Dhana ya Biblia Kuhusu Dhambi: Je, Wakristo Wanawezaje Kuepuka Dhambi?

23/07/2020

Bwana Yesu alisema, “Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele(Yohana 8:34-35). Maneno ya Bwana yanatuambia kwamba watu wasipojiepusha na utumwa na vipingamizi vya dhambi, na waendelee kutenda dhambi, basi wao ni watumishi wa dhambi na hawatawahi kuingia katika ufalme wa Mungu. Ndugu wengi waaminifu watakapokisoma kifungu hiki cha maandiko, watafikiria jinsi wanavyofanya dhambi mchana na kukiri usiku, na kwa hivyo watahisi wasiwasi kuwa wanaishi katika dhambi na hawawezi kuingia katika ufalme wa Mungu, na watahisi maumivu makali mioyoni mwao. Wanaamini katika Bwana, kwa hivyo ni kwa nini hawawezi kujiepusha na dhambi? Je, tunaweza kujiepusha vipi hasa na vipingamizi vya dhambi? Sasa tutashiriki juu ya kipengele hiki cha ukweli.

Dhana ya Biblia Kuhusu Dhambi: Je, Wakristo Wanawezaje Kuepuka Dhambi?

Kwa Nini Hatuwezi Kuepuka Dhambi Katika Imani Yetu Katika Bwana?

Inapofikia suala la ni kwa nini tunaamini katika Bwana lakini hatuwezi kujiepusha na dhambi, hebu kwanza tusome kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu …(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)). Maneno ya Mungu yanatuonyesha kuwa ingawa tumepitia ukombozi wa Bwana Yesu na dhambi zetu zimesamehewa, na ingawa, baada ya kutenda dhambi, tunaomba, tunakiri na kutubu kwa Bwana na Bwana hatuoni tena kama wenye dhambi, asili zetu zenye dhambi zinaendelea kuwepo; bado tuna uwezekano wa kutenda dhambi mara nyingi, kufunua tabia zetu potovu, na kuishi katika dhambi mchana na kukiri usiku. Kwa mfano, watu wengine wanaposema au kufanya kitu ambacho kinaumiza masilahi yetu, tunawachukia; tunajua vyema kuwa Mungu anapenda wale walio waaminifu, lakini mara nyingi sisi huzungumza uwongo na kudanganya kwa ajili ya maslahi yetu; tunapobarikiwa na Mungu, tunamshukuru Mungu siku zote; tunapokumbwa na maafa, tunaanza kunung'unika kuhusu Mungu, na labda hata tunaweza kumkosoa Mungu, tukimtusi waziwazi. Na kwa hivyo inaweza kuonekana kuwa ingawa dhambi zetu zimesamehewa, tabia zetu potovu zilizomo ndani yetu hazijatakaswa, kwa maana aliyoifanya Bwana Yesu ilikuwa kazi ya kusulubiwa na ya ukombozi wa wanadamu, si kazi ya kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kabisa. Tumepotoshwa na Shetani kwa maelfu ya miaka na tabia zetu za kishetani zimekita mizizi ndani ya asili zetu. Kiburi, majivuno, ubinafsi, aibu, usaliti, ujanja, uwongo, ulaghai, mabishano ya wivu, nia mbaya, ubaya, kuchukia ukweli, na uadui kwa Mungu—mambo haya yote ni thabiti zaidi kuliko dhambi na yanaweza kuwafanya watu wampinge Mungu moja kwa moja. Vyanzo hivi vikikosa kushughulikiwa, basi tutatenda dhambi leo na pia tutatenda dhambi kesho, tukishindwa kabisa kujiepusha na dhambi na vizuizi vya dhambi.

Dhana ya Biblia Kuhusu Dhambi: Je, Wakristo Wanawezaje Kuepuka Dhambi?

Je, Wakristo Wanawezaje Kujiepusha na Dhambi?

Kwa hivyo tunawezaje hasa kujiepusha kikamilifu na vipingamizi vya dhambi? Bwana Yesu alitabiri, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:47-48).

Maneno ya Mungu pia yanasema, “Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Maneno ya Mungu yanatuambia kuwa Mungu wa siku za mwisho atarudi kunena maneno Yake na kutekeleza kazi ya hukumu, Akitatua kabisa tabia potovu za mwanadamu na kumwokoa kutoka dhambini. Leo, Bwana Yesu amerejea katika mwili kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Juu ya msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi, Mwenyezi Mungu ametekeleza hatua moja ya kazi Yake, ile ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Ameonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu, Akitatua chanzo cha asili zetu zenye dhambi na kutuwezesha kuelewa ukweli, kujiepusha na dhambi, kuacha kutenda dhambi na kumpinga Mungu, na kuwa watu wanaomtii na kumcha Mungu na ni wakati huo ndipo tunapatwa na Mungu kwa kweli. Ni wakati tu ambapo tutakubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya kuhukumu ya siku za mwisho ndipo tutakapokuwa na nafasi ya kujiepusha na tabia zetu potovu na kutakaswa.

Je, Mungu Humtakasa na Kumhukumu Mwanadamu Vipi?

Kwa hivyo Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anatekelezaje hasa kazi ya hukumu ili kutakasa na kumwokoa mwanadamu, Akimwezesha mwanadamu kuondokana na dhambi? Hebu tusome kifungu kingine cha maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Kazi ya hukumu inapotajwa, watu wengine wanaweza kufikiri: Je, si hukumu ni laana ya Mungu? Je, mtu anawezaje hata hivyo kuokolewa na Mungu? Tuna mawazo kama haya kwa sababu hatujui kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Maneno ya Mungu yanatuambia kwamba kazi ya hukumu inayofanywa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho hasa ni kuonyeshwa kwa ukweli ili kumhukumu na kumtakasa mwanadamu, na hivyo kutufanya tutambue tabia zetu potovu kutokana na ufunuo wa maneno ya Mungu na kuona ukweli halisi wa upotovu wetu mikononi mwa Shetani. Maneno ya Mungu ni kama upanga ukatao kuwili; tunaposoma maneno ya Mungu, ni kana kwamba Anatuhukumu uso na uso, Akitufanya tutambue tabia zetu za kishetani, tabia ambazo ni zenye kiburi, majivuno, ubinafsi, aibu, usaliti, ujanja, ulafi na mbovu. Kwa mfano. tunapoanza kumwamini Bwana, tunafurahia neema ya Bwana, kuna amani na furaha mioyoni mwetu, na hasa baada ya kuona baraka na ahadi tulizopewa na Bwana, tunakuwa na shauku kubwa zaidi ya kujitumia kwa ajili Yake. Kamwe hatukosi kuhudhuria kusanyiko au kusoma Maandiko; sisi mara nyingi huwasaidia ndugu ambao ni wanyonge, tukieneza injili kila mahali tunapokwenda, tukivumilia katika kujitolea kwetu na wema wetu, tukitumaini kuwa tukijitumia kwa njia hii, Bwana atahakikisha kila kitu kitakwenda kwa utaratibu na vizuri kwetu, na kwamba baadaye tutaweza kuingia katika ufalme wa mbinguni na kupata uzima wa milele. Lakini msiba unapotupata, Bwana asipotutazama na kutulinda, tunajutia jinsi tulivyojitumia kwa ajili ya Bwana hapo awali, na hata tunaanza kumlaumu Mungu mioyoni mwetu. Tunapokubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, tunaona kwamba Anasema, “Hivi sasa watu wengi wako katika aina hii ya hali: ‘Ili kupata baraka ni lazima nijitumie kwa ajili ya Mungu na kulipa gharama kwa ajili Yake. Ili kupata baraka ni lazima niache kila kitu kwa ajili ya Mungu; lazima nikamilishe kile ambacho ameniaminia na kutekeleza wajibu wangu vizuri.’ Hili linatawaliwa na nia ya kubarikiwa; ni kutumika kwa kusudi la kupata thawabu za Mungu, kwa ajili ya kupata taji …(“Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila hasira iliyofichwa na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu).

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanafichua moja kwa moja motisha na taswira zisizo sahihi za imani yetu katika Mungu. Ni kupitia tu kutafakari kujihusu sisi wenyewe ndiyo tunagundua kuwa hatufanyi kazi kwa bidii kutokana na upendo wetu kwa Mungu na kwa sababu tunataka kumridhisha Mungu; badala yake, tunatarajia kujitumia ili kupata baraka na ahadi za Mungu—tabia na matendo yetu mazuri ni ya kufanikisha malengo yetu tu. Nyakati kama hizi, tunaona jinsi asili zetu zilivyo za ubinafsi na za aibu. Tunaishi kwa kufuata sheria ya kishetani ya, “Mbingu huwaangamiza wale ambao hawajiwakilishI”; kila kitu tunachofanya ni kwa manufaa yetu, na hata tunapojitumia kidogo katika imani yetu katika Mungu, hii pia ni ili kupata faida na baraka kutoka kwa Mungu. Tunataka kubadilisha matumizi kidogo na baraka nyingi, na tunatafuta kupata mara mia katika maisha haya na kupata uzima wa milele katika ulimwengu ujao. Hatujitumii hata kidogo ili kutekeleza wajibu wetu kama viumbe na kulipa upendo wa Mungu. Nia na tamaa zetu zinapokosa kutimizwa, tunakuwa hasi, tunalalamika, tunaasi na kumpinga Mungu. Tunapoona jinsi tulivyo wachafu na wapotovu, kwamba hatuna dhamiri na mantiki na hatufai kabisa kupokea thawabu na baraka za Mungu, mioyoni mwetu tunajuta na kujilaumu. Tunajidharau, na tunalazimika kuanguka mbele za Mungu kukiri dhambi zetu, tukitarajia kuanza upya, tukiwa tayari kujitumia kwa ajili ya Mungu, na hatuombi tena chochote kama malipo. Kwa kupitia hukumu na kuadibiwa na Mungu, tunakuja kutambua tabia zetu za kishetani, na tunaona kuwa Mungu hudharau dhambi za mwanadamu. Tunaona kwamba kila mahali kunapokuwa na uchafu, kuna hukumu ya Mungu, na tunakuja kujua kiini kitakatifu cha Mungu na tabia Yake ya haki na isiyodhurika, na kwa hivyo moyo wa kumcha Mungu unazaliwa ndani yetu. Chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, tunakuja kuelewa mapenzi na matakwa ya Mungu polepole, tunashikilia nafasi ya kiumbe aliyeumbwa kutekeleza wajibu kidogo wa mwanadamu, kuna mapatano machache zaidi ya kibiashara katika uhusiano wetu na Mungu, uhusiano wetu na Yeye unakuwa wa karibu zaidi, tabia zetu potovu zinapitia mabadiliko kiasi, na mwishowe tunaishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu wa kweli.

Kwamba tumeweza kubadilika kama tulivyobadilika leo ni matokeo yaliyofanikishwa ndani yetu na kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu. Wote ambao wamepitia hukumu na kuadibiwa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao kwa kweli wanapenda ukweli, baada ya miaka kadhaa wanaona waziwazi badiliko na kuvuna mavuno; mioyoni mwao, wanaweza kuhisi jinsi upendo wa Mungu kwa mwanadamu ulivyo mkuu na jinsi wokovu Wake kwa mwanadamu ulivyo mkuu, na wanatambua kwa kina jinsi kazi ya Mungu ilivyo halisi. Wanafahamu kuwa ni hukumu na kuadibu kwa Mungu pekee ndivyo wokovu wa kweli, na kwamba ni kwa kukubali tu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na kupitia hukumu na kuadibiwa Mungu, ndiyo wanaweza kutakaswa na kubadilishwa—hii ndio njia pekee ambayo tunaweza kujiepusha na dhambi.

Ukumbusho wa Mhariri: Je, ushirika huu umetatua kuchanganyikiwa kwako? Je, umepata njia ya kujiepusha na dhambi katika ushirika huu? Ikiwa unahisi kuwa ushirika huu umekusaidia, angalia kwa makini mtandao huu na tutaendelea kuusasisha na maudhui mapya. Ikiwa mtu unayemjua amechanganyikiwa tu kama wewe, tafadhali shiriki makala haya naye. Ikiwa una maswali au matatizo yoyote, jihisi huru kuwasiliana nasi wakati wowote, na tutaweza kuyachunguza na kutafuta pamoja!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Ukweli Kuhusu Kunyakuliwa

Li Huan Kama tu ndugu Wakristo wengine wengi, natamani sana kuja kwa mara ya pili kwa Bwana Yesu. Tunafuata fungu lifuatalo kutoka kwa...

Ishara za Nyakati za Mwisho: Mwezi Mkuu wa Damu Kutokea tena mnamo 2021

Katika miaka ya hivi karibuni, katika upeo wa mbingu “mwezi wa damu” umeonekana mara kwa mara. Majanga mbalimbali kama vile magonjwa ya mlipuko, tetemeko ya ardhi, na njaa zinazidi kuwa mbaya. Unabii wa Biblia kuhusu siku za mwisho tayari umetimia, na siku kuu na ya kutisha ya Yehova iko karibu. Majanga makubwa sasa iko juu yetu, kwa hivyo tunapaswaje kukaribisha kurudi kwa Bwana? Nakala hii ina jibu.

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp