Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, ambayo ina maana kwamba kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa ni kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu wakati mwanadamu alipopotoshwa. Kwa maneno mengine, usimamizi wa Mungu kwa mwanadamu ulianza kutokana na kazi ya kumwokoa mwanadamu, na wala haukutokana na kazi ya kuiumba dunia. Hakungekuwa na kazi ya kumsimamia mwanadamu pasipo kuwepo na tabia potovu ya mwanadamu, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu ina sehemu tatu, badala ya hatua nne, au enzi nne. Hii tu ndio njia sahihi ya kutaja kazi ya Mungu ya usimamizi wa mwanadamu. Enzi ya mwisho itakapofikia kikomo, kazi ya kumsimamia mwanadamu itakuwa imekamilika. Hitimisho la kazi ya usimamizi lina maana kuwa kazi ya kuwaokoa wanadamu wote imekamilika kabisa, na kwamba mwanadamu amefika mwisho wa safari yake. Bila kazi ya kuwaokoa wanadamu wote, kazi ya kuwasimamia wanadamu isingekuwepo, wala kusingekuwa na hatua tatu za kazi. Ilikuwa ni hasa kwa ajili ya upotovu wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu alihitaji wokovu kwa dharura, ndipo Yehova alihitimisha uumbaji wa dunia na kuanza kazi ya Enzi ya Sheria. Hapo tu ndipo kazi ya kumsimamia mwanadamu ilipoanza, kumaanisha kwamba hapo tu ndipo kazi ya kumwokoa mwanadamu ilipoanza. “Kumsimamia mwanadamu” haimaanishi kuongoza maisha ya mwanadamu aliyeumbwa upya duniani (ambayo ni kusema, mwanadamu ambaye alikuwa bado hajapotoshwa). Badala yake, ni wokovu wa mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani, ambapo ni kusema kwamba, ni kubadilishwa kwa mwanadamu aliyepotoshwa. Hii ndiyo maana ya kumsimamia mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu haihusishi kazi ya kuiumba dunia, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu haijumuishi kazi ya kuumba ulimwengu, na inahusisha tu hatua tatu za kazi zilizo tofauti na uumbaji wa ulimwengu. Ili kuelewa kazi ya kumsimamia mwanadamu, ni muhimu kuwa na ufahamu wa historia ya hatua tatu za kazi—hili ndilo jambo ambalo kila mtu anapaswa kulifahamu ili uweze kuokolewa. Kama viumbe wa Mungu, mnapaswa kutambua kuwa mwanadamu aliumbwa na Mungu, na unapaswa kufahamu chanzo cha upotovu wa mwanadamu, na, vilevile, kufahamu mchakato wa wokovu wa mwanadamu. Iwapo mnafahamu tu jinsi ya kutenda kulingana na mafundisho ili kupata neema ya Mungu, lakini hamna kidokezo kuhusu jinsi Mungu anavyomwokoa mwanadamu, au kuhusu chanzo cha upotovu wa mwanadamu, basi hili ndilo mnalokosa kama viumbe wa Mungu. Hupaswi kuridhika tu na kuelewa ukweli unaoweza kuwekwa katika vitendo, huku ukibakia kutojua upeo mpana wa kazi ya usimamizi ya Mungu—kama hivi ndivyo ilivyo, basi wewe ni mbishi sana. Hatua tatu za kazi ya Mungu ni hadithi za ndani za usimamizi wa Mungu wa mwanadamu, ni ujio wa injili ya ulimwengu mzima, ni fumbo kuu kati ya wanadamu wote, na pia ni msingi wa kueneza injili. Ikiwa utazingatia tu kuelewa kweli rahisi zinazohusiana na maisha yako, na hujui chochote kuhusu hili, siri kubwa zaidi ya zote na maono, basi je, maisha yako si sawa na bidhaa yenye kasoro, isiyofaa isipokuwa tu kutazamwa?
Ikiwa mwanadamu anazingatia tu utendaji, na kuiona kazi ya Mungu na maarifa ya mwanadamu kuwa kitu kisicho cha msingi, basi je, si hii ni sawa na kuzingatia mambo yasiyo muhimu huku akipuuza mambo yaliyo muhimu zaidi? Yale ambayo ni lazima uyajue, lazima uyajue, na yale ambayo ni lazima uyaweke katika vitendo, lazima uyaweke katika vitendo. Hapo tu ndipo utakuwa mtu anayejua jinsi ya kufuatilia ukweli. Siku yako ya kueneza injili itakapowadia, ikiwa utaweza kusema tu kuwa Mungu ni Mkuu na Mwenye haki, kuwa ni Mungu Mkuu, Mungu ambaye hakuna mwanadamu yeyote aliye mkuu anayeweza kulinganishwa Naye, na kwamba Yeye ni Mungu ambaye hakuna aliye juu Yake…, ikiwa unaweza tu kusema maneno haya yasiyo muhimu na ya juu juu, na huwezi kabisa kusema maneno yenye umuhimu zaidi, na yaliyo na kiini, kama huna lolote la kusema kuhusu kumjua Mungu, ama kazi ya Mungu, na zaidi ya hapo, huwezi kuelezea ukweli, au kutoa kile ambacho kinakosekana kwa mwanadamu, basi mtu kama wewe hana uwezo wa kutekeleza wajibu wake vyema. Kumshuhudia Mungu na kueneza injili ya ufalme si jambo rahisi. Lazima kwanza uwe na ukweli, na maono yatakayoeleweka. Unapokuwa na uwazi wa maono na ukweli wa masuala tofauti ya kazi ya Mungu, moyoni mwako unapata kujua kazi ya Mungu, na bila kujali anayoyafanya Mungu—iwe ni hukumu ya haki ama kusafishwa kwa mwanadamu—unamiliki maono makuu kama msingi wako, na unamiliki ukweli sahihi wa kuweka katika vitendo, basi utaweza kumfuata Mungu hadi mwisho. Lazima ujue kwamba bila kujali kazi ambayo Yeye anafanya, lengo la kazi ya Mungu halibadiliki, kiini cha kazi Yake hakibadiliki, na mapenzi Yake kwa mwanadamu hayabadiliki. Bila kujali maneno Yake ni makali kiasi gani, haijalishi mazingira ni mabaya kiasi gani, kanuni za kazi Yake, na nia Yake ya kumwokoa mwanadamu haitabadilika. Kama tu si kazi ya ufunuo wa matokeo ya mwanadamu au hatima ya mwanadamu, na si kazi ya awamu ya mwisho, au kazi ya kuleta mpango mzima wa usimamizi wa Mungu katika mwisho wake, na kama tu ni wakati Anapofanya kazi kwa mwanadamu, basi basi kiini cha kazi Yake hakitabadilika: Daima kitakuwa wokovu wa mwanadamu. Hili linapaswa kuwa msingi wa imani yenu katika Mungu. Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na mahitaji ya mwanadamu. Mara tu unapofahamu lengo la hatua hizi tatu za kazi, basi utafahamu jinsi ya kuthamini umuhimu wa kila hatua ya kazi, na utatambua jinsi ya kutenda ili kutosheleza shauku ya Mungu. Iwapo utaweza kufikia hatua hii, basi hili, ono kubwa kuliko yote, litakuwa msingi wa imani yako katika Mungu. Hupaswi kutafuta tu njia rahisi za kutenda au ukweli wa kina, lakini unapaswa kuunganisha maono na matendo, ili kwamba kuwe na ukweli unaoweza kuwekwa kwenye vitendo, na maarifa yaliyo na msingi wa maono. Ni hapo tu ndipo utakapokuwa mtu anayefuatilia ukweli.
Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani ya hizo kumeonyeshwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu; wale wanaoshikilia tu imara mafundisho ya dini yanayosalia kutoka katika hatua moja ya kazi ni watu wanaomwekea Mungu mipaka kwa mafundisho ya dini, na ni wale ambao imani yao kwa Mungu haina udhahiri na uhakika. Watu kama hao kamwe hawawezi kupokea wokovu wa Mungu. Ni hatua tatu tu za kazi ya Mungu zinazoweza kuonyesha kabisa ukamilifu wa tabia ya Mungu, na kuonyesha kabisa nia ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu wote, na mchakato mzima wa wokovu wa mwanadamu. Huu ni uthibitisho kwamba Amemshinda Shetani na kuwapata wanadamu; ni uthibitisho wa ushindi wa Mungu, na ni maonyesho ya tabia kamili ya Mungu. Wale wanaoelewa hatua moja tu kati ya hatua tatu za kazi ya Mungu wanajua tu sehemu ya tabia ya Mungu. Katika dhana za mwanadamu, ni rahisi kwa hatua hii moja ya kazi kuwa mafundisho ya kidini, na kuna uwezekano zaidi kwamba mwanadamu ataweka kanuni zisizobadilika kuhusu Mungu, na kutumia sehemu hii moja ya tabia ya Mungu kama kiwakilishi cha tabia nzima ya Mungu. Zaidi ya hayo, mawazo mengi ya mwanadamu yamechanganyika ndani, kiasi kwamba mwanadamu anaweka vizuizi thabiti kwa tabia, nafsi, na hekima ya Mungu, pamoja na kanuni za kazi ya Mungu, ndani ya vigezo vyenye mipaka, akiamini kwamba, kama Mungu alikuwa hivi wakati moja, basi Ataendelea kuwa hivyohivyo daima, na kamwe Hatabadilika. Ni wale tu wanaojua na kuthamini hatua tatu za kazi ndio wanaoweza kumjua Mungu kabisa na kwa usahihi. Angalau, hawatamfafanua Mungu kama Mungu wa Waisraeli, ama Wayahudi, na hawatamwona kama Mungu ambaye atasulubishwa msalabani milele kwa ajili ya mwanadamu. Kama utakuja kumjua Mungu kutokana na hatua moja tu ya kazi Yake, basi maarifa yako ni kidogo sana. Maarifa yako ni sawa na tone moja katika bahari. Kama sivyo, ni kwa nini walinzi wengi wa kidini wa zamani walimtundika Mungu msalabani Akiwa hai? Je, si kwa sababu mwanadamu anamwekea Mungu mipaka kwenye vigezo fulani? Je, watu wengi hawampingi Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu hawajui kazi mbalimbali na tofauti za Mungu, na, zaidi ya hayo, kwa sababu wanamiliki maarifa na mafundisho duni ya kupima kazi ya Roho Mtakatifu? Ingawa uzoefu wa watu kama hawa ni wa juujuu tu, ni wenye kiburi na wasiojizuia katika asili yao, na wanaichukulia kazi ya Roho Mtakatifu kwa dharau, wanapuuza nidhamu ya Roho Mtakatifu na, hata zaidi, wanatumia hoja zao ndogo ndogo za zamani ili kuthibitisha kazi ya Roho Mtakatifu. Pia wanajifanya, na wanashawishika kabisa na elimu yao na maarifa yao, na kuwa wanaweza kusafiri duniani kote. Je, watu hawa si ni wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na je, si wataondolewa na enzi mpya? Je, si wale wanaokuja mbele za Mungu na kumpinga waziwazi ni watu wajinga na wabaya wasio na ufahamu wa kutosha, ambao wanajaribu tu kuonyesha jinsi walivyo werevu? Wakiwa na maarifa kidogo tu ya Biblia, wanajaribu kutawala “taaluma” ya ulimwengu; kwa mafundisho ya juujuu ya dini ili kuwafundisha watu, wanajaribu kurudisha nyuma kazi ya Roho Mtakatifu, na kujaribu kuifanya izunguke kwenye mchakato wa mawazo yao wenyewe. Kwa kuwa hawaoni mbali, wanajaribu kutazama kwa mtazamo mmoja miaka 6,000 ya kazi ya Mungu. Watu hawa hawana mantiki yoyote hata kidogo! Kwa kweli, kadri maarifa ya watu kumhusu Mungu yanavyozidi kuwa mengi, ndivyo uwezekano wao wa kuhukumu kazi ya Mungu unavyokuwa mdogo. Zaidi ya hayo, wanazungumza tu kidogo kuhusu ufahamu wao wa kazi ya sasa ya Mungu, lakini hawafanyi hukumu za kiholela. Kadiri watu wanavyojua kidogo kumhusu Mungu, ndivyo wanavyokuwa na kiburi na wenye kujiamini kupita kiasi, na ndivyo wanavyozidi kutangaza hovyo jinsi Mungu alivyo—lakini wanazungumza tu kuhusu nadharia, na hawatoi ushahidi wowote wa kweli. Watu kama hao ndio wasio na thamani yoyote kabisa. Wale wanaoichukulia kazi ya Roho Mtakatifu kama mzaha ni wapuuzi! Wale wasio waangalifu wanapokumbana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu, ambao wanakimbilia kupayuka, ambao ni wepesi kuhukumu, ambao wanaruhusu silika yao ya asili ikane haki ya kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao pia wanaitukana na kuikufuru—je, watu kama hawa wasio na heshima si ni wale wasiojua kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu? Je, si wao ndio, hata zaidi, watu wenye kiburi kikubwa, watu ambao kwa asili wana majivuno na wasioweza kutawaliwa? Hata ikiwa siku itakuja ambapo watu hawa watakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, bado Mungu hatawavumilia. Sio tu kwamba wanawadharau wale wanaomfanyia Mungu kazi, bali pia wanamkufuru Mungu Mwenyewe. Watu kama hawa wasio na matumaini hawatasamehewa, katika enzi hii ama enzi itakayokuja na wataangamia kuzimuni milele! Watu kama hawa wasio na heshima, wenye kujifurahisha, wanajifanya kuwa wanamwamini Mungu, na kadiri wanavyozidi kufanya hivyo, ndivyo wanavyozidi kukosea amri za utawala wa Mungu. Je, wale wote wenye kiburi ambao kiasili hawazuiliki, na hawajawahi kumtii yeyote, si wote wanatembea kwenye njia hii? Je, hawampingi Mungu siku baada ya siku, Yeye ambaye daima ni mpya na wala Hazeeki? Leo, mnapaswa kuelewa kwa nini ni lazima mjue umuhimu wa hatua tatu za kazi ya Mungu. Maneno Ninayosema yana manufaa kwenu, wala si mazungumzo ya bure. Ukiyasoma tu kama mtu anayetazama na kupendezwa na maua huku ukipita mbio juu ya farasi, je, si bidii Yangu yote itakuwa kazi bure? Kila mmoja wenu anapaswa kujua asili yake. Wengi wenu ni hodari katika mabishano, majibu ya maswali ya nadharia yanatoka kinywani mwenu, lakini hamna la kusema kwa maswali kuhusu dutu. Hadi leo, bado mnashiriki mazungumzo ya kipuuzi, yasiyoweza kubadilisha asili yenu ya zamani, na wengi wenu hamna nia ya kubadilisha njia ambayo mnafuata ili kupata ukweli wa hali ya juu, mnaishi tu maisha yenu kwa shingo upande. Je, watu kama hao wanawezaje kumfuata Mungu hadi mwisho? Hata ikiwa mtafika mwishoni mwa safari, itakuwa na faida gani kwenu? Ni bora mbadili mawazo yenu kabla hamjachelewa, ama mfuatilie ukweli, au vinginevyo mjiondoe mapema. Kadri muda unavyokwenda utakuwa kimelea ambaye anaishi bila chochote—je, mko tayari kutekeleza jukumu kama hili la hali ya chini na lenye aibu?
Hatua tatu za kazi ni rekodi ya kazi nzima ya Mungu, ni rekodi ya wokovu wa Mungu kwa wanadamu, na si hadithi tu. Kama kweli mnataka kutafuta kujua tabia yote ya Mungu, basi ni lazima mfahamu hatua tatu za kazi zinazofanywa na Mungu, na, hata zaidi, hampaswi kuacha hatua yoyote. Hiki ndicho kiwango cha chini kinachopaswa kufikiwa na wale wanaotafuta kumjua Mungu. Mwanadamu mwenyewe hawezi kuvumbua maarifa ya Mungu. Si kitu ambacho mwanadamu mwenyewe anaweza kufikiria, wala si matokeo ya upendeleo maalum wa Roho Mtakatifu unaotolewa kwa mtu mmoja. Badala yake, ni maarifa yanayotokea mwanadamu anapopitia kazi ya Mungu, na ni maarifa ya Mungu yanayotokana tu na mwanadamu kupitia ukweli wa kazi ya Mungu. Maarifa kama haya hayawezi kufikiwa kwa ghafla, wala si jambo linaloweza kufundishwa. Inahusiana kabisa na uzoefu wa kibinafsi. Wokovu wa Mungu wa mwanadamu ndiyo kiini cha hatua hizi tatu za kazi, ilhali katika kazi ya wokovu kumejumuishwa mbinu kadhaa za kufanya kazi na namna ambavyo tabia ya Mungu imeonyeshwa. Hili ndilo jambo gumu sana kwa mwanadamu kutambua na kwa mwanadamu kuelewa. Mgawanyiko wa enzi, mabadiliko ya kazi ya Mungu, mabadiliko katika eneo la kazi, mabadiliko ya wanaopokea kazi na kadhalika—haya yote yamejumuishwa katika hatua tatu za kazi. Hasa, tofauti katika njia ya Roho Mtakatifu kufanya kazi, pamoja na mabadiliko katika tabia ya Mungu, sura, jina, utambulisho, au mabadiliko mengine, yote ni sehemu ya hatua tatu za kazi. Hatua moja ya kazi inaweza tu kuwakilisha sehemu moja, na imewekewa mipaka ndani ya wigo fulani. Haihusiani na mgawanyiko wa enzi, ama mabadiliko ya kazi ya Mungu, wala masuala mengine. Huu ni ukweli ulio wazi. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo ukamilifu wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu lazima ajue kazi ya Mungu, tabia ya Mungu katika kazi ya wokovu, na bila ukweli huu, maarifa yako kumhusu Mungu yatakuwa tu maneno matupu, ni mahubiri ya starehe tu. Maarifa kama haya hayawezi kumshawishi au kumshinda mtu, maarifa kama haya yako nje ya uhalisi, na si ukweli. Yanaweza kuwa mengi, na mazuri masikioni, lakini kama hayaambatani na tabia ya asili ya Mungu, basi Mungu hatakusamehe. Sio tu kwamba Hatayasifu maarifa yako, bali pia Atakuadhibu kwa kuwa wewe ni mtenda dhambi ambaye umemkufuru. Maneno ya kumjua Mungu hayazungumzwi kwa mzaha. Ingawa unaweza kuwa na ulimi laini wenye maneno matamu, na ingawa maneno yako ni yenye busara kiasi kwamba unaweza kubishana kitu kisichowezekana, bado huna elimu ya kuzungumza kuhusu maarifa ya Mungu. Mungu si mtu ambaye unaweza kumhukumu kwa pupa, ama kumsifu bila mpangilio, ama kumdharau bila kujali. Unamsifu mtu yeyote na kila mmoja, lakini unatatizika kupata maneno sahihi ya kuelezea neema kuu ya Mungu—hili ndilo ambalo kila aliyeshindwa anajifunza. Ingawa kuna wataalam wengi wa lugha wanaoweza kumwelezea Mungu, usahihi wa kile wanachoelezea ni asilimia moja tu ya ukweli unaozungumzwa na watu wa Mungu, watu ambao wana misamiati michache tu, lakini wana uzoefu mwingi wa kurejelea. Hivyo inaweza kuonekana kwamba maarifa ya Mungu yapo katika usahihi na vitendo, na wala si katika utumiaji mzuri wa maneno au misamiati mingi, na kwamba maarifa ya mwanadamu na maarifa ya Mungu hayahusiani kabisa. Somo la kumjua Mungu liko juu zaidi kuliko sayansi yoyote ya asili ya wanadamu. Ni somo linaloweza kufikiwa tu na idadi ndogo sana ya watu wanaotafuta kumjua Mungu, na haliwezi kufikiwa na mtu yeyote tu mwenye kipaji. Kwa hivyo hampaswi kuona kumjua Mungu na kufuatilia ukweli kana kwamba ni vitu ambavyo vinaweza kufikiwa hata na mtoto mdogo tu. Pengine umefanikiwa kikamilifu katika maisha yako ya kifamilia, ama kazi yako, ama katika ndoa yako, lakini inapofika kwenye ukweli, na somo la kumjua Mungu, huna lolote la kujivunia, hujatimiza malengo yoyote. Kuweka ukweli katika vitendo, inaweza kusemwa, ni jambo gumu kwenu, na kumjua Mungu ni tatizo kubwa hata zaidi. Hili ni tatizo lenu, na pia ni tatizo linalokabiliwa na wanadamu wote. Kati ya wale wenye mafanikio katika kumjua Mungu, karibu wote hawajafikia kiwango. Mwanadamu hajui maana ya kumjua Mungu, ama kwa nini ni muhimu kumjua Mungu, ama ni kiwango gani ambacho ni lazima mtu afikie ili aweze kumjua Mungu. Hiki ndicho kinachowachanganya sana wanadamu, na ni kitendawili kikubwa zaidi kinachokabiliwa na wanadamu—na hakuna anayeweza kujibu swali hili, wala aliye tayari kujibu swali hili, kwa sababu, hadi leo, hakuna kati ya wanadamu aliyefanikiwa katika kusomea kazi hii. Pengine, kitendawili cha hatua tatu za kazi kitakapofanywa kijulikane kwa wanadamu, kutatokea kwa mfululizo kundi la watu wenye vipaji wanaomjua Mungu. Bila shaka, Natumaini kuwa hivyo ndivyo ilivyo, na, hata zaidi, Niko katika harakati za kutekeleza kazi hii, na Ninatumaini kuona kujitokeza kwa vipaji zaidi kama hivi katika siku za hivi karibuni. Watakuja kuwa wale wanaoshuhudia ukweli wa hatua hizi tatu za kazi, na, bila shaka, watakuwa pia wa kwanza kushuhudia hizi hatua tatu za kazi. Lakini hakuna kitu ambacho kingekuwa cha kuhuzunisha na kusikitisha zaidi ikiwa watu kama hao wenye talanta hawatatokea siku ambayo kazi ya Mungu itafika mwisho, au ikiwa kuna mtu mmoja au wawili tu kama hao ambao wamekubali kibinafsi kufanywa wakamilifu na Mungu mwenye mwili. Ingawa, hii pekee ndio hali mbaya zaidi. Kwa vyovyote vile, Ninatumai kuwa wale wote wanaotafuta kwa kweli wanaweza kupata baraka hii. Tangu mwanzo wa wakati, hakujawahi kuwa na kazi kama hii, kazi kama hiyo haijawahi kutokea katika historia ya maendeleo ya mwanadamu. Kama kweli unaweza kuwa mmoja wa wale wa kwanza wanaomjua Mungu, je, si hii itakuwa heshima ya juu kuliko viumbe vyote vilivyoumbwa? Je, kuna kiumbe mwingine kati ya wanadamu anayeweza kusifiwa na Mungu zaidi? Kazi kama hii ni ngumu kutekeleza, lakini mwishowe bado itatoa matokeo. Bila kujali jinsia au utaifa wao, wale wote wenye uwezo wa kufikia maarifa ya Mungu, mwishowe, watapokea heshima kuu ya Mungu, na watakuwa tu wenye kumiliki mamlaka ya Mungu. Hii ndiyo kazi ya leo, na pia ndiyo kazi ya siku za usoni; ni kazi ya mwisho na ya juu zaidi kukamilishwa katika miaka 6,000 ya kazi, na ni njia ya kufanya kazi ambayo inafichua kila aina ya mwanadamu. Kupitia kazi ya kumfanya wanadamu amjue Mungu, madaraja tofauti ya mwanadamu yanadhihirishwa: Wale wanaomjua Mungu wamehitimu kupokea baraka za Mungu na kupokea ahadi zake, wakati wale wasiomjua Mungu hawajahitimu kupokea baraka za Mungu wala kupokea ahadi zake. Wale wanaomjua Mungu ni wandani wa Mungu, na wale wasiomjua Mungu hawawezi kuitwa wandani wa Mungu; wandani wa Mungu wanaweza kupokea baraka zozote za Mungu, lakini wale wasio wandani wa Mungu hawastahili kazi Yake yoyote. Iwe ni dhiki, usafishaji, au hukumu, mambo haya yote ni kwa ajili ya kumruhusu mwanadamu mwishowe aweze kufikia maarifa ya Mungu, na ili mwanadamu aweze kumtii Mungu. Hii ndiyo athari pekee ambayo hatimaye itapatikana. Hakuna chochote katika hatua tatu za kazi kilichofichwa, na hii ni ya manufaa kwa maarifa ya mwanadamu juu ya Mungu, na inamsaidia mwanadamu kupata maarifa kamili na ya kina zaidi kuhusu Mungu. Kazi hii yote ni ya manufaa kwa mwanadamu.
Kazi ya Mungu Mwenyewe ni maono ambayo mwanadamu lazima ayafahamu, kwa kuwa kazi ya Mungu haiwezi kutekelezwa na mwanadamu, wala haimilikiwi na mwanadamu. Hatua tatu za kazi ndizo ukamilifu wa usimamizi wa Mungu, na hakuna ono kuu kuliko hili linalopaswa kufahamika kwa mwanadamu. Kama mwanadamu hafahamu maono haya makuu, basi si rahisi kumjua Mungu, na si rahisi kujua mapenzi ya Mungu, na, zaidi ya hayo, njia ambayo mwanadamu anapitia itazidi kuwa ngumu. Bila maono, mwanadamu hangeweza kufika umbali huu. Ni maono ambayo yamemlinda mwanadamu hadi leo, na ambayo yamempa mwanadamu ulinzi mkubwa zaidi. Katika siku za usoni, maarifa yenu lazima yawe ya kina, na ni lazima mfahamu mapenzi Yake yote na kiini cha kazi Yake yenye hekima katika hatua tatu za kazi. Hiki tu ndicho kimo chenu cha kweli. Hatua ya kazi ya mwisho haisimami peke yake, ila ni sehemu ya yote iliyounganishwa pamoja na hatua mbili za awali, ambayo ni kusema kwamba haiwezekani kukamilisha kazi nzima ya wokovu kwa kufanya kazi ya hatua moja pekee. Ingawa hatua ya mwisho ya kazi inaweza kumwokoa mwanadamu kikamilifu, hii haimaanishi kwamba ni muhimu tu kutekeleza hatua hii pekee, na kwamba hatua mbili za hapo awali hazihitajiki kumwokoa mwanadamu kutokana na ushawishi wa Shetani. Hakuna hatua moja kati ya zote tatu inayoweza kuwekwa kama maono ya pekee ambayo ni lazima yajulishwe kwa wanadamu wote, kwa kuwa ukamilifu wa kazi ya wokovu ni hatua tatu za kazi, wala si hatua moja kati ya tatu. Maadamu kazi ya wokovu bado haijakamilishwa, usimamizi wa Mungu hautaweza kufikia mwisho kamili. Nafsi ya Mungu, tabia, na hekima zimeonyeshwa kikamilifu katika kazi ya wokovu, wala hazikufichuliwa kwa mwanadamu hapo mwanzo, lakini zimeonyeshwa hatua kwa hatua katika kazi ya wokovu. Kila hatua ya kazi ya wokovu huonyesha sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya nafsi Yake: hakuna hatua moja ya kazi inayoweza moja kwa moja na kwa ukamilifu kuonyesha nafsi yote ya Mungu. Kwa hivyo, kazi ya wokovu inaweza tu kuhitimishwa kikamilifu pale tu hatua tatu za kazi zitakapokamilika, na hivyo, maarifa ya mwanadamu ya ukamilifu wa Mungu hayawezi kutenganishwa na hatua tatu za kazi ya Mungu. Kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa hatua moja ya kazi ni tabia ya Mungu inayoonyeshwa katika sehemu moja tu ya kazi yake. Haiwezi kuwakilisha tabia na nafsi inayoonyeshwa katika hatua ya awali na ijayo. Hii ni kwa sababu kazi ya kumwokoa mwanadamu haiwezi kumalizika mara moja katika kipindi kimoja, ama katika eneo moja, lakini inakuwa ya kina hatua kwa hatua kulingana na kiwango cha ukuaji wa mwanadamu katika wakati na maeneo tofauti. Ni kazi inayofanywa hatua kwa hatua, na haikamilishwi katika hatua moja. Kwa hivyo, hekima yote ya Mungu inadhihirishwa katika hatua tatu, badala ya hatua moja. Nafsi yake yote na hekima yake yote zimewekwa wazi katika hatua hizi tatu, na kila hatua ina nafsi Yake, na ni rekodi ya hekima ya kazi Yake. Mwanadamu anapaswa kujua tabia yote ya Mungu iliyoonyeshwa katika hatua hizi tatu. Nafsi hii ya Mungu ndiyo ina maana zaidi kwa wanadamu wote, na ikiwa watu hawana maarifa haya wanapomwabudu Mungu, basi hawana tofauti na wale wanaomwabudu Budha. Kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu haijafichwa kwa mwanadamu, na inapaswa kujulikana na wale wote wanaomwabudu Mungu. Kwa sababu Mungu ametekeleza hatua tatu za kazi ya wokovu kati ya wanadamu, mwanadamu anapaswa kujua maonyesho ya kile Anacho na Alicho wakati wa hatua hizi tatu za kazi. Hili ndilo ambalo ni lazima lifanywe na mwanadamu. Kile ambacho Mungu anaficha kwa mwanadamu ni kile ambacho mwanadamu hawezi kutimiza, na kile ambacho mwanadamu hapaswi kujua, lakini yale ambayo Mungu anamfunulia mwanadamu ni yale ambayo mwanadamu anapaswa kujua na yale ambayo mwanadamu anapaswa kumiliki. Kila moja ya hatua tatu za kazi huendelea juu ya msingi wa hatua iliyopita; haitekelezwi peke yake, ikitofautishwa na kazi ya wokovu. Ingawa kuna tofauti kubwa katika enzi na aina ya kazi ambayo inafanywa, katika kiini chake bado ni wokovu wa mwanadamu, na kila hatua ya kazi ya wokovu ni ya kina kuliko iliyopita. Kila hatua ya kazi inaendelea kutoka kwa msingi wa hatua iliyopita, ambayo haijafutwa. Kwa njia hii, katika kazi Yake ambayo daima ni mpya na haijazeeka, Mungu mara kwa mara anaonyesha vipengele vya tabia Yake ambavyo havijawahi kuonyeshwa kwa mwanadamu hapo awali, na daima Anamfichulia mwanadamu kazi Yake mpya, na nafsi Yake mpya, na hata ingawa wazoefu wakongwe wa kidini wanafanya wawezavyo ili kupigana na hili, na kulipinga waziwazi, Mungu daima hufanya kazi mpya ambayo anakusudia kufanya. Kazi Yake daima hubadilika, na kwa sababu hii, daima inakabiliwa na upinzani wa mwanadamu. Kwa hivyo, pia, tabia Yake inabadilika daima, na vilevile enzi na wanaopokea kazi Yake. Zaidi ya hayo, kila mara Yeye hufanya kazi ambayo haijawahi kufanywa hapo awali, hata kutekeleza kazi ambayo inaonekana kwa mwanadamu kuwa inakinzana na kazi iliyofanywa hapo awali, inayoenda kinyume nayo. Mwanadamu anaweza tu kukubali aina moja ya kazi, au njia moja ya utendaji, na ni vigumu kwa mwanadamu kukubali kazi, au njia za utendaji, ambazo zipo kinyume nao, au za juu zaidi kuwaliko. Lakini Roho Mtakatifu daima anafanya kazi mpya, na hivyo kunatokea kundi baada ya kundi la wataalamu wa kidini wanaoipinga kazi mpya ya Mungu. Watu hawa wamekuwa wataalamu hasa kwa sababu mwanadamu hana maarifa ya jinsi Mungu huwa mpya wala hazeeki, na zaidi ya hayo, hana maarifa ya kanuni za kazi ya Mungu, na hata zaidi hawana maarifa ya njia nyingi ambazo Mungu anamwokoa mwanadamu. Kwa hivyo, mwanadamu hawezi kabisa kujua kama ni kazi inayotoka kwa Roho Mtakatifu, na kama ni kazi ya Mungu Mwenyewe. Watu wengi wanashikilia mtazamo ambao, kama kitu kinalingana na maneno yaliyokuja kabla, basi wanaweza kuikubali, na kama kuna tofauti zozote na kazi ya awali, basi wanaipinga na kuikataa. Je, ninyi nyote leo hamfuati kanuni kama hizi? Hatua tatu za kazi ya wokovu hazijawa na athari kubwa kwenu, na kuna wale wanaoamini kuwa hatua mbili za kazi zilizopita ni mzigo wasiohitaji kuujua. Wanafikiria kuwa hatua hizi hazifai kutangazwa kwa umati na zinafaa kufutwa haraka iwezekanavyo, ili watu wasihisi kwamba wamezidiwa na hatua mbili za awali kwa zile hatua tatu za kazi. Wengi wanaamini kuwa kuzifanya hatua mbili za kazi zilizopita zijulikane ni hatua ya mbali sana, wala haina faida yoyote katika kumjua Mungu—hivyo ndivyo mnavyofikiria. Leo, ninyi nyote mnaamini kuwa ni sawa kutenda kwa njia hii, lakini kuna siku itafika ambapo mtagundua umuhimu wa kazi Yangu: Mtajua kuwa Sifanyi kazi yoyote ambayo haina umuhimu. Kwa sababu Ninawatangazia hatua tatu za kazi, kwa hivyo lazima ziwe na faida kwenu; kwa sababu hatua hizi tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, lazima ziwe lengo la kila mtu katika ulimwengu wote. Siku moja, nyote mtagundua umuhimu wa kazi hii. Mjue kwamba mnapinga kazi ya Mungu, au mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa umakini wa kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kizuizi kwa kazi ya Roho Mtakatifu kumesababishwa na dhana zenu na kiburi cha asili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sahihi, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kuasi kiasili. Baada ya kuja kumwamini Mungu, baadhi ya watu hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, lakini wanathubutu kutoa hotuba za hadharani wakitathmini usahihi na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na wanawahutubia hata mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote ndani yao. Je, si kuna siku itafika ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumuelekeza Mungu jinsi ya kufanya kazi. Je, watu kama hao wasio na busara wanawezaje kumjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati wa mchakato wa kutafuta na kupitia; maarifa ya Mungu hayapatikani kupitia nuru ya Roho Mtakatifu kwa njia ya mwanadamu kutoa hukumu za kiholela. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, asili yako ya zamani, na ubinadamu wako, tabia na mtazamo wako wa kimaadili ndio “mtaji” ambao unatumia kumpinga Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale walio na dhana imara na wenye tabia ya kujiinua wamo hata zaidi katika uadui na Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.
Ni kwa kuweka tu kando dhana zako za zamani ndipo utakapoweza kupata maarifa mapya, ilhali maarifa ya zamani si lazima yawe dhana za zamani. “Dhana” inamaanisha vitu vinavyodhaniwa na mwanadamu ambavyo viko mbali na uhalisi. Kama maarifa ya zamani yalikuwa yamepitwa na wakati katika enzi ya kale, na yalimzuia mwanadamu kuingia katika kazi mpya, basi maarifa kama hayo pia ni dhana. Ikiwa mwanadamu ataweza kuchukua mtazamo sahihi wa maarifa hayo, na anaweza kuja kumjua Mungu kutoka kwa vipengele tofauti, kuunganisha ya zamani na mapya, basi maarifa ya kale yatamsaidia mwanadamu, na yatakuwa msingi wa mwanadamu kuingia katika enzi mpya. Somo la kumjua Mungu linahitaji kwamba uwe stadi wa kanuni nyingi: jinsi ya kuingia kwenye njia ya kumjua Mungu, ukweli gani unapaswa kuelewa ili kumjua Mungu, na jinsi ya kuondoa dhana zako na asili yako ya kale ili kwamba uweze kutii mipango yote ya kazi mpya ya Mungu. Ukitumia kanuni hizi kama msingi wa kuingia kwenye somo la kumjua Mungu, basi maarifa yako yatakuwa na kina zaidi na zaidi. Kama una maarifa ya wazi ya hatua tatu za kazi—ambayo ni kusema kwamba, ya mpango mzima wa usimamizi wa Mungu—na ikiwa utaweza kupatanisha hatua mbili za awali na hatua ya sasa, na unaweza kuona kwamba ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja, basi utakuwa na msingi imara zaidi. Hatua tatu za kazi zimefanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hakuna mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeweza kuifanya kazi Yake tangu mwanzo hadi leo. Ingawa hatua tatu za kazi ya Mungu zimefanywa katika enzi tofauti na maeneo tofauti, na ingawa kazi ya kila moja ni tofauti, yote ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja. Kati ya maono yote, hili ndilo ono kubwa zaidi ambalo mwanadamu anapaswa kulijua, na ikiwa litaeleweka kabisa na mwanadamu, basi ataweza kusimama imara. Leo, tatizo kubwa linalokabili dini na madhehebu kadhaa ni kwamba hazijui kazi ya Roho Mtakatifu, na hazina uwezo wa kutofautisha kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi isiyo ya Roho Mtakatifu—na kwa hivyo hawawezi kueleza kama hatua hii ya kazi, kama hatua mbili za awali, pia zimefanywa na Yehova Mungu. Ingawa watu wanamfuata Mungu, wengi hawawezi kueleza kama ni njia sahihi. Mwanadamu ana wasiwasi kama njia hii ndiyo njia inayoongozwa na Mungu Mwenyewe binafsi, na kama kupata mwili kwa Mungu ni ukweli, na watu wengi bado hawana fununu kuhusu jinsi ya kutambua inapokuja kwa mambo kama hayo. Wale wanaomfuata Mungu hawawezi kuamua njia, na hivyo habari zinazonenwa zina athari ya sehemu tu miongoni mwa watu hawa, na hazina uwezo wa kuwa na ufanisi kamili, na hivyo basi hii huathiri kuingia kwa maisha ya watu kama hao. Ikiwa mwanadamu anaweza kuona katika hatua tatu za kazi kuwa zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe kwa nyakati tofauti, katika maeneo tofauti, na kwa watu tofauti; ikiwa mwanadamu anaweza kuona kuwa ingawa kazi ni tofauti, zote zimefanywa na Mungu mmoja, na kwa kuwa ni kazi ambayo imefanywa na Mungu mmoja, basi lazima iwe sahihi, na bila dosari, na kwamba ingawa hailingani na dhana za mwanadamu, hakuna kupinga kuwa ni kazi iliyofanywa na Mungu mmoja—ikiwa mwanadamu anaweza kusema kwa uhakika kwamba ni kazi ya Mungu mmoja, basi dhana za mwanadamu zitakuwa ni jambo dogo tu, lisilostahili kutajwa. Kwa sababu maono ya mwanadamu hayako wazi, na mwanadamu anamjua tu Yehova kama Mungu, na Yesu kama Bwana, na ana mitazamo miwili kumhusu Mungu mwenye mwili wa leo, watu wengi wamejitoa kwa ajili ya kazi ya Yehova na Yesu, na wamezingirwa na dhana kuhusu kazi ya leo, watu wengi huwa na mashaka kila mara, na hawachukulii kazi ya leo kwa uzito. Mwanadamu hana dhana kuelekea hatua mbili za mwisho za kazi, ambazo hazikuonekana. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu haelewi uhalisi wa hatua mbili za mwisho za kazi, na yeye binafsi hakuzishuhudia. Ni kwa sababu haziwezi kuonekana ndiyo maana mwanadamu anawaza jinsi anavyopenda; bila kujali atakayodhania, hakuna ukweli wa kuthibitisha fikira hizo, na yeyote wa kurekebisha. Mwanadamu anaruhusu silika yake ya asili itawale, huku akikosa kujali na kuachilia mawazo yake yaende popote, kwa kuwa hakuna ukweli wa kuthibitisha dhana zake, na hivyo dhana za mwanadamu zinakuwa “ukweli,” bila kujali kama kuna uthibitisho wowote kwao. Kwa hivyo mwanadamu huamini katika Mungu wake aliyemuwazia akilini mwake, na hamtafuti Mungu wa kweli. Ikiwa mtu mmoja ana aina moja ya imani, basi kati ya watu mia moja kuna aina mia moja za imani. Mwanadamu ana imani kama hizi kwa maana hajaona uhalisi wa kazi ya Mungu, kwa sababu amesikia tu kwa masikio yake na hajaona kwa macho yake. Mwanadamu amesikia hekaya na hadithi—lakini amesikia kwa nadra kuhusu maarifa ya ukweli ya kazi ya Mungu. Hivyo ni kwa njia ya dhana zao wenyewe kwamba watu ambao wamekuwa waamini kwa mwaka mmoja tu wanaamini katika Mungu, na ndivyo ilivyo pia kwa wale ambao wamemwamini Mungu kwa maisha yao yote. Wale ambao hawawezi kuona ukweli daima hawawezi kuepuka imani ambayo ndani yake wana dhana kumhusu Mungu. Mwanadamu anaamini kuwa amejiweka huru kutokana na vifungo vya dhana zake za kale, na ameingia eneo jipya. Je, mwanadamu hajui kuwa maarifa ya wale wasioweza kuuona uso wa kweli wa Mungu si chochote ila ni dhana na uvumi? Mwanadamu anafikiria kuwa dhana zake ni sahihi, na wala hazina kasoro, na hufikiri kuwa hizi dhana zimetoka kwa Mungu. Leo, mwanadamu anaposhuhudia kazi ya Mungu, anaachilia dhana potovu ambazo zimejijenga kwa miaka mingi. Mawazo na dhana za awali zimekuwa vizuizi kwa kazi ya hatua hii, na inakuwa vigumu kwa mwanadamu kuachana na dhana kama hizo na kupinga mawazo kama hayo. Dhana kuelekea kazi hii ya hatua kwa hatua ya wengi wa wale wanaomfuata Mungu hadi leo zimekuwa za kuhuzunisha zaidi na watu hawa hatua kwa hatua wameunda uadui mkaidi kwa Mungu mwenye mwili, na chanzo cha chuki hii ni mawazo na dhana za mwanadamu. Ni hasa kwa sababu ukweli haumruhusu mwanadamu kuwa na uhuru wa hiari kwa mawazo yake, na, zaidi ya hayo, hauwezi kupingwa na mwanadamu kwa urahisi, na mawazo na dhana za mwanadamu hazistahimili uwepo wa ukweli, na hata zaidi ya hayo, kwa sababu mwanadamu hawezi kufikiria kuhusu usahihi na unyofu wa ukweli, na kwa nia moja tu huachilia mawazo yake, na hutumia dhana zake, kwamba dhana na mawazo ya mwanadamu zimekuwa adui wa kazi ya leo, kazi ambayo haiambatani na dhana za mwanadamu. Hili linaweza tu kusemwa kuwa ni kosa la dhana za mwanadamu, na haliwezi kusemwa kuwa ni kosa la kazi ya Mungu. Mwanadamu anaweza kufikiria lolote atakalo, lakini hawezi kupinga waziwazi hatua yoyote ya kazi ya Mungu au hata sehemu yoyote; ukweli wa kazi ya Mungu hauwezi kukiukwa na mwanadamu. Unaweza kuruhusu mawazo yako yatawale, na unaweza pia kujumuisha hadithi nzuri kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, lakini kamwe huwezi kupinga ukweli wa kila hatua ya kazi ya Yehova na Yesu; hii ni kanuni, na pia ni amri ya utawala, na mnapaswa kuelewa umuhimu wa masuala haya. Mwanadamu anaamini kuwa hatua hii ya kazi hailingani na dhana za mwanadamu, na hivi sivyo katika hatua mbili zilizopita za kazi. Katika mawazo yake, mwanadamu anaamini kuwa kazi ya hatua mbili zilizopita kwa hakika si sawa na kazi ya leo—lakini je, umewahi kufikiria kuwa kanuni zote za kazi ya Mungu ni sawa, na kuwa kazi Yake huwa ni ya kivitendo daima, na kwamba, bila kujali enzi, daima kutakuwa na halaiki ya watu wanaokataa na kuupinga ukweli wa kazi Yake? Wale wote ambao leo wanakataa na kuipinga hatua hii ya kazi bila shaka wangempinga Mungu wakati uliopita, kwa kuwa watu kama hawa daima watakuwa maadui wa Mungu. Watu wanaoujua ukweli wa kazi ya Mungu wataona hatua tatu za kazi kama kazi ya Mungu mmoja, na watatupilia mbali dhana zao. Hawa ni watu wanaomjua Mungu, na watu kama hawa ndio kwa kweli humfuata Mungu. Wakati ambapo usimamizi mzima wa Mungu utakaribia kufika mwisho, Mungu ataweka vitu vyote kulingana na aina. Mwanadamu aliumbwa kwa mikono ya Muumba, na mwishowe lazima kabisa Amrudishe mwanadamu chini ya utawala Wake; huu ndio mwisho wa hatua tatu za kazi. Hatua ya kazi ya siku za mwisho, na hatua mbili zilizopita katika Israeli na Yudea, ni mpango wa Mungu wa usimamizi katika dunia nzima. Hakuna anayeweza kupinga hili, na ni ukweli wa kazi ya Mungu. Ingawa watu hawajapata uzoefu ama kushuhudia mengi kuhusu kazi hizi, ukweli unabaki kuwa ukweli, na hauwezi kukanwa na mwanadamu yeyote. Watu wanaomwamini Mungu katika nchi zote duniani watakubali hatua tatu za kazi. Ikiwa unajua tu hatua moja mahususi ya kazi, na huelewi hatua nyingine mbili za kazi, huelewi kazi ya Mungu katika nyakati zilizopita, basi huwezi kuongea ukweli wote wa mpango mzima wa usimamizi wa Mungu, na maarifa yako ya Mungu yameegemea upande mmoja, kwa kuwa katika imani yako kwa Mungu humjui Yeye, au kumwelewa, na hivyo hufai kutoa ushuhuda kwa Mungu. Bila kujali kama maarifa yako ya sasa juu ya mambo haya ni ya kina sana ama ni ya juujuu tu, mwishowe, lazima uwe na maarifa, na ushawishike kabisa, na watu wote wataona ukamilifu wa kazi ya Mungu na kunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Mwishoni mwa kazi hii, madhehebu yote yatakuwa moja, viumbe vyote vilivyoumbwa vitarejea chini ya utawala wa Muumba, viumbe vyote vilivyoumbwa vitamwabudu Mungu mmoja wa kweli, na dini zote ovu zitakuwa bure, na hazitaonekana tena.
Kwanini tunarejelea kwa mfululizo hatua tatu za kazi? Kupita kwa enzi, maendeleo ya kijamii, na mabadiliko ya uso wa asili vyote hufuata mabadiliko katika hatua tatu za kazi. Mwanadamu hubadilika kwa wakati sawa na kazi ya Mungu, na wala haendelei peke yake. Kutajwa kwa hatua tatu za kazi ya Mungu ni ili kuleta viumbe vyote, na watu katika kila dini na madhehebu, chini ya utawala wa Mungu mmoja. Bila kujali wewe ni wa dini gani, mwishowe nyote mtanyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu anayeweza kufanya kazi hii; haiwezi kufanywa na kiongozi yeyote wa kidini. Kuna dini kadhaa kuu duniani, na kila moja ina mkuu, ama kiongozi, na wafuasi wameenea katika nchi tofauti na maeneo yote duniani; kila nchi, iwe ndogo au kubwa, ina dini tofauti ndani yake. Hata hivyo, bila kujali ni dini ngapi zilizopo duniani, watu wote wanaoishi duniani mwishowe wanaishi katika uongozi wa Mungu mmoja, na uwepo wao hauongozwi na viongozi wa kidini au wakuu. Ambayo ni kusema kwamba wanadamu hawaongozwi na mkuu fulani wa kidini ama kiongozi; badala yake wanadamu wote wanaongozwa na Muumba, aliyeziumba mbingu na nchi, na vitu vyote, na ambaye aliwaumba wanadamu—na huu ni ukweli. Hata ingawa dunia ina dini kadhaa kuu, bila kujali jinsi zilivyo kuu, zote zipo chini ya utawala wa Muumba, na hakuna inayoweza kuzidi wigo wa mamlaka hii. Maendeleo ya wanadamu, maendeleo ya kijamii, maendeleo ya sayansi ya asili—kila moja haitengani na mipango ya Muumba, na kazi hii sio kitu kinachoweza kufanywa na uongozi fulani wa dini. Viongozi wa dini ni viongozi tu wa dini fulani, na hawawezi kumwakilisha Mungu, ama Yule aliyeziumba mbingu na nchi na vitu vyote. Viongozi wa kidini wanaweza kuongoza wale wote walio katika dini yote, lakini hawawezi kuamrisha viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu—huu ni ukweli unaokubalika ulimwenguni mwote. Viongozi wa dini ni viongozi tu, na hawawezi kuwa sawa na Mungu (Muumba). Vitu vyote vipo mikononi mwa Muumba, na mwishowe vyote vitarejea mikononi mwa Muumba. Mwanadamu kiasili aliumbwa na Mungu, na haijalishi dini, kila mtu atarejea katika utawala wa Mungu—hili haliwezi kuepukika. Ni Mungu tu Aliye Juu Zaidi kati ya vitu vyote, na mtawala mkuu kati ya viumbe vyote lazima pia arejee chini ya utawala Wake. Bila kujali mwanadamu ana hadhi ya juu kiasi gani, hawezi kumfikisha mwanadamu kwenye hatima inayomfaa, wala hakuna anayeweza kuainisha kila kitu kulingana na aina. Yehova mwenyewe alimuumba mwanadamu na kumwainisha kila mmoja kulingana na aina na siku ya mwisho itakapowadia bado Atafanya kazi Yake Mwenyewe, kuainisha kila kitu kulingana na aina—hili haliwezi kufanywa na mwingine isipokuwa Mungu. Hatua tatu za kazi ambazo zilifanywa tangu mwanzo hadi leo zote zilitekelezwa na Mungu Mwenyewe, na zilitekelezwa na Mungu mmoja. Ukweli wa hatua tatu za kazi ni ukweli wa uongozi wa Mungu kwa wanadamu wote, ukweli ambao hakuna anayeweza kuupinga. Mwishoni mwa hatua tatu za kazi, vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina na kurejeshwa chini ya utawala wa Mungu, kwa kuwa duniani kote kuna Mungu mmoja tu, na hakuna dini nyingine. Yule asiyeweza kuiumba dunia hataweza kuiangamiza, ilhali Yule aliyeumba dunia hakika ataiangamiza, na kwa hivyo, kama mtu hana uwezo wa kutamatisha enzi na anaweza tu kumsaidia mwanadamu akuze akili yake, basi kwa hakika hatakuwa Mungu, na kwa hakika hatakuwa Bwana wa wanadamu. Hataweza kufanya kazi kuu kama hii; kuna mmoja tu anayeweza kufanya kazi kama hii, na wote wasioweza kufanya kazi hii kwa hakika ni maadui wala si Mungu. Dini zote ovu hazilingani na Mungu, na kwa sababu hazilingani na Mungu, zina uadui na Mungu. Kazi yote inafanywa na huyu Mungu mmoja wa kweli, na ulimwengu mzima unatawaliwa na huyu Mungu mmoja. Bila kujali kama Anafanya kazi Uchina ama Israeli, bila kujali kama kazi inafanywa na Roho ama mwili, yote hufanywa na Mungu Mwenyewe, na haiwezi kufanywa na mwingine yeyote. Ni kwa sababu haswa Yeye ni Mungu wa wanadamu wote kwamba Yeye hufanya kazi kwa uhuru, bila kuzuiliwa na masharti yoyote—na haya ndiyo maono makuu kuliko yote. Kama kiumbe wa Mungu, kama ungependa kutekeleza jukumu la kiumbe wa Mungu na kuelewa mapenzi ya Mungu, lazima uelewe kazi ya Mungu, lazima uelewe mapenzi ya Mungu kwa viumbe, lazima uelewe mpango Wake wa usimamizi, na lazima uelewe umuhimu wote wa kazi Anayofanya. Wale ambao hawaelewi hili hawana sifa za kuwa viumbe wa Mungu! Kama kiumbe wa Mungu, kama huelewi ulikotoka, huelewi historia ya mwanadamu na kazi yote iliyofanywa na Mungu, na, hata zaidi, huelewi jinsi mwanadamu ameendelea hadi leo, na huelewi ni nani anayewaamuru wanadamu wote, basi huna uwezo wa kutekeleza wajibu wako. Mungu amemwongoza mwanadamu hadi leo, na tangu alipomuumba mwanadamu duniani Hajawahi kumwacha. Roho Mtakatifu daima haachi kufanya kazi, hajawahi kuacha kuwaongoza wanadamu, na Hajawahi kuwaacha wanadamu. Lakini mwanadamu hatambui kuwa kuna Mungu, pia hamjui Mungu, na je, kuna jambo la kufedhehesha zaidi kuliko hili kwa viumbe wote wa Mungu? Mungu binafsi humwongoza mwanadamu, lakini mwanadamu haelewi kazi ya Mungu. Wewe ni kiumbe wa Mungu, ilhali huelewi historia yako mwenyewe, na wala hujui ni nani aliyekuongoza katika safari yako, hutambui kazi iliyofanywa na Mungu, na kwa hivyo huwezi kumjua Mungu. Ikiwa hujui sasa, basi hutawahi kuhitimu kutoa ushuhuda kwa Mungu. Leo, Muumba binafsi huwaongoza watu wote kwa mara nyingine, na kuwafanya watu wote waone hekima Yake, uweza, wokovu, na kustaajabisha Kwake. Ilhali bado hujatambua au kuelewa—na kwa hivyo, je, si wewe ndiwe utakayekosa kupokea wokovu? Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa. Wale wasioyaelewa mapenzi ya Mungu na hawaitambui kazi ya Mungu hawawezi kupata maarifa ya Mungu, na watu kama hawa hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu. Kama ungependa kumshuhudia Mungu, basi lazima umjue Mungu, na maarifa ya Mungu yanapatikana kwa kupitia kazi ya Mungu. Kwa ufupi, kama ungependa kumjua Mungu, basi lazima ujue kazi ya Mungu: Kufahamu kazi ya Mungu ndilo jambo la muhimu kabisa. Wakati hatua tatu za kazi zitakapofikia mwisho, patafanyika kundi la wale wanaotoa ushuhuda kwa Mungu, kundi la wale wanaomjua Mungu. Watu hawa wote watamjua Mungu na wataweza kuweka ukweli katika vitendo. Watakuwa na ubinadamu na hisia, na wote watajua hatua tatu za kazi ya Mungu ya wokovu. Hii ndiyo kazi itakayokamilishwa mwishoni, na watu hawa ni udhihirisho wa kazi ya miaka 6,000 ya usimamizi, na ni ushuhuda wenye nguvu zaidi wa kushindwa kwa mwisho kwa Shetani. Wale wanaoweza kumshuhudia Mungu wataweza kupokea ahadi na baraka za Mungu, na litakuwa ndilo kundi litakalosalia pale mwisho kabisa, ambalo linamiliki mamlaka ya Mungu na kutoa ushuhuda kwa Mungu. Pengine wale walio miongoni mwenu wanaweza wote kuwa sehemu ya kundi hili, ama pengine nusu tu, ama wachache tu—inategemeana na nia zenu na ufuatiliaji wenu.