Vurugu Kutoka kwa Uvumi wa “Mei 28” (Sehemu ya 2)
Baada ya hilo, sikujihadhari tena dhidi ya ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wakati wowote nilipokuwa na muda ningesoma neno la Mungu na kutazama video, filamu, video za muziki, nyimbo, filamu za muziki na maonyesho mengine yaliyotolewa na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kadiri nilivyozidi kutazama haya yote, ndivyo nilivyozidi kuhisi kupewa, na ndivyo nilivyozidi kuhisi raha. Nilidhibitisha kutoka kwa moyo wangu kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kuonekana kwa Bwana Yesu.