Matamko ya Kristo Mwanzoni—Sura ya 103

Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami. Wale wasiosikiza kile Ninachosema na hawatendi maneno Yangu wanahukumiwa vikali na kupokea laana ya ghadhabu Yangu. Sauti Yangu ni hukumu na ghadhabu, nami si mpole kwa yeyote na simwonei mtu yeyote huruma, kwa kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki Mwenyewe, na Mimi ni mwenye ghadhabu, Nina kuchoma, utakaso, na maangamizo. Ndani Yangu, hakuna kitu kilichofichika, au chenye mhemuko, lakini badala yake, kila kitu kiko wazi, chenye haki, na kisicho na upendeleo. Kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza tayari wako nami katika kiti cha enzi, wakitawala mataifa yote na watu wote, yale mambo na watu walio dhalimu na waovu wanaanza kuhukumiwa. Nitawafanyia uchunguzi mmoja baada ya mwingine, bila kukosa kitu chochote, Nikiwafichua kabisa. Kwa kuwa hukumu Yangu imefichuliwa kikamilifu na imefunguliwa kikamilifu, na hakuna chochote ambacho kimebakizwa; Nitatupa chochote kisichokubaliana na mapenzi Yangu na kukisababisha kiangamie kuzimu milele; Nitakisababisha kiungue kuzimu milele. Hii ni haki Yangu; huu ni uaminifu Wangu. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha hili, na lazima kinitii.

Watu wengi hupuuza maneno Yangu na kufikiri maneno ni maneno tu na ukweli ni ukweli. Wao ni wajinga! Hawajui kwamba Mimi ni Mungu mwaminifu Mwenyewe? Maneno Yangu na ukweli hutokea sawia—si hii kwa hakika ni kweli? Watu hawaelewi maneno Yangu kabisa, na wale tu ambao wamepata nuru wanaweza kuelewa kweli—huu ni ukweli. Mara tu watu wanapoona maneno Yangu wanaogopa sana, wakijificha kila mahali, sembuse wakati hukumu Yangu inaposhuka. Nilipoumba vitu vyote, Ninapouharibu ulimwengu, na Ninapowakamilisha wazaliwa wa kwanza—mambo haya yote yanatimizwa kwa neno moja kutoka katika kinywa Changu. Hii ni kwa maana neno Langu lenyewe ni mamlaka; hilo nihukumu. Inaweza kusemwa kuwa mtu Niliye ni hukumu na uadhama; huu ni ukweli usiobadilika. Huu ni upande mmoja wa amri Zangu za utawala; njia moja Kwangu kuwahukumu watu. Machoni Pangu, watu wote, masuala yote, na vitu vyote—vitu vyote kabisa—viko mikononi Mwangu na viko chini ya hukumu Yangu, hakuna mtu na hakuna kitu chochote kinachothubutu kutenda bila mpango na kwa makusudi, na yote lazima yatimizwe kwa mujibu wa maneno Ninayonena. Kutoka katika mawazo ya binadamu kila mtu anaamini maneno ya mtu Niliye. Wakati Roho Wangu anatoa sauti, watu wanakuwa na wasiwasi. Hawajui kudura Yangu kabisa, nao wananisingizia. Ninakuambia! Yeyote anayeyatilia shaka maneno Yangu, yeyote anayeyadharau maneno Yangu, hawa ndio watakaoangamizwa, ni wana wa kudumu wa kuangamia kabisa. Kutokana na hili inaweza kuonekana kuwa kuna wachache sana ambao ni wazaliwa wa kwanza, kwa sababu hii ndiyo mbinu Yangu ya kufanya kazi. Kama Nilivyosema, Sijitahidi kufanya lolote, lakini badala yake Mimi hutumia maneno Yangu tu kutimiza kila kitu. Hii, basi, ndipo ambapo kudura Yangu huwa. Katika maneno Yangu hakuna mtu anayeweza kupata chanzo na madhumuni ya hotuba Yangu. Watu hawawezi kutimiza hili, na wanaweza tu kutenda kulingana na mwongozo Wangu, na wanaweza tu kufanya kila kitu kulingana na mapenzi Yangu kufuatana na haki Yangu, ili familia Yangu iwe na haki na amani, ikiishi milele, thabiti na imara milele.

Hukumu Yangu inamjia kila mtu, amri Zangu za utawala zinamgusa kila mtu, na maneno Yangu na nafsi Yangu vinafichuliwa kwa kila mtu. Huu ndio wakati wa kazi kuu ya Roho Wangu (wakati huu wale watakaobarikiwa na wale watakaopitia taabu wanabainishwa). Mara tu maneno Yangu yatakapotamkwa, Nimewabainisha wale watakaobarikiwa na wale watakaopitia taabu. Yote ni dhahiri nami Ninaweza kuyaona mara moja. (Yanasemwa kuhusu ubinadamu Wangu, kwa hiyo hayahitilafiani na majaaliwa na uteuzi Wangu.) Ninatembeatembea hapa na pale milimani na mito na vitu vyote, anga ya ulimwengu, Nikichunguza kila mahali na kutakasa kila mahali, ili yale maeneo yasiyo safi na zile nchi zilizochangamana zote zitakoma kuwepo nazo zitateketea kabisa kwa sababu ya maneno Yangu. Kwangu, kila kitu ni rahisi. Ikiwa wakati huu ungekuwa wakati ambao Niliamua kabla kuiangamiza dunia, Ningeimeza kwa neno moja, lakini sasa si wakati. Lazima kila kitu kiwe tayari kabla Yangu kufanya kazi hii, ili visiuvuruge mpango Wangu na kuingilia usimamizi Wangu. Ninajua jinsi ya kufanya hivyo kwa busara: Nina hekima Yangu nami Nina mpango Wangu wenyewe. Watu hawapaswi kufanya lolote—jihadhari usiuawe kwa mkono Wangu; tayari hii inagusa amri Zangu za utawala. Kutokana na hili mtu anaweza kuona ukali wa amri Zangu za utawala, na mtu anaweza kuona kanuni za amri Zangu za utawala, ikiwa ni pamoja na vipengele viwili: kwa upande mmoja Ninawaua wote wasiokubaliana na mapenzi Yangu na ambao wanazikosea amri Zangu za utawala; kwa upande mwingine, Nikiwa na ghadhabu Ninawalaani wote wanaozikosea amri Zangu za utawala. Vipengele hivi viwili ni muhimu navyo ni kanuni zenye mamlaka ya uamuzi za amri Zangu za utawala. Kila mtu hutendewa kulingana na kanuni hizi mbili, bila hisia, bila kujali jinsi watu walivyo waaminifu. Hii inatosha kuonyesha haki Yangu na inatosha kuonyesha uadhama Wangu na ghadhabu Yangu, ambayo itaviteketeza vitu vyote ya kidunia, vitu vyote vya kidunia, na vitu vyote ambavyo havikubaliani na mapenzi Yangu. Katika maneno Yangu kuna siri zilizofichwa, na katika maneno Yangu pia kuna siri zilizofichuliwa, hivyo katika dhana ya binadamu, katika akili ya binadamu, maneno Yangu hayaeleweki milele na moyo Wangu haueleweki milele. Kwa maneno mengine, lazima Niwaondolee wanadamu dhana na kufikiria kwao. Hiki ni kipengee muhimu zaidi cha mpango Wangu wa usimamizi. Lazima Nifanye hivi ili Niwapate wazaliwa Wangu wa kwanza na ili Niyakamilishe mambo ambayo Nataka kufanya.

Maafa ya dunia yanakua makubwa zaidi siku baada ya siku, na kati ya familia Yangu misiba mikuu inakuwa yenye nguvu hata zaidi. Kwa kweli watu hawana mahali pa kujificha nao wana aibu na hawawezi kuonyesha nyuso zao. Kwa sababu mpito ni sasa, hakuna mtu anayejua wapi atapitia hatua yake inayofuata. Itakuwa dhahiri tu baada ya hukumu Yangu. Kumbuka! Hizi ndizo hatua za kazi Yangu, na ndiyo njia ambayo kwayo Mimi hufanya kazi. Nitawaliwaza wazaliwa Wangu wa kwanza wote mmoja mmoja, na kuwatia moyo hatua baada ya hatua; na kwa watendaji huduma wote, Nitawaondosha na kuwatelekeza mmoja baada ya mwingine. Hii ni sehemu moja ya mpango Wangu wa usimamizi. Baada ya watendaji-huduma wote kufichuliwa, wazaliwa Wangu wa kwanza watafichuliwa pia. (Kwangu, jambo hili ni rahisi sana. Baada ya wao kusikia maneno Yangu, watendaji-huduma wote hao wataondoka polepole chini ya hukumu na tishio la maneno Yangu, na wale watakaobaki watakuwa tu wazaliwa Wangu wa kwanza. Hili si jambo la hiari nalo si jambo ambalo ridhaa ya mwanadamu inaweza kubadilisha, bali ni Roho Wangu anayefanya kazi binafsi.) Hili si tukio la mbali, nanyi mnapaswa kulielewa kwa kiasi fulani kutoka ndani ya awamu hii ya kazi Yangu na maneno Yangu. Halieleweki kwa watu kwa nini Niseme mengi sana na hayatabiriki. Ninawazungumzia wazaliwa Wangu wa kwanza kwa sauti ya faraja, huruma, na upendo (kwa sababu daima Mimi huwapa nuru watu hawa na Sitawaacha, kwa kuwa Nimewajaalia), huku Nikiwatendea kwa hukumu kali watu wengine isipokuwa wazaliwa Wangu wa kwanza, kwa vitisho, na kwa kuwaogofya, Nikiwafanya kuwa na hofu daima kiasi kwamba wamesisimka daima. Wakati hali inapoendelea hadi kiwango fulani, basi watakimbia kutoka katika hali hii (Nitakapoiangamiza dunia, watu hawa watakuwa katika kuzimu), lakini hawatawahi kuepuka mkono Wangu wa hukumu, na hawataepuka hali hii kamwe. Hii, basi, ni hukumu yao; huku ndiko kuadibu kwao. Siku ambayo wageni watawasili Nitawafichua watu hawa mmoja baada ya mwingine. Hii ni hatua katika kazi Yangu. Sasa mnaelewa kwa nini Nilinena maneno hayo hapo awali? Kwa maoni Yangu jambo ambalo halijakamilishwa pia ni jambo ambalo limekamilishwa, lakini jambo lililokamilishwa si lazima liwe jambo ambalo limetimizwa, kwa sababu Nina hekima Yangu, nami Nina njia Yangu ya kufanya kazi, ambayo haieleweki kwa wanadamu kabisa. Wakati Nimepata matokeo katika hatua hii (wakati Nimewafichua wabaya wote wanaonipinga Mimi), kisha Nitaanza hatua inayofuata, kwa sababu mapenzi Yangu hayapingwi na hakuna mtu anayethubutu kuuzuia mpango Wangu wa usimamizi na hakuna kitu kinachothubutu kuweka vikwazo—wanapaswa kuondoka wanipishe! Wana wa joka kubwa nyekundu, sikilizeni! Nilitoka Sayuni na kuwa mwili katika ulimwengu ili Niwapate wazaliwa Wangu wa kwanza, ili Nimdhalilishe baba yenu (hii inazilenga dhuria za joka kubwa nyekundu), ili kuwaunga mkono wazaliwa Wangu wa kwanza, na kusahihisha makosa waliyotendewa wazaliwa Wangu wa kwanza. Kwa hiyo msiwe wakatili tena; Nitawafanya wazaliwa Wangu wa kwanza wawashughulikie. Wakati uliopita wana Wangu walidhulumiwa na kukandamizwa, na kwa kuwa Baba hushika madaraka kwa ajili ya wana, wana Wangu watarudi katika kumbatio Langu la upendo, wasidhulumiwe na kukandamizwa tena. Mimi si dhalimu; hii inaonyesha haki Yangu, na kwa kweli ni "kuwapendwa Ninaowapenda na kuwachukia Ninaowachukia." Ikiwa mnasema Mimi ni mdhalimu, mnapaswa kuondoka haraka. Msiwe wapujufu na kudoea katika familia Yangu. Unapaswa kurudi nyumbani kwako haraka ili Nisilazimike kukuona tena. Kuzimu ni hatima yenu napo ni mahali ambapo ninyi hupumzika. Mkiwa katika familia Yangu hakutakuwa na nafasi kwa ajili yenu kwa sababu ninyi ni wanyama wa kuchukua mizigo, ninyi ndizo zana ambazo Natumia. Nisipowatumia Nitawatupa ndani ya moto ili Niwateketeze. Hii ni amri Yangu ya utawala; lazima Niifanye hivi, na hii tu inaonyesha jinsi Ninavyofanya kazi na inaonyesha haki Yangu na uadhama Wangu. La muhimu zaidi ni kwamba njia hii pekee ndiyo inaweza kuwawezesha wazaliwa Wangu wa kwanza kutawala pamoja nami katika mamlaka.

Iliyotangulia: Matamko ya Kristo Mwanzoni—Sura ya 88

Inayofuata: Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima—Sura ya 4

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp