Katika Imani, Mtu Lazima Alenge Ukweli—Kujihusisha na Kaida za Dini Sio Imani

Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako? Ni mara ngapi umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, huku ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Vitendo kama hivi pekee ndivyo humridhisha Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli. Wanadamu wengine wana upendeleo wa kujivutia nadhari. Mbele ya ndugu zao, wanasema kweli ni wadeni wa Mungu, lakini akiwapa kisogo, hawatendi ukweli ila wanafanya tofauti kabisa. Je, hawa si ni Mafarisayo wa dini? Mtu ambaye anampenda Mungu kwa kweli na ana ukweli ni yule ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, lakini bila ya hafichui kwa nje. Yeye yuko tayari kutenda ukweli wakati mambo yanapotokea wala hasemi au kutenda kinyume cha dhamiri yake. Anaonyesha hekima wakati mambo yanapotokea na ni mwenye maadili katika matendo yake, bila kujali hali. Mtu kama huyu ni mtu ambaye anahudumu kwa kweli. Kuna watu wengine ambao mara nyingi shukrani zao kwa kuwa wadeni wa Mungu ni kwa mdomo tu. Siku zao huisha wakiwa na nyuso za wasiwasi, kuonekana wameathiriwa, na kuvalia nyuso za huzuni. Hali ya kuchukiza kweli! Na kama ungewauliza, “Ni kwa njia zipi wewe ni mdeni wa Mungu? Tafadhali niambie!” Hawangeweza kutamka lolote. Kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi usizungumze kwa nje kuhusu hilo; badala yake, onyesha upendo wako kwa Mungu kwa njia ya matendo halisi, na kumwomba kwa moyo wa kweli. Wale wanaotumia maneno pekee kushughulika na Mungu ni wanafiki wote! Baadhi yao husema kuwa wao ni wadeni kwa Mungu katika kila sala, na kuanza kulia wakati wowote wanaposali, hata bila kuguswa na Roho Mtakatifu. Watu kama hawa wamepagawa na kaidi na fikira za kidini; wanaishi kulingana na hizo kaidi na fikra, daima wakiamini kwamba matendo kama hayo humpendeza Mungu, na kwamba kumcha Mungu kijuujuu au machozi ya huzuni ndivyo Mungu hupendelea. Ni kitu kipi kizuri kinachoweza kutoka kwa watu kama hao wa kushangaza? Ili kuonyesha unyenyekevu wao, baadhi yao huonyesha neema bandia wakati wanapozungumza mbele ya watu wengine. Baadhi yao kwa makusudi ni wanyonge mbele ya watu wengine, kama mwanakondoo asiye na nguvu yoyote. Je, hii ni tabia ya watu wa ufalme? Mtu wa ufalme sharti awe wa kusisimua na aliye huru, asiye na hatia na aliye na uwazi, mwaminifu na wa kupendeza; mtu aishiye katika hali ya uhuru. Ana uadilifu na heshima, na anaweza kushuhudia kokote aendako; yeye ni yule anayependwa na Mungu na wanadamu. Wale ambao ni wanafunzi katika imani huwa na matendo mengi ya nje; lazima kwanza wapitie kipindi cha ushughulikiaji na kuvunjwa. Wale ambao wana imani kwa Mungu katika nyoyo zao hawawezi kutofautishwa na wengine kwa nje, lakini vitendo na matendo yao ni ya kupongezwa kwa wengine. Watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza chukuliwa kuwa wanaishi kwa kudhihirisha neno la Mungu. Ukihubiri injili kila siku kwa mtu huyu na yule, ukiwaleta kwa wokovu, ilhali mwishowe, wewe bado unaishi katika sheria na mafundisho, basi wewe huwezi kuleta utukufu kwa Mungu. Watu wa aina hii ni watu wa dini, na wanafiki pia.

Kila mara watu wa kidini kama hao wanapokusanyika, wanauliza, “Dada, umeshinda vipi siku hizi?” Anajibu, “Nahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu na siwezi kuridhisha matakwa ya moyo Wake.” Mwingine anasema, “Mimi, pia, ni mdeni wa Mungu na nimeshindwa kumkidhi.” Sentensi na maneno haya machache pekee yanaonyesha mambo maovu yaliyo ndani ya nyoyo zao. Maneno kama hayo ni ya kuchukiza zaidi na yenye makosa sana. Asili ya watu kama hao inampinga Mungu. Wale ambao huzingatia uhalisi huwasilisha vyovyote vilivyomo katika nyoyo zao na kufungua mioyo yao katika mawasiliano. Hakuna shughuli hata moja ya uongo, hakuna heshima ama salamu na mazungumzo matupu. Wao daima huwa na uwazi na hawafuati sheria za duniani. Kuna wale ambao wako na upendeleo wa kujionyesha kwa nje, hata bila maana yoyote. Wakati mwingine anaimba, yeye anaanza kukatika, bila hata kugundua kuwa wali katika sufuria yake umeshaungua. Watu wa aina hii si wacha Mungu au waheshimiwa, bali ni watu wa kijinga kupindukia. Hizi zote ni maonyesho ya ukosefu wa ukweli! Wakati watu wengine wanawasiliana kuhusu masuala ya maisha katika roho, ingawa hawasemi kuhusu kuwa wadeni wa Mungu, wao hubaki na upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Kuwa kwako mdeni kwa Mungu hakuhusiani na watu wengine; wewe ni mdeni kwa Mungu, si kwa mwanadamu. Kwa hiyo ina maana gani wewe daima kuzungumzia haya kwa watu wengine? Lazima uweke umuhimu kwa kuingia katika uhalisi, si kwa bidii au maonyesho ya nje.

Je, matendo mazuri ya kijuujuu ya mwanadamu yanawakilisha nini? Hayo huwakilisha mwili, na hata matendo yaliyo bora zaidi ya nje hayawakilishi maisha, ila tabia yako tu mwenyewe. Matendo ya nje ya mwanadamu hayawezi kutimiza matakwa ya Mungu. Wewe daima huzungumza kuhusu udeni wako kwa Mungu, lakini huwezi kuyaruzuku maisha ya wengine au kuwafanya wengine kumpenda Mungu. Je, unaamini kwamba matendo kama hayo yatamridhisha Mungu? Unaamini kwamba hii ndiyo matakwa ya moyo wa Mungu, kwamba haya ni ya roho, lakini kwa kweli huu ni ujinga! Unaamini kwamba yale yanayokupendeza wewe na unayotaka ni yale yanayomfurahisha Mungu. Je, yanayokupendeza yanaweza kuwakilisha yanayompendeza Mungu? Je, tabia ya mwanadamu inaweza kumwakilisha Mungu? Yale yanayokupendeza wewe ndiyo hasa yale humchukiza Mungu, na mienendo yako ni ile ambayo Mungu huchukia na kukataa. Kama unahisi kuwa wewe ni mdeni, basi nenda na usali mbele za Mungu. Hakuna haja ya kuzungumzia jambo hilo kwa watu wengine. Usipoomba mbele za Mungu na badala yake mara kwa mara unajivuta nadhari kwako mbele ya wengine, jambo hili linaweza kutimiza matakwa ya moyo wa Mungu? Kama matendo yako daima yanaonekana tu, hii ina maana kuwa wewe ni mtu bure zaidi ya wote. Ni mtu wa aina gani yule aliye na matendo mazuri ya kijuujuu tu lakini hana uhalisi? Watu kama hao ni Mafarisayo wanafiki na watu wa dini! Msipoacha matendo yenu ya nje na hamuwezi kufanya mabadiliko, basi dalili za unafiki ndani yenu zitazidi kuimarika. Kadiri dalili za unafiki zinavyozidi, ndivyo upinzani kwa Mungu unavyozidi, na mwishowe, watu wa aina hii hakika watatupiliwa mbali!

Iliyotangulia: Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Inayofuata: Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp