Siku Baada Ya Nyingine Katika Jela Ya Chama Cha Kikomunisti

10/03/2018

Na Yang Yi, China

Mimi ni Mkristo wa Kanisa la Mwenyezi Mungu. na nimekuwa mfuasi wa Mwenyezi Mungu kwa zaidi ya miaka kumi. Katika wakati huu, kitu kimoja ambacho sitawahi kusahau ni taabu mbaya sana nilipokamatwa na polisi wa CCP muongo mmoja uliopita. Wakati huo, licha ya mimi kuteswa na kukandamizwa na ibilisi waovu, na kuwa ukingoni mwa kifo mara kadhaa, Mwenyezi Mungu alitumia mkono Wake wa nguvu kuniongoza na kunilinda, kunirudisha kwa uhai, na kunirudisha kwa usalama…. Kupitia hili, kwa kweli nilipitia uvukaji mipaka na ukuu wa Mungu, na kupata utajiri wa thamani wa maisha niliyotunikiwa na Mungu.

Ilikuwa Januari 23, 2004 (siku ya pili ya Mwaka Mpya wa Kichina). Nilihitaji kuenda kumtembelea dada fulani kutoka kwa kanisa; alikuwa katika shida na alihitaji msaada kwa dharura. Kwa kuwa aliishi mbali sana, ilinibidi nirauke mapema ili kupata teksi ili niweze kurudi siku hiyo hiyo. Niliondoka nyumbani wakati tu mwanga ulichomoka. Kulikuwa na watu wachache sana barabarani, wafanyikazi wa kusafisha taka pekee. Kwa wasiwasi nilitafuta teksi, lakini hakukuwa na yoyote hapo. Nilienda kwa stesheni ya teksi kusubiri, na nikasongea kwa barabara kusimamisha moja nilipoiona ikija—lakini ikatokea kuwa ni gari la Shirika la Kulinda Mazingira. Waliniuliza mbona niliwasimamisha. “Naomba radhi, ilikuwa makosa, nilidhani mlikuwa teksi,” nilisema. “Tunafikiri ulikuwa ukitundika mabango yasiyo halali,” walijibu. “Je, mliniona? Yako wapi mabango niliyokuwa nikitundika?” nilisema. Bila kunipa fursa ya kujitetea, wao watatu walikimbia mbele na kwa nguvu walichunguza mfuko wangu. Walipekua kila kitu katika mfuko wangu—nakala ya mahubiri, kitabu cha kuandikia, pochi, simu ya rununu na bipa yenye sikuwa natumia na kadhalika. Kisha walichunguza kwa makini nakala hiyo ya mahubiri na kitabu cha kuandikia. Kwa kuona kwamba hakukuwa na mabango ndani ya mfuko wangu, waliinua nakala hiyo ya mahubiri na kusema: “Yaweza kuwa hukuwa ukitundika mabango yasiyo halali, lakini unamwamini Mwenyezi Mungu.” Kisha, walipigia simu Divisheni ya Dini ya Kikosi cha Usalama wa Taifa. Punde baadaye, watu wanne kutoka kwa Kikosi cha Usalama wa Taifa waliwasili. Walijua kwamba nilikuwa muumini wa Mwenyezi Mungu punde walipoona vitu ndani ya mfuko wangu. Bila kuniruhusu kusema lolote, walinitupa ovyo katika gari lao, kisha walifunga mlango kwa ufunguo ili kunikomesha kuhepa.

Tulipowasili katika Shirika la Usalama wa Umma, polisi waliniongoza kuingia katika chumba. Mmoja wao alichezacheza na bipa na simu yangu ya rununu, akitafuta dokezo. Aliwasha simu lakini ikaonyesha kwamba ilikuwa na betri ya chini, kisha betri ilikuwa imeisha chanji kabisa. Ingawa alijaribu sana, hangeweza kuiwasha. Akishika simu, alionekana kuwa na wasiwasi. Nilikanganywa pia—nilikuwa nimechaji simu hiyo asubuhi hiyo. Inawezekanaje iwe haina chaji? Ghafla nilitambua kwamba Mungu alikuwa amepanga hili kwa miujiza ili kuzuia polisi kupata taarifa yoyote kuhusu ndugu wengine. Pia nilielewa maneno yaliyonenwa na Mungu: “Vitu vyote, viwe hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu huongoza vitu vyote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu). Kweli, vitu vyote na matukio yote yako mikononi mwa Mungu. Viwe hai ama vilivyokufa, vitu vyote hupitia mabadiliko kulingana na fikira za Mungu. Wakati huu, nilipata ufahamu wa kweli wa jinsi Mungu anavyoshikilia enzi kuu na kupanga vitu vyote Zaidi ya hayo, nilipata ujasiri kukabili mahojiano yaliyokuwa njiani. Akiashiria vitu ndani ya mfuko wangu, afisa wa polisi aliuliza kwa shutuma: “Haya yanaonyesha kwamba kwa kweli wewe si mshirika wa kawaida wa kanisa. Lazima uwe mmoja wa kiongozi mkubwa, mtu ambaye ni muhimu, kwa maana viongozi wadogo hawana bipa ama simu za rununu. Niko sahihi?” “Sielewi unachosema,” nilijibu. “Unajifanya huelewi!” alisema kwa sauti kubwa, kisha akaniamuru kuchuchumaa na kuongea. Walipoona kwamba singeshirikiana, walinizingira na kuanza kunipiga ngumu na kunipiga teke—kiasi kana kwamba walitaka kuniua. Uso wangu ukiwa umejaa damu na kuvimba, mwili wangu mzima ukiuma kiasi cha kutovumilika, nilianguka sakafuni. Nilikasirishwa. Nilitaka kuzungumza maana kwao, kutoa sababu ya kuthibitisha hali yangu: Nimekosea wapi? Mbona mlinichapa hivyo? Lakini sikuwa na njia ya kuongea maana nao, kwa sababu serikali ya CCP haiongei maana. Nilichanganyikiwa, lakini sikutaka kukubali vipigo vyao. Nilipokuwa tu sijui la kufanya, ghafla nilifikiri jinsi, kwa kuwa hawa maofisa waovu wa serikali ya CCP walikuwa wapuuzi sana, kwa kuwa hawakuwa wakiniruhusu kuzungumza maneno yoyote ya maana, sikuhitaji kuwaambia chochote. Ilikuwa ni heri nibaki kimya—kwa njia hiyo singekuwa na manufaa yoyote kwao. Nilipofikiri hili, niliacha kutia maanani walichokuwa wakisema. Huku wakiona kuwa mtazamo huu haukuwa na athari yoyote kwangu, polisi hao waovu walikasirika sana na wakawa katili hata zaidi: Waligeukia mateso ili kutoa ili kunifanya nikiri. Walinitia pingu kwa kiti cha chuma kilichokazwa kwa skrubu sakafuni kwa njia ambayo singechuchumaa wala kusimama. Mmoja wao aliweka mkono wangu ambao hukuwa umetiwa pingu kwa kiti na kuupiga kwa kiatu, akikoma tu wakati upande wa nyuma wa mkono wangu ulikuwa umegeuka rangi kuwa mweusi na samawati: mwingine aliponda vidole vyangu vya miguu chini ya kiatu chake kuzungusha viatu vyake kuzunguka kwenye vidole vyangu ili kuviponda, ambayo ndio wakati nilipata maumivu ya ajabu, ambayo yalikwenda moja kwa moja moyoni mwangu. Baada ya hapo, polisi wasita ama saba walichukua zamu kwangu. Mmoja wao alilenga viungo vyangu, na kuvichuna kwa nguvu sana kiasi kwamba mwezi mmoja baadaye bado singeweza kuupinda mkono wangu. Mwingine alinyakua nywele zangu na kutingisha kichwa changu upande mmoja kuelekea upande mwingine, kisha akakivuta kwa ghafla nyuma ili nilikuwa nikiangalia juu. “Tazama anga na kuona iwapo kuna Mungu!” alisema kwa ukali. Waliendelea hadi usiku. Wakiona kwamba hawangepata chochote kutoka kwangu, na kwa sababu ilikuwa Mwaka Mpya wa Kichina, walinituma moja kwa moja hadi katika kizuizini.

Nilipowasili kizuizini mlinzi alimwamuru mfungwa wa kike kunivua nguo zote na kuzirusha katika pipa la takataka. Kisha walinifanya nivae sare chafu ya gereza, iliyokuwa ikinuka vibaya. Walinzi waliniweka katika seli na kisha wakawadanganya wafungwa wengine, wakisema: “Yeye alijitahidi kuvunja familia za watu wengine. Familia nyingi zimeharibiwa na yeye. Yeye ni mwongo, huwadanganya watu waaminifu, na kuvuruga utulivu wa umma….” Hivyo wakiwa wamedanganywa na walinzi hao, wafungwa wengine wote walisema nilikuwa nikisamehewa kwa urahisi sana, na kwamba kitu kizuri pekee kwa mtu ambaye ni mbaya kama mimi kilikuwa kikosi cha wauaji! Kusikia hili kulinikasirisha—lakini hakukuwa na chochote ambacho ningeweza kufanya. Majaribio yangu ya upinzani yalikuwa bure, yalileta tu mateso na ukatili zaidi. Katika, nyumba ya kuzuiliwa walinzi waliwafanya wafungwa kukariri amri kila siku: “Kiri uhalifu wako na kutii sheria. Kuwashawishi wengine kutenda uhalifu hakukubaliwi. Kuunda magenge hakukubaliwi. Kupigana hakukubaliwi. Kuwadhulumu wengine hakukubaliwi. Kutoa mashtaka yasiyo kweli dhidi ya wengine hakukubaliwi. Kuchukua chakula ama mali ya wengine hakukubaliwi. Kufanya hila kwa wengine hakukubaliwi. Wadhalimu wa gerezani wanapaswa kuchukuliwa hatua kali. Ukiukaji wowote wa sheria unapaswa kuripotiwa kwa wasimamizi ama polisi wenye madaraka mara moja. Unapaswa kutoficha ukweli ama kujaribu kulinda wafungwa ambao wamekiuka sheria na kufuatia kunapaswa kuwa kwa kwenye huruma. …” Kwa kweli, walinzi waliwatia moyo wafungwa wengine kunitesa, wakiwaruhusu kunitendea hila kila siku: Wakati ambapo halijoto ilikuwa digrii 8 ama 9 chini ya sufuri, walilowa viatu vyangu: kwa siri walimwaga maji kwenye chakula changu: jioni, nilipokuwa nikilala, walirowesha jaketi langu lililojazwa pamba: walinifanya nilale kando ya choo, mara kwa mara walivuta mfarishi wangu usiku, walivuta nywele zangu, ili kunizuia kulala; walininyang’anya andazi langu lilikopikwa kwa mvuke, walinilazimisha kusafisha choo, na kuingiza kwa nguvu dawa zao zilizosalia ndani ya mdomo wangu, hawakuniacha nikojoe…. Wakati sikufanya walichosema, wangechangia na kunipiga—na mara nyingi wakati kama huu wasimamizi ama polisi walio na mamlaka wangetoroka wasionekane ama kujifanya hawajaona chochote; wakati mwingine wangejificha mbali na kutazama. Iwapo wafungwa wangekaa siku chache bila kunitesa, wasimamizi wangewahochea kunichapa mimi. Mateso ya kikatili ya hao walinzi yalinijaza na chuki kwao. Iwapo singeshuhudia hili na macho yangu mwenyewe na kulipitia mimi binafsi, kamwe singeamini kwamba serikali ya CCP, ambayo inapaswa kuwa imejaa ukarimu na maadili, ingeweza kuwa ovu, ya kuogofya na mbaya—singewahi kuona sura yake ya kweli, sura ambayo ni danganyifu na yenye unafiki. Mazungumzo yake yote ya “kuhudumia watu, kutengeneza jamii iliyostaarabika na ya upatanifu”—huu ni uongo ulioundwa kuwadanganya na kuwahadaa watu, ni njia, hila, ya kujipendekeza na kupata heshima haifai kupata. Wakati huo, nilifikiri kuhusu maneno ya Mungu: “Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu bila hisia yoyote, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, wanaenda kinyume na dhamiri yote, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)). Ili kunilazimisha kukataa na kumsaliti Mungu CCP ilifanya kila kitu kunitesa na kuniangamiza—ilhali haikujua hata kidogo kwamba kadiri ilivyonitesa, ndivyo niliona sura yake ya ibilisi kwa wazi kabisa, na ndivyo nilivyoidharau na kuikataa zaidi kutoka kwa vina vya moyo wangu. Nilikuwa nimeamua zaidi kumfuata Mungu.

Kwa kuona kuwa hawangeniruhusu kusema chochote walichotaka, walitumia kila gharama—iwe nguvu, ama vifaa na rasilmali za fedha—kufanya juu chini kuuliza dhibitisho kwamba nilikuwa muumini wa Mungu. Baada ya miezi mitatu, kuharakisha kote kwao huku na kule hakukuwa kumezaa matunda. Mwishowe, walijaribu kupiku: Walimpata mhojaji stadi. Ilisemekana kwamba kila mtu aliyeletwa kwake alipitia aina zake tatu za mateso, na hakuna mbaye hakuwahi kukiri. Siku moja, maafisa wanne wa polisi walikuja na kuniambia: “Leo, tunakupeleka nyumbani mpya.” Kisha, walinisukuma kwa gari la kusafirisha wafungwa, kufunga pingu mikono yangu nyuma ya mgongo wangu, na kuweka kifuniko kichwani mwangu. Sikujua chenye walikuwa wamepanga, kunitesa, kwa hivyo nilijihisi uwoga. Wakati huo, nilifikiria maneno ya Bwana "Kwa maana yeyote atakayeokoa maisha yake atayapoteza; na yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata" (Mathayo 16:25). Maneno ya Bwana yalinipa imani na nguvu. Kama tunataka kumwamini na kumfuata Mungu katika mji huu wa mapepo wa china, nilazima tuwe jasiri kutoa uhai wetu. Nilikuwa tayari kufa kwa ajili ya Mungu. Kustaajabika, baada ya kuingia kwa gari, bila kuwa mwangalifu nilisikia bila kusudia mazungumzo baina ya polisi waovu. Ilionekana walikuwa wakinipeleka mahali pengine kuhojiwa. Ah! Hawakuwa wakinipeleka kuuawa—na nilikuwa nimejitayarisha kufa shahidi kwa ajili ya Mungu! Nilipokuwa tu nikifikiria hili, kwa sababu fulani zisizojulikana mmoja wa polisi alikaza kamba za ukaya kichwani mwangu. Punde baadaye, nilianza kuhisi kutotulia–ilihisi kana kwamba nilikuwa nikisongwa. Nilijipata nikijiuliza iwapo kwa kweli wangenitesa hadi nife. Wakati huo, nilifikiri kuhusu jinsi wanafunzi wa Yesu walikuwa wamejitoa kueneza injili. Singekuwa mwoga. Hata iwapo ningekufa, singewasihi wailegeze, hata zaidi singekubali kushindwa. Lakini sikuweza kujidhibiti: Nilizirai na kuwaangukia. Huku wakiona kilichokuwa kikitendeka, polisi kwa haraka walilegeza kifuniko. Nilianza kutoa povu mdomoni, kisha sikuweza kuacha kutapika. Ilihisi kana kwamba ningetapika mpaka matumbo yangu yatoke nje. Nilihisi kizunguzungu, kichwa changu kilikuwa kitupu, na singeweza kufungua macho yangu. Sikuwa na nguvu popote mwilini mwangu kana kwamba nilikuwa nimepooza. Ilihisi kana kwamba kulikuwa na kitu cha kunata mdomoni mwangu ambacho singeweza kutoa. Daima nilikuwa dhaifu, na baada ya kuteswa namna hii nilihisi kwamba nilikuwa taabani, kwamba ningeacha kupumua wakati wowote. Katikati ya uchungu, nilimwomba Mungu: “Ee Mungu! Ikiwa nitaishi au kufa niko tayari kukutii Wewe. Nikuomba Uulinde moyo wangu, ili kwamba niweze kutii yote ambayo Unapanga na kuweka kwa utaratibu.” Wakati mwingine baadaye, gari liliwasili kwa hoteli fulani. Wakati huo, mwili wangu wote ulihisi mnyonge na singeweza kufungua macho yangu. Walinibeba hadi kwa chumba kilichofungwa kabisa. Yote ambayo ningesikia ilikuwa sauti ya watumishi wengi wa serikali ya CCP waliokuwa wamesimama wakinizingira wakinijadili, wakisema kwamba kuniona kulikuwa kama kuona jinsi Liu Hulan alivyokuwa. Ilikuwa kitu kilichozindua, cha kuvutia sana! Yeye hata ni sugu kuliko jinsi Liu Hulan alivyokuwa! Kwa kusikia hili, moyo wangu ulifura kwa msisimko. Niliona kwamba kwa kutegemea imani na kumtumainia Mungu bila shaka Shetani angeshindwa, kwamba Shetani alikuwa chini ya miguu ya Mungu! Nilimshukuru na kumsifu Mungu. Wakati huu, nilisahau uchungu. Nilihisi kufurahishwa pakubwa mno kutukuzwa na Mungu. Punde baadaye, “mtaalamu wa mahojiano” ambaye polisi walimzungumzia aliwasili. Punde alipoingia, alipaza sauti: “Yuko wapi huyo mwanamke mjinga? Acha nimwone!” Alitembea mbele yangu na kunishika kwa nguvu. Bada ya kunizaba makofi mara kadhaa usoni, alinipiga ngumi za nguvu mara kadhaa kifuani na mgongoni, kisha akaondoa kiatu chake moja cha ngozi na kunipiga usoni nacho. Baada ya kuchapwa naye hivi, nilipoteza hisia kwamba kulikuwa na kitu ambacho singeondoa mdomoni ama tumboni mwangu. Sikuhisi mdhaifu tena na ningeweza kufungua macho yangu. Hisia polepole ilirudi katika viungo vyangu, na nguvu ilianza kurudi mwilini mwangu. Kisha, kwa ukali alinyakua mabega yangu na kunisukuma nyuma dhidi ya ukuta, akiniamuru nimwangalie na kujibu maswali yake. Kuona kwamba sikuwa namzingatia hata kidogo kulimfanya akasirike sana, na alijaribu kupata mjibizo kutoka kwangu kupitia kutukana, kukashifu na kumkufuru Mungu. Alitumia mbinu duni, za kustahili dharau kabisa kuniambika, na kusema kwa kuogofya: “Kwa makusudi nakutesa kwa kutumia kile kisichovumilika na mwili na nafsi yako, ili kukufanya upitie uchungu ambao hakuna mtu wa kawaida angeweza kupitia—utatamani heri ufe. Mwishowe, utaniomba nikuache uende na hapo ndipo utazungumza maana, na kusema kwamba majaliwa yako hayako mikononi mwa Mungu—yako mikononi mwangu. Nikitaka ufe, itafanyika mara moja; nikitaka uishi, utaishi; na taabu yoyote nyingine ninayotaka upitie, hiyo ndiyo utapitia. Mwenyezi Mungu wako hawezi kukuokoa—utaishi tu ukituomba tukuokoe.” Nikiwa nimekabiliwa na hawa wauaji, wanyama mwitu, ibilisi waovu wenye kustahili dharau, wasio na aibu na walio duni, nilitaka sana kupigana nao. “Vitu vyote mbinguni na duniani vinaumbwa na Mungu na kudhibitiwa na Yeye,” nilifikiri. “Majaliwa yangu pia yanatawaliwa na ukuu na mipango ya Mungu. Mungu ndiye Mpatanishi wa uhai na kifo; unadhani nitakufa tu kwa sababu unataka nife?” Wakati huo, moyo wangu ulijawa na ghadhabu. Matendo yote ya kustahili dharau ambayo polisi hao walinitendea na mambo yote ya kumkufuru na kumpinga Mungu ambayo walikuwa wamesema leo yalifunua waziwazi asili yao ya kishetani kama wanaochukia ukweli na kumpinga Mungu, na huu ungekuwa ushahidi unaohitajika kupata laana, adhabu na kuangamizwa na Mungu.

Kukataa kwangu kukiri kulikuwa kumemwaibisha sana huyo aliyedhaniwa mtaalamu. Kwa hasira alipinda mkono wangu mmoja nyuma ya mgongo wangu na kuvuta huo mwingine nyuma ya mabega yangu, kisha alitia pingu mikono yangu na kuibana pamoja. Baada ya chini ya nusu saa, matone makubwa ya jasho yalikuwa yakitiririka usoni pangu, na katika macho yangu kunizuia kuyafungua. Huku akiona kwamba bado singejibu maswali yake, alinirusha sakafuni, kisha aliniinua kwa pingu nyuma ya mgongo wangu. Mara moja, nilihisi uchungu mwingi mikononi mwangu kana kwamba ilikuwa imevunjwa. Ilitia uchungu sana kiasi kwamba nilipumua kwa shida. Kisha, alinirusha dhidi ya ukuta na kunifanya nisimame dhidi yake. Jasho ilikuwa ikitia waa macho yangu. Nilihisi uchungu sana kiasi kwamba mwili wangu wote ulijawa na jasho—hata viatu vyangu vililowa. Daima nilikuwa dhaifu, na wakati huu nilianguka. Yote ambayo ningefanya tu ilikuwa kuhema kupitia mdomo wangu. Ibilisi alisimama kwa upande mmoja akinitazama. Sikujua alichoona—pengine aliogopa angelaumiwa iwapo ningekufa—kwa haraka alichukua kiasi kidogo cha karatasi ya shashi na kupanguza jasho yangu, kisha akaninywesha kikombe cha maji. Alifanya hivi baada ya nusu saa na kadhalika. Sijui nilifanana vipi wakati huo. Nadhani lazima ilikuwa inaogofya sana, kwa sababu ningehema tu mdomo wangu ukiwa wazi: ilionekana nilikuwa nimepoteza uwezo wangu kupumua kupitia pua langu. Midomo yangu ilikuwa imekauka na kufanya upenyu na ilichukua nguvu yote niliyokuwa nayo kupumua tu. Nilihisi kifo kikikaribia tena—pengine wakati huu kwa kweli ningekufa. Lakini wakati huo, nilifikiria Luka, mtume mmoja wa Yesu, na uzoefu wake wa kuny’ongwa hadi kufa. Nilimfikiria Luka, mmoja wa wanafunzi wa Mungu, na uzoefu wake wa kuangikwa akiwa hai. Moyoni mwangu, nilipata tena nguvu yangu kwa hiari, na kuendelea kusema kitu kile kile tena na tena kujikumbusha: “Luka alikufa kwa kuangikwa akiwa hai. Mimi, pia, lazima niwe Luka, lazima niwe Luka, niwe Luka … Kwa hiari ninatii utaratibu na mipango ya Mungu, nataka kuwa mwaminifu kwa Mungu hadi kufa kama Luka.” Wakati ule ule maumivu yalipokuwa hayawezi kuvumilika na nilikuwa ukingoni mwa kifo, ghafla nilisikia polisi mmoja mwovu kisema kwamba ndugu kadhaa waliomwamini Mwenyezi Mungu walikuwa wamekamatwa. Moyoni mwangu, nilishtuka: Ndugu wengine kadhaa watateswa. Lazima watakuwa wagumu hasa kwa kaka. Moyo wangu ulijawa na wasiwasi. Niliendelea kuwaombea kwa ukimya, Pengine niliguswa na Roho Mtakatifu; kadiri nilivyoomba zaidi ndivyo nilivyotiwa moyo zaidi. Nilisahau uchungu wangu bila kufahamu. Nilijua vizuri sana kwamba hii ilikuwa mipango ya hekima ya Mungu; Mungu alijali udhaifu wangu, na alikuwa akiniongoza kupitia wakati wangu wa uchungu zaidi. Usiku huo, sikujali tena jinsi polisi waovu walivyonitendea, na sikutia maanani hata kidogo maswali yao. Huku wakiona kilichokuwa kikitendeka, polisi waovu walitumia ngumi zao kuupiga uso wangu kwa ukatili, kisha wakapinda nywele kwa panja langu vidoleni vyao na kuzivuta kwa ghafla. Masikio yangu yalikuwa yamevimba kwa ajili ya kupindwa, uso wangu ulikuwa usiotambulika, mapanja na chini za miguu yangu zilikuwa zimeachwa na majeraha, na kuchunuka waliponichapa na kipande kinene cha mbao, na vidole vyangu vya miguu, pia, vilikuwa vimeachwa vyeusi na samawati baada ya kupondwa na kipande cha mbao. Baada ya kuniangika juu kwa pingu kwa saa sita, wakati polisi waovu walifungua pingu, nyama kutoka kwa kidole changu gumba cha kushoto—kulisalia tu safu nyembamba kabla ya mfupa. Pingu pia zilikuwa zimeacha vifundo vyangu vikiwa vimefunikwa na lengelenge ya njano, na hakukuwa na njia ya kuirudisha. Wakati huo, polisi wa kike aliyeonekana mwenye madaraka makubwa aliingia. Alinitazama juu na chini, kisha akawaambia: “Hamwezi kumchapa huyu tena—yuko karibu kufa.” Polisi walinifungia katika chumba kimoja hotelini. Mapazia yake yalikuwa yamefungwa kwa kubanwa usiku kucha na mchana kutwa. Mtu fulani alipewa jukumu la kulinda mlango, na hakuna kati ya watumishi wa huduma aliyeruhusiwa kuingia, wala hakuna aliyeruhusiwa kuona matukio ya wao kunitesa na kunishambulia kikatili kule ndani. Walichukua zamu kunihoji bila pumziko. Kwa siku na usiku tano, hawakuniruhusu kulala, hawakuniruhusu kukaa wala kuchuchumaa, wala hawakuniruhusu kula chakula changu hadi kushiba. Niliruhusiwa tu kusimama nikiegemea dhidi ya ukuta. Siku moja, afisa mmoja alikuja kunihoji. Huku akiona kwamba nilikuwa nikimpuuza, alishikwa na hasira na kunipiga teke lililonirusha chini ya meza. Kisha, alinivuta kutoka hapo na kunipiga ngumi, akisababisha damu kububujika kutoka kwa kona ya mdomo wangu. Ili kuficha ukatili wake, kwa haraka alifunga mlango kuzuia yeyote kuingia. Kisha alirarua kiasi kidogo cha karatasi ya shashi na kupanguza damu yangu, akisafisha damu kutoka usoni pangu kwa maji na kusafisha damu kutoka kwenye sakafu. Niliacha damu kiasi kwa sweta yangu nyeupe kwa makusudi. Niliporudi katika chumba cha kuzuiliwa, hata hivyo, polisi waovu waliwaambia wafungwa wengine kwamba damu kwenye mavazi yangu ilitokana na wakati nilipokuwa nikithibitishwa katika hospitali ya wagonjwa wa akili, na kusema kwamba hapo ndipo nilipokuwa siku kadhaa zilizopita. Majeraha na damu mwilini mwangu yalikuwa yamesababishwa na wagonjwa, wao, polisi, hawakuwa wamenigusa…. Ukweli huu katili ulinionyesha ukatili, ujanja wenye kudhuru kwa siri, na unyama wa polisi wa watu na Wakati huo huo, nihisi kwa kweli ulinzi, na utuzaji wa Mungu. Kila wakati uchungu wangu ulipofika kiwango mbaya kabisa, Mungu kunitia nuru na kuniongoza, Akiongeza imani na nguvu yangu, kunipa ujasiri wa kusimama shahidi kwake. Wakati ambapo ukatili wa polisi waovu uliniacha karibu na kifo, Mungu aliniruhusu kusikia habari ya kukamatwa kwa ndugu, kutumia hili kunisisimua zaidi kuwaombea, ili kwamba nilisahau uchungu wangu na bila kujua kushinda vikwazo vya kifo. Kwa sababu ya utumbuizo wa Shetani mwovu, mkatili, niliona kwamba Mungu pekee ndiye ukweli, njia, na uhai, na kwamba tabia ya Mungu ni ishara ya haki na wema. Mungu pekee ndiye hutawala vitu vyote, na hupanga kila kitu, na Yeye Alitumia nguvu Yake kuu na hekima kuongoza kila hatua yangu katika kushinda kuzingirwa na ibilisi, katika kushinda udhaifu wa mwili na vikwazo vya kifo, kuniruhusu kwa kunata kuokoka katika pango hili ovu. Nilipokuwa nikifikiri kuhusu upendo na wokovu wa Mungu, nilihisi kutiwa moyo sana, na nikaamua kupigana na Shetani hadi mwisho kabisa. Hata ningedhoofika gerezani, ningesimama imara katika ushuhuda wangu na kumridhisha Mungu.

Baada ya kujaribu kila kitu walichoweza, polisi waovu hawakuwa wamepata chochote kutoka kwangu. Mwishowe, walisema kwa kusadiki sana: “CCP wametengenezwa kwa chuma, lakini wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu wametengenezwa kwa almasi—wao ni bora zaidi kuliko CCP katika kila hali.” Baada ya kusikia maneno haya, moyoni mwangu singeweza kujizuia kufurahia na kumsifu Mungu: Ee Mungu, nakushukuru na kukusifu! Kwa uweza na hekima Yako Umemshinda Shetani na kushinda maadui Wako. Wewe ni mamlaka ya juu zaidi, na naomba utukufu uwe Wako! Ni wakati huu tu ndio niliona kwamba bila kujali jinsi CCP ilivyo ovu, inadhibitiwa na kupangwa na mikono ya Mungu. Jinsi maneno ya Mungu yasemavyo: “Vitu vyote mbinguni na ardhini lazima zije chini ya utawala Wake. Haviwezi kuwa na hiari yoyote na vyote ni lazima vitii mipango Yake. Hii iliagizwa na Mungu, na ni mamlaka ya Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea).

Siku moja, polisi waovu walikuja kunihoji mara nyingine tena. Wakati huu, wote walionekana kuwa wa ajabu kidogo. Waliniangalia walipozungumza, lakini haikuonekana kama walikuwa wakinizungumzia. Walionekana kujadili kitu. Kama nyakati za awali, mahojiano haya yaliishia katika kushindwa. Baadaye, polisi waovu walinirudisha kwa seli. Njiani, nilisikia ghafla wakisema kwamba ilionekana kuwa ningeachiliwa siku ya kwanza ya mwezi ujao. Kwa kusikia hili, moyo wangu karibu ulipasuka kwa msisimko: Hili inamaanisha nitaondoka katika siku tatu! Hatimaye naweza kuondoka katika jahanamu hii ya shetani! Kwa kukandamiza furaha iliyokuwa moyoni mwangu, nilitarajia na kusubiri kila sekunde ilipokuwa ikipita. Siku tatu zilihisi zaidi kama miaka mitatu. Mwishowe, siku ya kwanza ya mwezi iliwadia! Siku hiyo, niliendelea kukodolea mlango macho, nikisubiri mtu aite jina langu. Asubuhi ilipita, na hakuna kilichofanyika, niliweka matumaini yangu yote katika kuondoka alasiri—lakini jioni ilipofika, bado hakuna kilichofanyika. Wakati ambapo ilikuwa wakati wa chakula cha jioni, sikuhisi kula. Moyoni mwangu, nilikuwa na hisia ya hasara; wakati huo, ilikuwa kana kwamba moyo wangu ulikuwa umeanguka kutoka mbinguni hadi jahanamu. “Mbona hali?” mlinzi aliuliza wafungwa wengine. “Hajala sana tangu aliporudi kutoka kwa mahojiano siku ile,” mfungwa mmoja alijibu. “Gusa panja lake; je, yeye ni mgonjwa?” mlinzi alisema. Mfungwa alikuja na kugusa panja langu. Alisema lilikuwa na joto sana, kwamba nilikuwa na homa. Kwa kweli nilikuwa na homa. Ugonjwa huo ulikuwa umekuja ghafla sana, na ulikuwa mkali sana. Wakati huo, nilianguka. Kwa kipindi cha saa mbili, homa ikawa mbaya na mbaya zaidi. Nililia! Wote, akiwemo mlinzi, walinitazama nikilia. Wote waliduwaza: Maoni yao kunihusu yalikuwa kama mtu ambaye hakushawishika kwa kivutio wala kuogopeshwa kwa vitisho, ambaye hakuwahi kutoa chozi hata moja kila wakati alipokabiliwa na mateso ya kuhuzunisha, ambaye alikuwa ameangikwa juu kwa pingu kwa saa sita bila kupiga kite. Ilhali, leo, bila mateso yoyote, nililia. Hawakujua machozi yangu yalitoka wapi—walifikiri tu kwamba lazima niwe mgonjwa sana. Kwa kweli, Mungu na mimi tu ndio tulijua sababu. Yote yalikuwa kwa sababu ya uasi na kutotii kwangu. Machozi haya yalitiririka kwa sababu nilihisi kukata tamaa wakati ambapo matarajio yangu yaliambulia patupu na matumaini yangu yalikuwa yamevunjika. Yalikuwa machozi ya uasi na lalamiko. Wakati huo, sikutaka tena kuweka azimio langu kumshuhudia Mungu. Hata sikuwa na ujasiri kujaribiwa hivi tena. Jioni hiyo, nililia machozi ya taabu, kwa sababu nilikuwa nimechoshwa na maisha gerezani, niliwadharau pepo hawa—na hata zaidi ya hilo, nilichukia kuwa mahali hapa pa pepo. Sikutaka kukaa sekunde nyingine hapo. Kadiri nilivyofikiri kuhusu hilo, ndivyo nilivyovunjika moya zaidi, na ndivyo nilivyohisi hisia kubwa ya taabu, ya huzuni, na upweke zaidi. Nilihisi kana kwamba nilikuwa mashua pweke juu ya bahari, moja ambayo ingemezwa na maji wakati wowote; zaidi ya hayo, nilihisi wale walionizunguka walikuwa wenye kudhuru kwa siri sana na wabaya sana kiasi kwamba wangetoa hasira yao kwangu wakati wowote.

Nilimwomba Mungu tena na tena, na haya maneno kutoka kwake yanilinijia: “Kwa kila mtu ambaye anatumai kumpenda Mungu, hakuna ukweli usioweza kupatikana, na hakuna haki wasioweza kusimama imara nayo. Unafaa kuishije maisha Yako? Unapaswa kumpenda Mungu vipi na kutumia upendo huu ili kukidhi hamu Yake? Hakuna kubwa zaidi katika maisha Yako. Zaidi ya yote, lazima uwe na matarajio hayo na uvumilivu, na hupaswi kuwa kama wanyonge wasio na nia. Lazima ujifunze jinsi ya kupitia maisha ya maana, na kuuona ukweli wa maana, na hupaswi kujichukua kipurukushani katika njia hiyo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu). Maneno ya Mungu yalinipa imani. Nilifikiria jinsi nilivyoapa kiapo mbele za Mungu kwamba bila kujali ni kiasi gani nitateseka, nitasimama shahidi na kumuaibisha Shetani. Lakini wakati nilikuwa nikikabiliwa na mateso ya polisi kwa muda mrefu, nilipoteza dhamira yangu na nilikuwa nikitarajia tu kwa siku ambayo ningeweza kukimbia mahali hapo mnyonge. Ilikuwaje aina yoyote ya utii? Ilikuwaje ushuhuda wa aina yoyote? Katika sala kwa Mungu, niliapa kwamba hata ikiwa inamaanisha kutumia maisha yangu yote gerezani, sitawahi kujitoa kwa Shetani. Ningesimama shahidi na kumdhalilisha Shetani. Halafu mnamo Desemba 6, 2005, niliachiliwa, nikikomesha maisha ya gerezani ya kuzimu.

Baada ya kupitia majaribu ya kukamatwa na kuteswa. ingawa mwili wangu ulikuwa umevumilia taabu kiasi, nilikuwa nimekuza umaizi na, utambuzi na kweli kuona kwamba serikali ya CCP ni mfano halisi wa Shetani ibilisi, kundi la wauaji ambao wangewaua watu kufumba kufumbua, lakini pia nilikuja kuelewa kudura na maarifa ya Mungu, na vilevile haki na utakatifu Wake, nilikuwa nimekuja kufahamu nia nzuri za Mungu katika kuniokoa, na utunzaji Wake na ulinzi Wake kwangu, Akiniruhusu, katika ukatili wa Shetani, kumshinda Shetani hatua moja kwa wakati na kusimama imara katika ushuhuda wangu. Kutoka siku hii kuendelea, ningetaka kutoa nafsi yangu yote kwa Mungu kikamilifu na kwa uthabiti ningemfuata Mungu, kwamba ningeweza kupatwa na Yeye mapema.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Bahati na Bahati Mbaya

Na Dujuan, JapaniNilizaliwa katika familia fukara katika kijiji cha mashambani. Tangu niwe mtoto, niliishi maisha magumu na nilidharauliwa...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp