Ufalme wa Milenia Umewasili

Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. Kutoka mbinguni Mungu alituma chakula, maji, na mana ili watu waweze kuvifurahia, na leo bado ni hivyo: Mungu mwenyewe ametuma vitu chini kwa ajili ya kula na kunywa ili watu wafurahi, na yeye mwenyewe ametuma laana ili kuwaadibu watu. Na hivyo kila hatua ya kazi Yake inafanywa na Mungu Mwenyewe. Leo, watu wanatamani utokeaji wa kweli, wanajaribu kuona ishara na maajabu, na kuna uwezekano mkubwa watu wa namna hiyo kutelekezwa, maana kazi ya Mungu inazidi kuwa halisi. Hakuna anayejua kwamba Mungu ameshuka kutoka mbinguni, bado hawajui kwamba Mungu ametuma chini chakula na maji ya kutia nguvu kutoka mbinguni, lakini Mungu kimsingi yupo, na mazingira mazuri ya Ufalme wa Milenia ambao watu wanaufikiria pia ni matamshi ya Mungu Mwenyewe. Huu ni ukweli, ni huu tu ndio unaotawala pamoja na Mungu duniani. Kutawala na Mungu duniani kunarejelea mwili. Kile ambacho si cha mwili hakipo duniani, na hivyo wale wote wanaojikita katika kusonga mbele katika mbingu ya tatu wanafanya hivyo bure. Siku moja, ambapo ulimwengu mzima utarudi kwa Mungu, kitovu cha kazi Yake katika ulimwengu wote kitafuata matamko ya Mungu; kwingineko watu watapiga simu, wengine watapanda ndege, wengine watapanda boti na kupita baharini, na wengine watatumia leza kupokea matamshi ya Mungu. Kila mmoja atakuwa anatamani na mwenye shauku, wote watakuja karibu na Mungu, na kukusanyika kwa Mungu, na wote watamwabudu Mungu—na yote haya yatakuwa matendo ya Mungu. Kumbuka hili! Mungu hawezi kuanza tena kwingineko. Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini itapitia njaa kubwa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea. Huo ndio utakuwa muda ambapo matendo ya Mungu yatafichuliwa, na Mungu atatukuzwa; watu wote katika ulimwengu wote watakuja na kumwabudu “mtu” asiyekuwa wa kawaida. Je, hii haitakuwa siku ya utukufu wa Mungu? Siku moja, wachungaji wa zamani watatuma ujumbe wakitafuta maji kutoka katika chemchemi za maji ya uzima. Watakuwa wazee, lakini watakuja kumwabudu mtu huyu ambaye walimdharau. Katika vinywa vyao watakiri na katika mioyo yao wataamini—je, hii si ishara na maajabu? Siku ambapo ufalme wote utafurahia ni siku ya utukufu wa Mungu, na mtu yeyote atakayewajia, na kupokea habari njema za Mungu atabarikiwa na Mungu, na nchi hizi na watu hawa watabarikiwa na kulindwa na Mungu. Mwelekeo wa maisha yajayo utakuwa hivi: Wale ambao watapata matamshi kutoka katika kinywa cha Mungu watakuwa na njia ya kutembea duniani, na wawe wafanya biashara au wanasayansi, au waelimishaji au wataalamu wa viwandani, wale ambao hawana maneno ya Mungu watakuwa na wakati mgumu wa kuchukua hata hatua moja, na watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Hiki ndicho kinamaanishwa na, “Ukiwa na ukweli utatembea ulimwengu mzima; bila ukweli, hutafika popote.” Ukweli ni huu: Mungu atatumia Njia (ikiwa na maana kwamba maneno Yake yote) kuuamuru ulimwengu wote na kumwongoza na kumshinda mwanadamu. Watu siku zote wanatarajia kuwa na mageuko makubwa katika namna ambayo Mungu anafanya kazi. Kuzungumza kwa wazi, ni kupitia maneno ndipo Mungu anawadhibiti watu, na unapaswa kufanya kile Anachokisema haijalishi kama unataka au hutaki; huu ni ukweli halisi, na unapaswa kutiiwa na watu wote, na hivyo haubadiliki, na kujulikana kwa wote.

Roho Mtakatifu anawapatia watu hisia. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, katika mioyo yao wamesimama imara, na wana amani, wakati wale ambao hawapati maneno ya Mungu wanajihisi watupu. Hiyo ni nguvu ya maneno ya Mungu—watu wanapaswa kuyasoma, baada ya kuyasoma wananawirishwa, na hawawezi kufanya chochote bila hayo. Ni kama ambapo watu wanatumia afyuni: Inawapatia nguvu, na bila hiyo wanahisi nguvu yake ya kuvuta, na wanakosa nguvu. Hayo ndiyo mazoea miongoni mwa watu leo. Kusoma maneno ya Mungu kunawapatia watu nguvu. Ikiwa hawayasomi, wanajiona hawana nguvu, lakini baada ya kuyasoma, wanainuka mara moja kutoka katika “kitanda cha mgonjwa.” Hii ni neno la Mungu kutawala duniani na Mungu kutawala ulimwenguni. Baadhi ya watu wanataka kuacha au wamechoshwa na kazi ya Mungu. Licha ya hayo, hawawezi kujitenganisha na maneno ya Mungu; bila kujali ni wadhaifu kiasi gani, bado ni lazima waishi kwa kutegemea maneno ya Mungu ili waishi, na haijalishi ni watu wa uasi kiasi gani, lakini bado hawathubutu kuacha maneno ya Mungu. Pale ambapo maneno ya Mungu yanaonyesha ukuu wao ndipo ambapo Mungu anatawala na kuchukua nguvu, na hivi ndivyo Mungu anavyofanya kazi. Hata hivyo, hii ndiyo njia ambayo kwayo Mungu anafanya kazi, na hakuna anayeweza kuiacha. Maneno ya Mungu yataenea katika nyumba zisizohesabika, yatafahamika kwa wote, na wakati huo tu ndipo kazi yake itaenea ulimwenguni kote. Ambapo ni sawa na kusema, ikiwa kazi ya Mungu itaenea ulimwenguni kote, basi maneno Yake ni lazima yaenee. Katika siku ya utukufu wa Mungu, maneno ya Mungu yataonesha nguvu yake na mamlaka. Kila neno Lake kuanzia wakati huo hadi leo litatimizwa na kuwa la kweli. Kwa njia hii, utukufu utakuwa wa Mungu duniani—ambavyo ni sawa na kusema, kazi yake itatawala duniani. Wote ambao ni waovu wataadibiwa na maneno katika kinywa cha Mungu, wale wote ambao ni wa haki watabarikiwa na maneno katika kinywa Chake, na wote watathibitishwa na kukamilishwa na maneno katika kinywa Chake. Wala hataonyesha ishara zozote na maajabu; yote yatakamilishwa na maneno Yake, na maneno Yake yatazalisha ukweli. Kila mtu duniani atasherehekea maneno ya Mungu, ama ni watu wazima au watoto, wanaume, wanawake, wazee, au vijana, watu wote watajinyenyekeza katika maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu yaonekana katika mwili, yakiwaruhusu watu kuyaona duniani, waziwazi na kufanana na kiumbe chenye uhai. Hii ndiyo maana ya Neno kufanyika mwili. Mungu amekuja duniani kwa lengo la kukamilisha ukweli wa “Neno kufanyika mwili,” ni sawa na kusema, Amekuja ili kwamba maneno Yake yaweze kutolewa kutoka katika mwili (sio kama wakati wa Musa katika Agano la Kale, ambapo Mungu alizungumza moja kwa moja kutoka mbinguni). Baada ya hapo, kila neno Lake litatimizwa wakati wa Enzi ya Ufalme wa Milenia, zitakuwa ni kweli ambazo zitaonekana katika macho ya watu, na watu watazitazama kwa kutumia macho bila tofauti hata kidogo. Hii ndiyo maana kuu ya Mungu kupata mwili. Ni sawa na kusema, kazi ya Roho imetimizwa kupitia mwili, na kupitia maneno. Hii ndiyo maana ya kweli ya “Neno kufanyika mwili” na “Neno Laonekana katika mwili.” Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuzungumza mapenzi ya Roho, na ni Mungu pekee katika mwili ndiye anayeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho; maneno ya Mungu yamewekwa wazi katika Mungu kupata mwili, na kila mtu anaongozwa nayo. Hakuna aliyeachwa, wote wanakuwa ndani ya mawanda haya. Ni kutoka tu katika matamshi haya ndipo watu wanaweza kujua; wale ambao hawatapata njia hii wanaota ndoto za mchana ikiwa wanadhani wanaweza kupata matamshi kutoka mbinguni. Hayo ndiyo mamlaka yaliyooneshwa katika mwili wa Mungu uliopata mwili: kuwafanya wote kuamini. Hata wataalamu wa kuheshimiwa sana na wachungaji hawawezi kuzungumza maneno haya. Wote ni lazima wajinyenyekeze chini yao, na hakuna anayeweza kuanza mwanzo mpya. Mungu atatumia maneno kuushinda ulimwengu. Atafanya hivi si kwa kupata kwake mwili, lakini kwa kutumia matamshi kutoka kwa Mungu katika mwili kushinda watu wote duniani; Namna hii tu ndiye Mungu katika mwili, na huu tu ndio kuonekana kwa Mungu katika mwili. Labda kwa watu, inaonekana kana kwamba Mungu hajafanya kazi kubwa—lakini Mungu analazimika kutamka maneno Yake ili watu washawishike kabisa, na wao kutishika kabisa. Bila kweli, watu wanapiga makelele na kupiga mayowe; kwa maneno ya Mungu, wote wananyamaza kimya. Mungu hakika atakamilisha ukweli huu, maana huu ni mpango ulioanzishwa na Mungu: kukamilisha ukweli wa Neno kuwasili duniani. Kimsingi, sina haja ya kuelezea—kuwasili kwa Ufalme wa Milenia duniani ni kuwasili kwa neno la Mungu duniani. Kushuka kwa Yerusalemu mpya kutoka mbinguni ni kuwasili kwa maneno ya Mungu kuishi miongoni mwa mwanadamu, kuenenda na kila tendo la mwanadamu, na mawazo yake yote ya ndani. Huu pia ni ukweli kwamba Mungu atatimiza, na mandhari mazuri kabisa ya Ufalme wa Milenia. Huu ndio mpango uliowekwa na Mungu: Maneno Yake yataonekana duniani kwa miaka elfu moja, na yatashuhudia matendo yake yote, na kukamilisha kazi Yake yote duniani, ambapo baada ya hatua hii mwanadamu atakuwa amefikia kikomo.

Iliyotangulia: Amri za Enzi Mpya

Inayofuata: Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp