Wimbo wa Maisha Katikati ya Uharibifu

26/01/2021

Na Gao Jing, Mkoa wa Henan

Mnamo mwaka wa 1999, nilibahatika kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Kupitia kusoma maneno ya Mungu, nilifahamu mamlaka na nguvu yaliyonayo, na nikahisi kuwa maneno haya yalikuwa sauti ya Mungu. Kuweza kusikia maneno ambayo wanadamu walionyeshwa na Muumba kulinigusa kupita uwezo wangu wa kueleza, na kwa mara ya kwanza, nilihisi ndani kabisa ya roho yangu hali ya amani na furaha ambayo kazi ya Roho Mtakatifu humletea mwanadamu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, nilizidi kuwa msomaji mwenye shauku wa maneno ya Mungu. Baada ya kujiunga na Kanisa la Mwenyezi Mungu, niliona kwamba kanisa hilo lilikuwa ulimwengu mpya kabisa, tofauti kabisa na ule wa jamii. Ndugu wote walikuwa wa kawaida na wema, safi na wachangamfu. Ingawa hatukuwa wa ukoo mmoja, na kila mmoja wetu alikua na malezi tofauti na tulikuwa na utambulisho wetu wenyewe, sote tulikuwa kama roho wa familia waliopendana, kusaidiana, na tuliunganishwa pamoja kwa furaha. Kuona hili kulinifanya nihisi jinsi maisha yaliyotumiwa kumwabudu Mungu yalivyo ya furaha na raha, jinsi yalivyo mazuri na matamu. Baadaye, niliona maneno haya ya Mungu: “Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Maneno ya Mungu yaliniruhusu nielewe kwamba, kama kiumbe aliyeumbwa, ninapaswa kuishi kwa ajili ya Muumba, na kwamba napaswa kuwa nikitoa na kutumia kila kitu changu ili kueneza na kushuhudia injili ya Mungu ya siku za mwisho—haya tu ndiyo maisha ya thamani na ya maana zaidi. Na hivyo, niliposikia kwamba watu wengi wanaoishi katika maeneo ya mbali hawakuwa wamesikia injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, niliwapa buriani kwa ushupavu ndugu waliokuwa katika makazi yangu ya kudumu na kuanza safari yangu ya kueneza injili ya ufalme.

Wimbo wa Maisha Katikati ya Uharibifu

Mnamo mwaka wa 2002, nilifika katika eneo la mbali lenye milima na lenye maendeleo kidogo katika Mkoa wa Guizhou kuhubiri injili. Kueneza injili huko kulinihitaji nitembee maili nyingi kwenye njia za mlima kila siku, na mara nyingi nililazimika kustahimili upepo na theluji. Hata hivyo, nikiwa na Mungu karibu yangu, sikuwahi kuhisi uchovu, au kwamba ilikuwa shida. Chini ya uongozi wa kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya injili ilianza punde huko, watu wengi zaidi wakiikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho na maisha ya kanisa yalijaa uchangamfu. Kwa ajili ya kongozwa na maneno ya Mungu, nilishinda miaka sita ya furaha na ya kukamilisha mahali hapo. Yaani, hadi mwaka wa 2008, wakati ambapo kitu cha kushangaza kilitokea ghafla, kitu ambacho kiliharibu kabisa furaha na utulivu wa maisha yangu …

Kilitokea karibu saa tano asubuhi ya mnamo Machi 15, mwaka wa 2008. Mimi na ndugu wawili tulikuwa kwenye mkusanyiko wakati ambapo polisi waliingia ghafla mlangoni na kutugandamiza sakafuni kwa haraka. Walitutia pingu bila kusema neno lolote, kisha wakatusukuma na kutukokota hadi kwenye gari la polisi la mizigo. Ndani ya gari hilo, wote walicheka kichinichini kwa uovu, wakitikisa virungu vyao vya umeme na kutupiga vichwani au kwenye mapingiti kwa nguvu mara chache. Walitutukana kwa ukatili, wakisema, “Wakorofi nyinyi! Ninyi ni wachanga sana na mnaweza kufanya chochote, lakini sivyo kabisa, ilikuwa ni lazima mumwamini Mungu! Kwa kweli hamna kitu bora cha kufanya?” Kukamatwa ghafla kuliniacha nikiwa na woga sana, na sikujua tulichotayarishiwa. Nilichoweza tu kufanya ni kumwita Mungu kimya moyoni mwangu, tena na tena: “Ee Mungu! Hali hii imetufika leo kwa idhini Yako. Nakuomba tu Utupe imani na Utulinde ili tuweze kuwa na ushuhuda Kwako.” Baada ya kuomba, mstari wa maneno ya Mungu ulinijia akilini: “Kuwa mwaminifu Kwangu bila kujali chochote, na usonge mbele kwa ujasiri; Mimi ni mwamba wako wa nguvu, kwa hivyo Nitegemee Mimi!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 10). “Naam!” Niliwaza. “Mungu ndiye tegemeo langu na Yeye ndiye msaada wangu thabiti na wenye nguvu. Bila kujali ninajikuta katika hali gani, almradi niweze kusalia mwaminifu kwa Mungu na kusimama pamoja na Yaye, basi hakika nitamshinda Shetani na kumwaibisha.” Nuru ya maneno ya Mungu iliniwezesha kupata nguvu na imani, na niliazimia kimya kimya: Ni afadhali nife kuliko kuacha njia ya kweli na kutokuwa shahidi kwa Mungu!

Mara tulipofika katika kituo cha polisi, polisi hao walituvuta kwa nguvu nje ya gari la mizigo, kisha wakatusukuma hadi kwenye kituo. Walitukagua kikamilifu na wakapata vifaa kadhaa fulani vya injili na simu ya rununu kwenye mifuko ya ndugu zangu wawili wa kanisa. Alipoona kwamba hawakuwa wamepata pesa yoyote, mmoja wa polisi waovu alimvuta mmoja wa wale ndugu na kumpiga mateke na kumchapa hadi akaanguka chini. Baada ya hapo, tulipelekwa katika vyumba tofauti ili kuhojiwa tukiwa tumetenganishwa. Walinihoji alasiri hiyo yote, lakini hawakupata neno kutoka kwangu. Ilikuwa baada ya saa 2 jioni hiyo walipotuandikisha kama watu watatu wasiojulikana walio kizuizini kabla ya kutupeleka wote kizuizini.

Mara tu tulipofika kizuizini, maafisa wa kike wa urekebishaji walinivua nguo zangu zote. Waliondoa chuma chochote kwenye nguo zangu na kuchukua gidamu zangu na mshipi wangu. Huku nikiwa pekupeku na nikishikilia suruali yangu nilienda kwenye seli yangu nikiwa na wasiwasi. Waliponiona nikiingia, wafungwa wa kike walinijia kama watu wenye kichaa na wakanizingira kabisa, wote wakiniuliza kunihusu kwa wakati mmoja. Mianga ilikuwa imefifia sana humo ndani kiasi kwamba macho yao yalionekana makubwa sana kama yaliyotoka kwa mshangao; walikuwa wakinikodolea macho na kuniangalia kwa udaku kuanzia juu hadi chini, huku wengine wakivuta mikono yangu kwa nguvu, wakigusa hapa na kufinya pale. Kwa kupigwa na bumbuazi, nilisimama tisti mahali hapo, nikihisi woga sana na sikuthubutu kusema neno. Nilipofikiria kuwa ningelazimika kuishi mahali hapa pabaya mno pamoja na wanawake hawa, nilihisi kuangua kilio kutokana na ukosefu wa haki katika hayo yote. Wakati huo huo, mfungwa mmoja ambaye alikuwa ameketi kwenye kitanda cha matofali bila kusema neno, ghafla alisema, “Tosha! Amefika tu na hajui lolote. Msimwogofye.” Baadaye alinipa mfarishi wa kujigubika. Nilihisi mfuro wa ukunjufu wakati huo, na nilijua vizuri kuwa si mfungwa huyu ambaye alikuwa mwema kwangu, lakini ni Mungu ambaye alikuwa akiwatumia watu waliokuwa karibu nami kunisaidia na kunitunza. Mungu alikuwa nami wakati wote, na sikuwa peke yangu hata kidogo. Kwa kuwa nilikuwa na upendo wa Mungu wa kukaa nami mahali hapa pabaya mno pa huzuni na pa kijinamizi, nilihisi faraja kubwa. Usiku wa manane baada ya wafungwa wengine wote kulala, bado sikuwa na fikira yoyote ya kulala. Nilifikiri juu ya jinsi ambavyo, asubuhi hiyo tu, nilikuwa nikifanya kazi yangu kwa furaha na ndugu zangu, lakini usiku huo nilikuwa nikilala mahali hapa pabaya mno panapofanana na kaburi, bila kujua ningeachiliwa lini—nilihisi huzuni na dhiki isiyoelezeka. Nilipokuwa tu nikizama katika mawazo yangu, upepo baridi ulipunga ghafla na nilitetemeka pasipo kutaka. Niliinua kichwa changu kutazama pande zote na wakati huo tu ndipo nilipogundua kuwa seli ilikuwa wazi kwa hali ya hewa. Kando na paa iliyokuwa juu ya eneo la kulala, sehemu nyingine ya seli ilikuwa na tundu la wavu juu yake iliyotengenezwa kwa fito nene za chuma zilizounganishwa kwa weko, na upepo baridi ulivuma upesi na kungia tu ndani moja kwa moja. Mara chache, niliweza pia kusikia nyayo za polisi walioshika doria wakitembea juu ya paa. Nilichoweza kuhisi tu ilikuwa hofu kuu, na woga wangu, kutojiweza kwangu, na hisia zangu za kudhulumiwa zote zilifurika moyoni mwangu; machozi yalitirika pasipo kutaka kutoka machoni pangu. Wakati huo huo, kifungu cha maneno ya Mungu kilinijia waziwazi akilini mwangu: “Unapaswa kujua kwamba vitu vyote vilivyo katika mazingira yanayo wazunguka vipo hapo kwa ruhusa Yangu, Mimi napanga yote. Oneni wazi na muridhishe moyo Wangu katika mazingira Niliyokupa. Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 26). “Naam,” niliwaza. “Mungu ameruhusu serikali ya CCP inikamate. Ingawa mahali hapa pana giza na panaogofya na sijui nitakuja kukabiliana na nini baadaye, Mungu ndiye msaada wangu kwa hivyo hakuna chochote cha kuogopa! Haidhuru, na ninakabidhi kila kitu mikononi mwa Mungu.” Baada ya kuelewa mapenzi ya Mungu, nilihisi kutulia zaidi, na kwa hivyo nikamwomba Mungu sala ya kimya: “Ee Mungu! Asante kwa nuru na mwangaza Wako ambao umeniwezesha kuelewa kwamba haya yote yanatendeka kwa idhini Yako. Natamani kujisalimisha kwa mipango na mipangilio Yako, kutafuta mapenzi Yako katika hali hii ngumu, na kupata ukweli Unaotaka kunipa. Ee Mungu! Ni kwamba tu mimi ni wa kimo kidogo, kwa hivyo nakuomba Unipe imani na nguvu na Unilinde ili, bila kujali mateso ninayoweza kukabiliwa nayo, sitawahi kukusaliti.” Baada ya kusali, nilipangusa machozi yangu na nikatafakari maneno ya Mungu, nilipokuwa nikisubiri kwa utulivu kuja kwa siku mpya.

Mapema siku iliyofuata, kulikuwa na sauti ya kishindo na mlango wa seli ukafunguliwa. Mmoja wa maafisa wa marekebisho alipiga kelele, “Toka nje, Jane Doe!” Nilikawia kwa muda kabla ya hatimaye kugundua kuwa alikuwa akiniita. Katika chumba cha mahojiano, polisi waliniuliza tena niwape jina langu na anwani, na niwaambie juu ya kanisa. Sikusema chochote, lakini niliketi tu kwenye kiti kichwa changu kikiwa kimeinama. Walinihoji kila siku kwa wiki moja, hadi mwishowe mmoja wao akanidukua kwa kidole na kunikaripia, “Mwanamke wewe! Tumeshinda siku nyingi na wewe na hujasema neno. Sawa, subiri tu. Tuna kitu cha kukuonyesha!” Baada ya kusema haya, polisi hao wawili waliondoka kwa hasira, na kufunga mlango kwa kishindo. Siku moja kulipozidi kuwa usiku, polisi walikuja tena kuniita. Walinitia pingu mikononi na kuniingiza ndani ya gari la mizigo la polisi. Nikiwa nimeketi nyuma ya gari hilo, sikuwa na budi kuhisi hofu ikianza kuibuka ndani yangu, na nikawaza: “Wananipeleka wapi? Je, wanaweza kuwa wakinipeleka mahali pasipojulikana ili kunibaka? Je, wataniingiza kwenye gunia na kunitupa ndani ya mto ili kulisha samaki?” Niliogopa sana, lakini wakati huo huo mistari kadhaa kutoka kwa wimbo wa kanisa unaoitwa “Ufalme” ilianza kuvuma katika masikio yangu: “Mungu ni msaada wangu, kuna nini cha kuhofu? Ninaahidi maisha yangu kupigana na Shetani mpaka mwisho. Mungu anatuinua, tunapaswa kuacha kila kitu nyuma na kupigana kuwa na ushuhuda kwa Kristo. Mungu atatekeleza mapenzi Yake duniani. Nitaandaa upendo wangu na uaminifu na kuvitoa kwa Mungu. Nitakaribisha kurudi kwa Mungu kwa shangwe atakaposhuka katika utukufu” (Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Baada ya sekunde, nguvu isiyoisha iliibuka ndani yangu. Niliinua kichwa changu na kutazama nje ya dirisha huku nikitafakari maneno ya wimbo huo kimya kimya. Mmoja wa polisi aligundua kuwa nilikuwa nikitazama nje kupitia dirishani na akavuta pazia haraka, kabla ya kunikaripia kwa hasira, “Unaangalia nini? Inamisha kichwa chako!” Kuzungumziwa kwa ghafla kwa sauti kubwa kulinifanya nitetemeke kwa mshtuko, na nikainamisha kichwa changu mara moja. Polisi wanne walikuwa wote wakivuta sigara ndani ya gari, wakitoa mawingu ya moshi kila mara, na baada ya muda mfupi tu hewa ndani ya gari lile la mizigo ilinuka kiasi cha kutovumilika; nilianza kukohoa. Mmoja wa polisi aliyekuwa amekaa mbele yangu aligeuka na kufinya taya yangu ya chini kwa vidole vyake kabla ya kutoa moshi moja kwa moja usoni pangu. Kisha akasema kwa uovu, “Wajua, unahitaji tu kutuambia kila kitu unachojua, na hutateseka hata kidogo; utaweza tu kwenda nyumbani. Wewe ni mwanamke mchanga, na unapendeza sana….” Alipokuwa akisema hivi, alipitisha vidole vyake usoni pangu na kunikonyezea jicho kiasherati, kisha akacheka kwa inda na kusema, “Labda tutakutafutia mchumba baadaye.” Niliuelekeza uso wangu mbali naye na nikainua mikono yangu iliyokuwa imefungwa minyororo ili kuondoa mkono wake. Huku akikasirika kwa sababu ya kutahayarika, alisema, “Ah, wewe ni hodari sana. Subiri tu hadi tufike tunakoenda, na ndipo utakaposhika adabu.” Gari lile liliendelea kwenda. Sikujua kile nilichokaribia kukikabili, na kwa hivyo nilichoweza tu kufanya ni kumwomba Mungu kimya moyoni mwangu: “Ee Mungu! Niko tayari kuhatarisha kila kitu sasa. Bila kujali hawa maafisa wabaya sana watatumia mbinu gani ni dhidi yangu, almradi nina pumzi moja iliyobaki mwilini mwangu, nitatoa ushuhuda thabiti na mkuu sana Kwako mbele ya Shetani!”

Baada ya zaidi ya nusu saa, gari lile lilisimama. Polisi walinivuta nje; niliyumbayumba na kutazama pande zote. Tayari kulikuwa na giza kabisa, na kulikuwa na majengo machache tu matupu yaliyokuwa yametapakaa bila hata taa moja ya kumulika—mahali kote kulionekana kuwa gizagiza na kwa kuogofya. Nilisindikizwa hadi katika mojawapo ya majengo. Ndani yake, kulikuwa na dawati na sofa, na balbu ya umeme iliyoning’inia darini ambayo iliangazia kila kitu kwa mwanga hafifu sana. Kulikuwa na kamba na minyororo ya chuma sakafuni, na katikati ya chumba kulikuwa na kiti kilichokuwa kimetengezwa kwa fito nene za chuma. Nilipokabiliwa na tukio hili la kutisha, sikujizuia kuanza kupata hofu. Miguu yangu ilitetemeka na nililazimika kuketi kwenye sofa ili nitulie. Wanaume kadhaa waliingia chumbani baadaye, na nilikaripiwa kwa sauti kubwa na mmoja wao. “Unafikiri unafanya nini, ukikaa hapo? Hicho kiti ni chako ukikalie? Simama!” Alipokuwa akiongea alinijia kwa haraka na kunipiga mateke mara kadhaa, kisha akakamata blauzi yangu kwenye upande wa mbele, akanivuta kwenye sofa na kunirudisha kwenye kiti cha chuma. Polisi mwingine aliniambia, “Unajua, hiki ni kitu kizuri sana, kiti hiki. Unahitaju tu kukikalia kwa muda kidogo na utapata ‘faida’ katika maisha yako yote. Kiti hiki kimetayarishwa hasa kwa ajili yenu ninyi waumini wa Mwenyezi Mungu. Haturuhusu mtu yeyote kukikalia. Kuwa tu msichana mzuri, fanya kile tunachosema, na ujibu maswali yetu kwa uaminifu, halafu hutalazimika kukikalia. Basi tuambie, kwa nini ulikuja Guizhou? Ulikuja kuhubiri injili yenu?” Sikujibu chochote. Polisi aliyeonekana kuwa sugu na ambaye alisimama upande mmoja aliashiria uso wangu na kunitukana, akisema, “Acha kujifanya bubu, ala! Usipozungumza, utapata ladha ya kiti hicho!” Nilisalia kimya.

Wakati huo huo, mwanamke aliyevaa nguo za kuvutia aliingia chumbani, na ikatukia kwamba alikuwa amealikwa na genge hili la polisi aje kunishawishi ili nikiri. Alinishawishi kwa upole wa kinafiki, akisema, “Sikiliza, wewe ni mgeni hapa, na huna jamaa au marafiki karibu. Tuambie tunachotaka kujua, sawa? Mara tu utakapotuambia kile tunachotaka kujua, nitakutafutia kazi, na kukutafutia mume hapa Guizhou. Ninaahidi kuwa nitakutafutia mtu mzuri pia. Lakini kama hutaki hayo, basi unaweza kuja kunifanyia kazi kama yaya wangu. Nitakulipa kila mwezi. Kwa njia hiyo, unaweza kufanya makazi na kuanzisha maisha mapya hapa.” Niliinua kichwa changu na kumtazama, lakini sikujibu. Nilijiwazia: “Pepo ni pepo. Hawatambui kuwepo kwa Mungu, lakini wao hufanya kila aina ya mambo mabaya kwa ajili tu ya pesa na faida. Sasa wanajaribu kutumia faida kunihonga na kunifanya nimsaliti Mungu. Ninawezaje kudanganywa na hila zao za kijanja na kuwa Yuda wa kuaibisha?” Aliona kuwa maneno yake “mema” hayakuwa na athari yoyote kwangu na akahisi kuwa alikuwa ameaibika mbele ya polisi wengine, kwa hivyo aliacha kuonyesha sura ya kinafiki mara moja na kuonyesha tabia yake halisi. Alitoa ukanda kutoka kwenye mkoba wake na kunichapa kikatili mara kadhaa, kisha akatupa mkoba wake kwa ujeuri kwenye sofa. Huku akitikisa kichwa chake kwa hasira, alienda kusimama upande mmoja. Alipoona kilichotokea, polisi mmoja mwovu na mnene alinijia, akanishika kwa nywele na akagongesha kichwa changu ukutani mara kadhaa, akinikaripia kwa meno yaliyokerezwa, “Hujui wakati ambapo mtu anajaribu kukusaidia? Eh? Hujui? Utazungumza au hutazungumza?” Kichwa changu kiligongeshwa ukutani mara nyingi sana kiasi kwamba niliona vimulimuli, kichwa kilikuwa kikizunguka, na nikaanguka sakafuni. Kisha akanivuta na kunirusha kwenye kiti cha chuma kana kwamba nilikuwa tu ndege mdogo. Ni baada tu ya kupata nafuu tena kidogo ndipo nilianza kufungua macho yangu kidogo—nikaona kwamba mkononi mwake bado alikuwa ameshikilia kamba ya nywele zangu zilizonyonyoka. Nilikuwa nimefungiwa kwenye kiti kuanzia kichwani hadi miguuni mwangu, na sahani nene ya chuma iliwekwa mbele ya kifua changu. Pingu zangu zilikuwa zimeshikizwa kwenye kiti, na pingu zenye uzito wa paundi nyingi sana zilikuwa pia zimeshikizwa kwenye miguu yangu, na kisha pia zilikuwa zimefungiwa kwenye kiti. Nilihisi kama sanamu, kutoweza kusogezaa msuli. Minyororo baridi na mizito, makufuli na pingu zilinizuilia kwenye kiti cha chuma—maumivu yangu hayangeelezeka. Waliponiona nikiwa na maumivu, wale polisi waovu waliridhika na wakaanza kunidhihaki, wakisema, “Si Mungu unayemwamini ni Mwenye uweza? Kwa nini haji kukuokoa? Kwa nini hakuokoi kutokana na kiti hiki cha mateso? Ni bora uanze kuongea. Mungu wako hawezi kukuokoa, sisi tu ndio tunaweza kufanya hivyo. Tuambie kile tunachotaka kujua, na tutakuacha uende. Unaweza kuwa na maisha mazuri. Kweli ni hasara kumwamini Mungu fulani!” Niliyakabili maneno ya kejeli ya wale polisi waovu kwa utulivu sana, kwa maana maneno ya Mungu yanasema: “Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuijua Kazi ya Mungu Leo). Kazi ambayo Mungu anafanya sasa ni kazi ya vitendo, si ya kimwujiza. Mungu hutumia maneno Yake kumkamilisha mwanadamu na huruhusu maneno Yake kuwa imani yetu na uzima wetu. Yeye hutumia hali ya kiutendaji kubadilisha tabia zetu za maisha, na ni aina hii ya kazi ya vitendo ndiyo inayoweza kufunua vizuri kabisa nguvu na hekima ya Mungu, na kumshinda Shetani vizuri kabisa kwa mara ya mwsiho. Nilikuwa nimekamatwa na nilikuwa nimepatwa na mateso ya kikatili ya serikali ya CCP kwa sababu Mungu alitaka kujaribu imani yangu Kwake na kuona ikiwa nilikuwa na uwezo wa kuishi kulingana na maneno Yake na kuwa shahidi Kwake. Kwa kuwa nilijua haya, nilitamani kujisalimisha kwa hali yoyote ambayo Mungu aliruhusu inifike. Kimya changu kilikasirisha genge la polisi waovu na walinijia kama kana kwamba wote walikuwa wamepata wazimu. Walinizingira na kunichapa vikali sana. Wengine walinipiga ngumi kwa nguvu kichwani na ngumi zao, wengine walinipiga teke kwenye miguu yangu kwa nguvu, na wengine walirarua nguo zangu na kunipapasa usoni. Nilijawa na hasira nilipokabiliwa na mapigo na uhuni wao wa kikatili. Nisingekuwa nimezuiliwa kabisa kwenye kiti hicho cha mateso, ningekuwa nimepigana vita bila matumaini! Kuhusiana na serikali ya CCP, shirika hilo halifu la kishetani, sikuhisi chochote ila chuki kabisa, na ilibidi tu nitoe uamuzi wa kimya: Kadiri inavyozidi kunitesa, ndivyo imani yangu itakavyozidi kukua, na nitamwamini Mungu mpaka mwisho kabisa! Kadiri inavyozidi kunitesa, ndivyo inavyozidi kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli, na ndivyo inavyozidi kuthibitisha kwamba ninafuata njia ya kweli! Nilipokabiliwa na ukweli huu, niligundua waziwazi kabisa kwamba hivi vilikuwa vita kati ya mema na mabaya, pambano kati ya uzima na kifo, na kwamba kile nilichopaswa kufanya ni kuapa kutetea jina la Mungu na ushuhuda wa Mungu, kumwaibisha Shetani kwa vitendo, na hivyo kumwezesha Mungu kupata utukufu. Wale polisi waovu walijaribu kunifanya nikiri kwa siku kadhaa za mateso na mahojiano, lakini sikuwaambia chochote kuhusu kanisa. Mwishowe, hawakuwa na chaguo, na wakasema, “Huyu ni mbabe. Tumekuwa tukimhoji kwa siku nyingi sasa, lakini hajasema neno.” Nilipokuwa nikiwasikiliza wakinijadili, nilijua kuwa maneno ya Mungu yalikuwa yamenisaidia kupitia katika kila lango la kishetani ambalo pepo hawa walikuwa wameweka mbele yangu, na kwamba Mungu alikuwa amenilinda ili niweze kuwa shahidi Kwake. Nilimshukuru kimya kimya na nikamsifu Mwenyezi Mungu kwa dhati!

Kwa zaidi ya siku kumi za kuhojiwa, nilikuwa nimekaa kwenye kiti hicho baridi cha mateso mchana na usiku, na mwili wangu wote ulihisi kana kwamba ulikuwa umetoswa ndani ya pango lenye barafu. Nilihisi baridi sana, na kila kiungo mwilini mwangu kilikuwa kana kwamba kimepasuliwa. Mmoja wa polisi waovu ambaye alikuwa mchanga kabisa aliniona nikitetemeka kutokana na baridi, na hivyo akachukua fursa ya hali hiyo kuniambia, “Ni bora uanze kuongea! Hata watu wenye nguvu hawawezi kudumu kwa muda mrefu kwenye kiti hiki. Ukiendelea hivi, utakuwa kiwete katika maisha yako yote.” Nilipomsikia akisema hivi, nilianza kudhoofika na kuhisi wasiwasi, lakini nikamwomba Mungu baadaye kimyakimya, nikimwomba Anipe nguvu ya kuvumilia mateso haya ya kinyama na kutofanya kitu chochote kinachoweza kumsaliti Mungu. Baada ya kusali, Mungu alinipa nuru kwa wimbo wa kanisa ambao nilipenda kuuimba kila mara: “Sijali jinsi njia ya imani katika Mungu ilivyo ngumu, natekeleza tu mapenzi ya Mungu kama wito wangu; sembuse kujali ikiwa nitapokea baraka au kuteseka katika siku zijazo. Sasa kwa kuwa nimeamua kumpenda Mungu, nitakuwa mwaminifu hadi mwisho. Bila kujali ni hatari au dhiki gani zinazojificha nyuma yangu, bila kujali mwisho wangu utakuwa upi, ili kukaribisha siku ya Mungu ya utukufu, nafuata kwa makini nyayo za Mungu na kujitahidi kuendelea mbele” (“Kutembea kwenye Njia ya Kumpenda Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kila neno la wimbo huo lilinitia msukumo, na niliimba tena na tena akilini mwangu. Sikuweza kujizuia kufikiria kiapo ambacho nilikuwa nimekila mbele ya Mungu, kwamba bila kujali nilipaswa kupitia mateso au dhiki gani, bado ningetumia maisha yangu kwa ajili ya Mungu na kuendelea kuwa mwaminifu Kwake mpaka mwisho. Lakini nilikuwa nikianza kuhisi dhaifu na mwoga baada ya kupitia maumivu madogo tu—huku kulikuwaje kuwa mwaminifu? Si nilikukuwa nikidanganywa na hila ya kijanja ya Shetani? Shetani alitaka niufikirie mwili wangu na kumsaliti Mungu, lakini nilijua nilihitajika kutomruhusu anidanganye. Kwamba niliweza kuteseka kwa sababu ya imani yangu katika Mungu kilikuwa kitu cha maana, na cha thamani zaidi, lilikuwa jambo la utukufu, na bila kujali niliteseka kiasi gani, sikuweza kujiruhusu kuwa mtu mdogo wa kusikitisha ambaye alikana imani na kumsaliti Mungu. Mara tu nilipofanya uamuzi huu wa kumridhisha Mungu, niliacha kuhisi baridi sana na maumivu yaliyokuwa moyoni mwangu yakatoweka polepole. Kwa mara nyingine, nilikuwa nimeshuhudia matendo ya Mungu ya ajabu na kupata upendo wa Mungu. Ingawa polisi hawakuwa wamefanikisha lengo lao, bado hawakuwa wamemalizana nami. Walianza kuchukua zamu kunitesa, na walinifanya niwe macho usiku kucha na mchana kutwa. Kama ningefumba macho yangu kwa sekunde moja, wangenichapa kwa ufito uliotengenezwa kwa mti mrefu mwebamba, la sivyo wangenipiga kwa nguvu kwa kirungu cha umeme. Kila walipofanya hivyo ningehisi umeme ukipita ndani yangu na mwili wangu wote ungetikisika sana. Maumivu yalikuwa mabaya sana kiasi kwamba yalinifanya nitamani kufa. Walipokuwa wakinipiga, walisema kwa sauti kuu, “Bado huwezi kutuambia kila kitu, ala, hata unataka kwenda kulala! Acha tuone ikiwa tunaweza kukutesa hadi ufe leo!” Vichapo vyao vilizidi kuwa vikali zaidi, na vibaya zaidi na zaidi, na kilio changu kisichokuwa na mategemeo kilipiga mwangwi chumbani kote. Kwa sababu nilikuwa nimefungiwa kikiki kwenye kiti cha mateso na sikuweza kusogeza musuli, sikuweza kufanya chochote ila kujisalimisha kwa ukatili wao. Wale polisi waovu waliridhika hata zaidi na mara chache waliangua kicheko cha kukwaruza. Nilikuwa nimepigwa mijeledi na kutiwa umeme kwa muda mrefu sana kiasi kwamba nilijawa na alama za mapigo na makato, uso, shingo na mikono ilijawa na michubuko ya zambarau, na mwili wangu wote ulikuwa umevimba. Hata hivyo, mwili wangu ulionekana kufa ganzi na sikuhisi uchungu mwingi. Nilijua kuwa ni Mungu aliyekuwa akinitunza na kupunguza maumivu yangu, na moyoni mwangu nilimshukuru Mungu tena na tena.

Nilivumilia haya kwa takribani mwezi mmoja hadi nikawa siwezi kwa kweli kuvumilia tena. Nilitaka sana kulala, hata kwa kitambo kidogo tu. Hata hivyo, pepo hao hawakuwa na ubinadamu hata kidogo. Pindi waliponiona nikiyafumba macho yangu walinitupia glasi nzima ya maji usoni pangu ili kunigutusha kutoka usingizini, na kwa mara nyingine ningelazimisha kusalia macho. Nguvu yangu iliisha kabisa—nilihisi kana kwamba maisha yangu yalikuwa yamekamilika. Lakini kila wakati Mungu alikuwa akinilinda, Akifanya akili yangu iwe bila wasiwasi na iwe tayari na imani yangu kuwa thabiti ili nisimsaliti. Walipoona kwamba hawakuwa wamepata habari yoyote kutoka kwangu hata kidogo na wakiogopa kwamba huenda nikafa kwa kweli, kitu tu ambacho wangeweza kufanya ni kunirudisha kizuizini. Siku tano au sita zilipita na bado sikuwa nimepata nafuu tena kutokana na mateso yao, lakini kwa mara nyingine walinivuta nje na kunifungia kwenye kiti cha mateso. Waliunganisha pingu zile nzito kwa miguu yangu tena, na tena wakajaribu kunifanya nikiri kwa adhabu, mateso na dhuluma. Niliteswa huko kwa karibu siku kumi zaidi, na ni wakati tu ambapo sikuweza kuvumilia tena ndipo mwishowe walinirudisha kizuizini. Siku tano au sita zilipita na wakafanya vilevile tena. Miezi sita ilipita kwa njia hii, na hata sijui walinifanya nipitie hayo mara ngapi—mateso yalikuwa hayo hayo tena na tena. Niliteswa hadi kufikia kiwango cha kuchoka kabisa na kikamilifu, na nikapoteza kabisa tumaini lote la maisha ya baadaye. Nilianza kukataa chakula na kwa siku kadhaa nilikataa kunywa hata tone moja la maji. Baadaye walianza kuninywesha maji kinywani mwangu kwa lazima; mmoja wao alishika kichwa changu huku mwingine akishika uso wangu, akafungua kinywa changu na kumwaga maji. Maji yalitiririka kandokando ya kinywa changu, hadi shingoni mwangu na kulowesha nguo zangu. Mwili wangu wote ulihisi baridi kali na nilijaribu kupambana, lakini sikuwa na nguvu ya kutikisa kichwa changu. Nilipoona kwamba kukataa chakula pia kuliambulia patupu, niliamua kuchukua fursa niliyopewa ya kwenda chooni kugongesha kichwa changu ukutani na kujiua. Nilipokuwa nikiburuta pingu zangu nzito, niliyumbayumba hatua baada ya hatua kuelekea chooni, nikishikilia ukuta hadi mwisho. Kwa sababu sikuwa nimekula kwa muda mrefu, macho yangu yalikuwa na ukungu na sikuweza kuona nilipokuwa nikienda; nilianguka mara nyingi njiani. Kupitia ukungu niliona kwamba vifundo vyangu vilikuwa vimeharibiwa na kuwa nyama ivujayo damu na pingu za chuma, na kwamba vilikuwa vikivuja damu mno. Nilipofika dirishani, niliinua kichwa changu na kutazama nje. Niliona watu kwa umbali wakienda huku na kule, wakiendelea na shughuli zao, na ghafla nikahisi msisimko mzuri ndani yangu, na nikawaza: “Kati ya mamilioni ya watu hawa, ni wangapi wanamwamini Mwenyezi Mungu? Mimi ni mmoja wa wale waliobahatika, kwani Mungu amenichuma mimi—mtu asiye wa ajabu kama mimi—kutoka kwa umati, na Ametumia maneno Yake kuninyunyizia na kuniruzuku, Akiniongoza katika kila hatua ya njia hadi kufikia sasa. Nimebarikiwa sana na Mungu, hivyo kwa nini ninatafuta kifo? Si nitamuumiza Mungu kwa kufanya hivyo?” Wakati huo huo, maneno ya Mungu yalinijia akilini mwangu: “Katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu). Kila neno, lililojaa matumaini na tarajio, lilitia moyo wangu ukunjufu na msukumo, na nilihisi kuguswa sana—nilikuwa nimepata ujasiri wa kuendelea. Nilijipa gumzo la ndani la kujisisimua: “Pepo wanaweza tu kuangamiza mwili wangu, lakini hawawezi kuharibu hamu yangu ya kumridhisha Mungu. Moyo wangu utakuwa wa Mungu milele. Nitakuwa hodari; Sitawahi kusalimu amri!” Kisha nikarudi nyuma, hatua kwa hatua, nikivuta pingu zangu nzito. Katika hali ya kuchanganyikiwa, nilifikiri kuhusu Bwana Yesu, akiwa amejawa kabisa na majeraha, Akitembea kwenye njia ya mateso kuelekea Golgotha, Akiwa amechoka kabisa na kubeba msalaba mzito mgongoni Mwake, kisha nikakumbuka maneno haya kutoka kwa Mwenyezi Mungu. “Alipokuwa njiani kuelekea Yerusalemu, Yesu alihisi maumivu makali, kama kwamba kisu kilikuwa kimedungwa ndani ya moyo Wake, ilhali hakuwa na nia yoyote ya kwenda kinyume cha Neno lake; kila mara kulikuwa na nguvu zenye uwezo mkuu zilizomvutia Yeye kuelekea mahali ambapo Angesulubiwa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu). Wakati huo, sikuweza kuzuia machozi yangu tena, na yalitiririka mashavuni mwangu bila kizuizi. Nilimwomba Mungu moyoni mwangu: “Ee Mungu! Wewe ni mtakatifu sana, na Una mamlaka makuu sana, lakini ili kutuokoa Wewe mwenyewe ulipata mwili. Ulipitia fedheha na maumivu mabaya na Ukasulibiwa kwa ajili yetu. Ee Mungu! Ni nani ambaye amewahi kujua huzuni Yako na maumivu Yako? Ni nani ambaye amewahi kuelewa au kutambua gharama ya biidii Uliyolipa kwa ajili yetu? Ninapitia dhiki hii sasa ili niweze kupata wokovu. Aidha, ninaipitia ili nione waziwazi asili mbovu ya serikali ya CCP ninapokuwa nikipitia udhalimu mikononi mwa pepo wake, ili nisije kamwe nikadanganywa au kughilibiwa nayo tena, na ili nipate kuondolewa ushawishi wake mwovu. Hata hivyo, sijaonyesha kudhukuru mapenzi Yako, lakini nimekuwa nikifikiria tu mwili wangu na kutamani kufa ili mateso ya maumivu haya yaishe. Mimi ni mwoga sana na mwenye kustahili kudharauliwa! Ee Mungu! Unajitumia na kuteseka kwa ajili yetu wakati wote, na Unatupa upendo Wako wote. Ee Mungu! Siwezi kufanya chochote sasa, lakini ninatamani tu kukutolea moyo wangu kabisa, kukufuata mpaka mwisho bila kujali ninaweza kuteseka kiasi gani, na kuwa shahidi kukuridhisha!” Sikuwa nimetoa machozi hata kidogo katika miezi kadhaa ya adhabu na mateso ya kikatili, kwa hivyo niliporudi kwenye chumba cha mahojiano wale polisi waovu waliona kuwa uso wangu ulikuwa na machozi na wakadhani kwamba nilikuwa tayari kukiri. Mmoja wao aliyekuwa mnene alionekana kuridhika mno na akatabasamu, akisema, “Umefikiria jambo hilo vizuri? Utashirikiana?” Nilimpuuza kabisa na uso wake ukageuka na kuwa zambarau mara moja. Ghafla, aliinua mkono na kunizaba kofi usoni mara nyingi sana. Uso wangu uliachwa ukiwasha kwa maumivu huku damu ikichuruzika kutoka pembe za kinywa changu na kuteremka sakafuni. Polisi mwingine mwovu alitupa glasi ya maji usoni pangu na kusema kwa sauti kubwa kwa meno yaliyokazwa sana, “Hatujali ikiwa hutashirikiana. Ulimwengu huu ni wa Chama cha Kikomunisti sasa, na usipozungumza, bado tunaweza kukuhukumu kifungo gerezani!” Lakini bila kujali jinsi ambavyo walijaribu kunitishia na kuniogofya, bado sikusema neno.

Wimbo wa Maisha Katikati ya Uharibifu

Ingawa polisi hawakuweza kupata ushahidi wowote wa kuunga mkono kunishtaki kwa uhalifu, bado hawakufa moyo, lakini waliendelea kujaribu kunitesa ili nikiri. Usiku mmoja wa manane, wengine wao kadhaa walilewa na kuyumbayumba hadi kufika katika chumba cha mahojiano. Mmoja wao, alipokuwa akinitazama kiasherati, alionekana kufikia wazo na akasema, “Mvue nguo zote na umning’inize. Halafu tutaona ikiwa atashirikiana.” Kusikia akisema hivi kuliniogofya, na moyoni mwangu nilimwita Mungu kwa kukata tamaa ili awalaani wanyama hawa na kuzuia hila zao zenye tamaa. Waliniachilia kutoka kwenye kiti cha mateso, lakini sikuweza kusimama kwa sababu ya zile pingu nzito zilizokuwa kwenye vifundo vyangu. Walinizingira na kuanza kunipiga mateke kama mpira wa kandanda, wakitema mbegu za tikiti maji usoni pangu na kusema kwa sauti kubwa tena na tena, “Utashirikiana? Usipokuwa mwema kwetu, basi tutahakikisha maisha yako hayatakuwa na maana! Mungu wako yuko wapi sasa? Si yeye ni Mwenye uweza? Acha Atupige!” Mwingine akasema, “Wang anahitaji mke, itakuwa vipi tukimpa? Haha….” Nilipoona sura zao katili, niliwachukia sana kiasi kwamba machozi yangu yote yakakauka. Nilichoweza tu kufanya ni kumwomba Mungu na kumsihi aulinde moyo wangu ili nisimsaliti, na ili niweze kutii mipango ya Mungu ikiwa ningeishi au kufa. Mwishowe, wale polisi waovu walikuwa wametumia mbinu zao zote lakini bado hawakuweza kupata neno moja kutoka kwangu. Kwa ajili ya kukosa la kufanya, hawakuweza kufanya chochote ila kupiga simu na kuripoti kwa wakubwa wao. “Mwanamke huyu ni shupavu sana. Yeye ni Liu Hulan wa kisasa. Tunaweza kumpiga hadi kufa na bado hawezi kuzungumza. Hakuna kingine tunachoweza kufanya!” Nilipowaona wakikata tamaa kabisa, nilimshukuru Mungu tena na tena moyoni mwangu. Ni mwongozo wa maneno ya Mungu ulioniwezesha kushinda mateso yao ya kikatili tena na tena. Utukufu wote uwe kwa Mwenyezi Mungu!

Licha ya ukweli kwamba mahojiano mengi sana hayakuleta chochote, serikali ya CCP ilinishtaki kwa kuzuia utekelezaji wa sheria na ikanihukumu kifungo cha miaka saba gerezani. Ndugu hao wawili ambao walikuwa wamekamatwa pamoja nami walishtakiwa pia na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani. Baada ya kupitia miezi minane ya mateso ya kikatili, sio tu kwamba kusikia uamuzi huu wa miaka saba gerezani hakukusababisha uchungu au huzuni, lakini badala yake, nilihisi utulivu na, hata zaidi, nilihisi kuheshimiwa. Hii ni kwa sababu katika miezi minane iliyopita, nilikuwa nimepata mwongozo wa Mungu katika kila hatua na nilikuwa nimefurahia upendo na ulinzi wa Mungu usio na mipaka. Jambo hili lilikuwa limeniwezesha kuokoka kimuujiza uharibifu mbaya ambao ungezidi upeo wa uvumilivu wangu, na nilikuwa nimeweza kuwa shahidi. Hii ilikuwa faraja kubwa zaidi ambayo Mungu angeweza kunipa, na nilitoa shukrani zangu na sifa kwa Mungu kwa dhati!

Mnamo Novemba 3, mwaka wa 2008, nilitumwa katika Gereza la Kwanza la Wanawake kutumikia kifungo changu, na kwa hivyo nilianza maisha yangu marefu gerezani. Kulikuwa na mfumo mkali wa sheria kiasi cha kushangaza gerezani; tuliamka saa 12 asubuhi na kuanza kazi, na kisha tukafanya kazi siku nzima mpaka usiku. Wakati wa kula na mapumziko ya kwenda chooni yalijaa wasiwasi kana kwamba tulikuwa kwenye ukanda wa vita, na wafungwa hawakuruhusiwa kuzembea hata kidogo. Walinzi wa gereza walitupa kazi kupita kiasi ili waweze kufaidi hata zaidi kutokana na kazi yetu, na walikuwa wakatili zaidi kwa wale waliomwamini Mungu. Kwa ajili ya kuishi katika mazingira kama haya, nilikuwa mwenye wasiwasi kila wakati—kila siku ilikuwa kama mwaka mzima. Nilipewa kazi ngumu zaidi na nzito zaidi gerezani, na chakula nilichopewa nile hakikufaa hata kwa mbwa—andazi dogo, jeusi, lililokuwa halijaiva vizuri, na lililopikwa kwa mvuke na majani kiasi ya kabichi yaliyochakaa na kukauka. Katika jitihada za kufanya kifungo changu kipunguzwe kwa ajili ya tabia nzuri, mara nyingi nilifanya kazi kwa bidii kadiri nilivyoweza kuanzia alfajiri hadi jioni, na hata kufanya kazi usiku kucha ili kutosheleza kiasi cha uzalishaji ambacho kilizidi uwezo wangu wa mwili. Nilisimama kila siku kwa saa 15 au 16 kwenye karakana, nikizungusha bila kukoma usukani wa mashine ya kutengeneza sweta iliyokuwa nusu otomatiki. Miguu yangu yote ilivimba na mara nyingi iliuma na kuhisi dhaifu. Bado, sikuwahi kuthubutu kupunguza mwendo, kwa sababu kulikuwa na walinzi wa gereza wenye virungu vya umeme waliofanya doria katika karakana ile, na walimwadhibu yeyote ambaye waliona kwamba hakufanya kazi kwa nguvu zote, na kuwanyima wafungwa alama za tabia nzuri. Kazi ngumu isiyoisha ilinichosha sana mwilini na akilini. Ingawa bado nilikuwa mchanga, nywele zangu nyingi ziligeuka kuwa kijivu, na mara nyingi nilikuwa karibu kuzimia kwenye mashine. Isingekuwa ulinzi wa Mungu, nisingeweza kuendelea kuishi. Mwishowe, chini ya ulinzi wa Mungu, nilipata nafasi mbili za kupunguziwa kifungo changu, na niliweza kuondoka mahali pale pabaya sana miaka miwili kabla ya muda niliowekewa.

Baada ya kupitia miezi minane ya mateso ya kinyama na miaka mitano ya kufungwa mikononi mwa serikali ya CCP, mwili wangu na akili ziliharibiwa vibaya. Niliogopa sana kukutana na wageni muda mrefu baada ya kuachiliwa. Hasa, wakati wowote nilipojikuta mahali penye shughuli nyingi na watu wengi waliotembea haraka, matukio ya wale polisi waovu wakinitesa yalijaa akilini, na ningepata hisia kuu za hofu na kutokuwa na utulivu ndani yangu. Mfuatano wangu wa hedhi ulikuwa umevurugwa kutokana na kufungiwa kwenye kiti hicho cha chuma kwa minyororo kwa muda mrefu sana, na niliathiriwa na kila aina ya magonjwa. Sasa ninapokumbuka miezi hiyo ya kuchosha na ya maumivu, ingawa nilipata maumivu na mateso mengi, niliona waziwazi kuwa “uhuru wa imani ya dini” na “haki halali na masilahi ya raia hulindwa na sheria” ambavyo hutangazwa mara nyingi na Serikali ya CCP ni hila tu za kuficha dhambi zao na asili yao mbovu. Wakati huo huo, pia nilikuja kwa kweli kupitia na kutambua uweza, ukuu, mamlaka na nguvu za Mungu, na niliweza kuhisi shauku ya Mungu na rehema Yake kwangu. Vitu hivi vyote vilikuwa utajiri wa thamani na mwingi wa maisha ambayo Mungu alinipa. Kazi ya Mungu ni ya vitendo na ya kawaida, na Yeye huruhusu mateso ya Shetani na pepo yatufike. Lakini pepo wanapokuwa wakitudhuru kwa hasira, Mungu yuko kila wakati, Akitulinda na kutukinga kimya kimya, Akitumia maneno Yake ya mamlaka na nguvu kutupa nuru na kutuongoza. Mungu hutupa imani na upendo, na Yeye hushinda na kumwangamiza adui Shetani, na hivyo kupata utukufu. Ninasifu hekima na uzuri wa Mungu kwa dhati!

Wimbo wa Maisha Katikati ya Uharibifu

Sasa nimerudi kanisani na nimerudi kuwa na ndugu zangu. Chini ya mwongozo wa upendo wa Mungu, ninaishi maisha ya kanisa, na pamoja na ndugu, kwa uwiano, tunaeneza injili ya ufalme. Maisha yangu yamejaa bidii na nguvu. Sasa nimejawa na imani kwa kazi ya Mungu. Kwa kweli naweza kuona maono mazuri ya ufalme wa Mungu yakijidhihirisha duniani, na sina budi kuimba sifa za Mungu! “Ufalme wa Kristo Umeshuka Duniani, Neno la Mungu limetawala duniani. Tunaweza kuliona lote kwa macho yetu wenyewe, vyote vimewezekana kwa neno la Mungu. Tunashangilia! Tunasifu! Ufalme wa Kristo tayari uko duniani. Neno la Mungu liko kati yetu, linaishi kati yetu, liko pamoja nasi katika kila hatua na mawazo yetu. … Uzuri wa ufalme wa Mungu ni mkuu na wa milele. Wote wanatangaza neno la Mungu, wakitii neno Lake na kumwabudu Yeye. Ulimwengu wote unagaagaa kwa furaha. Tunasherehekea kwamba kazi Yake imefanywa, kwamba Yeye ni mtakatifu, mwenye uweza, haki na hekima. Mungu anatuongoza kuingia Kanaani Mwenyewe, hivyo sisi pia tunaweza kufurahia utajiri Wake!” (“Ufalme wa Kristo Umeshuka Duniani” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ujana Usio na Majuto Yoyote

Xiaowen Jijini Chongqing“‘Upendo,’ kama unavyoitwa, unaashiria hisia safi isiyo na dosari, ambapo unatumia moyo wako kupenda, kuhisi,...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp