Matamko ya Kristo Mwanzoni—Sura ya 5
Milima na mito huenda ikibadilika, vijito hutiririka kwenye mikondo yao, na maisha ya mwanadamu ni yenye uvumilivu mdogo kuliko ardhi na anga. Mwenyezi Mungu pekee ndiye maisha ya milele yaliyofufuka milele, katika vizazi viishivyo milele! Vitu vyote na matukio viko katika mikono Yake, Shetani yuko chini ya miguu Yake.
Leo hii ni kwa sababu ya uteuzi wa Mungu ulioamuliwa kabla kwamba Ametuokoa kutoka kukamatwa na Shetani. Yeye kweli ni Mkombozi wetu. Uzima wa milele wa ufufuo wa Kristo unafanyika ndani yetu, kwa hiyo tumekusudiwa kuunganishwa na maisha ya Mungu, tunaweza kuwa naye uso kwa uso, kumla, kumnywa, na kumfurahia. Huku ni kujitolea kwa Mungu kwa bidi na kusio na ubinafsi.
Majira huja na kupita, yakipitia upepo na jalidi, yakikumbana na taabu, mateso na majonzi mengi sana ya maisha, kukataliwa na kukashifiwa duniani, shutuma za visingizio za serikali, imani ya Mungu haipungui, wala azimio Lake. Kwa ukamilifu kwa ajili ya mapenzi ya Mungu, ili usimamizi wa Mungu na mpango utimizwe, Yeye huweka maisha Yake Mwenyewe kando. Kwa ajili ya watu Wake wote, Yeye haachi juhudi yoyote, akiwalisha na kunyunyizia kwa uangalifu. Haidhuru kiasi cha ujinga, tu wagumu kiasi kipi, tunahitaji tu kutii mbele Yake, na maisha ya kufufuka kwa Kristo yatabadilisha asili yetu ya zamani…. Kwa wana hawa wazaliwa wa kwanza, Yeye hufanya kazi bila kuchoka, huachilia chakula na usingizi. Ni siku ngapi mchana na usiku, ni kupitia joto ngapi kali na baridi kali, Yeye hutazama kwa moyo wote katika Sayuni.
Ulimwengu, nyumba, kazi vimeachiliwa kabisa, bila kusita, bila raha za kidunia kumgusa…. Maneno kutoka kinywa Chake yanatupiga kwa ndani, yakifunua mambo yaliofichwa kwenye kina cha mioyo yetu. Ni vipi haturidhishwi? Kila sentensi inayotoka katika kinywa Chake inatendeka wakati wowote kwetu. Kila kitendo chetu, hadharani na faraghani, hakuna ambacho Yeye hakijui, hakuna Asichokijua. Kwa kweli vyote vitafichuliwa mbele Yake, licha ya mipango yetu wenyewe na matayarisho.
Tukiwa tumeketi mbele Yake, roho zetu hufurahia, kustareheshwa na tulivu, daima kuhisi tupu ndani, kwa kweli kuwiwa kwa Mungu. Hili ni jambo la ajabu lisilofikirika na lisiloweza kufanikishwa. Roho Mtakatifu anathibitisha vya kutosha kwamba Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja wa kweli! Asiyepingika! Sisi, kundi hili la watu, kwa kweli tumebarikiwa! Kama si kwa neema ya Mungu na rehema, lazima tuangamie milele na kumfuata Shetani. Ni Mungu Mwenyezi pekee Anayeweza kutuokoa!
Ah! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo! Ni Wewe ambaye Umefungua macho yetu ya kiroho, kwamba tumeweza kuona siri za dunia ya kiroho. Mandhari ya ufalme hayana mwisho. Kuweni waangalifu na wenye kusubiri. Siku haiwezi kuwa mbali sana.
Mioto ya vita huzunguka, moshi wa bunduki huelekea, hali ya hewa huwa vuguvugu, tabia ya nchi hubadilika, tauni litaenea, na watu lazima wafariki, na tumaini ndogo la kuishi.
Ah! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo! Wewe ni mnara wetu imara. Wewe ni kimbilio letu. Sisi tunakusanyika chini ya mabawa Yako, na janga haliwezi kutufikia. Huu ni utunzaji Wako mtakatifu.
Sisi sote tunainua sauti zetu, kuimba sifa, sifa ambazo zinavuma kote Sayuni! Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo ameandaa hatima hio tukufu kwa ajili yetu. Kuwa mwangalifu—mwangalifu! Wakati hauwezi kuwa mbali sana.