Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu
Kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, bila shaka, ikirejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu. Sizungumzii kazi ambayo inatokana na matakwa ya mwanadamu bali kazi ya mitume, watendaji kazi au ndugu wa kawaida waliopo katika mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hapa, kazi ya mwanadamu hairejelei kazi ya Mungu mwenye mwili bali kwa mawanda na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu. Ingawa kanuni hizi ni kanuni na mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu, hazifanani na kanuni na mawanda ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Kazi ya mwanadamu ina kiini na kanuni za mwanadamu, na kazi ya Mungu ina kiini na kanuni za Mungu.
Kazi katika mkondo wa Roho Mtakatifu, bila kujali ni kazi ya Mungu mwenyewe au ni kazi ya watu wanaotumiwa, ni kazi ya Roho Mtakatifu. Kiini cha Mungu Mwenyewe ni Roho, ambaye anaweza kuitwa Roho Mtakatifu au Roho mwenye nguvu mara saba. Kwa jumla, Wao ni Roho wa Mungu. Ni kwamba tu Roho wa Mungu anaitwa majina tofauti katika enzi tofauti tofauti. Lakini kiini Chao bado ni kimoja. Hivyo, kazi ya Mungu Mwenyewe ni kazi ya Roho Mtakatifu; kazi za Mungu mwenye mwili hazitofautiani na kazi za Roho Mtakatifu. Kazi ya wanadamu wanaotumiwa pia ni kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwamba tu kazi ya Mungu ni onyesho kamili la Roho Mtakatifu, ambalo ni ukweli kabisa, ilhali kazi ya watu wanaotumiwa inachanganyika na mambo mengi ya kibinadamu, na wala si uonyeshaji wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu, wala uonyeshaji kamili. Kazi ya Roho Mtakatifu ina mawanda mapana na wala haizuiliwi na hali yoyote ile. Kazi hiyo inatofautiana kwa watu tofauti tofauti, na kutoa viini tofauti tofauti vya kufanya kazi. Kazi pia inatofautiana katika enzi mbali mbali, kama pia ilivyo kazi tofauti katika nchi mbalimbali. Bila shaka, ingawa Roho Mtakatifu hufanya kazi katika njia nyingi tofauti tofauti na kulingana na kanuni nyingi, haijalishi kazi imefanyikaje au kwa watu wa aina gani, kiini ni tofauti daima, na kazi Anazofanya kwa watu tofauti zote zina kanuni na zote zinaweza kuwakilisha kiini cha mhusika anayefanyiwa kazi. Hii ni kwa sababu kazi ya Roho Mtakatifu ni mahususi kabisa kwa mapana yake na inapimika. Kazi inayofanywa katika mwili uliopatikana si sawa na kazi inayofanywa kwa watu, na kazi hii pia inatofautiana kulingana na ubora mbali mbali wa tabia za watu. Kazi inayofanywa katika mwili uliopatikana si sawa na kazi inayofanywa kwa watu, na katika mwili uliopatikana Hafanyi kazi ile ile kama aliyoifanya kwa watu. Kwa ufupi, haijalishi Anafanya kazi jinsi gani, kazi katika vitu mbalimbali haifanani, na kanuni ambazo Anazitumia kufanya kazi zinatofautiana kulingana na hali na asili ya watu mbalimbali. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa watu tofauti tofauti kulingana na kiini chao cha asili na haweki mahitaji ambayo ni zaidi ya kiini chao cha asili, na wala Hafanyi kazi zaidi ya ubora halisi wa tabia yao. Kwa hivyo, kazi ya Roho Mtakatifu kwa mwanadamu inawaruhusu watu kuona kiini cha lengo la kazi hiyo. Kiini asili cha mwanadamu hakibadiliki; ubora halisi wa tabia ya mwanadamu ina mipaka. Kama Roho Mtakatifu anawatumia watu au anafanya kazi kwa watu kazi, kazi hiyo siku zote inafanywa kulingana na tabia za watu ili waweze kunufaika kutoka kwayo. Roho Mtakatifu anapofanya kazi kwa wanadamu wanaotumiwa, karama zao na tabia zao halisi zinatumiwa pia na wala haziachwi. Tabia zao halisi zinatumiwa zote kwa ajili ya kutoa huduma kwa kazi. Tunaweza kusema kuwa Anafanya kazi kwa kutumia sehemu zilizopo za wanadamu ili kupata matokeo yatendayo kazi. Kinyume chake, kazi inayofanyika katika mwili uliopatikana ni yenye kumwonyesha Roho moja kwa moja na wala haichanganywi na akili na mawazo ya mwanadamu, haifikiwi na karama za mwanadamu, uzoefu wa mwanadamu au hali ya ndani ya mwanadamu. Kazi nyingi mno ya Roho Mtakatifu yote inalenga kumnufaisha na kumwadilisha mwanadamu. Lakini baadhi ya watu wanaweza kukamilishwa wakati wengine hawana vigezo vya kuweza kukamilishwa, ambayo ni kusema, hawawezi kukamilishwa na ni vigumu sana kuokolewa, na ingawa wanaweza kuwa walishakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, mwishowe wanaondolewa. Hii ni sawa na kusema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwaadilisha watu, hii haimaanishi kwamba wale wote waliokwisha kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu wanapaswa kukamilishwa kikamilifu, kwa sababu njia wanayoifuatilia watu wengi si njia ya kukamilishwa. Wana kazi moja tu ya Roho Mtakatifu, na wala si ushirikiano wa kibinafsi wa binadamu au njia sahihi za kibinadamu. Kwa njia hii, kazi ya Roho Mtakatifu kwa watu hawa inakuwa kazi katika huduma ya wale ambao wanakamilishwa. Kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kuonwa moja kwa moja na watu au kuguswa moja kwa moja na watu wenyewe. Inaweza kuonyeshwa tu kwa njia ya msaada wa watu wenye karama ya kufanya kazi, ikiwa na maana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu inatolewa kwa wafuasi kwa njia ya onyemaonyesho wanadamu.
Kazi ya Roho Mtakatifu inakamilishwa na kukamilika kupitia watu wa aina nyingi na hali nyingi tofauti tofauti. Ingawa kazi ya Mungu mwenye mwili inaweza kuwakilisha kazi ya enzi zote, na inaweza kuwakilisha uingiaji wa watu katika enzi nzima, kazi kwa watu wengi bado inahitajika kufanywa na wanadamu wanaotumiwa na Roho Mtakatifu na sio na Mungu mwenye mwili. Kwa hivyo, kazi ya Mungu, au huduma ya Mungu mwenyewe, ni kazi ya Mungu mwenye mwili na haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya Roho Mtakatifu imekamilishwa kupitia watu wa aina mbalimbali na haiwezi kukamilishwa na mtu mahususi mmoja tu, au kufafanuliwa kikamilifu kupitia mtu mmoja mahususi. Wale ambao wanaongoza kanisa pia hawawezi kuiwakilisha kazi ya Roho Mtakatifu kikamilifu; wanaweza kufanya tu kazi fulani ya kuongoza. Kwa njia hii, kazi ya Roho Mtakatifu inaweza kugawanywa katika sehemu tatu: Kazi ya Mungu mwenyewe, kazi ya wanadamu wanaotumiwa, na kazi kwa wale wote walioko katika mkondo wa Roho Mtakatifu. Miongoni mwa hizo tatu, kazi ya Mungu ni kuongoza enzi nzima; kazi ya wanadamu wanaotumiwa ni kuwaongoza wafuasi wote wa Mungu kwa kutumwa au kupokea maagizo kwa ajili ya kazi ya Mungu mwenyewe; na wanadamu hawa ndio wanaoshirikiana na kazi ya Mungu; kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa wale waliopo katika mkondo wake ni kudumisha kazi Yake yote, yaani, kudumisha usimamizi wote na kudumisha ushuhuda Wake, na wakati uo huo kuwakamilisha wale wanaoweza kukamilishwa. Sehemu hizi tatu ni kazi kamili ya Roho Mtakatifu, lakini bila kazi ya Mungu Mwenyewe, kazi yote ya usimamizi inaweza kutuama. Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mitindo ya kazi ya Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi. Kwa sababu ya utambulisho na uwakilishaji tofauti wa kazi hii, licha ya ukweli kwamba zote ni kazi za Roho Mtakatifu, kuna tofauti za wazi na bainifu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Aidha, kiwango cha kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa watu wenye tambulisho tofauti inatofautiana. Hizi ni kanuni na mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.
Kazi ya mwanadamu inawakilisha uzoefu wake na ubinadamu wake. Kile ambacho mwanadamu anatoa na kazi ambayo anafanya vinamwakilisha yeye. Kuona kwa mwanadamu, kufikiri kwa mwanadamu, mantiki ya mwanadamu na uwezo wake mkubwa wa kufikiri vyote vinajumuishwa katika kazi yake. Kimsingi, uzoefu wa mwanadamu, unaweza zaidi kuwakilisha kazi yake na kile ambacho mtu amekipitia kitakuwa ni sehemu ya kazi yake. Kazi ya mwanadamu inaweza kuonyesha uzoefu wake. Pale ambapo baadhi ya watu wanapitia hali ya kukaa tu bila kujishughulisha, sehemu kubwa ya ushirika wao inakuwa na vipengele vya uhasi. Kama uzoefu wao kwa kipindi cha muda ni mzuri na wanapita katika njia ya upande mzuri, kile wanachoshiriki kinatia moyo sana, na watu wanaweza kupokea mambo mazuri kutoka kwao. Mfanyakazi akiwa katika hali ya kukaa tu kwa kipindi cha muda, ushirika wake siku zote utakuwa na vipengele vya uhasi. Ushirika wa aina hii ni wa kuvunja moyo, na wengine watavunjika mioyo bila kujua kwa kufuata ushirika wa yule mfanyakazi. Hali ya wafuasi inabadilika kutegemea na hali ya kiongozi. Vile ambavyo mfanyakazi alivyo ndani, ndicho kile anachoonyesha, na kazi ya Roho Mtakatifu mara nyingi inabadilika kulingana na hali ya mwanadamu. Anafanya kazi kulingana na uzoefu wa mwanadamu na wala hamshurutishi mwanadamu bali anamsihi mwanadamu kulingana na hali yake ya kawaida ya uzoefu wake. Hii ni kusema kwamba ushirika wa mwanadamu unatofautiana na neno la Mungu. Kile ambacho mwanadamu hushiriki kinaeleza vile anavyotazama mambo na uzoefu wake, kinaonyesha kile wanachokiona na kupitia uzoefu kwa msingi wa kazi ya Mungu. Wajibu wao ni kutafuta, baada ya Mungu kufanya kazi au kuzungumza, kile wanachopaswa kufanya au kuingia kwacho, halafu kukiwasilisha kwa wafuasi. Hivyo, kazi ya mwanadamu inawakilisha kuingia au matendo yake. Bila shaka, kazi hiyo imechanganyika na masomo ya kibinadamu na uzoefu au mawazo ya kibinadamu. Haijalishi namna ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi, ama Anavyomfanyia kazi mwanadamu au Mungu mwenye mwili, siku zote watenda kazi ndio wanaoonyesha vile walivyo. Ingawa ni Roho Mtakatifu ambaye hufanya kazi, kazi hiyo imejengwa katika msingi wa mwanadamu alivyo kiasili, kwa sababu Roho Mtakatifu hafanyi kazi pasipo msingi. Kwa maneno mengine, kazi haifanyiki pasipokuwa na kitu, lakini siku zote hufanyika kulingana na mazingira halisi na hali halisi. Ni kwa njia hii pekee ndiyo tabia ya mwanadamu inaweza kubadilishwa, kwamba mitazamo yake ya zamani na mawazo yake ya zamani yanaweza kubadilishwa. Kile ambacho mwanadamu huonyesha ni kile anachokiona, kupitia uzoefu na kukitafakari. Hata kama ni mafundisho au fikira, haya yote hufikiwa na fikira za mwanadamu. Bila kujali ukubwa wa kazi ya mwanadamu, haiwezi kuzidi mawanda ya uzoefu wa mwanadamu, kile ambacho mwanadamu huona, au kile ambacho mwanadamu anaweza kukitafakari au kuingia akilini mwake. Kile ambacho Mungu anaonyesha ndivyo hivyo Mungu Mwenyewe alivyo, na hii ni nje ya uwezo wa mwanadamu, yaani, nje ya uwezo wa kufikiri kwa mwanadamu. Anaonyesha kazi Yake ya kuwaongoza wanadamu wote, na hii haihusiani na undani wa uzoefu wa mwanadamu, badala yake inahusu usimamizi Wake. Mwanadamu anaonyesha uzoefu wake wakati Mungu anaonyesha nafsi Yake—nafsi hii ni tabia Yake ya asili na iko nje ya uwezo wa mwanadamu. Uzoefu wa mwanadamu ni kuona kwake na kupata maarifa kulingana na uonyeshaji wa Mungu wa nafsi Yake. Kuona kama huko na maarifa kama hayo yanaitwa asili ya mwanadamu. Yanaonyeshwa kwa msingi wa tabia asili ya mwanadamu na ubora wa tabia yake halisi; hivyo pia vinaitwa nafsi ya mwanadamu. Mwanadamu anaweza kushiriki kile anachokipitia na kukiona. Kile ambacho hajawahi kukipitia au kukiona au akili yake haiwezi kukifikia, yaani, vitu ambavyo havipo ndani yake, hawezi kuvishiriki. Ikiwa kile ambacho mwanadamu anakionyesha sio uzoefu wake, basi ni mawazo yake au mafundisho ya kidini. Kwa ufupi, hakuna ukweli wowote katika maneno yake. Kama hujawahi kukutana na maswala ya jamii, hutaweza kushiriki kwa uwazi kwenye mahusiano changamani katika jamii. Kama huna familia na watu wengine wanazungumza juu ya masuala ya familia, huwezi kuelewa kiasi kikubwa cha kile walichokuwa wakisema. Kwa hivyo, kile ambacho mwanadamu anakifanyia ushirika na kazi anayofanya vinawakilisha asili yake ya ndani. Ikiwa mtu anafanya ushirika kuhusu ufahamu wake wa kuadibu na hukumu, lakini huna uzoefu wake, usithubutu kukana maarifa yake, badala yake kuwa na uhakika wa anachokisema kwa asilimia mia moja. Hii ni kwa sababu kile anachokifanyia ushirika ni kitu ambacho hujawahi kupata uzoefu wake, kitu ambacho hujawahi kukifahamu, na akili yako haiwezi kukitafakari. Unaweza tu kujifunza kutoka kwa ufahamu wake njia za maisha yajayo yanayohusiana na kuadibu na hukumu. Lakini njia hii inaweza kufanya kazi tu kama ufahamu uliojikita katika fundisho na haiwezi kuchukua nafasi ya ufahamu wako, na zaidi sana uzoefu wako. Pengine unafikiri kwamba kile anachokisema ni sahihi, lakini unapokipitia, unagundua kwamba hakitekelezeki katika mambo mengi. Pengine unahisi kwamba maarifa fulani unayoyasikia hayatekelezeki kabisa; unakuwa na mtazamo kuhusu maarifa hayo kwa wakati fulani, na ingawa unayakubali, unafanya hivyo shingo upande. Lakini unapopata uzoefu, maarifa yanayokupa mtazamo ndiyo yanayoongoza matendo yako. Na kadiri unavyotenda, ndivyo unavyozidi kuelewa thamani halisi na maana ya maneno yake. Baada ya kuwa na uzoefu, sasa unaweza kuzungumza juu ya maarifa unayopaswa kuwa nayo kuhusu vitu ulivyovipitia. Aidha, unaweza pia kutofautisha kati ya wale ambao maarifa yao ni halisi na ya utendaji na wale ambao maarifa yao yamejikita katika mafundisho ya kidini na hayana thamani. Kwa hivyo, kama maarifa ambayo unayazungumzia yanapatana na ukweli kwa kiasi kikubwa yanategemea na iwapo una uzoefu wa vitendo. Pale palipo na ukweli katika uzoefu wako, maarifa yako yatakuwa yanatekelezeka na yenye thamani. Kupitia uzoefu wako, pia unaweza kupata utambuzi na umaizi, kukuza maarifa yako, na kuongeza hekima yako na akili ya kuzaliwa katika kujiongoza. Maarifa yanayozungumzwa na watu ambao hawana ukweli ni fundisho la kidini tu, bila kujali yana nguvu kiasi gani. Mtu wa aina hii anaweza kuwa mwenye akili sana yanapokuja masuala ya kimwili lakini hawezi kutofautisha yanapokuja masuala ya kiroho. Hii ni kwa sababu watu kama hao hawana uzoefu wowote katika masuala ya kiroho. Hawa ni watu ambao hawajapata nuru katika masuala ya kiroho na hawaelewi mambo ya kiroho. Haijalishi aina ya maarifa unayoonyesha, ilimradi ni asili yako, basi ni uzoefu wako binafsi, maarifa yako halisi. Kile ambacho watu wenye mafundisho tu huzungumzia, yaani, wale ambao hawana ukweli au uhalisi, huzungumzia yaweza kusemwa kuwa ni asili yao, kwa sababu mafundisho yao yamefikiwa kwa njia ya kutafakari sana na ni matokeo ya akili yao kutafakari kwa kina, lakini ni mafundisho tu, si kitu chochote zaidi ya fikira. Uzoefu wa aina tofauti za watu unawakilisha vitu vilivyomo ndani yao. Wale wote ambao hawana uzoefu wa kiroho hawawezi kuzungumza juu ya maarifa ya ukweli, maarifa sahihi kuhusu aina mbalimbali za masuala ya kiroho. Kile ambacho mtu anakionyesha ndivyo alivyo ndani—hili ni hakika. Ikiwa mtu anatamani kuwa na maarifa ya masuala ya kiroho na ukweli, anapaswa kuwa na uzoefu halisi. Ikiwa huwezi kuzungumza wazi juu ya masuala ya kawaida yanayohusiana na maisha ya mwanadamu, basi utawezaje kuzungumzia masuala ya kiroho? Wale wanaoweza kuyaongoza makanisa, kuwaruzuku watu maisha, na kuwa mtume kwa watu, wanapaswa kuwa na uzoefu halisi, ufahamu sahihi wa masuala ya kiroho, kuelewa vyema na kuwa na uzoefu wa ukweli. Watu wa namna hiyo tu ndio wanaostahili kuwa watenda kazi au mitume wanaoyaongoza makanisa. Vinginevyo, wanaweza kutufuata tu kidogo na hawawezi kuongoza, sembuse kuwa mtume mwenye uwezo wa kuwapatia watu uhai. Hii ni kwa sababu kazi ya mitume siyo kukimbia au kupigana; ni kufanya kazi ya kutoa huduma ya maisha na kuwaongoza wengine katika kubadili tabia zao. Wale wanaofanya kazi hii wanaagizwa kubeba mzigo mkubwa, ambao si kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya. Kazi ya aina hii inaweza tu kufanywa na wale ambao wana maisha ya uwepo, yaani, wale ambao wana uzoefu wa ukweli. Haiwezi kufanywa na kila mtu ambaye anaweza kukata tamaa, anaweza kukimbia au yupo tayari kutumia pesa; watu ambao hawana uzoefu wa ukweli, wale ambao hawajapogolewa au kuhukumiwa, hawawezi kufanya kazi ya aina hii. Watu ambao hawana uzoefu, yaani, watu wasio na ukweli, hawawezi kuona ukweli kwa uwazi kwa kuwa wao wenyewe hawako katika hali hii. Hivyo, mtu wa aina hii si kwamba hawezi tu kufanya kazi ya kuongoza bali atakuwa mlengwa wa kuondolewa ikiwa hatakuwa na ukweli kwa muda mrefu. Kuona unakokuzungumzia kunaweza kuthibitisha ugumu ulioupitia maishani, katika masuala ambayo kwayo umeadibiwa na katika mambo ambayo umehukumiwa kwayo. Hii pia ni kweli katika majaribu: Vitu ambavyo mtu anasafishwa kwavyo, vitu ambavyo kwavyo mtu ni mdhaifu, hivi ni vitu ambavyo mtu ana uzoefu kwavyo, vitu ambavyo mtu anaelewa njia zake. Kwa mfano, kama mtu amekatishwa tamaa katika ndoa, muda mwingi atakuwa anafanya ushirika, “Asante Mungu, msifu Mungu, ni lazima nitimize matakwa ya Mungu, na kuyatoa maisha yangu yote, kuikabidhi ndoa yangu kikamilifu katika mikono ya Mungu. Niko radhi kuyatoa maisha yangu yote kwa Mungu.” Vitu vyote ndani ya mwanadamu vinaweza kuonyesha kile alicho kupitia katika ushirika. Mwendo wa usemi wa mtu, kama anazungumza kwa sauti kubwa au kwa sauti ya chini, masuala kama hayo ambayo si masuala ya uzoefu hayawezi kuwakilisha kile alicho nacho na kile alicho. Yanaweza kueleza tu iwapo tabia yake ni nzuri au mbaya, au kama asili yake ni nzuri au mbaya lakini haiwezi kulinganishwa na kama ana uzoefu. Uwezo wa mtu kujionyesha anapozungumza, ama ujuzi au kasi ya kuzungumza, ni suala tu la utendaji na haliwezi kuchukua nafasi ya uzoefu wake. Unapozungumza juu ya uzoefu wako binafsi, unafanya ushirika wa kile ambacho unakipatia umuhimu na vitu vyote ndani yako. Usemi Wangu unawakilisha asili Yangu, lakini kile Ninachokisema kiko nje ya uwezo wa mwanadamu. Kile Nikisemacho sio kile ambacho mwanadamu anakipitia, na sio kitu ambacho mwanadamu anaweza kukiona, pia si kitu ambacho mwanadamu anaweza kukigusa, lakini ndicho Nilicho. Baadhi ya watu wanakiri tu kwamba kile Ninachokifanyia ushirika ndicho kile Nimekipitia, lakini hawatambui kwamba ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Ni kweli, kile Ninachokisema ndicho kile Nimekipitia. Ni Mimi Ndiye Niliyefanya kazi ya usimamizi kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu sita. Nimepitia kila kitu kuanzia mwanzo wa uumbaji wa mwanadamu hadi leo; Nitashindwaje kukizungumzia? Linapokuja suala la asili ya mwanadamu, Nimeliona waziwazi, na Nimeliangalia toka zamani; sasa Nitashindwaje kuliongelea? Kwa kuwa nimeiona asili ya mwanadamu kwa uwazi, Nina sifa za kumrudi mwanadamu na kumhukumu, kwa sababu mwanadamu mzima ametoka Kwangu lakini ameharibiwa na Shetani. Kwa ukweli, Nimehitimu kutathmini kazi ambayo Nimeifanya. Ingawa kazi hii haijafanywa na mwili Wangu, ni uonyeshaji wa moja kwa moja wa Roho, na hiki ndicho Nilicho nacho na kile Nilicho. Kwa hivyo, Ninaweza kuonyesha na kufanya kazi ambayo Napaswa kufanya. Kile ambacho mwanadamu anakisema ni kile alichokipitia. Ni kile ambacho wamekiona, kile ambacho akili zao zinaweza kukifikia, na kile ambacho milango yao ya fahamu inaweza kuhisi. Hicho ndicho wanachoweza kukifanyia ushirika. Maneno yaliyosemwa na mwili wa Mungu ni onyesho la moja kwa moja la Roho na huonyesha kazi ambayo imefanywa na Roho. Mwili haujaipitia au kuiona, lakini bado huonyesha asili Yake kwa sababu kiini cha mwili ni Roho, na huonyesha kazi ya Roho. Ingawa mwili hauwezi kuifikia, ni kazi ambayo tayari imefanywa na Roho. Baada ya kufanyika mwili, kupitia uonyeshaji wa mwili, Anawasaidia watu kujua asili ya Mungu na kuwafanya watu kuiona tabia ya Mungu na kazi ambayo Ameifanya. Kazi ya mwanadamu inawawezesha watu kuelewa kwa uwazi kuhusu kile wanachopaswa kuingia kwacho na wanachopaswa kukielewa; inahusisha kuwaongoza watu kupata ufahamu na kuujua ukweli. Kazi ya mwanadamu ni kuwaendeleza watu; kazi ya Mungu ni kufungua njia mpya na kufungua enzi mpya kwa ajili ya binadamu, na kuwafunulia watu kile ambacho hakijafahamika kwa watu wenye mwili wa kufa, ikiwasaidia kuelewa tabia Yake. Kazi ya Mungu ni kuwaongoza wanadamu wote.
Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhusu kuwasaidia watu kupata faida; ni kuwaadilisha watu; hakuna kazi ambayo haiwanufaishi watu. Haijalishi kama ukweli ni wa kina au usio wa kina, na haijalishi tabia ya wale wanaopokea ukweli huo ilivyo, chochote ambacho Roho Mtakatifu anafanya, yote hayo huwanufaisha watu. Lakini kazi ya Roho Mtakatifu haiwezi kufanywa moja kwa moja; ni lazima ifanywe na wanadamu wanaoshirikiana na Yeye. Ni kwa njia hii pekee ndiyo matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu yanaweza kupatikana. Bila shaka, inapokuwa ni kazi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu, haijachanganywa na kitu chochote kabisa; lakini inapotumia mwanadamu kama chombo, inakuwa imechanganywa sana na sio kazi halisi ya Roho Mtakatifu. Kwa njia hii, ukweli hubadilika katika viwango tofauti. Wafuasi hawapokei nia halisi ya Roho Mtakatifu bali wanapokea muungano wa kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu na maarifa ya mwanadamu. Sehemu ya kazi ya Roho Mtakatifu inayopokelewa na wafuasi ni sahihi. Uzoefu na maarifa ya mwanadamu yanayopokewa yanatofautiana kwa sababu watenda kazi ni tofauti. Watenda kazi wanapokuwa na nuru na uongozi wa Roho Mtakatifu, wanakuwa wanapata uzoefu kulingana na nuru na uongozi huu. Ndani ya uzoefu huu kuna akili ya mwanadamu na uzoefu, vile vile asili ya ubinadamu, ambapo wanapata maarifa na kuona vile walivyopaswa kuona. Hii ndiyo njia ya kutenda baada ya mwanadamu kuujua ukweli. Namna hii ya kutenda siku zote haifanani kwa sababu watu wana uzoefu tofauti na vitu ambavyo watu wanavipitia ni tofauti. Kwa njia hii, nuru ile ile ya Roho Mtakatifu inaleta maarifa tofauti na desturi kwa sababu wale wanaopokea nuru hiyo ni tofauti. Baadhi ya watu hufanya makosa madogo wakati wa utendaji ilhali wengine hufanya makosa makubwa, na baadhi hawafanyi chochote ila ni makosa tu. Hii ni kwa sababu uwezo wa kuelewa mambo unatofautiana na kwa sababu tabia zao halisi pia zinatofautiana. Baadhi ya watu wanaelewa hivi baada ya kuusikia ujumbe, na baadhi ya watu wanauelewa vile baada ya kuusikia ukweli. Baadhi ya watu wanapotoka kidogo; na baadhi hawaelewi kabisa maana ya ukweli. Kwa hiyo, kwa jinsi yoyote mtu aelewavyo ndivyo atakavyowaongoza wengine; hii ni kweli kabisa, kwa sababu kazi yake inaonyesha asili yake tu. Watu wanaoongozwa na watu wenye ufahamu sahihi wa ukweli pia watakuwa na ufahamu sahihi wa ukweli. Hata kama kuna watu ambao uelewa wao una makosa, ni wachache sana, na sio watu wote watakuwa na makosa. Ikiwa mtu ana makosa katika anavyouelewa ukweli, wale wanaomfuata bila shaka pia watakuwa na makosa. Watu hawa watakuwa na makosa katika kila namna. Kiwango cha kuuelewa ukweli miongoni mwa wafuasi kinategemea kwa kiasi kikubwa watenda kazi. Bila shaka, ukweli kutoka kwa Mungu ni sahihi na hauna makosa, na ni hakika. Lakini, watenda kazi hawako sahihi kikamilifu na hatuwezi kusema kwamba ni wa kutegemewa kabisa. Ikiwa watenda kazi wana njia ya kuuweka ukweli katika njia ya matendo, basi wafuasi pia watakuwa na njia ya kuutenda. Ikiwa watenda kazi hawawezi kuuweka ukweli katika matendo bali wanashikilia mafundisho tu, wafuasi hawatakuwa na uhalisia wowote. Ubora wa tabia na asili ya wafuasi vinaukiliwa na kuzaliwa na havihusiani na watenda kazi. Lakini kiwango ambacho kwacho wafuasi wanauelewa ukweli na kumfahamu Mungu kinategemeana na watenda kazi (hii ni kwa baadhi ya watu tu). Vyovyote alivyo mtenda kazi, hivyo ndivyo wafuasi anaowaongoza watakavyokuwa. Kile ambacho mtenda kazi anakionyesha ni asili yake mwenyewe, bila kuacha chochote. Yale anayowaambia wafuasi wake watende ndiyo yeye mwenyewe yuko radhi kuyafikia au ni yale anayoweza kutimiza. Watenda kazi wengi huwaambia wafuasi wao kufuata mambo fulani kulingana na yale wao wenyewe wanayoyafanya, licha ya kuwepo mengi ambayo watu hawawezi kuyafikia kabisa. Kile ambacho watu hawawezi kufanikisha kinakuwa kizuizi katika kuingia kwao.
Kuna mkengeuko mdogo zaidi katika kazi ya wale ambao wamepitia kupogolewa, kushughulikiwa, hukumu na kuadibu, na uonyeshaji wa kazi zao ni sahihi zaidi. Wale wanaotegemea asili yao katika kufanya kazi wanafanya makosa makubwa sana. Kuna uasili mwingi sana katika kazi ya watu ambao si wakamilifu, kitu ambacho kinaweka kizuizi kikubwa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi ubora wa tabia ya mtu ulivyo mzuri, lazima pia apitie upogoaji, ashughulikiwe, na kuhukumiwa kabla aweze kufanya kazi ya agizo la Mungu. Kama hajapitia hukumu kama hiyo, kwa namna yoyote nzuri ile atakavyofanya, haiwezi kuambatana na kanuni za ukweli na ni uasili kabisa na uzuri wa mwanadamu. Kazi ya wale ambao wamepitia kupogolewa, kushughulikiwa, na hukumu ni sahihi zaidi kuliko kazi ya wale ambao hawajapogolewa, kushughulikiwa, na hukumiwa. Wale ambao hawajapitia hukumu hawaonyeshi chochote isipokuwa mawazo ya kibinadamu, yakiwa yamechanganyika na ufahamu wa kibinadamu na talanta za ndani. Sio maonyesho sahihi wa mwanadamu wa kazi ya Mungu. Watu wanaowafuata wanaletwa mbele yao kwa tabia yao ya ndani. Kwa sababu wanaonyesha vitu vingi vya kuona na uzoefu wa mwanadamu, ambavyo takribani havina muungano na nia ya asili ya Mungu, na hutofautiana sana nayo, kazi ya mtu wa aina hii haiwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu, bali badala yake huwaleta mbele ya mwanadamu. Hivyo, wale ambao hawajapitia hukumu na kuadibu, hawana sifa za kufanya kazi ya agizo la Mungu. Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu. Anaweza kuwaleta watu katika kanuni tu; kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu mwingine; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu. Katika kazi ya aina hii kunakuwa na kanuni nyingi sana na mafundisho mengi sana, na haiwezi kuwaleta watu katika uhalisia au katika hali ya kawaida ya kukua katika uzima. Inaweza kuwawezesha watu tu kusimama kwa kanuni chache zisizokuwa na maana. Uongozi wa namna hii unaweza tu kuwapotosha watu. Anakuongoza ili uwe kama yeye; anaweza kukuleta katika kile anacho na kile alicho. Kwa wafuasi kutambua endapo viongozi wana sifa, jambo la muhimu ni kuangalia njia wanayoiongoza na matokeo ya kazi yao, na kuangalia iwapo wafuasi wanapokea kanuni kulingana na ukweli, na kama wanapokea namna ya kutenda kunakowafaa wao ili waweze kubadilishwa. Unapaswa kutofautisha kati ya kazi tofauti za aina tofauti za watu; haupaswi kuwa mfuasi mpumbavu. Hili linaathiri suala la kuingia kwako. Kama huwezi kutofautisha ni uongozi wa mtu yupi una njia na upi hauna, utadanganywa kwa urahisi. Haya yote yana athari ya moja kwa moja katika maisha yako. Kuna mambo mengi ya asili katika kazi ya mtu ambaye hajakamilishwa; matakwa mengi ya kibinadamu yamechanganywa humo. Hali yao ni ya asili, kile walichozaliwa nacho, si maisha baada ya kupitia kushughulikiwa au uhalisia baada ya kubadilishwa. Ni kwa namna gani mtu wa aina hii ya mtu anaweza kuunga mkono utafutaji wa uzima? Maisha halisi ya mwanadamu ni akili au talanta yake ya ndani. Aina hii ya akili au talanta ni kinyume cha kile hasa ambacho Mungu anamtaka mwanadamu afanye. Ikiwa mwanadamu hajakamilishwa na tabia yake potovu haijapogolewa na kushughulikiwa, kutakuwa na pengo kubwa kati ya kile anachokionyesha na ukweli; utachanganywa na vitu visivyoeleweka vizuri kama vile tafakari zake na uzoefu wa upande mmoja, n.k. Aidha, bila kujali jinsi anavyofanya kazi, watu wanahisi kwamba hakuna lengo la jumla na hakuna ukweli ambao unafaa kwa kuingia watu wote. Matakwa mengi yanawekwa kwa watu wakitakiwa kufanya kile ambacho ni nje ya uwezo wao, kumwingiza bata katika kitulio cha ndege. Hii ni kazi ya matakwa ya binadamu. Tabia potovu ya mwanadamu, mawazo yake na fikira vinaenea katika sehemu zote za mwili wake. Mwanadamu hakuzaliwa na tabia ya kutenda ukweli, na wala hana tabia ya kuuelewa ukweli moja kwa moja. Ikiongezwa kwa upotovu ya mwanadamu—mtu wa aina hii ya asili anapofanya kazi, je, si yeye husababisha ukatizaji? Lakini mwanadamu ambaye amekamilishwa ana uzoefu wa ukweli ambao watu wanapaswa kuuelewa, na maarifa ya tabia yao potovu, ili kwamba vitu visivyoeleweka vizuri na visivyokuwa halisi katika kazi yake vididimie kwa taratibu, ughushi wa binadamu upungue, na kazi na huduma yake yakaribie zaidi viwango vinavyohitajika na Mungu. Hivyo, kazi yake imeingia katika uhalisi wa ukweli na pia imekuwa halisi zaidi. Mawazo katika akili ya mwanadamu yanazuia kazi ya Roho Mtakatifu. Mwanadamu ana fikira nzuri na mwenye mantiki ya maana na uzoefu mkongwe katika kukabiliana na mambo. Kama haya yote hayatapitia kupogolewa na kusahihishwa, yote yanakuwa vizuizi katika kazi. Hivyo kazi ya mwanadamu haiwezi kufikia kiwango cha juu cha usahihi, hususan kazi ya watu ambao hawajakamilishwa.
Kazi ya mwanadamu ina mipaka na kadiri inavyoweza kufika. Mtu mmoja anaweza tu kufanya kazi ya wakati fulani na hawezi kufanya kazi ya enzi nzima—vinginevyo, angewaongoza watu katika kanuni. Kazi ya mwanadamu inaweza kufaa tu katika kipindi au awamu fulani. Hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu una mawanda. Mtu hawezi kulinganisha kazi ya mwanadamu na kazi ya Mungu. Njia za mwanadamu kutenda na maarifa yake ya ukweli yote yanatumika tu katika mawanda fulani. Huwezi kusema kwamba njia ambayo mwanadamu anaiendea ni matakwa ya Roho Mtakatifu kabisa, kwa sababu mwanadamu anaweza kupewa nuru na Roho Mtakatifu tu na hawezi kujazwa kikamilifu na Roho Mtakatifu. Vitu ambavyo mwanadamu anaweza kuvipitia vyote vipo ndani ya mawanda ya ubinadamu na haviwezi kuzidi mawanda ya fikira katika akili ya kawaida ya mwanadamu. Wale wote wanaoweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli hupitia ndani ya mawanda haya. Wanapoupitia ukweli, siku zote ni uzoefu wa maisha ya kawaida ya mwanadamu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu, sio kupitia uzoefu kwa namna ambayo inakengeuka kutoka kwa maisha ya kawaida ya mwanadamu. Wanapitia uzoefu wa ukweli ambao unatiwa nuru na Roho Mtakatifu katika msingi wa kuishi maisha yao ya kibinadamu. Aidha, ukweli huu unatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, na kina chake kinahusiana na hali ya mtu huyo. Mtu anaweza kusema kwamba njia anayoipitia ni maisha ya kawaida ya kibinadamu ya mwanadamu kufuatilia ukweli na kwamba hiyo ndiyo njia ambayo mtu wa kawaida ambaye amepata nuru ya Roho Mtakatifu anaipita. Huwezi kusema kwamba njia wanayoipitia ni njia ambayo inafuatwa na Roho Mtakatifu. Katika uzoefu wa kawaida wa binadamu, kwa sababu watu wanaoutafuta ukweli hawafanani, kazi ya Roho Mtakatifu pia haifanani. Aidha, kwa sababu mazingira wanayoyapitia na kiwango cha uzoefu wao havifanani, kwa sababu ya mchanganyiko wa akili na mawazo yao, uzoefu wao pia umechanganyika kwa kiwango tofauti. Kila mtu anaelewa ukweli kulingana na hali yake tofauti ya kibinafsi. Ufahamu wao wa maana halisi ya ukweli hauko kamili, na ni kipengele chake kimoja tu au vichache. Mawanda ambayo ukweli unaeleweka kwa mwanadamu siku zote umejikita katika hali tofauti tofauti za watu, na hivyo hazifanani. Kwa njia hii, maarifa yanayoonyesha ukweli ule ule na watu tofauti havifanani. Huu kusema, uzoefu wa mwanadamu siku zote una mipaka, na hauwezi kuwakilisha kikamilifu matakwa ya Roho Mtakatifu, na kazi ya mwanadamu haiwezi kuchukuliwa kama kazi ya Mungu, hata kama kile kinachoonyeshwa na mwanadamu kinafanana kwa karibu sana na mapenzi ya Mungu, hata kama uzoefu wa mwanadamu unakaribiana sana na kazi ya ukamilifu itakayofanywa na Roho Mtakatifu. Mwanadamu anaweza kuwa tu mtumishi wa Mungu, akifanya kazi ambayo Mungu amemwaminia. Mwanadamu anaweza kuonyesha maarifa tu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu na ukweli alioupata kutokana na uzoefu wake binafsi. Mwanadamu hana sifa na hana vigezo vya kuwa njia ya Roho Mtakatifu. Hana uwezo wa kusema kuwa kazi ya mwanadamu ni kazi ya Mungu. Mwanadamu ana kanuni za kufanya kazi za mwanadamu, na wanadamu wote wana uzoefu tofauti na wana hali zinazotofautiana. Kazi ya mwanadamu inajumuisha uzoefu wake wote chini ya nuru ya Roho Mtakatifu. Uzoefu huu unaweza tu kuwakilisha asili ya mwanadamu na hauwakilishi asili ya Mungu, au mapenzi ya Roho Mtakatifu. Kwa hivyo, njia anayoipita mwanadamu haiwezi kusemwa kuwa njia anayoipita Roho Mtakatifu, kwa sababu kazi ya mwanadamu haiwezi kuwakilisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu na uzoefu wa mwanadamu sio matakwa ya Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu ina hatari ya kuangukia katika kanuni, na mbinu za kazi yake zimefinywa katika uelewa wake finyu na hawezi kuwaongoza watu katika njia huru. Wafuasi wengi wanaishi ndani ya mawanda finyu, na uzoefu wao pia unakuwa ni finyu. Uzoefu wa mwanadamu siku zote ni finyu; mbinu ya kazi yake pia ni finyu na haiwezi kulinganishwa na kazi ya Roho Mtakatifu au kazi ya Mungu Mwenyewe—hii ni kwa sababu uzoefu wa mwanadamu, hatimaye, ni finyu. Hata hivyo Mungu anafanya kazi Yake, hakuna kanuni kwa kazi yake; vyovyote vile inavyofanywa, haifungwi na njia moja. Hakuna kanuni za aina yoyote ile katika kazi ya Mungu—kazi Yake yote ni huru na ni bure. Haijalishi ni muda kiasi gani mwanadamu anatumia kumfuata Yeye, hawawezi kutengeneza sheria zozote za njia anavyofanya kazi. Ingawaje kazi Yake inaongozwa na kanuni, siku zote inafanywa katika njia mpya na siku zote inakuwa na maendeleo mapya ambayo yanazidi uwezo wa mwanadamu. Katika kipindi fulani, Mungu anaweza kuwa na njia nyingi tofauti tofauti za kazi na njia tofauti za kuongoza, Akiruhusu watu siku zote kuwa na kuingia kupya na mabadiliko mapya. Huwezi kuelewa sheria za kazi Yake kwa sababu siku zote Anafanya kazi katika njia mpya. Ni kwa njia hii tu ndiyo wafuasi wa Mungu hawawezi kuanguka katika kanuni. Kazi ya Mungu Mwenyewe siku zote inaepuka mitazamo ya watu na kupinga mitazamo yao. Ni wale tu ambao wanamfuata Yeye kwa moyo wote ndio wanaoweza kubadilishwa tabia zao na wanaweza kuishi kwa uhuru bila kuwa chini ya kanuni zozote au kufungwa na mitazamo yoyote ya kidini. Madai ambayo kazi ya mwanadamu inawawekea watu yamejikita katika uzoefu wake mwenyewe na kile ambacho yeye mwenyewe anaweza kutimiza. Kiwango cha matakwa haya kimejifunga ndani ya mawanda fulani, na mbinu za kutenda pia ni finyu sana. Kwa hivyo wafuasi bila kutambua huishi ndani ya matakwa finyu; kadiri muda unavyokwenda, yanakuwa kanuni na taratibu za kidini. Ikiwa kazi ya kipindi fulani inaongozwa na mtu ambaye hajapitia kukamilishwa na Mungu na hakupokea hukumu, wafuasi wake wote watakuwa wadini na wataalamu wa kumpinga Mungu. Kwa hivyo, ikiwa mtu fulani ni kiongozi aliyehitimu, mtu huyo anapaswa kuwa amepitia hukumu na kukubali kukamilishwa. Wale ambao hawajapitia mchakato wa hukumu, hata kama wanaweza kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu, wanaonyesha vitu ambavyo si dhahiri na visivyokuwa halisi. Kadiri muda unavyozidi kwenda, watawaongoza watu katika kanuni zisizoeleweka vizuri na za kimuujiza. Kazi ambayo Mungu anafanya haiambatani na mwili wa mwanadamu; haiambatani na mawazo ya mwanadamu bali inapinga mitazamo ya mwanadamu; haijachanganyika na mitazamo ya kidini isiyoeleweka vizuri. Matokeo ya kazi Yake hayawezi kupatikana kwa mwanadamu ambaye hajakamilishwa na Yeye na yapo nje ya uwezo wa fikira za mwanadamu.
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho yao mengi ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufichua fikira zao, sembuse kuwapogoa watu kwa ajili ya upungufu wao wa dhambi. Wengi wanaowafuata wanahudu kwa vipaji vyao, na yote wanayotoa ni fikira za kidini na nadharia za theolojia, ambazo haziambatani na uhalisi na haziwezi kabisa kuwapa watu uzima. Kwa kweli, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza. Kwa miaka elfu sita ya kazi ya Mungu unaweza kupata sheria zozote kuihusu? Kuna kanuni na vizuizi vingi katika kazi ambayo mwanadamu hufanya, na ubongo wa mwanadamu umejazwa na mafundisho mengi ya kidini. Hivyo mwanadamu anachokionyesha ni kiasi cha maarifa na utambuzi ndani ya uzoefu wake wote. Mwanadamu hawezi kuonyesha kitu chochote zaidi ya hiki. Uzoefu au maarifa ya mwanadamu hayaibuki kutoka ndani ya karama zake za ndani au tabia yake; vinaibuka kwa sababu ya uongozi wa Mungu na uchungaji wa moja kwa moja wa Mungu. Mwanadamu ana ogani tu ya kupokea uongozi huu na sio ogani ya kuonyesha moja kwa moja uungu. Mwanadamu hana uwezo wa kuwa chanzo, anaweza kuwa tu chombo ambacho hupokea maji kutoka kwa chanzo; hii ni silika ya mwanadamu, ogani ambayo mtu anapaswa kuwa nayo kama mwanadamu. Ikiwa mtu anapoteza ogani ya kukubali neno la Mungu na kupoteza silika ya kibinadamu, mtu huyo anapoteza pia kile ambacho ni cha thamani sana, na anapoteza wajibu wa mwanadamu aliyeumbwa. Ikiwa mtu hana maarifa au uzoefu wa neno la Mungu au kazi Yake, mtu huyo anapoteza wajibu wake, wajibu anaopaswa kuutimiza kama kiumbe aliyeumbwa, na kupoteza heshima ya kiumbe aliyeumbwa. Ni silika ya Mungu kuonyesha uungu ni nini, kama unaonyeshwa katika mwili au moja kwa moja na Roho Mtakatifu; hii ni huduma ya Mungu. Mwanadamu anaonyesha uzoefu wake mwenyewe au maarifa (yaani, anaonyesha kile alicho) wakati wa kazi ya Mungu au baada yake; hii ndiyo silika ya mwanadamu na wajibu wa mwanadamu, ndicho kitu ambacho mwanadamu anapaswa kukifikia. Ingawa maonyesho ya mwanadamu ni duni sana kuliko kile ambacho Mungu anaonyesha, na kuna kanuni nyingi katika kile ambacho mwanadamu huonyesha, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu anaopaswa kutimiza na kufanya kile anachopaswa kufanya. Mwanadamu anapaswa kufanya kitu chochote kinachowezekana kwa mwanadamu kufanya ili kutimiza wajibu wake, na hapaswi kuacha kitu hata kidogo.
Baada ya kufanya kazi kwa miaka mingi, mwanadamu atakuwa na uzoefu wa miaka hii yote, vile vile atakuwa na hekima na kanuni alizozipata. Yeye anayefanya kazi kwa muda mrefu anajua jinsi ya kuelewa kusonga kwa Roho Mtakatifu, anajua ni wakati gani Roho Mtakatifu anafanya kazi na wakati gani Hafanyi; anajua jinsi ya kufanya ushirika akiwa amebeba mzigo, anaitambua hali ya kawaida ya kazi ya Roho Mtakatifu na hali ya kawaida ya ukuaji wa watu katika maisha. Huyo ni mtu ambaye amefanya kazi kwa miaka mingi na anaijua kazi ya Roho Mtakatifu. Wale ambao wamefanya kazi kwa muda mrefu wanazungumza kwa uhakika na bila haraka; hata wakati ambapo hawana kitu cha kusema wanakuwa watulivu. Kwa ndani, wanaweza kuendelea kuomba ili kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kupata utiifu wa kweli kwa Mungu; wana uzoefu katika kufanya kazi. Mtu ambaye amefanya kazi kwa muda mrefu na ana masomo na uzoefu mkubwa ana vitu vingi ndani ambavyo vinazuia kazi ya Roho Mtakatifu; hii ni dosari ya kufanya kazi kwa muda mrefu. Mtu ambaye ameanza tu kufanya kazi hajaleta katika kazi masomo au uzoefu wa kibinadamu, hususan kuhusu jinsi ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi. Hata hivyo, wakati wa kufanya kazi, taratibu anaanza kuelewa jinsi ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi na anakuwa na utambuzi wa jinsi ya kufanya ili kupata kazi ya Roho Mtakatifu, kile cha kufanya ili kupiga udhaifu wa wengine kabisa, na ufahamu mwingine wa kawaida ambao wale wanaofanya kazi wanapaswa kuwa nao. Kadiri muda unavyokwenda, anapata kujua hekima hiyo na maarifa ya kawaida kuhusu kufanya kazi kwa ufasaha mkubwa sana, na anaonekana kuyatumia kwa urahisi anapofanya kazi. Hata hivyo, Roho Mtakatifu anapobadilisha namna Anavyofanya kazi, bado anakuwa amejikita katika maarifa yake ya zamani ya kufanya kazi na kanuni zake za zamani za kufanya kazi na anajua kidogo sana kuhusu harakati mpya za kufanya kazi. Miaka mingi ya kufanya kazi na kuwa katika uongozi na uwepo kamili wa Roho Mtakatifu kunampa masomo mengi zaidi ya kufanya kazi na uzoefu mwingi. Vitu kama hivyo vinamjaza kujiamini ambako sio kiburi. Kwa maneno mengine, anafurahishwa kabisa na kazi yake mwenyewe na kuridhika sana na maarifa ya kawaida aliyoyapata kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu. Hasa, vitu vile ambavyo watu wengine hawakuvipata au kuvitambua vinampatia kujiamini zaidi kwa nafsi yake; inaonesha kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ndani yake haiwezi kuzimwa kamwe, na wengine hawana sifa ya kutendewa hivi. Watu wa aina hii ambao wamefanya kazi kwa miaka mingi na ambao wameitumia thamani ndio wana sifa ya kuifurahia. Vitu hivi vinakuwa ni kikwazo kikubwa katika kukubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Hata kama anaweza kuikubali kazi mpya, si kitu cha kuibuka mara moja. Kwa uhakika atapitia michakato kadhaa kabla ya kuikubali. Hali hii inaweza kugeuka taratibu baada ya fikira zake za zamani kushughulikiwa na tabia yake ya zamani kuhukumiwa. Bila ya kupitia hatua hizi, habadiliki na kukubali kwa urahisi mafundisho mapya na kazi ambayo haikubaliani na fikira zake za zamani. Hiki ndicho kitu kigumu zaidi kushughulika nacho katika mwanadamu, na sio rahisi kuibadilisha. Ikiwa, kama mtenda kazi, ana uwezo wa kupata na kuielewa kazi ya roho Mtakatifu na kuutambua mchakato wake, vile vile ana uwezo wa kutozuiwa na uwezo wake wa kufanya kazi na kuwa na uwezo wa kuikubali kazi mpya katika mwanga wa kazi ya zamani, ni mtu mwenye hekima na mtenda kazi mwenye sifa. Wanadamu huwa hivi mara nyingi: Wanafanya kazi kwa miaka mingi bila kuweza kufupisha uzoefu wao wa maisha, ama baada ya kufupisha uzoefu na hekima yao, wanazuiwa kukubali kazi mpya na hawawezi kuelewa kwa usahihi au kuishughulikia kwa usahihi kazi ya zamani na mpya. Wanadamu hakika ni wagumu kuwaongoza! Wengi wenu mko hivi. Wale ambao wamepitia uzoefu wa miaka katika kazi ya Roho Mtakatifu wanaona vigumu kuikubali kazi mpya, mara nyingi wanakuwa wamejazwa mitazamo ambayo wanaona ni vigumu kuiacha, ilhali mtu ambaye ameanza tu kazi anakosa maarifa ya kawaida kuhusu kufanya kazi na hajui hata jinsi ya kushughulikia masuala rahisi kabisa. Nyinyi watu ni wagumu kweli kweli! Wale wenye vyeo fulani nyuma yao wana kiburi na majivuno kweli kiasi kwamba wamesahau kule walikotoka. Siku zote wanawadharau wadogo, ila bado hawawezi kukubali kazi mpya na hawawezi kuachana na fikira walizoikusanya na kuziweka kwa miaka mingi sana. Ingawa hao watu wadogo wasiokuwa na maarifa wanaweza kukubali kiasi kidogo cha kazi ya Roho Mtakatifu na wana shauku kubwa, daima wanachanganyikiwa na hawajui cha kufanya wanapokutana na matatizo. Ingawa wana shauku, wao ni wajinga mno. Wana ufahamu mdogo tu wa kazi ya Roho Mtakatifu na hawawezi kuutumia katika maisha yao; huwa ni mafundisho tu ambayo hayana maana kabisa. Kuna watu wengi kama wewe; ni wangapi wanafaa kwa ajili ya kutumika? Kuna wangapi wanaoweza kutii nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu na waweze kutimiza mapenzi ya Mungu? Inaonekana kwamba wale ambao mmekuwa wafuasi hadi sasa mmekuwa watiifu, lakini kwa kweli, hamjaachana na fikira zenu, bado mnatafuta kwenye Biblia, mkiamini mambo yasiyo dhahiri, au kuzurura katika fikira. Hakuna yeyote ambaye huchunguza kazi halisi ya leo au kuzama ndani yake. Mnaikubali njia ya leo kwa mitazamo yenu ya zamani. Mtafaidika vipi na imani kama hiyo? Inaweza kusemwa kuwa ndani yenu mmefichwa fikira nyingi ambazo zinafichuliwa, na kwamba mnafanya tu jitihada kubwa kuificha na msiweze kuifunua kwa urahisi. Hamkubali kazi mpya kwa uaminifu na hampangi kuachana na fikira zenu za zamani; mna falsafa nyingi sana za kuishi nazo ni kubwa sana. Hamwachi fikira zenu za zamani na kwa shingo upande mnashughulika na kazi mpya. Mioyo yenu ni miovu sana, na hamchukui hatua ya kazi mpya katika moyo. Mtu mzembe kama nyinyi anaweza kufanya kazi ya kueneza injili? Mnaweza kuchukua kazi mpya ya kueneza injili katika ulimwengu mzima? Matendo yenu haya yanawazuia kubadilisha tabia yenu na kumjua Mungu. Mkiendelea hivi, mwisho wake mtaondolewa.
Mnapaswa kujua jinsi ya kutofautisha kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Mnaweza kuona nini katika kazi ya mwanadamu? Kuna vitu vingi ambavyo ni uzoefu wa mwanadamu katika kazi ya mwanadamu; kile ambacho mwanadamu anakionyesha kile alicho. Kazi ya Mungu pia inaonyesha kile Alicho, lakini kile Alicho ni tofauti na mwanadamu alivyo. Kile mwanadamu alicho ni kiwakilishi cha uzoefu na maisha ya mwanadamu (kile ambacho mwanadamu anakipitia au kukabiliana nacho katika maisha yake, au falsafa za kuishi alizo nazo), na watu wanaoishi katika mazingira tofauti huonyesha nafsi tofauti. Kama una uzoefu wa kijamii au la na jinsi ambavyo unaishi na kupitia uzoefu katika familia yako inaweza kuonekana katika kile unachokionyesha, wakati ambapo huwezi kuona kutoka kwa kazi ya Mungu mwenye mwili kama Ana uzoefu wa maisha ya kijamii au Hana. Anatambua vizuri asili ya mwanadamu, Anaweza kufunua aina za matendo yote yanayohusiana na kila aina ya watu. Ni mzuri hata katika kufunua tabia ya dhambi ya mwanadamu na tabia yake ya uasi. Haishi miongoni mwa watu wa kidunia, lakini Anatambua asili ya watu wenye mwili wa kufa na upotovu wote wa watu wa duniani. Hicho ndicho Alicho. Ingawa Hashughuliki na dunia, Anajua kanuni za kushughulika na dunia, kwa sababu Anaielewa vizuri asili ya mwanadamu. Anajua kuhusu kazi ya Roho ambayo jicho la mwanadamu haliwezi kuiona na kwamba masikio ya mwanadamu hayawezi kusikia, wanadamu wa leo na wanadamu wa enzi zote. Hii inajumuisha hekima ambayo sio falsafa ya kuishi na makuu ambayo ni ngumu kwa watu kuelewa. Hiki ndicho Alicho, kuwekwa wazi kwa watu na pia kufichika kwa watu. Kile Anachoonyesha sio kile ambacho mwanadamu asiye wa kawaida alicho, bali ni tabia za asili na uungu wa Roho. Hasafiri ulimwenguni mzima lakini anajua kila kitu kuhusu ulimwengu. Anawasiliana na “sokwe” ambao hawana maarifa au akili, lakini Anaonyesha maneno ambayo ni ya kiwango cha juu kuliko maarifa na juu ya watu wakubwa duniani. Anaishi miongoni mwa kundi la wanadamu wapumbavu na wasiojali ambao hawana ubinadamu na ambao hawaelewi mila na desturi za ubinadamu na maisha, lakini Anaweza kumwambia mwanadamu kuishi maisha ya kawaida, na kwa wakati uo huo kufichua ubinadamu duni na wa chini wa binadamu. Haya yote ndiyo kile Alicho, mkuu kuliko vile ambacho mwanadamu yeyote wa damu na nyama alicho. Kwake Yeye, si lazima kupitia maisha ya kijamii magumu na changamani, ili Aweze kufanya kazi Anayotaka kufanya na kwa kina kufichua asili ya mwanadamu aliyepotoka. Maisha duni ya kijamii ambayo hayauadilishi mwili Wake. Kazi Yake na maneno Yake hufichua tu kutotii kwa mwanadamu na hayampi mwanadamu uzoefu na masomo kwa ajili ya kushughulika na ulimwengu. Hahitaji kuipeleleza jamii au familia ya mwanadamu wakati Anapompa mwanadamu uzima. Kumweka wazi na kumhukumu wanadamu sio maonyesho wa uzoefu wa mwili Wake; ni kufichua vile mwanadamu asivyokuwa na haki baada ya kufahamu kutotii kwa mwanadamu na kuchukia upotovu wa mwanadamu. Kazi yote Anayoifanya ni kufichua tabia Yake kwa mwanadamu na kuonyesha asili Yake. Ni Yeye tu ndiye anayeweza kuifanya kazi hii, sio kitu ambacho mtu mwenye mwili na damu anaweza kukipata. Kwa kuangalia kazi Yake, mwanadamu hawezi kuelezea Yeye ni mtu wa aina gani. Mwanadamu hawezi kumwainisha kama mtu aliyeumbwa kwa misingi ya kazi Yake. Kile Alicho pia kinamfanya Asiweze kuainishwa kama mtu aliyeumbwa. Mwanadamu anaweza kumwona tu kama Asiye mwanadamu, lakini hajui amwainishe katika kundi gani, kwa hivyo mwanadamu analazimika kumwainisha katika kundi la Mungu. Si busara kwa mwanadamu kufanya hivi, kwa sababu Amefanya kazi kubwa miongoni mwa watu, ambayo mwanadamu hawezi kufanya.
Kazi ambayo Mungu anafanya haiwakilishi uzoefu wa mwili Wake; kazi ambayo mwanadamu anafanya inawakalisha uzoefu wa mwanadamu. Kila mtu anazungumza kuhusu uzoefu wake binafsi. Mungu anaweza kuonyesha ukweli moja kwa moja, wakati mwanadamu anaweza tu kuonyesha uzoefu unaolingana na huo baada ya kupata uzoefu wa ukweli. Kazi ya Mungu haina masharti na haifungwi na muda au mipaka ya kijiografia. Anaweza kuonyesha kile Alicho wakati wowote, mahali popote. Anafanya kazi vile Anavyopenda. Kazi ya mwanadamu ina masharti na muktadha; vinginevyo hana uwezo wa kufanya kazi na hawezi kuonyesha ufahamu wake wa Mungu au uzoefu wake wa ukweli. Unatakiwa tu kulinganisha tofauti baina yao ili kuonyesha kama ni kazi ya Mungu mwenyewe au kazi ya mwanadamu. Kama hakuna kazi inayofanywa na Mungu Mwenyewe, na kuna kazi tu ya mwanadamu, utajua tu kwamba mafundisho ya mwanadamu ni makuu, zaidi ya uwezo wa mtu yeyote yule; toni yao ya kuzungumza, kanuni zao katika kushughulikia mambo na uwezo wao katika kufanya kazi ni zaidi ya uwezo wa wengine. Nyinyi nyote mnavutiwa na watu hawa wa ubora mzuri wa tabia na maarifa ya juu, lakini hamwezi kuona kutoka katika kazi na maneno ya Mungu jinsi ubinadamu Wake ulivyo wa juu. Badala yake, Yeye ni wa kawaida, na Anapofanya kazi, Yeye ni wa kawaida na halisi lakini pia hapimiki kwa watu wenye mwili wa kufa, kitu ambacho kinawafanya watu wahisi kumheshimu sana. Pengine uzoefu wa mtu katika kazi yake ni mkubwa sana, au mawazo na fikira zake ni za juu sana, na ubinadamu wake ni mzuri hasa; hivi vinaweza kutamaniwa na watu tu, lakini visiamshe kicho na hofu yao. Watu wote wanawatamani wale ambao wana uwezo wa kufanya kazi na ambao wana uzoefu wa kina na wanaweza kuutenda ukweli, lakini hawawezi kuvuta kicho, bali kutamani na kijicho. Lakini watu ambao wamepitia uzoefu wa kazi ya Mungu hawamtamani Mungu, badala yake wanahisi kwamba kazi Yake haiwezi kufikiwa na mwanadamu na haiwezi kueleweka na mwanadamu, na kwamba ni nzuri na ya kushangaza. Watu wanapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu, ufahamu wao wa kwanza kumhusu ni kwamba Yeye ni asiyeeleweka, ni mwenye hekima na wa ajabu na wanamcha bila kujua na kuihisi siri ya kazi Anayoifanya, ambayo inapita akili ya mwanadamu. Watu wanataka tu kuwa na uwezo wa kukidhi matakwa Yake, kuridhisha matamanio Yake; hawatamani kumpita Yeye, kwa sababu kazi anayoifanya inazidi fikira za mwanadamu na haiwezi kufanywa na mwanadamu kama mbadala. Hata mwanadamu mwenyewe hayajui mapungufu yake, wakati Amefungua njia mpya na kumleta mwanadamu katika dunia mpya zaidi na nzuri zaidi, kwamba mwanadamu amefanya maendeleo mapya na kuwa na mwanzo mpya. Kile ambacho watu wanahisi kumhusu Mungu, sio matamanio, au sio matamanio tu. Uzoefu wake wa kina ni kicho na upendo, hisia zake ni kwamba Mungu kweli ni wa ajabu sana. Anafanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya na kusema mambo ambayo mwanadamu hawezi kusema. Watu ambao wamepitia kazi ya Mungu daima wana hisia isiyoweza kuelezeka. Watu wenye uzoefu wa kina kutosha wanaweza kuelewa ukweli wa Mungu; wanaweza kuhisi uzuro Wake, kwamba kazi Yake ni ya hekima sana, ya ajabu sana, na hivyo hii inazalisha nguvu isiyokoma ndani yao. Si woga au upendo wa mara moja moja na heshima, bali hisia za ndani za upendo wa Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Hata hivyo, watu ambao wamepata uzoefu wa kuadibu na hukumu Yake wanamhisi kuwa Yeye mtukufu na asiyekosewa. Hata watu ambao wamepitia uzoefu mkubwa wa kazi Yake pia hawawezi kumwelewa; watu wote wanaomcha wanajua kwamba kazi Yake hailingani na fikira za watu lakini siku zote inakwenda kinyume na fikira zao. Haihitaji watu wamtamani kabisa au kuwa na kuonekana kwa kujikabidhi Kwake, badala yake anataka wawe na uchaji wa kweli na kutii kikamilifu. Katika nyingi ya kazi Yake, mtu yeyote mwenye uzoefu wa kweli anahisi heshima Kwake, ambayo ni ya juu kuliko matamanio. Watu wameiona tabia Yake kwa sababu ya kazi Yake ya kuadibu na hukumu, na kwa hiyo wanamcha mioyoni mwao. Mungu anapaswa kuchiwa na kutiiwa, kwa sababu uungu Wake na tabia Yake havifanani kama ule wa watu walioumbwa na vikuu juu ya vile vya watu walioumbwa. Mungu hategemei chochote kuwepo na ni wa milele, Yeye siye kiumbe Aliyeumbwa, na ni Mungu tu anayestahili uchaji na utiifu; mwanadamu hana sifa ya kupewa hivi. Hivyo, watu wote waliopitia uzoefu wa kazi Yake na kweli wanamjua wanampatia heshima. Hata hivyo, wale ambao hawaachani fikira zao kumhusu, yaani, wale ambao hawamwoni kuwa Mungu, hawana uchaji wowote Kwake, na hata ingawa wanamfuata hawajashindwa; ni watu wasiotii kwa asili yao. Anafanya kazi hii ili apate matokeo kwamba viumbe vyote vilivyoumbwa vinaweza kumcha Muumbaji, vimwabudu Yeye, na kujikabidhi katika utawala Wake bila masharti. Haya ni matokeo ya mwisho ambayo kazi Yake yote inalenga kuyapata. Ikiwa watu ambao wamepitia kazi hiyo hawamchi Mungu, hata kidogo, kama kutotii kwao kwa zamani hakutabadilika kabisa, basi watu hawa ni hakika wataondolewa. Kama mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu ni kumtamani au kuonyesha heshima kwa mbali na sio kumpenda, hata kidogo, hivi ndivyo mtu bila moyo wa kumpenda Mungu anapofikia, na mtu wa aina hiyo anakosa hali za kumwezesha kukamilishwa. Ikiwa kazi nyingi vile haiwezi kupata upendo wa kweli wa mtu, hii ina maana kwamba mtu huyo hajampata Mungu na kwa uhalisi hatafuti kuujua ukweli. Mtu ambaye hampendi Mungu hapendi ukweli na hivyo hawezi kumpata Mungu, sembuse kupata ukubali wa Mungu. Watu kama hao, bila kujali jinsi wanavyopata uzoefu wa Roho Mtakatifu, na bila kujali jinsi gani wanapitia uzoefu wa hukumu, bado hawawezi kumcha Mungu. Hawa ni watu ambao asili yao haiwezi kubadilishwa, ambao wana tabia ya uovu uliokithiri. Wale wote ambao hawamchi Mungu wataondolewa, na kuwa walengwa wa hukumu, na kuadhibiwa kama tu wale ambao wanafanya uovu, watateseka hata zaidi ya wale ambao wamefanya matendo maovu.