Sura ya 53
Mimi ndiye mwanzo, na Mimi ndiye mwisho. Mimi ndiye Mungu mmoja wa kweli aliyefufuka na kamili. Ninazungumza maneno Yangu mbele yenu, na lazima msadiki kabisa Ninachosema. Mbingu na dunia zinaweza kupita lakini hakuna herufi moja au nukta moja ya kile ninachosema kitawahi kupita. Kumbuka hili! Kumbuka hili! Punde ambapo Nimezungumza, hakuna neno lililowahi kurudishwa na kila neno litatimizwa. Sasa wakati umefika na lazima muingie haraka katika uhalisi. Hakuna muda mwingi. Nitawaongoza wana Wangu katika ufalme mtukufu na kile ambacho mmekipigania na kukitamani kitatimia. Wanangu! Inukeni upesi mnifuate! Tayari hakuna muda sasa wa ninyi kuwa mnafikiria juu yake. Muda uliopotezwa hautarudi kamwe, baada ya giza kuna nuru, na unyakuzi uko mbele ya macho yako. Je, mnaelewa? Fungueni macho yenu! Amkeni upesi! Hamruhusiwi sasa katika kuwasiliana miongoni mwenu kushiriki katika kupiga domo au kusema chochote kisicho cha maana katika ujenzi wa kanisa, kilicho cha muhimu ni kuwaruzuku ndugu na uzoefu wako wa utendaji au jinsi unavyoangazwa mbele ya Mungu na kujijua; yeyote anayeweza kutoa hili atakuwa na kimo! Sasa watu wengine hawaogopi, na bila kujali kile Ninachosema au kiasi gani Ninachokuwa na wasiwasi, bado hauogopi; nafsi yako nzee haijiruhusu kuguswa, kwa hivyo unaweza kuendelea kwa njia hii! Ona ni nani atakayeangamizwa! Daima unafikiri kuhusu kuishika dunia, ukitamani sana utajiri, na kuhisi uhusiano wa karibu sana na wana wako wa kike, wa kiume na mume wako. Haya, unaweza kuendelea kuhisi uhusiano wa karibu! Sio kwamba maneno Yangu hayajazungumzwa kwenu, na mnaweza kuendelea jinsi mnavyotaka! Katika siku za usoni za karibu mtaelewa kila kitu, lakini mtakuwa mmechelewa sana tayari na yote yanayowangoja ni hukumu.