Majukumu ya Viongozi na Wafanyakazi (1)
Kwa Nini Ni Muhimu Kutambua Viongozi Wa Uwongo
Sasa kwa kuwa tumemaliza ushirika juu ya udhihirisho mbalimbali ya wapinga Kristo, leo tutashiriki juu ya mada mpya—udhihirisho mbalimbali ya viongozi wa uwongo. Katika miaka hii ya kuamini katika Mungu, nyinyi mmekumbana na maonyesho na mazoea ya kila aina ya viongozi wa uwongo. Katika mchakato wa nyumba ya Mungu kuwafukuza viongozi wa uwongo katika viwango vyote, watu wengi wanapata utambuzi kiasi kwa kiwango fulani kuhusu viongozi wa uwongo; yaani, watu wengi wanapata uelewa kiasi wa udhihirisho fulani maalum wa viongozi wa uwongo. Lakini haijalishi kiwango cha ufahamu wako au unaelewa kiasi gani, hatimaye sio wenye utaratibu au mahsusi vya kutosha. Wakati wa uchaguzi wa kanisa, watu wengi hukosa kuelewa kanuni za kuwachagua viongozi, ni mtu wa aina gani wa kuchaguliwa kama kiongozi na ni mtu wa aina gani akiwa kiongozi anaweza kuwaleta ndugu katika uhalisi wa maneno ya Mungu, na anafikia viwango vinavyohitajika kwa kiongozi. Hawana ufahamu sana au kuelewa mambo haya. Kuna hata baadhi ya watu waliochanganyikiwa na wasio na utambuzi ambao huchagua viongozi wa uwongo moja kwa moja wakati wa uchaguzi, wakichagua yeyote aliye kama kiongozi wa uwongo huku wakikosa kumwona yeyote anayestahili kwa kweli na anayeweza kuwa kiongozi, aliye na ubora wa tabia na ubinadamu wa kiongozi. Wale ambao kimsingi hawana ubora wa tabia na ubinadamu wa kuwa viongozi wanachaguliwa kwa sababu ya shauku yao ya nje au tabia fulani nzuri, na kwa sababu wanaridhisha mawazo ya watu ya kuwa “wema,” huku wale ambao kwa kweli wana sifa zote za kuwongoza hawatachaguliwa kamwe. Wale wanaotafuta umaarufu na kujitumia kwa shauku—lakini hawana uwezo wowote wa kazi—wataonekana kila mara katika mandhari ya kila aina, wakionekana wenye kujishughulisha hasa, na watu wengi watafikiri mtu wa aina hii ana sifa na anafaa kuchaguliwa. Matokeo ni kwamba, baada ya watu kama hao kuchaguliwa, hawawezi kufanya kazi yoyote. Hawawezi hata kutekeleza mipangilio ya kazi ya Aliye juu, wala hawajui jinsi ya kutekeleza. Ingawa wao hujishughulisha kwa shauku, baada ya kuwongoza kwa kipindi cha muda fulani hakuna mabadiliko na maendeleo kiasi kidogo katika kazi yoyote ya kanisa, na mara nyingi hali hutokea ambapo kazi ya kanisa imevurugika au watu wametengana, kwa sababu ya usumbufu au unyakuzi wa mamlaka na watu waovu. Haya ni matokeo yanayoletwa na kazi ya viongozi wa uwongo. Baada ya kiongozi wa uwongo kuchaguliwa, mbali na maisha ya akina ndugu kuathiriwa na kupata pigo, pia wakati huo huo vipengele mbalimbali vya kazi ya kanisa vitaathiriwa kwa uhasi, kiasi kwamba kazi ya kueneza injili haitaweza kuendeshwa vizuri au kwa ufanisi. Hili kwa kiasi fulani ni tatizo linalosababishwa na kiongozi wa uwongo mwenyewe, lakini pia linahusiana kwa kiasi fulani na wale wanaomchagua. Ikiwa huelewi kanuni za ukweli, huna utambuzi, na wewe ni kipofu na huwezi kung’amua watu kiasi kwamba unaishia kumchagua kiongozi wa uwongo, basi hujidhuru wewe mwenyewe na wengine tu, lakini kazi ya kanisa inapata pigo pia. Hii ni athari na uharibifu unaosababishwa na viongozi wa uwongo juu ya kuingia kwa maisha kwa watu wateule wa Mungu na kazi ya kanisa. Kwa hivyo, ni lazima tutambue na kuorodhesha udhihirisho mbalimbali wa viongozi wa uwongo, na kwa msingi huo nitawawezesha kuelewa ni tabia zipi kiongozi ambaye anafikia viwango vinavystahili anapaswa kuonyesha, ni kazi gani anayopaswa kufanya, na upeo wa majukumu yao ni uoi hasa. Mada ya kuwatambua viongozi wa uwongo ni yenye umuhimu mkubwa, kwani inagusa kazi ya kanisa, uingiaji katika maisha wa kila mmoja wa watu wateule wa Mungu, na hasa, jinsi kila jukumu linavyoendelea. Wengine wanaweza kusema: “Sina nia ya kugombea katika uchaguzi, wala sina matamanio au hamu ya kuwa kiongozi au mfanyakazi. Ninajitambua, na inatosha kuwa mwumini wa kawaida, kwa hivyo kipengele hiki cha kanuni za ukweli hakinihusu mimi. Nikitaka kusikiliza, nitasikiliza kitu kinachohusu kuingia kwangu kwa maisha na wokovu wangu mwenyewe. Udhihirisho mbalimbali wa viongozi wa uwongo na ukweli unaohusika na hayo si vya maana katika kuingia katika uzima yangu, kwa hivyo si lazima nisikilize, au naweza kusikiliza bila kutilia maanani au shingo upande na nipitie tu katika mchakato huo bila kutilia maanani.” Je, huu ni mtazamo mzuri? (Hapana, sio.) Wengine husema: “Sina matamanio, na sitaki kugombea uongozi. Tangu nilipokuwa mtoto, sikuwahi kukusudia kuwa kiongozi au kusifika kati ya wengine, napenda tu kuwa mtu wa kawaida, mtu asiye tofauti na wengine. Nimetamani kuwa mfuasi tangu nilipoanza kumwamini Mungu. Ninapenda kufuata maagizo ya wengine, na mimi hufanya chochote wanachoniomba nifanye. Ni jambo la kudhalilisha sana kuwa mtu wa aina! Mimi ni mtu wa kawaida tu, kwa hiyo sina haja ya kusikia mambo haya, wala sitaki kuyasikia.” Je, mtazamo huu ni sahihi au la? (Sio sahihi.) Je, ni nini si sahihi kuhusu hilo? (Ingawa hataki kuwa kiongozi, ikiwa haelewi kipengele hiki cha ukweli na hawezi kutambua viongozi wa uwongo, basi, wakati wa uchaguzi, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kumchagua kiongozi wa uwongo, jambo ambalo litaathiri kazi ya kanisa na kuingia katika uzima kwa watu wateule wa Mungu.) Hiki ni kipengele kimoja. Kitu kingine chochote? (Tatizo la viongozi wa uwongo lipo ndani ya kila mmoja wetu, na tunapaswa kuchunguza, kujitafakari, na kujielewa wenyewe.) (Ikiwa hatuwezi kutambua viongozi wa uwongo basi hatutajua hata wakati tumepotoshwa na mmoja wao, na maisha yetu wenyewe yatapata pigo.) (Mtazamo wa aina hii ni udhihirisho wa kutofuatilia ukweli. Kuwa kiongozi katika nyumba ya Mungu si sawa na kuwa mwenye matamanio makuu na kutaka kuwa kiongozi wa dunia. Kuwa kiongozi ni kufuatilia ukweli vyema zaidi, kubeba mzigo kwa ajili ya kazi ya kanisa, na kujali kuhusu nia za Mungu. Huku ni kujitahidi kuelekea ukweli.) (Kama mmoja wa watu wateule wa Mungu, tuna wajibu na jukumu la kuwaripoti viongozi wa uwongo. Ikiwa hatuwezi kutambua viongozi wa uwongo, basi tunaweza kumwacha mtu achukue mamlaka na kuathiri kazi ya kanisa.) Je, ni vipengele vingapi? (Vipengele vitano.) Kila moja ya vipengele hivi vitano ni sahihi, na sahihi kabisa. Kuchanganua kiini cha tatizo hili kwa kuzingatia mtazamo wa aina ya mtu Niliyemtaja hivi punde, kimsingi kuna vipengele hivi vitano. Bila kujali kama wewe unataka kuwa kiongozi au la, kama mmoja wa watu wateule wa Mungu unapaswa kuchukua jukumu la usimamizi kuelekea viongozi na wafanyakazi. Nyumba ya Mungu ni nyumba yako pia, na kiongozi ni kama mtunza nyumba mdogo. Asiposimamia mambo vizuri, wewe pia utaathirika na kuhusishwa, kwa hivyo una jukumu na wajibu wa kusimamia kazi zao zote.
Muhtasari wa Majukumu Kumi na Tano ya Viongozi na Wafanyakazi
Si vigumu kutambua viongozi wa uwongo, kwa sababu mtu wa aina hii hakosi ndani ya kanisa; wamekuwepo tangu kuanza kwa viongozi wa kanisa na kazi ya kanisa. Ubora wao wa tabia na uwezo wa ufahamu, tabia na njia wanayoichagua zote zina udhihirisho mwingi dhahiri. Kabla ya kuchanganua udhihirisho huu dhahiri, kwanza tunapaswa kuelewa majukumu ya viongozi na wafanyakazi ni yapi, na ni kazi gani mahususi inayojumuishwa kimsingi. Ni wale tu wanaoweza kufanya kazi hii mahususi vizuri ndio walio katika kiwango kinachohitajika kama viongozi na wafanyakazi; wale wasioweza kufanya kazi hii ni viongozi wa uwongo. Pengine watu wengi bado hawana njia ya kutambua viongozi wa uwongo, hawawezi kufahamu kanuni za msingi na hawajui ni vipengele vipi ambavyo ni muhimu sana kutambua. Leo, hebu kwanza tushiriki kwa utaratibu kuhusu majukumu ya viongozi na wafanyakazi ni yapi hasa, tukiyaorodhesha moja baada ya lingine ili kila mtu ajue wazi wazi. Baada ya kuelewa kanuni hizi, basi unapowachagua viongozi na wafanyakazi tena, utakuwa na kiwango sahihi cha kupima jinsi hasa ya kuchagua na ni nani hasa anayestahili kuchaguliwa. Kwa hivyo, hebu kwanza tuorodheshe majukumu ya viongozi na wafanyakazi.
Majukumu ya viongozi na wafanyakazi:
1. Kuwaongoza watu kula na kunywa maneno ya Mungu na kuyaelewa, na kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu.
2. Kufahamu hali za kila aina ya mtu, na kusuluhisha matatizo mbalimbali yanayohusiana na kuingia katika uzima wanayokumbana nayo katika maisha yao halisi.
3. Kushiriki kanuni za ukweli zinazopaswa kueleweka ili kutekeleza kila wajibu ipasavyo.
4. Kufahamu hali ya wasimamizi wa kazi mbalimbali na wafanyakazi wanaohusika na kazi mbalimbali muhimu, na kurekebisha mara moja kazi zao au kuwatimua inapobidi, ili kuzuia au kupunguza hasara zinazosababishwa na kutumia watu wasiofaa, na kuhakikisha ufanisi na maendeleo sambamba ya kazi.
5. Kudumisha ufahamu wa sasa na uelewa wa hali na maendeleo ya kila kipengele cha kazi, na kuweza kusuluhisha matatizo mara moja, kurekebisha mikengeuko, na kurekebisha kasoro katika kazi ili iendelee sambamba.
6. Kuendeleza na kukuza kila aina ya talanta inayostahili ili wote wanaofuatilia ukweli waweze kuwa na fursa ya kujifunza na kuingia katika uhalisi wa ukweli haraka iwezekanavyo.
7. Kuwatenga na kuwatumia watu wa aina tofauti kwa busara, kwa kuzingatia ubinadamu na nguvu zao, ili kila mmoja atumike kadiri ya ubora wake.
8. Kuripoti kwa haraka na kutafuta jinsi ya kutatua mikanganyiko na matatizo yaliyojitokeza katika kazi.
9. Kuwasiliana kwa usahihi, kutoa, na kutekeleza mipango mbalimbali ya kazi ya nyumba ya Mungu kulingana na mahitaji yake, ukitoa mwongozo, usimamizi, na himizo, na kukagua na kufuatilia hali ya utekelezaji wake.
10. Kulinda vizuri na kutenga kwa busara vitu mbalimbali vya nyumba ya Mungu (vitabu, vifaa mbalimbali, nafaka, na kadhalika), na kufanya ukaguzi, matengenezo, na ukarabati wa mara kwa mara ili kupunguza uharibifu na hasara; pia kuzuia watu waovu wasivimiliki.
11. Kuwachagua watu wanaotegemewa ambao ubinadamu wao unafikia kiwango kinachostahili kwa ajili ya kazi ya kusajili, kujumlisha na kulinda matoleo kwa utaratibu; kupitia mara kwa mara na kuangalia mapato na matumizi ili visa vya ubadhirifu au uharibifu, pamoja na matumizi yasiyo ya busara, viweze kutambuliwa mara moja—kukomesha mambo kama hayo na kudai fidia inayofaa; zaidi ya hayo, kuzuia, kwa njia yoyote ile, matoleo yanayoanguka mikononi mwa watu waovu na kumilikiwa na wao.
12. Kutambua kwa haraka na kwa usahihi watu mbalimbali, matukio, na mambo ambayo yanavuruga na kusumbua kazi ya Mungu na utaratibu wa kawaida wa kanisa; kuwakomesha na kuwazuia, na kubadilisha mambo; zaidi ya hayo, shiriki ukweli ili watu wateule wa Mungu wakuze utambuzi kupitia mambo kama hayo na wajifunze kutokana nayo.
13. Kuwalinda watu wateule wa Mungu wasisumbuliwe, kupotoshwa, kudhibitiwa, na kudhuriwa vibaya sana na wapinga Kristo, na kuwawezesha watambue wapinga Kristo na kuwatelekeza kutoka mioyoni mwao.
14. Kutambua upesi, na kisha kuwaondoa au kuwafukuza watu waovu na wapinga Kristo wa kila namna.
15. Kulinda wafanyakazi muhimu wa kila aina, kuwalinda kutokana na kuingiliwa na ulimwengu wa nje, na kuwaweka salama ili kuhakikisha vipengele mbalimbali muhimu vya kazi vinaweza kuendelea kwa utaratibu.
Majukumu ya viongozi na wafanyakazi yamefupishwa katika jumla ya vipengele kumi na tano, na tutashiriki kuzingatia haya. Hebu kwanza tuangalie kila moja ya kazi katika vipengele hivi kumi na tano. Vitatu vya kwanza vinagusia suala la watu kuelewa ukweli, na kuingia katika uzima. Hii ndiyo kazi ya msingi kabisa ambayo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya, na ndiyo mojawapo ya vitengo vikuu. Kama kiongozi au mfanyakazi, kimsingi ni lazima uweze kufanya kazi hizi, uwe na ubora wa tabia wa aina hii, uwe na mzigo wa aina hii, na uweze kuchukua jukumu hili. Haya ndiyo mambo ya msingi sana unayopaswa kuwa nayo. Viongozi na wafanyakazi lazima waweze kushiriki juu ya maneno ya Mungu, wapate njia ya utendaji kutoka kwayo, wawaongoze watu kuelewa maneno ya Mungu, na kuwaongoza watu kupitia na kuingia katika maneno ya Mungu katika maisha halisi na kuweza kuwaleta katika maisha halisi, kuyatumia kutatua shida au matatizo mbalimbali yanayokabili maisha halisi na katika njia ya kufanya wajibu wao. Ikiwa watu wateule wa Mungu wana matatizo ambayo yanamhitaji kiongozi au mfanyakazi kutatua, lakini kiongozi au mfanyakazi hawezi kutumia ukweli kutatua matatizo hayo, basi kiongozi huyo au mfanyakazi hana maana, hawezi kufanya hata kazi ya msingi kabisa. Kiongozi au mfanyakazi wa aina hii hafikii kiwango kinachohitajika. Kipengele cha nne na cha tano vinahusiana na vitu mbalimbali vya kazi ya kanisa na wasimamizi wa vipengele hivyo vya kazi. Ikiwa viongozi na wafanyakazi hawatasimamia wasimamizi ipasavyo, basi kazi ya kanisa inaweza kuvurugwa au kusumbuliwa na watu waovu, hii inaweza kuathiri ufanisi na maendeleo ya kazi, na kazi yenyewe inaweza hata kulemazwa. Kwa hivyo, kazi ya nne na ya tano pia ni zile ambazo kiongozi aliyefikia kiwango kinachohitajika lazima afanye vizuri. Kipengele cha sita na cha saba vinagusia upandishaji vyeo, kukuza na kuwatumia watu wa kila aina. Kanuni ya kuwatumia watu ni kumtumia vyema kabisa kila mtu, na watu wa kila aina wanaweza kutekeleza wajibu wao mradi tu ubinadamu wao unafikia kiwango kinachohitajika na wanaweza kufikia viwango vinavyohitajika vya nyumba ya Mungu. Yaani, kuwaruhusu watu wa kila aina kuweza kutekeleza wajibu uonaofaa; hakuna haja ya kujaribu kumlazimisha samaki aukwee mti, au kumlazimisha nguruwe kupaa, inatosha kwamba mtu anafaa kwa kazi fulani, anaweza kuifanya vizuri, na ana maarifa. Zaidi ya hayo, baadhi ya kazi zinahusisha vipengele vya kiufundi, kitaaluma, na baadhi ya watu wanaweza kuzifahamu vizuri lakini hawajafanya kazi yoyote katika sehemu ile, wala hawaelewi kanuni zinazofaa. Kwa watu hawa, ikiwa wanafikia kiwango kinachostahili cha kupandishwa cheo na kukuzwa katika nyumba ya Mungu, basi wanapaswa kupewa nafasi na kupandishwa cheo na kukuzwa, ili waweze kujifunza. Kwa njia hii, kazi mbalimbali katika nyumba ya Mungu zinaweza kuwa na watu wanaofaa zaidi kuzifanya, na hakutakuwa na mapengo wakati wowote ambapo kanisa linahitaji watu kwa ajili ya kazi mbalimbali. Haya ni masuala ya vipengele viwili vya kuwapandisha vyeo na kuwakuza watu, na kuwatumia watu. Hebu tuangalie kipengele cha nane na tisa: Mambo haya mawili yanagusia mtazamo ambao viongozi na wafanyakazi huwa nao wanaposhughulikia kazi, yaani, iwapo wanaweza kutimiza wajibu wao, kuwa na uaminifu, na kuwa na uwezo wa kufanya kazi nzuri katika kushughulikia mahitaji ya Mungu na mipango ya nyumba ya Mungu na huku wakikumbana na matatizo katika kazi. Jambo la kumi na la kumi na moja yanagusa kanuni za utunzaji wa matoleo na mali ya kila aina katika nyumba ya Mungu. Kwa namna moja, vitu hivi viwili vinagusia ubora wa tabia wa watu na uwezo wa kufanya kazi, na katika hali nyingine vinagusa masuala ya ubinadamu, kama mtu ana uaminifu, na kama anaweza kutimiza majukumu yake. La kufuatia, hebu tuangalie vipengele vya kumi na mbili, kumi na tatu, na kumi na nne, kuhusiana na hali fulani za kipekee zinazotokea kanisani—kwa mfano, ikiwa mtu anavuruga na kusumbua, na kuyakoroga maisha ya kawaida ya kanisa. Bila shaka, jambo baya zaidi ni kuonekana kwa wapinga Kristo au watu wa aina nyingine ambao wanapaswa kuondolewa au kutimuliwa. Jinsi gani ya kuwashughulika na watu wa aina hii, na chini ya kanuni zipi, pia ni kazi ndani ya upeo wa wajibu wa viongozi na wafanyakazi. Kuweza kugundua matatizo mara moja, na kuweza kusitisha mara moja, kushughulikia, na kutatua unapopata kwamba mtu fulani anasababisha vurugu na usumbufu, na kuhakikisha kwamba kazi ya kanisa na maisha ya kanisa hayasumbuliwi—haya ni masuala ambayo vipengele hivi vitatu vinagusia. Kipengele cha mwisho kinagusia suala la usalama wa kibinafsi wa wafanyakazi muhimu wa kazi wa kila aina, pamoja na suala la iwapo usalama wa kazi muhimu ya kila aina unaweza kuhakikishiwa. Kazi inaweza kuendelea wakati wafanyakazi wako salama, lakini ikiwa shida au hatari zilizofichika zitatokea katika usalama wa wafanyakazi basi suala huibuka la iwapo kazi inaweza kuendelea au la. Acha turejelee nyuma na tuone kuna vitengo vingapi vikuu kwa jumla. Kipengele cha kwanza, cha pili, na cha tatu ni vya kitengo cha kwanza: kuingia katika uzima kwa mwanadamu. Cha nne na cha tano ni kitengo cha pili: vipengele mbalimbali vya kazi ya kanisa na wasimamizi wa vipengele hivyo vya kazi. Cha sita na cha saba ni kitengo cha tatu: matumizi, kukuza, na kuwapandisha cheo watu wa kila aina. Cha nane na cha tisa ni vya kile cha nne: mipango ya kazi ya nyumba ya Mungu na matatizo katika kazi. Cha kumi na cha kumi na moja ni kitengo cha tano: matoleo na mali ya nyumba ya Mungu. Cha kumi na mbili, kumi na tatu, na kumi na nne ni kitengo cha sita: hali za kipekee ambazo hutokea kanisani. Cha kumi na tano ni kitengo cha saba: kazi muhimu ya kanisa na usalama wa wafanyakazi. Kuna vitengo saba kwa jumla, vinavyohusisha vipengele kumi na tano. Vitengo hivi saba viko ndani ya upeo wa majukumu ya viongozi na wafanyakazi, na ni sehemu ya kazi yao. Kama kiongozi au mfanyakazi, kazi zako za msingi zaidi ni vitengo hivi saba, na vitengo hivi saba ni upeo wa mahitaji ya nyumba ya Mungu kwa kiongozi au mfanyakazi. Ikiwa tunataka kupima iwapo kiongozi anaweza kufanya kazi nzuri, kama ana uwezo wa kufanya kazi, kama ana ubora wa tabia wa kuwa kiongozi, na kama anafikia kiwango kinachohitajika kama kiongozi, tunapaswa kutumia vitengo hivi saba. Baada ya kuelewa hili, kwa kuzingatia vitengo hivi saba vikuu, tutashiriki na kuchanganua udhihirisho na matendo mahususi ya viongozi wa uwongo mmoja baada ya lingine, pamoja na yale ambayo wamefanya wakati wao kama viongozi ambayo yanathibitisha kuwa wao ni viongozi wa uwongo na wala sio wale wanaofikia kiwango kinachohitajika. Inapopimwa kulingana na vitengo hivi saba kuna ushahidi kamili, na hii ni haki na jambo la busara. Hebu Niambieni, je, tufanye ushirika juu ya hivi vitengo saba kimoja baada ya kingine, au vile vipengele kumi na tano? Njia ipi ni bora zaidi? (Shiriki juu ya vipengele kumi na tano kimoja baada ya kingine.) Hiyo inalingana na mapendeleo yenu—ikiwa na maelezo zaidi, ni bora zaidi, sivyo? Basi, tutaanza rasmi ushirika wetu juu ya udhihirisho mbalimbali wa viongozi wa uwongo.
Kipengele cha Kwanza: Kuwaongoza watu kula na kunywa maneno ya Mungu na kuyaelewa, na kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu
Viongozi wa Uwongo Hawana Ubona wa Tabia na Uwezo wa Kuelewa Maneno ya Mungu
Kiongozi wa uwongo ni nini? Hakika, ni mtu ambaye hawezi kufanya kazi halisi, mtu ambaye hashughulikii wajibu wake kama kiongozi. Hafanyi kazi yoyote halisi au muhimu; anafanya tu baadhi ya mambo ya jumla na baadhi ya kazi za kijuu juu, mambo ambayo hayana uhusiano wowote na kuingia katika uzima au ukweli. Haijalishi ni kiasi gani cha kazi hii anachofanya, hakuna umuhimu wa kuifanya. Ndio maana viongozi kama hao wanachukuliwa kama waongo. Kwa hivyo mtu anawezaje kumtambua kiongozi wa uwongo? Hebu sasa tuanze uchanganuzi wetu. Ni lazima kwanza ifahamike wazi kwamba jukumu la kwanza la kiongozi au mfanyakazi ni kuwaongoza wengine katika kula na kunywa maneno ya Mungu na kushiriki ukweli kwa njia ambayo wengine wanaweza kuuelewa na kuingia katika uhalisi wa ukweli. Hiki ndicho kigezo muhimu zaidi cha kuangalia iwapo kiongozi ni wa kweli au wa uwongo. Ona iwapo anaweza kuwaongoza wengine katika kula na kunywa maneno ya Mungu na kuuelewa ukweli, na kama anaweza kutumia ukweli kutatua matatizo. Hicho ndicho kigezo pekee cha kuangalia ni ubora wa tabia upi na uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu kiongozi au mfanyakazi anao, na kama anaweza kuwaongoza watu wateule wa Mungu kuingia katika ukweli. Ikiwa kiongozi au mfanyakazi ana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu kwa ukamilifu na kuuelewa ukweli, anapaswa kutatua dhana na mawazo ambayo watu wanayo kuhusu imani katika Mungu kulingana na maneno ya Mungu, na kuwasaidia watu kuelewa utendaji wa kazi ya Mungu. Anapaswa pia kutatua matatizo halisi yanayowapata watu wateule wa Mungu kulingana na maneno Yake, hasa inapokuja kwa maoni potofu waliyo nayo katika imani yao au kutoelewa walio nako kuhusu kufanya wajibu. Ni lazima pia watumie maneno ya Mungu kutatua matatizo yanayojitokeza wakati watu wanakabiliwa na majaribio na dhiki tofauti, na waweze kuwaongoza watu wateule wa Mungu kuelewa na kutenda ukweli, na kuingia katika uhalisi wa neno Lake. Wakati huo huo, lazima wachanganue tabia mbalimbali potovu za watu kulingana na hali potovu zinazofunuliwa katika maneno ya Mungu, ili watu wateule wa Mungu waweze kuona ni yapi kati ya haya yanawahusu, wapate maarifa kujihusu wenyewe na kumchukia na kumwasi Shetani, na hivyo kuwawezesha watu wateule wa Mungu kusimama imara katika ushuhuda wao, kumshinda Shetani, na kumpa Mungu utukufu katikati ya majaribu ya kila aina. Hii ndiyo kazi ambayo viongozi na wafanyakazi wanapaswa kufanya. Ni kazi ya kanisa ya msingi, muhimu, na inayohitajika kufanywa zaidi. Ikiwa watu wanaohudumu kama viongozi wana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu na ubora wa tabia wa kuelewa ukweli, hawataweza tu kuelewa maneno ya Mungu na kuingia katika uhalisi wake, wataweza pia kuwaelekeza, kuwaongoza, na kuwasaidia wale wanaowaongoza kuelekea kwa ufahamu wa maneno ya Mungu na kuingia katika uhalisi wake. Lakini ubora wa tabia wa kuelewa maneno ya Mungu na kuelewa ukweli ndio hasa viongozi wa uwongo wanakosa. Hawaelewi maneno ya Mungu, hawajui tabia potovu ambazo watu hufunua katika mazingira tofauti ambayo yanafichuliwa katika maneno Yake, au ni hali zipi ambazo huleta upinzani, malalamiko, na usaliti dhidi ya Mungu, na kadhalika. Viongozi wa uwongo hawawezi kujitafakari au kuyahusisha maneno ya Mungu kwao wenyewe, wanaelewa tu mafundisho kidogo na kanuni chache kutoka kwa maana halisi ya maneno ya Mungu. Wanaposhiriki na wengine, wanakariri tu baadhi ya maneno Yake, kisha wanaeleza maana yake halisi. Na kwa hayo, wanafikiri kuwa wanashiriki ukweli na kufanya kazi halisi. Mtu akiweza kusoma na kukariri maneno ya Mungu kama anavyofanya yeye, atamwona kama mtu anayependa na kuuelewa ukweli. Kiongozi wa uwongo anaelewa tu maana halisi ya maneno ya Mungu; kimsingi haelewi ukweli wa maneno ya Mungu, na hivyo hawezi kuzungumza kuhusu maarifa yake ya uzoefu kuyahusu. Viongozi wa uwongo hawana uwezo wa kufahamu maneno ya Mungu; wanaweza tu kuelewa maana yake ya juu juu, lakini waamini kwamba ni kuyafahamu maneno Yake na kuuelewa ukweli. Katika maisha ya kila siku wao daima hutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu ili kuwashauri na kuwasaidia wengine, wakiamini kwamba kufanya hivyo ni kufanya kazi, na kwamba wanawaongoza watu kula na kunywa maneno ya Mungu na kuingia katika uhalisi wake. Ukweli ni kwamba ingawa viongozi wa uwongo mara nyingi hushiriki na wengine kwa njia hii kuhusu maneno ya Mungu, hawawezi kutatua tatizo halisi hata dogo, na watu wateule wa Mungu wameachwa wakiwa hawawezi kutenda au kupitia maneno Yake. Haijalishi wanahudhuria mikutano kiasi gani au kula na kunywa maneno ya Mungu, bado hawaelewi ukweli, wala hawana uingiaji katika uzima, na hakuna hata mmoja wao anayeweza kuzungumzia maarifa yake ya kupitia. Hata kama kuna watu waovu na wasioamini wanaosababisha usumbufu kanisani, hakuna mtu anayeweza kuwatambua. Kiongozi wa uwongo anapomwona mtu asiyeamini au mtu mwovu akisababisha usumbufu, hatumii utambuzi, bali anamwonyesha upendo na kumpa himizo, akiwaomba wengine wawe wastahimilivu na wavumilivu kwake, akihusiana na watu hawa huku wakiendelea kusababisha usumbufu katika kanisa. Hili linapelekea kila kipengele cha kazi ya kanisa kutozaa matunda kabisa. Haya ni matokeo ya kiongozi wa uwongo kushindwa kufanya kazi halisi. Viongozi wa uwongo hawawezi kutumia ukweli kutatua matatizo, jambo ambalo linatosha kuonyesha kwamba hawana uhalisi wa ukweli. Anapozungumza, yeye hueneza tu maneno na mafundisho, na yote anayowaambia wengine wayatende ni mafundisho na kanuni. Kwa mfano, wakati mtu anakuza hali ya kutomwelewa Mungu, viongozi wa uwongo watawaambia, “Maneno ya Mungu yamegusia haya yote tayari: Chochote ambacho Mungu hufanya, ni wokovu wa mwanadamu, ni upendo. Angalia jinsi maneno Yake yalivyo wazi, jinsi maneno Yake yalivyo dhahiri. Je, utaweza kutomwelewa?” Hii ndiyo aina ya maagizo ambayo viongozi wa uwongo huwapa watu. Wao hueneza maneno na mafundisho ya kuwahimiza watu, kuwabana, na kuwafanya wafuate kanuni. Hili halina ufanisi hata kidogo, na haliwezi kutatua matatizo yoyote. Viongozi wa uwongo wanaweza tu kuzungumza maneno na mafundisho ili kuwaelekeza watu, jambo ambalo linawafanya watu hao wafikiri kwamba kuwa na uwezo wa kuzungumza mafundisho kunamaanisha kwamba wameingia katika uhalisi wa ukweli. Lakini wakati ugumu unawapata, hawajui jinsi ya kutenda, hawana njia, na maneno na mafundisho yote waliyoelewa hupotea. Je, hii inaonyesha nini? Inaonyesha kwamba kuelewa mafundisho sio muhimu au jambo la thamani hata kidogo. Kitu cha pekee ambacho viongozi wa uwongo wanaelewa ni mafundisho. Hawawezi kushiriki kuhusu ukweli ili kutatua matatizo; hakuna kanuni kwa matendo yao, na katika maisha yao wanafuata tu baadhi ya kanuni ambazo wanaona ni nzuri. Watu kama hao hawana uhalisi wa ukweli. Ndiyo maana, viongozi wa uwongo wanapowaongoza watu kula na kunywa maneno ya Mungu, hakuna matokeo ya kweli. Wanaweza tu kuwafanya watu waelewe maana halisi ya maneno ya Mungu, na hawawezi kuwasaidia kupata nuru kutoka katika maneno ya Mungu au kuelewa ni aina gani ya tabia potovu walizo nazo. Viongozi wa uwongo hawaelewi hali za watu ni zipi au watu wanafunua kiini cha tabia gani katika hali yoyote, ni maneno yapi kati ya maneno ya Mungu yanayopaswa kutumika kutatua hali hizi potovu na tabia potovu, kile ambacho maneno ya Mungu yanasemwa kuzihusu, mahitaji na kanuni za maneno ya Mungu, au ukweli ulio ndani. Viongozi wa uwongo hawaelewi chochote kuhusu uhalisi wa ukweli huu. Wanawashauri tu watu kwa kusema, “Kuleni na kunywa zaidi maneno ya Mungu. Kuna ukweli ndani yake. Utaelewa utakaposoma zaidi maneno Yake. Ikiwa huelewi baadhi ya maneno hayo, unapaswa tu kuomba, kutafuta, na kuyatafakari zaidi.” Hivi ndivyo wanavyowashauri watu, na hawawezi kutatua matatizo kwa kufanya hivyo. Haijalishi ni nani anayekumbana na shida na anakuja kutafuta kutoka kwao, wanasema kitu kile kile. Baadaye, mtu huyo bado hajitambui na bado haelewi ukweli. Hataweza kutatua tatizo lake mwenyewe halisi, au kuelewa jinsi anapaswa kutenda maneno ya Mungu, na atafuata tu maana halisi ya maneno ya Mungu na kanuni. Inapokuja kwa kanuni za ukweli za kutenda maneno ya Mungu au ni uhalisi gani wanapaswa kuingia, bado hawaelewi. Hiki ndicho kinachotokana na kazi ya viongozi wa uwongo: hakuna matokeo yoyote ya kweli.
Mungu anawataka watu wavae kwa kujisitiri na kwa adabu, kwa heshima ya utakatifu. “Kwa kujisitiri na kwa adabu, kwa heshima ya utakatifu”—maneno tisa kwa jumla, lakini je, mnaelewa maana yake? (Sote tunajua kwamba kimafundisho, Mungu anahitaji watu wavae kwa kujisitiri na kwa adabu, kwa heshima ya utakatifu, lakini tunapovaa sisi wenyewe hatujui jinsi ya kupima kile ambacho ni cha kusitiri au cha heshima.) Hili linagusa tatizo la iwapo ukweli unaeleweka au la. Ikiwa huwezi kupima hili, basi inathibitisha kwamba huelewi maneno ya Mungu. Kwa hivyo, kuelewa maneno ya Mungu kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuelewa vigezo vya kujisitiri na adabu ambavyo Mungu huzungumzia au, kwa mahususi zaidi, rangi na mtindo wa mavazi. Ni rangi zipi na mitindo ipi ndiyo ya kusitiri na ya heshima? Wale walio na uwezo wa kuelewa ukweli wanajua kujisitiri na heshima ni nini, na kile ambacho ni cha ajabu. Ingawa nguo zingine ni za kujisitiri na za heshima, zina mtindo wa kizamani. Mungu hapendi mambo ya kizamani, na hawaambii watu waige mitindo ya zamani au wawe Mafarisayo wanafiki. Anachomaanisha Mungu kwa “kujisitiri na heshima” ni kuwa na sura ya kawaida ya binadamu, kuonekana mtukufu, wa kifahari, na mwenye hadhi. Mungu hawaambii watu wavae nguo za ajabu, wala wavae matambara kama masikini, lakini Anawauliza watu wavae kwa kujisitiri na kwa adabu, kwa heshima ya utakatifu. Huu ni ufahamu wa watu wa kawaida. Lakini baada ya kusikia hayo, kiongozi mmoja wa uwongo alikasirika, akisema: “Maneno ya Mungu yanatupa upeo wa jinsi ya kuvaa. ‘Kwa kujisitiri na kwa adabu, kwa heshima ya utakatifu’—tukiyashika maneno haya tisa basi tunamtukuza Mungu, hatumletei aibu, na tutakuwa watu wenye heshima kubwa miongoni mwa wasioamini. Tukizungumza juu ya watakatifu, kwa ujumla tunarejelea watakatifu wa zamani, basi lazima tuige mtindo wa watakatifu wa kale, lakini ukitembea ukiwa umevalia nguo za kale, basi watu watafikiria kwamba wewe ni wazimu. Hili halilingani na kanuni ya kumheshimu Mungu, lakini kunapaswa kuwa na ushahidi wa nguo ambazo watakatifu walivaa katika siku za hivi karibuni ambazo tunaweza kufuatilia. Hali ya kijamii ilikuwa bora katika miongo kadhaa iliyopita. Watu walikuwa wa kawaida zaidi, na walivaa kihafidhina na ipasavyo. Ikiwa ungevaa kulingana na kiwango hiki basi wewe ungekuwa mwenye kujisitiri na mwenye heshima, na ungekuwa na heshima ya mtakatifu. Hii ndiyo njia ya kutenda.” Alipogundua kwamba watu katika miaka ya 1970 na 1980 walivaa mashati meupe na suruali ya bluu, aliwaambia akina ndugu, “Nimeona nuru katika maneno ya Mungu. Watu wa miaka ya 70 na 80 walivaa mavazi yanayofaa na sahili kabisa. Hayangeweza kusemwa kuwa ya heshima, lakini yanaonekana kulingana na matakwa ya Mungu, kwa hivyo tutavaa kulingana na kiwango hiki.” Kiongozi aliongoza kwa kuvaa hivi, na kila mtu alifikiri kuwa yanaonekana vizuri, yenye heshima na sahili. Kiongozi huyo alisema: “Mungu alisema tusivae mavazi ya ajabu. Kwanza kabisa, vifungo kwenye shati lazima vifungwe hadi shingoni, na vifungo vyote kwenye mkono lazima pia vifungwe. Viwiko vya mikono havipaswi kuonekana, shati lazima liwekwe ndani ya suruali, na kila kitu lazima kifunikwe vizuri, bila kifua au mgongo kuwa wazi. Ona jinsi yalivyo ya kusitiri na yenye heshima! Je, si haya ni ya kusitiri na kuheshimiwa, na si yanalingana na heshima ya utakatifu, kama anavyohitaji Mungu?” Kiongozi hasa alifurahishwa na vazi alilokuwa amevalia wakati huo, na wakati huo huo aliwataka wengine pia wavalie, “Nguo zenu ni za kisasa sana, za mitindo sana. Zinamletea Mungu aibu, na Yeye hazipendi. Kila mtu, fanya hima uvae kile nilichovalia, uwe kama mimi!” Watu wasio na utambuzi walifuata mfano huo, wakitafuta na kuvaa mavazi yanayoitwa ya kujisitiri na ya heshima ambayo yaliambatana na heshima ya utakatifu, na watu wengi hata walidhani lilikuwa jambo zuri. Lakini baadhi ya watu walichukizwa mioyoni mwao na mambo haya ya kizamani, na waliona kwamba kufanya hivi hakukufaa, na ufahamu huu wa maneno ya Mungu ulipotoka. Watu hawa, licha ya kutokuwa na uwezo wa kusema wazi ikiwa ni sawa au sio sawa kumsikiliza kiongozi na kutothubutu kutoa hitimisho, walitetea kutofuata umati bila kufikiria. Waliamini kwamba alichosema kiongozi huyo hakikuwa sahihi kabisa, na hawakufuata. Wale wapumbavu tu, wale watu ambao hawana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu, ambao hawakusoma maneno ya Mungu wenyewe, walifuata chochote kile ambacho kiongozi wa uwongo alisema, na kufanya chochote walichoambiwa kufanya namna walivyoambiwa kukifanya. Walimfuata kiongozi wa uwongo na kumwiga, wakivaa alivyovaa wakati wa kwenda nje. Kila walipotoka nje katika umati, walifurahi sana, wakiwaza “Tunamwamini Mwenyezi Mungu, na kuna heshima nyingi ya utakatifu katika vazi langu. Je, ninyi mmevalia nini? Ni maridadi kiasi gani, ya kisasa kiasi gani, ni maovu yalioje! Hebu tuangalie sisi, hatufunui chochote!” Walifikiri walikuwa wa ajabu. Kiongozi wa uwongo mbali na kukosa kutambua kwamba hii ilikuwa tafsiri potofu ya maneno ya Mungu, pia kwa kweli alifikiri alikuwa akitenda maneno ya Mungu na kuingia katika uhalisi wake. Hivi ndivyo viongozi wa uwongo wanavyofanya. Kwa yale yaliyo mepesi na rahisi hata zaidi kuelewa katika matakwa ya Mungu kwa watu, viongozi wa uwongo hawawezi kuelewa kikweli kile ambacho maneno ya Mungu hurejelea, viwango vyake vinavyohitajika, au kanuni. Je, basi wanaweza kuelewa kile ambacho Mungu anasema kuhusu tabia potovu ya wanadamu, au kuhusu aina zote za hali za kibinadamu? Je, wanaweza kujua kwa hakika ukweli ni nini hapa? Bila shaka hawawezi.
Viongozi wa uwongo hawana uwezo wa kufahamu maneno ya Mungu; wanajua tu kutoka kwa maana halisi ya maneno ya Mungu kile ambacho Mungu amesema lakini hawaelewi ni ukweli upi ambao maneno ya Mungu huonyesha, kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa watu, au ni kanuni zipi za ukweli ambazo watu wanapaswa kuelewa. Kwa hivyo, wanaposhiriki kuhusu maneno ya Mungu, wanatoa tu tafsiri za maana halisi na kuwapa watu masharti fulani, sheria fulani za kufuata, wakitumia hizi kuthibitisha kwamba wao pia wanaelewa maneno ya Mungu na wamefanya kazi. Baadhi ya viongozi wa uwongo hata wanafikiri kwamba maneno ya Mungu tayari yako wazi, ni kwamba tu watu daima hushindwa kuyala na kuyanywa au kuweka jitihada. Wakiwaona wote wakiwa na vitabu vya maneno ya Mungu mikononi mwao, wanaona kuwaongoza watu kula na kunywa maneno ya Mungu kama jambo lisilohitajika. Kwa hivyo, wanapopata matatizo wakati wa mikutano au wanapofanya wajibu wao, wanawatumia watu baadhi ya vifungu vilivyochaguliwa tu vya maneno ya Mungu, wakiwaambia mambo kama, “Soma kifungu hiki cha maneno ya Mungu “; “Soma kifungu kile cha maneno ya Mungu “; au “Maneno ya Mungu yanasema hivi kuhusu kipengele hiki, na vile kuhusu kipengele kile. “Wanawatumia watu vifungu vilivyochaguliwa tu vya maneno ya Mungu, wakitumia njia ya ushawishi kuwahimiza watu wasome maneno ya Mungu, wakiamini kwamba hii ndiyo njia ya kuwaongoza watu kula na kunywa maneno ya Mungu na kwamba wanatimiza wajibu wa kiongozi. Baada ya kuona maneno haya, watu husema, “Mimi pia nimeyasoma maneno haya ya Mungu; je, si jambo la ziada kwako wewe kunikusanyia maneno haya? “Hata hivyo, viongozi wa uwongo huwaza, “Nisipokutumia, hutaweza kupata maneno haya yako katika sura gani au ukurasa upi. Hujui hata Mungu aliyasema maneno haya katika muktadha gani. Kama kiongozi, ninapaswa kuchukua jukumu hili, kukutumia maneno ya Mungu wakati wowote, mahali popote. “Baadhi ya viongozi wa uwongo, kwa wingi wa upendo, hata humtumia mtu vifungu kumi hadi ishirini vya maneno ya Mungu kwa siku, ili kuonyesha uaminifu wao kwa kazi yao na azimio lao la kuwaongoza watu katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Maneno haya ya Mungu yanatumwa kwa watu, lakini, je, matatizo yao yanatatuliwa? Je, wanatimiza jukumu ambalo kiongozi anapaswa kutimiza? Mara nyingi, hawatimizi jukumu hili, kwa sababu kama watu wangeweza kuelewa maneno haya wenyewe, hawangehitaji kiongozi. Vifungu vya maneno ya Mungu vinavyotumwa na viongozi wa uwongo kwa kweli vinajulikana sana na wale wanaosoma maneno ya Mungu mara kwa mara, lakini watu wanakosa nini? Matatizo na shida zao ni zipi? Ni kwamba, inapokuja kwa masuala yanayohusisha ukweli huu, wanapokabiliwa na matatizo, watu hawawezi kung’amua kiini cha matatizo haya, hawajui wapi pa kuanzia kuyatatua, na hawajui jinsi ya kuingia katika ukweli huu—na viongozi wa uwongo hawajui pia. Basi, je, wametimiza wajibu wao katika jambo hili? Je, wana uwezo katika kazi ya uongozi? Bila shaka, hawajatimiza wajibu huu. Kwa mfano, watu wanaposoma kuhusu kuwa mtu mnyofu katika maneno ya Mungu, kiongozi wa uwongo, kwa sababu hajui jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu na anakosa ubora wa tabia wa kufahamu na kuelewa ukweli, angesema: “Mahitaji ya Mungu si ya juu. Mungu anatwambia tuwe watu wanyofu, na kuwa mnyofu kunamaanisha kusema ukweli. Je, maneno ya Mungu hayajasema yote: ‘Acheni maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; La, la’ (Mathayo 5:37)? Maneno ya Mungu ni wazi kabisa! Sema tu chochote unachowaza moyoni mwako; ni jambo rahisi sana! Kwa nini huwezi kufanya hivyo? Neno la Mungu ni ukweli, lazima tulitende. Kutotenda ni kuasi, na, je, Mungu huwaokoa wale wanaomwasi? Hawaokoi. “Baada ya kusikia hili, watu hujibu, “Kila kitu unachosema ni sahihi, lakini bado hatujui jinsi ya kuwa watu wanyofu. Kwa sababu mara nyingi, kusema uongo ni jambo lisilozuilika, au ni jambo ambalo mtu hufanya wakati hana chaguo lingine, na kuna sababu ya hilo. Hili linapaswa kutatuliwaje? “Kiongozi wa uwongo angesema nini? “Je, si hili ni jambo rahisi kushughulikia? Je, maneno ya Mungu hayajaweka hili wazi? Kuwa mtu mnyofu ni kama kuwa mtoto; ni jambo rahisi sana! Haijalishi una umri gani, je, huwezi kuwa kama mtoto? Angalia tu jinsi watoto wanavyotenda. “Msikilizaji kisha anatafakari: “Tabia kuu za mtoto ni kuwa asiye na hatia na mchangamfu, akirukaruka, asiyekomaa, na kuelewa mambo mengi. Kwa kuwa kiongozi amesema hivyo, basi nitafanya hivi. “Siku iliyofuata, mtu huyu mwenye umri wa miaka thelathini au arubaini anasuka nywele zake katika misongo miwili midogo anavaa utepe wa waridi na vibanio vya nywele, anavalia shati la waridi, viatu, na soksi, akijipamba kabisa kwa rangi ya waridi. Baada ya kuona hili, kiongozi anasema, “Hapo sasa! Tembea zaidi kama mtoto, ukirukaruka. Nena kwa njia isiyo na hatia zaidi kama mtoto, na macho yasiyo na uovu, na tabasamu usoni mwako—je, huku si kurudi katika tabia mtoto? Huu ndio mwonekano wa mtu mnyofu! “Kiongozi anafurahishwa sana, huku wengine wakiona hili kama tabia ya kipumbavu, isiyo ya kawaida. Huyu kiongozi wa uwongo hakukosa tu kutatua tatizo tu bali pia hakujua jinsi ya kutafuta kanuni za ukweli hata kidogo, akiwaongoza watu kwenye njia ya upuuzi. Hata kwa ukweli rahisi zaidi wa kuwa mtu mnyofu, kiongozi wa uwongo hajui jinsi ya kuuelewa kwa usahihi na kwa usafi, akiamua kutumia kanuni bila kufikiri, akiuelewa kwa njia potovu kiasi cha kuwachukiza wale wanaoisikia. Hiki ndicho viongozi wa uwongo hufanya.
Viongozi wa uongo huelewa maneno ya Mungu kwa njia tofautitofauti, wakija na mitazamo mbalimbali ya ajabu na ya pekee. Pia hupeperusha bendera ya kutenda na kufuata maneno ya Mungu, wakiwataka wengine wayakubali na kufuata ufahamu wao. Kwa ufupi, watu kama hawa viongozi wa uongo mara nyingi huwa na ufahamu mdogo na uliopotoka wa maneno ya Mungu. Kwa kutumia neno la kiroho kufafanua, tungesema “Wanakosa ufahamu wa kiroho. “Sio tu kwamba uelewa wao wa maneno ya Mungu umepotoka, lakini pia mara nyingi wao huwataka wengine wafuate mafundisho na kanuni hizi zilizopotoka kama wao. Wakati ule ule, wanatumia uelewa wao uliopotoka kuwashutumu wale walio na uelewa safi wa ukweli. Viongozi hawa wa uongo, wakikosa uelewa wa kiroho, hawachunguzi na kuchanganua maneno ya Mungu kama wapinga Kristo wanavyofanya. Kutoka nje, inaonekana kana kwamba wanayachukulia maneno ya Mungu kwa mtazamo wa unyenyekevu wa kula na kunywa na kukubali. Hata hivyo, kwa sababu ya ubora wao duni wa tabia na kutoweza kuelewa maneno ya Mungu, wanayachukulia maneno ya Mungu kana kwamba ni kitabu cha kiada, wakiamini maneno ya Mungu kufuata mantiki ya “moja jumlisha na moja ni mbili, mbili jumlisha na mbili ni nne. “Hawajui kwamba maneno ya Mungu ndiyo ukweli, na ili kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, mtu lazima aelewe ukweli unaozungumzwa katika maneno ya Mungu unamaanisha nini, na hali na maudhui mbalimbali ambayo ukweli huu unahusisha ni yapi. Wengine wanapoelewa maneno ya Mungu kwa njia thabiti na ya vitendo, wanayaona kuwa ya juu juu na hayafai kusikilizwa, wakisema, “Ninayaelewa yote, ninajua kila kitu. Mnachozungumzia tayari kimeelezwa wazi katika maneno ya Mungu, kwa nini ukiseme tena? “Kwa kweli, hawajui kwamba kile ambacho wengine wanajadili kinahusisha maudhui mahususi yanayohusiana na ukweli katika maneno ya Mungu. Kwa sababu viongozi hawa wa uongo hawana uelewa wa kiroho na hawana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu, wanafikiri kwamba ukweli wote ni sawa tu, bila tofauti maalum kati ya masuala yanayogusiwa na ukweli; wanaamini kwamba licha ya kuzungumza bila kikomo kuhusu mambo haya, yote ni suala moja kimsingi. Imani hii inaonyesha tatizo kubwa, na inawapelekea watu kama hao kutoelewa ukweli kamwe.
Viongozi wa Uwongo Hawawezi Kuwaongoza Watu Kuingia Katika Uhalisi wa Ukweli
Sasa, kuna watu wenye ubora mzuri wa tabia na wenye uwezo wa kuelewa ambao tayari wamepata uzoefu kiasi na kuingia katika maneno ya msingi ya Mungu na wana uhalisi fulani wa ukweli, lakini wanahitaji mwongozo na uongozi maalum zaidi ili kuingia kwao kuweze kuwa bora na kwa undani zaidi. Ni viongozi wa uongo pekee wanaoshindwa kuelewa maelezo mahususi ya ukweli yanamaanisha nini au kwa nini yanazungumziwa kwa njia hiyo, wakifikiri inafanya mambo kuwa magumu bila sababu au kucheza na maneno. Hawafahamu au hawajui jinsi ya kuelewa au kupitia vipengele mbalimbali vinavyohusika katika ukweli. Kwa hivyo, wanachoweza kufanya baada ya kuwa viongozi ni kuwaongoza tu watu kula na kunywa maneno ya Mungu yanayoshirikiwa kwa kawaida, kisha wanazungumza kuhusu baadhi ya mafundisho, na kufupisha baadhi ya mbinu za kutenda za kuzingatia kanuni, na kile ambacho watu hupata kutoka kwao ni maneno ya kiroho ya juu juu tu na maneno na mafundisho, kanuni, na kauli mbiu zinazozungumzwa kwa kawaida. Kwa wale ambao ni waumini wapya, mahubiri ya viongozi wa uongo yanaweza kutosheleza kwa mwaka mmoja au miwili, lakini baada ya mwaka mmoja au miwili, wale ambao wameelewa baadhi ya ukweli wataanza kutambua mipangilio ya kauli na mbinu za viongozi wa uongo. Kuhusu wale ambao kimsingi hawana uwezo wa kuelewa, haijalishi viongozi wa uongo huhubiri vipi, hawahisi chochote, hawana ufahamu, na wanashindwa kutambua kwamba kile ambacho viongozi hawa wanahubiri ni maneno na mafundisho tu, na kwamba kile wanachoelewa ni nadharia, kauli mbiu, na kanuni zisizo na maana, ambazo si ukweli hata kidogo. Kulingana na udhihirisho huu, je, viongozi wa uongo wanaweza kutimiza jukumu la “Kuwaongoza watu kula na kunywa maneno ya Mungu na kuyaelewa, na kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu “? Je, wanaweza kutimiza jukumu hili? Je, wanaweza kutimiza majukumu yao? (Hapana.) Kwa nini wasiweze? Suala kuu ni lipi? (Watu kama hao hawana uelewa wa kiroho na hawawezi kuufahamu ukweli.) Hawana uelewa wa kiroho na hawawezi kuufahamu ukweli, lakini bado wanataka kuwaongoza wengine—hili haliwezekani kabisa! Kutarajia viongozi wa uongo wawaongoze watu kuyaelewa maneno ya Mungu na kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu ni kama kujaribu kuyapachika jeli ukutani—haiwezekani! Chukua kuwa mtu mwaminifu, kwa mfano: maneno ya Mungu ni rahisi sana katika jambo hili, ni sentensi chache tu, si ngumu. Mtu yeyote aliye na elimu kiasi anajua maana ya maneno haya. Lakini viongozi wa uongo, ili kuthibitisha kwamba wana uwezo wa kazi na wanaweza kuwaongoza watu, wanafafanua kwa msingi wa maneno ya Mungu: “Umuhimu wa hitaji la Mungu kwa watu kuwa waaminifu ni upi? Ni kwamba kuwa mtu mwaminifu ndicho Mungu anapenda. Wasioamini si waaminifu, hawasemi ukweli, na wanachosema ni uongo na maneno ya udanganyifu; dunia nzima ni taifa kubwa la uwongo. Kwa hivyo, jambo la kwanza ambalo Mungu anadai anapokuja leo ni watu kuwa waaminifu. Kama wewe si mtu mwaminifu, Mungu hatakupenda; kama wewe si mtu mwaminifu, huwezi kuokolewa, wala huwezi kuingia katika ufalme; kama wewe si mtu mwaminifu, huwezi kutenda ukweli, na bila shaka wewe ni mtu mdanganyifu; kama wewe si mtu mwaminifu, hufikii kiwango kinachohitajika kama kiumbe aliyeumbwa. “Je, mnaelewa jinsi ya kuwa mtu mwaminifu sasa? (Hapana.) Hata hivyo, bado haijakuwa wazi. Waumini wapya wanaposikia haya, wanahisi kwamba maneno haya ni bora zaidi, kitu ambacho hawajasikia katika miaka yao ishirini au thelathini katika dini. Hata baadhi yao husema, “Maneno haya yana nguvu, kila sentensi inastahili ‘Amina.’ Mahubiri haya ni mazuri sana, ni mahubiri ya Enzi ya Ufalme! “Viongozi wa uongo kisha wanaendelea: “Mungu anatuambia tuwe watu waaminifu, kwa hiyo, je, sisi ni watu waaminifu? “Baadhi yao hutafakari hili: “Kwa kuwa Mungu anatuambia tuwe watu waaminifu, ina maana kwamba sisi bado si watu waaminifu. “Baadhi hubaki kimya, wakiwaza, “Ninajiona kama nisiye na hatia kabisa. Sijawahi kupigana na wengine, na ninapofanya biashara, sithubutu kumdanganya mtu yeyote. Wakati mwingine, nikichukua fursa ndogo kudanganya, siwezi hata kulala usiku. Je, mimi ni mtu mwaminifu? Nadhani mimi ni mtu asiye na hila, na, je, si hiyo ni sawa na kuwa mtu mwaminifu? “Wengine husema, “Kwa kawaida siwezi kusema uongo. Mimi hushikwa na haya kila ninaposema jambo lisilo la kweli, kwa hivyo lazima mimi ni mtu mwaminifu, sivyo? “Viongozi wa uongo kisha huongeza, “Haijalishi kama wewe ni mtu mwaminifu, kwa kuwa neno la Mungu linatutaka tuwe waaminifu, basi ni muhimu kwako wewe kuwa mtu mwaminifu. Ukitenda kulingana na maneno ya Mungu, wewe ni mtu mwaminifu. Kisha wewe hujitenga na udanganyifu, kutoka kwa minyororo ya ushawishi wa giza wa Shetani. Mara tu unapokuwa mtu mwaminifu, unaingia katika uhalisi wa ukweli, unaweza kutimiza majukumu yako, na unaweza kumtii Mungu. “Je, mnaelewa jinsi ya kuwa mtu mwaminifu sasa? (Hapana.) Lakini, baadhi yenu wamefurahi: “Maneno haya yana nguvu. Amina! Kila sentensi ni sahihi. Hakuna hata moja kati ya hayo linalotoka katika maneno ya Mungu moja kwa moja, lakini yote yanaeleweka kutoka katika maneno ya Mungu. Uelewa huu ni wa ajabu! Kwa nini nisiweze kuelewa hivi? Inaonekana kiongozi huyu kweli anastahili cheo hicho, anastahili kuwa kiongozi! “Watu wenye ubora wa tabia na busara hutafakari baada ya kusikia haya: “Hujaeleza mtu mwaminifu ni nini. Mtu anawezaje kuwa mtu mwaminifu? “Viongozi wa uongo huendelea: “Kuwa mtu mwaminifu kunamaanisha kutosema uongo. Kwa mfano, ikiwa umefanya uasherati hapo awali, basi unamwomba Mungu na kukiri ni mara ngapi umefanya hivyo, na umefanya na nani. Ikiwa unahisi kwamba huwezi kumwona au kumgusa Mungu, basi lazima uungame kwa kiongozi, ukifafanua kila kitu. Kukiri kwa uwazi ni sharti la msingi zaidi la kuwa mtu mwaminifu. Zaidi ya hayo, ni kuhusu kuzungumza kwa dhati, kutochanganya uongo katika chochote. Jinsi unavyofikiria kuhusu chochote, nia ulizonazo, upotovu unaofunua, unayemchukia au kumlaani moyoni mwako, unayetaka kumdhuru au kupanga njama dhidi yake—yote yanapaswa kukiriwa kwa watu hao. Kwa kufanya hivyo, unakuwa wazi na mkweli, ukiishi katika mwanga. Hii ndiyo maana ya kuwa mtu mwaminifu. Mtu mwaminifu lazima aache ubinafsi wake; lazima aweze kuonyesha na kuchanganua sehemu mbaya na zenye giza zaidi za moyo wake. Baada ya kusikia haya, mnaelewa sasa jinsi ya kuwa mtu mwaminifu? (Bado hatuelewi.) Hata baada ya kusikiliza, ni mafundisho tu ambayo mtu anaelewa, si utendaji mahususi. Wakiwa na ufahamu kama huo wa maneno ya Mungu, viongozi wa uongo huwaongoza watu kula na kunywa maneno ya Mungu kwa njia hii, na pia hushiriki kwa njia hii, wakidhani wanaelewa maneno ya Mungu zaidi, kwamba wana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu, na wanaweza kuwaongoza watu katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Kwa kweli, wanachoelewa na kushiriki ni mafundisho na kauli mbiu tu, ambazo hazileti msaada wowote kwa wale wanaotaka kutafuta ukweli na kuelewa kanuni za ukweli. Hata hivyo, viongozi wa uongo bado wanaamini kwamba wana uwezo mkubwa wa kuelewa, wana ufahamu wa kipekee katika maneno ya Mungu, na ni bora zaidi kuliko watu wa kawaida. Wanazunguka kila pahali wakihubiri mafundisho na kauli mbiu hizi, hata wakijihusisha na kujilinganisha na wengine, mara nyingi wakitumia mafundisho na kauli mbiu hizi kujihusisha na mabishano ya maneno, na hata kuzitumia mara kwa mara kufundisha, kupogoa, kuhukumu, na kuwashutumu watu. Wanafikiri kwamba kwa kufanya hivyo, wanafanya kazi, wakileta maneno ya Mungu katika maisha halisi, na kuyatumia Maneno ya Mungu. Je, hili si jambo la kusumbua? Viongozi wa uongo hawawezi kuyaelewa maneno ya Mungu, hawawezi kuwaongoza watu katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, wanaweza tu kushiriki baadhi ya maneno na mafundisho, na bado wanazungukazunguka wakihubiri na kuyaonyesha. Hata hivyo, kwa kweli, hawaelewi ukweli wowote katika maneno ya Mungu. Kwa mfano, hawaelewi maneno mengine ya kiroho yanayofanana au misemo inayofanana, wala hawajui tofauti kati yao au jinsi ya kuyatumia katika hali halisi. Mbali na kufuata kanuni na kutamka maneno na mafundisho, hawana utambuzi wa kweli wa maneno ya Mungu na hawayatendi kwa kweli. Kwa hivyo, ni wazi kwamba viongozi wa uongo wenyewe hawaelewi ukweli, wala hawana uwezo wa kuwaongoza watu kuyaelewa maneno ya Mungu na kuingia katika uhalisi wa ukweli. Tumeonyesha hili kwa mfano wa kuwa mtu mwaminifu. Viongozi wa uongo, bila kujua jinsi ya kutambua ukweli wa kuwa mtu mwaminifu, huamua kutamka maneno na mafundisho na kuhubiri kauli mbiu, wakiwapotosha wanaoboronga na waliochanganyikiwa wasio na uelewa wa kiroho, na kuwaacha wamechanganyikiwa. Baada ya kusikiliza maneno na mafundisho haya, wao hasa huwaabudu viongozi wa uongo na, baada ya kuwafuata kwa miaka kadhaa, huishia kutoelewa hata ukweli wa msingi, wakiishia kutokuwa na uingiaji hata kidogo. Tutahitimisha ushirika wetu kuhusu jambo hili hapa.
Kipengele cha Pili: Kufahamu hali za kila aina ya mtu, na kusuluhisha matatizo mbalimbali yanayohusiana na kuingia katika uzima wanayokumbana nayo katika maisha yao halisi (Sehemu ya Kwanza)
Viongozi wa Uwongo Hawawezi Kung’amua Hali za Kila Aina ya Mtu
Jukumu la pili la viongozi na wafanyakazi ni kufahamu hali za kila aina ya mtu, na kusuluhisha matatizo mbalimbali yanayohusiana na kuingia katika uzima wanayokumbana nayo katika maisha yao halisi. Viongozi wa uongo hufanyaje kazi hii? Je, wana uwezo wa kazi hii? Hebu tuchanganue jambo hili. Kufahamu hali za kila aina ya mtu—hili linatimizwa kwa msingi gani? Linatimizwa kwa msingi wa kuelewa maneno ya Mungu yanayofichua tabia na kiini potovu cha watu mbalimbali. Ili kuelewa hali za watu mbalimbali, mtu lazima kwanza aelewe maneno ya Mungu yanayofichua hali mbalimbali, tabia potovu, na kiini potovu cha watu, na aweze kuvilinganisha na nafsi yake. Aina ya tabia zinazofichuliwa na Mungu inarejelea aina gani ya watu, ubinadamu wao ukoje, aina gani ya udhihirisho na ufunuo walio nao, na mtazamo wao kwa Mungu, maneno ya Mungu, na wajibu wao ni upi; hali hizi lazima zilingane na maneno ya Mungu, na kwa kufanya hivyo, mtu anaweza kuelewa hali za watu mbalimbali. Kwa hivyo, kufahamu hali za watu mbalimbali kwanza kunapatikana kwa msingi wa kuelewa maneno ya Mungu na kuwa na uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu. Viongozi wa uongo hawana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu, kwa hivyo, je, wanaweza kuelewa ukweli tata kuhusu aina mbalimbali za watu waliofichuliwa na maneno ya Mungu, na vile vile hali mbalimbali na asili potovu zinazofichuliwa? (Hapana.) Hawaelewi, hawajui uhusiano unaohusika hapa, na hawajui ukweli unaohusika. Kwa sababu hawana uwezo wa kufahamu maneno ya Mungu, kuelewa hali za watu mbalimbali—jambo hili la maana na muhimu sana—ni kazi tata sana na ngumu kwa viongozi wa uongo.
Viongozi wa uongo wanaelewaje hali za watu mbalimbali? Wao huwaza, “Mtu huyu ana shauku, yule ni mwenye chukichuki, huyu anapenda kuvaa vizuri, yule ana imani ndogo…. “Wao huangalia tu matukio haya ya juu juu, lakini hawajui mtazamo wa mtu kuelekea maneno ya Mungu na ukweli ni upi hasa, na kiini cha asili yake ni nini hasa. Kwa mfano, mtu ana imani ya kweli na ana nguvu katika kufanya wajibu wake, lakini matatizo na mikazo ya kifamilia yao huathiri matokeo ya majukumu yake; viongozi wa uongo, wanapoona hili, watawaita vibaya, wakisema, “Mtu huyu ni asiyeamini. Hawezi kujitenga na familia yake. Daima anawafikiria watoto wake. Ana akiba nyumbani lakini hawezi kutoa matoleo. Kwa hivyo mtu huyu ni msumbufu sana, na hawezi kutumika kwa kazi muhimu katika siku zijazo. “Kwa kweli, suala la mtu huyu si kubwa; ni kwa sababu tu amemwamini Mungu kwa muda mfupi tu na ana ufahamu mdogo wa ukweli kwamba hawezi kung’amua mambo mengi. Hajui jinsi ya kuishughulikia familia na watoto wake, au jinsi ya kuishughulikia mali zake. Yeye bado yuko katika kipindi cha kuomba na kutafuta, na bado hajapata kanuni na mbinu sahihi za utendaji. Ana azimio la kutenda ukweli, lakini anapokabiliwa na misukosuko na matatizo ya kifamilia, huwa dhaifu kwa muda na hafanyi kazi sana katika kutekeleza wajibu wake. Hata hivyo, anaweza kukamilisha kazi aliyopewa na kanisa kwa dhati, jambo ambalo watu wengi hawawezi kufanya. Kwa kuzingatia ubora wake wa tabia, ubinadamu, na mtazamo wake kuelekea ukweli, yeye ni mtu mwema. Lakini viongozi wa uongo hawaoni hivi kwa sababu hawayaelewi maneno ya Mungu na hawajui jinsi ya kutumia maneno ya Mungu kama kiwango cha kupima asili ya mtu, au kama hali aliyomo mtu ni kwa sababu ya asili yake au udhaifu wa muda, au ni suala la kimo; hawawezi kupima mambo haya. Matatizo ambayo mtu wa aina hii hukumbana nayo ni yale yanayotokea katika maisha halisi na yanahusiana na kuingia katika uzima—je, viongozi wa uongo wanaweza kushughulikia masuala ya aina hii? Je, wanaweza kutatua matatizo ya watu hawa? (Hapana.) Kwa sababu viongozi wa uongo hawawezi kuelewa kwa usahihi hali za watu mbalimbali na hawawezi kutambua kwa usahihi uzuri na ubaya wa asili ya watu mbalimbali, pia hawawezi kutatua kwa usahihi matatizo na shida za watu mbalimbali. Kinyume chake, wakitegemea shauku pekee wanawaona wale ambao wanaweza kukimbia huku na kule wakijitumia, kuvumilia magumu, na kulipa gharama, lakini wana ubora duni wa tabia na hawana uwezo wa kuelewa, kama walengwa muhimu wa ukuzaji, na wanafanya ushirika kutatua matatizo yao watu hawa wanapokumbana nayo. Lakini kwa wale ambao hakika wana ubora mzuri wa tabia na ubinadamu mzuri, wanapokumbana na matatizo na ni dhaifu kidogo, viongozi wa uongo huyatatua na kuyashughulikiaje? Watu hawa wanapokabiliana na matatizo na kwa kweli ni dhaifu kidogo, kulingana na hali hiyo, wanapaswa kuungwa mkono na kusaidiwa; mtu anapaswa kushiriki nia za Mungu kwao—hawapaswi kupuuziliwa mbali, sembuse kuitwa majina mabaya. Lakini viongozi wa uongo hutatuaje matatizo ya watu kama hao? Wao husema, “Kazi ya Mungu tayari imefikia hatua ya aina hii, lakini bado wewe unaendelea kushikilia na mumeo, watoto wako; hata mnawaacha watoto wenu wasome chuo kikuu na kufuatilia matarajio yao. Kadri majanga yanavyozidi kuwa makubwa, je, bado kuna matarajio yoyote katika ulimwengu huu? Huwezi hata kutunza maisha yako mwenyewe, unawezaje kujali mambo hayo? Kazi ya Mungu inakaribia kukamilika, muda ni mchache mno! Usipojitolea kikamilifu, je, bado unaweza kuitwa kiumbe aliyeumbwa? Je, bado wewe ni binadamu? “Je, matatizo ya watu hawa yanahusiana na haya kweli? (Hapana.) Sababu ya watu hawa kuwa dhaifu kidogo wanapokabiliwa na magumu ni kwa sababu tu ya kimo chao kidogo, si kwa sababu hawapendi ukweli au hawataki kufanya wajibu wao. Kwa hivyo, kile ambacho viongozi wa uwongo wanasema hakilingani na hali yake; ni wazi kwamba ni hali ya kumweka katika kitengo kibaya, kutoelewa kiini au kipengele muhimu cha hali yake, kutoelewa anachofikiria kweli, ni mtu wa aina gani, na jinsi anavyopaswa kuongozwa na kusaidiwa kutatua matatizo yake. Viongozi wa uongo hawajui jinsi ya kutatua matatizo haya. Kwa hivyo, mtu anapaswa kutatuaje mambo kama hayo yanapotokea? Unaweza kusema, “Suala unalokabiliana nalo ni tatizo ambalo watu wengi hukumbana nalo. Wale ambao wanaweza kuacha familia zao na kujitoa kwa moyo wote kwa ajili ya Mungu hawafanyi kwa msukumo, bali wamejiandaa kwa muda mrefu. Kwanza, wameelewa ukweli wa kutosha na wana azimio la kweli la kujitenga na familia zao, kujituma kwa moyo wote katika nyumba ya Mungu, na wanaweza kuhakikisha kwamba hawatajuta baadaye—wamefikiria kuhusu kila kitu. Zaidi ya hayo, katika kipindi hiki, pia wanamwomba Mungu kwa ajili ya maandalizi na kufungua njia ya kusonga mbele, huku wakiendelea kujiandaa na ukweli, wakijiruhusu kuuelewa ukweli zaidi, na kuwa na imani zaidi katika kuweka kando kila kitu ili wajitumie kwa moyo wote kwa ajili ya Mungu. Hili linahitaji muda, maombi, na bila shaka, uongozi na mipango ya Mungu. Ukiwa na azimio hili, usiwe na wasiwasi. Mwombe Mungu na usubiri kimya kimya, na Mungu atakufanyia mipango. Maombi yako na azimio lako yakilingana na nia za Mungu na kupokea kibali cha Mungu, ukiwa uko tayari na utatii bila kujali Mungu anafanya nini na hutajuta, basi Mungu hakika atakufungulia njia. Katika kipindi hiki, kile ambacho watu wanapaswa kufanya ni kujiandaa na kusubiri; kitu pekee wanachoweza kufanya ni kujiandaa na ukweli, kuelewa nia za Mungu, na kuruhusu kimo chao kikue polepole. Mungu anapoweka mazingira mbalimbali, ukiweza kuchagua kutii mamlaka na mipango ya Mungu bila malalamiko yoyote, huku ndiko kuwa na kimo—bila kujali Mungu anafanya nini au jinsi Anavyopanga, wewe utaweza kutii. “Mnaonje kuhusu mwongozo wa aina hii? (Ni mzuri.) Kwa upande mmoja, unatimiza jukumu lako, ukiwasaidia watu waelewe nia za Mungu; wakati huo huo, huwalazimishi zaidi ya uwezo wao, lakini unawatendea kulingana na hali yao halisi. Je, huku si kutatua matatizo kutumia maneno ya Mungu? Je, huku si kutatua matatizo ambayo watu hukabiliana nayo katika maisha halisi kulingana na hali yao? (Ndiyo.)
Katika utendaji wa wajibu wao, baadhi ya watu huwa wenye kufanya mambo ili kutimiza wajibu tu na hawaonyeshi kujukumika hata kidogo, huwa wanajichukulia kuwa wenye madaraka, na ni wenye kiburi, wenye kujihesabia haki, na wasioweza kushirikiana na wengine, na huleta hasara kwa kazi ya kanisa bila kuhisi hata chembe ya hatia. Kiongozi wa uongo, anapoona hali kama hiyo, huanza kushughulikia na kutatua suala hilo, akisema, “Mtu huyu ana jukumu muhimu sana katika kazi hii. Inaonekana hakuna mtu anayefaa kabisa kuchukua nafasi yake, kwa hivyo tunahitaji kushirikiana na yeye ili tutatue matatizo yake.” Wakati wa ushirika, kiongozi wa uongo hugundua kwamba mtu huyu hataki kufanya wajibu wake hata kidogo. Anataka kufuatilia mambo ya kidunia, kuchuma pesa kutokana na kazi yake na kuishi maisha mazuri, na anaona kulazimishwa kufanya wajibu wake kama kumlazimisha afanye asichotaka. Anahisi kwamba kufanya wajibu wake katika nyumba ya Mungu kunamaanisha kuwa na shughuli nyingi kila siku, si tu kuharibu maisha yake ya kibinafsi ya familia lakini pia kufanya iwe vigumu kudumisha uhusiano na watu wa familia, na kwamba akikiuka kanuni anapofanya wajibu wake anapaswa kuvumilia kupogolewa. Anaona maisha kama hayo kuwa machungu sana na hataki kuishi hivyo. Suala liko wazi: Tabia yake inaonyesha kwamba yeye ni asiyeamini. Lakini kiongozi wa uongo anashughulikiaje jambo hilo? Kiongozi wa uongo huwaza, “Mtu huyu ana kipaji miongoni mwa wasioamini; si rahisi kupata mtu kama yeye. Hali yake imekuwa ya matatizo; Ninahitaji kuweka kando haraka shughuli nyingi zaidi ninayoifanya sasa ili nifanye ushirika na yeye, nimsaidie kutatua hili. Nalitatuaje? Maneno ya Mungu ndiyo yenye nguvu zaidi; kwanza, nitamsomea vifungu vichache vya maneno ya Mungu ili kutatua kutokuwa kwake radhi kufanya wajibu wake.” Kiongozi wa uongo huwaambia, “Sasa kwa kuwa majanga yamekuja, watu hawawezi tena kuishi maisha mazuri. Bado unataka kuchuma pesa kupitia kwa kazi na kuishi maisha rahisi ya familia, lakini hivi karibuni ulimwengu mzima utakuwa katika machafuko, na hakutakuwa na familia za kawaida tena. Je, huwezi kung’amua mambo haya? Unahitaji kumwomba Mungu zaidi. Kumwomba Mungu kutakupa imani. Pia unahitaji kula na kunywa maneno ya Mungu zaidi. Baada ya kula na kunywa maneno ya Mungu mara chache, tatizo lako litatatuliwa.” Kisha, anatafuta vifungu vitano au kumi vya maneno ya Mungu vya kusoma na kushiriki na yeye. Mtu huyo anajibu, “Ushirika umetosha. Ninaelewa maneno haya yote ya Mungu; mimi ni msomi kukushinda. Usijionyeshe.” Siku nzima ya ushirika na hakuna kinachotatuliwa. Kiongozi wa uongo hujiwazia, “Nimekuwa nikifanya kazi ya kanisa kwa miaka mingi sana; siamini kwamba siwezi kutatua tatizo lako.” Jioni, anaendelea na ushirika haraka, “Unahitaji kumpenda na kumwabudu Mungu! Una tumaini la kuwa kiumbe aliyeumbwa ambaye anafikia kiwango kinachohitajika. Wajibu huu si rahisi kuupata; lazima uithamini fursa hii, kwani ukiikosa, hakutakuwa na nyingine. Ukiwa na ubora wako wa tabia na hali ikiwa nzuri sana, je, halitakuwa jambo la kusikitisha ukikosa kufanya wajibu wako? Mtu mwenye talanta kama yako anapaswa kukuzwa na kutumika katika nyumba ya Mungu; wewe una matarajio makubwa hapa!” Mtu huyo anasema, “Acha kuzungumza. Ukinilazimisha nifanye wajibu wangu, mtazamo wangu utabaki vile vile. Kama sitaruhusiwa kufanya hivyo, nitaondoka mara moja. Sio eti naomba nibaki hapa!” Kiongozi huyo wa uongo anamaliza maneno yake yote lakini hawezi kumshawishi mtu huyu au kutatua tatizo lake. Kwa nini? Ni kwa sababu hawezi kuelewa tatizo kuu la mtu huyu ni lipi. Mtu huyu, anapofanya wajibu wake, ni mzembe kila anapohisi kufanya hivyo, hudanganya kila anapohisi akifanya hivyo, na hutenda kwa njia isiyo ya dhati tu kama ndivyo anavyohisi kufanya; haijalishi anafanya kazi gani, hana uwajibikaji. Hataki kuweka juhudi kidogo zaidi au kusema maneno machache zaidi ili kutatua baadhi ya masuala, akiona ni ya kusumbua na kutatiza. Anajua wazi jinsi ya kufanya wajibu wake kwa njia ambayo ni ya kiwango kinachohitajika na jinsi ya kutenda ipasavyo lakini hataki kufanya hivyo. Bado, anaendelea kufanya wajibu wake katika nyumba ya Mungu. Asili ya hali hii ni gani? Tatizo hapa ni lipi? (Alikuja na nia ya kupata baraka na kufanya mikataba.) Alikuja na matumaini makubwa; watu kama hao wanajulikana kama watu wanaojali maslahi yao wenyewe. Wanasema, “Nilisikia kwamba dunia itaisha hivi karibuni, mwisho wa dunia umewadia, kwa hivyo sihitaji kwenda kazini tena; nimepata pesa nyingi za kutosha hata hivyo. Ni bora nije nyumbani kwa Mungu kwa tiketi ya mlo wa bure na kujipatia nafasi, ili niweze kuwa na tumaini la kupokea baraka baadaye.” Kwa kuzingatia mtazamo wake na nia yake katika kufanya wajibu wake, imani yake kwa Mungu ni ya kutegemea fursa; amekuja nyumbani kwa Mungu ili kudoea, si kwa imani ya kweli. Mtazamo wake anapofanya wajibu wake ni wa kupuuza hasa. Ili kumtumia, kanisa linapaswa kumshawishi na kujadiliana naye, na bado, hafanyi vizuri. Je, mtu ambaye hana dhamiri anaweza kufanya wajibu wake kweli? Anajihusisha tu na kutegemea fursa na kudoea, yeye ni asiyeamini. Tukiangalia asili ya vipengele viwili vya suala hili, katika kujaribu kulitatua, je, kiongozi huyo wa uongo alielewa kiini chake? (Hapana.) Kwa kushindwa kuelewa kiini cha suala hilo, bado alimwona mtu huyu kama mwumini wa kweli, mtu asiyeelewa ukweli tu, mwenye kimo kidogo, dhaifu kwa muda na anayehitaji msaada. Kutokana na mitazamo hii, alijaribu kufanya ushirika na kusaidia, lakini akaambiwa, “Acha kuzunguza. Mafundisho hayo unayoyazungumzia hayana maana. Ninajua yote hayo, ninaelewa zaidi kuliko wewe. Je, ni mafundisho mangapi unayoyaelewa kweli? Je, una elimu ya kiwango gani? Nimesoma vitabu vingi kuliko ulivyokula milo!” Asili yake imejifunua, sivyo? Kiongozi wa uongo bado anaamini kwamba anafanya kazi, bila kutambua kwamba mtu huyu kwa kweli ni asiyeamini. Wakati wasioamini wanapofanya wajibu wao katika nyumba ya Mungu, hata kazi yao haifikii kiwango kinachohitajika. Je, watu kama hao wanapaswa kuruhusiwa kuwa karibu? (Hapana.) Kwa hivyo, hii ndiyo kanuni ya kumshughulikia mtu wa aina hii katika nyumba ya Mungu: Ikiwa anaweza na yuko tayari kufanya kazi, mruhusu awepo; ikiwa hataki, msafishe haraka, bila kumhimiza akae au kumsihi. Je, kiongozi wa uongo anajua kanuni hii? Hajui. Anawatendea wafu kana kwamba wako hai, akiwalisha na kuwapa maji; sivyo? Viongozi wa uongo hufanya mambo ya kipumbavu kama hayo.
Viongozi wa Uwongo Hawawezi Kutatua Shida na Matatizo Ambayo Watu Hukumbana Nayo Katika Kuingia Kwao Katika Uzima
Katika hali mbalimbali, watu tofauti wanapofichua hali na udhihirisho mbalimbali, viongozi wa uongo hushindwa kuelewa kiini cha ufunuo huu na hawawezi kutatua matatizo yanayotokana nao. Kwa sababu hawaelewi ukweli, huita majina kimakosa na kujihusisha na mwenendo mbaya wa kiholela, wakiwakosea wale ambao ni dhaifu kwa muda au wakati mwingine ni hasi kwa wasioamini na watu wanaomsaliti Mungu. Wakati huo huo, wale wasioamini ambao kwa juu juu wana vipawa fulani, ambao wanaweza kufanya kazi rahisi na kujitahidi, wanachukuliwa kuwa walengwa muhimu wa kuungwa mkono. Watu hawa wanaona aibu kusema moja kwa moja kutokuwa radhi kwao kufanya wajibu wao, lakini viongozi wa uongo hushindwa kung’amua hili na huendelea kuwashawishi wabaki. Viongozi wa uongo hawafanyi chochote ila kufanya vitendo vya kipumbavu; watu waovu husumbua kanisa, lakini hubaki vipofu kwa hili na hawashughulikii suala hilo. Je, huku si kujihusisha na mwenendo mbaya wa kiholela? Utendaji mbaya wa viongozi wa uongo hutokeaje? Hawana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu na hawaelewi ukweli, kwa hivyo wanapokabiliwa na hali mbalimbali, wao hugeukia mafundisho ya juu juu zaidi wanayoyaelewa, wakiyatumia mara kwa mara kwa njia ambayo hutumika tu kusababisha ukatizaji na usumbufu. Mara nyingi, sio tu kwamba wanashindwa kutatua matatizo ambayo watu hukutana nayo katika kuingia katika uzima na si tu kwamba wanashindwa kuwasaidia watu kutoka katika udhaifu hadi kuwa na uwezo, lakini pia husababisha watu kuwa na mawazo na suitafahamu kuhusu Mungu, na kuwafanya wafikiri kanisa linajaribu kuwaajiri ili watumie huduma yao, kana kwamba nyumba ya Mungu haina watu wenye talanta na hawawezi kupata watu wanaofaa. Hii ni athari mbaya inayotokana na kazi ya viongozi wa uongo. Hili hutokeaje? (Viongozi wa uongo hawawezi kuufahamu ukweli, hawaelewi ukweli, na wanapokutana na hali fulani, hutumia kanuni tu.) Hawawezi kuufahamu ukweli, wanaweza tu kukariri maneno na misemo isiyobadilika. Hawana uelewa halisi wa uzoefu na uthamini wa ukweli. Kwa hivyo, matatizo yanapotokea hatimaye, wanaweza kusema tu misemo michache mikavu: “Mpende Mungu”; “Kuweni waaminifu”; “Kuweni watiifu na wanyenyekevu mnapokabiliwa na hali”; “Fanyeni wajibu wenu vizuri”; “Mnahitaji kuwa waaminifu”; “Lazima muuasi mwili”; “Mnahitaji kujitumia kwa ajili ya Mungu.” Wanatumia mafundisho haya matupu, kauli mbiu, na misemo ili kujipamba, na pia kuwafundisha wengine, wakitumaini kuwashawishi na kuwa na athari chanya—lakini haileti matokeo yoyote, na haibadilishi chochote. Kwa hivyo, viongozi wa uongo hawawezi kukamilisha kazi yoyote. Kwa kuwa hawawezi hata kutatua matatizo ambayo watu wateule wa Mungu hukutana nayo katika kuingia katika uzima, basi wanawezaje kufanya kazi nzuri ya kuliongoza kanisa?
Watu wanapokumbana na matatizo mbalimbali katika maisha halisi na hawajui jinsi ya kuyakabili, wala jinsi ya kutenda ukweli, wanahitaji kutafuta ukweli katika maneno ya Mungu ili kutatua masuala haya. Ikiwa mtu mwenye kimo kidogo hajui jinsi ya kutafuta ukweli katika maneno ya Mungu, wala jinsi ya kupata maneno husika ya Mungu, basi anapaswa kutafuta wale wanaoelewa ukweli kwa ajili ya kufanya ushirika ili kutatua suala hilo, huku pia akiwafundisha jinsi ya kupata maneno husika ya Mungu na jinsi ya kuelewa ukweli. Hii inamaanisha kupata kutoka katika maneno ya Mungu ni kanuni na viwango vipi vya Mungu vinavyohitajika, jinsi Mungu anavyofafanua jambo hili na anachotaka kulihusu, na kama kuna maelezo yoyote mahususi yaliyoelezwa. Ikiwa maneno ya Mungu kuhusu mada hii ni rahisi kiasi, yakielezea tu kanuni bila kutoa mifano ya kina, basi unapaswa kujifunza kutafakari. Ikiwa huwezi kuyaelewa kwa kutafakari, tafuta watu zaidi wa kufanya ushirika nao, shiriki katika mikutano, na utafute huku na kule katika mchakato wa kufanya wajibu wako, upate nuru na mwangaza, na hivyo polepole uelewe kiini cha suala lililopo ni nini. Hatimaye, ingia kulingana na kanuni za maneno ya Mungu ili kufikia suluhu ya matatizo haya. Kwa mfano, baadhi ya watu ni wavivu na hawawezi kamwe kupata nguvu za kufanya wajibu wao; lakini taja kula, kunywa, na kufurahi, nao huchangamka na kujaa nguvu, kana kwamba wamechangamka ghafla. Viongozi wa uongo hutatuaje masuala kama hayo? Wao pia wana njia: kuwapa watu hawa kazi zaidi, bila kuwaacha na muda wa kufanya kazi. Je, mbinu hii inaweza kutatua tatizo? Baadhi ya watu wanasita kufanya hata kiasi kidogo cha kazi waliyopewa; wanataka tu kujinyima, wakiona ni bora kutofanya kazi yoyote! Tatizo ni nini kwa watu wavivu sana? Hili linahusiana na asili yao, kama wanapenda mambo chanya, na pia mapendeleo na shughuli zao. Kuna baadhi ya watu ambao wana sifa kidogo; ikiwa ni wafuasi wa kawaida tu bila mzigo wowote uliowekwa juu yao, hawana nguvu ya kufanya kazi yao na hawapati kupendezwa nayo. Hata hivyo, ikiwa, kulingana na ubora wao wa tabia na wajibu wanaoweza kufanya, wamepewa mzigo wa kuwa msimamizi, kuruhusiwa kushikilia cheo na kutekeleza majukumu fulani, shauku yao katika kazi huchochewa. Wakati mwingine, wanapokosa kuwajibika katika kazi yao au kuwa wavivu, wanaweza kupogolewa; wakati mwingine, wanaweza kutiwa moyo na kusifiwa. Hivyo, watu hawa, wanaojali kuonekana kwao, wanapenda hadhi, na hufurahia kusifiwa, hupata nguvu ya kufanya wajibu wao. Wanapofikiria kulegea, wanafikiria, “Kwa ajili ya hadhi, kwa ajili ya mzigo ninaoubeba, lazima nifanye vizuri.” Kwa njia hii, uvivu wa watu kama hao unaweza kutatuliwa kwa kiasi. Viongozi wa uongo wanapokutana na masuala ya aina hii yanayohusiana na ubinadamu au hali zinazohusisha kuingia katika uzima zinazotokea katika mchakato wa kufanya wajibu, wanaona kuwa magumu na changamoto sana kuyatatua. Hawajui jinsi ya kutatua hali na matatizo haya, au ni maneno gani ya Mungu ya kutumia kwa azimio lenye lengo. Mara nyingi, mbinu yao ni kuwashawishi au kuwarairai watu wafanye vizuri; ikiwa ushawishi na kurairai hakufanyi kazi, wao huamua kukasirika na kuwapogoa. Kupogoa kusipofanya kazi, wanasoma vifungu kadhaa vya maneno makali ya Mungu kama onyo, wakiwajulisha watu kwamba wanapaswa kujipanga. Ikiwa hilo bado halina matokeo, suluhisho lao la mwisho ni kupanga mtu wa kuwatunza na kuwasimamia. Wana mbinu hizi chache tu, na ikiwa hizi hazifanyi kazi, hawana chaguo lingine.
Kwa muhtasari, bila kujali tatizo ambalo viongozi wa uongo wanakabiliana nalo katika kazi yao, hawawezi kung’amua kiini cha tatizo, wanajitahidi kuelewa hali na asili halisi za watu mbalimbali, na hata zaidi hawawezi kung’amua kiini cha tatizo kilipo au wapi pa kuanzia ili kulitatua ipasavyo. Hawana kanuni na mbinu hizi za kushughulikia matatizo, kwa hivyo kazi ya viongozi wa uongo haiwezi kutatua masuala mbalimbali halisi. Wanaweza tu kuhubiri mafundisho fulani, kuropoka kauli mbiu, kufuata kanuni fulani, na kutenda kwa njia isiyo ya dhati. Watu kama hao wanawezaje kuwa na uwezo katika kazi ya uongozi wa kanisa? Haijalishi wamepata mafunzo kiasi gani au wataamini kwa miaka mingapi zaidi, hawatakuwa na uwezo katika kazi ya uongozi wa kanisa. Je, Mumekutana na mifano yoyote ya hili? (Katika kanisa letu, kulikuwa na mtu aliyekuwa akifanya kazi ya mwenyeji ambaye kila mara alitoa matamshi ya kuhukumu na kushambulia, akiathiri utendaji wetu wa wajibu na kusababisha usumbufu na misukosuko. Baada ya kuripoti hili kwa kiongozi, alisisitiza tu kwamba tujijue na tutiicmazingira yaliyowekwa na Mungu, bila kutatua tatizo halisi, ambalo liliathiri kazi ya kanisa. Ilikuwa tu baada ya mabadiliko ya uongozi ndipo tatizo lilitatuliwa.) Huu ni udhihirisho wa kawaida wa viongozi wa uongo. Huyu ni aina ya kawaida ya kiongozi wa uongo: wale ambao hawawezi kumtambua mtu mwovu au mpinga Kristo wanapokutana naye, na kuwaambia wengine wawe wavumilivu na wastahimilivu, kujifunza kutokana na uzoefu, na kumtii mtu mwovu au mpinga Kristo. Hawatambui wapinga Kristo au watu waovu, wala hawafanyi chochote kuwahusu. Baada ya ushirika mwingi kuhusu njia ambazo wapinga Kristo hujitokeza, kila mtu anayeelewa ukweli lazima sasa aweze kuwatambua wachache wao. Lakini, je, watu kama viongozi wa uongo wanaweza kutafuta jinsi ushirika huo unavyolingana na tabia ya mpinga Kristo? Je, wanaweza kuwatambua wapinga Kristo? (Hapana.) Na kitu gani kinachotokana na kutoweza kwao kuwatambua wapinga Kristo? Inawezekana kwamba mpinga Kristo atawanyang’anya mamlaka, kwamba watamruhusu mpinga Kristo atawale kanisa na, mwishowe, wasifanye chochote wakati mpinga Kristo anapoanzisha ufalme huru. Ikiwa hawawezi kumtambua mpinga Kristo, hawana njia ya kumchukulia mpinga Kristo kama adui yao na kumfichua, kumtambua, na kumkataa; ikiwa hawawezi kumtambua mpinga Kristo, kuna uwezekano mkubwa wa kumchukulia mpinga Kristo kama ndugu, kwa uvumilivu na ustahimilivu, jambo ambalo husababisha mpinga Kristo kuingia madarakani kanisani na kulidhibiti. Kwa hivyo, matokeo ya kutoweza kuwatambua wapinga Kristo ni makubwa, mabaya kupita kiasi. Viongozi wa uongo hawaelewi ukweli; hawawezi kutambua kiini cha watu wa aina tofauti. Wanachofanya ni kuhubiri maneno na mafundisho na kutumia kanuni, wakionyesha upendo kwa wote, kumwacha kila mtu atubu, na kumpa kila mtu nafasi, yeyote yule. Je, hii si njia ya makasisi wa kidini? Je, hii si njia ya Mafarisayo? Viongozi wa uongo, wanapokutana na wapinga Kristo, kwa kawaida huchagua kukubaliana na kutoa njia, hata kupata kisingizio au sababu ya kudai kuwa huku ni kuwatendea wengine kwa upendo. Wakijua kwamba mtu ni msumbufu na ni mpinga Kristo, hawathubutu kumkabili wala hawana ujasiri wa kumtambua na kumfichua; hivi ndivyo viongozi wa uongo wanavyofanya. Hata wakati baadhi ya ndugu tayari wamegundua kwamba mtu huyo ni mwovu au mpinga Kristo, viongozi wa uongo bado watasema, “Hatuwezi kuwahukumu watu au kuwashutumu kirahisi. Mtu huyo ana shauku kubwa ya kujituma na yuko tayari kulipa gharama—sio mpinga Kristo au mtu mwovu. Kwa sababu tu mtu anasema maneno machache makali haimaanishi kwamba yeye ni mwovu, sivyo?” Viongozi wa uongo hawawezi kuona kiini cha watu, wala hawawezi kuona matokeo ya matendo ya wapinga Kristo, bado wakionyesha upendo, uvumilivu, na ustahimilivu kwa wapinga Kristo, hata kuwatia moyo wapinga Kristo kutafakari, kujijua wenyewe, na kutubu kweli. Haijalishi jinsi mpinga Kristo anavyojaribu kujijua, je, asili yake inaweza kubadilika? Je, anaweza kujijua mwenyewe kweli? Hawezi kabisa. Ingawa wapinga Kristo wanaweza kuonekana kuacha mambo fulani na kujitumia kidogo juujuu, ndani yao wana matamanio na mipango mikubwa. Sababu ya viongozi wa uongo kutoweza kuwang’amua watu kama hao kuwa wapinga Kristo ni kwamba viongozi wa uongo hawaelewi ukweli, wala hawawezi kutambua aina tofauti za watu. Hawawezi kuona kiini cha asili cha watu mbalimbali, wala hawajui jinsi ya kuwatendea au kuwashughulikia watu wa aina tofauti. Wanapowaona wengine wakiwafichua wapinga Kristo, hawathubutu kujiunga nao, na wanaogopa zaidi kuchukua hatua dhidi ya wapinga Kristo, wakiogopa kulipiza kisasi ikiwa watawakosea wapinga Kristo. Mbinu yao kwa wapinga Kristo imekuwa tu kuhubiri mafundisho na kusihi. Mbali na kutoweza kuwatambua watu waovu na wapinga Kristo, viongozi wa uongo pia hawawezi kutatua masuala mbalimbali yaliyopo miongoni mwa watu wateule wa Mungu. Hili linathibitisha kwamba viongozi wa uongo hawana uelewa wa ukweli hata kidogo; hawawezi kutatua matatizo halisi na hawawezi kuwaongoza watu wateule wa Mungu kuingia katika uhakika wa ukweli. Haijalishi viongozi wa uongo wanasema au kufanya nini, hutasikia maneno yoyote ya kutia nuru yanayochochewa na kutiwa nuru na Roho Mtakatifu, sembuse kuona kwamba wana ukweli wowote halisi. Kwa hivyo, viongozi wa uongo hawaleti faida au msaada wowote katika suala la kuingia kwa watu katika uzima; kazi ndogo wanayofanya inahusisha kuhubiri maneno na mafundisho, kuropoka kauli mbiu, na kutenda kwa njia isiyo ya dhati. Wanashindwa kabisa kutimiza jukumu ambalo kiongozi anapaswa kufanya.
Huo ndio mwisho wa ushirika wetu kwa leo. Kwaherini!
Januari 9, 2021