Mateso na Taabu Zilinifanya Nimpende Mungu Hata Zaidi

26/01/2021

Na Liu Zhen, Mkoa wa Shandong

Jina langu ni Liu Zhen. Nina umri wa miaka 78, na mimi ni Mkristo wa kawaida tu katika Kanisa la Mwenyezi Mungu. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuniteua mimi, mwanamke mkongwe kutoka kijiji cha mashamba ambaye si wa ajabu machoni pa watu. Baada ya kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, kila siku nilimwomba Mungu, nikasikiliza masimulizi ya neno la Mungu, na kuenda katika mikutano na kufanya ushirika na ndugu zangu, na polepole, nilianza kufahamu ukweli fulani na kuwa na ufahamu dhahiri kuhusu mambo fulani. Nilihisi kujawa na furaha, na niliishi kwa furaha ambayo sikuwahi kuhisi hapo awali. Kwa sababu mimi ni mzee na huwa na shida kutembea, sikuweza kutoka nyumbani kwenda kuhudhuria mikutano ya kanisa, kwa hivyo kwa sababu ya kunijali, ndugu zangu walifanya mikutano nyumbani kwangu. Hawakuwahi kukosa kuhudhuria mkutano wowote kwa sababu ya baridi ya majira ya baridi au joto la majira ya joto, na upepo, mvua na theluji havikuwazuia kamwe kuja kunitembelea na kunitunza, mwanamke mzee tu kama mimi. Hasa tuliposoma neno la Mungu, ikiwa kuna kitu chochote ambacho sikukielewa, kila wakati wangeshiriki nami kwa uvumilivu kukihusu, na kamwe hawakunipuuza au kunidharau. Niliguswa sana na haya, kwa sababu isingekuwa upendo wa Mungu, ni nani angeonyesha uvumilivu na upendo kama huo kwangu? Katika maingiliano yangu na ndugu zangu, niliona kuwa walikuwa tofauti sana na watu wasio wataalam. Walichoishi kwa kudhihirisha kilikuwa stahamala na upendo, na waliweza kufungua mioyo yao na kutendeana kwa uaminifu, bila kizuizi chochote au utengano wowote baina yao. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana kama familia, na hili lilinifanya nihisi hakika hata zaidi kuhusu kazi ya Mwenyezi Mungu. Nilipokuwa nikianza kufahamu ukweli zaidi, niligundua kwamba ninapaswa kutekeleza wajibu wangu kama kiumbe aliyeumbwa, kwa hivyo niliambia kanisa kuwa nilitaka kuchukua wajibu. Kwa sababu umri wangu ulinizuia kufanya kazi nyingi, hata hivyo, kanisa lilinipa wajibu wa kuandaa mikutano nyumbani kwangu. Nilikubali, nikimshukuru Mungu kwa kunipa wajibu kulingana na uwezo wangu. Na kwa hivyo, nilielewana na ndugu zangu vizuri sana, na nilihisi utulivu mkubwa katika mwili na mawazo. Magonjwa kadhaa ambayo nilikuwa nikiugua pia yalianza kupona, na kwa hivyo nilimshukuru Mwenyezi Mungu hata zaidi kwa ajili ya neema na rehema Zake.

Hata hivyo, nyakati nzuri hazikudumu kwa muda mrefu, kwa sababu mimi na ndugu zangu kijijini tulishtakiwa na mtu mpotovu. Ndugu zangu wote walikamatwa na polisi, na wakamwamuru katibu wa Chama wa kijiji anipeleke katika kituo cha polisi. Mara tu nilipofika huko, polisi waliniuliza, “Je, ulikuja kumwamini Mungu vipi? Kwa nini unamwamini Mungu?” Nikasema, “Kumwamini Mungu ni kanuni isiyoweza kubadilika. Kwa kusoma neno la Mungu kila siku, tunaweza kuelewa ukweli mwingi, kuwa watu wazuri kulingana na neno la Mungu, na kutembea katika njia inayofaa maishani. Waumini wa Mungu hawapigi au kuwatusi wengine, na sisi hufuata sheria kila wakati, kwa hivyo kuna nini kibaya katika kumwamini Mungu? Mbona mnatukamata?” Afisa huyo alinitazama kwa dharau na kuniuliza kwa ukali, “Ni nani aliyekuhubiria injili? Je, kuna mtu mwingine yeyote katika familia yako anayeamini?” Nilisema kuwa ni mimi tu katika familia yangu niliyeamini. Waliona kwamba hawangepata habari yoyote kutoka kwangu, kwa hivyo waliniachilia siku hiyo hiyo. Baada ya kuondoka, nilijiuliza ni kwa nini polisi waliniachilia huru kwa urahisi sana. Ni mara tu niliporudi nyumbani ndipo nilipata habari kuwa, familia yangu ilipogundua kuwa nilikuwa nimepelekwa katika kituo cha polisi, walikuwa wametumia mahusiano yao na kuwalipa polisi yuani 3,000 ili waniachilie. Lakini polisi walikuwa bado wakieneza ugomvi kati ya mimi na familia yangu, kwani walikuwa wameiambia familia yangu inizuie kumwamini Mungu. Mkwe wangu aligombana na mwanangu kuhusu jambo hili na akatishia kujiua kwa kunywa kiuadudu ikiwa ningeendelea kumwamini Mungu. Wakati huo ndipo niligundua kuwa polisi wa CCP walikuwa waovu mno. Nilikuwa na familia yenye amani sana, ilhali sasa walikuwa wamechochea mambo sana kiasi kwamba sote tulikuwa tukigombana! Nilimwamini Mungu mmoja wa kweli aliyeumba vitu vyote mbinguni na duniani, na leo, Mwenyezi Mungu amekuja kutuokoa kwa kutuhimiza tufahamu ukweli, tuishi kwa kudhihirisha mfanano wa binadamu, tuzungumze na kutenda kwa njia ambazo zinakubaliana na dhamiri yetu na kile kilicho chema, na tusifanye mambo ambayo yanakwenda kinyume na ubinadamu wetu au maadili yetu. Nilichofanya tu ni kukaa nyumbani na kusoma neno la Mungu, kufanya mikutano, na kutimiza wajibu wangu, lakini polisi wa CCP walinisingizia na kunishtaki kwa kosa la “kuvuruga amani ya umma.” Walikuwa wakipotosha ukweli waziwazi, wakibadili ukweli kimakusudi, kuwashtaki watu kiholela kwa uhalifu wa uwongo! Shetani ni mwenye kudharauliwa kweli. Halikuwa lingine ila uchongezi na kashfa za wazi za nia mbaya. Polisi walikuwa wamepata habari kutoka kwa kijumbe mtoa habari kwamba nilikuwa nikiandaa mikutano na ndugu zangu nyumbani kwangu, kwa hivyo hawakuacha kunisumbua baada ya hapo. Muda mfupi baadaye, walinipeleka katika kituo cha polisi ili kunihoji, na kunitisha kwa kusema, “Tuambie majina ya viongozi wa kanisa lako na watu unaowaalika kwenye mikutano. Ikiwa hutatuambia, tutakutia gerezani!” Kwa ukali lakini kwa haki, nilijibu, “Sijui chochote! Sina chochote cha kuwaambia!” Polisi walikasirika sana kiasi kwamba hawangezungumza, lakini kwa sababu Mungu alinilinda, hawakuthubutu kunifanyia lolote.

Baada ya polisi kuniachilia, waliendelea kunipeleleza, wakitarajia bila mafanikio kunitumia kama chambo ili kumkamata “samaki mkubwa zaidi.” Niliogopa kuwaingiza ndugu zangu lawamani, kwa hivyo sikuthubutu tena kuwasiliana nao, na baadaye niliacha maisha ya kanisa. Bila maisha ya kanisa, moyo wangu ulihisi mtupu na usio na kimbilio, na polepole nilitenganishwa na Mungu. Niliishi kila siku katika hofu na woga, nikihofia sana polisi wangekuja kunikamata tena. Hapo zamani, nilikuwa nikitumia kila siku kusikiliza neno la Mungu na Mahubiri na Ushirika, lakini sasa hayo hayangewezekana, kwa sababu ikiwa wangeniona nikisali au hata ningetaja neno “Mungu,” ningepata karipio kubwa kutoka kwa familia yangu. Mkwe wangu alinizungumzia bila upendo wakati wote kwa sababu nilikuwa nimepigwa faini na polisi, na mume wangu pamoja na mwanangu walinikemea daima. Familia ambayo hapo nyuma iliunga mkono imani yangu katika Mwenyezi Mungu sasa ilinipinga na kunitesa jinsi walivyoweza. Hili lilinisikitisha sana, roho yangu ilihisi kukandamizwa sana, na niliishi katika giza na maumivu ambayo sikuwahi kuhisi hapo awali. Kwa sababu sikuwa na masimulizi ya neno la Mungu ya kusikiliza na sikuweza kushiriki na ndugu zangu, roho yangu ilihisi iliyokauka sana. Kila usiku niligaagaa na kugeuka kitandani na sikuweza kulala, na kila mara nilikumbuka nyakati za furaha nilizokuwa nazo katika mikutano pamoja na ndugu zangu. Nyakati kama hizi, niliichukia serikali ya CCP. Ilikuwa imesababisha taabu hizi zote, ilinifanya nipoteze haki zote za kiumbe aliyeumbwa za kumwamini na kumwabudu Mungu bila kizuizi, ilinifanya nipoteze maisha yangu ya kanisa, ilinizuia kushiriki juu ya neno la Mungu pamoja na ndugu zangu, na kunizuia kutekeleza wajibu wangu. Katika taabu yangu, niliweza tu kumwomba Mungu kimoyomoyo: “Ee Mungu! Ninaishi gizani, ninahisi kama roho yangu imekauka, na ninataka kuishi maisha ya kanisa pamoja na ndugu zangu. Ee Mungu! Ninakuomba unifungulie njia!”

Nilienda mbele za Mungu na kuendelea kumwomba kwa namna hii, na Mungu kwa kweli alisikia maombi yangu, kwani Alipanga ndugu zangu wanitembelee. Dada yangu mmoja alijua kwamba mimi mara nyingi nilikwenda kwenye shamba la pamba ili kuchuna pamba, kwa hivyo alikwenda huko kisirisiri kuniona, na tulipanga wakati wa kufanya mikutano huko. Kila wakati tulipokutana, nilikuwa nje shambani nikichuna pamba mapema, na wakati kila mtu alikuwa akila chakula cha mchana, nilichuchumaa pamoja na dada yangu shambani ili kusoma neno la Mungu. Kumwona dada yangu kulikuwa kama kumuona jamaa aliyepotea kwa muda mrefu. Sikuweza kuzuia machozi ya furaha kutiririka. Nilimweleza kuhusu udhalimu na taabu ambayo nilikuwa nimevumilia, pamoja na suitafahamu za familia yangu. Alinifariji wakati maneno ya Mungu yalikuwa yakininyunyizia, na alifanya ushirika pamoja nami kuhusu mapenzi ya Mungu, na polepole, hali yangu ilianza kuwa nzuri zaidi. Hivi ndivyo mateso ya serikali ya CCP ilivyofanya niweze tu kufanya mikutano nikichuchumaa katika shamba la pamba. Siku moja, tulisoma kifungu cha neno la Mungu: “Kati yenu, hamna mtu mmoja anayepokea ulinzi wa sheria; badala yake, unaadhibiwa na sheria, na ugumu mkubwa zaidi ni kuwa hapana mtu anayekuelewa, awe ni jamaa yako, wazazi wako, marafiki wako, ama watendakazi wenzako. Hakuna anayekuelewa. Mungu ‘Anapokukataa,’ hapana uwezekano wako kuendelea kuishi duniani. Hata hivyo, watu hawawezi kumwacha Mungu; huu ndio umuhimu wa ushindi wa Mungu kwa watu, na huu ni utukufu wa Mungu. … Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa ajili ya Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la mwisho la kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?). Neno la Mungu lilinifanya nifahamu kwamba mateso yangu ya wakati huo yalikuwa kitu ambacho nilipaswa kuvumilia. China ni nchi inayotawaliwa na ukanaji Mungu ambapo waumini wa Mungu wanateswa na kuaibishwa, lakini mateso haya yalikuwa ya muda mfupi na yalikuwa na kikomo, na yalipangwa na Mungu kwa uangalifu ili kukamilisha imani na utiifu wangu Kwake, ili niweze kupokea vizuri ahadi na baraka za Mungu katika siku za usoni. Sasa sikuwa na tamaa nyingine tena, kwa sababu kuwa na Mungu kulitosha. Wakati huo huo, niliona kwamba sheria zilizotungwa na serikali ya CCP ni hila tu za kuwadanganya watu. Kwa watu wengine ulimwenguni inadai kwamba inaunga mkono uhuru wa kidini, lakini kwa kweli, waumini wa Mungu hata hawana haki ya kusoma neno la Mungu au kufanya mikutano. Haivumilii kabisa uwepo wa waumini wa Mungu, na haiwaruhusu watu kumfuata Mungu au kutembea katika njia inayofaa maishani. Kama vile tu maneno ya Mwenyezi Mungu yasemavyo: “Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)). Mbingu na dunia zilizoundwa na Mungu ni kubwa, lakini nchini China waumini katika Mungu hawana hata mahali pa usalama. Mtu yeyote anayemwamini Mungu hukamatwa na kuteswa na uhuru wao kuwekewa mipaka. CCP inataka tu kumuua kila muumini wa Mungu na kuigeuza China kuwa taifa lisilomtambua Mungu. CCP ni potovu, mbaya, na ya kupinga maendeleo sana. Kwa kweli haiwezi kupatanishwa na Mungu, ni adui wa Mungu ambaye hawezi kuvumilia uwepo Wake!

Na kwa hivyo, niliendelea kukutana na dada yangu kisirisiri katika shamba la pamba. Lakini wakati ulipita, na hatimaye ikakuwa majira ya baridi. Majani ya mimea ya pamba ilinyauka na kuanguka, na shamba la pamba halikuwa tena na maficho yoyote kwetu kufanyia mikutano, kwa hivyo nilijikuta tena bila ndugu wa kushiriki nao kuhusu neno la Mungu. Mwanzoni, niliweza kuhifadhi neno la Mungu na kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lakini bila ruzuku na unyunyizaji wa neno la Mungu, roho yangu ilizidi kuwa tupu na kavu, na muda si muda, niliingia gizani tena. Nilihisi kuwa nilikuwa nimeshuka kutoka mbinguni na kuingia kuzimuni, na nilikuwa katika taabu sana kiasi kwamba kifo kingekuwa heri. Familia yangu iliamini uwongo wa polisi, kwa hivyo walinilinda kila siku, na kunitishia kwa adhabu ikiwa ningeendelea kumwamini Mwenyezi Mungu. Nyumbani, sikuthubutu kuomba. Ningeweza kusali tu nikijificha ndani ya blanketi zangu usiku au wakati ambapo hakukuwa na mtu mwingine nyumbani, na niliishi kila siku kwa njia hii. Kando na kuvumilia shitaka baada ya shitaka ya familia yangu, pia ilinibidi nivumilie uvumi na udaku wa wanakijiji. Nikikabili haya yote, nilihisi mwenye taabu hasa, kiroho nilihisi dhaifu na asiyejiweza, na nilikuwa na huzuni kila siku. Nilihisi kuwa, baada ya kupoteza maisha ya kanisa, kutokuwa na uwezo wa kusoma neno la Mungu, na kutokuwa na uwezo wa kuwaona ndugu zangu, kuwa hai tu kulikuwa taabu, kwamba kulikuwa kumepoteza furaha yake yote. Nilifikiria jinsi hapo zamani, nilipohisi dhaifu na mwenye taabu, maneno ya Mungu yalinifariji kila wakati, ndugu zangu walinihimili kwa subira, na baada ya kufahamu mapenzi ya Mungu, ningehisi raha na huru mara moja, na uchangamfu wangu ungeongezeka tena. Lakini sasa, kwa sababu ya mateso na upelelezi wa polisi, nilikuwa nimepoteza haki ya kusoma neno la Mungu, na hata singeweza kuwaona ndugu zangu. Kila siku ilikuwa mapambano marefu, magumu kuvumiliwa, na nilipoona jinsi nilivyoishi bila kuhisi uchangamfu, kana kwamba nilikuwa mfu, na kuzingatia jinsi nilivyokuwa mchangamfu hapo zamani nilipokuwa nikiishi mbele za Mungu kanisani, nilihisi uchungu na mwenye taabu. Na nilipofikiria jinsi familia yangu ilikuwa imepumbazwa na kudanganywa na CCP, jinsi hawakunielewa, na jinsi walivyokuwa wamekubaliana na CCP katika kuzuia uhuru wangu, nilihisi mwenye huzuni zaidi. Lakini nilipokuwa tu nikihisi kama sikuwa na la kufanya, nilimwomba Mungu mara kwa mara na nikamsihi anifungulie njia: “Ee Mungu! Sasa, siwezi kusoma neno lako, wala siwezi kuishi maisha ya kanisa, na maisha haya ni magumu mno kwangu kuvumilia. Ee Mungu! Familia yangu imedanganywa na serikali ya CCP na inajaribu kwa nguvu zake zote kunizuia nikuamini. Tafadhali, nisaidie, Uniruhusu nishuhudie matendo Yako, na Uwazuie kudanganywa na kutumiwa na Shetani tena. Ee Mungu! Ningependa kukabidhi familia yangu Kwako, na ninaomba Unionyeshe njia ya kutoroka hali hii.”

Namshukuru Mungu, Alisikiza sala zangu kwa kweli. Muda fulani baadaye, nilizirai ghafla mbele ya kitanda changu jioni moja. Mume wangu alitishika sana na hakujua cha kufanya, kwa hivyo mwanangu alipigia huduma za dharura simu upesi. Hospitali ya kwanza kujibu iliposikia kuwa mgonjwa alikuwa mwanamke mkongwe ambaye alikuwa mgonjwa sana, walikataa kunipokea. Mwanangu alipiga simu kwa nambari ya dharura ya hospitali nyingine, na daktari alisema hakukuwa na matumaini makubwa kwangu kupata fahamu, kwamba hakukuwa na haja ya kufanya chochote kuniokoa, na kwamba familia yangu inapaswa kujiandaa kupata mkasa. Lakini mwanangu alikataa kukata tamaa, na aliwasihi hadi wakakosa lingine la kufanya ila kutulia na kunipeleka hospitalini. Hata hivyo, hata baada ya utaratibu wa uokoaji wa dharura, nilibaki bila fahamu. Hakuna kitu ambacho madaktari wangeweza kufanya, na familia yangu ilikuwa na hakika kuwa singeendelea kuishi. Ila kwa Mungu, hakuna lisilowezekana, kwa sababu wakati huo ndipo muujiza ulitokea! Baada ya kuzimia kwa muda wa saa 18, nilipata tena fahamu polepole. Kila mtu aliyekuwepo hapo alipigwa na butwaa. Nilipofungua macho yangu na kuwaona madaktari, nilidhani kuwa nilikuwa nikiwaangalia malaika. Niliwauliza nilipokuwa, mmoja wao aliniambia nipo hospitalini, na walipokuwa wakikagua viungo vyangu muhimu kwa haraka, waliendelea kusemea chinichini, “Huu kweli ni muujiza....” Muda si muda, niliketi, na kuhisi njaa sana. Muuguzi alinilisha, na baada ya kumaliza kula, nilihisi niliyejawa nishati na nguvu. Nilijua kuwa hii ilikuwa mojawapo ya vitendo vya kimiujiza vya Mwenyezi Mungu, kwamba Mungu alikuwa amesikia maombi yangu na kunifungulia njia. Nilipokuwa nikiketi kitandani sikuweza kujizuia kuimba kwa kumsifu Mungu. Daktari aliyeshangaa hakuweza kujizuia kuuliza, “Mama, ni Mungu gani huyu unayemwamini?” Nikasema, “Ninamwamini Mungu mmoja wa kweli aliyeumba vitu vyote mbinguni na duniani—Mwenyezi Mungu!” Daktari alijibu kwa kuniangalia kwa mshtuko, na familia yangu ilionekana kushangazwa na kufurahi walipokuwa wakiniona nikiimba. Baada ya kutoka hospitalini, nilienda nyumbani, na mmoja baada ya mwingine majirani zangu walikuja kuniona, wakisema, “Ni jambo la kushangaza! Madaktari wote walisema hakukuwa na tumaini kwako, lakini kwa kweli uliamka. Ni muujiza!” Nilimshuhudia Mungu kwao, nikisema kwamba hii ilikuwa kwa sababu ya nguvu kubwa ya Mungu, kwamba Mungu alikuwa ameniokoa, kwamba bila Mungu ningekuwa nimekufa sasa, na kwamba ni Mungu aliyekuwa amenipa nafasi ya pili maishani. Niliwaambia kwamba wanadamu wote waliumbwa na Mungu, kwamba Mungu hutupa uhai, kwamba Mungu husimamia na kutawala maisha yetu, na kwamba watu hawawezi kukataa mwongozo wa Mungu, kwa sababu kumkataa Mungu kunamaanisha kifo. Baada ya kupitia haya, familia yangu haikupinga tena imani yangu katika Mungu, na Mungu pia alinipa baraka isiyotarajiwa—mume wangu pia alikubali kazi ya Mungu ya hatua ya sasa. Baada ya hapo, mume wangu alikwenda mikutanoni mara kwa mara nami ili kushiriki, na nilihisi furaha, amani, na salama sana. Kisha niliishi kila siku katika furaha, kwa sababu nilikuwa kweli nimeona uweza na hekima ya Mungu, na nikamshukuru na kumsifu Mungu kwa dhati!

Kupitia uzoefu wangu, nilikuja kutambua kwa kweli kuwa bila kujali kile Mungu anachomfanyia mtu, Yeye hufanya hivyo kwa ajili ya upendo. Msingi Wake wa kumruhusu Shetani anitese ni nia njema za Mungu. CCP ilitaka kutumia kukamatwa na kuteswa kwangu kunifanya nimwepuke Mungu na nimsaliti Mungu, lakini haikujua kwamba hekima ya Mungu hutumika kulingana na hila za Shetani. Ukandamizaji wa CCP haukushindwa tu kunifanya nimwepuke Mungu au nimsaliti Mungu, lakini badala yake uliniruhusu nifahamu dhahiri asili mbaya yaa CCP ya kumpinga Mungu na kutenda kinyume na Mbingu, na ukaimarisha zaidi uhakika wangu kwamba neno la Mwenyezi Mungu ndilo kweli, njia, na uzima! Pia uliniruhusu kuona nguvu kubwa na matendo ya miujiza ya Mungu, na kwa njia hiyo kuimarisha upendo wangu na uaminifu wangu kwa Mungu. Kama vile tu neno la Mwenyezi Mungu linavyosema: “Katika mpango Wangu, Shetani amewahi kushindana na kila hatua, na, kama foili[a] ya hekima Yangu, amejaribu siku zote kutafuta njia na namna za kuvuruga mpango Wangu wa awali. Lakini Ningeweza kushindwa na njama zake danganyifu? Vyote mbinguni na duniani vinanitumikia—njama danganyifu za Shetani zingeweza kuwa tofauti? Huku ndiko hasa kukutana kwa hekima Yangu, ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu matendo Yangu, na ni kanuni ya utendaji ya mpango Wangu mzima wa usimamizi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 8). Kadiri CCP inavyompinga Mungu bure na kuwatesa watu walioteuliwa na Mungu, ndivyo tunavyoweza kuitambua na kuiacha zaidi, na ndivyo tunavyoweza kufahamu ukweli na kujua hekima na matendo ya miujiza ya Mungu zaidi. Imani yetu katika kumfuata Mungu pia huongezeka, na tunaweza zaidi kutoa ushuhuda mkubwa sana kwa ajili ya Mungu. Kupitia mateso ya CCP, nilifahamu wazi kuwa, katika kazi ya Mungu, Shetani hufanya kazi kama foili tu, na ni chombo cha huduma cha Mungu, na pia nilikuja kujua wazi zaidi mapenzi ya Mungu ya dhati ya kuwaokoa wanadamu. Katika siku zijazo, bila kujali ni dhiki gani au vizuizi vipi ninavyokabili, natamani kutekeleza wajibu wangu kwa uwezo wangu wote na kufanya niwezalo kuridhisha mapenzi ya Mungu.

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp