Fumbo la Kupata Mwili (2)

Wakati huo Yesu alipofanya kazi Yudea, Alifanya hivyo kwa uwazi, lakini sasa, Ninafanya kazi na kunena miongoni mwenu kwa siri. Wasioamini hawana habari nayo kabisa. Kazi Yangu miongoni mwenu imefungwa kwa wale walio nje. Maneno haya, kuadibu huku na hukumu hii, vinajulikana tu kwako na sio mwingine. Kazi hii yote inatendeka kati yenu na kuonekana tu kwenu; hakuna yeyote asiyeamini anayefahamu haya, kwani muda haujafika. Watu hawa hapa wako karibu kukamilishwa baada ya kustahimili kuadibu, lakini walio nje hawajui lolote kuhusu hilo. Kazi hii imefichwa sana! Kwao, Mungu mwenye mwili ni siri, lakini kwa wale walio katika mkondo, Anaweza kuchukuliwa kuwa wazi. Ingawa katika Mungu yote yako wazi, yote yanafichuliwa, na yote yamewekwa huru, hii ni kweli tu kwa wale wanaomwamini; kwa habari ya hao wengine, wasioamini, hakuna kinachojulikana. Kazi inayofanywa kwa sasa miongoni mwenu na huko Uchina imefungwa vikali, ili kuwazuia wasijue. Iwapo wangeifahamu kazi hii, basi ambacho wangefanya ni kuishutumu na kukabili mateso. Hawangeiamini. Kufanya kazi katika taifa la joka kuu jekundu, mahali palipo nyuma zaidi, sio kazi rahisi. Kama kazi hii ingewekwa wazi na kujulikana, basi ingekuwa vigumu kuendelea. Hatua hii ya kazi haiwezi kuendelea katika sehemu hii. Wangestahimili vipi kama kazi hii ingeendelezwa kwa uwazi? Hii haingeleta hata hatari kubwa zaidi? Kama kazi hii haingefichwa, na badala Yake kuendelea kama wakati wa Yesu Alivyowaponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa njia ya kustaajabisha, basi si ingekuwa tayari “imeshanyakuliwa” na ibilisi? Je, wangestahimili uwepo wa Mungu? Kama sasa ningeingia kwenye sinagogi kuwahadhiria wanadamu, je, si ningekuwa nimeshapasuliwa katika vipande kitambo? Na ikiwa hivyo, kazi Yangu itawezaje kuendelea kufanyika? Sababu ambayo ishara na miujiza haitendeki wazi wazi ni kwa ajili ya kujificha. Kwa hivyo kazi Yangu haiwezi kuonekana, kujulikana wala kugunduliwa na wasioamini. Iwapo hatua hii ya Kazi ingefanyika kwa njia sawa na kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, haingekuwa thabiti sana. Kwa hivyo, kazi hii kufichwa namna hii ni ya manufaa kwenu na kwa kazi yote. Wakati kazi ya Mungu duniani inafika kikomo, kumaanisha, wakati kazi hii katika siri inakamilika, hatua hii ya kazi italipuka na kuwa wazi. Watu wote watajua kwamba kuna kundi la washindi ndani ya taifa la Uchina; kila mwanadamu atafahamu kuwa Mungu katika mwili yuko Uchina na kwamba kazi Yake imefika kikomo. Hapo tu ndipo kutampambazukia mwanadamu: Ni kwa nini taifa la Uchina halijaonyesha kudhoofika wala kuporomoka? Inaonekana kuwa Mungu anaendeleza kazi Yake binafsi katika taifa la China na amefanya kuwa kamilifu kundi la watu na kuwafanya washindi.

Mungu mwenye mwili Anajidhihirisha mwenyewe kwa watu kadhaa wanaomfuata Anapofanya kazi Yeye binafsi, na sio kwa viumbe wote. Alifanyanyika mwili ili tu Akamilishe hatua ya kazi Yake, na sio ili amwonyeshe mwanadamu mfano Wake. Hata hivyo, kazi Yake lazima ifanywe na Yeye binafsi, kwa hivyo inalazimu Afanye kazi hiyo katika mwili. Kazi hii inapokamilika, Ataondoka duniani; Hawezi kusalia duniani kwa muda mrefu kwa hofu ya kuzuia kazi inayokuja. Anachokionyesha kwa halaiki ni tabia Yake ya haki na matendo Yake yote, na sio umbo la wakati Amefanyika mwili mara mbili, kwa maana mfano wa Mungu unaweza tu kuonyeshwa kupitia kwa tabia Yake, na si kubadilishwa na mfano wa mwili Wake wa nyama. Mfano wa mwili Wake wa nyama huonyeshwa kwa watu wachache tu, kwa wale wanaomfuata Anapofanya kazi katika mwili. Hiyo ndio maana kazi inayofanywa wakati huu inafanywa kwa siri. Ni kama tu vile Yesu alivyojionyesha kwa Wayahudi pekee yao Alipofanya kazi Yake, na hakujionyesha hadharani kwa mataifa mengine. Hivyo, pindi Alipomaliza kazi Yake, Aliondoka miongoni mwa wanadamu na hakukawia; baadaye, haikuwa Yeye, sura hii ya mwanadamu, Aliyejionyesha kwa mwanadamu, bali Roho Mtakatifu ambaye Alitekeleza kazi moja kwa moja. Mara tu kazi ya Mungu katika mwili inapokamilika, Anaondoka katika dunia ya mwanadamu, na kamwe Hafanyi tena kazi sawa na ile Aliyofanya Akiwa katika mwili. Kazi inayofuata hufanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Wakati huu, mwanadamu hawezi kuona mfano Wa Mungu katika mwili; Yeye Hajionyeshi wazi kwa mwanadamu hata kidogo, na daima Anabaki mafichoni. Muda wa kazi ya Mungu mwenye mwili ni mchache, ambayo lazima ifanywe katika Enzi bayana, muda, taifa na kati ya watu bayana. Kazi kama hiyo inawakilisha tu kazi ya wakati wa Mungu katika mwili, na inalenga enzi fulani, ikiwakilisha kazi ya Roho wa Mungu katika enzi moja hasa, na sio ujumla wa kazi Yake. Kwa hivyo, umbo la Mungu mwenye mwili halitaonyeshwa kwa kila mwanadamu. Kinachoonyeshwa kwa halaiki ni haki ya Mungu na tabia Yake kwa ukamilifu, na wala sio mfano Wake Alipokuwa mwili mara mbili. Sio sura inayoonyeshwa kwa mwanadamu, wala mifano yote miwili ikijumlishwa. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba mwili wa Mungu uondoke duniani baada ya kukamilisha kazi Anayohitajika kufanya, kwa kuwa Anakuja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya, na sio kuwaonyesha wanadamu mfano wa umbo Lake. Ingawa umuhimu wa kuingia katika mwili umeshatimizwa na Mungu mara mbili Akifanyika mwili na nyama, bado hatajionyesha wazi kwa taifa ambalo halijawahi kumwona awali. Yesu hatajionyesha tena kwa Wayahudi kama Jua la haki, wala hatapanda Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa watu wote; yote ambayo Wayahudi wameona ni picha ya Yesu wakati wa Uyahudi. Hii ni kwa sababu kazi ya Yesu katika kupata mwili Kwake ilimalizika miaka elfu mbili iliyopita; Hatarudi Uyahudi kwa sura ya Myahudi, sembuse kujionyesha katika sura ya Myahudi kwa nchi yoyote ya Mataifa, kwa maana sura ya Yesu kufanyika mwili ni sura ya Myahudi tu, na si sura ya Mwana wa Adamu ambaye Yohana alimwona. Ingawa Yesu aliwaahidi wafuasi Wake kwamba Angerudi tena, Hatajionyesha tu Mwenyewe katika sura ya Myahudi kwa wote walio katika nchi za Mataifa. Mnapaswa kujua kwamba kazi ya Mungu katika mwili inafaa kufungua enzi mpya. Kazi hii ni ya muda wa miaka michache tu, na Hawezi kukamilisha kazi yote ya Roho wa Mungu. Hii ni sawia na vile umbo la Yesu kama Myahudi linaweza tu kuwakilisha mfano wa Mungu alivyofanya kazi katika Yudea, na Angefanya tu kazi ya msalabani. Wakati ambao Yesu Alikuwa katika mwili, Hangefanya kazi ya kutamatisha enzi au kumwangamiza mwanadamu. Kwa hivyo, baada ya kusulubiwa na kukamilisha kazi Yake, Alipaa juu na daima Akajificha kutoka kwa mwanadamu. Kutoka wakati huo kuendelea, wale waumini wa mataifa waliweza tu kuiona picha Yake ambayo walibandika kwenye kuta zao, na sio udhihirisho wa Bwana Yesu. Picha hii imechorwa na mwanadamu tu, na si mfano ambao Mungu Mwenyewe Alimwonyesha mwanadamu. Mungu Hatajionyesha kwa halaiki wazi wazi katika mfano ambao Yeye Alikuwa nao mara mbili Akiwa katika mwili. Kazi Anayofanya miongoni mwa wanadamu ni kuwaruhusu kuelewa tabia Yake. Yote haya yanaonyeshwa kwa mwanadamu kwa njia ya kazi za enzi tofauti; yanakamilishwa kupitia tabia ambazo Ameziweka wazi na kazi ambayo Amefanya, na bali si kupitia kwa udhihirisho wa Yesu. Hiyo ni kusema, umbo la Mungu halionyeshwi kwa mwanadamu kupitia katika mfano wa Mungu mwenye mwili, lakini ni kwa kupitia katika kazi iliyotekelezwa na Mungu mwenye mwili wa sura na umbo; na kupitia kazi Yake, mfano Wake unaonekana na tabia Yake inajulikana. Huu ndio umuhimu wa kazi Angependa kufanya katika mwili.

Mara tu kazi ya Mungu kupata mwili mara mbili inapofikia mwisho, Ataanza kuonyesha tabia Yake ya haki katika mataifa yote, kuruhusu umati kuona sura Yake. Atadhihirisha tabia Yake na kwa njia hii ataweka wazi mwisho wa kategoria mbalimbali za mwanadamu, na hivyo kuleta mwisho kabisa enzi nzee. Kazi Yake katika mwili haitendeki katika sehemu pana (kama vile Yesu Alivyofanya kazi katika sehemu ya Yudea peke Yake, na leo hii Ninafanya kazi miongoni mwenu pekee) kwa sababu kazi Yake katika mwili ina mipaka na kingo. Anafanya tu kazi ya muda mchache katika mfano wa kawaida na mwili wa kawaida, badala ya kufanya kazi ya milele kupitia kwa Mungu mwenye mwili, ama kufanya kazi ya kuwaonekania watu wote wa mataifa. Kazi hii katika mwili lazima izuiliwe katika mawanda (kama vile kufanya kazi katika Yudea ama kati Yenu), kisha kupanua kazi iliyofanyika katika mipaka hii. Bila shaka, kazi ya upanuzi huu huendeshwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja na haiwezi kuwa kazi ya mwili Wake wa nyama. Kwa maana kazi katika mwili iko na mipaka na haiwezi kuenea katika pembe zote za ulimwengu. Hauwezi kuyatekeleza haya. Kupitia kwa kazi katika mwili, Roho Wake hutekeleza kazi inayofuatia. Kwa hivyo, kazi inayofanywa katika mwili ni ya matayarisho inayotekelezwa ndani ya mipaka; Roho Wake kisha Anaendeleza kazi hii, na kuipanua.

Kazi ambayo Mungu anakuja kufanya katika dunia hii ni kuongoza enzi tu, kufungua enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Hajakuja kuishi kulingana na maisha ya mwanadamu wa kawaida kwa kikamilifu, kupitia Mwenyewe raha na machungu ya maisha kama mwanadamu, au kumfanya mtu fulani mkamilifu kwa mkono Wake au kumtazama binafsi mtu Fulani anavyokua. Hii sio kazi Yake; Kazi Yake ni kufungua tu enzi mpya na kukomesha ile ya zamani. Hiyo ina maana, Atafungua enzi mpya, akamilishe iliyotangulia, amshinde shetani kwa kufanya kazi Yake binafsi. Kila wakati Anapofanya kazi Yake Mwenyewe, ni kana kwamba Anaweka mguu kwenye uwanja wa vita. Kwanza, Anaushinda ulimwengu na kumshinda Shetani katika mwili; Anachukua utukufu wote na kuinua pazia juu ya ukamilifu wa kazi ya miaka elfu mbili, akiifanya ili watu wote duniani wawe na njia sahihi ya kufuata na maisha ya amani na furaha. Hata hivyo, Mungu hawezi kuishi na mwanadamu duniani kwa muda mrefu, kwa maana Mungu ni Mungu, ni si kama mwanadamu kamwe. Hawezi kuishi urefu wa maisha ya mwanadamu wa kawaida, hiyo ina maana, Hawezi kuishi duniani kama mwanadamu ambaye si wa kawaida, kwa maana Yuko na sehemu ndogo ya ubinadamu wa kawaida wa mtu wa kawaida kumuwezesha kuishi vile. Kwa maneno mengine, Mungu anawezaje kuanzisha familia, kuwa na kazi na kulea watoto duniani? Je, si hii itakuwa ni aibu? Kwamba Yeye amejaliwa na ubinadamu wa kawaida ni kwa minajili tu ya kutekeleza kazi Yake kwa njia ya kawaida, na sio kumwezesha Yeye kuwa na familia na kazi kama mtu wa kawaida. Hisia Zake za kawaida, mawazo ya kawaida, na kula kwa kawaida na nguo za mwili Wake yanatosha kuthibitisha kuwa Yuko na ubinadamu wa kawaida; hakuna haja Yake kuwa na familia au kazi ili athibitishe kwamba Yeye kweli yuko na ubinadamu wa kawaida. Hiyo haina maana hata kidogo! Mungu anakuja duniani, kumaanisha Neno linageuka kuwa mwili; Kwa urahisi Anamruhusu mwanadamu kulielewa neno Lake na kuliona neno Lake, hiyo ni, kumruhusu mwanadamu kuona kazi inayotekelezwa na mwili. Nia Yake sio kwamba wanadamu wautendee mwili Wake kwa njia Fulani, bali kwamba mwanadamu awe mtiifu mpaka mwisho, kumaanisha, aweze kutii maneno yote yanayotoka katika kinywa Chake, na kunyenyekea na kukubali kazi yote Anayofanya. Yeye Anafanya kazi katika mwili tu; Haombi kwa makusudi mwanadamu kuinua ukuu na utakatifu wa mwili Wake, bali kumwonyesha mwanadamu hekima ya kazi Yake na mamlaka yote Aliyo nayo. Kwa hivyo, ingawa Anao ubinadamu wa kipekee, Hafanyi matangazo yoyote, na Anatilia tu maanani kazi ambayo Anapaswa kufanya. Mnapaswa kujua ni kwa nini Mungu Alipata mwili na ilhali hatangazi wala kushuhudia juu ya ubinadamu Wake wa kawaida, lakini badala yake Anatekeleza tu kazi ambayo Angependa kufanya. Hii ndio sababu mnaona tu uwepo wa uungu katika Mungu mwenye mwili, kwa sababu Hatangazi kuwa Kwake katika mwili ndio mwanadamu aige. Ni pale tu mwanadamu anapowaongoza watu ndipo anapozungumza jinsi alivyo kibinadamu, ndivyo apate heshima na utii wao vyema zaidi na hivyo kufanikisha uongozi wa wengine. Kinyume na hilo, Mungu huwashinda watu kupitia katika kazi Yake pekee (hiyo ni, kazi isiyoweza kufanywa na mwanadamu); hakuna shaka ya mwanadamu kuvutiwa na Yeye au kumfanya mwanadamu amwabudu. Yote Anayofanya ni kuweka tu katika mwanadamu hisia za uchaji Kwake au kumfanya mwanadamu aweze kujua kuhusu kutowezekana kwa kumchunguza Yeye. Hakuna haja ya Mungu kumpendeza mwanadamu. Kile anachohitaji ni kuwa wewe umheshimu na kumwabudu mara tu unaposhuhudia tabia Yake. Kazi ambayo Mungu hufanya ni Yake mwenyewe; haiwezi kufanywa na mwanadamu badala Yake, wala kuweza kutimizwa na mwanadamu. Ni Mungu Mwenyewe tu ndiye Anaweza kufanya kazi Yake mwenyewe na kuanzisha enzi mpya ili kumwongoza mwanadamu katika maisha mapya. Kazi ambayo Yeye hufanya ni kumwezesha mwanadamu kupokea maisha mapya na kuingia katika enzi mpya. Kazi nyingine yote hupokezwa kwa wale wanadamu wa ubinadamu wa kawaida na ambao wanapendwa na wengine. Kwa hivyo, katika Enzi ya Neema, Alikamilisha kazi ya miaka elfu mbili katika miaka mitatu na nusu tu kati ya miaka Yake thelathini na mitatu katika mwili. Mungu Anapokuja duniani kutekeleza kazi Yake, Yeye hukamilisha kazi ya miaka elfu mbili au ya enzi nzima ndani ya muda mfupi zaidi wa miaka michache. Yeye hachelewi, na Hasimami; Yeye hufupisha tu kazi ya miaka mingi ili ikamilishwe katika miaka michache tu mifupi. Hili ni kwa sababu kazi ambayo Yeye hufanya Mwenyewe ni kuifungua tu njia mpya na kuiongoza enzi mpya.

Iliyotangulia: Fumbo la Kupata Mwili (1)

Inayofuata: Fumbo la Kupata Mwili (3)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp