Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho Chaguzi

Yaliyomo

Tamko La Kumi

Enzi ya Ufalme ni, baada ya yote, tofauti na nyakati za kale. Haihusu kile anachofanya mwanadamu. Badala yake, Mimi binafsi hutekeleza kazi Yangu baada ya kushuka duniani—kazi ambayo wanadamu hawawezi kuelewa wala kukamilisha. Tangu kuumbwa kwa ulimwengu mpaka leo, hii miaka yote daima imehusu kujenga kanisa, lakini hakuna mtu kamwe husikia kuhusu kujenga ufalme. Japokuwa Nazungumza kuhusu haya kwa kinywa Changu mwenyewe, yupo ambaye anajua asili yake? Wakati mmoja Nilishuka kwenye ulimwengu wa binadamu Nikashuhudia na Nikayaona mateso yao lakini bila ya kutimiza lengo la kupata mwili Kwangu. Wakati ujenzi wa ufalme unapoendelea, Mimi Niliyepata mwili huanza rasmi kufanya huduma; hiyo ni, Mfalme wa ufalme rasmi Anachukua uwezo wa mamlaka Yake ya ukuu. Kutokana na hili, ni dhahiri kwamba asili ya ufalme katika ulimwengu wa binadamu, mbali na kuwa tu suala la maneno na kuonekana, ni moja ya ukweli halisi. Hii ni maana mojawapo ya kipengele hiki “uhalisi wa kutenda.” Mwanadamu hajawahi kuona hata mojawapo ya matendo Yangu, hajawahi kusikia hata mojawapo ya matamshi Yangu. Hata kama angekuwa ameona, yeye angegundua nini? Na kama angenisikia nikiongea, yeye angeelewa nini? Duniani kote, ubinadamu wote hukaa chini ya upendo Wangu, huruma Yangu, lakini pia ubinadamu wote hukaa chini ya hukumu Yangu, na vivyo hivyo chini ya majaribu Yangu. Nimekuwa mwenye huruma na upendo kwa mwanadamu, hata wakati watu wote walikuwa wamepotoshwa kwa kiwango fulani; Nimekuwa Nikitoa kuadibu kwa watu, hata wakati watu wote walinyenyekea mbele ya kiti Changu. Lakini, yupo binadamu yeyote ambaye hayuko katikati ya mateso na usafishaji Niliotuma? Ni watu wangapi wanapapasa kwenye giza kutafuta mwangaza, ni wangapi wanajitahidi kwa uchungu kwa njia ya majaribio yao? Ayubu alikuwa na imani, na kwa hivyo, kwa hayo yote, hakuwa anajitafutia njia yake mwenyewe? Nyinyi kama watu Wangu, ingawa mnaweza kusimama imara katika majaribio, kunaye yule, bila kuongea kwa sauti, anaamini katika moyo wake? Je, si anaona ni afadhali kuongea kuhusu imani yake ilhali anaishuku moyoni mwake? Hakuna binadamu ambaye amesimama imara katika majaribio, yule anayetoa utiifu wa kweli katika majaribio. Kama Singefunika uso Wangu ili kuepuka kuangalia dunia hii, uanadamu mzima ungeporomoka chini ya macho Yangu ya kuchoma, kwa maana Siulizi chochote kutoka kwa ubinadamu.

Wakati saluti kwa ufalme inapolia—ambayo pia ni wakati sauti saba za radi zinanguruma—sauti hii inatetemesha mbingu na dunia, kutetemesha mbingu na kusababisha mishipa ya moyo wa kila binadamu kutetemeka. Wimbo wa taifa kwa ufalme unainuka kwa shangwe juu ya taifa la joka kuu jekundu, kuthibitisha kwamba Nimeliangamiza taifa la joka kuu jekundu na kuanzisha ufalme Wangu. Hata la muhimu zaidi, ufalme Wangu unaimarishwa duniani. Wakati huu, Ninatuma malaika Wangu kwa kila mtu wa mataifa ya dunia ili waweze kuwachunga wanangu, watu Wangu; hii pia ni kukidhi mahitaji ya hatua ya pili ya kazi Yangu. Lakini Mimi binafsi Naenda mahali joka kuu jekundu limelala likiwa limejikunja, Nipigane nalo. Na wakati ubinadamu wote unapata kunijua Mimi kutoka ndani ya mwili, na kuwa na uwezo wa kuyaona matendo Yangu kutoka ndani ya mwili, kisha makazi ya joka kuu jekundu yatageuzwa kuwa jivu na kuteketea yasipatikane tena. Kama watu wa ufalme Wangu, kwa kuwa mnalichukia joka kuu jekundu katika mifupa yenu, ni lazima muuridhishe moyo Wangu na matendo yenu na kwa njia hii muweze kuleta aibu juu ya joka. Je, mnahisi kwamba joka kuu jekundu ni lenye chuki? Je, mnahisi kweli kwamba yeye ndiye adui wa Mfalme wa ufalme? Je, mna imani kwamba mnaweza kuwa na ushuhuda wa ajabu Kwangu? Je, mna imani ya kumshinda joka? Haya ndiyo Ninayotaka kutoka kwenu. Yote Ninayohitaji kutoka kwenu ni kwamba muweze kufika mpaka hatua hii; je, mtaweza kufanya hili? Je, mna imani kwamba mnaweza kufikia hili? Ni nini binadamu ana uwezo wa kufanya? Si ni afadhali Nifanye hivyo Mwenyewe? Mbona Ninasema kwamba Mimi binafsi Nateremka mahali ambapo vita hujiunga? Kile ambacho Nataka ni imani yenu, si vitendo vyako. Wanadamu hawana uwezo wa kupokea maneno Yangu kwa njia ya moja kwa moja, lakini wanachungulia tu kutoka kando. Na nyinyi mmefikia malengo haya kwa njia hii? Mmekuja kunijua kwa njia hii? Kwa kusema ukweli, binadamu wa ulimwengu, hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuniangalia Mimi moja kwa moja katika uso Wangu, hakuna mmoja aliye na uwezo wa kupokea usafi na maana nadhifu ya maneno Yangu. Na pia Nimeweka mwendo wa kufaa usiokuwa wa kawaida wa uhandisi juu ya dunia, ili kufikia lengo Langu na kuanzisha mfano wa kweli Wangu mwenyewe katika mioyo ya watu, na katika njia hii kutamatisha kipindi cha wakati fikira huwa na mamlaka juu ya wanadamu.

Leo hii, Sishuki tu juu ya taifa la joka kuu jekundu, Mimi pia Nageuza uso Wangu kuelekea ulimwengu mzima, mpaka kila kitu cha mbingu kinatetemeka. Kunayo sehemu hata moja isiyopitia hukumu Yangu? Kunayo sehemu isiyo chini ya mijeledi Ninayocharaza kuelekea chini? Kila Ninapoenda Nimesambaza “mbegu za majanga” ya kila aina. Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na ni bila shaka kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo. Nataka kufanya hata watu zaidi wapate kunijua Mimi, waweze kuniona Mimi, na kwa njia hii wapate kumwogopa Mungu ambaye wao hawajamwona kwa miaka mingi lakini ambaye, leo hii, ni halisi. Ni kwa sababu gani Niliumba hii dunia? Kwa sababu gani, wakati mwanadamu alipogeuka na kuwa mpotovu, Sikuweza kumwangamiza kabisa? Kwa sababu gani wanadamu wanaishi chini kwa mipigo? Ni kwa sababu gani Mimi Mwenyewe niliuvaa mwili? Wakati Mimi Nafanya kazi Yangu, ubinadamu haujui tu ladha ya uchungu bali pia utamu. Kati ya watu wa dunia, ni nani asiyeishi ndani ya neema Yangu? Je, Sikuwapa wanadamu baraka na mali, ambayo wataweza kujifurahisha na kujitosheleza katika ulimwengu? Hakika, kuwaruhusu kuchukua nafasi kama watu Wangu si baraka pekee niliyowapa, sivyo? Na kama msingekuwa watu Wangu na badala yake muwe wajakazi, hamngekuwa mnaishi ndani ya baraka Zangu? Hapana mmoja kati yenu anayeweza kuelewa mahali maneno Yangu hutoka. Ubinadamu—mbali na kuthamini majina ambayo Nimeweka juu yenu, wengi wenu, mnapoitwa “watenda-huduma,” wanauguza chuki katika nyoyo zenu, na wengi, wakiitwa “watu Wangu,” huzalisha upendo katika nyoyo zenu. Usijaribu kunidanganya—macho Yangu huona na kupenya kila mahali! Ni nani kati yenu hupokea kwa hiari, ni nani kati yenu hunipa heshima kamilifu? Iwapo saluti kwa ufalme haingelia, je mngeweza kutii mpaka mwisho? Kile ambacho mwanadamu ana uwezo wa kufanya, kufikiria, anaweza kwenda umbali gani—haya yote Nimeyapangia tangu kitambo.

Idadi kubwa ya watu hukubali moto Wangu katika mwanga wa uso Wangu. Idadi kubwa ya watu, wakitiwa moyo na kutumainisha Kwangu, hujiamsha wenyewe kusonga mbele katika kufuata. Wakati majeshi ya Shetani hushambulia watu Wangu, Mimi Niko pale kuwafukuzilia mbali; wakati mipango ya Shetani inaleta madhara katika maisha ya watu Wangu, Nampiga akimbie kwa kujiuzulu, na asiweze kurudi tena. Duniani, kila aina ya pepo wabaya wana wasiwasi wa kutafuta mahali pa kupumzika, na bila kusita wanatafuta maiti za watu wazile. Watu Wangu! Lazima mbaki ndani ya huduma Yangu na ulinzi. Kamwe usiwahi kuishi katika hali ya upotovu! Msiwahi tenda mambo kiholela! Badala yake, salimisha uaminifu wako katika nyumba Yangu, na ni kwa uaminifu tu ndio unaweza kupinga hila ya Shetani. Katika hali yoyote, usiishi kama ilivyokuwa katika siku za awali, kufanya jambo moja mbele Yangu na jingine nyuma Yangu—ukifanya hivyo umeshapita kiwango cha kukombolewa. Hakika Nimetamka vya kutosha maneno ya aina hii, sivyo? Ni kwa sababu asili ya mwanadamu ni isiyorekebika ndiyo maana Nimerudia na kumkumbusha haya. Usichoke na kupoteza uchangamfu! Haya yote Niyasemayo ni kwa mujibu wa kuhakikisha hatima yenu! Kile Shetani anahitaji kwa hakika ni uchafu na pahali pabaya; na zaidi mnavyokosa matumaini, na zaidi upotovu wenu unavyozidi, mnavyozidi kukataa kujiwasilisha kwa hali ya kujizuia, ndivyo roho wachafu watakavyojiwasilisha katika nafasi yoyote ya kupenyeza. Mara mnapowasili katika hii nafasi, uaminifu wenu utakuwa kelele tupu, bila ukweli wowote, na azimio lenu kuliwa na pepo wachafu, na kugeuzwa kuwa uasi au hila ya Shetani na kutumiwa kuzuia kazi Yangu. Papo hapo Nitawapiga mpaka ufe wakati wowote na popote Nitakavyotaka. Hakuna mtu anayejua uzito wa hali hii; wote wanachukulia mambo wanayosikia kuwa hali ya maneno matupu na hawachukui tahadhari kwa lolote. Sikumbuki kile kilichofanywa katika siku za nyuma. Je, bado unasubiri Mimi niwe mpole kwako Nisahau kwa mara nyingine tena? Ingawa ubinadamu unanipinga Mimi, Sitashikilia lolote dhidi yake, kwa maana kimo cha mwanadamu ni kidogo mno, na hivyo Sina mahitaji makubwa kwake. Yote Ninayotaka ni kwamba yeye asijitumie mwenyewe kwa ubadhirifu na kujiwasilisha kwa kujizuia. Hakika si zaidi ya uwezo wenu kufikia hitaji hili moja? Wengi wa watu wanasubiri Nifichue mafumbo zaidi ili walishe macho yao. Ilhali, iwapo utakuja kuelewa maajabu yote ya mbinguni, je, ni nini utakalofanya na hayo maarifa? Je, yataweza kuongeza upendo wako Kwangu? Je, yatachochea upendo wako Kwangu? Mimi Siwezi kumdharau mwanadamu, wala kukata kauli kwa wepesi juu yake. Isipokuwa kwa ukweli, Mimi kamwe Sitawahi kuweka kitambulisho chenye maelezo juu ya kichwa cha mwanadamu ili avae kama taji. Fikiria kuhusu siku za nyuma: Kumekuwepo na nyakati zozote ambazo Nimewahi kuwatukana nyinyi? Wakati wowote ambao Niliwadharau nyinyi? Wakati wowote ambao Nimewachunga bila ya kuzingatia mazingira yenu? Wakati wowote ambao Nilichosema kilishindwa kujaza nyoyo zenu na vinywa vyenu na kusadikisha kabisa? Wakati wowote ambao Nimenena bila ya kuwa na sauti ya undani ndani yenu? Ni nani kati yenu ambaye amesoma maneno Yangu bila hofu na kutetemeka, kwa undani akiwa na hofu kwamba Nitampiga chini kumwingiza kwenye shimo lisilo na kina? Ni nani asiyeweza kuvumilia majaribio ndani ya maneno Yangu? Ndani ya maneno Yangu kuna mamlaka, lakini hii si kwa kupitisha hukumu ya kawaida juu ya mtu; Badala yake, kwa kujali hali halisi ya mwanadamu, daima Nimeiweka wazi kwa mwanadamu maana inayoyahusisha maneno Yangu. Katika hatua ya uhakika, yupo aliye na uwezo wa kutambua nguvu za milele katika maneno Yangu? Yupo ambaye anaweza kupokea ndani ya nafsi yake dhahabu safi ambayo maneno Yangu yanaundwa nayo? Nimezungumza maneno mangapi, lakini kuna yeyote ambaye amewahi kuyathamini?

Machi 3, 1992