Nuru ya Mungu Huniongoza Kupitia Dhiki
Nlipokuwa mtoto, niliishi milimani. Sikuwa kamwe nimepata kuzuru maeneo mengi ya ulimwengu na kwa kweli sikuwa na hamu yoyote kubwa zaidi. Niliolewa na kupata watoto, wanangu wawili walikua na kuwa wenye busara na watiifu, na mume wangu alikuwa mwenye bidii. Ingawa hatukuwahi kuwa na pesa nyingi, tuliishi pamoja kwa amani kama familia, na nilihisi furaha sana na kuridhika. Mnamo mwaka wa 1996, ghafla nilipatwa na ugonjwa hatari ambao ulinipelekea kumwamini Bwana Yesu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, nilisoma Biblia mara kwa mara na nilihudhuria mikusanyiko ya kanisa kwa bidii. Jambo la kushangaza ni kwamba ugonjwa wangu ulianza kupona polepole, na kwa hivyo imani yangu ya kumfuata Bwana Yesu iliendelea kuwa thabiti hata zaidi.
Hata hivyo, kitu ambacho kwa kweli singeweza kutarajia kilitokea mnamo mwaka wa 1999, nilipokamatwa na polisi kwa ajili ya imani yangu katika Bwana Yesu. Nilizuiliwa siku nzima na kutozwa faini ya yuani 240. Ingawa hizi zinaweza kuonekana kama pesa zisizo nyingi, kwetu sisi wakulima masikini wanaoishi katika eneo fukara la mlima, hizo si pesa kidogo! Ili kukusanya pesa za kutosha, niliuza njugu zote ambazo nilikuwa nimezipanda kwa bidii katika kipande changu cha ardhi. Kile ambacho sikuweza kuelewa ni kwa nini serikali ya CCP ilinipachika jina la mhalifu ambaye “alishiriki katika mashirika yanayopinga maendeleo.” Pia waliitisha familia yangu nzima, wakisema kwamba hata kama wanangu wangehitimu katika chuo kikuu, bado hawangeweza kupata kazi. Kwa hivyo, mume wangu, wazazi wangu, jamaa na marafiki wote walianza kunishinikiza, walijaribu kukomesha na kuzuia imani yangu. Walinilazimisha nifanye kazi zote zilizo ngumu na za kuchosha, na kile ambacho niliweza kukifanya tu ni kuvumilia kimyakimya.
Mnamo mwaka wa 2003, nilikuwa na bahati ya kutosha kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Kupitia kusoma maneno ya Mungu, nilianza kuwa na uhakika kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi. Nilisisimka kabisa, na nilihisi kwamba kuweza kuunganishwa tena na Mungu katika maisha yangu mwenyewe kwa kweli ilikuwa baraka kubwa zaidi kabisa! Hata hivyo, kuanzia wakati huo na kuendelea, shinikizo nililowekewa na serikali ya CCP na familia yangu liliendelea kuwa kubwa zaidi. Nilipokabiliwa na hali kama hii, nilifanya azimio kwa Mungu: “Bila kujali hali itakuwa gumu kiasi gani au nitateseka kiasi gani, Nitakufuata hadi mwisho!” Polisi wa CCP baadaye walikuja nyumbani kwangu na kunitisha, wakisema, “Je, wajua kwamba imani yako katika Mungu si halali, na kuwa haikubaliki katika nchi hii? Ikiwa utadumisha imani yako utaishia kufungwa!” Mume wangu alipoyasikia haya, alianza kuniongezea shinikizo zaidi na zaidi. Mara nyingi angenipiga na kunikaripia, na hangeniruhusu nikae nyumbani kwetu. Kwa kuwa sikuwa na lingine la kufanya, nilichoweza kufanya ni kuficha uchungu niliohisi ndani na kuondoka nyumbani ili kuepuka mateso na kukamatwa na serikali ya CCP. Wakati huo, ingawa mateso ya CCP yalikuwa yamenilazimisha niondoke kutoka katika mji wangu na kwenda katika maisha ya uzururaji na, bado sikuwa na utambuzi kuhusu chanzo kibaya kilichosababisha kuvunjika kwa familia yangu. Ni wakati tu nilipopitia maisha gerezani mimi binafsi na mashambulizi yasiyodhibitiwa na mashtaka ya uwongo yaliyotolewa dhidi yangu na serikali ya CCP ndipo nilipopata ufahamu fulani wa kweli kuhusu asili potovu na ya kupinga maendeleo ya CCP, na niligundua kuwa CCP ndiye mhalifu mkuu ambaye huangamiza familia za watu zenye furaha na kuwasababishia watu majanga mabaya.
Mnamo Desemba 16, mwaka wa 2012, mimi na ndugu watano tulikuwa tukihubiri injili wakati ghafla polisi wanne walitujia kwa gari waliloendesha kwa mwendo wa kasi na kutukamata. Walitupeleka kwenye kituo cha polisi na, baada ya kunitia pingu mikononi, mmoja wao alisema kwa sauti kubwa, “Hebu niwaeleze ninyi watu, mnaweza kwenda kuiba na kupora mali, mnaweza kuua na kuchoma kwa makusudi, mnaweza kwenda kufanya ukahaba, hatujali. Lakini kumwamini Mungu ni jambo moja ambalo hamwezi kulifanya! Kwa kumwamini Mungu, mnajiwekea uadui dhidi ya Chama cha Kikomunisti, na sharti mwadhibiwe!” Alinipiga kofi kwa nguvu na kunipiga teke kwa ukali alipokuwa akizungumza. Nilihisi kuwa singeweza kuvumilia zaidi baada ya kichapo hicho, kwa hivyo nilimwomba Mungu moyoni mwangu tena na tena: “Ee Mungu! Sijui hata kidogo polisi hawa wabaya watanitesa kwa muda gani, na nahisi kama siwezi kustahimili muda mrefu zaidi. Lakini afadhali nife kuliko nigeuke kuwa Yuda—Sitakusaliti. Tafadhali nilinde, unikinge na uniongoze.” Baada ya kuomba, niliamua kimya kimya moyoni: “Nitaendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu hadi kifo changu, nitakabiliana na Shetani hadi mwisho, na nitakuwa shahidi ili kumridhisha Mungu!” Baadaye, mmoja wa polisi alinipekua na kukuta yuani 230 nilizokuwa nazo pesa taslimu. Akitabasamu kwa uovu, alisema, “Pesa hizi ni bidhaa zilizoibiwa na zinapaswa kuchukuliwa ngawira.” Alipokuwa akizungumza aliweka pesa ndani ya mfuko wake mwenyewe na kujihifadhia. Kisha wakaanza kutuhoji. “Ninyi watu mnatoka wapi? Majina yenu ni yapi? Ni nani aliyewatuma hapa?” Baada ya kuwaambia jina langu na anwani, kwa upesi walipata maelezo ya familia yangu yote kwenye kompyuta yao. Niliwapatia tu maelezo yangu ya msingi ya kibinafsi, lakini nilikataa kujibu swali lolote kuhusu kanisa.
Kisha polisi wakatekeleza moja ya hila zao. Walipata watu zaidi ya kumi mtaani ambao hawamwamini Mungu na kuwashurutisha watoe ushahidi kwamba nilikuwa nikihubiri injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu. Kisha wakawaambia watu hao uwongo mtupu na mashtaka ya uwongo juu yangu. Watu hao wote walinidhihaki, walinikashifu na kunitukana; nilihisi nilyeonewa kabisa. Sikujua jinsi nilivyopaswa kustahimili hali hii, kwa hivyo niliendelea tu kumwomba Mungu moyoni mwangu anipe imani na nguvu. Wakati huohuo, sehemu ya wimbo wa maneno ya Mungu iliingia akilini mwangu polepole: “Hupitia kila aina ya kejeli, shutuma, hukumu, na lawama. Yeye pia hufuatwa na shetani na Anakataliwa na kupingwa na jamii za kidini. Hakuna mtu anayeweza fidia kwa ajili ya madhara haya katika moyo Wake! Haya ni mambo ya kuumiza. Yeye Huokoa binadamu mpotovu kwa njia ya uvumilivu uliokithiri; Anawapenda watu walio na moyo uliovilia. Hii ni kazi ya kuumiza zaidi. Upinzani mkali wa wanadamu, lawama na masingizio, mashtaka ya uongo, mateso na uwindaji wao na uchinjaji yanasababisha mwili wa Mungu kukumbwa na hatari kubwa katika kufanya kazi hii. Yeye huteseka na maumivu haya, bali nani anaweza kumwelewa na kumfariji?” (“Mungu Ampenda Mwanadamu na Majeraha” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Awali, nilikuwa nikielewa kinadharia tu mateso ambayo Mungu huteseka ili amwokoe mwanadamu, na wakati huo tu, nilipojikuta katika hali halisi kama hiyo, ndipo mwishowe nilianza kutambua vyema jinsi mateso ya Mungu yalivyo makubwa! Mungu, mwenye haki na mtakatifu, amekuwa mwili ili aishi pamoja nasi, watu waovu na wapotovu; Amevumilia kila aina ya dhihaka na matusi, shutuma na kashfa, mateso na kuandamwa ili kutuokoa. Hata sisi ambao tunamwamini Mungu mara nyingi hatumwelewi, na hata tunamwelewa visivyo na kumlaumu. Mapigo haya yote ni machungu sana kwa Mungu, na bado Yeye hubeba makovu Yake na kumpenda mwanadamu—tabia Yake ni adhimu sana, na ya heshima sana! Ingawa nimeyasoma haya katika Bibilia hapo zamani: “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24-25). Ni leo tu ndipo nilipoona kwamba maneno haya yalikuwa yametimia hasa! Hili lilinisikitisha sana, na nilijuta kuwa sikuwahi kuonyesha nadhari kwa mapenzi ya Mungu hapo awali…. Kabla ya kuweza kupata umakini tena, polisi walitundika ishara ya kusema “Mwanachama wa Xie Jiao” shingoni mwangu na kunipiga picha. Kisha waliniamuru nichutame na kuelekezea kidole vifaa fulani vya injili walipokuwa wakinipiga picha kadhaa. Miguu yangu iliuma sana hata sikuweza kusalia nimechutama. Wakati huo huo, simu yangu ya rununu ilianza kulia, na nikishtuka, niliwaza: “Lazima iwe ni ndugu kutoka kanisani anayepiga simu. Siwezi kabisa kumwingiza hatarini!” Kwa upesi nilikamata simu yangu ya rununu na kuiponda sakafuni kwa nguvu, na kuivunja vipande vipande. Hili liliwaghadhibisha polisi mara moja. Walionekana kushikwa na kichaa—waliinua kola yangu, kisha wakanipiga usoni kwa nguvu mara kadhaa. Uso wangu ulianza kuunguza kama moto mara moja na masikio yangu yalikuwa yakiwangwa sana kiasi kwamba singeweza kusikia chochote. Kisha wakaanza kunipiga miguu kwa nguvu zao zote, wakiwa bado hawajamaliza kuonyesha hasira zao, polisi hao waovu walinikokota hadi kwenye chumba chenye giza na kunishurutisha nisimame mgongo wangu ukiwa dhidi ya ukuta huku wakinipiga usoni. Kisha walinipa kichapo kingine kibaya. Niliweza kuzuia machozi wakati haya yalikuwa yakitendeka, na nilimwomba Mungu kimya kimya: “Ee Mwenyezi Mungu, naamini kuwa mapenzi Yako mema ndiyo kiini cha kila kitu kinachonipata sasa. Bila kujali jinsi polisi hawa waovu watakavyonitesa, nitakuwa shahidi Kwako na sitajisalimisha kwa Shetani!” Nilishangaa, niliposema sala hii, ghafla nilipata tena kusikia masikioni mwangu, na yote niliyoweza kusikia ni mmoja wa polisi waovu akisema, “Huyu mwanamke ni mkaidi sana. Hajadondokwa na machozi hata kidogo wala hajalia. Labda hatujampiga kiasi cha kutosha. Kilete kidude cha umeme kisha tutaona iwapo atalia!” Polisi mwingine alichukua kirungu cha umeme na kukifinya kwa nguvu kwenye paja langu. Maumivu makali yaliniingia mara moja, yakiuma sana hivi kwamba nilianguka sakafuni mara moja. Kichwa changu kiligonga ukuta na damu ilianza kuchirizika. Polisi walinielekezea vidole na kusema kwa sauti kubwa, “Acha kujifanya. Simama! Tutakupa muda wa dakika tatu. Ikiwa hutasimama, tutakupiga tena. Hata usifikirie kujifanya umekufa!” Lakini bila kujali waliongea kwa sauti kubwa kiasi gani, kwa kweli sikuweza kusonga, na kwa hivyo mwishowe walinipiga mateke mengine makali kabla ya kukoma.
Kwa kweli sikuweza kuvumilia kwa muda mrefu zaidi dhidi ya mateso ya kikatili na ya kinyama yaliyotolewa na polisi hao. Nilimwomba Mungu kwa dhati: “Ee Mwenyezi Mungu! Siwezi kuendelea kwa muda mrefu zaidi. Tafadhali nipe imani na nguvu!” Katikati ya mateso yangu makali sana, nilikumbuka wimbo wa maneno ya Mungu: “Kwa kuwa unamwamini Mungu, ni lazima uukabidhi moyo wako mbele ya Mungu. Ukiutoa moyo wako na kuuweka mbele ya Mungu, basi wakati wa usafishaji, haitawezekana wewe kumkana Mungu, au kumwacha Mungu. … Siku itakapokuja na majaribu ya Mungu yakufike kwa ghafla, hutaweza tu kusimama kando ya Mungu, bali pia utaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu. Wakati huo, utakuwa kama Ayubu, na Petro. Baada ya kuwa na ushuhuda kwa Mungu, utampenda kwa kweli, na utamtolea maisha yako kwa furaha; utakuwa shahidi wa Mungu, na yule ambaye ni mpendwa wa Mungu. Upendo ambao umepitia usafishaji ni wa nguvu, na sio dhaifu. Haijalishi ni lini au vipi Mungu anakufanya upatwe na majaribu Yake, unaweza kutojali ikiwa unaishi au unaangamia, kuachana na kila kitu kwa furaha kwa ajili ya Mungu, na kuvumilia chochote kwa furaha kwa ajili ya Mungu—na hivyo upendo wako utakuwa safi, na imani yako halisi. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu anayependwa na Mungu kwa kweli, na ambaye amefanywa kamili na Mungu kwa kweli” (“Toa Moyo Wako Mbele za Mungu Ikiwa Wamwamini” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nuru ya Mungu iliniwezesha kufahamu mapenzi Yake, na pia ilinipa imani na nguvu isiyokwisha. Nilimwomba Mungu tena: “Ee Mungu! Naamini kwamba kila kitu kinachonitokea leo kinatendeka kwa idhini Yako, na mapenzi Yako mema ndiyo chanzo cha yote. Kupitia kwa utendaji unaofanywa na pepo hawa, mwishowe naona kuwa mashirika ya kutekeleza sheria yanayofanya kazi chini ya CCP ni mashirika katili na siwezi kujisalimisha kwao. Natamani tu kukupa moyo wangu na kusimama upande Wako. Ee Mungu! Najua kuwa ni kupitia tu kwa majaribu na utakaso kama huu ndiyo upendo wangu Kwako unaweza kuimarika. Ikiwa Shetani atachukua maisha yangu leo, bado sitasema neno hata moja la malalamiko. Kuweza kuwa na ushuhuda kwa ajili Yako ni heshima yangu kama kiumbe aliyeumbwa. Wakati uliopita sikutimiza wajibu wangu vizuri na nina deni Lako kubwa sana. Kuwa na nafasi ya kufa leo ndilo jambo lenye maana zaidi. Ningependa Kukutii.” Nilihisi kuguswa sana baada ya ombi hili, na nilihisi kwamba kupitia mateso haya kwa sababu ya kumfuata Mungu lilikuwa jambo lenye maana sana, na kwamba lilikuwa linastahili hata ikiwa ningekufa!
Ilikuwa labda baada ya zaidi ya dakika 10 ndipo afisa wa kike alikuja na kunisaidia kusimama na, akisingizia wema, alisema, “Jitazame katika umri wako, ukiwa na watoto wako wawili chuoni. Je, ni jambo linalostahili kwako kupitia haya yote? Tuambie tu kile tunachotaka kukijua na kisha utaweza kuondoka mara moja.” Aliona kwamba sikujibu, na kwa hivyo aliendelea, “Wewe ni mama, kwa hivyo unapaswa kuwafikiria wana wako. Tunaishi sasa katika miliki ya Chama cha Kikomunisti, na serikali ya CCP inapinga na kukomesha imani zote za kidini. Inawadharau hasa ninyi ambao mnamwamini Mwenyezi Mungu. Ikiwa utasisitiza kuendelea kupingana na serikali, je, huna wasiwasi kuhusu kuingiza familia yako yote hatarini? Kufikia wakati fulani, wazazi wako na mumeo watahusishwa, na wana wako pamoja na wajukuu wanapaswa kusahau kuhusu kujiunga na jeshi, kuwa maofisa wa jeshi au kuwa watumishi wa serikali. Hakuna mtu anayeweza hata kuwaajiri kuwa walinzi. Je, unataka watoto wako wawe wafanyakazi wakiwa watu wazima, na wafanye kazi za pembeni kama wewe na kuwa masikini maisha yao yote?” Wakati ambapo Shetani alikuwa akitekeleza njama zake za hila dhidi yangu, maneno ya Mungu ghafla yakanijia akilini mwangu: “Kwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni, hakuna kitu Nisichokuwa na usemi wa mwisho kukihusu. Ni kitu gani kilichopo ambacho hakiko mikononi Mwangu? Chochote Nisemacho hufanyika, na miongoni mwa wanadamu, ni nani aliyepo anayeweza kuyabadilisha mawazo Yangu?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 1). Maneno ya Mungu yaliniwezesha kufahamu njama za Shetani za hila, na niligundua kwamba walikuwa wakijaribu kunishurutisha nizungumze kwa kutumia mustakabali wa watoto wangu kama nguvu. Nilijua, hata hivyo, kuwa majaliwa yetu kama wanadamu hayapo mikononi mwetu, wala katika mikono ya polisi, lakini yapo mikononi mwa Mungu. Kazi yoyote ambayo watoto wangu wangekuwa nayo katika siku za usoni na iwapo wangekuwa matajiri au masikini yote yalikuwa ya kuamuliwa na Mungu. Kwa kuwaza haya kwa makini, sikuhisi kubanwa na polisi hata kidogo. Uongozi wa maneno ya Mungu uliniwezesha kufambua kwa kweli kuwa Mungu alikuwa pamoja nami, akinilinda, na nilianza kumtumainia Mungu kwa uthabiti zaidi. Na hivyo, niligeuza kichwa changu upande mmoja na kukaa kimya. Afisa alinipa ukaripiaji mkali na kisha akaondoka akiwa na huzuni.
Jioni ilikuwa inakaribia. Walipoona kwamba hawangepata habari yoyote kutoka kwangu au kwa dada zangu wa kanisa, walichoweza kufanya tu ni kutupeleka kwenye Kituo cha Kizuizi cha Kaunti. Lakini polisi huko walisema kwamba kesi yetu ilikuwa nzito sana, na kwamba ilitubidi kwenda kwenye Nyumba ya Kizuizi cha Manispaa. Kufikia wakati tulipofika hapo, tayari ilikuwa imepita saa saba usiku na kile ambacho niliweza kuona ni safu baada ya safu ya malango makubwa yaliyotengenezwa kwa mihimili ya chuma—yote yalionekana yenye kuhuzunisha na ya kutisha. Kwenye lango la kwanza, tulilazimika kuondoa mavazi yote na kujisalimisha kwa upekuzi wa miili yetu. Kisha walikata vifungo vyangu na zipu zote na ilinibidi nivalie nguo zilizochana; nilihisi kama ombaomba. Katika lango la pili, tulilazimika kupitia uchunguzi wa mwili. Waliona vilio vya damu kwenye miguu yangu vilivyotokana na kupigwa na polisi na kwamba nilikuwa nikiona vigumu kutembea, lakini walinikodolea macho tu na kusema uwongo, wakisema, “Hii ni kawaida kabisa. Hakuna jambo la kutia wasiwasi.” Imeelezwa waziwazi katika kanuni za gereza kwamba matibabu yanapaswa kuagizwa ikiwa ugonjwa wowote au jeraha litapatikana wakati wa uchunguzi wa mwili, lakini katika hali halisi, hawajali ikiwa wafungwa wataishi au kufa. Waliniambia kwa kejeli, “Ninyi waumini katika Mwenyezi Mungu mna Mungu wa kuwalinda. Unaweza kukabiliana na hali ilivyo.” Nilipelekwa kwenye seli, na mfungwa alichomoza kichwa chake chini ya shuka yake na kusema kwa sauti kubwa, “Vua nguo zako zote!” Nilimsihi asinishurutishe nivue chupi langu, lakini alinitabasamia tu kwa nia mbaya na kusema, “Ukija mahali hapa lazima ufuate sheria.” Wafungwa wengine wote kisha walichomoza vichwa vyao kutoka ndani ya shuka zao na kuanza kupiga kelele za kuogofya za kila aina. Kulikuwa na wafungwa 18 waliozuiliwa katika seli hiyo yenye kipimo cha zaidi tu ya mita 20 mraba: Walikuwa walanguzi wa dawa za kulevya, wauaji, wabadhirifu na wezi. Kazi ya “bosi” wa mahali hapo, mwenye kutawala, ilikuwa kuwaadhibu watu kwa njia zote kila siku—yeye aliwatesa watu ili kujifurahisha tu. Asubuhi, mdogo wake kwa cheo alinifundisha sheria na kuniambia kwamba nilipaswa kupiga deki mara mbili kila siku. Daima alikuwa akipata shughli za kunipa, na aliniambia kwamba wakati wote nilipaswa kukamilisha sehemu yangu za uzalishaji, na kwamba nilipaswa kuharakisha, vinginevyo ningeadhibiwa. Walinzi wa gereza walitenda kama wanyama wa porini na mara nyingi waliwaadhibu wafungwa bila sababu pia. Mmoja wao alinitishia, akisema, “Ninachokisema lazima kitatiiwa. Sijali ikiwa utanishtaki. Nenda ukapige ripoti ikiwa unataka, na nitakupa mateso zaidi ya uliyoyatarajia! …” Maafisa hao waovu wa gereza walikuwa hawana kizuizi kabisa na hawakujizuia hata kidogo. Humo ndani, pesa ilikuwa muhimu sana, na ilimradi mtu alimkabidhi afisa wa gereza pesa, hakuwa chini ya “sheria.” Mfungwa mmoja alikuwa mke wa mtu mwenye madaraka ambaye alibadhiri kiasi kikubwa cha pesa. Mara nyingi aliwapa walinzi wa gereza pesa, na kila siku alikuwa akimnunulia “bosi” kumbwe ndogo za kukaanga. Kwa kufanya hivyo, hakuhitajika kufanya kazi yoyote siku nzima, na angeweza kuwashinikiza wengine kuosha vyombo vyake na kukunja shuka yake. Ingawa nilikuwa nikiishi kwenye seli hii mbaya mno, pasi na pesa na haki, na ilibidi nivumilie kila aina ya uyanyasaji na mateso kila siku, jambo pekee ambalo lilinifariji ni kwamba dada wawili wa kanisa walikuwa pamoja nami humo ndani. Tulikuwa kama familia. Kupitia wakati huu mgumu tungeshirikiana kila wakati tulipopata nafasi; tulihimiliana na kusaidiana. Tulimtegemea Mungu wakati wote, tukimwomba atupe imani na nguvu. Sisi sote tuliwasaidia na kuwahimili wengine, na kwa pamoja tulistahimili wakati huu mbaya.
Nilihojiwa na polisi mara nne zaidi nilipokuwa kwenye nyumba ya kizuizini. Moja ya nyakati hizo, wanaume waliokuja kunihoji walijitambulisha kuwa ni wa kutoka kwenye Ofisi ya Usalama wa Umma ya Manispaa na kutoka kwenye Shirika la Usalama ya Kitaifa. Nilijiuliza: “Mtu kutoka kwenye Ofisi ya Usalama wa Umma ya Manispaa kwa hakika laziwa awe na ubora wa juu zaidi na mwenye elimu zaidi kuliko polisi katika kituo cha polisi cha eneo langu. Lazima atekeleze sheria kwa njia ya haki.” Lakini hali halisi haikuwa kama nilivyofikiria. Pindi tu mtu huyo kutoka kwenye Ofisi ya Usalama wa Umma wa Manispaa alipoingia ndani ya chumba hicho ndipo tu alijipolaza chali kwenye kiti akiwa na miguu yake mezani. Mwili wake wote ulionyesha majivuno, na aliangaza macho yake kwangu akiwa na sura ya dharau. Kisha akasimama na kuelekea kwangu. Alivuta mkupuo mzito wa sigara yake kisha akafuka moshi usoni mwangu. Nilipoona haya, hatimaye niligundua kuwa polisi wote wa CCP walikuwa sawa, na singejizuia kujichekelea kwa kufikiria kuwa mtu huyu angekuwa tofauti. Sikujua ni hila gani wangejaribu kwangu baadaye, kwa hivyo nilimwomba Mungu kimya kimya: “Ee Mwenyezi Mungu. Tafadhali unipe hekima ya kumshinda Shetani na uniwezeshe Nikutukuze na kuwa na ushahidi kwako!” Wakati huo, polisi kutoka kwenye Shirika la Usalama ya Kitaifa alisema, “Tayari tunajua yote kukuhusu. Shirikiana nasi na tutakuruhusu uondoke.” Nilimtupia jicho na nikacheka kicheko kisichokuwa na furaha. Wakidhani nilikuwa tayari kulegeza msimamo, walisema, “Uko tayari kushirikiana sasa?” Nilimjibu, “Nilisema kila kitu nilichohitaji kusema muda mrefu uliopita.” Hili mara moja liliwafanya polisi waovu wagadhibike sana, na wakaanza kunitupia maneno machafu kwa sauti kubwa “Tunajaribu kukupa suluhisho la heshima, na unakataa! Ikiwa hutazungumza leo, nina wakati mwingi sana wa kushinda nawe. Nitawaondoa watoto wako shuleni na kuhakikisha kwamba hataweza kumaliza masomo yao.” Kisha wakatoa simu yangu ya rununu na kunitishia, wakisema, “Nambari kwenye kadiwia yako ni za nani? Ikiwa hutatuambia leo utapata kifungo cha miaka saba au nane. Tutawafanya wafungwa wengine wakutese kila wakati, na utatamani kufa!” Bila kujali alinishinikiza kiasi gani, sikujibu. Sikuogopa hata, kwa maana maneno ya Mungu yalinipa nuru moyoni: “Kwa sababu lazima ustahimili mateso kama haya ili kuokolewa na kunusurika, na yote haya yamepangiliwa awali. Hivyo kwa mateso haya kukukumba wewe ni baraka kwako. … Maana yake fiche ni ya kina sana, muhimu sana” (“Wale Waliopoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Raundi hiyo ya mahojiano iliendelea kwa muda wa saa mbili na nusu. Walipoona kuwa hawakuwa wamepata habari yoyote kutoka kwangu, walinielekezea vitisho vingine zaidi kisha wakaondoka wakionekana wenye huzuni.
Mnamo Januari 6, mwaka wa 2013, polisi walitumia mbinu tofauti na walisema kwamba watanipeleka nyumbani. Walinifanya nivalie sare na pingu za mfungwa, na nilirudishwa kwenye kituo cha polisi cha eneo langu katika gari la gereza. Nilipofika huko, niliambiwa kwamba polisi hao waovu walikuwa wamewapata wanangu na wakwe zangu, wamepekua nyumba yetu, na walikuwa wamewauliza watu kadhaa na kupata uelewa mzuri wa kile ambacho nilikuwa nikifanya katika miaka michache iliyopita. Mmoja wa polisi hapo alisema, “Tumekuwa tukimtafuta huyu mama kwa miaka na hatukuwahi kumkamata. Mumewe alipokufa, alikaa tu usiku mmoja nyumbani. Tulipoteza siku nyingi nyumbani kwake tukimsubiri. Mwanawe alipofanyiwa upasuaji wa moyo, tulikwenda hospitalini kumkamata, lakini hakujitokeza. Anamwamini Mungu sana mpaka ametelekeza familia yake yote. Sasa kwa kuwa tumemkamata, inatubidi tumshughulikie kwa mara ya mwisho!” Nilipomsikia akiyasema haya, moyo wangu ulianza kulalamika: “Je, ni wakati gani ambapo sikutaka kamwe kwenda nyumbani? Kifo cha mume wangu kilikuwa cha kuumiza sana, na nilikuwa na wasiwasi mkubwa sana wakati mwanangu alifanyiwa upasuaji wa moyo. Nilitaka sana kuwa karibu na mwanangu. Si kwamba nilikuwa nimewatekeleza, ilikuwa kwamba serikali ya CCP ilikuwa ikinitesa bila huruma na kunitafuta, ikifanya isiwezekane kwangu kurudi nyumbani!” Gari liliekea nyumbani kwangu kwa muda wa kasi, na nililia kimya kimya moyoni mwangu. Nilimwomba Mungu bila kukoma: “Ee Mungu! Nimekuwa mbali na makao yangu kwa miaka kwa sababu ya mateso ya CCP. Hivi karibuni nitaiona familia yangu, na naogopa kuwa nitadhoofika nitakapowaona na kwamba nitashindwa na njama za Shetani zenye hila. Tafadhali nisaidie na uniwezeshe kuishi na hadhi na ujasiri wa mmoja wa waumini wa Mungu hata mbele za Shetani. Usiruhusu nidanganywe nao. Naomba tu kuwa shahidi Kwako ili nikuridhishe!” Maombi yangu yalipomalizika, nilihisi kutulia zaidi na nikahisi hisia za kuwa huru. Nilijua kuwa huyu ni Mungu aliyekuwa akiandamana nami na akinipa nguvu. Tulipokaribia nyumba yangu, polisi waliegesha gari kando ya barabara kuu. Nikivalia sare zangu na pingu za mfungwa, nililazimishwa niwaongoze kwa miguu kuelekea nyumbani kwangu. Majirani zangu wote walisimama kwa mbali wakinitazama na kuashiria kwenye mwelekeo wangu; niliweza kuwasikia wakinitusi na kunidhihaki kisirisiri. Tulipoingia kwenye lango ambalo lilielekea kwenye ua, moja kwa moja nilimwona mwanangu akizifua nguo. Alinisikia nikiingia lakini hakuinua kichwa chake, na nilijua wakati huo kuwa alinichukia. Nywele za wakwe zangu zilikuwa zimejaa mvi, na mama mkwe wangu akatoka na kuwasalimia maafisa hao waovu, lakini baadaye alikaa kimya. Polisi mwovu aliuliza, “Je, mwanamke huyu ni binti mkwe wako?” Alikubali kidogo kwa kichwa. Kisha akaanza kuwatishia wakwe zangu, akisema, “Asiposhirikiana nasi, tutalazimika kupiga simu shuleni na hivi karibuni wana wake watafukuzwa. Hata tutafuta malipo yenu ya uzeeni pamoja na kila ruzuku mnayopokea.” Nyuso za wakwe zangu wakongwe zilikwajuka alipokuwa akiwatishia, na sauti zao zilitetemeka walipokuwa wakizungumza. Walikiri kwa haraka sana kwamba nilikuwa nimeondoka kwa muda wa miaka sita au saba na kwamba nilikuwa nikitenda kwa mujibu wa imani yangu mahali pengine. Polisi kisha waliwafokea, “Chama pamoja na watu wamewatunza vizuri sana katika miaka hii yote. Tuambie, je, Chama cha Kikomunisti ni kizuri?” Mama mkwe wangu aliogopa sana, akajibu papo hapo, “Ndio, ni kizuri.” Kisha polisi akauliza, “Je, sera zake za sasa ni nzuri?” Akajibu, “Ndiyo, ni nzuri.” “Na janga zote ambazo zimetokea katika familia yako,” polisi aliendelea, “na kifo cha mwanao, si yote yalisababishwa na binti mkwe wako? Je, si yeye ndiye mwenye kuleta bahati mbaya kwa familia yako?” Mama mkwe aliinamisha kichwa chake na akatoa ishara ya kichwa kwa kukubali shingo upande. Walipoona kwamba njama yao imefaulu, polisi walinivuta hadi ndani na kunilazimisha nitazame tuzo zote ambazo mtoto wangu ameshinda ambazo zilikuwa zimebadikwa kwenye ukuta. Mmoja wao kisha alijigamba na kunielekezea kidole, akinikemea na kuniambia, “Sijawahi katika maisha yangu kukutana na mtu yeyote anayekosa ubinadamu kama wewe. Mwana mzuri kama huyo na unamtelekeza tu na kukimbia kwenda kumwamini Mungu! Unafaidi nini kwa kufanya hivyo?” Nikitazama tuzo zote ambazo mwanangu alishinda zilizofunika ukuta, nilifikiria kuhusu jinsi imani yangu ilivyoathiri masomo yake, kuhusu jinsi wakwe zangu walikuwa wakiogopeshwa na kutishiwa—familia yangu ilikuwa imetenganishwa! Lakini ni nani aliyesababisha yote? Je, ni kwa sababu tu ya imani yangu? Imani yangu katika Mungu ni kufuatilia ukweli na kutembea katika njia sahihi maishani. Kuna nini kibaya kuhusu hilo? Kama CCP haingenitafuta na kunitesa, je, ningelazimika kukaa mbali na makao yangu na kwenda mafichoni kwa miaka hiyo yote? Na bado walikuwa wakinishutumu kwa uwongo kwamba siijali familia yangu na siishi maisha yangu. Kwa kufanya hivyo, je, hawakuwa wakipotosha ukweli waziwazi na kugeuza ukweli? Wakati huo huo, chuki ambayo nilihisi ndani kwa ajili ya pepo hawa wa Shetani iliibuka na ikakaribia kububujika kutoka kwangu kama kufoka kwa volkano—nilitaka kulalamika: “Pepo wa Shetani! Nawachukia! Nawachukia kabisa! Je, si mateso ya serikali ya CCP ambayo yamenizuia kuwa nyumbani kwangu miaka hii yote? Sikutaka kuwa karibu na mwanangu kumpa upendo na utunzaji wa mama? Je, sikutaka kuishi na familia yangu kwa amani na furaha? Na bado ninyi pepo wa Shetani sasa mmebadilika ghafla na kujifanya kuwa watu wazuri, mkipingana nasi na kutia lawama kwa kila jambo baya ambalo limetokea kwa familia yetu mlangoni mwa Mungu, na kusukuma jukumu la yote hayo mabegani mwangu. Mnawasilisha ukweli visivyo na kunena upuuzi mtupu! Ninyi roho wabaya ni wapotovu sana, na mnajisingizia kuwa wasio na hatia ilhali ninyi ni wahalifu waovu zaidi ya wote. Ninyi ndinyi hirizi inayosababisha bahati mbaya, kisirani halisi, wenye kuleta bahati mbaya! Serikali ya CCP ndiyo tatizo kuu iliyosababisha kuvunjika kwa familia yangu! Je, kuna furaha gani kuzungumzia kuhusu watu wanaoishi katika nchi hii?” Mara tu walipomaliza udanganyifu wao, waliniambia kwa sauti kubwa “Songa!”, na kuniamuru niondoke nyumbani. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kuniwezesha kufahamu njama za Shetani za hila, kuweza kuona uovu wa kupinga maendeleo wa CCP, na kusimama kidete katika ushuhuda wangu!
Mnamo Januari 12, polisi walinihoji kwa mara ya mwisho. Polisi wawili kwa mara nyingine walijaribu kunilazimisha niwasaliti ndugu zangu, lakini bila kujali jinsi walivyonitishia na kunishurutisha, nilisema tu sijui. Waliponisikia nikisema kuwa sijui chochote, walikasirika mara moja na wakaanza kunipiga kofi usoni kwa nguvu, na walizivuta nywele zangu kana kwamba walikuwa wameshikwa na kichaa. Walisimama pande zangu zote mbili, wakinisukuma hapa na pale na kupiga miguu yangu kwa nguvu walivyoweza. Kisha wakanigonga kichwani na bomba la shaba, wakisema kwa sauti kubwa, “Je, unafikiri kwamba siwezi kukupiga? Utafanya nini kulihusu kwa hata hivyo? Hebu tuone jinsi ulivyo thabiti!” Mshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda. Ingawa walinipitisha kwenye mateso kama haya, yote niliyoweza kuhisi ni mwili wangu kufa ganzi; Nilihisi maumivu madogo sana. Wale polisi wawili waovu walinitesa kwa muda wa saa nane hadi walipokuwa wachovu kabisa na kutokwa na jasho jingi sana, na ndipo tu walipokoma. Waliketi kwenye kochi, wakihema na kusema, “Sawasawa, subiri tu hadi utakapotumikia kifungo cha maisha gerezani. Halafu hutawahi kuwa huru tena, hata ukifa!” Sikuhisi chochote wakati niliposikia wakisema haya, kwa sababu tayari nilikuwa nimeacha kujali na kuapa kwamba sitajisalimisha kwa pepo hawa hata kwa gharama ya maisha yangu mwenyewe. Nilimwomba Mungu kimya: “Ee Mungu, ningependa kujisalimisha Kwako. Hata kama polisi waovu watanifunga maisha yangu yote, bado Nitakufuata mpaka mwisho. Nitakusifu hata ikiwa nitawekwa kuzimu!” Niliporudi kwenye seli yangu, nilitarajia kabisa kupelekwa gerezani kufungwa maisha yangu yote, kwa hivyo nilishangaa wakati Mungu alinifungulia njia. Alasiri ya Januari 16, bila kutarajia polisi waliniruhusu niondoke bila mashtaka yoyote.
Tukio hili la kuhuzunisha sana lilikuwa kama ndoto baya ambalo siwezi kuvumilia kulikumbuka. Kamwe sikudhani kabisa kuwa mwanamke wa kawaida kama mimi atakuwa “mlengwa wa kuvutia” kwa polisi kwa ajili ya kumwamini Mungu tu, au kwamba ningechukuliwa kama adui na serikali ya CCP na kufunuliwa kwa hatari ya kusababisha mauti namna hiyo. Wakati mmoja, wakati wa mahojiano, niliwauliza, “Nimefanya nini kibaya? Nimevunja sheria gani? Ni mambo gani nimesema dhidi ya Chama au dhidi ya watu? Kwa nini nimekamatwa?” Polisi hawakuweza kujibu maswali yangu, na kwa hivyo walinifokea kwa sauti kubwa, “mnaweza kwenda kuiba na kupora mali, mnaweza kuua na kuchoma kwa makusudi, mnaweza kwenda kufanya ukahaba, hatujali. Lakini kumwamini Mungu ni jambo moja ambalo hamwezi kulifanya! Kwa kumwamini Mungu, mnaeka mnajiwekea uadui dhidi ya Chama cha Kikomunisti, na sharti mwadhibiwe!” Maneno kama hayo ya kuamrisha, ya kidikteta, ya kupotosha ukweli yalitoka moja kwa moja kinywani mwa ibilisi! Kumwamini Mungu na kumwabudu Mungu ni kanuni isiyobadilika; inaambatana na mapenzi ya mbinguni na inalingana na mioyo ya watu. Serikali ya CCP inampinga Mungu na inawakataza watu kufuata njia sahihi. Badala yake, inaweka lawama kwa waathiriwa wake na kudai bila aibu kwamba sisi ni maadui wake, na hivyo kufichua kabisa asili yake ya shetani! Serikali ya CCP haipingi tu hasira kazi ya Mungu na kuwakamata waumini kwa hasira, bali pia inabuni uvumi wa kuwadanganya watu ili kila mtu aamini uwongo wake na amkane Mungu, ampinge Mungu; pia huharibu nafasi za watu za kupata wokovu wa kweli. Vitu vibaya ambavyo CCP imefanya kweli ni vingi mno kuorodhesha, na imechochea gadhabu ya wanadamu na ya Mungu! Baada ya kupitia mateso yaliyosababishwa na pepo hao, nilikuja kuona waziwazi asili ya CPP inayompinga Mungu, inayopinga maendeleo, inayopinga mapenzi ya Mbingu, na kwa kweli nikakuja kufahamu upendo na utunzaji wa Mungu. Niliona kuwa asili ya Mungu ni uzuri na wema; kila wakati nilipokuwa na maumivu makali sana au kuona mateso yangu kuwa magumu sana kuvumilia, maneno ya Mungu yalikuwa ndani yangu, yakiniongoza na kunipa nuru, yakinipa nguvu na kunipa imani, na yaliniwezesha kufahamu njama za Shetani za hila na kuchukua msimamo thabiti. Nilihisi kweli uwepo na mwongozo wa Mungu, na wakati huo ndipo tu niliweza kushinda kila changamoto na kusimama kidete katika ushuhuda wangu—upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Kuanzia leo hii, nitajitolea kwa dhati kulipa upendo wa Mungu, na nitatafuta kupata ukweli na kuishi maisha yenye maana.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?