Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa vitendo Mwenyewe. Ikiwa unamjua tu Mtu huyo—ikiwa unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au kile ambacho Roho hufanya katika mwili, na ukizingatia tu Roho, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo. Ufahamu wa Mungu wa vitendo unajumuisha kujua na kuyapitia maneno Yake, na kuelewa sheria na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na jinsi Roho wa Mungu anavyofanya kazi katika mwili. Kwa hivyo, pia, inajumuisha kujua kwamba kila tendo la Mungu katika mwili linaongozwa na Roho, na kwamba maneno Anenayo ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Hivyo, ukitaka kumjua Mungu wa vitendo, lazima kimsingi ujue jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi katika ubinadamu na katika uungu; hili, kwa upande wake, linahusu maonyesho ya Roho, ambayo watu wote hujihusisha nayo.

Ni nini kilichomo katika maonyesho ya Roho? Wakati mwingine Mungu hufanya kazi katika ubinadamu, na wakati mwingine katika uungu—lakini kwa ujumla, katika hali zote mbili Roho ndiye anayeamuru. Hata iwe ni roho gani ndani ya watu, hivyo ndivyo huwa maonyesho yao ya nje. Roho hufanya kazi kwa kawaida, lakini kuna sehemu mbili kwa uelekezaji Wake kwa Roho: Sehemu moja ni kazi Yake katika ubinadamu, na nyingine ni kazi Yake kupitia uung. Unafaa kujua haya wazi wazi. Kazi ya Roho inatofautiana kulingana na hali: Wakati kazi Yake ya kibinadamu inapohitajika, Roho huongoza kazi hii ya kibinadamu, na wakati kazi Yake ya Uungu inahitajika, uungu huonekana moja kwa moja ili kuitekeleza. Kwa sababu Mungu hufanya kazi katika mwili na kujionyesha katika mwili, Anafanya kazi katika ubinadamu na katika uungu. Kazi Yake katika ubinadamu inaongozwa na Roho, na ili kuyaridhisha mahitaji ya kimwili ya watu, kuwezesha ushirikiano wao Naye, kuwafanya waone uhalisi na ukawaida wa Mungu, na kuwafanya waone kuwa Roho amekuja katika Mwili, na Yuko miongoni mwa wanadamu, Anaishi pamoja na wanadamu, na Hushirikiana na wanadamu. Kazi Yake ya uungu ni kwa ajili ya kuwapa watu uzima, na kuwaelekeza watu katika kila kitu kwa upande mzuri, na kubadili tabia za watu na kuwafanya waone kwa kweli kuonekana kwa Roho katika mwili. Kwa kiwango kikubwa, ukuaji katika maisha ya mwanadamu unapatikana moja kwa moja kupitia kazi ya Mungu na maneno katika uungu. Ikiwa tu watu wataikubali kazi ya Mungu ya uungu wataweza kubadili tabia zao, na hapo tu ndipo wataweza kushibishwa katika roho zao; ni ikiwa tu, ikiongezwa kwa hili, ndipo kutakuwa na kazi katika ubinadamu—uchungaji wa Mungu, usaidizi, na riziki kwa ubinadamu—ndipo matokeo ya kazi ya Mungu yanaweza kufanikishwa kikamilifu. Mungu wa vitendo Mwenyewe ambaye Anazungumziwa leo hufanya Kazi katika uungu na ubinadamu. Kazi ya Roho inatofautiana kulingana na hali: Wakati kazi Yake ya kibinadamu inapohitajika, Roho huongoza kazi hii ya kibinadamu, na wakati kazi Yake ya Uungu inahitajika, uungu huonekana moja kwa moja ili kuitekeleza. Ubinadamu na uungu wake vimeungwa kuwa kitu kimoja, na kazi ya pande zote mbili inakamilishwa kupitia maneno; iwe katika ubinadamu au uungu, Ananena maneno. Mungu anapofanya Kazi katika ubinadamu, Anazungumza lugha ya ubinadamu, ili watu waweze kushiriki na kuelewa. Maneno Yake yanasemwa waziwazi, na ni rahisi kueleweka, kiasi kwamba yanaweza kutolewa kwa watu wote; bila ya kujali kuwa hawa watu wana ufahamu au hawajasoma vyema, wote wanaweza kupokea maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu katika uungu vilevile inaweza kufanywa kupitia maneno, lakini imejawa na riziki, imejawa na uzima, haijatiwa dosari na mawazo ya mwanadamu, haihusishi mapenzi ya mwanadamu, na haina mipaka ya binadamu, iko nje ya mipaka ya ubinadamu wowote wa kawaida; vilevile, inafanywa katika mwili, lakini ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Kama watu wanaikubali kazi ya Mungu katika ubinadamu tu, basi watajiwekea mipaka katika upeo fulani, na hivyo milele watahitaji kushughulikiwa, kupogolewa, na kufundishwa nidhamu ili kwamba pawepo na mabadiliko kidogo ndani yao. Bila ya Kazi au uwepo wa Roho Mtakatifu, ingawa, watairudia mienendo yao ya awali; ni kupitia kazi ya uungu tu ndio haya maradhi na upungufu vitaweza kurekebishwa, hapo ndipo watu wanafanywa kuwa wakamilifu. Badala ya kushughulikia na kupogoa mara kwa mara, kinachohitajika ni matokeo mazuri, kwa kutumia maneno kufidia upungufu wote, kutumia maneno ili kufichua hali zote za watu, kutumia maneno kuyaelekeza maisha yao, kila matamshi yao, kila tendo lao, ili kuziweka wazi nia na motisha yao; hii ni kazi halisi ya Mungu wa vitendo. Na kwa hivyo, katika mwelekeo wako kwa Mungu wa vitendo unafaa kunyenyekea mbele ya ubinadamu Wake, ukimkubali na kumtambua, na zaidi, unapaswa kukubali na kutii kazi ya uungu na maneno. Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kuwa kazi yote na maneno ya Roho wa Mungu yanafanywa katika ubinadamu wake wa kawaida, na kupitia mwili Wake uliopatikana. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu huelekeza kazi Yake ya ubinadamu na hutekeleza kazi Yake ya uungu katika mwili, na katika Mungu kupata mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi kamili ya uungu; huu ndio umuhimu wa utendaji hata zaidi wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili. Ikiwa unaweza kuliona hili kwa uwazi, utaweza kuhusisha sehemu zote tofauti za Mungu, na utakoma kuweka thamani kubwa sana kwa kazi Yake katika uungu, na kudharau sana kazi Yake katika ubinadamu, wala hautapita mipaka, wala kupita njia za michepuo. Kwa ujumla, maana ya Mungu wa vitendo ni kuwa kazi Yake ya ubinadamu na kazi Yake ya uungu, kama inavyoelekezwa na Roho, inaonyeshwa kupitia mwili Wake, ili watu waone kuwa Yeye ni wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, na ni halisi na wa hakika.

Kazi ya Roho wa Mungu katika ubinadamu ina awamu za mpito. Kwa kufanya ubinadamu kuwa mkamilifu, Anawezesha ubinadamu Wake kupokea mwelekeo wa Roho, ambapo baadaye ubinadamu Wake unaweza kuyakimu na kuyachunga makanisa. Hii ni aina moja ya maonyesho ya kazi ya kawaida ya Mungu. Hivyo, ukiweza kuona wazi kanuni za kazi ya Mungu katika ubinadamu, basi itakuwa vigumu kwako kuwa na dhana kuhusu kazi ya Mungu katika ubinadamu. Bila kujali kitu kingine chochote, Roho wa Mungu hawezi kukosea. Yuko sahihi, na Hana dosari; Hawezi kufanya kitu chochote kimakosa. Kazi ya uungu ni maonyesho ya moja kwa moja ya mapenzi ya Mungu, bila maingilio ya ubinadamu. Haipitii ukamilifu, ila inatoka moja kwa moja kwa Roho. Na bado, kufanya Kwake kazi katika uungu ni kwa sababu ya ubinadamu Wake wa kawaida; si miujiza, na kazi inaonekana kana kwamba imefanywa na mwanadamu wa kawaida; Kimsingi Mungu alitoka mbinguni kuja duniani ili kuonyesha maneno ya Mungu kupitia mwili, kukamilisha kazi ya Roho wa Mungu kwa kutumia mwili.

Ufahamu wa watu leo kuhusu Mungu wa vitendo bado unaegemea upande mmoja, na ufahamu wao kuhusu umuhimu wa kupata mwili bado ni mdogo sana. Kuhusu suala la mwili wa Mungu, watu huona kupitia katika kazi na maneno Yake kwamba Roho wa Mungu ana mengi, kwamba yeye ni tajiri. Lakini, hata hivyo, ushuhuda wa Mungu hatimaye hutoka kwa Roho wa Mungu: Anachokifanya Mungu katika Mwili, ni kanuni gani anatumia, anachokifanya katika ubinadamu, na anachokifanya katika uungu. Watu lazima wawe na ufahamu wa hili. Leo unaweza kumwabudu huyu mtu, lakini kwa hakika unamwabudu Roho. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa kinachopaswa kufahamiwa kuhusu ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliyepata mwili: kujua kiini cha Roho kupitia kwa mwili, kujua kazi ya uungu ya Roho katika mwili na kazi ya mwanadamu katika mwili, kukubali maneno yote ya Roho na matamshi katika mwili, na kuona jinsi Roho wa Mungu anauelekeza mwili na kudhihirisha uwezo Wake katika mwili. Hivi ni kusema kuwa, mwanadamu anapata kumjua Roho aliye mbinguni kupitia kwa mwili; kuonekana kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe miongoni mwa wanadamu kumemwondoa Mungu asiye yakini kutoka katika dhana za wanadamu; ibada ya watu kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe imeongeza utiifu wao kwa Mungu; na kupitia kwa uungu wa kazi ya Roho wa Mungu katika Mwili, na kazi ya mwanadamu katika mwili, mwanadamu hupata ufunuo, na kuongozwa, na mabadiliko hupatikana katika tabia ya maisha yake. Hii tu ndiyo maana halisi ya ujio wa Roho katika mwili, kimsingi, ili kwamba watu waweze kushirikiana na Mungu, kumtegemea Mungu, na kuupata ufahamu wa Mungu.

Kwa kiasi kikubwa, ni mtazamo upi watu wanapaswa kuwa nao kuhusu Mungu wa vitendo? Unajua nini kuhusu kupata mwili, kuhusu kuonekana kwa Neno katika mwili, kuhusu kuonekana kwa Mungu katika mwili, na matendo ya Mungu wa vitendo? Mada kuu za kuzungumziwa leo ni zipi? Kupata mwili, ujio wa Neno katika mwili, kuonekana kwa Mungu katika mwili yote ni masuala ambayo ni lazima yaeleweke. Ni lazima mpate kuyaelewa haya masuala hatua kwa hatua na muwe na ufahamu ulio wazi kuyahusu katika uzoefu wenu wa maisha, kwa msingi wa kimo chenu na kwa msingi wa enzi. Mchakato ambao watu huyapitia maneno ya Mungu ni sawa na mchakato ambao kwao wanafahamu kuonekana kwa maneno ya Mungu katika mwili. Kadiri watu wanavyoyapitia maneno ya Mungu, ndivyo wanavyomjua Roho wa Mungu; kwa kuyapitia maneno ya Mungu, watu wanaelewa kanuni za kazi ya Roho na kupata kumjua Mungu wa vitendo Mwenyewe. Kwa hakika, Mungu anapowafanya watu kuwa wakamilifu na kuwapata, Anawafanya wayajue matendo ya Mungu wa vitendo; Anatumia kazi ya Mungu wa vitendo kuwaonyesha watu umuhimu halisi wa kupata mwili, na kuwaonyesha kuwa Roho wa Mungu hakika ameonekana kwa mwanadamu. Watu wakipatwa na kufanywa wakamilifu na Mungu, maonyesho ya Mungu wa vitendo yamewashinda, maneno ya Mungu wa vitendo yamewabadilisha, na kutoa uzima Wake ndani yao, kuwajaza na kile Alicho (iwe ni uwepo wake wa binadamu, au ule wa uungu), kuwajaza kwa kiini cha maneno Yake, na kuwafanya watu waishi kwa kudhihirisha maneno Yake. Mungu akiwapata watu, kimsingi Anafanya hivyo kwa kutumia maneno na matamko ya Mungu wa vitendo ili kuushughulikia upungufu wa watu, na kuhukumu na kufichua tabia zao za uasi, kuwafanya wapate wanachokihitaji, na kuwaonyesha kuwa Mungu yuko miongoni mwa wanadamu. Muhimu zaidi, kazi ifanywayo na Mungu wa vitendo ni kumwokoa kila mtu kutoka katika ushawishi wa Shetani, kuwatoa katika nchi ya uchafu, na kuziondoa tabia zao potovu. Umuhimu mkubwa zaidi wa watu kupatikana na Mungu wa vitendo ni kuwa na uwezo wa kumfanya Mungu wa vitendo kielelezo, na kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, kuweza kutenda kulingana na maneno na mahitaji ya Mungu wa vitendo, bila upotofu au kuteleza, kutenda kama Asemavyo, na kuweza kufanikisha lolote Atakalo. Kwa njia hii, utakuwa umepatwa na Mungu. Ukipatwa na Mungu, hupati tu kazi ya Roho Mtakatifu; kimsingi, unaweza kuishi kulingana na matakwa ya Mungu wa vitendo. Kuwa tu na kazi ya Roho Mtakatifu hakumaanishi kuwa una uzima. Cha muhimu ni kama unaweza kuishi kwa kudhihirisha mahitaji ya Mungu wa vitendo, ambayo inahusiana na kama unaweza kupatikana na Mungu. Haya mambo ndiyo muhimu zaidi katika kazi ya Mungu wa vitendo katika mwili. Ambayo ni kusema, Mungu analipata kundi la watu kwa kuonekana halisi na hakika katika mwili na kuwa wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, Akionekana na watu, hasa Akifanya kazi ya Roho katika mwili, na kwa kuwa kielelezo kwa watu katika mwili. Kimsingi, ujio wa Mungu katika mwili ni kuwawezesha watu kuona matendo halisi ya Mungu, kumfanya Roho asiye na umbo kuwa bayana katika mwili, na kuwapa watu fursa ya kumwona na kumgusa. Kwa njia hii, wanaokamilishwa Naye wataishi kwa kumfuata Yeye, watamfaidi na kuupendeza moyo Wake. Mungu angalinena kutoka mbinguni tu, na hakika asije duniani, basi bado watu hawangeweza kumjua, wangeweza tu kuyahubiri matendo ya Mungu kwa kutumia nadharia tupu, na hawangekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Mungu amekuja duniani kimsingi kuwa mfano na kielelezo kwa wale ambao wamepatwa na Mungu; ni kwa njia hii pekee ndio watu wanaweza kumjua Mungu kwa hakika, na kumgusa Mungu, na kumwona, na hapo ndipo wanaweza kupatikana na Mungu kwa kweli.

Iliyotangulia: Ufalme wa Milenia Umewasili

Inayofuata: Kuijua Kazi ya Mungu Leo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp