Je, Maafa Yatakapofika, Utakuwa Umetimiza Toba ya Kweli?

23/07/2020

Na Xiaoyu, Amerika

Mnamo 2020, virusi vya COVID-19 vilienea ulimwenguni, vikisababisha ulimwengu kuwa na hofu. Kilichoshangaza pia ni idadi kubwa ya nzige waliojaa barani Afrika. Kuja kwa tauni na njaa, wengi wa wale wanaomwamini Bwana wameanza kuhisi kwamba siku ya kuwasili kwa Bwana imekaribia, na kwamba ufalme wa Mungu uko karibu kuja. Bwana Yesu aslisema wakati mmoja, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu(Mathayo 4:17). Bwana anamsihi kila mmoja wetu afanye hivyo. Tukitubu kwa kweli pekee ndiyo tutalindwa na Mungu na kuletwa katika ufalme wa mbinguni kabla ya dhiki kuu. Kwa hivyo toba ya kweli ni nini hasa, na tunawezaje kuifanikisha?

Tubuni kwa Kuwa Ufalme wa Mbinguni U Karibu: Jinsi ya Kutimiza Toba ya Kweli

Je, Mwenendo Mzuri Ni Ishara ya Toba ya Kweli?

Toba inapotajwa, waumini wengi wa Bwana watasema, “Sasa kwa kuwa tunamwamini Bwana, hatutusiani au kupigana, tunawavumilia na kuwastahimili wengine, sisi huomba na kukiri kwa Bwana mara nyingi, tunafanya kazi na kujitumia kwa ajili ya Bwana, na hata hatulikani jina la Bwana baada ya kuwekwa gerezani. Mienendo hii mizuri inathibitisha kwamba kweli tumetubu. Bwana atakaporudi, tutaingia katika ufalme wa mbinguni pamoja na Yeye.” Baada ya kuanza kumwamini Bwana, tuliacha tabia zetu mbaya; tulikuwa wanyenyekevu, wavumilivu, tuliwasaidia wengine, na tukawa na uwezo wa kuviacha vitu na kujitumia kwa ajili ya kueneza injili na kumshuhudia Bwana. Kwa kweli kulikuwa na mabadiliko kadhaa katika mienendo yetu, lakini bila shaka hatujaondokana na pingu za dhambi, na bado mara nyingi tunaishi dhambini, pasipo kuweza kutoroka. Kwa mfano, mtu anaposema jambo linalotuumiza ambalo haliingilii masilahi yetu ya msingi, tunaweza kuwa na uvumilivu, na hatutamshambulia kwa ajili hilo. Lakini mtu anaposema jambo linaloumiza sifa na hadhi yetu na linalotufedhehesha, ingawa huenda tusisiseme lolote la kuwakosoa, kuna maudhi na chuki kuhusiana nao mioyoni mwetu, na tunaweza hata kufikiria kuhusu kulipiza kisasi. Katika mambo mengi, ingawa tunaweza kuonekana hatutendi uovu wowote mkubwa, mioyo yetu mara nyingi hufichua mawazo mabaya. Wakati mwingine, tunaweza kuwa na uwezo wa uvumilivu na kujidhibiti kwa muda, lakini tunapozidiwa, bado tuna uwezekano wa kutenda maovu. Mambo kama hayo yanapofunuliwa na kudhihirishwa ndani yetu, na bado hatujaepuka pingu za dhambi, inaweza kusemekana kwamba tumetubu kwa kweli?

Hebu tusome kifungu cha maneno ya Mungu, “Mabadiliko katika tabia tu hayawezi kudumu. Kama hakuna mabadiliko katika tabia ya maisha ya watu, basi siku moja upande wao wa uovu utajionyesha. Kwa sababu kiini cha mabadiliko katika mienendo yao ni bidii, pamoja na kazi ya Roho Mtakatifu wakati huo, ni rahisi sana kwao kuwa na bidii, ama kuonyesha ukarimu kwa muda. Kama wasioamini wanavyosema, ‘kufanya tendo moja zuri ni rahisi, kilicho kigumu ni kufanya matendo mazuri maishani.’ Watu hawana uwezo wa kufanya matendo mazuri katika maisha yao yote. Mienendo yao inaongozwa na maisha hayo; maisha yao yalivyo, ndivyo mwenendo wao ulivyo, na kile tu kinachofichuliwa kwa asili kinawakilisha maisha hayo, na asili ya mtu. Vitu vilivyo vya bandia haviwezi kudumu. Mungu anapofanya kazi ili kumwokoa mwanadamu, si kwa ajili ya kumpamba mwanadamu kwa mwenendo mzuri—kazi ya Mungu ni kwa ajili ya kubadilisha tabia za watu, kuwafanya wazaliwe na kuwa watu wapya. … Kuwa na tabia nzuri si sawa na kumtii Mungu, hasa si sawa na kulingana na Kristo. Mabadiliko katika tabia yanategemea mafundisho, na kuzaliwa na juhudi—hayategemei maarifa ya kweli kumhusu Mungu, ama juu ya ukweli, hasa hayategemei uongozi wa Roho Mtakatifu. Ingawa kuna nyakati ambapo baadhi ya yale watu wanayofanya yanaongozwa na Roho Mtakatifu, haya si maonyesho ya maisha, sembuse kuwa sawa na kumjua Mungu; haijalishi mienendo ya mtu ni mizuri kiasi gani, haithibitishi kwamba anamtii Mungu, ama kwamba anauweka ukweli katika matendo. Mabadiliko ya tabia ni udanganyifu wa muda, ni udhihirisho wa bidii, nayo si maonyesho ya maisha hayo(“Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo).

Maneno ya Mungu yanatuonyesha kwamba ingawa mienendo yetu iliboreka baada ya kuanza kumwamini Mungu, hii haimaanishi kumekuwa na mabadiliko katika tabia yetu ya maisha. Mienendo mingi mizuri ni matokeo ya bidii, ni mienendo iliyotokana na mafundisho na sheria, la sivyo ni desturi inayotokana na kuguswa na Roho Mtakatifu. Sio kwa sababu tunaelewa ukweli, sio kwa sababu tuna maarifa juu ya Mungu, na si desturi ambayo hutokana kwa kawaida na hamu yetu ya kumridhisha na kumpenda Mungu. Tumepotoshwa na Shetani kwa maelfu ya miaka, tumejawa na kila aina ya tabia potovu ya kishetani—kiburi, majivuno, ubinafsi, aibu, usaliti na ujanja. Tabia hizi zikiachwa bila kutatuliwa, basi hata ingawa tunaweza kufuata sheria fulani na tunaweza kuonekana kuwa wacha Mungu kwa nje, hii haidumu kwa muda mrefu, na tunapokutana na jambo baya, hatuwezi kujizuia kutenda dhambi. Kwa mfano, huku tukidhibitiwa na asili yetu ya kishetani ya kiburi na majivuno, sisi daima hujaribu kuwafanya wengine watuheshimu, na wengine wasipofanya tunachosema, tunaghadhabika na kuanza kuwakaripia. Huku tukiongozwa na asili yetu ya ubinafsi, kila kitu tunachofanya huzingatia masilahi yetu wenyewe; kila kitu nyumbani kinapokwenda kwa utaratibu, tuko tayari kuachana na mambo na kujitumia kwa ajili ya Mungu, na tunaweza kuvumilia shida yoyote. Lakini msiba unapokuja, tunamlaumu Mungu kwa kukosa kutulinda. Tunaweza hata kuanza kujutia yale ambayo tumeachana nayo, na kukusudia kumsaliti Mungu. Wakati mwingine tunaangalia kwa makini matendo ya kina ndugu kanisani ambao bila shaka wamekiuka mafundisho ya Mungu, na ambao hata wanadhuru masilahi ya kanisa, na tunapaswa kuwaambia jambo. Lakini, tukiwa tumechochewa na falsafa za kishetani za kuishi kama vile, “Kuwa mnyamavu kwa dosari za rafiki wa maana hufanya urafiki kuwa wa muda mrefu na mzuri” na “Taabu ndogo zaidi, bora zaidi,” tunanyamaza, tukipendelea kutoa masilahi ya kanisa kama kafara ili kudumisha uhusiano wetu nao. Orodha ya mambo hayo yaendelea. Hii inaonyesha kuwa tabia zetu potovu zisipotatuliwa, hatuwezi kutenda ukweli au kumtii Mungu, na hata tunaweza kumpinga. Chukua Mafarisayo wa miaka elfu mbili iliyopita, kwa mfano. Kwa nje, hawakuonekana kutenda uovu wowote. Walisafiri kotekote wakieneza injili, mara nyingi waliwafasilia watu maandiko, na kuwafundisha watu kutii sheria. Mienendo ya mingi ilikuwa mizuri, lakini Bwana Yesu alipoonekana na kuanza kazi Yake, kwa sababu Alionekana wa kawaida sana kwa nje na hakuitwa Masihi, na kwa sababu kila kitu kumhusu kilitofautiana na mawazo yao, tabia zao za kishetani za kiburi na majivuno ziliwekwa wazi. Walimlaani na kumkufuru Bwana Yesu waziwazi, hawakujali kama ujumbe ulionenwa na Bwana Yesu ulikuwa ukweli, walimpuuza bila kujali Alifanya ishara na miujiza mingapi, na mwishowe, walifanya njama na mamlaka ya Kirumi kumsulubisha Bwana Yesu.

Yaliyo hapo juu yanaonyesha kuwa ingawa kunaweza kuwa na mabadiliko katika mienendo yetu ya nje, ikiwa hakuna mabadiliko katika tabia zetu za ndani za maisha, bado tutatawaliwa na tabia zetu potovu za kishetani na tutakuwa na uwezekano wa kutenda dhambi na kumpinga Mungu wakati wowote. Watu kama hao pia hawajatubu kwa kweli na kimsingi hawana sifa ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kama tu Biblia inavyosema, “Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele(Yohana 8:34-35).

Toba ya Kweli Ni Nini?

Kwa hivyo toba ya kweli ni nini? Biblia inasema, “Wamebarikiwa wale wanaofanya amri zake, ili wawe na haki ya mti wa uzima, na waweze kuingia mjini humo kupitia malango yake(Ufunuo 22:14). “Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu(Walawi 11:45). Mungu ni mtakatifu. Anadharau dhambi za mwanadamu, na kwa hivyo kipimo cha toba ya kweli ni wakati ambapo tabia mbalimbali za kishetani zilizo ndani ya watu—kiburi, majivuno, ubinafsi, aibu, usaliti, na ujanja—zimesafishwa na kubadilishwa, wanapoweka maneno ya Mungu kwenye vitendo bila kujali mazingira, hawatendi dhambi tena au kumpinga Mungu, lakini wanamtii na kumcha Mungu kwa kweli, na wakati ambapo wamepatwa kabisa na Mungu. Ni watu kama hao pekee ndio waliotubu kwa kweli.

Kwa Nini Hatujatimiza Toba ya Kweli Katika Imani Yetu Katika Bwana

Watu wengine wanaweza kuuliza, “Kwa nini tumekubali ukombozi wa Bwana na dhambi zetu zimesamehewa, lakini hatuwezi kutimiza toba ya kweli?” Hii hasa ni kwa sababu katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi, ambayo haikuwa kazi ya kubadilisha tabia potovu za watu. Hebu tusome kifungu kingine cha maneno ya Mungu, “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji). Hii inatuarifu kuwa katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alitikeleza tu kazi ya ukombozi wa wanadamu, ambayo matokeo yake yalipaswa kuwafanya watu wakiri na kutubu. Kama sehemu ya kazi ya ukombozi, Bwana Yesu alizungumza juu ya njia ya toba, Aliwafundisha watu jinsi ya kukiri na kutubu dhambi zao, kuubeba msalaba na kumfuata Bwana. Kwa hivyo, lazima pia wawapende wengine kama wanavyojipenda, lazima wawe wanyenyekevu, wenye subira, na wavumilivu, na wawasamehe watu mara sabini mara saba, na kadhalika. Haya yote yalikuwa mahitaji ya mwanadamu kulingana na kimo cha watu wakati huo; watu walipotenda dhambi, walikuja mbele za Bwana Yesu kukiri dhambi zao na kutubu, dhambi zao zilisamehewa, na walikuwa na haki ya kuja mbele za Mungu na kuendelea kumwabudu Mungu. Yote yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu yalikuwa ukweli ambao uliweza kueleweka na watu wa wakati huo. Lakini hii haikujumuisha kubadilisha tabia za watu, na kwa hivyo bila kujali tunasoma Biblia kwa kiasi gani, jinsi tunavyokiri dhambi zetu na kutubu, au jinsi tunavyojishinda, tunasalia bila uwezo wa kuepuka dhambi na kutimiza toba ya kweli.

Jinsi ya Kutimiza Toba ya Kweli

Kwa hivyo, tunaweza kutimiza toba ya kweli vipi? Bwana Yesu alitabiri, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). “Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:48). “Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli(Yohana 17:17). Maneno haya yanatuonyesha kuwa kwa sababu vimo vya watu wa wakati huo vilikuwa vya chini sana, wakati wa Enzi ya Neema Bwana Yesu hakuonyesha ukweli mwingi sana au kutupa njia ya kutatua asili zetu za kishetani. Kwa hivyo Bwana alitabiri kwamba Angerudi, kwamba Angeonyesha ukweli mwingi zaidi na muhimu zaidi, na kwamba Angefanya kazi ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu, na hivyo kutufanya tuondokane na pingu za dhambi, na tutakaswe na kubadilishwa, na ni kwa kukubali kazi ya hukumu na utakaso wakati wa kurudi kwa Bwana tu ndiyo tunaweza kutimiza toba ya kweli.

Leo, Bwana Yesu amerudi: Yeye ndiye Mwenyezi Mungu mwenye mwili. Juu ya msingi wa kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi, Mwenyezi Mungu amefanya kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu, Ameonyesha ukweli wote ulio muhimu kwa wokovu wa wanadamu, na Amekuja kuwahukumu, kuwatakasa, na kuwakamilisha wale wanaokubali wokovu Wake wa siku za mwisho. Mwenyezi Mungu anasema, “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli).

Mwenyezi Mungu anapoonyesha ukweli na kutekeleza kazi ya kuhukumu na kumtakasa mwanadamu katika siku za mwisho, Yeye hatuambii tu njia kadhaa za kutubu, lakini Anaonyesha maneno ya kuhukumu, Anafichua asili na viini vyetu ambavyo humwasi na kumpinga Mungu, na ukweli wa upotovu wetu; Anatupa ukweli mbalimbali, kama vile jinsi ya kuwa mwaminifu, jinsi ya kumtii Mungu, jinsi ya kumpenda Mungu, na kadhalika, na hivyo kutupa njia ya kutenda katika vitu vyote vinavyotupata. Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu, tunakuja kuona polepole jinsi ambavyo tumepotoshwa sana na Shetani, na kwamba asili na viini vyetu vimejaa tabia za kishetani za ufidhuli na kujidai, ubinafsi na aibu, ulaghai na ujanja. Tunapoishi kulingana na mambo haya, hatudhihirishi ubinadamu wowote, tunawachukiza wengine na, zaidi ya hayo, tunamkirihi na kumchukiza Mungu. Katikati ya maneno ya Mungu ya hukumu, tunaona kuwa hatuna aibu na tu waovu, hatufai kuishi mbele za Mungu, na wakati huo tu ndipo tunaanza kuchukia dhambi zetu na kutamani kutubu. Wakati huo huo, tunakuja kujua tabia ya Mungu ya haki ambayo haivumilii dhambi na kwamba tusipoweka ukweli kwenye vitendo, basi bila shaka tutachukiwa na kukataliwa na Mungu. Ni wakati huo tu ndipo uchaji Mungu unazaliwa ndani yetu, tunaanza kuukana mwili na kuweka ukweli kwenye vitendo, tunakuwa na uhalisi wa utiifu kwa Mungu polepole, na hatuasi na kumpinga Mungu tena.

Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, tunaepuka dhambi kabisa, hatuzuiwi tena na asili zetu za kishetani, na tuko huru kuweka maneno ya Mungu kwenye vitendo na kumtii na kumwabudu Mungu. Ni wakati huo tu ndipo tunaweza kusemekana kuwa tumetubu na kubadilika kwa kweli, na wakati huo tu ndipo tunastahili kuingia katika ufalme wa mbinguni. Bila shaka, kukubali kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho ndiyo njia pekee ya kutimiza toba na mabadiliko ya kweli. Kwa wakati huu, ninaamini kuwa sasa umeanza kuona njia ya kutimiza toba ya kweli—kwa hivyo tunapaswa kufanya maamuzi gani sasa?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp