Wengi Wanaitwa, lakini Wachache Wanachaguliwa
Nimetafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Miongoni mwa wafuasi hawa wote, kuna wale wanaotumika kama makasisi, wale wanaoongoza, wale ambao ni wana wa Mungu, wale ambao ni watu wa Mungu, na wale wanaotoa huduma. Ninawaainisha kulingana na uaminifu wanaonionyesha Mimi. Wote watakapokuwa wameainishwa kulingana na aina zao, yaani, wakati asili ya kila aina ya mtu imefunuliwa, Nitampanga kila mmoja wao katika kundi lake linalostahili na kuweka kila aina katika mahali pake panapofaa, ili kufikia lengo Langu la kuwaokoa watu. Ninawaita wale Ninaotaka kuwaokoa kwenye nyumba Yangu kwa makundi, na kisha kuwafanya wote waikubali kazi Yangu ya siku za mwisho. Wakati huo huo, Ninawaainisha kulingana na aina, kisha kumtuza au kumwadhibu kila mtu kwa msingi wa matendo yake. Hizi ndizo hatua zinazojumuisha kazi Yangu.
Leo, Ninaishi duniani, na Ninaishi miongoni mwa wanadamu. Watu wanapitia kazi Yangu, na wananitazama Nikinena, na pamoja na hili Ninampa kila mmoja wa wafuasi Wangu ukweli wote, ili waweze kupokea uzima kutoka Kwangu na hivyo kupata njia ya kufuata. Kwa maana Mimi ni Mungu, Mtoaji wa uzima. Katika miaka Yangu mingi ya kazi, watu wamepata mengi, na kuacha mengi, lakini bado Ninasema kwamba hawaniamini kwa kweli. Kwa maana watu wanakiri tu kwamba Mimi ni Mungu kwa vinywa vyao, lakini hawakubaliani na ukweli Ninaouonyesha, na, zaidi ya hayo, hawatendi ukweli ambao Ninawataka watende. Yaani, watu wanakiri tu uwepo wa Mungu, lakini si uwepo wa ukweli; watu wanakiri tu uwepo wa Mungu, lakini si uwepo wa uzima; watu wanakiri tu jina la Mungu, lakini si kiini Chake. Ninawachukia kwa shauku yao, kwa kuwa wanatumia tu maneno yanayosikika vizuri kunidanganya Mimi, na hakuna hata mmoja wao anayeniabudu kwa moyo wa kweli. Maneno yenu yana kishawishi cha nyoka; na ni yenye kiburi kupindukia, tangazo la hakika la malaika mkuu. Zaidi ya hayo, matendo yenu yameraruka na kuchanika hadi kiwango cha aibu, na matamanio yenu ya kupita kiasi na nia zenu za kutamani vinachukiza masikioni. Ninyi nyote mmekuwa nondo katika nyumba Yangu, vitu vya kuchukiwa na Mimi. Kwa maana hakuna hata mmoja wenu anayependa ukweli; badala yake, mngependa kubarikiwa, kupaa mbinguni, kutazama maono makuu ya Kristo Akishika madaraka Yake duniani. Lakini, je, mmewahi kufikiria jinsi watu kama ninyi, mliotoka sana, msiojua kile Mungu alicho, mnaweza kustahili kumfuata Mungu? Mnawezaje kupaa mbinguni? Mnawezaje kustahili kutazama mandhari mazuri ya maono hayo makuu ambayo hayajawahi kushuhudiwa? Vinywa vyenu vimejaa maneno yanayonidanganya, maneno ya uchafu, ya kunisaliti, na maneno ya kiburi. Hamjawahi kuzungumza maneno ya unyofu Kwangu, wala maneno yaliyotakaswa, wala maneno ya kupitia neno Langu na kunitii. Mwishowe, imani yenu ikoje? Hakuna chochote isipokuwa tamaa na pesa katika mioyo yenu, na hakuna chochote isipokuwa vitu vya maada katika akili zenu. Kila siku, mnapiga hesabu jinsi ya kupata kitu kutoka Kwangu. Kila siku, mnahesabu ni utajiri kiasi gani na ni vitu vingapi vya maada ambavyo mmepata kutoka Kwangu. Kila siku, mnangojea baraka zaidi na zaidi zije kwenu ili mweze kufurahia vitu vingi zaidi, vya juu zaidi vinavyoweza kufurahiwa. Si Mimi niliye katika mawazo yenu kila wakati, wala ukweli unaotoka Kwangu, bali ni mume au mke wenu, watoto wenu, na vitu mnavyokula na kuvaa. Mnafikiria jinsi mnavyoweza kupata starehe bora zaidi, ya juu zaidi. Lakini hata mkijaza matumbo yenu hadi kupasuka, je, si ninyi bado ni maiti tu? Hata mkijipamba kwa mavazi mazuri kama hayo, je, ninyi bado si maiti zinazotembea zisizo na uhai? Mnamenyeka kwa ajili ya matumbo yenu, hadi kufikia hatua ambapo nywele zenu zinakuwa na mvi, lakini hakuna hata mmoja wenu anayetoa unywele mmoja kwa ajili ya kazi Yangu. Mnazunguka huku na kule daima, mkiichosha miili yenu na kupiga bongo zenu, kwa ajili ya miili yenu wenyewe, na kwa ajili ya wana na binti zenu—lakini hakuna hata mmoja wenu anayeonyesha wasiwasi au kujali nia Zangu. Ni nini ambacho bado mnatumainia kupata kutoka Kwangu?
Sina haraka kamwe Ninapofanya kazi. Haijalishi jinsi watu wanavyonifuata Mimi, Ninafanya kazi Yangu kulingana na hatua Zangu mwenyewe na mpango Wangu mwenyewe. Kwa hivyo, ingawa ninyi ni waasi sana dhidi Yangu, bado Ninafanya kazi bila kukoma, na bado Ninaendelea kunena maneno Ninayokusudia kunena. Ninawaita kwenye nyumba Yangu wale Niliowaamulia kimbele, ili waweze kuwa wasikilizaji wa maneno Yangu. Kisha, wale wote wanaotii maneno Yangu, wanaotamani maneno Yangu, Ninawaleta mbele ya kiti Changu cha enzi; wale wote wanaosaliti maneno Yangu, wasionisikia au kunitii, na kunipinga waziwazi, Ninawatupa upande mmoja ili wangojee adhabu yao ya mwisho. Watu wote wanaishi katikati ya upotovu na chini ya mkono wa yule mwovu, na hivyo si wengi kati ya wale wanaonifuata Mimi wanaotamani sana ukweli. Yaani, wengi hawaniabudu kwa kweli; hawaniabudu kwa ukweli, bali wanajaribu kupata imani Yangu kupitia upotovu na uasi, kwa njia za udanganyifu. Ni kwa sababu hii ndiyo Ninasema: Wengi wanaitwa, lakini wachache wanachaguliwa. Wale wanaoitwa wote wamepotoshwa sana na wote wanaishi katika enzi moja—lakini wale wanaochaguliwa ni sehemu moja tu yao, wao ni wale wanaoamini katika ukweli na kuukiri, na wanaotenda ukweli. Watu hawa ni sehemu ndogo sana tu ya wote, na kutoka miongoni mwao Nitapokea utukufu zaidi. Mkishapimwa kwa kulinganishwa na maneno haya, je, ninyi mnajua kama ninyi mmo miongoni mwa wale waliochaguliwa? Matokeo yenu yatakuwaje?
Kama Nilivyosema, wale wanaonifuata ni wengi lakini wale wanaonipenda kwa kweli ni wachache. Pengine wengine wanaweza kusema, "Je, ningelipa gharama nyingi hivi kama singekupenda Wewe? Je, ningefuata hadi hatua hii kama singekupenda Wewe?" Ni kweli, wewe una sababu nyingi, na upendo wako ni mkuu sana, lakini kiini cha upendo wako Kwangu kiko wapi? "Upendo," kama unavyoitwa, unarejelea hisia iliyo safi na isiyo na dosari, ambapo unatumia moyo wako kupenda, kuhisi, na kujali. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna shaka, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna miamala, na hakuna uchafu wa aina yoyote. Ukiwa na upendo, basi hutadanganya, wala kulalamika, wala kusaliti, wala kuasi, wala kudai, wala kutafuta kupata kitu au kupata kiasi fulani cha kitu. Ukiwa na upendo, basi utajitolea kwa furaha na kuteseka kwa furaha, utalingana na Mimi, na utaacha yote uliyo nayo kwa ajili Yangu, ukiiacha familia yako, matarajio yako, ujana wako, na ndoa yako. Ikiwa sivyo, upendo wako hautakuwa upendo hata kidogo, bali udanganyifu na usaliti! Upendo wako ni wa aina gani? Je, ni upendo wa kweli? Au wa uwongo? Umeacha kiasi gani? Umetoa kiasi gani? Nimepokea upendo kiasi gani kutoka kwako? Je, wewe unajua? Mioyo yenu imejaa uovu, usaliti, na udanganyifu—kwa hivyo, je, kuna uchafu kiasi gani katika upendo wenu? Ninyi mnafikiri kwamba tayari mmeacha vya kutosha kwa ajili Yangu; mnafikiri kwamba upendo wenu Kwangu tayari unatosha. Lakini basi kwa nini maneno na matendo yenu daima yana uasi na udanganyifu? Ninyi mnanifuata, lakini hamkiri neno Langu. Je, huu ni upendo? Ninyi mnanifuata, lakini kisha mnanikataa. Je, huu ni upendo? Ninyi mnanifuata, lakini mnanitilia Mimi shaka. Je, huu ni upendo? Ninyi mnanifuata Mimi, lakini hamwezi kukubali uwepo Wangu. Je, huu ni upendo? Ninyi mnanifuata, lakini hamnitendei kulingana na kile Nilicho, na mnafanya mambo kuwa magumu Kwangu kila wakati. Je, huu ni upendo? Ninyi mnanifuata, lakini mnajaribu kunipumbaza na kunidanganya katika kila jambo. Je, huu ni upendo? Ninyi mnanitumikia, lakini hamniogopi. Je, huu ni upendo? Ninyi mnanipinga katika kila namna na mambo yote. Je, kuna lolote kati ya haya ambalo ni upendo? Ninyi mmejitolea sana, ni kweli, lakini ninyi hamjawahi kutenda kile Ninachowataka ninyi mtende. Je, huu unaweza kuwa upendo? Hesabu makini inaonyesha kwamba ninyi hamna hata chembe ya upendo Kwangu. Baada ya miaka mingi sana ya kazi na maneno mengi sana ambayo Nimeyatoa, ninyi mmepata kiasi gani hasa? Je, hili halistahili kutafakariwa kwa makini? Ninawaonya ninyi: Wale Ninaowaita Kwangu si wale ambao hawajawahi kupotoshwa; badala yake, wale Ninaowachagua ni wale wanaonipenda Mimi kwa kweli. Kwa hivyo, ninyi lazima muwe waangalifu katika maneno na matendo yenu, na mchunguze nia na mawazo yenu ili yasivuke mipaka. Katika wakati wa siku za mwisho, fanyeni juu chini kutoa upendo wenu mbele Yangu, la sivyo ghadhabu Yangu haitaondoka kwenu kamwe!