Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 6

Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, na kufanya kuwa binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu. Nimetembea ulimwenguni kwa miguu Yangu, Nikinyoosha macho Yangu juu ya anga yake nzima, na Nimetembea miongoni mwa wanadamu wote, Nikionja ladha tamu, ya asidi, chungu, na kali za uzoefu wa binadamu, lakini mwanadamu hakuwahi kweli kunitambua, wala hakuniona Nikitembea ng’ambo. Kwa sababu Nilikuwa kimya, na Sikutenda matendo yasiyo ya kawaida, kwa sababu ya hili hakuna yeyote aliyeniona kwa kweli. Mambo hayako sasa kama yalivyokuwa wakati mmoja: Naenda kufanya mambo ambayo, tangu mwanzo wa uumbaji, dunia haijawahi kuyaona, Naenda kusema Maneno ambayo, kupitia enzi nyingi, wanadamu hawajawahi kuyasikia, kwa sababu Nauliza kwamba binadamu wote waje kunijua katika mwili. Hizi ndizo hatua kwa usimamizi Wangu, ambazo binadamu hawazijui hata kidogo. Hata Ninapozizungumzia wazi, mwanadamu bado amechanganyikiwa sana kwa akili yake mpaka haiwezekani kumwelezea kila kitu kuzihusu. Kutoka hapa kuna unyenyekevu dhalili wa mwanadamu, sivyo? Hii hasa ndiyo Nataka kurekebisha kwake, sivyo? Hii miaka yote, Sijafanya kazi yoyote kwa mwanadamu; hii miaka yote, hata waliowasiliana moja kwa moja na mwili Wangu hawakusikia sauti iliyotoka moja kwa moja kwa uungu Wangu. Na hivyo haiwezi kuepukika kwamba wanadamu wanakosa ujuzi wao Kwangu, lakini hiki kitu kimoja pekee hakijaathiri upendo wa binadamu Kwangu katika enzi. Sasa, hata hivyo, Nimekufanyia kazi nyingi ya kimiujiza na isiyoeleweka na pia kukwambia maneno mengi. Na bado, hata chini ya hali kama hizi, watu wengi bado wananipinga mbele Yangu. Wacha Nikupe mifano michache:

Kila siku unasali kwa Mungu asiye dhahiri, ukijaribu kufahamu nia Zangu, na kupata kuhisi maisha. Ilihali, mnapokabiliwa na maneno Yangu, mnayaangalia tofauti; Mnayachukua maneno Yangu na Roho Wangu kwa ujumla, ijapo mnamweka kando nafsi Yangu, mkiamini kwamba mtu Niliye hawezi kuyatamka kimsingi maneno yaliyo mfano wa haya, kwamba badala yake ni matokeo ya kupangwa na Roho Wangu. Utajuaje kuhusu hali kama hii? Unayaamini maneno Yangu kwa kadiri fulani, lakini kwa mwili Ninaovaa, kwa kiasi kikubwa au kidogo unayafikiria mawazo yako mwenyewe, unayoyatafakari siku kwa siku, ukisema: “Mbona Anafanya mambo kwa njia hiyo? Inaweza kuwa kwamba hii inatoka kwa Mungu? Haiwezekani! Kwa mtazamo wangu, Yeye ni sawa nami—mtu wa kawaida na wastani,” Tena, unawezaje kuelezea hali kama hii?

Kuhusu niliyoyasema hapo juu, kuna yeyote miongoni mwenu asiye nayo? Yeyote asiyeyamiliki? Ingeonekana kuwa kitu unachoshikilia kama kipande cha mali binafsi, na wakati huu wote umekuwa ukisita kukiachilia. Bado hujakuwa tayari kufuata juhudi amilifu; badala yake unanisubiri Nifanye kazi mwenyewe. Ukweli usemwe, hakuna binadamu hata mmoja ambaye, bila kunitafuta, anakuja kunijua kwa urahisi. Hakika, haya si maneno ya juujuu ambayo Nakuhubiria somo, kwa sababu Naweza kutoa mfano kutoka kwa pembe tofauti kwa kirejeo chako.

Punde tu anapotajwa Petro, kila mtu anajawa na sifa, akikumbushwa mara moja hizi hadithi zote kumhusu Petro—jinsi alikana kumjua Mungu mara tatu na zaidi ya hayo kumhudumia Shetani, na hivyo kumjaribu Mungu, lakini mwishowe alisulubiwa juu chini kwa ajili Yake, na kadhalika. Sasa Naweka umuhimu mkubwa juu ya kukusimulia jinsi Petro alikuja kunijua na pia matokeo yake ya mwisho. Huyu mwanadamu Petro alikuwa wa kimo bora sana, lakini hali yake ilikuwa tofauti na ile ya Paulo. Wazazi wake walinitesa, walikuwa wa mapepo yaliyomilikiwa na Shetani, na kwa sababu hii mtu hawezi kusema kwamba walipitisha njia kwa Petro. Petro alikuwa na busara nyepesi, alipewa akili asili, kupendwa sana kutoka utotoni na wazazi wake; baada ya kukua, hata hivyo, akawa adui zao, kwani daima alitaka kunijua, na hii ilimfanya kuwapuuza wazazi wake. Hii ilikuwa kwa sababu, kwanza kabisa, aliamini kwamba mbingu na dunia na mambo yote yako mikononi mwa Mwenyezi, na kwamba mambo yote mazuri yanatoka kwa Mungu na yanakuja moja kwa moja kutoka Kwake, bila kupitia usindikaji wowote na Shetani. Na mfano usiofaa wa wazazi wake kuwa kama kikwazo, hii ilimwezesha kwa urahisi kutambua upendo na huruma Yangu, na hivyo kuchochea ndani yake hamu kubwa zaidi ya kunitafuta. Alikuwa makini sana sio tu kula na kunywa maneno Yangu, lakini hata zaidi kufahamu nia Zangu, na daima alikuwa na busara na tahadhari katika mawazo yake, kwa hivyo daima alikuwa mwerevu kwa makini ndani ya roho yake, na hivyo aliweza kuniridhisha kwa vyote alivyofanya. Kwa maisha ya kawaida, alikuwa makini kuunganisha katika maisha[a] masomo ya wale walioshindwa katika siku za nyuma ili kujichochea mwenyewe kufanya juhudi kubwa zaidi, akihofia sana kwamba anaweza kuanguka ndani ya nyavu za ushinde. Alikuwa pia makini kupata imani na upendo wa wote ambao kupitia enzi nyingi walikuwa wamempenda Mungu. Kwa njia hii, aliharakisha maendeleo ya ukuaji wake sio tu kwa masuala hasi, lakini hasa kwa masuala chanya, hadi akawa katika uwepo Wangu mwanadamu pekee aliyenijua bora kabisa. Kwa sababu hii, si vigumu kuwazia jinsi alivyoweza kuweka yote aliyokuwa nayo mikononi Mwangu, kukosa kuwa tena bwana wake mwenyewe hata kwa kula, kuvaa, ama mahali aliishi, lakini alifanya kuniridhisha kwa mambo yote msingi ambao alifurahia fadhila Yangu. Mara nyingi Nilimweka chini ya jaribio, ambalo hakika lilimwacha nusu mfu, lakini hata katikati ya haya mamia ya majaribio, hakupoteza imani Kwangu hata mara moja ama kusikitishwa nami. Hata Niliposema nimemtupa kando, hakufa moyo wala kukata tamaa, lakini aliendelea kama mbeleni akitekeleza kanuni zake ili kunipenda kwa njia ya vitendo. Nilimwambia kwamba, ingawa alinipenda, Sikumsifu ila Ningemtupa katika mikono ya Shetani mwishowe. Katikati ya majaribio haya, ambayo hayakufikia mwili wake lakini yalikuwa majaribio ya njia ya maneno, bado alisali Kwangu: “Ee, Mungu! Miongoni mwa mbingu na dunia na mambo lukuki, kuna mwanadamu yeyote, kiumbe chochote, ama kitu chochote kisicho mikononi Mwako, Mwenyezi? Unapotaka kunionyesha huruma, moyo wangu unafurahishwa sana na huruma Yako; unapotaka kunihukumu, ingawa sifai, nahisi hata zaidi siri ya kushangaza ya matendo Yako, kwa sababu Umejawa na mamlaka na hekima. Ingawa mwili wangu unapitia mateso, roho yangu ina faraja. Ningewezaje kutosifu hekima Yako na matendo Yako? Hata kama nitafa baada ya kuja kukujua, kamwe nitakuwa tayari. Ee, Mwenyezi! Hakika si kwamba Wewe kweli hutaki kuniruhusu nikuone? Hakika si kwamba sistahili kweli kupokea hukumu Yako? Inaweza labda kuwa kwamba kuna kitu ndani yangu usichotaka kuona?” Katikati ya majaribu ya aina hizi, hata kama Petro hakuweza kufahamu nia Zangu kwa usahihi, ni wazi kwamba aliliona kuwa suala la fahari na utukufu binafsi kutumiwa na Mimi (iwe tu kupokea hukumu Yangu ili binadamu waweze kuuona ukuu na ghadhabu Yangu), na hakuwa mwenye huzuni kwa ajili ya kuwekwa chini ya jaribio. Kwa sababu ya uaminifu wake mbele Yangu, na kwa sababu ya baraka Zangu juu yake, amekuwa mfano mwema na mfano wa kuigwa kwa mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Je, huui si hasa mfano unaopaswa kufuata? Wakati huu, unapaswa kufikiria sana na kujaribu kutatua mbona Nimepeana ripoti ndefu ya Petro. Hii inapaswa kukutumikia kama kanuni ya maadili.

Hata kama kuna watu wachache sana wanaonijua, Sitatoa, kwa ajili ya hayo, hasira Yangu kwa binadamu, kwa sababu wanadamu wana dosari nyingi mpaka ni vigumu kwao kufikia kiwango ninachowauliza. Na hivyo Nimekuwa na huruma kwa binadamu kwa maelfu ya miaka, hadi wa leo. Lakini Natumai kwamba hamtakuwa tayari sana, kwa sababu ya huruma Yangu, kujishughulikia wenyewe; mnapaswa badala yake, kupitia Petro, kuja kunijua na kunitaka; kutokana na yale aliyofanya mnafaa kuangaziwa zaidi ya jinsi mlikuwa hapo awali na hivyo kufikia maeneo ambayo hayajafikiwa na mwanadamu. Kote ulimwenguni na maeneo yasiyo na kikomo ya anga, kati ya vyote vinavyopatikana mbinguni kama ilvyo duniani, vitu vyote lukuki duniani, na mambo lukuki mbinguni yote yanatoa juhudi zote kwa ajili ya ukamilisho wa kazi Yangu. Hakika hamtamani kubakia tu kama watazamaji walio kando, ambao huendeshwa hapa na pale na nguvu za Shetani? Shetani daima anagugumia maarifa ambayo wanadamu wameshikilia kunihusu mioyoni mwao, na daima, kwa meno na makucha wazi, akishiriki kwa maumivu ya mwisho ya mapambano yake ya kifo. Je, unataka kukamatwa na mipango yake danganyifu wakati huu? Unataka, wakati awamu ya mwisho ya kazi Yangu imekamilika, kukata maisha yako mwenyewe? Hakika bado hunisubiri Nisambaze huruma Yangu mara moja tena? Kutaka kunijua ni jambo muhimu, lakini hupaswi pia kupuuza kuwa makini kwa mazoezi halisi. Nafichua ufahamu kwako moja kwa moja kwa maneno Yangu, kwa matumaini kwamba utaweza kuukubali mwongozo Wangu, na kukoma kuyafikiria matarajio ama miundo yako mwenyewe.

Februari 27, 1992

Tanbihi:

a. Nakala ya awali imeacha “katika maisha yake mwenyewe.”

Iliyotangulia: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 5

Inayofuata: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 8

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp