Sura ya 52

Ninatokea kama Jua la haki, na nyinyi pamoja na Mimi tunashiriki utukufu na baraka nzuri, milele na milele! Huu ni ukweli thabiti, na tayari umeanza kutimizwa kwenu. Kwa yote ambayo Nimewaahidi, Nitawatimizia; yote Nisemayo ni ya kweli, na hayatarudi tupu. Baraka hizi nzuri ziko juu yenu, hakuna yeyote mwingine anayeweza kuzidai; ni matunda ya utumishi wenu kwa kukubaliana na Mimi kwa maafikiano. Zitupilie mbali dhana zenu za kidini; yaamini maneno Yangu kuwa ya kweli na msiwe wenye shaka! Mimi sifanyi utani na nyinyi, Namaanisha Ninayoyasema; wale ambao Nawakirimu baraka ndio wanaozipokea; wale ambao Siwapi baraka hawazipokei; hili linaamuliwa na Mimi. Baraka nzuri ya kidunia ni nini? Kwa mtazamo Wangu si kitu ila kinyesi cha mnyama, yenye thamani chini ya senti. Kwa hivyo msizithamini sana starehe za kidunia; si kufurahia baraka za mbinguni na Mimi ni ya maana zaidi, kitu cha thawabu zaidi?

Awali ukweli haukuwa umefunuliwa, na Mimi Sikuwa Nimeonekana waziwazi; nyinyi mlinishuku Mimi na hamkuthubutu kuwa wenye uhakika kunihusu. Hata hivyo, sasa mambo yote yamefunuliwa, na Nimejitokeza kama Jua la haki; kama bado mko katika shaka, mnasema nini kuhusu hilo? Wakati giza lilipofunika dunia, ya kwamba hamkuweza kuuona mwanga iliweza kusamehewa, lakini sasa jua limeangaza pembe zote zenye giza; yaliyofichwa hayajafichika tena, yaliyosetiriwa hayajasetiriwa tena; kama bado mko na shaka, basi Sitawasamehe kwa urahisi! Sasa ni wakati wa kuwa na uhakika kabisa kunihusu, wakati wa kuwa tayari kujitolea Kwangu na kugharimika kwa ajili Yangu. Yeyote anayenipinga kwa njia yoyote ndogo ile atashambuliwa mara moja kwa mioto ya hukumu bila kuwaza tena au kusita. Kwani sasa ni wakati ambao hukumu isiyo na huruma imefika; kwa wale ambao fikra na mioyo yao si minyofu, kutakuwa na hukumu ya papo hapo; hii ndiyo maana ya kweli ya “Kazi Yangu ni kama umeme unaomulika” kama ilivyozungumziwa.

Inaendelea haraka; haina budi ila kuwashangaza watu, haina budi ila kuwafanya watu wahisi woga, haiwezi kucheleweshwa tena na haiwezi kusimamishwa. Kadiri kazi Yangu inavyozidi kutekelezwa, ndivyo inavyosonga mbele kwa kasi; asiyekuwa macho na kujiandaa daima hubeba hatari ya kutupwa kando; usijaribu tena kujaribu moyoni mwako. Kazi Yangu imeanza kikamilifu, ikienea kwa Mataifa na ulimwengu dunia. Mioto ya hukumu ni katili na bila huruma au upendo kwa mtu yeyote. Wale ambao ni waaminifu kwa Mungu lakini bado wako na fikra na mawazo yasiyo sahihi, au hata wanapinga kidogo, watahukumiwa bila shaka. Yeyote ambaye mwanga Wangu unamwangazia ataishi ndani ya mwanga, na kutenda katika mwanga, na kunitumikia hadi mwisho wa barabara. Wale ambao hawaishi katika mwanga wanaishi gizani. Nitafanya uamuzi baada ya kuwahukumu, kulingana na msimamo wao kuhusu hatia yao.

Siku Yangu imefika, Siku Yangu iliyotajwa awali sasa iko mbele ya macho yenu, kwa kuwa nyinyi mnashuka pamoja na Mimi. Mimi na nyinyi, nyinyi na Mimi, tumekutana angani, tukishiriki utukufu pamoja. Siku Yangu kwa kweli imefika kabisa!

Iliyotangulia: Sura ya 51

Inayofuata: Sura ya 53

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp