Christian Testimony Video | Kusikiliza Sauti ya Mungu na Kumkaribisha Bwana (Swahili Subtitles)

17/08/2020

Mhusika mkuu alikuwa mhubiri katika kanisa la nyumbani. Alimfanyia Bwana kazi kwa miaka mingi na kila mara alitamani sana Bwana Yesu arudi. Anaamini kwa uthabiti kwamba Atakaporudi katika siku za mwisho, Ataonekana hadharani Akiwa juu ya wingu katika mwili Wake wa kiroho uliofufuka. Anaposikia habari ya kufurahisha ya kwamba Bwana amekuwa mwili na Amerudi katika siku za mwisho, haamini au hata kuchunguza hayo. Kisha katika mkutano mmoja, anaona kwamba kuna unabii mwingi, kama vile “ujio wa Mwana wa Adamu,” “Mwana wa Adamu anakuja,” na Bwana anakuja “kama mwizi.” Huu wote ni unabii unaosema kwamba Bwana atakapokuja tena katika siku za mwisho, Atakuja katika mwili na kwa siri. Hathubutu kuendelea kushikilia maoni yake mwenyewe, kwa hivyo anaanza kutafakari na kutafuta. Kwa hivyo Bwana anakuja na kuonekana kwetu katika siku za mwisho kwa njia ipi? Je, mhusika mkuu anamkaribisha vipi Bwana? Tazama Kusikiliza Sauti ya Mungu na Kumkaribisha Bwana ili ujue.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp