Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Mwanadamu daima ameishi akiwa amegubikwa chini ya ushawishi wa giza, akiwa ameshikwa katika utumwa wa ushawishi wa Shetani, asiweze kutoroka, na tabia yake, baada ya kufinyangwa na Shetani, imezidi kuwa potovu. Inaweza kusemwa kwamba mwanadamu daima ameishi katikati ya tabia yake potovu ya kishetani na hawezi kumpenda Mungu kweli. Hili likiwa hivi, mwanadamu akitaka kumpenda Mungu, lazima atupe mbali kujihesabia haki kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na mengine kama hayo—kila kitu ambacho ni cha tabia ya Shetani. La sivyo, upendo wake ni upendo usio safi, upendo wa kishetani, na ule ambao kamwe hauwezi kupata kibali cha Mungu. Bila kufanywa kuwa mtimilifu, kuvunjwa, kupogolewa, kuadhibiwa, kurudiwa, na kusafishwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu, hakuna mtu anayeweza kumpenda Mungu kwa kweli. Ukisema kwamba sehemu ya tabia yako inamwakilisha Mungu na kwa hivyo unaweza kumpenda Mungu kweli, basi wewe ni mtu ambaye maneno yako ni yenye kiburi, na ni wa upuuzi. Watu kama hao ni malaika wakuu! Asili ya kuzaliwa nayo ya mwanadamu haiwezi kumwakilisha Mungu moja kwa moja; lazima atupe mbali asili yake ya maumbile kupitia kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu, na hapo tu—kwa kuijali nia ya Mungu, kuiridhisha nia ya Mungu, na zaidi ya hayo kupitia kazi ya Roho Mtakatifu—ndipo kile anachoishi kwa kukidhihirisha kinaweza kutambuliwa na Mungu. Hakuna mtu anayeishi katika mwili anayeweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja, isipokuwa kama ni mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, hata kwa mtu kama huyu, haiwezi kusemwa kwamba tabia yake na kile anachoishi kwa kukidhihirisha vinamwakilisha Mungu kikamilifu; inaweza tu kusemwa kwamba kile anachoishi kwa kukidhihirisha kinaelekezwa na Roho Mtakatifu. Tabia ya mtu kama huyo haiwezi kumwakilisha Mungu.

Ingawa tabia ya mwanadamu imeamuriwa kabla na Mungu—hili halina shaka na linaweza kuchukuliwa kuwa kitu chanya—imefinyangwa na Shetani, na hivyo tabia yote ya mwanadamu ni tabia ya Shetani. Watu wengine wanasema kwamba tabia ya Mungu ni kufanya mambo kwa namna ya wazi ya, “moja ni moja, mbili ni mbili”, kwamba hili pia limedhihirishwa ndani yao, na kwamba haiba yao pia ni kama hivi, na hivyo wanasema kwamba tabia yao inamwakilisha Mungu. Wao ni watu wa aina gani? Je, tabia potovu ya kishetani inaweza kumwakilisha Mungu? Wote wanaosema kwamba tabia yao inamwakilisha Mungu wanamkufuru Mungu na wanamtukana Roho Mtakatifu! Mbinu ambayo kwayo Roho Mtakatifu anafanya kazi inaonyesha kwamba kazi ya Mungu duniani ni kazi ya ushindi pekee. Hivyo, tabia nyingi potovu za kishetani za mwanadamu bado hazijatakaswa, kile anachoishi kwa kukidhihirisha bado ni mfano wa Shetani, ni kile ambacho mwanadamu anaamini kuwa chema, na kinawakilisha matendo ya mwili wa mwanadamu; kwa usahihi zaidi, kinamwakilisha Shetani, na kamwe hakiwezi kumwakilisha Mungu. Hata kama mtu tayari anampenda Mungu kwa kiwango kwamba anaweza kufurahia maisha ya mbinguni duniani, na anaweza kutoa kauli kama vile: “Mungu! Siwezi kukupenda vya kutosha,” na amefikia hali ya juu zaidi, bado haiwezi kusemwa kwamba anaishi kwa kumdhihirisha Mungu au anamwakilisha Mungu, kwa maana kiini cha mwanadamu ni tofauti na kile cha Mungu, na mwanadamu hawezi kamwe kuishi kwa kumdhihirisha Mungu, sembuse kuwa Mungu. Kile anachoishi mwanadamu kwa kukidhihirisha chini ya maelekezo ya Roho Mtakatifu ni kulingana tu na kile ambacho Mungu anahitaji kutoka kwa mwanadamu.

Matendo na vitendo vyote vya Shetani vinadhihirishwa ndani ya mwanadamu. Leo, matendo na vitendo vyote vya mwanadamu ni onyesho la Shetani na kwa hiyo haviwezi kumwakilisha Mungu. Mwanadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Watu wengine wana haiba njema; Mungu anaweza kufanya mambo fulani kupitia haiba ya watu kama hao, na mambo wanayofanya yanaelekezwa na Roho Mtakatifu. Lakini tabia yao haiwezi kumwakilisha Mungu. Katika kufanya kazi juu yao, Mungu anatumia tu kile ambacho tayari kipo ndani yao na kutoka kwa “mali ghafi” iliyopo. Wawe ni manabii katika enzi zilizopita au wale waliotumiwa na Mungu, hakuna anayeweza kumwakilisha Yeye moja kwa moja. Watu wote wanakuja kumpenda Mungu tu chini ya shinikizo la hali, na hakuna hata mmoja anayejitahidi kushirikiana kwa hiari yake mwenyewe. Vitu chanya ni nini? Vyote vinavyotoka moja kwa moja kwa Mungu ni chanya; tabia ya mwanadamu, hata hivyo, imefinyangwa na Shetani, na haiwezi kumwakilisha Mungu. Ni upendo tu, azimio la kuteseka, haki, utii, na unyenyekevu na kufichika kwa Mungu mwenye mwili ndivyo vinavyomwakilisha Mungu moja kwa moja. Hii ni kwa sababu Alipokuja, Alikuja bila asili ya dhambi na alikuja moja kwa moja kutoka kwa Mungu, bila kufinyangwa na Shetani. Yesu yumo tu katika mfano wa mwili wenye dhambi na hawakilishi dhambi; kwa hivyo, matendo, vitendo, na maneno Yake, hadi wakati kabla ya kufanikishwa kwa kazi Yake kupitia kusulubiwa (pamoja na wakati wa kusulubiwa Kwake), vyote vinamwakilisha Mungu moja kwa moja. Mfano wa Yesu unatosha kuthibitisha kwamba yeyote mwenye asili ya dhambi hawezi kumwakilisha Mungu, na kwamba dhambi ya mwanadamu inamwakilisha Shetani. Yaani, dhambi haimwakilishi Mungu, na Mungu hana dhambi. Hata kazi iliyofanywa kwa mwanadamu na Roho Mtakatifu inaweza tu kuchukuliwa kuwa ilielekezwa na Roho Mtakatifu, na haiwezi kusemwa kuwa ilifanywa na mwanadamu kwa niaba ya Mungu. Lakini, kwa kadiri inavyomhusu mwanadamu, si dhambi yake wala tabia yake inayomwakilisha Mungu. Kwa kuchunguza kazi ambayo Roho Mtakatifu amefanya kwa mwanadamu kutoka zamani hadi sasa, mwanadamu ana kile anachoishi kwa kukidhihirisha yote kwa sababu Roho Mtakatifu amefanya kazi juu yake. Ni wachache sana wanaoweza kuishi kwa kuudhihirisha ukweli baada ya kupogolewa na kuadhibiwa na Roho Mtakatifu. Yaani, ni kazi ya Roho Mtakatifu pekee ndiyo iliyopo; ushirikiano kwa upande wa mwanadamu haupo. Je, unaliona hili wazi sasa? Hili likiwa hivi, utafanyaje uwezavyo ili kushirikiana na Yeye na kutimiza wajibu wako Roho Mtakatifu anapofanya kazi?

Iliyotangulia: Mtazamo Ambao Waumini Wanapaswa Kuwa Nao

Inayofuata: Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp