Siri ya Majina ya Mungu
“Ingawa Yehova, Yesu, na Masihi yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria tu enzi tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, nayo hayaniwakilishi katika ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza kwa ufasaha tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tofauti tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Na hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina Langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, wala Masihi, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitatamatisha enzi nzima” (Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wimbo huu wa maneno ya Mungu ulinionyesha kuwa kuna maana katika jina la Mungu katika kila enzi. Jina moja halingeweza kuiwakilisha tabia ya Mungu kikamilifu na kile Alicho. Jina linawakilisha tu tabia Anayoonyesha katika enzi hiyo. Nafsi ya Mungu ni inayojumuisha yote na yenye wingi. Watu hawawezi kumwekea Mungu mipaka au kusema kwamba jina Lake ni lisilobadilika. Muda fulani uliopita, sikuelewa kweli maana ya jina ambalo Mungu huchukua katika kila enzi, kwa hivyo nilikuwa na hakika jina Lake haliwezi kubadilika. Nilishikilia jina la Bwana Yesu na sikumkubali Mwenyezi Mungu. Ilikuwa nusura niipoteze nafasi yangu ya kumkaribisha Bwana.
Bibi yangu alinipeleka kanisani tangu nilipokuwa mdogo. Mchungaji alikuwa akinukuu aya hizi: “Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima” (Waebrania 13:8). “Wala hakuna wokovu kwa mwingine yeyote: kwani hakuna jina lingine chini ya mbingu lililopewa miongoni mwa wanadamu, linalotupasa kuokolewa kulipitia” (Matendo 4:12). Nilikuwa na hakika ya kwamba ni Bwana Yesu tu ndiye aliyekuwa Mungu wa kweli na mradi nilishikilie jina Lake na njia Yake, Atakaporudi, ningechukuliwa mbinguni.
Mnamo mwaka wa 2017, mke wangu alikubali injili ya ufalme ya Mwenyezi Mungu. Na alinitaka nisikie Kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, kwa hivyo alimleta dada mmoja afanye ushirika, nami nikasikiliza. Lakini aliposema Bwana Yesu alikuwa tayari amerudi, kama Mwenyezi Mungu sikutaka kusikia neno lingine. Niligundua kwamba mke wangu alimfuata Mwenyezi Mungu, kwa hivyo nilimzuia. Nilisema “Kuna jina moja tu ambalo kwalo tumeokolewa. Tunahitaji kuwa waaminifu jina la Bwana Yesu. Baada ya miaka yako mingi ya imani, unapaswa kujua vyema.” Kukemea kwake kulikuwa, “Jina la Bwana Yesu lilituokoa, kumaanisha dhambi zetu zilisamehewa, kwa hivyo hatuhukumiwi, lakini bado tunaishi katika hali ya kufanya dhambi na kukiri. Hatujaondokana na dhambi. Bwana Yesu amerudi na kuanzisha Enzi ya Ufalme kwa jina Mwenyezi Mungu. Yeye anafanya kazi ya hukumu. Anaonyesha ukweli ili kufichua asili zetu za kishetani ambazo zinampinga Mungu, anahukumu dhambi za binadamu na kutupa njia ya kutatua asili yetu ya dhambi. Lazima tukubali kazi ya Mwenyezi Mungui ya hukumu ya siku za mwisho, ili tuingie katika ufalme wa Mungu.” Lakini nilikuwa nimejaa maoni na sikuelewa kile alichosema. Nilijua kwamba yeye aliwasikiliza wazazi wake kila wakati, kwa hivyo niliomba msaada wao ili kumzuia. Lakini alisisitiza kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi na hata akatutia moyo tulichunguze hilo.
Nilijaribu kuizuia imani yake katika Mwenyezi Mungu. Nilifanya uchunguzi katika Biblia kila nilipoweza na nilipata mahubiri mtandaoni kutoka kwa wachungaji maarufu ambayo nilikuwa nikipakua na kumchezea. Nilidhani yeye atabadilisha mawazo yake. Lakini kwa kweli alinihubiria badala yake. Hilo lilinikasirisha lakini sikuwa na la kufanya. Sote tuliendelea kutenda imani yetu wenyewe. Kwa hivyo nilihakikisha ninampinga. Alisoma maneno ya Mwenyezi Mungu, mimi nilisoma Biblia. Alicheza nyimbo za kanisa lake na mimi nilimsifu Bwana. Wakati anasikiliza mahubiri ya kanisa lake, mimi niliwasikiliza wachungaji. Tulibishana juu ya Biblia mara nyingi hata ingawa hakulingana na mimi hapo awali katika ufasaha. Kila kitu alichosema sasa kweli kilikuwa chenye umaizi. Maneno yake yalikuwa na uzito na majibu yake yaliniacha nikikosa la kusema na nikiwa nimeshindwa. Sikuweza kumdhalilisha. Nilifikiria kwa kuwa sikulingana naye katika maarifa yangu ya sasa ya Biblia, ilinibidi nisome Biblia ili nishinde.
Siku moja niliona haya katika Kutoka Sura ya 3: “Na Mungu akasema zaidi kwa Musa, Utawaambia hivi wana wa Israeli, Yehova Mungu wa baba zenu, Mungu wake Ibrahimu, Mungu wake Isaka, na Mungu wake Yakobo, amenituma kwa ninyi: jina langu ni hili milele, na hili ni kumbukumbu yangu kwa vizazi vyote” (Kutoka 3:15). Kisha nilijiuliza, kwa kuwa neno la Mungu linasema wazi kwamba Yehova ndilo jina Lake milele, kwa nini aliitwa Yesu katika Enzi ya Neema? Agano la Kale linasema: “Mimi, hata mimi, ni Yehova; na isipokuwa mimi hakuna mwokozi” (Isaya 43:11). Katika Agano Jipya: “Wala hakuna wokovu kwa mwingine yeyote: kwani hakuna jina lingine chini ya mbingu lililopewa miongoni mwa wanadamu, linalotupasa kuokolewa kulipitia” (Matendo 4:12). Je, yote haya yalimaanisha nini? Nilisoma aya hizi tena na tena, lakini ziliniacha tu nikiwa nimechanganyikiwa zaidi. “Je, Bwana Yesu sio Mwokozi wetu? Kwa kuwa Yehova na Yesu ni Mungu mmoja, kwa nini majina yao ni tofauti sana? Je, inaweza kuwa kweli, kwamba jina la Mungu hubadilika, kama vile mke wangu alivyosema?” Niligundua kupitia mijadala yetu kwamba ufahamu wa mke wangu ulikuwa umekua tangu alipoanza kuamini katika Mwenyezi Mungu. Maneno yake yalikuwa yenye uzito. Bila kazi ya Roho Mtakatifu, hakuna mtu ambaye angeweza kuendelea namna hiyo peke yake.” Nilianza kujiuliza, “Je, mimi ndiye nimekosea? Je, Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana aliyerudi? Je, Umeme wa Mashariki ndiyo njia ya kweli? Ikiwa ndilo njia ya kweli, na mimi nimzuiye mke wangu, si nitakuwa nikimpinga Mungu?” Nilikuwa katika hali ngumu sana. Nilitaka kuelekewa hili vizuri lakini sikuwa tayari kuacha kiburi changu.
Nikijaribu kuelewa hili Nilijisajili na nikaanza kutembelea idhaa ya YouTube ya Kanisa Mwenyezi Mungu, nikiangalia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Siku moja, niliona kifungu cha maneno ya Mungu kiitwacho “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”. Mwenyezi Mungu anasema, “‘Yehova’ ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. ‘Yesu’ ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. … Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. ‘Yehova’ linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. ‘Yesu’ linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote” (Neno Laonekana katika Mwili). Niliyafikiria haya akilini mwangu. Maelezo ya Mwenyezi Mungu juu ya umuhimu wa majina ya Yehova na Yesu yapo wazi kabisa. Niliona kwamba jina la Mungu katika kila enzi linawakilisha tu enzi hiyo. “Yehova” lilikuwa jina ambalo Mungu alichukua kwa ajili ya kazi Yake katika Enzi ya Sheria Akionyesha tabia Yake ya huruma na laana. “Yesu” lilikuwa jina la Mungu katika Enzi ya Neema Akionyesha tabia Yake ya upendo. Mwishowe niliona kwamba jina la Mungu si lisilobadilika. Hatua mpya ya kazi ya Mungu pia inamaanisha jina jipya. Kwa hivyo wakati Bwana atakaporudi katika siku za mwisho Atakuwa na jina jipya.
Kisha, nikaona maneno haya ya Mwenyezi Mungu. “Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari” (Neno Laonekana katika Mwili). Maneno haya yana mamlaka. Kila neno, liliitikisa roho yangu. Lazima yalikuwa maneno ya Mungu mwenyewe. Ni nani mwingine angeweza kufichua siri ya majina ya Mungu? Kadiri nilivyoona zaidi, ndivyo nilivyohisi zaidi kwamba ilikuwa sauti ya Mungu. Kisha nikakumbuka Yohana 16:13: “Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo.” Kwa hivyo, Yeye atuambiaye ukweli huu si mwingine bali Mungu? Nilikuwa nimewasikia wachungaji wengi sana wakihubiri lakini hakuna aliyeeleza maana ya majina ya Mungu kama Yehova katika Agano la Kale na Yesu katika Agano Jipya. Ilionekana Mwenyezi Mungu alikuwa kuonekana kwa Bwana Yesu! Nilihisi aibu sana wakati nilifikiria nyakati ambapo nilikuwa nimemkana Mwenyezi Mungu na nikajaribu kumvuta mke wangu pamoja na mimi. Nilijuta kuihukumu kazi ya Mungu bila kuichunguza. Huo ulikuwa ujinga kwa upande wangu. Zamani wakati Mafarisayo waliishutumu kazi ya Bwana Yesu kwa kuzingatia maoni yao na maana halisi ya Maandiko. Si wote waliadhibiwa na Mungu? Kwa hivyo nafaa kujifunza funzo hili na niichunguze kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Sikutaka kuwa Mfarisayo wa siku za sasa.
Baada ya hapo, kila wakati nilipokuwa na muda wa ziada nilisoma maneno ya Mwenyezi Mungu na kutazama sinema za kanisa. Niliguswa hasa na Siri za Uungu na Imani katika Mungu. Uzoefu wa kina ndugu ulikuwa halisi na ushirika wao ulikuwa wazi kama nuru. Nilielewa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Bwana aliyerejea. Kwa hivyo niliamua kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu na nilitaka kumwarifu mke wangu lakini niliona aibu. Siku moja alipokuja nyumbani, nilimuuliza, “Kwa hivyo, mlishiriki nini katika ushirika leo?” Alionekana kushtuka sana na akauliza, “Ungependa ushirika kiasi? Hiyo ndiyo maana unauliza? Naweza kumleta mtu kutoka kanisani azungumze, ungependa hivyo?” Nilifurahi sana aliposema hivyo, lakini bado niliona aibu. Nilisema, “Sawa, ikiwa ungependa hivyo.”
Dada wawili, kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu walikuja, kwa hivyo nilishiriki mkanganyiko wangu. “Nimekuwa nikisoma maneno ya Mwenyezi Mungu kwenye mtandao na sasa naelewa kwamba jina la Mungu hubadilika kadiri enzi inavyobadilika, lakini bado mambo mengine hayaeleweki. Biblia inasema: ‘Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima’ (Waebrania 13:8). ‘Wala hakuna wokovu kwa mwingine yeyote: kwani hakuna jina lingine chini ya mbingu lililopewa miongoni mwa wanadamu, linalotupasa kuokolewa kulipitia’” (Matendo 4:12). “Biblia inasema kwamba, jina la Bwana Yesu haliwezi kubadilika, kwa nini mumwite Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na si Yesu?” Hivyo, walisoma maneno ya Mwenyezi Mungu: “Kiini chake na anachomiliki na kile Anacho na alicho kamwe hakitabadilika. Kazi yake, hata hivyo, daima inaendelea mbele, daima inaenda ndani zaidi, kwa kuwa Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani. Katika kila enzi Mungu huchukua jina jipya, katika kila enzi anafanya kazi mpya, na katika kila enzi Yeye huwaruhusu viumbe Wake kuona mapenzi Yake mapya na tabia Yake mpya.” “Wengine wanasema kwamba jina la Mungu halibadiliki, hivyo, mbona basi jina la Yehova likawa Yesu? Ilitabiriwa kuja kwa Masihi, hivyo mbona basi mwanadamu kwa jina Yesu alikuja? Mbona jina la Mungu lilibadilika? Kazi kama hiyo haikufanyika muda mrefu uliopita? Hawezi Mungu leo kufanya kazi mpya? Kazi ya jana inaweza kubadilishwa, na kazi ya Yesu inaweza kufuata baada ya hiyo ya Yehova. Haiwezi kazi ya Yesu kurithiwa na kazi nyingine? Ikiwa jina la Yehova linaweza kubadilishwa kuwa Yesu, basi jina la Yesu haliwezi kubadilishwa pia? Hakuna jambo lolote hapa lisilo la kawaida; ni kwamba tu watu ni punguani sana. Mungu daima atakuwa Mungu. Bila kujali mabadiliko ya kazi Yake na jina Lake, tabia na maarifa Yake hayabadiliki milele. Ikiwa unaamini kwamba Mungu anaweza tu kuitwa na jina Yesu, basi unajua machache sana.” “Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima Atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha kipengele cha wakati cha tabia ya Mungu katika enzi fulani; yote linahitaji kufanya ni kuwakilisha kazi Yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima” (Neno Laonekana katika Mwili).
Mmoja wao kisha alishiriki haya na mimi: “Kusema Mungu habadiliki kamwe kunarejelea kiini Chake na tabia Yake, hakurejelei jina Lake. Kazi ya Mungu daima husonga mbele daima na Yeye hulifanya upya jina Lake kutegemea na mabadiliko ya enzi. Kila jina linawakilisha enzi na hatua moja ya kazi ya Mungu. Kusema jina la Mungu halibadiliki kunamaanisha kuwa halitabadilika kwa kipindi cha enzi hiyo na litasalia mpaka kazi Yake katika enzi hiyo ikamilike.” “Lakini Mungu anapoanza kufanya kazi katika enzi mpya, Anabadilika jina Lake pamoja na kazi Yake mpya. Akiikaribisha enzi mpya jina la Mungu linawakilisha kazi Yake na tabia Yake katika enzi hiyo. Jina la Mungu lilikuwa, Yehova katika Enzi ya Sheria na kwa hivyo, Alifanya kazi chini ya jina hilo. Alitoa sheria na amri ili kuwaongoza binadamu, ili kwamba wajue dhambi ni nini na jinsi ya kumwabudu Yehova, wafuate sheria na amri na wabarikiwe na Mungu. Mtu yeyote ambaye alivunja sheria aliadhibiwa. Jina Yehova, liliwakilisha uadhama, laana, huruma na ghadhabu ya tabia ya Mungu katika Enzi ya Sheria. Mwishoni mwa enzi hiyo, watu walikuwa wanazidi kuwa wapotovu na hawakuweza kufuata sheria. Wote walikuwa katika hatari ya mara kwa mara kwa kukiuka sheria.” “Mungu alipata mwili kulingana na mpango Wake wa kazi na mahitaji ya upotovu wa wanadamu. Alianzisha Enzi ya Neema na kuitamatisha Enzi ya Sheria akiitwa ‘Yesu’. Aliwakomboa wanadamu na Akatupa njia ya toba, akionyesha tabia ya upendo ya Mungu na kuwapa wanadamu neema nyingi. Mwishowe Alisulibiwa ili atukomboe kutoka katika dhambi zetu. Tangu wakati huo, tuliomba katika jina la Bwana Yesu ili tusamehewe dhambi zetu na kufurahia neema nyingi za Mungu. Jina la Yesu linawakilisha ukombozi na linamaanisha sadaka ya dhambi, linalowakomboa wanadamu wapotovu kwa upendo na huruma. Kuna maana katika jina ambalo Mungu huchukua katika kila enzi. Kila jina linawakilisha tabia na kazi Yake katika enzi hiyo. Kazi ya Mungu daima husonga mbele na jina Lake linabadilika na kila hatua ya kazi Yake. Katika Enzi ya Neema kama Mungu angeshikilia jina la Yehova alipokuja duniani, kazi Yake ingebaki katika Enzi ya Sheria na wanadamu wasingepata ukombozi wa Mungu kamwe. Wangeishia kuadhibiwa kwa kukiuka sheria. Ikiwa Bwana angeendelea kuitwa ‘Yesu’ wakati wa kurudi Kwake, wanadamu wasingeweza kusonga mbele kutoka Enzi ya Neema. Hatungewekwa huru kutoka dhambini, kuokolewa kabisa na kuingia katika ufalme wa Mungu kamwe.”
Kisha yule dada mwingine akaendelea: “Ingawa Bwana Yesu alitusamehe dhambi zetu katika Enzi ya Neema, sisi sote bado ni wenye dhambi kwa asili. Tuna kiburi, ni wenye kustahili dharau, wabinafsi na pia walafi. Upotovu wetu bado umekita mizizi ndani yetu na hutufanya tumpinge Mungu katika dhambi. Tunaishi katika hali ya kutenda dhambi na kukiri. Hatuwezi kuingia katika ufalme Wake bado. Kwa sababu ya utakatifu wa Mungu, hatustahili kuingia katika ufalme Wake. Mungu amerudi katika siku za mwisho na jina Mwenyezi Mungu, akianzisha Enzi ya Ufalme kuwaokoa binadamu kutokana na upotovu.” Dada huyo alisema Bwana sasa anataitwa Mwenyezi Mungu ikitimiza unabii: “Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu Wangu, na hatatoka nje tena: na nitaandika kwake jina lake Mungu Wangu, na jina la mji wa Mungu Wangu … na nitaandika kwake jina langu jipya” (Ufunuo 3:12). “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi” (Ufunuo 1:8). Ufunuo 11:17: “Tunakupa shukrani, Ee BWANA Mungu Mwenyezi, ambaye uko, na ulikuwa, utakuwa, kwa kuwa umeichukua nguvu yako kuu, na umetawala.” “Mwenyezi Mungu ahukumu katika siku za mwisho. Yeye hunena ukweli ili kufunua upotovu wa wanadamu ili tuweze kuelewa kiini cha yote haya, tuone ukweli wa kupotoshwa kwetu na Shetani na tujue tabia ya haki ya Mungu. Hivyo tunapata kuweza kujikana, kutenda maneno ya Mungu na kumcha Mungu na kuepuka maovu. Tutaokolewa hatua kwa hatua kutoka kwa tabia zetu za kishetani, tutakaswe na kuokolewa kikamilifu.” “Mungu pia anawatenga watu kulingana na aina yao kupitia kazi Yake ya hukumu, akifichua tabia Yake ya haki na adhimu ambayo haivumilii kosa lolote. Mwishowe Yeye atauangamiza ulimwengu huu wa zamani Akiutamatisha mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000. Wote wanaolikubali jina la Mwenyezi Mungu, ambao wanapitia hukumu na wanatakaswa wataletwa katika ufalme wa Mungu. Wale wanaochukia ukweli, wanaompinga na kumlaani Mwenyezi Mungu watatupwa nje na kuadhibiwa katika msiba mkubwa. Hiyo italeta kazi ya usimamizi ya Mungu kufika tamati. Kisha Mungu hatakuwa na jina fulani mahsusi lakini utambulisho Wake wa asili utarejeshwa—Muumba.” “Ni kama tu vile Mungu alivyosema: ‘Siku itawadia ambapo Mungu hataitwa Yehova, Yesu, au Masihi—Yeye Ataitwa tu Muumba. Wakati huo, majina yote ambayo Alichukua hapa duniani yatafikia kikomo, kwa kuwa kazi yake hapa duniani itakuwa imefika mwisho, na baada ya hapo Mungu hatakuwa na jina. Wakati mambo yote yatakuja kuwa chini ya utawala wa Muumba, kwa nini umwite kwa jina sahihi ila bado halijakamilika? Je, bado unatafuta jina la Mungu sasa? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaitwa tu Yehova? Je, bado unathubutu kusema kuwa Mungu Anaweza tu kuitwa Yesu? Je, unaweza kubeba dhambi ya kumkufuru Mungu?’” (Neno Laonekana katika Mwili). Ushirika wa kina dada hao ulinigusa. Niliona maana ya majina ya Mungu. Kama Muumba, Hakuhitaji jina. Lakini Amechukua majina tofauti ili kuwaokoa wanadamu. Yehova, Yesu na Mwenyezi Mungu wote ni mmoja. Amefanya kazi za hatua tatu katika enzi tatu tofauti na kila jina lina umuhimu wake hasa. Yote yanasimamia kazi na tabia ya Mungu katika kila enzi. Mwishowe niliikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.
Nikikumbuka nyuma, nachukia jinsi nilivyokuwa mpumbavu na kipofu. Nililichukulia Andiko kwa hali halisi na nikadhani jina la Mungu halitabadilika kamwe, kwamba angeitwa Yesu daima. Bila Mwenyezi Mungu kuonyesha ukweli wa kazi Yake, ningeishikilia Biblia na singeelewa kamwe maana ya majina ya Mungu, na hasa kazi ya Mungu. Ningeipinga kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na ningeondolewa. Nina shukrani kubwa kwa ajili ya mwongozo wa Mungu. Aliniruhusu niisikie sauti Yake, na kuja mbele Yake. Nampa Mwenyezi Mungu shukrani!
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?