Uzoefu wa Mkristo Kutoka Myanmari Kuzimuni Baada ya Kifo

03/04/2023

Na Dani, Myanmari

Nilivutiwa na Ukristo nilipokuwa mdogo, lakini kwa kuwa familia yangu ilizingatia imani ya Buddha, sikuwa Mkristo. Nilikuwa nimesikia kuhusu kuzimuni wakati huo, lakini sikuamini kuhusu jambo hilo kabisa.

Mnamo Aprili 2022, rafiki yangu alinialika nijiunge na mkutano wa mtandaoni, ambayo ilikuwa mara yangu ya kwanza kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu. Nilihisi kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yalikuwa Muumba wa mbinguni akizungumza na wanadamu. Baada ya hapo nilisoma maneno mengi ya Mwenyezi Mungu mtandaoni. Nilifahamu kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mmoja wa kweli, na kwamba Mungu ameshuka duniani ili kuwaokoa wanadamu. Lakini kwa kuwa familia yangu ilinizuia, na pia kwa sababu nilikuwa nikishikilia mambo ya ulimwengu, sikuhudhuria mikutano mara kwa mara na hata nilijiondoa kutoka kwenye kikundi changu cha mikutano kwa muda kidogo.

Kisha, takribani saa tatu unusu asubuhi mnamo Februari 3, 2023, nilikuwa nimechoka baada ya mkutano, kwa hivyo nilijilaza ili nipumzike. Baadaye kakangu mdogo aliniambia kwamba familia yangu ilijaribu kuniamsha kutoka usingizini humo bila mafanikio, kwa hiyo walinikimbiza hospitalini kwa ajili ya matibabu ya dharura. Daktari alinichunguza na kusema kwamba tayari nilikuwa nimeacha kupumua, kwa hiyo alitoa cheti cha kifo. Familia yangu haikuwa na budi ila kunirudisha nyumbani. Waliwajulisha jamaa na majirani zetu, na wakajiandaa kufanya mazishi na kunizika siku tatu baadaye.

Sikujua kilichokuwa kikiendelea nyumbani kwetu wakati huo. Nilichojua ni kwamba nilienda katika ulimwengu mwingine. Nilikuwa nimevalia joho nyeupe, nikitembea peke yangu kwenye njia isiyo na mwanga na yenye moshi. Sikuweza kuona anga au kile kilichokuwa mbele yangu. Njia ilikuwa ya kuteremka, yenye matuta, iliyojaa mashimo, yenye isiyo nyoofu na yenye kupindapinda. Pande zote mbili za njia hiyo, niliona tu kila aina ya mimea ya ajabu ambayo sikuwa nimewahi kuiona hapo awali ambayo ilijaa miiba. Pia niliweza kusikia milio ya wanyama pande zote…. Nilikuwa nikitembea bila viatu kwenye njia hiyo, na ilikuwa ikiingia kwenye miguu yangu. Mwili wangu mzima ulikuwa unawaka moto na niliishiwa pumzi kidogo. Nilitembea kwa muda mrefu, kisha nikakutana na pepo aliyevaa nguo nyeusi. Ilikuwa nyeusi kuanzia utosini hadi wayoni—singeweza kuona uso au miguu yake. Alisema, “Nifuate!” Sauti yake ilikuwa ya kutisha sana. Kwa hofu, nilijitahidi kusema, “Unanipeleka wapi? Sijawahi kwenda huko—siendi. Nataka kwenda nyumbani.” Nilitaka kukimbia. Hapo hapo, pepo wanne au watano waliovalia mavazi meusi walielea, wakanishika na kusema, “Umekufa—huwezi kurudi nyuma. Umetenda dhambi nyingi, na sharti uadhibiwe kwa ajili ya dhambi ulitenda maishani mwako."

Kisha wakanipeleka mbele ya lango kubwa ambapo niliona mapepo kadhaa wakiwa wamesimama wakilinda. Walikuwa warefu, wenye macho na masikio makubwa, na wengine walikuwa na meno makali yaliyotoka nje, wakiwa na sura za kushtua. Walikuwa wameshikilia silaha na walikuwa bila nguo kuanzia kiunoni kurudi juu, wakiwa wamevalia mikufu iliyotengeneza kwa mifupa na mafuvu ya wafu ikiwa imening'inia kwenye miili yao. Walijawa na makovu kwenye miili. Nilisikia mayowe mengi na ya uchungu punde tu walinzi walipofungua lango hilo. Kila pahali, mahali hapo palikuwa pamjeaa sauti za mapambano kutokana na uchungu wa kutisha. Kulikuwa na moto mkali pale, mkali kupindukia. Niliogopa sana, na nikauliza mapepo, “Nilifanya makosa yapi? Sipaswi kuwa hapa.” Walinionyesha dhambi zote nilikuwa nimefanya katika maisha yangu, moja baada ya nyingine, siku niliyozitenda, na saa niliyozitenda, na hata dakika na sekunde niliyofanya mambo hayo. Hata uwongo niliosema na sikuuwazia ulirekodiwa hapo waziwazi kabisa. Hapa kuna baadhi ya mifano. Mnamo Septemba 5, 2022, akina ndugu walinipigia simu kunialika kwenye mkutano, lakini nilikuwa dhaifu kutokana na shinikizo la familia, na sikuhudhuria. Mnamo Septemba 10, 2022, sikuhudhuria mkutano huo na sikujibu simu za akina ndugu, sikutaka kuwaona. Mnamo Oktoba 5, 2022, nilijiondoa kutoka katika vikundi vyote vya mikutano na kukata mawasiliano na washiriki wengine wa kanisa. Mnamo Oktoba 6, 2022, nilienda mbali na Mungu nikipendelea mitindo ya ulimwengu na kujiburudisha. Nilipigwa na butwaa. Kuona idadi ya dhambi nilikuwa nimetenda kuliniogovya sana.

Kisha, yule pepo aliyevalia mavazi meusi alinipeleka mahali palipokuwa na kibao, kilichosema hapa ndipo wale wanaodanganya, kuhukumu, au kumkufuru Mungu wanaadhibiwa. Hapa ndipo nilipoona adhabu kali zaidi. Aina ya kwanza ya adhabu ilikuwa wadudu kutoka ndani ya midomo na ngozi ya wale waadhibiwa na kuwauma, hivyo kwamba wadudu walikuwa wakiwatafuna kila mahali—lilikuwa jambo la kutisha sana. Katika aina ya pili, watu waliokuwa wakiadhibiwa walikuwa uchi, na walielekezwa kwenye ubao mrefu mmoja baada ya mwingine, ambapo watu 10 waliadhibiwa mara moja. Walilazimika kupiga magoti, mikono yao ilikuwa imefungwa nyuma ya migongo yao, na videvu vyao vimewekwa kwenye ubao. Walikuwa na kamba shingoni mwao, na kamba zilipovutwa, ndimi zao zilitoka nje. Kando ya ubao, pepo mwovu mwenye pembe kichwani alitia ndoano kwenye ndimi zao, kisha akazivuta kwa nguvu; wengine ndimi zao zilirefushwa mara mbili ya urefu wao. Kisha, pepo huyo alitumia msumari mrefu unaotoshana na kalamu kuzipigilia kwenye ubao, ambao ulikuwa na moto unaowaka chini yake. Pepo huyo pia alikuwa akimwagilia maji ya moto yanayochemka sana kwenye ndimi hizo bila kukoma. Maji haya yanayofanana na moto yalikuwa yakiletwa kutoka kwenye kidimbwi kilichokuwa mbali, na yalipewa pepo wote bila kukoma. Ilipomiminwa kwenye ulimi wa mtu, ulimi uliharibiwa kabisa. Macho ya watu wengine hata yalianguka nje. Kisha, roho waovu wakamwaga maji ya moto juu ya miili yao yote, hivyo wakaangamizwa kabisa. Wale waliokuwa wakiadhibiwa walilia kwa huzuni hadi kufa. Lilikuwa jambo la kutisha. Baadhi ya watu hawakuweza kustahimili na wakafariki muda si mrefu, lakini kama bado wangehitaji kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi zaidi, wangefufuliwa ili waendelee kuadhibiwa. Ikiwa bado hawakuwa wamekufa baada ya adhabu yao, wadudu wangetoka kwenye miili yao na kuwala, kisha wangefufuliwa na kuadhibiwa kwa njia nyingine.

Aina ya tatu ya adhabu ilikuwa ni kutupwa kwenye dimbwi la maji ya moto mkali sana. Niliona bamba kubwa la mviringo la chuma lililofungwa kamba nne. Watu takribani mia moja au mia mbili walikuja kutoka katika sehemu nyingine ya kuadhabiwa katika sekunde chache tu, wakitokea kwenye bamba hilo. Walipiga magoti kwenye sahani hiyo ya moto iliyokuwa inawaka wakiwa uchi kabisa huku kamba zenye miiba zikiwafunga moja kwa moja mikono na sehemu za juu za mwili. Watu hawa walitoka katika dini na makabila mbalimbali. Wengine wao hawakumwamini Mungu, lakini wengine walikuwa Wakristo au Wabudha. Walikuwa wakiadhibiwa kwa sababu hawakuwa wameikubali kazi mpya ya Mungu, na walikuwa wamemkufuru na kumhukumu Mungu. Ingawa baadhi yao walikuwa wameikubali kazi mpya ya Mungu, imani yao ilikuwa ya kijuujuu tu, ya kutimiza wajibu tu, na ya udanganyifu kwa Mungu. Mtu wa aina hiyo pia aliadhibiwa na Mungu. Wote walikuwa wakimwita mungu wa imani yao. Wengine walimwita mungu huyu, na kisha mungu yule. Kulikuwa na sauti nyingi tofauti tofauti, na sikuweza kuzisikia vizuri. Hata hivyo, haijalishi jinsi walivyopiga kelele; hawakupata jibu. Baada ya hapo, watu hao walipelekwa kwenye dimbwi kubwa, na ndani ya dimbwi hilo kulikuwa na maji ya moto yaliyokuwa yakichemka. Kamba zilizowafunga zililegea moja kwa moja, bamba la chuma walilokuwa juu yake likainama, na wote wakaanguka ndani ya dimbwi. Walikuwa wakichemka na kukaangwa, wakichomeka hadi walipiga mayowe kwa uchungu mwingi. Baadhi ya watu walikuwa ukingoni, wakijaribu kwa nguvu zao zote ili kujivuta watoke kwenye dimbwi hilo, lakini walianguka tena ndani. Muda si muda, sauti ya mayowe iliisha. Kila mtu alikuwa amekufa, akielea juu ya uso wa dimbwi la maji ya moto. Wakati wote walikuwa wamekufa, wavu mkubwa uliwanyakua wote, na wakafufuka tena kwa ajili ya kupata adhabu inayofuata.

Kisha nikapelekwa mahali pengine. Wale waliokuwa huko walikuwa wakiadhibiwa kwa kila namna kwa kuwatusi wazazi wao, wazee, au walimu wao. Baadhi yao walikuwa uchi, wakiwa wamefungwashingoni, mikononi na miguuni kwa minyororo yenye miiba. Walichapwa kwa mijeledi wakivuja damu kiasi kwamba nyama na damu yao ilitiririka. Walikuwa wakihangaika na kulia kwa uchungu. Mashetani wa kuzimuni walitumia shoka kukata mikono na miguu yao, na walitumia kitu kama nyundo kuwaponda. Huku wakiadhibiwa waliulizwa, “Je, ulifikiria kutotenda dhambi hii wakati huo?” Walitubu, lakini hakuna aliyeweza kuwaokoa, na waliteswa hadi kufa. Baada ya hapo, walifufuka na kupokea adhabu inayofuata. Baadhi ya watu walizikwa wakiwa hai. Ardhi ya mahali hapo ilikuwa ikisonga, ikiyumba, na moto ulikuwa ukiwaka kwenye udongo. Wale walioadhibiwa walikuwa wakivutwa polepole kwenda chini, wakizama ardhini hadi wakafa.

Kisha nikapelekwa mahali ambapo wazinzi walikuwa wanaadhibiwa. Walikuwa wakikimbia kuyaokoa maisha yao. Baadhi yao walipigwa na kuuawa kwa mishale, huku wengine wakidungwa hadi kufa. Wengine walifukuzwa na kuumwa na wanyama hadi wakafa. Hatimaye, hakuna aliyeweza kutoroka, na kila mmoja wao alikufa. Wale waliokufa kisha walifufuka ili kupokea adhabu iliyofuata.

Niliona mahali pengine palipokuwa pa kuwaadhibu wale ambao walikuwa wamedanganya au waliokuwa na nia mbaya kwa wengine, ambao walikuwa wamewanyanyasa watu wengine, au ambao walikuwa na njama au kuwaonea wivu wengine. Kulikuwa na daraja la kuning’inia lenye kupambwa kwa mbao na kamba zenye miiba pande zote mbili. Kushikilia zile kamba zenye miiba kuliwatoa damu, lakini wangeanguka bila kujishikilia pale, na kulikuwa na ziwa la moto chini. Hata kama hawangeanguka, ilikiwa lazima wapitie kwenye mashine ya kusaga nyama na kusagwa, kisha waishie kwenye ziwa la moto.

Baadhi ya watu walikuwa wamejali sana kuhusu walivyoonekana, wakipoteza muda wao kujaribu kuvaa vizuri, lakini hawakumwamini Mungu hata kidogo, na hata walikuwa wamemhukumu na kumkufuru. Nyuso zao zililiwa kidogo kidogo na wadudu. Kando na hao, pia kulikuwa na watu walioadhibiwa kwa kuwalaani wengine, kuiba vitu, na kadhalika. Kulingana na dhambi walizotenda, watu waliadhibiwa mara kwa mara kwa njia moja kabla ya kusonga kwaaina nyingine ya adhabu. Kuona tukio hili kuliniacha mwili mzima ukitetemeka kwa hofu. Kwa kweli kuadhibiwa kwa njia hiyo litakuwa jambo baya kabisa! Nilijutia dhambi nilizotenda, lakini sikujua nimlilie nani, ni nani angeweza kuniokoa. Wakati huo, nilikariri sutra nikiwa nimepigwa na butwaa, lakini hakukuwa na jibu, na woga wangu haukupungua pia. Ghafla nilikumbuka kwamba nilimwamini Mungu mmoja wa kweli—Mwenyezi Mungu. Kitu ambacho Mwenyezi Mungu alisema kilinijia akilini. “Katika maisha yako ya kila siku, bila kujali magumu yoyote unayokumbana nayo, lazima uje mbele za Mungu; jambo la kwanza unalopaswa kufanya ni kupiga magoti mbele ya Mungu katika maombi, hili ndilo jambo muhimu zaidi” (Neno, Vol. 3. Majadiliano ya Kristo wa Siku za Mwisho. Katika Kumwamini Mungu, Kupata Ukweli Ndilo Jambo Muhimu Zaidi). Nilijua kwamba Mungu anatawala juu ya kila kitu, na kile nilichokuwa nikikabiliwa nacho kilikuwa kikitokea kwa idhini Yake, kwa hiyo nilipaswa kumwita. Niliwaza kuhusu dhambi zangu mbalimbali. Nilikuwa mzembe katika kushughulika na Mungu na nilimpuuzilia. Niliitenda imani yangu na kuhudhuria mikutano nilipokuwa nikihisi vizuri, lakini nilikosa kuhudhuria mikutano wakati sikuhisi vizuri. Nilikuwa Mkristo, lakini sikuwa na imani ya kweli kwa Mungu. Nilikuwa mwenye kutekeleza wajibu tu na nilikuwa mdanganyifu Kwake. Nilifurahi kuutumia muda wangu kujifurahisha, lakini sikutumia muda wowote kumwabudu Mungu. Nilijuta sana nilipofikiria hayo yote na nikamwomba Mungu moyoni mwangu, “Mungu Mwenyezi, nimetenda dhambi nyingi. Nimekuwa nisiyejali na mwenye kukupuuza, nikistarehe katika furaha ya kutenda dhambi na kutotekeleza wajibu wangu vizuri. Sasa ninaogopa sana na nimejaa majuto. Sitaki kuja hapa niadhibiwe kwa ajili ya dhambi hizo. Niko tayari kutubu—tafadhali nipe nafasi ya kufanya hivyo. Ninataka kuitii mipango Yako na kufanya kila kitu kulingana na mapenzi Yako.” Niliomba na kuungama kwa njia hii tena na tena, nikitubu kwa Mungu kwa ajili ya dhambi nilizokuwa nimetenda, moja baada ya nyingine. Nilitulia taratibu na sikuwa na woga sana tena. Baadaye, nilihisi kama kwamba kulikuwa na sauti iliyokuwa ikiliita jina langu. Kisha nikaona mwali wa mwanga, na sauti ikatoka kwenye mwanga huo na kuniambia, “Dani, je, umetubu? Umetenda dhambi nyingi. Unahitaji kumtegemea Mungu na uache kutenda dhambi hizi—hupaswi kusubiri hadi adhabu ifikapo ndipo utubu. Yaweke maneno ya Mungu ndani ya moyo wako na uufuatilie ukweli. Kile unachoelewa na kuweka katika vitendo lazima kiwe sahihi. Hii ndiyo nafasi yako ya mwisho, na wakati ujao hutapata wokovu tena. Ukiwa hai, fanya bidii kutekeleza wajibu wako vizuri na kuingia katika ufalme wa Mungu. Usirudie dhambi zako au makosa yako, na usifanye mambo ambayo utajutia. Kwa kuwa hujakamilisha wajibu wako, hutakufa. Unakwenda kuwaokoa wale walioanguka katika maafa.”

Sauti hiyo haikuwa ya mtu yeyote niliyemfahamu. Ilionekana kuzungumza kwa sauti ya upepo. Haikusikika wazi wazi kabisa, lakini niliweza kuielewa. Ingawa maneno hayo yalikuwa makali, yalikuwa ya kusihi na yalinifanya nihisi amani. Yalikuwa ya dhati, na yenye hisia ya usalama. Nilihisi furaha ambayo sikuwa nimewahi kuhisi hapo awali. Nilijua kwamba Mungu alikuwa akiniokoa, akinipa nafasi nyingine maishani. Taratibu, nilianza kupata fahamu baada ya kuisikia sauti hii.

Baada ya kuamka, nilikuwa nikitetemeka, nikiwa bado mwenye hofu sana. Nilihisi vibaya na kujuta sana kwa kutenda dhambi nyingi sana. Nilijua kwamba hii ilikuwa onyo kwangu kutoka kwa Mungu. Kila kitu ambacho Mungu alisema kilikuwa kweli. Ilinibidi niamini kile Alichosema na nimsikilize. Singeweza kuendelea kumpuuza na kuwa mzembe. Mungu alikuwa akinipa nafasi ambayo singeweza kuipoteza tena. Nilimwambia kakangu mdogo, “Nataka kuzungumza na Dada Summer.” Dada Summer alikuwa mnyunyizaji katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, ambaye tulikusanyika pamoja mtandaoni sana. Dada Summer alinitumia baadhi ya maneno ya Mungu baada ya kujua kuhusu hali yangu. Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu anawajibika kwa kila uhai wa binadamu na anawajibika hadi mwisho. Mungu Anawakimu, hata kama umeugua kutokana na mazingira yaliyoharibiwa na Shetani, au kuathiriwa na uchafuzi au kupata madhara mengine, haijalishi; Mungu Anakukimu na Atakuacha uendelee kuishi. Mnapaswa kuwa na imani katika hili. Mungu hatamkubali mwanadamu afe kwa urahisi(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII). “Kutoka ulipozaliwa hadi sasa, Mungu amefanya kazi nyingi sana kwako, lakini Hakupi maelezo moja baada ya nyingine ya kila kitu Amefanya. Mungu hakukuruhusu kujua, na Hakukwambia. Hata hivyo, kwa mwanadamu, kila kitu anachofanya Mungu ni muhimu. Kwa Mungu, ni kitu ambacho lazima Afanye. Katika moyo wake kuna kitu muhimu Anapaswa kufanya ambacho kinazidi yoyote ya mambo haya. Yaani, kutoka alipozaliwa mwanadamu hadi sasa, Mungu lazima ahakikishe usalama wao. … Usalama huu unamaanisha humezwi na Shetani. Je, jambo hili ni muhimu? Wewe humezwi na Shetani, kwa hivyo hili linahusisha usalama wako, au la? Hili linahusisha usalama wako binafsi, na hakuwezi kuwa na lolote muhimu zaidi. Baada ya wewe kumezwa na Shetani, nafsi yako wala mwili wako si vya Mungu tena. Mungu hatakuokoa tena. Mungu huacha nafsi kama hiyo na huacha watu kama hao. Kwa hivyo Nasema kitu muhimu sana ambacho Mungu anapaswa kufanya ni kuhakikishia usalama wako, kuhakikisha kwamba hutamezwa na Shetani. Hili ni muhimu kiasi, silo?(Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI).

Kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu kulinifanya nihisi salama, kana kwamba nilikuwa na kitu cha kutegemea. Tukio hili lilinionyesha hata kwa uwazi zaidi, kwamba tangu kuzaliwa hadi sasa, Mungu amekuwa akituongoza, akitulinda na kutuchunga kila wakati. Ninapaswa kuja mbele za Mungu, nitende wajibu wangu, na nilipe neema Yake ya ajabu. Nilihitaji kushuhudia kwamba Mungu kweli anatawala juu ya vitu vyote, ukiwemo ulimwengu wa kiroho ambao hauonekani kwa macho yetu. Kuzimu kweli ipo. Sikupitia mateso ya adhabu ya kuzimuni, lakini nilijionea watu wakiadhibiwa kuzimuni. Kuna watu wengi karibu nami wanaofuatilia mitindo ya ulimwengu, wakimfuata Shetani. Hawakuja mbele za Mungu. Nina wasiwasi sana kwa niaba yao, na sitaki watu ninaowajua waende kuzimuni, kuteseka kwa namna hiyo. Waikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho au la, nitatimiza majukumu yangu na kutoa ushuhuda kwao kwamba kuzimuni ipo kwa kweli, na kwamba mamlaka ya Mungu kweli yapo. Ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye awezaye kutuokoa kutoka katika dhiki ya kuzimuni. Ningependa kusoma kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya wale ambao hawajakuja mbele Yake, na kwa wale ambao wamemkubali Mwenyezi Mungu, lakini hawauthamini wokovu Wake.

Mwenyezi Mungu anasema, “Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mabadiliko ya Mwigizaji

Mwenyezi Mungu anasema, “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda...

Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

Xiaoxiao Jijini Xuzhou, Mkoani Jiangsu Kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya kanisa, nilihamishwa mpaka mahali pengine ili kutimiza wajibu...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp