Wimbo wa Injili | Sifa kwa Mwenyezi Mungu Haitakoma Kamwe (Music Video) | Sauti za Sifa 2026

14/01/2026

1

Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho,

Anaonyesha ukweli na Anaonekana Mashariki akiwa amejaa utukufu.

Tunasikia sauti ya Mungu na tunarejea mbele Zake.

Tunafurahia neno la Mungu na kuhudhuria karamu ya arusi ya Mwanakondoo.

Ndugu! Imbeni! Msifuni Mungu kwa kuja miongoni mwa wanadamu!

Dada! Njooni mcheze! Maisha katika ufalme ni ya ajabu kweli!

Lo! Ni baraka iliyoje kuishi katika uwepo wa Mungu!

2

Hukumu katika siku za mwisho inaanza katika nyumba ya Mungu.

Ufichuzi na hukumu ya neno Lake vinatuacha bila mahali pa kujificha kwa aibu.

Baada ya kupitia usafishaji na maumivu mengi sana,

tabia yetu potovu inatakaswa;

tunapata ukweli na uzima, na tumebarikiwa kweli.

Ndugu! Njooni mtazame! Jinsi karamu ya ufalme ilivyo tele!

Dada! Njooni msikilize! Neno la Mungu lina mamlaka,

na tayari limeshinda mioyo ya mamilioni!

3

Katika kupitia hukumu ya Mungu, tunaiona haki Yake;

tunamcha Mungu na tunatii mipango Yake yote.

Tunaachana na mitego ya kidunia na kujitumia kwa moyo wote kwa ajili ya Mungu;

tunaishi bila huzuni au maumivu ndani ya maneno ya Mungu.

Ndugu! Njooni! Sote na tumshuhudie Mungu!

Dada! Msisimame!

Na tutoe mioyo yetu ya kweli ili kumridhisha Mungu!

Na tutimize wajibu wetu kwa moyo na akili zetu zote!

4

Mungu amefanya kundi la washindi.

Watu wa Mungu wote wanapanda na kushuhudia kazi Yake.

Injili ya ufalme inaenea katika nchi zote ulimwenguni kote.

Tunashangilia na kumsifu Mungu kwa uweza na hekima Yake.

Ndugu! Imbeni nyimbo mpya! Msifuni Mungu kwa kupata utukufu!

Dada! Njooni mcheze! Sifuni kukamilika kwa kazi kuu ya Mungu!

Kamwe hatutaacha kumsifu Mwenyezi Mungu!

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp