Sera ya Faragha ya Tovuti za Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sera hii ya Faragha inafichua desturi za faragha za tovuti rasmi za Kanisa la Mwenyezi Mungu (hidden-advent. org, godfootsteps. org) na tovuti za injili za Kanisa la Mwenyezi Mungu (kingdomsalvation.org, holyspiritspeaks.org, easternlightning.org). Tovuti za Kanisa la Mwenyezi Mungu zimeanzishwa kuhubiri injili ya ufalme ya Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, na hazihusiani kabisa na shughuli zozote ya kibiashara. Tovuti hizi zinalenga kutoa hali inayofaa kwa wale wote ambao wanatafuta ukweli, kuchunguza njia ya kweli na kuwa na shauku ya kuonekana kwa Mungu. Nyenzo zote katika tovuti hii ni bure kusoma na kupakua. Kwa manufaa yako, tovuti hizi huenda zikawa na viungo vya kukuelekeza kwa tovuti zingine. Huwa hatuchukui wajibu wa mazoea na maudhui ya sera za faragha za tovuti hizi zilizounganishwa.

Habari Tunazokusanya

1. Tovuti za Kanisa la Mwenyezi Mungu hukusanya taarifa zifuatazo:

(1) Barua pepe na jina ambalo unalijaza wakati unawasiliana nasi kwa njia ya tovuti au kwa kutumia chaguo la maoni.

(2) Kumbukumbu za kuingia za mtandao wa kompyuta (Apache httpd) unapozuru tovuti.

(3) Taaluma ya Google (Google Analytics) itaweka vidakuzi kwenye kivinjari cha kifaa chako na kukusanya taarifa husika za takwimu za nyendo.

2. Apache httpd (http://httpd.apache.org) na Taaluma ya Google (Google Analytics) (http://www.google.com/analytics/) hukusanya taarifa zifuatazo:

(1) Taarifa ya kifaa. Maelezo yasiyo ya binafsi ya kompyuta, simu za mkononi na vifaa vingine ambavyo unatumia kutembelea tovuti zetu, kama vile anwani ya IP, GPS, vitambulisho vya kipekee vya kifaa, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari.

(2) Habari za kuvinjari. Unavyofikia tovuti hii (utafutaji kwa google, kiungo ulichoshirikishwa kutoka Facebook au kupiga taipu katika URL moja kwa moja) na kumbukumbu ya kuvinjari tovuti hii, ikiwa ni pamoja na kurasa za tovuti unazoangalia, muda unaokaa kwa kila ukurasa, na ukurasa wa mwisho wa tovuti uliouvinjarii.

(3) Maelezo yanayohusiana ambayo Taaluma ya Google (Google Analytics) hukusanya ikitumia vidakuzi. Tafadhali rejelea “Vidakuzi na teknolojia sawa” (http://www.google.com/intl/en-us/policies/privacy/).

Sababu Yetu Kukusanya Habari Hizi

1. Mawasiliano ya Barua Pepe. Sisi hurekodi habari zako za barua pepe tu ili kuwasiliana nawe kupitia barua pepe.

2. Uchambuzi wa Takwimu. Sisi hujifunza jinsi watumiaji hutumia tovuti zetu kwa kuunda takwimu kutoka kwa kumbukumbu za kuingia mtandao za Apache httpd na kuzichanganya na Taaluma ya Google (Google Analytics).

Tutachambua habari pamoja na idadi ya kila siku ya wageni wa tovuti (idadi za anwani za IP) au idadi katika kipindi cha muda, idadi ya mitazamo ya ukurasa, wakati katika kila ukurasa, kiwango cha kuruka tovuti, maenezi ya jiografia ya watumizi, asilimia ya vifaa vya kuzuru tovuti, upendeleo wa kivinjari, jinsi watumiaji hupata tovuti zetu (kwa kuchapa anwani moja kwa moja, kwa kutafuta, au kwa kubonyeza viungo kwenye watu wa tatu kama Facebook na Twitter) na asilimia. Hii inaturuhusu kuchambua nyendo katika tovuti, kuboresha uzoefu wa mtumiaji ipasavyo, na kukuza tovuti zetu (SEO na ukuzaji kwenye majukwaa ya tatu kama Facebook na Twitter).

Ahadi na Chaguo

Tovuti za Kanisa la Mwenyezi Mungu zaahidi kukusanya tu habari iliyoelezewa hapo juu kutoka kwako na kuitumia kwa mujibu wa sababu zilizotolewa hapo juu tu. Sisi kamwe hatutatoa, kuuza, kuhamisha, kukodisha au kutoa habari zako kwa mtu mwingine yeyote.

Unaweza kupanga kivinjari chako kizuie vidakuzi vya Taaluma vya Google (Google Analytics cookies).

Kama una maswali yoyote au mapendekezo, tafadhali jisikie huru kututumia barua pepe katika info@almightygod.church.

Kutengeneza Upya Sera Yetu ya Faragha

Huenda mara kwa mara tukatengeneza upya taarifa hii ya faragha. Kama kuna mabadiliko yoyote, tutaongeza “*” kwa kiungo cha “Taarifa ya Faragha” chini ya tovuti.

Sera hii ya Faragha ilitengenezwa upya mara ya mwisho tarehe 17 January, 2017.