Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu

Kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu, haiwezekani kwa dhuria ya Moabu kufanywa kuwa kamili, wala hawana sifa za kufanywa hivyo. Watoto wa Daudi, kwa upande mwingine, hakika wana tumaini, na kwa kweli wanaweza kufanywa kuwa kamili. Ikiwa mtu ni dhuria ya Moabu, hawezi kufanywa kuwa kamili. Hata sasa, ninyi bado hamjui umuhimu wa kazi inayofanywa miongoni mwenu; hata katika hatua hii, ninyi bado mnashikilia matarajio yenu ya baadaye mioyoni mwenu, na mnasita kuyaacha. Hakuna anayejali kwa nini leo Mungu amechagua tu kufanya kazi juu ya kundi la watu wasiostahili kabisa kama ninyi. Je, inaweza kuwa kwamba Yeye amefanya kosa katika kazi hii? Je, kazi hii ni kosa la muda? Kwa nini Mungu, ambaye daima amejua ninyi ni watoto wa Moabu, ameshuka hasa kufanya kazi miongoni mwenu? Je, hili haliwajii akilini kamwe? Je, Mungu hafikirii hili kamwe anapofanya kazi Yake? Je, Yeye hutenda kwa pupa? Je, Yeye hakujua tangu mwanzo kwamba ninyi ni dhuria ya Moabu? Je, ninyi hamjui kufikiria mambo haya? Fikira zenu zimeenda wapi? Je, kufikiri kwenu huko kuzuri kumevurugika? Werevu wenu na hekima yenu imeenda wapi? Je, ni kwamba ninyi mna tabia ya kuu sana kiasi kwamba hamtilii maanani mambo madogo kama haya? Akili zenu ni nyepesi sana kuhusiana na mambo kama vile matarajio yenu ya baadaye na majaliwa yenu wenyewe, lakini linapokuja suala la kitu kingine chochote, zimekufa ganzi, ni butu, na hazijui chochote kabisa. Ni nini hasa ambacho ninyi mnaamini? Je, ni matarajio yenu ya baadaye? Au Mungu? Je, si kile unachoamini ni hatima yako nzuri? Je, si ni matarajio yako ya baadaye? Umeelewa kiasi gani cha njia ya uzima? Je, umepata kiasi gani? Je, unafikiri kwamba kazi inayofanywa sasa kwa dhuria ya Moabu inafanywa ili kuwafedhehesha ninyi? Je, inafanywa kwa makusudi ili kufichua ubaya wenu? Je, inafanywa kwa makusudi ili kuwafanya ninyi mkubali kuadibu, na kisha kuwatupa ninyi katika ziwa la moto? Sikusema kwamba ninyi hamna matarajio ya baadaye, sembuse kwamba ninyi mnapaswa kuangamizwa au kuingia katika mateso ya milele. Je, nimetangaza mambo kama haya hadharani? Unasema huna tumaini, lakini, je, huu si uamuzi ambao wewe mwenyewe umepitisha? Je, hii si athari ya mtazamo wako mwenyewe? Je, maamuzi yako mwenyewe yanahesabika? Nikisema wewe hujabarikiwa, basi hakika wewe utakuwa mlengwa wa maangamizi; na Nikisema wewe umebarikiwa, basi hakika wewe hutaangamizwa. Ninasema tu kwamba wewe ni dhuria ya Moabu; Sikusema kwamba wewe utaangamizwa. Ni kwamba tu dhuria ya Moabu umelaaniwa, na ni aina moja ya wanadamu wapotovu. Dhambi ilitajwa hapo awali; je, ninyi nyote si wenye dhambi? Je, wenye dhambi wote hawajapotoshwa na Shetani? Je, wenye dhambi wote hawampingi na kumwasi Mungu? Je, wale wanaompinga Mungu hawapaswi kulaaniwa? Je, si wenye dhambi wote wanapasa kuangamizwa? Katika hali hiyo, ni nani miongoni mwa watu wa nyama na damu ambaye anaweza kuokolewa? Je, ninyi mngeweza kunusurika hadi leo? Ninyi mmekuwa hasi kwa sababu ninyi ni dhuria ya Moabu; je, ninyi pia hamhesabiki kama wanadamu, ambao ni wenye dhambi? Ninyi mmedumuje hadi leo? Utimilifu unapotajwa, ninyi mnakuwa na furaha, na mnaposikia kwamba mtapitia dhiki kuu, mnahisi kwamba hili linawafanya mbarikiwe hata zaidi. Mnafikiri kwamba kuwa washindi baada ya kutoka katika dhiki kutakuwa baraka kuu zaidi ya Mungu na kuinuliwa Kwake kukuu kwenu. Moabu anapotajwa, mfadhaiko huibuka miongoni mwenu; watu wazima na watoto vile vile huhisi huzuni isiyoelezeka na hamna furaha kabisa mioyoni mwenu, na ninyi mnajuta kuzaliwa. Ninyi hamwelewi umuhimu wa hatua hii ya kazi inayofanywa kwa dhuria ya Moabu; mnajua tu kufuatilia vyeo vya juu, na wakati wowote mnapotambua kwamba hakuna tumaini, mnarudi nyuma. Inapotajwa kufanywa kuwa watimilifu na hatima ya baadaye, ninyi mnahisi furaha. Ninyi mnamwamini Mungu ili kupata baraka na ili muweze kuwa na hatima nzuri. Watu wengine sasa wanahisi hofu kwa sababu ya hadhi yao. Kwa sababu wao ni wa thamani ya chini na hadhi ya chini, hawataki kutafuta kufanywa kuwa watimilifu. Kwanza, utimilifu ulizungumziwa, na kisha dhuria ya Moabu ikatajwa, kwa hivyo watu walikana njia ya kufanywa kuwa watimilifu iliyotajwa hapo awali. Hii ni kwa sababu kuanzia mwanzo hadi mwisho, ninyi hamjawahi kujua umuhimu wa kazi hii, wala ninyi hamjali kuhusu umuhimu wake. Ninyi ni wenye kimo kidogo sana, na hamwezi kustahimili hata vurugu ndogo zaidi. Mnapoona kwamba utambulisho wenu ni wa chini sana, mnakuwa hasi na kupoteza imani ya kuendelea kufuatilia. Watu huchukulia tu kupata neema na kufurahia amani kama ishara za imani, na wanaona ufuatiliaji wa baraka kama msingi wa imani yao katika Mungu. Watu wachache sana hutafuta kumjua Mungu au kutafuta mabadiliko katika tabia yao. Katika imani yao, watu hutafuta kumfanya Mungu awape hatima inayofaa na neema yote wanayotaka, kumfanya Yeye kuwa mtumishi wao, kumfanya Yeye adumishe uhusiano wa amani na wa kirafiki na wao ili kwamba, bila kujali ni wakati gani, kusiwe kamwe na mzozo wowote kati yao. Yaani, imani yao katika Mungu inadai kwamba Yeye aahidi kutimiza mahitaji yao yote na kuwapa chochote wanachoomba, kulingana na maneno ambayo wamesoma katika Biblia, "Nitasikiliza yote ambayo ninyi mnaomba." Wanamtaka Mungu asimhukumu au kumpogoa mtu yeyote, kwa maana Yeye daima amekuwa Mwokozi Yesu mwenye rehema ambaye hudumisha uhusiano mzuri na watu nyakati zote na mahali pote. Namna ambayo watu wanamwamini Mungu ni kama ifuatavyo: Wao hutoa madai kwa Mungu bila aibu, wakiamini kwamba iwe wao ni waasi au watiifu, Yeye anapaswa tu kuendelea kuwapa kila kitu. Wao huendelea tu "kukusanya madeni" kutoka kwa Mungu, wakiamini kwamba Yeye anapaswa "kuwalipa" bila upinzani wowote na, zaidi ya hayo, alipe maradufu. Wanafikiri, iwe Mungu amepata chochote kutoka kwao au la, Yeye anaweza tu kutawaliwa nao, na Yeye hawezi kuwapanga watu jinsi Apendavyo, sembuse kuwafunulia watu hekima Yake na tabia Yake yenye haki, ambavyo vimefichwa kwa miaka mingi, wakati wowote Anapotaka na bila ruhusa yao. Wao huungama tu dhambi zao kwa Mungu, wakiamini kwamba Yeye anapaswa tu kuwasamehe, bila kuwa kinyume na hilo, na kwamba hili litaendelea milele. Wao humwamuru Mungu tu, wakiamini kwamba Yeye anapaswa tu kuwatii, kwa sababu imeandikwa katika Biblia kwamba Mungu hakuja kuhudumiwa na wanadamu, bali kuwahudumia, na kwamba Yeye alikuja kuwa mtumishi wao. Hata sasa, je, si ninyi bado mnaamini kwa njia hii? Wakati wowote mnaposhindwa kupata kitu kutoka kwa Mungu, ninyi hutamani kutoroka; mnapokosa kuelewa kitu, mnakuwa wenye chuki sana, na hata kufikia hatua ya kumtupia Yeye matusi ya kila aina. Ninyi hamtamruhusu Mungu Mwenyewe aonyeshe kikamilifu hekima na maajabu Yake; badala yake, ninyi mnataka tu kufurahia raha na faraja ya muda. Hadi sasa, mtazamo wenu katika imani yenu kwa Mungu umejumuisha tu mitazamo ileile ya zamani. Mungu akiwaonyesha ninyi uadhama Wake kidogo tu, mnakosa furaha. Je, ninyi mnaona sasa kimo chenu ni kikubwa kiasi gani hasa? Msifikiri kwamba ninyi nyote ni waaminifu kwa Mungu wakati ambapo kwa kweli mitazamo yenu ya zamani haijabadilika. Wakati hakuna jambo linalokupata, wewe unaamini kwamba kila kitu kinaenda sawa, na upendo wako kwa Mungu unafikia kilele. Jambo dogo linapokutendekea, unaanguka chini Kuzimu. Je, huku ni kuwa mwaminifu kwa Mungu?

Hatua ya mwisho ya kazi ya ushindi ingeanzia Israeli, basi kazi kama hiyo ya ushindi haingekuwa na maana yoyote. Kazi hii ina umuhimu mkubwa zaidi inapofanywa Uchina, na inapofanywa kwenu ninyi watu. Ninyi ndio watu wa hali ya chini kabisa, watu walio na hadhi ya chini kabisa; ninyi ndio mlio katika kiwango cha chini kabisa cha jamii hii, na ninyi ndio mliomtambua Mungu kwa kiwango cha chini kabisa hapo mwanzo. Ninyi ndio watu ambao mmepotea mbali kabisa kutoka kwa Mungu na ambao mmedhuriwa vibaya kabisa. Kwa sababu hatua hii ya kazi ni kwa ajili ya ushindi tu, je, si inafaa kabisa ninyi kuchaguliwa ili kuwa na ushuhuda wa baadaye? Ikiwa hatua ya kwanza ya kazi ya ushindi haingefanywa kwenu ninyi watu, basi ingekuwa vigumu kuendeleza kazi ya ushindi inayokuja, kwa maana kazi ya ushindi itakayofuata itapata matokeo kulingana na ukweli wa kazi hii inayofanywa leo. Kazi ya sasa ya ushindi ni mwanzo tu wa kazi ya ushindi ya jumla. Ninyi ni kundi la kwanza kushindwa; ninyi ni wawakilishi wa binadamu wote watakaoshindwa. Watu ambao kwa kweli wana maarifa wataona kwamba kazi yote anayofanya Mungu leo ni kuu. Yeye hawaruhusu tu watu kujua uasi wao wenyewe, bali pia anafunua utambulisho wao. Kusudi na maana ya maneno Yake si kuwafanya watu wawe hasi, wala si kuwaangusha. Ni kwa ajili yao kupata nuru na wokovu kupitia maneno Yake; ni kuamsha roho zao kwa njia ya maneno Yake. Tangu kuumbwa kwa dunia, mwanadamu ameishi chini ya nguvu za Shetani, bila kujua wala kuamini kwamba kuna Mungu. Kwamba watu hawa wanaweza kupokea wokovu mkuu wa Mungu na kuinuliwa kukuu kwa kweli kunaonyesha upendo wa Mungu; wale wote ambao kwa kweli wana maarifa watafikiri kwa njia hii. Vipi kuhusu wale ambao hawana maarifa kama hayo? Watasema, "Ah, Mungu alisema sisi ni dhuria ya Moabu; Yeye alisema hili kwa maneno Yake Mwenyewe. Je, bado tunaweza kupata matokeo mazuri? Sisi ni dhuria ya Moabu, na tumempinga Yeye hapo zamani. Mungu amekuja kututia hatiani; je, huoni jinsi Yeye daima ametuhukumu, tangu mwanzo kabisa? Kwa kuwa tumempinga Mungu, hivi ndivyo tunavyopaswa kuadibiwa." Je, maneno haya ni sahihi? Leo Mungu anawahukumu ninyi, anawaadibu ninyi, na kuwatia hatiani ninyi, lakini unapaswa kujua kwamba lengo la kutiwa hatiani kwako ni ili ujijue. Yeye anatia hatiani, analaani, anahukumu, na anaadibu ili upate kujijua, ili tabia yako ipate kubadilika, na, hata zaidi ya hili, ili upate kujua thamani yako, na kuona kwamba matendo yote ya Mungu ni yenye haki na yanalingana na tabia Yake na mahitaji ya kazi Yake, kwamba Yeye anafanya kazi kulingana na mpango Wake kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na kwamba Yeye ni Mungu mwenye haki ambaye anampenda na kumwokoa mwanadamu, na ambaye anamhukumu na kumwadibu mwanadamu pia. Ikiwa unajua tu kwamba wewe ni wa hadhi ya chini, kwamba wewe ni mpotovu na mwasi, lakini hujui kwamba Mungu ana nia ya kufunua wokovu Wake kupitia hukumu na kuadibu anakokufanyia leo, basi huna njia ya kupitia mambo, sembuse kuwa na uwezo wa kuendelea mbele. Mungu hajakuja kuwapiga au kuwaangamiza watu, bali kuwahukumu, kuwalaani, kuwaadibu, na kuwaokoa. Hadi mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000 utakapofikia kikomo—kabla Yeye hajafunua matokeo ya kila kikundi cha mwanadamu—kazi ya Mungu duniani ni kwa ajili ya wokovu kikamilifu; madhumuni yake ni kuwafanya wale wanaompenda Yeye kuwa kamili kabisa na kuwaleta wajisalimishe chini ya utawala Wake. Haijalishi Mungu anawaokoaje watu, yote yanafanywa kwa kuwafanya wajitenge na asili yao ya zamani ya kishetani; yaani, Yeye anawaokoa kwa kuwafanya wafuatilie uzima. Wasipofanya hivyo, basi hawatakuwa na njia ya kukubali wokovu wa Mungu. Wokovu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, na ufuatiliaji wa uzima ni kitu ambacho mwanadamu lazima awe nacho ili kukubali wokovu. Machoni pa mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, hukumu, na laana; wokovu lazima uwe na rehema, wema, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, pamoja na baraka zisizo na mipaka zinazotolewa na Mungu. Watu wanaamini kwamba Mungu anapomwokoa mwanadamu, Yeye hufanya hivyo kwa kumgusa kwa baraka na neema Zake, ili aweze kumpa Mungu moyo wake. Yaani, kule kumgusa Kwake mwanadamu ndiko kumwokoa Kwake. Wokovu wa aina hii ni ya mabadilishano. Ni wakati tu Mungu anapompa mara mia ndipo mwanadamu atakuja kujisalimisha mbele ya jina la Mungu, na hivyo kumfanya Mungu ajivunie na kumletea sifa. Hii si nia ya Mungu kwa wanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi duniani ili kuwaokoa biadamu wapotovu; hakuna uongo katika hili. Isingekuwa hivi, hakika Yeye asingekuja kufanya kazi Yake Mwenyewe. Hapo zamani, njia Yake ya wokovu ilihusisha kuonyesha rehema na wema mkuu zaidi, kiasi kwamba Alitoa yote Aliyokuwa nayo kwa Shetani badala ya wanadamu wote. Sasa si kama zamani: Wokovu wenu leo unatokea wakati wa siku za mwisho, ambapo kila mmoja anaainishwa kulingana na aina yake; njia ya wokovu wenu si rehema au wema, bali kuadibu na hukumu, ili mwanadamu apate kuokolewa kikamilifu zaidi. Hivyo, yote mnayopokea ni kuadibu, hukumu, na kipigo kisicho na hisia, lakini jueni hili: Katika kipigo hiki kisicho na hisia hakuna adhabu hata kidogo. Haijalishi maneno Yangu yanaweza kuwa makali vipi, kile kinachowajia ni maneno machache tu ambayo yanaweza kuonekana kutokuwa na huruma kabisa kwenu, na haijalishi Ninaweza kuwa na hasira kiasi gani, kile kinachowajia bado ni maneno ya kushutumu, na Sina nia ya kuwadhuru au kuwaua. Je, haya yote si ukweli? Jueni kwamba siku hizi, iwe ni hukumu yenye haki au usafishaji na kuadibu kusiko na hisia, kila kitu ni kwa ajili ya wokovu. Bila kujali kama leo kila mmoja ataainishwa kulingana na watu wa aina zote watafunuliwa, madhumuni ya maneno na kazi yote ya Mungu ni kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kweli. Hukumu yenye haki inaletwa ili kumtakasa mwanadamu, na usafishaji usio na hisia unafanywa ili kumtakasa; maneno makali au kurudi, yote yanafanywa ili kutakasa na ni kwa ajili ya wokovu. Hivyo, mbinu ya leo ya wokovu ni tofauti na ile ya zamani. Leo, hukumu yenye haki inatumika kama wokovu wenu, na kama chombo kizuri cha kuwaainisha ninyi kila mmoja wenu kulingana na aina yake, na kuadibu kusiko na hisia kunatumika kama wokovu wenu mkuu. Mna nini cha kusema mbele ya kuadibu na hukumu kama hiyo? Je, hamjafurahia wokovu daima, kuanzia mwanzo hadi mwisho? Mmemwona Mungu mwenye mwili na kutambua uweza na hekima Yake; kwa kuongezea, mmepitia kupigwa na kutiwa adabu mara kwa mara. Hata hivyo, je, ninyi pia hamjapokea neema kuu? Je, baraka zenu si kubwa zaidi kuliko za mtu mwingine yeyote? Neema zenu ni nyingi hata kuliko utukufu na utajiri alioufurahia Sulemani! Fikirieni kuhusu hili: Kama nia Yangu ya kuja ilikuwa kuwatia hatiani na kuwaadhibu badala ya kuwaokoa, je, siku zenu zingeweza kudumu kwa muda mrefu hivyo? Je, ninyi viumbe wenye dhambi wa nyama na damu mngeweza kunusurika hadi leo? Kama lengo Langu lilikuwa tu kuwaadhibu, basi kwa nini Ningepata mwili na kuanza kazi kubwa kama hii? Je, kuwaadhibu ninyi watu duni hakungeweza kufanywa tu kwa kutamka neno moja? Je, bado Ningehitaji kuwaangamiza baada ya kuwatia hatiani kwa makusudi? Je, bado hamwamini haya maneno Yangu? Je, Ningeweza kumwokoa mwanadamu kupitia rehema na wema pekee? Au Ningeweza tu kutumia kusulubiwa ili kumwokoa mwanadamu? Je, tabia Yangu yenye haki haifai zaidi katika kumfanya mwanadamu awe mtiifu kabisa? Je, haina uwezo zaidi wa kumwokoa mwanadamu kikamilifu?

Ingawa maneno Yangu ni makali, yote ni wokovu kwa mwanadamu, kwa kuwa Ninasema maneno tu na Siuadhibu mwili wa mwanadamu. Maneno haya yanamfanya mwanadamu aishi katika nuru, ajue kwamba nuru ipo, ajue kwamba nuru ni ya thamani, na, hata zaidi, ajue jinsi maneno haya yalivyo ya manufaa kwake, na pia kujua kwamba Mungu ni wokovu. Ingawa Nimetamka maneno mengi ya kuadibu na hukumu, hakuna chochote ambacho kwa kweli kimewajia ninyi. Nimekuja hasa kufanya kazi Yangu na kunena maneno Yangu, na ingawa maneno Yangu ni makali, yananenwa katika hukumu ya upotovu wenu na uasi wenu. Kusudi la Mimi kufanya hili linabaki kuwa kumwokoa mwanadamu kutoka kwa nguvu za Shetani. Kusudi ni kutumia maneno Yangu kumwokoa mwanadamu; si kumdhuru mwanadamu kwa maneno Yangu. Maneno Yangu ni makali ili kupata matokeo katika kazi Yangu. Ni kupitia tu kazi kama hiyo ndiyo mwanadamu anaweza kuja kujijua na kujitenga na tabia yake ya uasi. Umuhimu mkuu zaidi wa kazi ya maneno ni kwamba inawawezesha watu kutia ukweli katika vitendo wanapouelewa, na hivyo kufikia mabadiliko katika tabia yao, na kupata maarifa kujihusu wao wenyewe na kuhusu kazi ya Mungu. Kufanya kazi kwa njia ya kunena maneno pekee ndiko kunaweza kuunganisha uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, na maneno pekee ndiyo yanaweza kueleza ukweli. Kufanya kazi kwa njia hii ndiyo mbinu bora zaidi ya kumshinda mwanadamu; mbali na matamko ya maneno, hakuna mbinu nyingine inayoweza kuwawezesha watu kuelewa ukweli na kazi ya Mungu kwa uwazi zaidi. Hivyo, katika hatua Yake ya mwisho ya kazi, Mungu anatumia mbinu ya kuzungumza na mwanadamu ili kumfungulia ukweli wote na mafumbo ambayo haelewi, akimruhusu kupata kutoka kwa Mungu njia ya kweli na uzima, na hivyo kuridhisha nia Zake. Madhumuni ya kazi ya Mungu kwa mwanadamu ni kumwezesha aridhishe nia za Mungu, na inafanywa ili kumwokoa. Kwa hivyo, wakati wa wokovu Wake kwa mwanadamu, Yeye hafanyi kazi ya kumwadhibu. Wakati akimwokoa mwanadamu, Mungu haadhibu maovu au kutuza mema, wala Hafunui hatima za kila aina ya watu. Badala yake, ni baada tu ya hatua ya mwisho ya kazi Yake kukamilika ndipo Atafanya kazi ya kuadhibu maovu na kutuza mema, na hapo tu ndipo Yeye atafunua matokeo ya watu wa kila aina. Wale wanaoadhibiwa watakuwa wale ambao kwa kweli hawawezi kuokolewa, huku wale ambao wanaokolewa watakuwa wale ambao wamepata wokovu wa Mungu wakati wa wokovu Wake kwa mwanadamu. Wakati akifanya kazi Yake ya wokovu, Mungu humwokoa kila mtu anayeweza kuokolewa kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo, na hamtupi yeyote kati yao, kwa maana madhumuni ya kazi ya Mungu ni kumwokoa mwanadamu. Wale wote ambao, wakati wa wokovu wa Mungu kwa mwanadamu, hawawezi kufikia mabadiliko katika tabia yao—pamoja na wale wote ambao hawawezi kumtii Mungu kikamilifu—watakuwa walengwa wa adhabu. Hatua hii ya kazi—kazi ya maneno—inawafungulia watu Neno lote ambalo hawaelewi, pamoja na mafumbo yote ambayo hayaeleweki kwao. Hili linawaruhusu waelewe nia za Mungu na matakwa ya Mungu kwao, na wawe na masharti ya kutia maneno ya Mungu katika vitendo na wafikie mabadiliko katika tabia yao. Mungu anatumia maneno tu kufanya kazi Yake na hawaadhibu watu kwa kuwa waasi kidogo. Hii ni kwa sababu sasa ndio wakati wa kazi ya wokovu, na kama watu wangeadhibiwa wakati wowote walipokuwa waasi, hakuna ambaye angekuwa na fursa ya kuokolewa, na kila mtu angeadhibiwa na kuanguka chini Kuzimu. Madhumuni ya kutumia maneno kumhukumu mwanadamu ni kumruhusu ajijue na amtii Mungu; si kumwadhibu kwa hukumu kama hiyo. Wakati wa kazi ya maneno, watu wengi watafichua uasi na upinzani wao, pamoja na ukosefu wao wa utii kwa Mungu mwenye mwili. Hata hivyo, Yeye hatawaadhibu watu hawa wote kutokana na hilo, lakini badala yake atawatupa kando tu wale ambao ni wapotovu hadi kwenye kiini na ambao hawawezi kuokolewa. Yeye atautoa mwili wao kwa Shetani, na, katika visa vichache, kuukomesha mwili wao. Wale waliosalia wataendelea kufuata na kupitia kupogolewa. Ikiwa, wakati wakifuata, watu hawa bado hawawezi kukubali kupogolewa, na wanazidi kuzorota zaidi na zaidi, basi watakuwa wamepoteza fursa yao ya wokovu. Kila mtu ambaye amekubali kushindwa na maneno ya Mungu atakuwa na fursa kadhaa za wokovu; katika wokovu wa Mungu kwa kila mtu Yeye atampa nafasi kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo. Kwa maneno mengine, wataonyeshwa uvumilivu mkuu zaidi. Maadamu watu wanageuka kutoka katika njia mbaya, na maadamu wanaweza kutubu, Mungu atawapa fursa za kupata wokovu Wake. Wanadamu wanapomwasi Mungu kwa mara ya kwanza, Yeye hana hamu ya kuwapiga; badala yake, Yeye hufanya kila awezalo ili kuwaokoa. Ikiwa mtu kwa kweli hana nafasi ya wokovu, basi Mungu atamtelekeza. Sababu ya Mungu kukawia kumwadhibu mtu ni kwamba Yeye anataka kumwokoa kila mtu anayeweza kuokolewa. Yeye anatumia tu maneno kuwahukumu, kuwatia nuru, na kuwaongoza watu; Yeye hatumii fimbo kuwapiga. Kutumia maneno kuwaletea wanadamu wokovu ndilo kusudi na umuhimu wa hatua ya mwisho ya kazi.

Iliyotangulia: Kuhusu Majina na Utambulisho

Inayofuata: Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp