Kufuata Nyayo za Mwanakondoo
“Kwa kuwa mwanadamu anamwamini Mungu, ni sharti afuate kwa ukaribu nyayo Zake, hatua kwa hatua; anapaswa ‘kumfuata Mwanakondoo popote Aendapo.’ Hawa tu ndio watu wanaotafuta njia ya kweli, na wao tu ndio wanaoifahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanaofuata tu kanuni na mafundisho ya dini kiutumwa ni wale ambao wameondolewa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba ‘Yehova ni Mungu’ na ‘Yesu ni Kristo,’ ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ni wale tu wanaofuata nyayo za Mwanakondoo hadi mwisho kabisa ndio wanaoweza kufaidi baraka za mwisho” (Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya Mungu kwamba ni muhimu sana kufuata kazi ya Mungu na nyayo Zake. Hapo awali, sikuelewa ukweli, bali nilishikilia tu mawazo yangu mwenyewe, nikifikiri kwamba almradi nilikuwa mwaminifu kwa jina la Bwana Yesu, Atanichukua mbinguni pamoja na Yeye. Hii ndiyo sababu sikutafuta au kuchunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu ya siku za mwisho. Nilikaribia sana kukosa nafasi ya kumkaribisha Bwana.
Siku moja, ilikuwa mnamo Agosti 2012, nilikuwa nikijinyoosha kwenye kitanda chetu, nikipumzika baada ya chajio, mke wangu alipokuwa amekaa mkabala nami akiwa na hedifoni. Na nakumbuka, nikisikia muziki fulani uliokuwa na sauti ya kuvutia. Nilimwuliza, “Ni nini hiyo? Unasikiliza nini?” Alisema, “Nyimbo kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu.” Niliketi upesi na kutaka kujua kwa nguvu, “Umesema Mwenyezi Mungu? Je, umemsaliti Bwana Yesu?” Alijibu mara moja kwa sauti kali, “Hujui unachosema! Bwana Yesu amerudi. Ametamatisha Enzi ya Neema na kuanzisha Enzi ya Ufalme. Mwenyezi Mungu ndiye Bwana aliyerejea, kwa hivyo simsaliti Bwana, bali naenda sawa na nyayo za Mwanakondoo. Kama Biblia isemavyo, ‘Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo’ (Ufunuo 14:4). Hebu fikiri, Bwana Yesu alipoonekana na kufanya kazi, watu wengi waliondoka hekaluni na kukubali kazi Yake. Je, unaweza kusema kwamba walimsaliti Yehova Mungu? Hawakumsaliti Yehova Mungu, bali waliendelea sawa na kazi ya Mungu, na Bwana aliwaokoa wote.” “Kwa kweli, ni makuhani wakuu, waandishi na Mafarisayo ambayo walishikilia sheria zilizokuwa katika Maandiko, wakimshutumu Bwana Yesu, wakidhani kwamba walimcha Yehova Mungu, na wakaishia kuadhibiwa na kulaaniwa na Mungu. Hujui hilo kwa kweli?” Wakati huo sikujua jinsi ya kumkanusha, kwa hivyo nilisema tu, “Bwana ametubariki. Hatuna budi kuwa waaminifu kwa jina na njia Yake bila kujali lolote. Hatuwezi kuwa watovu wa shukurani!” Baada ya hapo, nilikasirika sana na kuondoka kwa ghadhabu. Ili kumkomesha mke wangu, nilimwambia binti yetu kuhusu kile kilichotokea, na aliniunga mkono. Kisha baadaye siku hiyo, mke wangu alihudhuria mkutano, na binti yetu akahudhuria ili kuzua ghasia. Niligundua hilo baada ya kazi. Na nikamwambia, “Ulifanya vizuri leo. Endelea vivyo hivyo, heko! Mwangalie mama yako kwa makini kila siku wakati ambapo nipo kazini. Lazima tutafute jinsi ya kumshawishi amfuate Bwana Yesu tena.” Lakini siku chache baadaye, binti yetu alirudi shuleni. Kwa kuwa niliogopa kwamba mke wangu atahudhuria mikutano mingi zaidi, nilimrai mwana wetu mwenye umri wa miaka kumi amchunge ili aone iwapo alikwenda mikutanoni. Aliniambia mahali alipokwenda kila siku baada ya mimi kutoka kazini. Nilianza kutulia kidogo niliposikia kwamba alikuwa akienda kazini. Lakini kulikuwa na kitu kisicho cha kawaida. Hakuwa akicheza mahjong tena. Badala yake, aliisafisha nyumba na hata alimaliza kazi shambani. Nilikanganyikiwa. Alikuwa akicheza mahjong na kutelekeza kaya daima, na sikuweza kumshawishi aache kufanya hivyo. Alikuwa hata ameomba na kukiri kwa Bwana, lakini hakuwahi kubadilika. Hivyo kwa nini alikuwa amebadilika? Sikujua.
Usiku mmoja, niliamka na niliona mwangaza mdogo uking'aa kwenye pazia. Nilijiuliza mwangaza huo ulikuwa ukitokea wapi. Niligundua kwamba uikuwa ukitoka kwenye blanketi ya mke wangu. Nilijiuliza, “Anafanya nini?” Nilitoka kitandani kwa uangalifu, na kunyatia upande huo mwingine, na kuchungulia ndani ya matandiko kwa makini. Alikuwa akisoma kitabu na kutumia tochi. Niliwaza, “Bado anawamini Mwenyezi Mungu? Bado anasoma kitabu hicho. Kina nini ambacho kinamfanya akisome hivi? Na kwa nini hata nikipinga, ameazimia kuendelea kuamini?” Sikuweza kuelewa. Niliwazia tena jinsi alivyopenda kucheza mahjong, na hakutunza kaya. “Nini kilitokea?” Nilijiuliza. “Yawezekana kwamba kitabu hicho kilimbadilisha?” Na kisha niliwaza, Lazima nijue ni nini kimendikwa mle ndani kwa kweli.” Siku moja mke wangu alipoondoka baada ya kiamsha kinywa, nilifikiri kuhusu kitabu hicho tena. Nilikagua kila dawati, nilikagua kila kitu lakini sikuweza kukipata. Kisha nikatambua kwamba huenda alikificha kati ya rundo la nguo. Bila shaka, hivyo ndivyo nilivyokipata. Vizuri. Nilipokichukua, niliona kitabu kinene kilichokuwa na jalada gumu: Neno Laonekana katika Mwili. Nilipokifungua, nilivutiwa na sura moja. “Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote.” Na niliisoma yote, kuanzia mwanzo hadi mwisho, na niliguswa sana na kifungu kimoja. “Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama tu ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni. Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.” Niliwaza, “Maneno haya yana nguvu sana. Hakuna mwanadamu ambaye angeyanena! Je, haya ni maneno ya Roho Mtakatifu? Mke wangu alisema kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, kwamba kumwamini ni kufuata nyayo za Mwankondoo. Ikiwa hiyo ni kweli, kumzuia kutakuwa kumpinga Mungu.” “Je, hilo halitanifanya niwe kama tu Mafarisayo? “Mafarisayo walishikilia sheria na hawakumkubali Bwana Yesu. Walimshutumu vikali, mwishowe wakashiriki katika kusulubiwa Kwake, na Mungu akawalaani wote.” Nilijiuliza, “Ikiwa Mwenyezi Mungu kwa kweli ndiye kurudi kwa Bwana, je, sitakuwa nikifanya dhambi kwa kuipinga kazi mpya ya Mungu?” “Matokeo yatakuwa yasiyowazika!” Nilikumbuka kwamba kitabu kilisema, “Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake.” Niliwaza, “Siwezi kuendelea kuihukumu kazi ya Mwenyezi Mungu bila kufikiri. Napaswa kusoma kitabu hiki kwa uangalifu na kukichunguza.”
Kuanzia wakati huo, nilisoma Neno Laonekana Katika Mwili kila wakati ambapo mke wangu hakuwa nyumbani. Wakati mmoja aliniambia kwamba alilazimika kufanya kazi ya ovataimu, kwa hivyo nilimaliza kazi yangu mapema kisha nikakwenda nyumbani upesi kwa baiskeli yangu ili niwe na wakati zaidi wa kusoma kitabu hicho. Kisha niliona kifungu hiki: “Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.” “Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imeisha, kazi ya Mungu imeendelea mbele. Kwa nini Ninasema mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya siku hii ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na maendeleo ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata kwa karibu. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya ile iliyofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingejengwa juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi kusulubiwa kwingine kufanyike katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kiwango cha kazi kimewekwa juu kabisa kuliko kilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na kwenye mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii inajengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita” (Neno Laonekana katika Mwili). Kusoma haya kulinifanya nijiulize iwapo mke wangu alikuwa anasema ukweli: Je, kazi ya Mwenyezi Mungu ilikuwa ikifanywa juu ya msingi wa kazi ya Bwana Yesu? Na kusogeza mbele kazi ya Enzi ya Neema? Kitabu hicho kilinijaza udadisi na hamu. Nilisoma kitabu hicho kisirisiri wakati ambapo niliweza.
Ningependa kushiriki nanyi kifungu kimoja nilichosoma wakati mmoja. “Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja” (Neno Laonekana katika Mwili). Maneno hayo yalionekana kuwa ya vitendo sana kwangu. Kisha nikafikiria jinsi ambavyo, katika miaka yangu ya imani, nilikiri na kutenda dhambi tena kila wakati. Sikuwa nimekwepa dhambi kwa kweli. Sikuwa na hakika kwamba nitaingia katika ufalme wa mbinguni. Niliwaza, “Itakuwaje ikiwa haya yote ni kweli? Itakuwa vipi nikikosa hatua moja, itakuwa vipi ikiwa kukubali kazi ya Bwana hakutoshi?” Kadiri nilivyozidi kusoma, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba kulikuwa na ukweli katika kitabu hicho. Hakiwezi kuwa kitu kilichobuniwa tu. Je, kilitokana kweli na Mungu Mwenyewe? Wazo hilo lilinichochea. Na nilizidi kusoma kitabu hicho.
Baadaye, mke wangu alifahamu kwamba sikumpinga tena Mwenyezi Mungu. Aliacha kusoma sirini. Na wakati mwingine, alikisoma kwa sauti kubwa ili niweze kusikia. Siku moja nilipofika nyumbani, alikuwa akisoma maneno ya Mungu, na aliponiona, alisema kwa furaha, “Li Zhong, njoo usome maneno ya Mwenyezi Mungu. Neno Laonekana katika Mwili ni matamshi ya Mungu katika siku za mwisho. Kinafichua ukweli wote ambao hatukuwahi kuelewa hapo zamani. Unaonaje nikikusomea vifungu vichache?” Nami nikawaza, “Nimekuwa nikisoma maneno ya Mwenyezi Mungu, pengine nimesoma mengi kama wewe.” Wakati ambapo sikupinga, alichukua kitabu na kusoma. “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.” “Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso.” “Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu. Sasa, lazima uelewe kwamba kazi yote kutoka awamu ya kwanza hadi leo ni kazi ya Mungu mmoja, ni kazi ya Roho mmoja, ambapo hakuna shaka” (Neno Laonekana katika Mwili). Nilimsihi mke wangu anieleze haya kwa kina. Alishtuka, lakini alishiriki nami: “Kumwamini Mwenyezi Mungu, ni kumwamini Bwana Yesu. Kwa kweli, Yehova, Bwana Yesu, na Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja. Mungu hufanya kazi tofauti, katika enzi tofauti.” “Katika Enzi ya Sheria, Yehova Mungu alitoa sheria, ili iwaongoze wanadamu wa kale katika maisha yao duniani. Kwa hivyo walijua dhambi ilikuwa nini na jinsi ya kumsifu Mungu. Lakini kufikia mwisho wa Enzi ya Sheria, kulikuwa na kutenda dhambi zaidi na hakuna mtu aliyefuata sheria na wote wangehukumiwa kifo. Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili na Aliwakomboa na kuwaokoa wanadamu. Alituonyesha tabia Yake ya huruma na upendo, Akitumiminia neema kwa wingi. Mwishowe, Alisulibiwa msalabani kama sadaka ya dhambi. Tunapotenda dhambi, tunachotakiwa kufanya ni kukiri na kutubu tu, na Mungu atatusamehe.” “Lakini Bwana Yesu alitukomboa tu toka katika dhambi zetu. Asili zetu za dhambi hazijatatuliwa. Bado hatuwezi kujizuia kusema uwongo mara kwa mara na kutenda dhambi. Tuna kiburi, ubinafsi, ulafu ... na sisi hupenda kujionyesha. Hata waumini ambao hujitolea na kuteseka kidogo, hufanya hayo ili tu wapate baraka za ufalme wa mbinguni. Tunapokabiliwa na dhiki kuu au janga halisi, sisi humlaumu tu Bwana, na hata wakati mwingine sisi humsaliti. Kazi ya Mungu inapotofautiana na mawazo yetu, sisi humhukumu, humshutumu na hata kumpinga. Mungu ni mtakatifu, kwa hivyo sisi ambao, bado tunaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu, tunawezaje kungia katika ufalme wa mbinguni?” “Hii ndiyo sababu Bwana Yesu aliahidi kwamba Atarudi na kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Mwenyezi Mungu amekuja katika siku za mwisho, Akionyesha ukweli ili kufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu, juu ya msingi wa kazi ya Bwana Yesu. Amekuja kutakasa asili zetu, za dhambi na upotovu wetu. Kisha tutaweza kuokolewa kikamilifu, na kukombolewa toka dhambini.” “Hii inatimiza unabii wa Bwana Yesu: ‘Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote’ (Yohana 16:12-13). ‘Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho’ (Yohana 12:48). Hata ingawa Mungu hufanya kazi tofauti, katika enzi tofauti, na kwa majina tofauti pia, yote hufanywa na Mungu mmoja.” “Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme ni hatua Zake tatu za kazi, kila enzi ikiwa ya maana zaidi, kuliko iliyoitangulia. Kila hatua huiendeleza hatua iliyoitangulia na zote zinahusiana kwa karibu. Ni hatua tatu pekee kwa pamoja ndizo zinaweza kumwokoa mwanadamu. “Hii ndiyo maana mimi kumwamini Mwenyezi Mungu si kumsaliti Bwana Yesu. Ni kufuata hatua za kazi ya Mungu, na kumkaribisha Bwana.”
Baada ya ushirika wake, tulitazama video. Mwenyezi Mungu anasema, “Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari” (Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kutazama filamu hii, moyo wangu ulichangamka. Niliona kwamba Yehova, Bwana Yesu na Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja. ambaye Amefanya kazi tofauti katika enzi tofauti. Kazi ya Yehova Mungu katika Enzi ya Sheria ilikuwa kutoa sheria, kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema ilikuwa kuwakomboa wanadamu wote, sasa kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, ni kumhukumu na kumtakasa mwanadamu kwa ukweli. Mungu atawaokoa wanadamu kwa hizi hatua tatu kulingana na mahitaji yetu. Najua moyoni mwangu kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, na kumkubali ni kufuata nyayo za Mwanakondoo. Nilifurahi sana na nilimwambia mke wangu, “Naelewa imani yako katika Mwenyezi Mungu haimsaliti Bwana Yesu!” Kisha nilimwambia mwishowe “Nimekuwa pia nikisoma maneno ya Mwenyezi Mungu.”
Alishangaa na akasema, “Eti nini... Tangu lini? Sikujua kabisa!” Nilichukua muda kabla ya kujibu, niliinamisha kichwa changu kidogo, na kusema kimyakimya, “Ulipomfuata Mwenyezi Mungu mara ya kwanza, mbali na kukuzuia, pia niliwashawishi watoto wetu wakuchunge. Na kwa kweli natamani singalifanya hilo. Kufanya hivyo kulikuwa kumpinga Mungu, na kwenda kinyume na Yeye. Lakini Mungu ni mwenye huruma, na Alikuwa akinielekeza kwa maneno Yake. Sasa nina hakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana, Yeye ndiye tumekuwa tukimsubiri!” “Ninamkubali Mwenyezi Mungu rasmi.” Nilikuwa na mhemko mkuu usiku huo. Nililiita jina la Mwenyezi Mungu nilipokuwa nikiomba. “Shukrani kwa Mungu kwa kunichagua, na kuniruhusu nifuate nyayo Zako, na kuhudhuria karamu ya Mwanakondoo!”
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?