. Mimi ni mzuri sana katika kazi hii, nina talanta sana!” Je, si huku ni kutokuwa na haya? Wao ni vipofu wa macho na moyo kiasi kwamba hawawezi kuona kazi zozote za kufanywa na hawawezi kugundua matatizo yoyote. Katika baadhi ya maeneo, kazi imekwama, lakini wao wako pale, wameridhika, wakiwaza, “Ndugu na dada wote ni vijana, wote ni damu mpya. Wanatekeleza wajibu wao kwa ari na moto; hakika wanaweza kufanya kazi vizuri.” Kwa kweli, vijana hawa hawana uzoefu, hawana uelewa wa ustadi wowote wa kitaaluma. Ni lazima wajifunze wanapoendelea. Ni sawa kusema kwamba hawajui jinsi ya kufanya kazi yoyote bado: Wengine wanaweza kuelewa kidogo, lakini si wataalamu, na hawazielewi kanuni, na wanapokuwa wamefanya kazi, inahitaji kusahihishwa mara kwa mara au hata kurudiwa mara kwa mara. Pia kuna baadhi ya vijana ambao hawajapata mafunzo na hawajapitia upogolewaji. Wao ni duni na wavivu mno, na wenye tamaa ya starehe; hawakubali hata ukweli kidogo, na wanapoteseka kidogo, wananung’unika bila kukoma. Wengi wao ni wapotovu wanaofanya kazi kijuujuu na wanaotamani starehe. Kwa vijana wa aina hii ni lazima ushiriki na wao kabisa mara kwa mara kuhusu ukweli, na hata zaidi ni lazima uwapogoe. Vijana hawa lazima wawe na mtu anayewasimamia na kuwatazama. Lazima kuwe na kiongozi au mfanyakazi pale wa kuwajibika binafsi kwa kazi yao na kutoa usimamizi na mwongozo wa kibinafsi. Hapo ndipo kazi yao inaweza kuzaa matunda kiasi. Ikiwa kiongozi au mfanyakazi ataondoka mahali pa kazi na asishughulikie kazi au kuuliza kuihusu, watu hawa watasambaratika, na utendaji wao wa wajibu wao hautazaa matunda hata kidogo. Lakini viongozi wa uwongo hawawezi kuliona jambo hili kwa undani. Wanamwona kila mtu kama ndugu na dada, kama watu walio watiifu na wanyenyekevu, na hivyo wanawaamini sana, na kuwapa kazi kisha hawafuatilii tena—huu ndio ushahidi bora zaidi wa upofu wa macho na moyo wa viongozi wa uwongo. Viongozi wa uwongo hawaelewi ukweli hata kidogo, hawawezi kuyaona mambo kwa uwazi, na hawawezi kufichua matatizo yoyote, lakini wanafikiri wanaendelea vizuri. Wanashinda siku nzima wakiwaza nini? Wanawaza jinsi ya kutenda kama warasimu na kufurahia manufaa ya hadhi. Viongozi wa uwongo, kama watu wasiofikiri, hawajali hata kidogo nia ya Mungu. Hawafanyi kazi halisi, lakini wanasubiri nyumba ya Mungu iwasifu na kuwapandisha cheo. Kwa kweli, hawana aibu!

Viongozi wa uwongo ni bure kabisa wanapofanya kazi yao, na haina chochote cha kusifiwa kuwahusu. Wanashindwa kushika kanuni zinazohusiana na taswira kamili, sembuse zile zinazohusiana na kazi yenye maelezo mahsusi ya kina. Kwa mfano, watu wengine wana weledi mkubwa lakini ubinadamu wao ni duni kupita kiasi, ilhali wengine hawana matatizo katika ubinadamu wao, lakini wana ubora duni wa tabia na weledi duni. Linapokuja suala la jinsi watu hawa wanavyopaswa kutumiwa na kugawiwa kazi kwa njia inayofaa, viongozi wa uwongo hawajui hata kidogo zaidi kuhusu mambo haya maalum na ya kina zaidi. Kwa hivyo wakati wowote viongozi wa uwongo wanapoulizwa kama wamempata yeyote mwenye ubora mzuri kiasi wa tabia anayeweza kukuzwa, wanasema bado hawajampata yeyote. Viongozi wa uwongo ni vipofu sana—wanawezaje kumpata mtu yeyote? Ukimuuliza Dada fulani na fulani yukoje, watasema anatamani starehe za mwili; ukimuuliza Kaka fulani yukoje, watasema mara nyingi yeye huwa hasi; ukiwauliza kuhusu mtu mwingine, watakuambia mtu huyo hajamwamini Mungu kwa muda mrefu na hana msingi. Machoni pao, hakuna anayefikia kiwango kinachostahili. Wanatazama tu kasoro, mapungufu, na makosa ya watu wengine; hawawezi kuangalia kama mtu anapatana na kanuni za nyumba ya Mungu za kuteua na kukuza, au kama yeye ni mgombea anayefaa kuteuliwa na kukuzwa. Hawawezi kutambua ni nani anayefaa kweli kuteuliwa na kukuzwa, lakini wao huwapandisha cheo wale wasiotimiza matakwa na kanuni za nyumba ya Mungu kwa shauku na kasi kubwa. Wanawateua wanawake wote matajiri, wanaume wenye mali, na wana na binti wa familia za kitajiri kanisani, na pia wale ambao wamekuwa maafisa ulimwenguni, wale walio na ufasaha wa kuongea, na wale wanaojua kudanganya na kutapeli—kwa vyovyote vile, wao humpandisha cheo yeyote aliyejulikana na mwenye hadhi ulimwenguni na yeyote anayependa kuwa kitovu cha angalizo. Wanaamini kwamba watu hawa ndio watu pekee wenye talanta, na hawamtambui wala kumteua hata mtu mmoja ambaye kwa kweli ana uwezo wa kuelewa na anaweza kuukubali ukweli. Itakuwa vigumu zaidi kwa kiongozi wa uwongo kuipa nyumba ya Mungu talanta moja ya kweli inayostahili kuliko yeye kuruka hadi kwenye mwezi. Kwa mfano, tuseme kwamba kwa sasa nyumba ya Mungu inahitaji watu wenye talanta kwa ajili ya kazi ya maandishi—kuna mtu wa aina hii katika kanisa ambalo kiongozi wa uwongo anasimamia, lakini kiongozi huyo wa uwongo hapendekezi jina la mtu huyu. Kiongozi huyo wa uwongo anapoulizwa kwa nini hakumteua au kumkuza mtu huyo, anasema: “Mtu huyo alifanya uzinzi mara mbili alipokuwa katika chuo kikuu, lakini hajafanya tena tangu afunge ndoa. Sikujua kama anapaswa kuteuliwa au la.” Hii ni kauli ya aina gani? Je, unaweza kuhakikisha kwamba watu matajiri na wenye nguvu unaowateua hawajawahi kufanya uzinzi? Je, watu hao hawafanyi hivyo hata zaidi? Kwa nini huoni hilo? Viongozi wa uwongo hujifanya wa kiroho, wakijidai kuwa wanajua kanuni fulani, na kutafuta visingizio vya kuhalalisha kutowateua wale wanaopaswa kuteuliwa na kukuzwa. Machoni pao, kila mtu ni duni kuliko wao. Mwishowe hutokea nini? Je, “watu wa tabaka la juu” na “watu wenye talanta” waliopandishwa cheo na viongozi wa uwongo wamesimama imara? Hatusemi kwamba watu hawa bila shaka si watu wema. Tunachofichua hasa ni kwamba kanuni ya viongozi wa uwongo ya jinsi wanavyowatendea watu ni kutumia mawazo ya kibinadamu kama kipimo chao, badala ya ukweli, na kwamba kanuni yao ya kuwateua na kuwakuza watu ni kufuata mawazo, dhana, na mapendeleo yao wenyewe, na kwa ukamilifu ndio mtazamo wa wasioamini, badala ya kutumia viwango vinavyohitajika vya nyumba ya Mungu kama kipimo chao. Kwa nini viongozi wa uwongo wanaweza kufanya hivi? Kwa sababu hawaelewi ukweli au nia ya Mungu, wanaweza kuwateua wale ambao hawafikii kabisa matakwa ya nyumba ya Mungu, wakazingatia kuwakuza, na kuwaacha washikilie kazi muhimu katika nyumba ya Mungu. Hiyo ndiyo kazi wanayoifanya viongozi wa uwongo. Waangalieni viongozi wa uwongo walio karibu nanyi; je, si hivi ndivyo wanavyofanya kazi na kuwatendea watu?

Kuna mtazamo fulani unaodhihirika mara kwa mara kwa viongozi wa uwongo: Wanafikiri kwamba wale wenye maarifa, wenye hadhi, na wale ambao wamekuwa maafisa ulimwenguni wote ni watu wenye talanta, na kwamba watu kama hao wanapaswa kukuzwa na kutumiwa na nyumba ya Mungu baada ya kuanza kumwamini Mungu. Wanawaheshimu na kuwaabudu watu hao kwa kweli—hata wao huwatendea kama jamaa na wanafamilia wao. Wanapowatambulisha watu hawa kwa wengine, mara nyingi wao huzungumzia jinsi ulimwenguni, walivyokuwa wakubwa wa kampuni fulani, au viongozi wa idara fulani ya serikali, au wahariri wa gazeti fulani, au wakurugenzi fulani katika idara ya usalama wa umma, au wao huzungumzia jinsi walivyo matajiri. Viongozi wa uwongo huwaona watu kama hao kuwa wa maana sana. Ninyi mnasemaje, je, viongozi wa uwongo wana ubora wa tabia? Je, si ni kweli kwamba wao hujifanya wa kiroho, na hawawezi kung’amua mambo? Viongozi wa uwongo wanafikiri kwamba kwa kuwa watu hawa walikuwa watu wenye talanta katika jamii, nyumba ya Mungu inapaswa kuwakuza na kuwapa jukumu muhimu la kutekeleza wanapokuja hapa. Je, mtazamo huu ni sahihi? Je, unapatana na kanuni za ukweli? Ikiwa watu hawa hawapendi ukweli hata kidogo, na hawana dhamiri na mantiki, je, wanaweza kukuzwa na kupewa jukumu muhimu na nyumba ya Mungu? Hawana sifa za kukuzwa. Ukweli kwamba walikuwa watu wenye talanta miongoni mwa wasioamini haimaanishi wao ni watu wenye talanta katika nyumba ya Mungu, lakini viongozi hawa wa uwongo hupenda kuwa maafisa, na hasa wao huwaabudu wengine ambao wamekuwa maafisa. Wakati wowote wanapowaona watu ambao wamekuwa maafisa au walikuwa na hadhi ulimwenguni, wao huwainamia na kujipendekeza kwa unyenyekevu mwingi, kama watumwa mbele ya bwana wao; wanatamani sana kuwaita mama au baba, au dada mkubwa au kaka mkubwa, na pia wanatamani kuwafanya watu hawa wateuliwe kuwa viongozi au wafanyakazi kanisani. Hebu Niambieni, je, hawa ni watu wanaofuatilia ukweli? Kuwa na hadhi kidogo na kufurahia sifa kiasi ulimwenguni kunamaanisha wao wanafaa kutumika kama kiongozi au mfanyakazi katika nyumba ya Mungu? Ikiwa hawaelewi ukweli na wamejawa na tabia za kiburi na majivuno, je, wanastahili kuwa kiongozi au mfanyakazi katika nyumba ya Mungu? Je, kuwateua watu kwa kuzingatia tu hadhi na sifa zao, na kupuuza sifa zao inapatana na kanuni? Je, viongozi wa uwongo wanajua ni watu wa aina gani ambao Mungu anawapenda, ni watu wa aina gani Anaowateua na kuwatumia? Mara kwa mara, mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu imesisitiza kwamba watu wanapaswa kuteuliwa na kukuzwa kulingana na viwango vitatu: Cha kwanza, ni lazima wawe na ubinadamu, dhamiri, na busara; cha pili, ni lazima wawe ni mtu anayependa ukweli na anayeweza kuukubali ukweli; na cha tatu, ni lazima wawe na kiwango fulani cha ubora wa tabia na wawe na uwezo wa kazi. Ni wale tu wanaotimiza viwango hivi vitatu ndio wanaoweza kuteuliwa na kukuzwa, na wana sifa za kuwa wagombea na kuwa viongozi au wafanyakazi. Kuwa na ubora wa tabia na talanta pekee hakufai hata kidogo. Sifa huja kwanza, na pili, ni muhimu kuweza kuukubali ukweli—hivi viwili ndivyo viwango muhimu zaidi. Watu waovu wasiopenda ukweli wakiteuliwa, matokeo yatakuwa ya madhara makubwa, kwa hivyo wale wasio na ubinadamu hawaruhusiwi kabisa kuteuliwa. Lakini viongozi wa uwongo huyapuuza matakwa ya nyumba ya Mungu. Wanawapochagua na kuwatumia watu, wao daima huzingatia kama mtu ana hadhi katika jamii, asili na cheo chake ni vipi, kama amepata elimu ya juu, na jinsi sifa yake ilivyo kuu katika jamii—hivi ndivyo vipengele wanavyovizingatia wanapowateua na kuwakuza watu. Je, hili linapatana na kanuni zilizowekwa na nyumba ya Mungu? Je, hili linapatana na ukweli wa maneno ya Mungu? Watu hao wenye hadhi katika jamii ni watu gani? Inaweza kusemwa kwamba wote ni watu wanaopigania mamlaka na hadhi kwa vyovyote vile, na kwamba wao ni wa Shetani. Ikiwa watashika mamlaka katika nyumba ya Mungu, je, nyumba ya Mungu bado ingekuwa kanisa la Mungu? Lengo la viongozi wa uwongo katika kuwateua watu walio wa Shetani kuwa viongozi ni lipi? Je, kutenda hivyo kunapatana na kanuni za nyumba ya Mungu za kuwakuza na kuwatumia watu? Je, si ni kuvuruga na kuiharibu kazi ya kanisa waziwazi? Uteuzi na ukuzaji wa watu usiofuata kanuni unaofanywa na viongozi wa uwongo ndio husababisha vurugu na usumbufu mkuu zaidi kwa kazi ya kanisa, na ni njia ya kumpinga Mungu.

Viongozi wa uwongo wana ubora duni sana wa tabia na hawana uwezo wa kuuelewa ukweli. Haijalishi wanasikiliza mahubiri mangapi au wanasoma maneno mangapi ya Mungu, bado hawaelewi kwa usafi, au kuuelewa ukweli, na haijalishi wamehubiri mafundisho kwa miaka mingapi, hawaelewi kile wanachosema, yote ni maneno matupu tu yasiyoeleweka! Wanaweza kukumbuka na kuhubiri mafundisho kidogo, kwa hivyo wanafikiri wana uhalisi wa ukweli, lakini hakuna chochote wanachofanya kinachohusiana na ukweli—hawa ni Mafarisayo halisi. Kwa nje inaonekana kwamba mara nyingi huwahubiria watu, na kusema mambo yanayosikika vizuri, kana kwamba wanauelewa ukweli, lakini kile wanachofanya ni kinyume na ukweli na kinapingana na ukweli. Pia wanadai kwamba wanamtumikia Mungu na kufanya kazi ya kanisa, ilhali kwa kweli kila kitu wanachofanya ni cha uhasama kabisa kwa Mungu. Viongozi wa uwongo hawawateui kamwe watu wenye talanta walio na manufaa kwa nyumba ya Mungu, na huwapuuza na kuwafumbia macho watu wanyoofu kiasi wanaofuatilia ukweli kwa kweli. Badala yake, wao huwapandisha cheo na kuwakuza wale wanaojipendekeza, wale walio walaini na wadanganyifu, na wale walio na tamaa ya makuu na matamanio ya kuchukua kazi kanisani. Matokeo ya yote haya ni kwamba, pindi watu hao wanapokuwa katika kazi kwa kipindi fulani, vipengele mbalimbali vya kazi ya kanisa husimama na kwa kweli huingia katika hali ya kupooza, na hivyo kazi ya kanisa huharibiwa mikononi mwa viongozi hawa wa uwongo. Je, si viongozi wa uwongo wa aina hii wanachukiza? Je, wanapaswa kutimuliwa? Ni lazima watimuliwe! Kila siku ya kuchelewa huathiri kazi ya kanisa kwa siku nzima. Baadhi ya viongozi wa uwongo, ingawa wanajua kwamba hawawezi kufanya kazi halisi, hawako tayari kujiuzulu kwa hiari, na kila mara wanatamani mno manufaa ya hadhi, na hata wangefika mbali kiasi cha kuiharibu kazi ya kanisa. Je, watu hawa wana hata chembe ndogo kabisa ya busara? Viongozi wa uwongo hawana uwezo wa kuelewa, wala vipaji na maarifa ya kweli, na si watu wanaofuatilia ukweli, na pia wanatamani manufaa ya hadhi—wao ni watu wasio na aibu; kwa hivyo ni lazima wasipandishwe vyeo na kukuzwa kabisa. Ikiwa unafikiri kwamba una ubora duni sana wa tabia, na kwamba huna uwezo wa kutofautisha mema na mabaya, na kwamba huna uwezo wa kuuelewa ukweli, basi chochote unachofanya, usizifuate tamaa zako za makuu na matamanio, na usitafakari jinsi ya kujitahidi kuwa afisa fulani kanisani—kuwa kiongozi wa kanisa—kuwa kiongozi si rahisi hivyo. Ikiwa wewe si mtu mnyoofu na huna upendo kwa ukweli, basi punde tu unapokuwa kiongozi, utakuwa mpinga Kristo au kiongozi wa uwongo. Wapinga Kristo na viongozi wa uwongo wote ni watu wasio na dhamiri na mantiki, na watu wanaoweza kutenda maovu na kusumbua kazi ya kanisa. Ingawa ni kweli kusema kwamba wapinga Kristo ni ibilisi na Mashetani, viongozi wa uwongo si watu wema pia; angalau, wao ni watu wasio na aibu waziwazi, wasio na dhamiri na mantiki. Je, kuna utukufu wowote katika kuwa kiongozi wa uwongo na kutimuliwa? Ni aibu, ni doa, na hakuna utukufu wowote kabisa kuhusiana na hilo. Kama una hisia ya mzigo kuhusu kazi ya kanisa, na unatamani kushiriki katika kazi hiyo, hili ni jambo jema; lakini ni lazima utafakari kama unauelewa ukweli, kama unaweza kushiriki ukweli ili kutatua masuala, kama unaweza kuitii kazi ya Mungu kweli, na kama unaweza kuitekeleza kazi ya kanisa ipasavyo kulingana na mipango ya kazi. Ikiwa unatimiza vigezo hivi, unaweza kugombea kuwa kiongozi au mfanyakazi. Ninachomaanisha kwa kusema hivi ni kwamba angalau, ni lazima watu wawe na hali ya kujielewa. Kwanza angalia kama unaweza kuwapambanua watu, kama unaweza kuuelewa ukweli na kufanya mambo kulingana na kanuni. Ikiwa unatimiza matakwa haya, unafaa kuwa kiongozi au mfanyakazi. Ikiwa huwezi kujipima, unaweza kuwauliza watu walio karibu nawe wanaokufahamu au walio karibu nawe. Wote wakisema kwamba huna ubora wa kutosha wa tabia wa kuwa kiongozi, na kwamba kufanya tu kazi yako ya sasa vizuri tayari kunatosha, basi unapaswa kujitambua haraka. Kwa kuwa una ubora duni wa tabia, usitumie wakati wako wote kutaka kuwa kiongozi—fanya tu kile unachoweza, tekeleza wajibu wako ipasavyo na kwa uhalisi, ili uweze kuwa na amani mawazoni. Hili, pia, ni jambo jema. Na ikiwa una uwezo wa kuwa kiongozi, ikiwa kweli una ubora wa tabia na talanta ya aina hiyo, ikiwa una uwezo wa kazi, na una mzigo, basi wewe ndiye hasa aina ya mtu mwenye talanta ambaye nyumba ya Mungu inamkosa, na hakika utapandishwa cheo na kukuzwa; lakini kuna wakati wa Mungu katika mambo yote. Tamaa hii—tamaa ya kuteuliwa—si tamaa ya makuu, lakini ni lazima uwe na ubora wa tabia, na utimize vigezo, vya kuwa kiongozi. Ikiwa una ubora duni wa tabia lakini bado unatumia wakati wako wote kutaka kuwa kiongozi, au kuchukua jukumu fulani muhimu, au kuwajibika kwa kazi ya jumla, au kufanya kitu kinachokuruhusu ujitofautishe, basi Ninakuambia: Hii ni tamaa ya makuu. Tamaa ya makuu inaweza kuleta maafa, kwa hivyo unapaswa kujihadhari nayo. Watu wote wana hamu ya kupiga hatua na wote wako tayari kujitahidi kuelekea ukweli, jambo ambalo si tatizo. Watu wengine wana ubora wa tabia, wanatimiza vigezo vya kuwa viongozi, na wana uwezo wa kujitahidi kuelekea ukweli, na hili ni jambo jema. Wengine hawana ubora wa tabia, kwa hivyo wanapaswa kushikilia wajibu wao wenyewe, wakitekeleza wajibu ulio mbele yao ipasavyo na kuufanya kulingana na kanuni, na kulingana na matakwa ya nyumba ya Mungu; kwao, hilo ni jambo bora zaidi, salama zaidi, na la uhalisi zaidi.

Wale wanaochaguliwa kuwa viongozi na wafanyakazi au kupandishwa cheo na kukuzwa hawapaswi kujihusisha na ndoto za mchana, kwa kuhisi kwamba, “Ndugu wamenichagua kutoka miongoni mwa watu wengi sana, nyumba ya Mungu imenipandisha cheo, kwa hivyo kwa kweli nina talanta kiasi, na mimi ni bora kuliko watu wa kawaida; dhahabu ya kweli lazima ing’ae hatimaye.” Je, ni vizuri kufikiri hivi? Je, si ni udhihirisho wa tabia potovu? (Ndiyo.) Kupandishwa cheo na kukuzwa ni jambo jema na fursa nzuri, lakini kama unaweza kutembea katika njia hii vizuri au la inategemea jinsi unavyoichukulia fursa hii na kama unaweza kuithamini. Mungu amekupa fursa hii, lakini hiyo haimaanishi kwamba wewe kweli ni bora kuliko mtu mwingine yeyote; inaweza kuwa kwamba ubora wako wa tabia ni bora kidogo kuliko wengine au kwamba una karama fulani, lakini ni vigumu kusema kuingia kwako katika uzima kukoje na kama una uhalisi wa ukweli—kwa sababu tabia potovu za kila mtu ni sawa, na wewe pia ni mshiriki wa jamii ya wanadamu waliopotoka. Ikiwa unaweza kutambua hili, utaweza kuchukulia kwa usahihi upandishwaji cheo na ukuzaji wako na nyumba ya Mungu. Usijione kama mtu mwenye talanta, wala usifikiri kwamba una uhalisi wa ukweli. Ni kwamba tu una ubora kiasi wa tabia na pia unaweza kujitahidi kuelekea ukweli, kwa hivyo umewezeshwa kujifundisha. Hiki ni kipindi cha majaribio, na bado haijathibitishwa kama wewe kwa kweli ni mtu anayefuatilia ukweli, au kama unastahili kukuzwa. Ni vigumu kusema kama utaweza kusimama imara baada ya kupewa fursa ya kujaribu katika kipindi hiki. Inaweza kuwa kwamba utabakishwa ili uendelee kukuzwa, au inaweza kuwa kwamba utaondolewa—yote inategemea ni juhudi kiasi gani unazoweka. Hivi ndivyo kuteua watu kuwa viongozi na wafanyakazi kulivyo, na unapaswa kuelewa hilo. Haina maana wewe mwenyewe kufikiri kwamba wewe ni mtu mwenye talanta. Ikiwa nyumba ya Mungu haikupandishi cheo na kukukuza, basi wewe si kitu. Ikiwa hufuatilii ukweli na hauko tayari kutumiwa na nyumba ya Mungu, basi huwezi kutimiza chochote. Ikiwa basi unasema, “Nyumba ya Mungu hainitumii, nitaenda katika jamii,” basi, nenda katika jamii ujaribu, uone ni nani atakayekuteua, na uone ni nini unachoweza kutimiza. Ninachomaanisha kwa kusema hivi ni kuwaambia ninyi kwamba ni lazima muwe na uelewa na mtazamo sahihi kuelekea uteuzi na ukuzaji wenu na nyumba ya Mungu. Wale wenye ubora duni au wa wastani wa tabia na ambao hawawezi kufikia kiwango kinachohitajika kwa ajili ya upandishwaji cheo na ukuzaji katika nyumba ya Mungu wanahitaji tu kutimiza wajibu wao kwa utiifu na uthabiti. Maadamu unafanya wajibu wako kwa moyo na akili yako yote, Mungu hatakutendea isivyo haki. Kwa hivyo, msipiganie masuala ya uteuzi na ukuzaji, lakini msiyakatae pia, acheni tu kila kitu kifuate mkondo wake wa asili; kwa upande mmoja, ni lazima mtii mipango ya nyumba ya Mungu, na kwa upande mwingine, ni lazima muwe na moyo wa utii kwa Mungu—hii ndiyo njia sahihi. Je, ni rahisi kufanya hivi? (Ndiyo, ni rahisi.) Je, kuna manufaa yoyote kwa mtu mwenye ubora duni wa tabia kuwa kiongozi? Mwishowe, anapoainishwa kama kiongozi wa uwongo na kuondolewa, atahisi vipi kuhusu hili? Je, litakuwa ndilo jambo mlilotaka? (Hapana.) Mtabeba jina la “kiongozi wa uwongo” juu ya kichwa chenu, na popote mnapoenda, watu watasema, “Mtu huyu aliwahi kuwa kiongozi wa uwongo.” Je, hilo ni jambo jema au baya? Si jambo jema, na si kitu cha utukufu. Ni lazima watu wawe na uelewa na mtazamo sahihi kuelekea uteuzi na ukuzaji; katika masuala haya, ni lazima wautafute ukweli, na wasifuate mapenzi yao wenyewe, au kuwa na tamaa ya makuu na matamanio. Ikiwa unahisi kwamba una ubora mzuri wa tabia lakini nyumba ya Mungu haijawahi kukupandisha cheo, wala haina mipango yoyote ya kukukuza, basi usifadhaike au kuanza kulalamika, zingatia tu kufuatilia ukweli na kujitahidi kusonga mbele. Utakapokuwa na kimo kiasi na kuweza kufanya kazi halisi, watu wateule wa Mungu watakuchagua kwa kawaida kuwa kiongozi. Na ukihisi kwamba una ubora duni wa tabia, na kwamba huna nafasi yoyote ya kupandishwa cheo au kukuzwa, na kwamba haiwezekani kwa tamaa zako za makuu kutimizwa, je, hili si jambo jema? Hili litakulinda! Kwa kuwa una ubora duni wa tabia, ukikutana na kundi la watu vipofu waliochanganyikiwa wanaokuchagua kuwa kiongozi wao, je, hutakuwa unatembea juu ya makaa ya moto? Huwezi kufanya kazi yoyote na macho yako na akili yako ni vipofu. Kila kitu unachofanya ni mvurugo; kila hatua yako ni kutenda maovu. Ingekuwa afadhali ufanye kazi ya wajibu wako wa sasa vizuri; angalau hutajiaibisha, na ni bora kuliko kuwa kiongozi wa uwongo na kuwa mlengwa wa ukosoaji pasipo wewe kujua. Kama mtu, ni lazima ujitambue, ni lazima uwe na hali ya kujielewa kiasi; ukifanya hivyo, utaweza kuepuka kuchukua njia isiyo sahihi na kufanya makosa makubwa.

Je, mnatamani kuwa kiongozi wa uwongo, au mfuasi wa kawaida? (Mfuasi wa kawaida.) Akina ndugu wakikuchagua, jaribu; pengine mtazamo wao kukuhusu ni sahihi zaidi kuliko hisia zako mwenyewe kujihusu. Ikiwa ndugu wanafikiri kwamba unaweza kufanya hivyo, unapaswa kujitolea kabisa. Ikiwa kwa kweli unajaribu uwezavyo lakini bado unashindwa katika kazi yako, na moyo wako unawaka kwa wasiwasi kiasi kwamba huwezi kula na unakosa usingizi kwa ajili yake, na huelewi tu jinsi ya kuifanya ipasavyo, basi acha kuwa kiongozi au mfanyakazi—ni vigumu sana kwako. Ukiendelea, kuna uwezekano utakuwa kiongozi wa uwongo, kwa hivyo unapaswa kuandika barua ya kujiuzulu bila kuchelewa, ukitoa taarifa kwamba: “Kwa sababu mimi ni mwenye ubora duni wa tabia na siwezi kufanya kazi halisi, nikiendelea kuwa kiongozi, baada ya muda mfupi bila shaka nitaishia kuwa kiongozi wa uwongo, kwa hivyo ninaomba kujiuzulu, na kwa hiari ninaachilia wadhifa huu.” Huu ndio mwendo wa busara zaidi, na jambo linalofaa zaidi kufanya! Ni jambo la busara, na ni bora kuliko kushikilia wadhifa na kuwa kiongozi wa uwongo. Ikiwa unajua fika kwamba una ubora duni wa tabia na huwezi kuwa kiongozi lakini unang’ang’ania hadhi, na unajiambia, “Kwa nini siwezi kufanya hivi? Ni nani anayeweza kunisaidia? Ingekuwa vizuri namna gani kama ningedumisha hadhi yangu kama kiongozi huku mtu mwingine akinipangia mipango na mikakati yote! Sasa hivi hakuna mtu anayefaa kuchukua nafasi yangu, kwa hivyo ninaweza tu kuendelea kuwa kiongozi na kufurahia starehe zake kila siku nikiwa kazini; hata kama siwezi kufanya kazi, mimi bado ni kiongozi, na kuwa kiongozi ni bora kuliko kuwa ndugu wa kawaida. Ikiwa nyumba ya Mungu haitanitimua na nisiondolewe na akina ndugu, basi sitajiuzulu.” Je, hili linafaa? (Hapana.) Kwa nini halifai? (Si jambo la busara; ikiwa siwezi kufanya kazi halisi na bado sijiuzulu, hili litachelewesha tu kazi ya kanisa.) Kutenda hivyo huchelewesha kazi ya kanisa—kunawadhuru wengine, na kunakudhuru wewe mwenyewe. Je, unajua maana ya kuwa kiongozi? Inamaanisha una uhusiano wa moja kwa moja na kuingia katika uzima kwa watu wengi, na uongozi wako una uhusiano wa moja kwa moja na jinsi wanavyotembea katika njia iliyo mbele yao. Ukiwaongoza vizuri na uwaelekeze kwenye njia sahihi, wataweza kuitembea njia sahihi. Ukiwaongoza vibaya na uwapotoshe, na wakawa Mafarisayo kama wewe, basi dhambi yako ni kubwa! Na baada ya wewe kutenda dhambi hii kubwa, je, huo utakuwa mwisho wake? Itaandikwa na Mungu! Unajua fika kwamba ubora wako wa tabia ni duni, kwamba wewe ni kiongozi wa uwongo, na kwamba huwezi kufanya kazi halisi, lakini hukubali makosa yako na kujiuzulu, bali unashikilia wadhifa wako bila aibu, na humwachii mtu mwingine yeyote. Hii ni dhambi, na Mungu ataiweka katika hesabu. Na, je, Yeye kuiweka katika hesabu kutakuwa jambo jema au baya kwako katika siku zijazo? Wewe utakuwa matatani! Nitakuambia ukweli mtupu: Mungu huweka hesabu ya mambo kama hayo kwa kila mtu, na kila kipengele kimeandikwa waziwazi. Ikiwa jambo zito kama hili lingetokea katika njia yako ya wokovu, basi athari kwako ingekuwa kubwa sana! Chochote unachofanya, usiitembee njia hii, na usiwe mtu wa aina hii.

Tumeshiriki kwa ufupi kuhusu baadhi ya matendo na udhihirisho wa viongozi wa uwongo kuhusiana na kupandisha cheo na kukuza aina mbalimbali za watu wenye talanta. Kwa muhtasari, aina ya mtu ambaye ni kiongozi wa uwongo hafanyi kazi halisi, na hawezi kufanya kazi halisi. Ubora wake wa tabia ni duni, macho yake na akili zake ni yenye upofuu, hawezi kugundua matatizo, na hawawezi kuwang’amua watu wa aina mbalimbali, kwa hivyo hawawezi kubeba kazi muhimu ya kuteua na kukuza aina mbalimbali za watu wenye talanta. Hivyo basi, hana namna ya kuifanya kazi ya kanisa vizuri, na atasababisha matatizo mengi kwa watu wateule wa Mungu katika kuingia kwao katika uzima. Kwa kuzingatia mambo haya, ni wazi kwamba viongozi wa uwongo hawafai kuwa viongozi wa kanisa. Kuna viongozi wengine wa uwongo ambao hawafanyi kazi maalum ya kanisa na hawawasiliani na wasimamizi wa kazi maalum, kwa hivyo hawajui ni watu wepi wenye talanta wanaoweza kufanya kazi gani, wala ni wepi wanaofaa kwa kazi gani, wala kama kazi yao inapatana na kanuni. Hivyo basi, hawawezi kuwateua na kuwakuza watu wenye talanta. Basi, watu kama hao wanawezaje kuifanya kazi ya kanisa vizuri? Sababu kuu inayowafanya viongozi wa uwongo wasiweze kufanya kazi halisi ni kwamba ubora wao wa tabia ni duni; hawana utambuzi wa jambo lolote na hawajui kazi halisi ni nini. Hili husababisha hali za mara kwa mara za kudumaa au kupooza katika kazi ya kanisa. Haya yanahusiana moja kwa moja na kushindwa kwa viongozi wa uwongo kufanya kazi halisi. Kwa miaka kadhaa iliyopita, nyumba ya Mungu imesisitiza, mara kwa mara, kwamba watu waovu na wasioamini lazima waondolewe na viongozi wa uwongo na wafanyakazi wa uwongo watimuliwe. Kwa nini watu mbalimbali waovu na wasioamini lazima waondolewe? Kwa sababu baada ya miaka mingi ya kumwamini Mungu, watu hawa bado hawaukubali ukweli hata kidogo, na wamefikia hatua ambapo hawana tumaini la wokovu. Na kwa nini viongozi wote wa uwongo na wafanyakazi wa uwongo lazima watimuliwe? Kwa sababu hawafanyi kazi halisi, na hawawapandishi cheo au kuwakuza kamwe wale wanaofuatilia ukweli; badala yake, wanajishughulisha tu na juhudi zisizo na maana. Hili huisababisha kazi ya kanisa iingie katika machafuko na kupooza, huku matatizo yaliyopo yakidumu bila kutatuliwa, na pia hupunguza kasi ya kuingia katika uzima kwa wateule wa Mungu. Ikiwa viongozi hawa wote wa uwongo na wafanyakazi wa uwongo wangetimuliwa, na ikiwa watu hawa wote waovu na wasioamini wanaolisumbua kanisa wangeondolewa, kazi ya kanisa kwa kawaida ingeenda kwa wepesi, maisha ya kanisa kwa kawaida yangekuwa bora zaidi, na wateule wa Mungu wangekuwa na uwezo wa kula na kunywa maneno ya Mungu na kutekeleza wajibu wao kwa kawaida, na kuingia katika njia sahihi ya imani katika Mungu. Hiki ndicho ambacho Mungu angependa kuona.

27 Februari, 2021

Iliyotangulia: Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (4)

Inayofuata: Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (6)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp