Fumbo la Utatu Linafichuliwa

02/12/2019

Na Jingmo, Malaysia

Nilikuwa na bahati katika mwaka wa 1997 kukubali injili ya Bwana Yesu na nilipobatizwa, mchungaji aliomba na kunibatiza katika jina la Utatu—Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Kuanzia wakati huo kuendelea, kila nilipoomba, nilitoa sala yangu katika jina la Utatu, ukiwa Baba wa mbinguni mwenye upendo, Bwana Yesu Mwokozi, na Roho Mtakatifu. Lakini daima kulikuwa na shaka fulani moyoni mwangu: Watatu wanawezaje kuwa mmoja? Sikuweza kueleza kwa ufasaha au kuelewa kwa ukamilifu Utatu ulihusu nini.

Miaka miwili baadaye, niligeuka kuwa shemasi kanisani mwangu, na nilipoandamana na waumini wa kutazamiwa katika mafunzo yao ya kidini, mara nyingi kungekuwa na mtu fulani akiniuliza Utatu ulimaanisha nini. Mara nyingi watu wangeuliza kuhusu Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wakati wa ungamo pia. Kwa kuwa sikuelewa fumbo hili pia, sikuweza kamwe kuwajibu, na hili lilinihuzunisha sana. Nilitaka sana kupata uwazi kuhusu suala hili, na kwa hiyo nilimwuliza mchungaji na wahubiri wanielezee, kwa tumaini la kupata jibu la wazi. Hata hivyo, jibu lao kimsingi lilijumuisha: “Mungu ni Utatu, ukijumuisha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Baba anaweka mipango ya wokovu wetu, Mwana anaitamatisha, wakati ni Roho Mtakatifu anayetekeleza mpango. Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu, na Roho Mtakatifu ni Mungu, pia—nafsi tatu, ambazo kwa pamoja zinaunda Mungu mmoja, wa kweli.” Maelezo haya yalinikanganya hata zaidi tu, na nikauliza, “Lakini ikiwa Yeye ni nafsi tatu, Anawezaje kuwa Mungu mmoja?” Kisha waliniambia, “Utatu ni fumbo. Usilifikirie sana. Tegemea tu imani yako na uiamini, na hilo tu ndilo unalohitaji kufanya.” Ingawa bado nilihisi kukanganywa sana na hili, nilijilazimisha kulikubali, nikiwaza: “Usilifikirie zaidi. Liamini tu!” Nilipoomba, bado niliomba kwa Utatu: Baba wa mbinguni mwenye upendo, Bwana Yesu Mwokozi, na Roho Mtakatifu. Nilihisi kana kwamba ni kwa kuomba tu kwa njia hii ndipo Mungu angesikiza maombi yangu, na niliogopa kwamba, ningeomba tu kwa nafsi moja ya Mungu, basi Hangenisikiza. Na kwa hiyo, niliendelea katika mkanganyiko huo kwa miaka mingi, nikiamini Utatu wa mawazo yangu mwenyewe. Baada ya hapo wakati wowote ndugu kanisani wangeniuliza Utatu ulimaanisha nini, bado sikujua jinsi ya kujibu. Nilichoweza kufanya tu kilikuwa kuwajibu kulingana na kile mchungaji alikuwa ameniambia, ingawa ningeweza kujua kutoka kwa nyuso zao kwamba kweli hawakuelewa. Hili lilinipa hisia ya kutojiweza, na nilichoweza kufanya tu ni kuja mbele za Bwana katika sala: “Nakupa shukrani, Baba mpendwa wa mbinguni! Ndugu na waumini wa kutazamiwa wanaponiuliza maswali kuhusu Utatu, sijui jinsi ya kuwajibu. Nakuomba Unisaidie. Naomba Roho Mtakatifu aniongoze ili nipate kuelewa Utatu unamaanisha nini, ili nisikanganywe tena na suala hili, na naomba watu zaidi waje kukujua.”

Fumbo la Utatu Linafichuliwa

Mnamo Mei mwaka wa 2017, nilikutana na dada kwenye Facebook. Alikuwa mwenye upendo na subira sana, na baada ya sisi kushiriki na kujadili vifungu vichache vya Maandiko, niliona kwamba kulikuwa na mwanga katika ushirika wake. Nilipata mengi kutoka katika ushirika huo, na nilikuwa na bidii kubadilishana mawazo naye. Baadaye alinichukua mimi na ndugu wachache kwenda kwenye baadhi ya mikutano. Kupitia ushirika uliotolewa katika mikutano hii, nilipata kuelewa ukweli fulani ambao sikuwahi kuelewa awali, kama vile kupata mwili kulikuwa nini na jinsi ambavyo Bwana atakuja, na kadhalika. Nilifaidika sana kutokana na ushirika huo na kupata ufahamu wazi zaidi wa vifungu fulani vya Maandiko. Nilipomwuliza dada huyo kwa nini aliweza kuelewa mengi sana kutokana na kusoma Biblia, ilhali mimi sikuweza, aliniambia, “Kila kitu ninachokielewa kimetokana na kusoma maneno ya Mungu. Bwana wetu Yesu amerudi tayari. Amepata mwili kama Mwana wa Adamu kuonyesha maneno Yake na kutekeleza kazi mpya katika siku za mwisho….” Nilishangazwa na kusisimshwa na habari hii, na nikamuuliza dada huyo maswali mengi kwa mfululizo: “Ni kweli? Bwana kweli amerudi?” Alijibu kwa uhakika, “Ndiyo, ni kweli!” Aliendelea kusema kwamba Bwana alikuwa amerudi katika umbo la mwili katika siku za mwisho, lakini kwamba jina la Mungu lilikuwa limebadilika. Sasa Mungu aliitwa Mwenyezi Mungu, akiwa “Mwenye uweza” aliyetabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo. Punde niliposikia jina “Mwenyezi Mungu,” moyo wangu ulishtuka, na nikajiwazia: “Mwenyezi Mungu? Je, hiyo si Umeme wa Mashariki? Mchungaji wetu alituomba tujihadhari dhidi ya Umeme wa Mashariki na akatuambia tusijihushe na wao hata kidogo. Aidha, tunamwamini Bwana Yesu, lakini dada huyu anasema kwamba Bwana Yesu amerudi na amechukua jina la Mwenyezi Mungu, kwa hiyo mbona jina Lake ni tofauti? Je, nitaishia kupotoka?” Lakini nikafikiria: “Tangu nimjue dada huyu, nimegundua kwamba ushirika wake unakubaliana na Biblia, na pia unaangaza sana, na ni dhahiri kwamba una nuru ya Roho Mtakatifu. Ikiwa njia hii si sahihi, inawezaje kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu? Niendelee kumsikiza au la?”

Nilipokuwa tu nikihisi kukanganywa na hisia zisizokubaliana, ghafla nilikumbuka kifungu ambacho dada huyo alikuwa ameshiriki nami awali: “Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Kifungu hiki kinamtaja Kristo na kusema kwamba Kristo anaweza kuwapa watu ukweli. Katika Injili ya Yohana, sura ya 14, mstari wa 6, Bwana Yesu anasema: “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu.” Bwana Yesu ni Kristo, Mungu aliyepata mwili, na Alisema, “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai.” Maneno ya Mwenyezi Mungu na ya Yesu yanataja Kristo na ukweli. Nilifikiria, “Ikiwa Mwenyezi Mungu ni Kristo, basi hakika anaweza kuonyesha ukweli na kutoa ruzuku kwa maisha ya watu.” Nilifikiria kuhusu maneno mengi ya Mwenyezi Mungu ambayo dada huyu alikuwa amenisomea karibuni. Nilipokuwa nikiyasikiza, niliyahisi yakiwa na mamlaka na nguvu, na nilihisi kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu kweli yalikuwa ukweli na kwamba yalikuwa yametoka kwa Roho Mtakatifu! Kwa hiyo niligundua kwamba hii njia lazima iwe njia ya kweli, na kwamba haiwezi kuwa si sahihi. Biblia inasema: “Hivyo basi imani huja kupitia kusikia, na kusikia huja kupitia neno lake Mungu” (Warumi 10:17). Ikiwa Mwenyezi Mungu angekuwa Bwana Yesu aliyerudi na ningekosa kutafuta au kuchunguza njia hii, lakini niamini bila kufikiria kile wachungaji na wazee wa kanisa walichosema, basi singepoteza wokovu wa Mungu na kutoweza kukaribisha kurudi Kwake? Nikifikiria hili, niliamua kuhudhuria mikutano mingine michache ili niweze kuelewa vyema zaidi kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.

Katika mkutano mwingine, dada huyu alishiriki nasi kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Kazi inayofanywa kwa sasa imesukuma mbele kazi ya Enzi ya Neema; yaani, kazi katika mpango mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita imesonga mbele. Ingawa Enzi ya Neema imeisha, kazi ya Mungu imeendelea mbele. Kwa nini Ninasema mara kwa mara kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria? Hii ina maana kwamba kazi ya siku hii ni mwendelezo wa kazi iliyofanyika katika Enzi ya Neema na maendeleo ya kazi iliyofanyika katika Enzi ya Sheria. Hatua hizi tatu zinaingiliana kwa karibu na kuunganika moja kwa inayofuata kwa karibu. Kwa nini pia Ninasema kwamba hatua hii ya kazi inajengwa juu ya ile iliyofanywa na Yesu? Tuseme kwamba hatua hii haingejengwa juu ya kazi iliyofanywa na Yesu, ingebidi kusulubiwa kwingine kufanyike katika hatua hii, na kazi ya ukombozi ya hatua iliyopita ingelazimika kufanywa upya tena. Hii isingekuwa na maana yoyote. Kwa hiyo, sio kwamba kazi imekamilika kabisa, bali ni kwamba enzi imesonga mbele, na kiwango cha kazi kimewekwa juu kabisa kuliko kilivyokuwa kabla. Inaweza kusemwa kwamba hatua hii ya kazi imejengwa juu ya msingi wa Enzi ya Sheria na kwenye mwamba wa kazi ya Yesu. Kazi hii inajengwa hatua kwa hatua, na hatua hii sio mwanzo mpya. Ni muungano tu wa hatua tatu za kazi ndio unaweza kuchukuliwa kuwa mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili). Kisha dada huyo alifanya ushirika akisema, “Kazi ya Mungu husonga mbele daima, na Anatenda kazi tofauti na kuchukua majina tofauti katika enzi tofauti kulingana na mahitaji ya mwanadamu. Lakini bila kujali ni hatua gani ya kazi Mungu anatenda kwa jina lipi, kimsingi, daima ni Mungu Mwenyewe anayetenda kazi kuwaokoa wanadamu. Katika Enzi ya Sheria, Mungu alichukua jina Yehova kutenda kazi Yake: Alitangaza sheria na amri ili kuongoza maisha ya mwanadamu duniani, na Alimruhusu mwanadamu kujua dhambi ilikuwa nini, ni sheria zipi anapaswa kufuata, jinsi anavyopaswa kumwabudu Mungu, na kadhalika; katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili na kuchukua jina Yesu, na juu ya msingi wa kazi ya Enzi ya Sheria, Alitenda kazi ya kusulubiwa ili kuwaokoa wanadamu, matokeo yake yakiwa kwamba dhambi za mwanadamu zilisamehewa. Sasa, katika Enzi ya mwisho ya Ufalme, Mungu amepata mwili kwa mara ya pili, na Akichukua jina Mwenyezi Mungu, Anatenda kazi Yake ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu juu ya msingi wa kazi ya ukombozi. Matokeo ya hili ni kwamba asili ya dhambi na tabia potovu ambazo mwanadamu anazo zinaondolea, na sababu asili ya mwanadamu kutenda dhambi na kumpinga Mungu inaondolewa kabisa. Hatua tatu za kazi zinakamilishana vizuri sana, huku kila hatua ya kazi ikiwa ya juu zaidi na ya kina zaidi kuliko iliyoitangulia. Hakuna hatua ya kazi ya Mungu inayoweza kusimama peke yake—ni hatua tatu za kazi zilizofumana pamoja ndizo zinaunda kazi kamili ya kuwaokoa wanadamu ambayo inatendwa na Mungu, na kwa pamoja zinaunda mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita kwa ajili ya wanadamu. Mungu anatumia jina Lake kutenga enzi na kubadili enzi tu, na hiyo ndiyo maana tunaona kwamba jina la Mungu daima linabadilika pamoja na enzi. Lakini bila kujali jinsi jina la Mungu linaweza kubadilika, Mungu bado ni Mungu mmoja.” Baada ya kusikiza maneno ya Mungu na ushirika wa dada, nilishangaa. Nilikuwa nimemwamini Bwana wakati huo wote na sikuwahi kukutana na yeyote aliyeweza kuelezea kazi ya Mungu ya usimamizi ya miaka elfu sita, lakini maneno ya Mwenyezi Mungu yalikuwa yamefunua fumbo hili—maneno haya kweli yalikuwa sauti ya Mungu! Sikuwa nimepotoka katika imani yangu: Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi. Ni vile tu Mungu hubadili jina Lake kutoka enzi moja hadi nyingine, hayo tu. Lakini Yeye bado ni Mungu mmoja.

Niliendelea kuchunguza hili kwa siku nyingine chache. Dada huyo alitupa ushirika kuhusu vipengele vya ukweli kama vile kazi ya hukumu atendayo Mungu katika siku za mwisho na umuhimu wa majina ya Mungu, na kadiri nilivyosikiza zaidi, ndivyo nilivyoelewa zaidi. Siku moja, alisema, “Maneno ya Mungu yamefichua mafumbo yote ya Biblia,” na niliposikia hili, moyo wangu ulichangamka mara moja; nilimwambia kuhusu suala la Utatu ambalo lilikuwa linanisababishia fadhaa kubwa kwa miaka mingi sana. Kisha dada alinisomea kifungu cha maneno ya Mungu. Mwenyezi Mungu asema: “Ikiwa yeyote miongoni mwenu anasema kwamba hakika Utatu upo, basi eleza huyu Mungu mmoja katika nafsi tatu ni nini hasa. Baba Mtakatifu ni nini? Mwana ni nini? Roho Mtakatifu ni nini? Je, Yehova ni Baba Mtakatifu? Je, Yesu ni Mwana? Basi, Roho Mtakatifu je? Je, Baba si Roho? Je, kiini cha Mwana vilevile si Roho? Je, kazi ya Yesu haikuwa ya Roho Mtakatifu? Je, kazi ya Yehova haikufanywa wakati ule na Roho sawa tu na kazi ya Yesu? Mungu Anaweza kuwa na Roho wangapi? Kulingana na maelezo yako hizi nafsi tatu, yaani, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni mmoja; kama ni hivyo, kuna Roho watatu lakini kuwa na Roho watatu kunamaanisha kuwa kuna Mungu Watatu. Hii inamaanisha kuwa hakuna Mungu Mmoja wa kweli; Mungu wa aina hii anawezaje kuwa kiini asili cha Mungu? Kama unakubali kuwa kuna Mungu mmoja tu, basi Anawezaje kuwa na Mwana na awe Baba? Je, hizi si fikra zako mwenyewe? Kuna Mungu Mmoja tu, nafsi moja katika Mungu huyu, na Roho mmoja tu wa Mungu sawa tu na ilivyoandikwa katika Biblia kwamba ‘Kuna tu Roho Mtakatifu mmoja na Mungu mmoja tu.’ Haijalishi kama Baba na Mwana unaowazungumzia wapo, kuna Mungu mmoja tu, na kiini cha Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu mnaowaamini ni kiini cha Roho Mtakatifu. Kwa maneno mengine, Mungu ni Roho, ila Ana uwezo wa kupata Mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu na vilevile kuwa juu ya vitu vyote. Roho Wake anajumuisha kila kitu na Anapatikana kila mahala. Anaweza kuwa katika mwili na wakati huo huo awe ndani na juu ya ulimwengu. Kwa kuwa watu wanasema kwamba Mungu ndiye tu Mungu wa kweli, basi kuna Mungu mmoja, ambaye hawezi kugawanywa kwa mapenzi ya awaye yote! Mungu ni Roho mmoja tu, na nafsi moja; na huyo ni Roho wa Mungu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?).

Fumbo la Utatu Linafichuliwa

Dada huyo alitoa ushirika akisema, “Maneno ya Mungu ni dhahiri sana. Mungu ni wa pekee na kuna Mungu mmoja tu. Pia kuna Roho Mtakatifu mmoja tu. Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni wa asili moja, ambayo ni ile ya Roho. Mungu anaweza kufanya kazi katika Roho, kama Yehova, lakini pia Anaweza kufanya kazi kwa kupata mwili kama Mwana wa Adamu, kama Yesu na Mwenyezi Mungu. Lakini Mungu afanye kazi katika Roho au katika mwili, kimsingi, bado ni Roho wa Mungu akitenda kazi Yake mwenyewe. Kwa hiyo, dhana ya Utatu inahusu fikira na mawazo ya mwanadamu na haiwezi kutetewa kabisa. Kwa kweli, dhana ya Utatu ilianzishwa zaidi ya miaka 300 baada ya Bwana, katika mtaguso wa Nisea. Katika mtaguso huo, wataalamu wa kidini kutoka mataifa yote ya Kikristo walishiriki katika majadiliano ya kusisimua kuhusu asili moja na nyingi za Mungu hadi mwishowe walianzisha dhana ya Utatu kwa msingi wa fikira, mawazo na mahitimisho yao yenye mantiki. Kuanzia hapo kuendelea, watu walimfafanua Mungu mmoja, wa kweli aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote kama Utatu, kwa imani kwamba, kando na Mwana Mtakatifu Bwana Yesu, kuna Baba Mtakatifu mbinguni na pia chombo kinachotumika na Baba na Mwana, ambacho ni Roho Mtakatifu. Huu ni upuuzi tu. Tukifuata maelezo ya dunia ya dini na tuamini katika Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, basi hilo linamaanisha kwamba kuna Roho watatu na Mungu watatu, na je, si hilo linakinzana na ukweli kwamba kuna Mungu mmoja, wa pekee? Kusema ukweli, Utatu haupo. Haya ni maelezo yaliyotoka kikamilifu katika akili ya mwanadamu na ni hitimisho lililobuniwa na wanadamu wapotovu kwa msingi wa fikira na mawazo yetu. Mungu hakuwahi kusema jambo kama hilo, hakuna nabii ama mtume aliyetiwa msukumo na Mungu aliyewahi kusema jambo kama hilo, na hakuna rekodi ya jambo kama hilo popote katika Biblia.”

Bado kulikuwa na mkanganyiko fulani moyoni mwangu nilipokuwa nikisikiza maneno ya Mungu na ushirika wa dada huyo, na kwa hiyo niliuliza, “Biblia inasema kwamba baada ya Yesu kubatizwa, mbingu zilifunguka na Roho Mtakatifu akaja kama njiwa na kutua juu ya Yesu, na sauti kutoka mbinguni ikasema: ‘Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye(Mathayo 3:17). Pia, kabla ya Yeye kusulubiwa, Bwana Yesu aliomba na kusema: ‘Ee Baba yangu, kama inawezekana, hebu kikombe hiki cha mateso kinipite: hata hivyo si kama nitakavyo Mimi, ila kama utakavyo wewe(Mathayo 26:39). Maandiko yanasema kwamba Mungu mbinguni alimwita Yesu Mwana Wake mpendwa, na Yesu alimwita Mungu mbinguni Baba Yake alipoomba. Kwa hiyo, hapa tuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu—si hili linaonyesha kwamba Mungu ni Utatu? Kwa nini maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema kwamba Utatu haupo na kwamba ni fikira na mawazo ya mwanadamu tu? Haya yote yanamaanisha nini?”

Ili kujibu swali langu, dada huyo alitoa ushirika, akisema, “Hakuna kabisa dhana kama ya Utatu katika Agano la Kale. Ni baada tu ya Bwana Yesu kupata mwili na kuja duniani kutenda kazi Yake ndipo tulipata maelezo ya ‘Baba na Mwana.’ Imerekodiwa katika injili ya Yohana kwamba Filipo hakumjua Mungu na aliamini kwamba, kando na Bwana Yesu duniani, pia kulikuwa na Baba Mtakatifu mbinguni, na kwa hiyo alimwambia Yesu, ‘Bwana, tuonyeshe Baba.’ Bwana Yesu alisahihisha maoni yake yenye makosa na kufunua fumbo hili, akimwambia Filipo, ‘Nimekuwa nanyi kwa muda mrefu, na bado hujanijua, Filipo? Yeye ambaye ameniona amemwona Baba; na unasemaje basi, Tuonyeshe Baba?(Yohana 14:9). Pia Alisema, ‘Niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani ya mimi(Yohana 14:10). ‘Mimi na yeye Baba yangu tu mmoja(Yohana 10:30). Baba ndiye Mwana, naye Mwana ndiye Baba; Baba na Mwana ni sawa, Wao ni wa Roho mmoja. Kwa kusema hili, Bwana Yesu alikuwa akituambia kwamba Yeye na Baba ni Mungu mmoja, sio wawili.”

Kisha dada alinionyesha dondoo nzuri sana ya filamu iliyoitwa Kufichua Fumbo la “Baba na Mwana.” Baadaye, tuliendelea kusoma kifungu cha maneno ya Mwenyezi Mungu: “Aidha kuna wale wasemao, ‘je, si Mungu alitaja wazi kuwa Yesu ni Mwanawe mpendwa?’ Yesu ni Mwana mpendwa wa Mungu, ambaye anapendezwa naye—haya bila shaka yalitamkwa na Mungu Mwenyewe. Huyu alikuwa Mungu akijitolea ushuhuda Mwenyewe, ila kutoka katika mtazamo tofauti, ule wa Roho aliye mbinguni akitolea ushuhuda kupata Mwili Kwake. Yesu ni kupata mwili Kwake, si Mwanake mbinguni. Je, unaelewa? Je, maneno ya Yesu, ‘Mimi ni ndani ya Baba naye Baba yu ndani yangu,’ hayaonyeshi kuwa Wao ni Roho mmoja? Na si kwa sababu ya kupata mwili kulikosababisha kutenganishwa Kwao kati ya mbinguni na duniani? Uhalisi ni kwamba Wao ni kitu kimoja; hata iweje, ni Mungu anajitolea ushuhuda Mwenyewe. … Kwa kuwa Alikuwa Mwili, Aliitwa Mwana mpendwa wa Mungu na kutokana na hili, kukazuka uhusiano wa Baba na Mwana. Ni kwa sababu tu ya utengano kati ya mbingu na dunia. Yesu aliomba kutokana na msimamo wa mwili. Kwa sababu Alikuwa Amepata mwili wa ubinadamu wa kawaida, ni kutokana na msimamo wa mwili ndipo Alisema: ‘Umbo Langu la nje ni la kiumbe. Kwa sababu Nilijivisha mwili kuja duniani, sasa Niko mbali, mbali sana na mbinguni.’ Kwa sababu hii, Angeomba tu kwa Baba kutokana na msimamo wa mwili. Huu ulikuwa wajibu Wake, ambao ni sharti Roho wa Mungu aliyepata mwili anapaswa kupewa. Haiwezekani kusema kwamba Hawezi kuwa Mungu kwa sababu tu Anamwomba Baba kutokana na msimamo wa mwili. Ijapokuwa Anaitwa Mwana mpendwa wa Mungu, Yeye bado ni Mungu Mwenyewe, ni vile tu Yeye ni mwili wa Roho, na kiini chake bado ni Roho(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?).

Dada huyo alisema, “Mungu alipopata mwili mara ya kwanza kama Bwana Yesu na kuja kutenda kazi Yake, hakuna aliyemjua Mungu, hawakuelewa ukweli wa kupata mwili, na hawakujua maana ya kupata mwili. Ikiwa Bwana Yesu angewaambia moja kwa moja kwamba Alikuwa Yehova Mungu waliyemwabudu, hawangeweza kukubali hili kwa sababu ya vimo vyao wakati huo, na Bwana Yesu angehukumiwa na kukataliwa na wanadamu kabla Aanze kutenda kazi Yake. Kazi ya Mungu ya kuwakomboa wanadamu haingewezekana basi, na wanadamu hawangewahi kumpata Yesu kama kafara ya dhambi. Ili wanadamu wamkubali Bwana Yesu, wamwamini na kupata wokovu wa Mungu, kabla ya Yesu kuanza kazi Yake kirasmi, Mungu alijishuhudia kutoka kwa mtazamo wa Roho Wake na kuiita nafsi Yake ya mwili Mwana Wake, ili watu waweze kuona kwamba Yesu kweli alitoka kwa Mungu; hili lilisaidia kuturahisishia sisi kukubali wokovu wa Bwana Yesu. Na Bwana Yesu alipoomba na kumwita Baba mbinguni Baba Yake, huku kulikuwa Mwana wa Adamu aliyepata mwili kumwita Roho aliyekuwa ndani Yake Baba kutoka kwa mtazamo wa mwili. Hili lilifanywa kwa msingi wa tofauti kati ya Roho na mwili; halikumaanisha kwamba kulikuwa na Baba na Mwana waliotengana. Kwa kweli, ufafanuzi wa Baba na Mwana ulifaa tu katika wakati wa Mungu kupata mwili. Kazi ya Mungu duniani ilipohitimishwa, yaani, Bwana Yesu alipomaliza kazi ya ukombozi, akafufuka na kupaa mbinguni, hapakuwa na haja tena ya ufafanuzi wa Baba na Mwana. Kwa hiyo hatuwezi kuchukua ufafanuzi wa Baba na Mwana uliobuniwa na fikira za wanadamu na kuutumia kikamilifu kwa Mungu, tukisema ndani ya Mungu kuna Baba na Mwana, na kwamba pia kuna chombo kinachotumiwa na Baba na Mwana—Roho Mtakatifu—na kwamba Mungu ni Utatu. Kusema jambo kama hilo kunatofautiana na neno la Mungu na kutofautiana na ukweli. Hatukuelewa ukweli awali, na kwa hiyo tuliposema jambo kama hilo, Mungu hakutuhukumu. Lakini sasa Mungu amefichua kabisa ukweli na fumbo hili, na lazima tukubali ukweli na kumjua Mungu katika nuru ya maneno Yake. Hili tu ndilo sahihi, na hili tu ndilo linalokubaliana na mapenzi ya Mungu.”

Kupitia ushirika wa dada huyu, nilipata kuelewa mbona Bwana Yesu alimwita Baba wa mbinguni Baba Yake. Ilikuwa kwa sababu Alikuwa amepata mwili kama Mwana wa Adamu na alikuwa akimwomba Baba wa mbinguni kutoka katika mtazamo wa mwanadamu. Mungu alimshuhudia Yesu kama Mwana Wake mpendwa, na huku kulikuwa Mungu kushuhudia mwili Wake mwenyewe kutoka kwa mtazamo wa Roho. Mmoja alikuwa mbinguni na Mmoja alikuwa duniani lakini kiasili, Walikuwa wa Roho mmoja. Ni kwamba tu Mungu alikuwa akisema mambo haya kutoka katika mitazamo tofauti, na kwa hiyo ufafanuzi wa “Baba na Mwana” yakaibuka. Mungu ndiye Mungu mmoja, wa kweli, Yeye ni Roho mmoja, anayejumuisha yote na mwenye kupatikana kila mahali. Anaweza kuwa mbinguni, Anaweza kuwa duniani, na Anaweza kupata mwili. Punde nilipoelewa haya yote, kila kitu kilikuwa wazi ghafla, mkanganyiko uliokuwa mwandani wangu wa daima kwa miaka mingi ulitoweka mara moja, na nikahisi hisia ya ajabu sana ya kuangaziwa na kuachiliwa.

Baadaye, dada huyu alinionyesha filamu ya ushuhuda wa injili iliyoitwa Uchunguzi wa “Utatu” ambamo niliona maneno haya kutoka kwa Mungu: “Katika miaka hii yote, nyinyi mmegawanya Mungu namna hii, na kuendelea kugawanywa zaidi katika kila kizazi kiasi kwamba Mungu mmoja amegawanywa kuwa Mungu watatu. Na sasa haiwezekani kabisa kwa mwanadamu kumuunganisha Mungu kuwa mmoja kwani mmemgawanya zaidi. Ingekuwa si kazi yangu ya upesiupesi kabla ya muda kuyoyoma, haijulikani mngeishi hivi kwa muda gani! Kuendelea kumgawanya Mungu namna hii, Anawezaje kuendelea kuwa Mungu wenu? Je, bado mngeendelea kumtambua Mungu? Je, bado mngemkiri Yeye kama baba yenu na mumrudie? Ningechelewa hata kidogo, inaonekana kwamba mngewarudisha ‘Baba na Mwana,’ Yehova na Yesu kwenda Israeli na mdai kwamba nyinyi wenyewe ni sehemu ya Mungu. Kwa bahati nzuri, sasa ni siku za mwisho. Hatimaye, siku Niliyoitarajia kwa hamu imewadia, na ni baada tu ya kuifanya hatua hii ya kazi kwa mikono Yangu ndipo kumgawanya kwenu Mungu Mwenyewe kumesitishwa. Isingekuwa hivi, mngezidisha, hadi kuwaweka Mashetani wote miongoni mwenu kwenye meza zenu kwa ajili ya ibada. Hii ndiyo njama yenu! Mbinu yenu ya kumgawanya Mungu! Je, mtaendelea kufanya hivyo sasa? Hebu Niwaulize: Kuna Mungu Wangapi? Ni Mungu Yupi atawaletea wokovu? Je, ni Mungu wa kwanza, wa pili au wa tatu mnayemwomba? Ni nani kati Yao mnayemwamini? Je, ni Baba? Au ni Mwana? Au ni Roho? Niambie ni nani unayemwamini. Ijapokuwa kwa kila neno unasema unamwamini Mungu, mnachokiamini hasa ni akili zenu! Hamna Mungu mioyoni mwenu kabisa! Na bado akilini mwenu mna ‘Utatu Mtakatifu’ kadhaa. Hamkubaliani na hili?(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Utatu Upo?).

Baada ya sisi kumaliza filamu hiyo nilihisi furaha, lakini pia nilihisi fadhaa na kuhisi kujilaumu kiasi. Nilikuwa na furaha kwa sababu mkanganyiko ambao ulikuwa nami kwa miaka mingi ulikuwa umetatuliwa hatimaye: Mungu ni mmoja, na ufafanuzi wa Utatu haupo kabisa. Kumwamini Mungu mmoja, wa kweli pekee ndiko kunakubaliana na mapenzi ya Mungu, na sikulazimika tena kumwomba Mungu dakika moja, na kisha kumwomba Roho Mtakatifu ama Mwana dakika nyingine jinsi nilivyofanya awali—nilihisi utulivu sana. Lakini nilihisi fadhaa na kujilaumu kwa sababu nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka mingi sana lakini sikuwa nimemjua Mungu. Kile nilichokuwa nikiamini kilikuwa tu Mungu aliyebuniwa na fikira na mawaz0 yangu—Mungu asiye dhahiri wa ngano. Sikuwa nikimwamini Mungu halisi na aidha, nilikuwa nikimpinga Mungu na kumgawanya kwa Mungu vipandevipande—kwa kweli nilikuwa nikimkufuru Mungu! Shukrani kwa Mungu, kwani ni kuja kwa Mwenyezi Mungu ambako kumefichua upuzi wote wa imani ya wanadamu potovu, na ni Mwenyezi Mungu ambaye amefunua fumbo hili ambalo daima limeitatiza dunia ya kidini. Bila shaka Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi, Bwana aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote. Yeye ndiye Mungu mmoja, wa kweli!

Fumbo la Utatu Linafichuliwa

Baadaye, kupitia kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, niliona kwamba maneno yote ya Mungu ni ukweli na kwamba ni sauti ya Mungu. Bila kusita, niliikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na kuanza kuwa sambamba na nyayo za Mwanakondoo. Sasa ninapoomba, sina haja ya kuwaomba Mungu watatu. Naomba tu katika jina la Mwenyezi Mungu, na hili linanifanya nihisi utulivu, amani na furaha sana. Sina haja tena ya kuwa na wasiwasi ninapoomba kwamba siombi vya kutosha kwa nafsi moja ama nyingine ya Mungu, na kwamba kwa sababu hiyo, Mungu hatasikia maombi yangu. Kweli nimepitia ufunguliwaji, uhuru, raha na furaha yanayotokana na kuelewa ukweli na kumjua Mungu. Shukrani ziwe kwa Mungu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Niliupata Mwanga wa Kweli

Qiuhe, Japani Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki. Tangu nilipokuwa mdogo, nilihudhuria Misa kanisani na babu na bibi yangu. Kutokana...

Sauti Hii Yatoka Wapi?

Na Shiyin, ChinaNilizaliwa katika familia ya Kikristo, na jamaa wangu wengi ni wahubiri. Nilimwamini Bwana pamoja na wazazi wangu tangu...

Upendo wa Aina Tofauti

Na Chengxin, BrazilNafasi ya bahati mnamo mwaka wa 2011 iliniruhusu nije Brazili kutoka China. Nilipokuwa nimewasili tu, nilizidiwa na...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp