Tofauti ya Kimsingi Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu
Ni miaka mingi ambayo Roho wa Mungu amekuwa akitafuta Anapofanya kazi duniani, na ni wengi ambao Mungu amewatumia kufanya kazi Yake katika enzi na vizazi vyote. Hata hivyo kwa wakati huu wote, Roho wa Mungu amekuwa bila mahali pa kupumzika panapofaa, ndiyo maana Mungu hubadilisha kati ya watu tofauti ili kufanya kazi Yake. Kwa jumla, ni kupitia kwa watu ndiyo kazi Yake inafanywa. Yaani, kwa miaka hii yote, kazi ya Mungu haijawahi kusimama, lakini imeendelea kusongeshwa mbele ndani ya watu, wakati wote hadi leo. Ingawa Mungu amenena maneno mengi sana na kufanya kazi nyingi sana, mwanadamu bado hamjui Mungu, yote kwa sababu Mungu hajawahi kumtokea mwanadamu na pia kwa sababu Yeye hana umbo linalogusika. Na hivyo Mungu lazima aikamilishe kazi hii—kazi ya kuwafanya watu wote wajue umuhimu halisi wa Mungu wa vitendo. Ili kufikia lengo hili, lazima Mungu amfunue Roho Wake kwa njia inayogusika kwa wanadamu na kufanya kazi Yake katikati yao. Yaani, ni wakati tu Roho wa Mungu anapochukua umbo la kimwili, anapovalia nyama na mifupa, na kutembea kwa kuonekana miongoni mwa watu, akiandamana nao katika maisha yao, wakati mwingine Akijionyesha na wakati mwingine Akijificha, ndipo tu watu wanaweza kufikia uelewa wa kina zaidi kumhusu Yeye. Ikiwa Mungu angebaki tu katika mwili, Hangeweza kukamilisha kazi Yake kwa ukamilifu wake. Na baada ya kufanya kazi katika mwili kwa kipindi cha muda, kutimiza huduma inayohitajika kufanywa katika mwili, Mungu atauacha mwili na kufanya kazi katika ulimwengu wa kiroho katika mfano wa mwili, kama vile tu Yesu alivyofanya hivyo baada ya Yeye kufanya kazi kwa kipindi cha muda katika ubinadamu wa kawaida na kukamilisha kazi yote Aliyohitaji kukamilisha. Mnaweza kukumbuka kifungu hiki kutoka katika “Njia … (5)”: “Ninakumbuka Baba Yangu akiniambia, ‘Duniani, tafuta tu kufuata mapenzi ya Baba Yako na kukamilisha agizo Lake. Hakuna kingine kinachokuhusu wewe.’” Unaona nini katika kifungu hiki? Mungu anapokuja duniani, Yeye hufanya tu kazi Yake ndani ya uungu, ambayo ndiyo Roho wa mbinguni amemwainia Mungu mwenye mwili. Anapokuja, Ananena tu kote nchini, kutoa sauti kwa matamko Yake kwa njia tofauti na kutoka katika mitazamo tofauti. Yeye kimsingi huchukua kumkimu mwanadamu na kumfundisha mwanadamu kama malengo Yake na kanuni Yake ya kufanya kazi, na Hajishughulishi na mambo kama vile uhusiano kati ya watu au mambo ya ndani ya maisha ya watu. Huduma Yake kuu ni kunena kwa niaba ya Roho. Yaani, Roho wa Mungu anapoonekana kwa namna inayogusika katika mwili, Yeye hukimu tu uzima wa mwanadamu na kuachilia ukweli. Yeye hajihusishi katika kazi ya mwanadamu, yaani, Yeye hashiriki katika kazi ya wanadamu. Wanadamu hawawezi kufanya kazi ya uungu, na Mungu hashiriki katika kazi ya binadamu. Katika miaka yote tangu Mungu aje katika dunia hii kufanya kazi Yake, Yeye daima ameifanya kupitia kwa watu. Watu hawa, hata hivyo, hawawezi kuchukuliwa kuwa Mungu mwenye mwili—wao ni watu tu wanaotumiwa na Mungu. Mungu wa leo, wakati huo huo, Anaweza kunena moja kwa moja kutoka katika mtazamo wa uungu, akionyesha sauti ya Roho na kufanya kazi kwa niaba ya Roho. Wale wote ambao Mungu amewatumia katika enzi na vizazi vyote ni, vivyo hivyo, mifano ya Roho wa Mungu akifanya kazi ndani ya mwili wa nyama—hivyo kwa nini hawawezi kuitwa Mungu? Lakini Mungu wa leo pia ni Roho wa Mungu akifanya kazi moja kwa moja katika mwili, na Yesu pia alikuwa Roho wa Mungu akifanya kazi katika mwili; Wote Wawili wanaitwa Mungu. Basi tofauti ni nini? Watu ambao Mungu amewatumia katika enzi zote wote wamekuwa na uwezo wa mawazo na busara ya kawaida. Wote wameelewa kanuni za kujiendesha na kushughulikia mambo. Wamekuwa na fikira za kawaida za binadamu, na wamekuwa na vitu vyote ambavyo watu wa kawaida wanapaswa kuwa navyo. Wengi wao wamekuwa na talanta ya kipekee na akili ya kuzaliwa nayo. Katika kufanya kazi juu ya watu hawa, Roho wa Mungu hutumia talanta zao, ambazo ni karama zao. Roho wa Mungu huwezesha talanta zao kutumika, akitumia ubora wao katika huduma ya Mungu. Hata hivyo kiini cha Mungu hakina dhana au fikira, hakijachanganywa na mawazo ya binadamu, na hata kinakosa kile ambacho wanadamu wa kawaida wanacho. Yaani, hata Hafahamu vizuri kanuni za kujiendesha na kushughulikia mambo. Hivi ndivyo ilivyo wakati Mungu wa leo Anapokuja duniani. Kazi Yake na maneno Yake hayajachanganywa na mawazo ya binadamu au fikira za binadamu, bali ni udhihirisho wa moja kwa moja wa mawazo ya Roho, na Yeye hufanya kazi moja kwa moja kwa niaba ya Mungu. Hii inamaanisha kwamba Roho ananena moja kwa moja, yaani, uungu unafanya kazi moja kwa moja, bila kuchanganya hata chembe ya mawazo ya mwanadamu. Yaani, Mungu mwenye mwili anadhihirisha uungu moja kwa moja, Hana mawazo au dhana za kibinadamu, na Hana ufahamu wa kanuni za watu za kushughulika na ulimwengu. Ikiwa uungu pekee ndio ungefanya kazi (ikimaanisha ikiwa Mungu Mwenyewe pekee ndiye angefanya kazi), kusingekuwa na njia ya kazi ya Mungu kutekelezwa duniani. Kwa hivyo Mungu anapokuja duniani, lazima Awe na idadi ndogo ya watu Anaowatumia kufanya kazi ndani ya ubinadamu kwa ushirikiano na kazi ambayo Mungu hufanya katika uungu. Yaani, Yeye hutumia kazi ya kibinadamu kutegemeza kazi Yake ya uungu. La sivyo, kusingekuwa na njia kwa mwanadamu kujihusisha moja kwa moja na kazi ya uungu. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu na wanafunzi Wake. Wakati Wake duniani, Yesu alifuta sheria za zamani na kuanzisha amri mpya. Pia Alinena maneno mengi. Kazi hii yote ilifanywa katika uungu. Wengine, kama vile Petro, Paulo, na Yohana, wote waliweka kazi yao iliyofuata kwenye msingi wa maneno ya Yesu. Yaani, Mungu alifanya kazi Yake ya kwanza katika enzi hiyo, akiongoza mwanzo wa Enzi ya Neema; yaani, Aliongoza enzi mpya, akifuta enzi ya zamani, na pia kutimiza maneno, “Mungu ndiye Mwanzo na Mwisho.” Yaani mwanadamu lazima atekeleze kazi ya kibinadamu juu ya msingi wa kazi ya uungu. Punde tu Yesu alipokuwa amenena yote Aliyohitaji kunena na kumaliza kazi Yake duniani, Alimwacha mwanadamu. Baada ya haya, watu wote, katika kufanya kazi, walifanya hivyo kulingana na kanuni zilizoonyeshwa katika maneno Yake, na walitenda kulingana na ukweli Aliozungumzia. Watu hawa wote walimfanyia Yesu kazi. Ikiwa angekuwa Yesu pekee akifanya kazi, haijalishi Angenena maneno mangapi, watu hawangekuwa na njia ya kujihusisha na maneno Yake, kwa sababu Angekuwa akifanya kazi katika uungu na Angeweza tu kunena maneno ya uungu, na Hangeweza kuwafafanulia watu mambo na kuwafanya watu wa kawaida waelewe maneno Yake. Na hivyo Angelazimika kuwa na mitume na manabii waliokuja baada Yake ili kuongezea kazi Yake. Hii ndiyo kanuni ya jinsi Mungu mwenye mwili Anavyofanya kazi Yake—kutumia mwili uliopatwa kunena na kufanya kazi ili kukamilisha kazi ya uungu, na kisha kutumia watu wachache, au labda zaidi, ambao wanalingana na nia za Mungu ili kuongezea kazi Yake. Yaani, Mungu huwatumia watu ambao wanalingana na nia Zake kufanya kazi ya kuchunga na kunyunyizia katika ubinadamu ili watu wateule wa Mungu waweze kuingia katika uhalisi wa ukweli.
Ikiwa, Alipokuja katika mwili, Mungu angefanya tu kazi ya uungu, na kusingekuwa na watu wanaolingana na nia Zake kushirikiana na Yeye, basi mwanadamu hangeweza kuelewa nia za Mungu au kujihusisha na Mungu. Mungu lazima awatumie watu wa kawaida ambao wanalingana na nia Zake kukamilisha kazi hii, kulinda na kuyachunga makanisa, ili kiwango ambacho michakato ya utambuzi ya mwanadamu, ubongo wake, ina uwezo wa kufikiria kiweze kufikiwa. Yaani, Mungu hutumia idadi ndogo ya watu wanaolingana na nia Zake “kutafsiri” kazi Anayofanya ndani ya uungu Wake, ili iweze kufunguliwa—kubadilisha lugha ya uungu kuwa lugha ya kibinadamu, ili watu waweze kuifahamu na kuielewa. Mungu asingefanya hivyo, hakuna mtu ambaye angeelewa lugha ya uungu ya Mungu, kwani watu ambao wanalingana na nia za Mungu ni wachache sana, na uwezo wa mwanadamu wa kufahamu ni dhaifu. Hiyo ndiyo maana Mungu huchagua mbinu hii Anapofanya kazi katika mwili wa Mungu mwenye mwili. Ikiwa kungekuwa tu na kazi ya uungu, kusingekuwa na njia kwa mwanadamu kumjua au kujihusisha na Mungu, kwa sababu mwanadamu haelewi lugha ya Mungu. Mwanadamu anaweza kuelewa lugha hii kupitia tu uwakala wa watu wanaolingana na nia za Mungu, ambao hufafanua maneno Yake. Hata hivyo, ikiwa kungekuwa tu na watu kama hao wakifanya kazi ndani ya ubinadamu, hilo lingeweza tu kudumisha maisha ya kawaida ya mwanadamu; halingeweza kubadilisha tabia ya mwanadamu. Kazi ya Mungu isingeweza kuwa na mahali papya pa kuanzia; kungekuwa tu na nyimbo zilezile za zamani, maneno yaleyale ya zamani yasiyo na maana. Ni kupitia tu uwakala wa Mungu mwenye mwili, ambaye hunena yote yanayohitajika kunenwa na kufanya yote yanayohitajika kufanywa wakati wa kipindi cha kupata mwili Kwake, ambapo baada ya hapo watu hufanya kazi na kupitia kulingana na maneno Yake, ni hivi tu ndivyo tabia yao ya maisha itaweza kubadilika, na ni hivi tu ndivyo wataweza kwenda na wakati. Yeye anayefanya kazi ndani ya uungu Anamwakilisha Mungu, huku wale wanaofanya kazi ndani ya ubinadamu ni watu wanaotumiwa na Mungu. Yaani, Mungu mwenye mwili kimsingi ni tofauti na watu wanaotumiwa na Mungu. Mungu mwenye mwili Anaweza kufanya kazi ya uungu, ilhali watu wanaotumiwa na Mungu hawawezi. Mwanzoni mwa kila enzi, Roho wa Mungu hunena binafsi na kuzindua enzi mpya ili kumleta mwanadamu katika mwanzo mpya. Anapomaliza kunena, hili linaashiria kwamba kazi ya Mungu katika uungu Wake imekamilika. Baadaye, watu wote hufuata uongozi wa wale wanaotumiwa na Mungu ili kuingia katika upitiaji wao wa uzima. Vilevile, hii pia ndiyo hatua ambayo Mungu humleta mwanadamu katika enzi mpya na kuwapa watu mahali papya pa kuanzia—wakati ambapo kazi ya Mungu katika mwili inahitimika.
Mungu haji duniani kukamilisha ubinadamu Wake wa kawaida. Haji kufanya kazi ya ubinadamu wa kawaida; Anakuja tu kufanya kazi ya uungu katika ubinadamu wa kawaida. Kile ambacho Mungu anazungumza kuhusu ubinadamu wa kawaida si kama watu wanavyofikiria. Mwanadamu hufafanua “ubinadamu wa kawaida” kama kuwa na mke, au mume, na wana na binti, jambo ambalo ni uthibitisho kwamba mtu ni mtu wa kawaida; Mungu, hata hivyo, Halioni hivi. Yeye huona ubinadamu wa kawaida kama kuwa na mawazo ya kawaida ya binadamu, maisha ya kawaida ya binadamu, na kuzaliwa na watu wa kawaida. Lakini ukawaida Wake haujumuishi kuwa na mke, au mume, na watoto kwa njia ambayo mwanadamu anazungumza kuhusu ukawaida. Yaani, kwa mwanadamu, ubinadamu wa kawaida ambao Mungu anazungumzia ni kile ambacho mwanadamu angekiona kama ukosefu wa ubinadamu, karibu kukosa hisia na kuonekana kutokuwa na mahitaji ya kimwili, kama tu Yesu, ambaye alikuwa tu na sura ya nje ya mtu wa kawaida na kuchukua mwonekano wa mtu wa kawaida, lakini katika kiini kwa ukamilifu hakuwa na yote ambayo mtu wa kawaida anapaswa kuwa nayo. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba kiini cha Mungu mwenye mwili hakijumuishi ukamilifu wa ubinadamu wa kawaida, bali tu sehemu ya mambo ambayo watu wanapaswa kuwa nayo, ili kutegemeza taratibu za maisha ya kawaida ya binadamu na kudumisha busara ya kawaida ya binadamu. Lakini mambo haya hayana uhusiano wowote na kile ambacho mwanadamu anakiona kuwa ubinadamu wa kawaida. Ni yale ambayo Mungu mwenye mwili anapaswa kuwa nayo. Kuna wale wanaoshikilia, hata hivyo, kwamba Mungu mwenye mwili anaweza kusemwa kuwa na ubinadamu wa kawaida tu Akiwa na mke, wana na mabinti, familia; bila mambo haya, wanasema, Yeye si mtu wa kawaida. Ninakuuliza basi, “Je, Mungu ana mke? Je, inawezekana kwa Mungu kuwa na mume? Je, Mungu anaweza kuwa na watoto?” Je, huu si uwongo? Hata hivyo Mungu mwenye mwili hawezi kuchipuka kutoka katika ufa kati ya miamba au kuanguka kutoka angani. Anaweza tu kuzaliwa katika familia ya kawaida ya binadamu. Hiyo ndiyo maana Ana wazazi na dada. Haya ni mambo ambayo ubinadamu wa kawaida wa Mungu mwenye mwili unapaswa kuwa nayo. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu; Yesu alikuwa na baba na mama, dada na kaka, na haya yote yalikuwa ya kawaida. Lakini kama Angekuwa na mke na wana na mabinti, basi Wake haungekuwa ubinadamu wa kawaida ambao Mungu alikusudia Mungu mwenye mwili awe nao. Kama ingekuwa hivi, Asingeweza kufanya kazi kwa niaba ya uungu. Ilikuwa hasa kwa sababu Hakuwa na mke au watoto, na bado alizaliwa na watu wa kawaida katika familia ya kawaida, ndiyo Aliweza kufanya kazi ya uungu. Ili kufafanua hili zaidi, kile ambacho Mungu anakiona kuwa mtu wa kawaida ni mtu aliyezaliwa katika familia ya kawaida. Ni mtu kama huyo tu ndiye anayestahili kufanya kazi ya uungu. Ikiwa, kwa upande mwingine, mtu huyo angekuwa na mke, watoto, au mume, mtu huyo hangeweza kufanya kazi ya uungu, kwa sababu angekuwa tu na ubinadamu wa kawaida ambao wanadamu wanahitaji lakini si ubinadamu wa kawaida ambao Mungu anahitaji. Kile kinachoonekana na Mungu, na kile ambacho watu wanaelewa, mara nyingi ni tofauti sana, tofauti kubwa sana. Katika hatua hii ya kazi ya Mungu kuna mengi ambayo yanakinzana na yanatofautiana sana na fikira za watu. Mtu anaweza kusema kwamba hatua hii ya kazi ya Mungu inajumuisha kabisa uungu ukifanya kazi moja kwa moja, huku ubinadamu ukichukua nafasu ya kusaidia. Kwa sababu Mungu anakuja duniani kufanya kazi Yake Mwenyewe, badala ya kumruhusu mwanadamu kuweka mkono wake kwayo, Yeye apata mwili (katika mtu asiye kamili, wa kawaida) ili kufanya kazi Yake. Anatumia fursa inayotolewa na kupata mwili huku ili alete mbele ya wanadamu enzi mpya, awaambie wanadamu kuhusu hatua inayofuata katika kazi Yake, na kuwataka watu watende kulingana na njia iliyofafanuliwa katika maneno Yake. Hivyo ndivyo kazi ya Mungu katika mwili inavyohitimishwa; Yuko karibu kumwacha mwanadamu na kutengana na mwanadamu, Haishi tena katika mwili wa ubinadamu wa kawaida, bali Anasonga mbali na mwanadamu ili aendelee na sehemu nyingine ya kazi Yake. Kisha, akitumia watu wanaolingana na nia Zake, Yeye anaiendeleza kazi Yake duniani miongoni mwa kundi hili la watu, lakini katika ubinadamu wao.
Mungu mwenye mwili hawezi kukaa na mwanadamu milele kwa sababu Mungu ana kazi nyingine nyingi zaidi za kufanya. Hawezi kufungwa kwenye mwili; lazima auvue mwili ili kufanya kazi Anayopaswa kufanya, ingawa Yeye anaifanya kazi hiyo katika mfano wa mwili. Mungu anapokuja duniani, Yeye hasubiri hadi Awe amefikia umbo ambalo mtu wa kawaida anapaswa kufikia kabla ya kufa na kuwaacha wanadamu. Haijalishi mwili Wake una umri gani, kazi Yake inapokamilika, Yeye anaondoka na kumwacha mwanadamu. Hakuna kitu kama umri Kwake, Yeye hahesabu siku Zake kulingana na muda wa maisha ya mwanadamu; badala yake, Yeye huhitimisha uzima Wake katika mwili kulingana na hatua za kazi Yake. Kunaweza kuwa na wale wanaohisi kwamba Mungu, katika kuja katika mwili, lazima azeeke kwa kiwango fulani, lazima akue na kuwa mtu mzima, afikie uzee, na aondoke tu wakati mwili huo unaposhindwa. Haya ni mawazo ya mwanadamu; Mungu hafanyi kazi hivi. Anakuja katika mwili tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya, na si kuishi maisha ya mtu wa kawaida ya kuzaliwa na wazazi, kukua, kuunda familia na kuanzisha kazi, kuwa na watoto na kuwalea, au kustahimili dhoruba za maisha—shughuli zote za watu wa kawaida. Mungu anapokuja duniani, huyu ni Roho wa Mungu akivalia mwili, akija katika mwili, lakini Mungu haishi maisha ya mtu wa kawaida. Anakuja tu kukamilisha sehemu moja katika mpango Wake wa usimamizi. Baada ya hapo Atawaacha wanadamu. Anapokuja katika mwili, Roho wa Mungu hakamilishi ubinadamu wa kawaida wa mwili. Badala yake, wakati ambao Mungu ameamua kimbele, uungu hufanya kazi moja kwa moja. Kisha, baada ya kufanya yote Anayohitaji kufanya na kukamilisha kikamilifu huduma Yake, kazi ya Roho wa Mungu katika hatua hii imekamilika, ambapo uzima wa Mungu mwenye mwili pia unahitimishwa, bila kujali kama mwili Wake wa nyama umeishi urefu wote wa muda wake wa kuishi. Yaani, ni hatua gani ya uzima ambayo mwili wa nyama unafikia, na unaishi duniani kwa muda gani, yote mawili yanaamuliwa na kazi ya Roho, na hayana uhusiano wowote na kile ambacho mwanadamu anakiona kuwa ubinadamu wa kawaida. Mchukue Yesu kama mfano. Aliishi katika mwili kwa miaka thelathini na mitatu na nusu. Kwa upande wa muda wa maisha wa mwili wa binadamu, Hakupaswa kufa katika umri huo, na Hakupaswa kuondoka. Lakini hili halikumhusu Roho wa Mungu. Kazi Yake ikiwa imekamilika, wakati huo mwili ulichukuliwa, ukatoweka pamoja na Roho. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika mwili. Na hivyo, kusema kweli, ubinadamu wa Mungu mwenye mwili si wa umuhimu wa msingi. Bado inarudi kwenye jambo lilelile: Haji duniani kuishi maisha ya binadamu wa kawaida. Yeye haanzishi kwanza maisha ya kawaida ya binadamu na kisha kuanza kufanya kazi. Badala yake, maadamu Anazaliwa katika familia ya kawaida ya binadamu, Anaweza kufanya kazi ya uungu, kazi ambayo haina dosari ya mawazo ya mwanadamu, ambayo si ya kimwili, ambayo hakika haichukui njia za jamii au kuhusisha mawazo au fikira za mwanadamu, na, zaidi ya hayo, ambayo haihusishi falsafa za mwanadamu za shughuli za kidunia. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu mwenye mwili anakusudia kufanya, na pia ni umuhimu wa vitendo wa kupata mwili Kwake. Mungu anakuja katika mwili kimsingi kufanya hatua ya kazi inayohitajika kufanywa katika mwili, bila kupitia michakato mingine isiyo muhimu sana, na, kuhusu upitiaji wa kawaida wa binadamu, Yeye hana. Kazi ambayo mwili wa Mungu uliopatwa unahitaji kufanya haijumuishi uzoefu wa kawaida wa binadamu. Kwa hivyo Mungu anakuja katika mwili kwa ajili ya kukamilisha kazi Anayohitaji kukamilisha katika mwili. Mengine hayamhusu Yeye; Yeye hapitii michakato mingi isiyo muhimu sana. Punde tu kazi Yake inapokamilika, umuhimu wa kupata mwili Kwake pia unahitimishwa. Kukamilisha hatua hii kunamaanisha kazi Anayohitaji kufanya katika mwili imehitimishwa, na huduma ya mwili Wake imekamilika. Lakini Hawezi kuendelea kufanya kazi katika mwili kwa muda usiojulikana. Lazima Asonge hadi mahali pengine kufanya kazi, na auache mwili. Ni hivi tu ndivyo kazi Yake inaweza kutekelezwa kikamilifu, na kusonga mbele kwa ufanisi zaidi. Mungu hufanya kazi kulingana na mpango Wake wa asili. Ni kazi gani Anayohitaji kufanya na ni kazi gani ambayo Amehitimisha, Anajua waziwazi kama kiganja cha mkono Wake. Mungu humwongoza kila mtu kutembea katika njia ambayo tayari Ameiamua kabla. Hakuna anayeweza kuepuka hili. Ni wale tu wanaofuata uelekezaji wa Roho wa Mungu ndio wataweza kuingia katika pumziko. Inaweza kuwa kwamba, katika kazi ya baadaye, hatakuwa Mungu akinena katika mwili kumwongoza mwanadamu, bali Roho aliye na umbo linalogusika akiongoza maisha ya mwanadamu. Ni kwa namna hii tu ndiyo mwanadamu ataweza kumgusa Mungu kwa njia thabiti, kumtazama Mungu, na kuingia vizuri zaidi katika uhalisi ambao Mungu anahitaji, ili kufanywa kuwa timilifu na Mungu wa vitendo. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu anakusudia kukamilisha, na kile Alichopanga zamani. Kutokana na hili, ninyi nyote mnapaswa kuona njia mnayopaswa kuchukua!