Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 5

Wakati Roho Wangu anatoa sauti, Anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, ninyi mnalifahamu hili? Kutolifahamu hili katika hatua hii itakuwa sawa na kunipinga moja kwa moja. Je, kweli mmeona umuhimu ulioko humu? Je, mnajua kweli juhudi kiasi gani, kiasi gani cha nguvu, Ninatumia juu yenu? Je, mnaweza thubutu kuweka wazi kile mlichofanya mbele Yangu? Na mna ujasiri wa kujiita watu Wangu usoni Mwangu—hamna hisia ya aibu, sembuse mantiki yoyote! Siku moja, watu kama hawa watafukuzwa kutoka katika nyumba Yangu. Usithubutu kunidanganya, ukifikiri kwamba umesimama kwa ajili ya ushuhuda Wangu! Je, hili ni jambo ambalo binadamu ana uwezo wa kufanya? Iwapo hakungekuwa na kitu kilichobakia katika nia na malengo yako, ungekuwa umeshika njia tofauti zamani. Je, unafikiri kuwa Sijui ni kiasi gani moyo wa binadamu unaweza kustahimili? Kuanzia wakati huu na kuendelea, katika mambo yote lazima uingie katika ukweli wa kutenda; kupiga domo tu, kama ulivyokuwa ukifanya, hakutakusaidia tena. Katika siku zilizopita, wengi wenu mlifaulu kudoea chini ya paa Langu; ni kwa sababu ya ukali wa maneno Yangu ndio umeweza kusimama imara leo. Je, unafikiri kwamba maneno Yangu huzungumzwa tu kiholela bila lengo? Haiwezekani! Mimi huangalia chini juu ya mambo yote kutoka juu, na Ninatoa mamlaka juu ya mambo yote kutoka juu. Kwa njia iyo hiyo, Nimeutuma wokovu Wangu juu ya dunia. Kamwe hakuna wakati ambapo Mimi Sitazami, kutoka mahali Pangu pa siri, kila hatua ya binadamu, kila wanachosema na kutenda. Binadamu Kwangu wako wazi kabisa: Mimi Nawaona na kuwajua kila mmoja. Mahali hapo pa siri ni makaazi Yangu, na mbingu ndiyo kitanda ambamo Mimi hujilaza. Nguvu za shetani haziwezi kunifikia, kwa maana Mimi nimejawa na uadhama, haki na hukumu. Siri isiyoelezeka imo katika maneno Yangu. Wakati Naongea, mnakuwa kama ndege waliotupwa majini, wakazidiwa na kuchanganyikiwa, au watoto ambao wamepatwa na hofu hivi karibuni, wakionekana kutojua lolote, kwa sababu roho zenu imeingia katika hali ya bumbuazi. Kwa nini Nasema kwamba mahali pa siri ni makaazi Yangu? Je, unajua maana ya ndani ya yale Ninayosema? Ni nani katika ya binadamu wote ana uwezo wa kunijua Mimi? Nani ana uwezo wa kunijua Mimi kama vile anavyomjua baba yake na mama yake? Ninapopumzika katika makaazi Yangu, Mimi huchunguza kwa karibu: Watu wote duniani wamo katika pilkapilka, “wakisafiri duniani kote” na kukimbia huku na kule, yote kwa ajili ya hatima yao, maisha yao ya baadaye. Lakini hakuna hata mmoja ana nguvu ya kutosha kwa ajili ya kujenga ufalme Wangu, hata nguvu kiasi ambayo mtu hutumia kuvuta pumzi. Mimi Niliumba wanadamu, na Nimewaokoa mara nyingi kutoka katika dhiki, lakini hawa binadamu wote ni wasio na shukrani: Hakuna hata mmoja miongoni mwao anayeweza kuhesabu matukio yote ya wokovu Wangu. Imekuwa miaka mingapi, zimekuwa karne ngapi tangu kuumbwa kwa dunia mpaka siku ya leo, na ni miujiza ngapi Niliyofanya, mara ngapi Nimeweka wazi hekima Yangu? Lakini mwanadamu, kama mwendawazimu anayeteseka na kichaa na ulegevu au, wakati mwingine kama mnyama mwitu anayeputa huku na kule katika msitu, hana nia hata kidogo ya kuyajali mambo Yangu. Mara nyingi Nimempa mwanadamu hukumu ya kifo na kumhukumu afe, lakini mpango wa usimamizi Wangu hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote. Kwa hivyo mwanadamu bado yuko katika mikono Yangu, akiegemea vile vitu vya kale anavyokwamilia. Kwa sababu ya hatua za kazi Zangu, mimi, kwa mara nyingine tena, Nimewaokoeni, ninyi viumbe mliozaliwa katika familia kubwa zenye upotovu, uozo, uchafu, na aibu.

Kazi Niliyopanga inaendelea kusonga mbele bila kukoma hata kwa muda kidogo. Baada ya kuingia katika Enzi ya Ufalme, na baada ya kukuingiza katika ufalme Wangu kama watu Wangu, Nitakuwa na madai mengine ya kuweka dhidi yenu; hiyo ni kusema, Nitaanza kutangaza rasmi mbele yenu katiba ambayo Nitatumia kuongoza enzi hii:

Kwa sababu mnaitwa watu Wangu, mnapaswa kuwa na uwezo wa kulitukuza jina Langu, yaani, kushuhudia wakati wa majaribio. Mtu yeyote akijaribu kunirairai na kunificha ukweli, au kushiriki katika shughuli zisizo za heshima nyuma Yangu, bila ubaguzi Nitamfukuza nje, aondolewe kutoka katika nyumba Yangu akisubiri Mimi nimshughulikie. Wale ambao hawajakuwa waaminifu na wasio na upendo wa mtoto kwa mzazi Kwangu zamani, na leo hii wanainuka tena kunihukumu hadharani, wao pia watafukuzwa kutoka kwa nyumba Yangu. Wale ambao ni watu Wangu lazima wajali kuhusu mizigo Yangu kila mara na vile vile kutafuta kujua maneno Yangu. Ni watu kama hawa tu ndio Nitakaowapa nuru, na wao kwa hakika wataishi chini ya uongozi Wangu na nuru, na kamwe hawatakutana na kuadibu. Wale ambao, kwa kutojali mizigo Yangu, wanamakinika na kupanga mustakabali yao wenyewe, yaani, wale ambao hawalengi kwa matendo yao kukidhi Moyo Wangu bali wanataka kuomba omba vya bure, viumbe hawa walio kama waombaji, Ninakataa kata kata kuwatumia, kwa sababu tangu walipozaliwa hawajui chochote kuhusu maana ya kujali mizigo Yangu. Wao ni watu wasiokuwa na akili ya kawaida; watu kama hawa wanaugua kutokana na “utapiamlo” wa ubongo, na wanahitaji kwenda nyumbani wapate “lishe.” Siwahitaji watu wa aina hii. Miongoni mwa watu Wangu, kila mtu atatakiwa kuzingatia kunijua kama wajibu wa lazima unaotakiwa kutekelezwa mpaka mwisho, kama kula, kuvaa, na kulala, mambo ambayo mtu kamwe hawezi kusahau hata kwa muda mfupi, ili kwamba mwishowe kunijua litakuwa jambo la kawaida kama vile kula, jambo ambalo wewe hufanya bila jitihada yoyote, kwa mkono uliozoea. Kuhusu maneno Ninayoyanena, kila neno lazima lichukuliwe kwa uhakika mkubwa na lichukuliwe kikamilifu; hakuwezi kuwa na hatua nusu za uzembe. Yeyote asiyekuwa makini na maneno Yangu ataonekana kama ananipinga Mimi moja kwa moja; mtu yeyote asiyeyala maneno Yangu, au hatafuti kuyajua, ataonekana kama ambaye hanizingatii, na moja kwa moja atafagiliwa nje ya mlango wa nyumba Yangu. Kwa maana, kama Nilivyosema zamani, Ninachotaka sio watu wengi ila wateule wachache. Kati ya watu mia, kama mmoja tu anaweza kunijua kupitia maneno Yangu, basi bila kusita Ningewatupilia mbali wengine wote ili Nizingatie kumpa nuru na mwangaza mmoja huyu. Kutokana na hili unaweza kuona kuwa, si lazima iwe ukweli kwamba idadi kubwa pekee ndio inaweza kunidhihirisha, kuishi kulingana na Mimi. Ninachotaka ni ngano (hata ingawa viini vya mbegu huenda havijajaa) na sio magugu (hata wakati viini vya mbegu vimejaa vya kutosha kutamanika). Na kuhusu wale wasiojali kuhusu kutafuta lakini badala yake kuwa na tabia za kuzembea, wanapaswa kuondoka kwa hiari yao wenyewe; Mimi sitaki kuwaona tena, wasije wakaleta aibu kwa jina Langu. Kuhusu yale Ninayohitaji kutoka kwa watu Wangu, Nitakomea katika maagizo hayo kwa sasa, na Nitasubiri kuweka vikwazo zaidi kulingana na jinsi hali zitakavyobadilika.

Katika siku zilizopita, idadi kubwa ya watu walifikiri kuwa Mimi nilikuwa Mungu Mwenyewe mwenye hekima, kwamba mimi ndiye Nilikuwa Mungu aliyeona ndani kwa kina ya mioyo ya watu; lakini yote yalikuwa maneno ya juu juu tu. Kama mwanadamu angenijua kwa kweli, hangethubutu kufikia uamuzi bila kutafakari, ila angezidi kujaribu kunijua kupitia maneno Yangu. Wakati tu alifika katika hatua ambapo kweli angeona matendo Yangu kweli, ndipo angestahili kusema kwamba Nilikuwa mwenye Hekima, kwamba Mimi nilikuwa wa Ajabu. Ufahamu wenu kunihusu ni mdogo mno. Katika enzi zote, ni watu wangapi wamenihudumia kwa miaka mingapi, na baada ya kuona matendo Yangu, wakaja kujua kwa hakika kitu kunihusu; na basi daima wakawa na moyo wa unyenyekevu Kwangu, na kutothubutu kuwa na nia hata kidogo ya upinzani Kwangu, kwa sababu ya jinsi ilivyo vigumu kutafuta nyayo Zangu. Kama uongozi Wangu ungekosekana miongoni mwa watu hawa, hawangethubutu kutenda bila kwa pupa, na hivyo, baada ya kuishi kwa uzoefu wa miaka mingi, hatimaye walijumlisha sehemu ya ufahamu kunihusu, wakisema kwamba Mimi ni mwenye Hekima, wa Ajabu na Mshauri, kwamba maneno Yangu ni kama upanga wenye makali pande mbili, kwamba matendo Yangu ni makuu, ya kustaajabisha, na kupendeza, kwamba Mimi Nimevikwa uadhama, kwamba hekima Yangu inafika juu kuliko anga, na ufahamu mwingine. Lakini leo mnanijua tu kwa misingi ambayo waliweka, kwa hivyo idadi kubwa kati yenu, kama kasuku, mnayarudia tu maneno waliyosema. Ni kwa sababu tu Mimi huzingatia jinsi njia mnayonijua ni wa juu juu na jinsi “elimu” yako ilivyo duni ndio maana Nimewasamehe kuadibu kwingi. Lakini hata hivyo, idadi kubwa kati yenu bado hawajijui wenyewe, au mnafikiri tayari mshayafikia mapenzi Yangu katika matendo yenu, na kwa sababu hii mmeepuka hukumu. Au mnafikiri kwamba, baada ya kupata mwili, Nimekosa kujua kabisa mwelekeo wa matendo ya mwanadamu, na kwa sababu hii pia mmeepuka kuadibu. Ama mnafikiri kwamba Mungu mnayemwamini hayuko katika maeneo mapana ya ulimwengu, na kwa hivyo mmeweka kumjua Mungu kama shughuli ya kufanya wakati hamna shughuli nyingine badala ya kukuweka katika mioyo yenu kama wajibu ambao lazima utekelezwe, na kutumia imani katika Mungu kama njia ya kuchangamsha wakati ambao labda ungetumiwa kwa kuzembea. Kama Singeonea huruma ukosefu wenu wa sifa za kustahili, mantiki, na ufahamu, basi nyote mngeangamia katika kuadibu Kwangu, kutokuwepo tena. Lakini hadi wakati Kazi Yangu hapa duniani itakapomalizika, Mimi Nitabaki mwenye huruma kwa wanadamu. Hili ni jambo ambalo lazima nyote mlijue na mkome kuyachanganya mazuri na mabaya.

Februari 25, 1992

Iliyotangulia: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 4

Inayofuata: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 6

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp