Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?

Je, unaweza kuwasilisha tabia inayoonyeshwa na Mungu katika kila enzi kwa njia thabiti, kwa lugha inayofaa na inayowasilisha umuhimu wa enzi hiyo? Je, wewe unayepitia kazi ya Mungu ya siku za mwisho unaweza kueleza tabia ya Mungu yenye haki kwa utondoti? Je, unaweza kushuhudia kuhusu tabia ya Mungu kwa uwazi na usahihi? Je, utazungumzia vipi yale uliyoyaona na kuyapitia kwa wale waumini wa kidini wenye kusikitisha, duni, na wacha Mungu ambao wana njaa na kiu ya haki na wanakungoja wewe uwachunge? Ni watu wa aina gani ndio wanokungoja wewe uwachunge? Unaweza kuwaza kweli? Je, unafahamu mzigo ulio mabegani mwako, agizo lako, na jukumu lako? Hisia yako ya misheni ya kihistoria iko wapi? Utatumikiaje ipasavyo kama bwana wa enzi ijayo? Je, una hisia thabiti ya kuwa bwana? Bwana wa vitu vyote anapaswa kuelezwaje? Je, kwa kweli ni bwana wa viumbe hai wote na vitu vyote vya kimwili ulimwenguni? Una mipango gani ya maendeleo ya awamu inayofuata ya kazi? Ni watu wangapi wanaokungoja wewe uwachunge? Je, kazi yako ni nzito? Wao ni duni, wa kusikitisha, vipofu, na waliochanganyikiwa, wakilomboleza gizani—njia iko wapi? Jinsi wanavyotamani nuru, kama nyota inayochomoka, ishuke ghafla na kuondoa nguvu za giza ambazo zimemkandamiza mwanadamu kwa miaka mingi. Wanatumaini kwa hamu, na kutamani, mchana na usiku—ni nani anayeweza kujua hili kikamilifu? Hata siku ambayo nuru inapita kwa kasi, watu hawa wanaoteseka sana hubaki wamefungwa katika gereza la giza bila tumaini la kuachiliwa; watalia hadi lini? Ni bahati mbaya iliyoje ya roho hizi dhaifu ambazo hazijawahi kupata pumziko, na kwa muda mrefu zimefungwa katika hali hii kwa minyororo isiyo na huruma na historia iliyoganda. Na ni nani amesikia sauti ya kilio chao? Ni nani aliyeona hali yao ya kuhuzunisha? Je, umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyo na huzuni na wasiwasi? Anawezaje kuvumilia kuuona wanadamu wasio na hatia, ambao Yeye aliwaumba kwa mikono Yake Mwenyewe, wakiteseka mateso kama hayo? Wanadamu, hata hivyo, ndio wahasiriwa ambao wametiwa sumu. Na ingawa mwanadamu ameokoka hadi leo, ni nani angejua kwamba wanadamu kwa muda mrefu wametiwa sumu na yule mwovu? Je, umesahau kwamba wewe ni mmoja wa wahasiriwa? Je, huna nia ya kujitahidi, kwa sababu ya upendo wako kwa Mungu, kuwaokoa wasaliaji hawa wote? Je, huna nia ya kutoa nguvu zako zote ili kumlipa Mungu, anayewapenda wanadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe? Unaelewaje hasa kuhusu kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, kweli una azimio na imani ya kuishi maisha ya maana ya mtu mcha Mungu, anayemtumikia Mungu?

Iliyotangulia: Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)

Inayofuata: Ufahamu wako wa Baraka ni Upi?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp