Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 26

Ni nani ameshinda nyumbani Kwangu? Ni nani amesimama kwa ajili Yangu? Ni nani ameteseka kwa ajili Yangu? Ni nani ameweka ahadi yake mbele Zangu? Ni nani amenifuata hadi leo lakini hajakuwa wa kutojali? Mbona wanadamu wote wana ubaridi na hawana hisia? Mbona binadamu ameniacha? Mbona mwanadamu amechoka na Mimi? Mbona hakuna joto katika ulimwengu wa mwanadamu? Nikiwa Zayuni, Nimeonja joto lililo mbinguni, na Nikiwa Zayuni Nimefurahia baraka iliyoko mbinguni. Tena, Nimeishi miongoni mwa binadamu, Nimeuhisi uchungu ulioko katika ulimwengu wa binadamu, Nimeona kwa macho Yangu hali zote tofauti zilizopo miongoni mwa wanadamu. Bila kujua, mwanadamu amebadilika pamoja na mabadiliko Yangu, na ni katika njia hii pekee ndio amepata kufika siku ya leo. Sihitaji kwamba mwanadamu aweze kufanya chochote kwa ajili Yangu, wala Sihitaji kwamba aongeze chochote kwa mujibu Wangu. Nataka tu aweze kukubaliana na mpango Wangu, bila kutonitii ama kuwa kigezo cha aibu Kwangu, na kuwa na ushuhuda unaovuma kwa sababu Yangu. Miongoni mwa wanadamu, kumekuwa na wale ambao Wamenitolea ushuhuda mzuri na kulipa jina Langu utukufu, lakini matendo ya mwanadamu, tabia ya mwanadamu vitawezaje kuutosheleza moyo Wangu? Atawezaje kufikia matakwa Yangu ama kutimiza mapenzi Yangu? Kwa milima yote na maji katika dunia, na maua, nyasi, na miti iliyo duniani, hapana hata moja isiyoonyesha kazi ya mikono Yangu, hakuna hata moja isiyokuwepo kwa ajili ya jina Langu. Ilhali mbona mwanadamu hawezi kufikia kiwango kile Ninachohitaji? Je, inaweza kuwa kwa sababu ya hali yake ya chini mno? Je, inaweza kuwa ni kwa sababu ya kuinuliwa kwake na Mimi? Je, inaweza kuwa ni kwa sababu Mimi ni mkatili kwake? Mbona kila wakati mwanadamu ana hofu kwa sababu ya mahitaji Yangu? Leo, miongoni mwa wengi katika ufalme, ni kwa nini mnasikia tu sauti Yangu lakini hamtaki kuuona uso Wangu? Mbona mnayaangalia tu maneno Yangu bila kujaribu kuyalinganisha na Roho Wangu? Mbona mnanitofautisha juu mbinguni na chini duniani? Je, yawezekana kwamba Mimi, Nikiwa duniani, Siko sawa na Mimi niliye mbinguni? Je, yawezekana kwamba Mimi, Ninapokuwa mbinguni, Siwezi kushuka chini duniani? Je, yawezekana kwamba Mimi, Nikiwa duniani, Sistahili kuwa wa mbinguni? Ni kana kwamba Mimi, Ninapokuwa duniani, Mimi ni kiumbe duni, kana kwamba Mimi, Ninapokuwa mbinguni, Mimi ni kiumbe Aliyetukuzwa, na kama kwamba kuna shimo kubwa lisilopitika kati ya mbinguni na dunia. Lakini katika dunia ya wanadamu wanaonekana kutojua kitu chochote kuhusu asili ya vitu hivi, lakini wakati huo wote wamekuwa wakienda kinyume na Mimi, kana kwamba maneno Yangu yana sauti tu na hayana maana. Wanadamu wote wanaweka bidii kwa maneno Yangu, wakifanya uchunguzi wao kuhusu sura Yangu ya nje, lakini wote wanapata kushindwa, bila matokeo yoyote ya kuonyesha, badala yake, wanapigwa chini na maneno Yangu na hawawezi thubutu kusimama tena.

Nikiiweka imani ya binadamu katika majaribu, hakuna hata mwanadamu mmoja aliye na uwezo wa kuwa na ushuhuda wa kweli, hakuna hata mmoja anayeweza kujitoa kikamilifu; badala yake, mwanadamu anashinda akijificha na kukataa kujifungua na kuwa wazi, kana kwamba Ninaenda kuupora moyo wake. Hata Ayubu hakustahimili majaribu, wala hakufurahia katika mateso. Watu wote wanatoa dokezo iliyofifia ya kijani kibichi katika joto la majira ya kuchipua; wao hawasalii kwenye hali ya kijani kibichi chini ya mlipuko wa baridi wa majira ya baridi. Akiwa mwenye mifupa na mkonde na gofu kwa kimo, mwanadamu hawezi kutimiza nia Zangu. Katika binadamu wote, hakuna hata mmoja anayeweza kutumika kuwa mfano kwa wengine, kwa sababu wanadamu ni sawa tu, bila tofauti kati yao, na kuna kidogo kinachowatofautisha mmoja na mwingine. Kwa sababu hii, hata leo wanadamu bado hawana uwezo wa kuijua kazi Yangu. Ni wakati ambao kuadibu Kwangu kutawashukia wanadamu ndipo wanadamu, bila kujua, wataifahamu kazi Yangu, na bila Mimi kufanya lolote ama kumlazimisha yeyote, wanadamu watakuja kunijua, na hivyo kupata kuiona kazi Yangu. Huu ni mpango Wangu, ni kipengele cha kazi Yangu ambayo ni wazi, na ni kile mwanadamu lazima afahamu. Katika ufalme, vitu vingi visivyohesabika vya uumbaji vinaanza kufufuka na kupata nguvu ya maisha yao. Kwa sababu ya mabadiliko katika hali ya dunia, mipaka kati ya nchi moja na nyingine pia inaanza kusonga. Hapo awali, Nimetabiri: Wakati ardhi itagawanywa kutoka kwa ardhi, na ardhi kujiunga na ardhi, huu ndio utakuwa wakati ambao Nitayapasua mataifa kuwa vipande vidogo. Katika wakati huu, Nitafanya upya uumbaji wote na kuugawa tena ulimwengu mzima, hivyo kuweka ulimwengu katika mpangilio, Nikibadilisha hali yake ya awali kuwa mpya. Huu ndio mpango Wangu. Hizi ni kazi Zangu. Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:

Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.

Sauti Yangu inapoimarika kwa uzito, pia Ninaichunguza hali ya ulimwengu. Kupitia kwa maneno Yangu, vitu visivyohesabika vya uumbaji vyote vinafanywa upya. Mbingu inabadilika, kama ifanyavyo dunia. Binadamu wanafunuliwa wakiwa katika hali yao halisi na, polepole, kila mtu anatengwa kulingana na aina yake, na kutafuta njia bila kujua wanajipata wakirejea katika ngome za familia zao. Hii itanifurahisha sana. Niko huru kutokana na vurugu, na bila kutambulika, kazi Yangu kuu inatimizwa, na vitu visivyohesabika vya uumbaji vinabadilishwa, bila kujua. Nilipoumba ulimwengu, Niliunda kila kitu kulingana na aina yake, Nikiweka vitu vyote vilivyo na maumbo pamoja na mifano zao. Wakati mpango wa usimamizi Wangu unapokaribia tamati, Nitarejesha hali ya awali ya uumbaji, Nitarejesha kila kitu kiwe katika hali ya awali, Nikibadilisha kila kitu kwa namna kubwa, ili kila kitu kirudi ndani ya mpango Wangu. Muda umewadia! Hatua ya mwisho katika mpango Wangu iko karibu kutimika. Ah, dunia ya kitambo yenye uchafu! Kwa hakika mtaanguka chini kwa maneno Yangu! Kwa hakika mtafanywa kuwa bure kwa mujibu wa mpango Wangu! Ah, vitu visivyo hesabika vya uumbaji! Wote mtapata maisha mapya katika maneno Yangu—utapata uhuru wako Bwana Mkuu! Ah, dunia mpya, safi isiyo na uchafu! Kwa kweli mtafufuka katika utukufu Wangu! Ah Mlima Zayuni! Usiwe kimya tena. Nimerudi kwa ushindi! Kutoka miongoni mwa uumbaji, Ninaichunguza dunia nzima. Duniani, wanadamu wameanza maisha mapya, wameshinda tumaini mpya. Ah, watu Wangu! Mtakosaje kurudi kwa maisha ndani ya mwanga Wangu? Mtakosaje kuruka kwa furaha chini ya uongozi Wangu? Ardhi zinapiga kelele kwa furaha, maji yanapiga kelele kali na vicheko vya furaha! Ah, Israeli iliyofufuka! Mtakosaje kuhisi fahari kwa mujibu wa majaaliwa Yangu? Ni nani amelia? Ni nani ameomboleza? Israeli ya kitambo haiko tena, na Israeli ya leo imeamka, imara na kama mnara, katika dunia, imesimama katika mioyo ya binadamu wote. Israeli ya leo kwa hakika itapata chanzo cha uwepo kupitia kwa watu Wangu! Ah, Misri yenye chuki! Hakika, bado hamsimami dhidi Yangu? Mnawezaje kuichukulia huruma Yangu kimzaha na kujaribu kuepuka kuadibu Kwangu? Mtakosaje kuwa katika kuadibu Kwangu? Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, ghadhabu, na kuadibu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!

Machi 29, 1992

Iliyotangulia: Furahini, Enyi Watu Wote!

Inayofuata: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 29

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp