Mwisho wa Wakati Umewadia: Je, Sisi Wakristo Tutanyakuliwa Vipi Kabla ya Dhiki Kuu?
Siku hizi, maafa ulimwenguni kote yanazidi kuwa mabaya zaidi. Taarifa ya habari imejawa na visa vya mapigo, matetemeko ya ardhi, mafuriko, na ukame. Je, umewahi kufikiri: Unabii wa kurudi kwa Bwana umetimia, kwa hivyo ni kwa nini bado hatujamkaribisha Bwana? Jambo hili likiendelea, dhiki kuu itakapofika, si sisi pia tutatumbukia katika maafa? Bwana atatupeleka lini hasa katika ufalme wa mbinguni?
Tutakaponyakuliwa, Tutainuliwa Angani kwa Kweli?
Waumini wengi wa Bwana wamesoma maneno haya katika Biblia: “Baada ya hayo sisi ambao tuko hai na kusalia tutachukuliwa pamoja na wao mawinguni, kwa ajili ya kukutana na Bwana katika hewa: na hivyo tutakuwa naye Bwana daima” (1 Wathesalonike 4:17). Wanatamani sana kuinuliwa angani na kukutana na Bwana atakapokuja. Lakini kwa kweli, maneno haya hayakusemwa na Bwana Yesu, wala si unabii wa Kitabu cha Ufunuo. Hayo ni maneno tu ya mtume Paulo. Je, ni sahihi kutegemea maneno ya Paulo katika suala la kukaribisha ujio wa Bwana? Je, maneno ya Paulo yanaweza kuwakilisha yale ya Bwana? Jinsi Bwana wa siku za mwisho atakavyowadia, na jinsi atakavyowaingiza wale wanaomwamini katika ufalme ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Paulo alikuwa mtume tu aliyemwenezea Bwana ujumbe; angewezaje kujua mambo kama hayo? Kukaribisha ujio wa Bwana ni jambo muhimu sana, ambalo ni sawa kwetu sisi kutegemea maneno ya Bwana Yesu. Bwana Yesu alisema, “Ombeni basi kwa namna hii: Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako ufike, Mapenzi yako yafanywe duniani, kama ilivyo mbinguni” (Mathayo 6:9-10). Kitabu cha Ufunuo pia kina unabii ufuatao: “Na mimi Yohana nikauona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukija chini kutoka kwa Mungu mbinguni.… Na nikasikia kutoka mbinguni sauti kuu ikisema, Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao” (Ufunuo 21:2-3). “Naye malaika wa saba akalipiga baragumu; na kukawa na sauti kubwa mbinguni, zikisema, falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake; na yeye atatawala milele na milele” (Ufunuo 11:15). Katika unabii huu, maneno “kutoka mbinguni,” “hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu,” na “falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake,” yanaonyesha kuwa Mungu ataanzisha ufalme Wake duniani, na kwamba hatima aliompanga mwanadamu pia upo duniani. Je, si hamu yetu ya kila siku ya kuinuliwa hadi mbinguni ni maoni na mawazo yetu wenyewe? Na je, huku si kutembea njia tofauti na ya Mungu?
Ukweli ni kwamba Mungu hajawahi kusema juu ya kuwainua watu hadi angani, na hili jambo ambalo tunaweza kulitambua kutoka kwa ukweli wa kazi ya Mungu. Mwanzoni, Mungu alimuumba mwanadamu kutoka kwa mavumbi na kumweka kwenye Bustani ya Edeni, ambapo aliishi na kumwabudu Mungu vizuri. Wakati wa Nuhu, Mungu hakumwinua Nuhu na familia yake angani ili watoroke mafuriko, pia; badala yake, Alimwagiza Nuhu achukue hatua ya utendaji ya kujenga safina duniani. Mwishoni mwa Enzi ya Sheria, watu walikabili hatari ya kuuawa kwa kukiuka sheria za Mungu. Mungu hakuiinua angani kupata sadaka za dhambi, lakini badala yake alikuwa mwili na kuja duniani binafsi, ambapo kwa kweli alisulibiwa kwa ajili ya wanadamu, Akiwaokoa wanadamu kutoka dhambini. Kutoka kwa hili tunaweza kuona kwamba Mungu daima amefanya kazi duniani kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, Akiwaongoza wanadamu katika kuishi na kumwabudu Mungu. Tamaa yetu ya kila siku ya kuinuliwa angani bila shaka haipatani na mapenzi ya Mungu!
Je, Unyakuo Kabla ya Dhiki Kuu Ni Nini?
Wengine wenu huenda hawana hakika “kunyakuliwa” kunahusu nini kwa kweli. Ili kuelewa hili, hebu kwanza tuone maneno ya Mungu yanasema nini. Mungu alisema, “‘Kunyakuliwa’ si kuchukuliwa kutoka mahali pa chini kwenda mahali pa juu jinsi watu wanaweza kufikiria; hiyo ni fikira potovu sana. ‘Kunyakuliwa’ kunaashiria kujaaliwa Kwangu halafu kuchagua. Hii inawalenga wale wote ambao Nimewaamua kabla na kuwachagua. Wale wote wataonyakuliwa ni watu waliopata hadhi ya wazaliwa wa kwanza, au wana, auwale ambao ni watu wa Mungu. Hili halilingani kabisa na mawazo ya watu. Wale walio na sehemu katika nyumba Yangu katika siku zijazo wote ni watu ambao wamenyakuliwa mbele Yangu. Hii ni kweli kabisa, haibadiliki kamwe, na haiwezi kukataliwa na mtu yeyote. Hili ni jibu la mapigo dhidi ya Shetani. Mtu yeyote Niliyemwamua kabla atanyakuliwa mbele Yangu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 104). Maneno haya yanatuambia kuwa kunyakuliwa si kuchukuliwa angani kukutana na Bwana kama tulivyofikiri; badala yake, kunamaanisha kuweza kukubali na kutii kazi mpya ya Mungu baada ya kusikia sauti Yake, kufuata kwa karibu nyayo za Mwanakondoo, na kuja mbele ya Mungu wakati atakapokuja duniani na kufanya kazi. Huu pekee ndio unyakuo wa kweli. Ni kama tu Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi ya ukombozi: Petro, mwanamke Msamaria, Yakobo na wengine waliitambua sauti ya Bwana waliposikia maneno Yake na wakabainisha kwamba Yeye ndiye Masihi aliyepaswa kuja. Kwa hivyo, walipokea wokovu wa Bwana na wote waliinuliwa mbele za Bwana katika Enzi ya Neema. Wote ambao katika siku za mwisho wanakaribisha kurudi kwa Bwana na kukubali kazi ya sasa ya Mungu ni wale wanaofuata nyayo za Mwanakondoo, na ambao wanainuliwa mbele za Bwana!
Jinsi ya Kunyakuliwa Kabla ya Dhiki Kuu
Kwa hivyo tufanye nini hasa ili kumkaribisha Bwana na kunyakuliwa kabla ya maafa? Hii ilitabiriwa zamani katika Biblia, Bwana Yesu aliposema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13). Sura ya 2 na ya 3 ya Kitabu cha Ufunuo zinatabiri mara nyingi: “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa.” Kuna pia sura ya 3, Aya ya 20: “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” Maneno ya Mungu yasema, “Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya). Maneno ya Mungu yanatuambia kwamba ikiwa tunataka kumpokea Bwana, kutafuta kazi na maneno ya Mungu ni muhimu. Hakuna kitu cha muhimu zaidi kuliko kutafuta mahali ambapo maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa yapo siku hizi, na mahali ambapo kuonekana kwa Mungu na kazi Yake vipo siku hizi. Tusipojitolea kutafuta nyayo za Mungu, tusipotilia maanani kuisikia sauti ya Mungu, lakini badala yake tukazie macho mawingu angani bila kufanya chochote, tukingoja kwa uvivu Bwana aje na kutupeleka hewani, je, si mawazo kama haya ni ya ndoto tu? Na basi si hatuwezi kuwa na uwezo wa kumkaribisha Bwana milele, hatimaye tukiharibu nafasi ya kunyakuliwa na Yeye?
Basi nyayo za Bwana zi wapi? Na Mungu hunenea maneno Yake wapi? Leo, ni Kanisa la Mwenyezi Mungu pekee linaloshuhudia wazi kwa wanadamu kuwa Bwana tayari amerudi: yaani, Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ameonyesha mamilioni ya maneno, Akafunua ukweli na siri kadhaa, na pia Akafichua mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita wa Mungu, siri ya kupata mwili, na siri za Biblia. Kwa hivyo, pia, Ameonyesha maneno ya kuwahukumu na kuwafunua wanadamu, na kufunua ukweli wa kweli wa upotovu wetu mikononi mwa Shetani na tabia zetu mbalimbali za kishetani. Kwa kukubali maneno ya Mungu ya hukumu na yenye kuadibu, tunajua upotovu wetu, na tunaona kwamba kila kitu tunachofunua ni tabia za kishetani za kiburi, ubinafsi, aibu, udanganiyfu, na ujanja, na kwamba hatuna dhamiri na mantiki. Tumeridhishwa kabisa na maneno ya Mungu, tunasujudu mbele za Mungu, tukijawa na majuto, na tuna maarifa kiasi kuhusu tabia ya Mungu ya haki na takatifu; heshima na utiifu kwa Mungu vimezaliwa ndani yetu, na tunathibitisha kutoka mioyoni mwetu kuwa yote ambayo yameonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, na yanaweza kuwatakasa na kuwabadilisha watu.
Leo, maneno ya Mwenyezi Mungu yanaenea kati ya wanadamu. Wengi kutoka kwa madhehebu mbalimbali ya Wakristo ambao ni waumini wa kweli na wanapenda ukweli kwa kweli wameisikia sauti ya Mungu, wameamshwa na maneno ya Mungu, na kurudishwa mbele ya kiti Chake cha enzi. Wanafurahia unyunyizi na riziki ya maneno Yake, na wanahisi jinsi maneno haya yalivyo na mamlaka na nguvu, wamebainisha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu. Ni wale ambao wamenyakuliwa kabla ya dhiki kuu! Wacha tusome kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu: “Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Kama mtoto mchanga aliyezaliwa hivi karibuni, wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye ‘Mlima wa Mizeituni’ wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni ‘mtoto mchanga’ Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni).
Je, unahisi nini baada ya kusoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu? Je, hapana msisimko ndani ya moyo wako? Je, unahisi kuwa maneno hayo ni Muumba akiwazungumzia wanadamu wote? Je, unahisi kuwa Mungu anatuambia sasa kwamba tayari amerudi? Lolote unaloweza kuhisi, tuna kazi ya haraka mbele yetu: Lazima tuwe wanawali wenye busara, sikiliza maneno yaliyonenwa na Mwenyezi Mungu, na utafute kazi Yake ya siku za mwisho ukiwa tayari kupokea mawazo mapya. Hakuna njia nyingine ya kunyakuliwa kabla ya dhiki kuu!
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?