Sura ya 37

Kwa kweli hamna imani mbele Yangu na mara kwa mara mnajitegemea wenyewe kufanya mambo. “Hamuwezi kufanya chochote bila Mimi!” Lakini nyinyi watu wapotovu daima mnachukua maneno Yangu ndani ya sikio moja na linatokea nje ya lile nyingine. Maisha siku hizi ni maisha ya maneno; bila maneno hakuna maisha, hakuna uzoefu, wala hakuna imani. Imani iko katika maneno; ni kwa kuegemea zaidi ndani ya maneno ya Mungu ndio mnaweza kuwa na kila kitu. Msihangaike kuhusu kutokomaa; maisha huja kupitia kwa ukuaji, sio kupitia kuhangaika.

Daima nyinyi ni wepesi wa kuwa na wasiwasi na hamsikizi maagizo Yangu. Daima mnataka kuzidi mwendo Wangu. Hilo linahusu nini? Ni tamaa ya makuu yasiyostaarabika ya watu. Mnapaswa kutofautisha wazi kile kinachokuja kutoka kwa Mungu na kile kinachotoka kwenu. Shauku haitasifiwa kamwe mbele Yangu. Ninataka muwe na uwezo wa kunifuata kwa dhati hadi mwisho kuanzia mwanzo. Lakini mnaamini kwamba kutenda hili ni kujitolea kwa Mungu. Wanadamu vipofu! Mbona msije mbele Yangu zaidi na kutafuta? Mbona mnatenda tu bila kufikiri? Lazima muone kwa wazi! Bila shaka sio mtu ambaye anafanya kazi sasa, lakini badala yake ni Mkuu wa yote, Mungu mmoja wa kweli—Mwenye uweza! Ni lazima msipuuze, bali daima mshikilie kila kitu mlicho nacho, kwa sababu siku Yangu i karibu. Je, bado hamwamki wakati huu? Je, bado hamuoni wazi? Bado mnaandamana na dunia na hamuwezi kujitenganisha nayo. Kwa nini? Je, kweli mnanipenda? Je, mnaweza kufichua wazi mioyo yenu Kwangu ili Niione? Je, mna uwezo wa kujitoa kikamilifu Kwangu?

Fikiria kuhusu maneno Yangu zaidi, na daima muwe na ufahamu dhahiri kuyahusu. Msiwe wa kuvurugwa na kuchanganyikiwa au kuwa wa shingo upande. Tumia muda zaidi mbele Yangu, pokea maneno Yangu yaliotakaswa zaidi, na msielewe visivyo nia Yangu. Ni nini zaidi Ninaweza kusema kwenu? Mioyo ya watu ni ngumu na fikira za watu ni nzito mno. Daima wao hufikiri kupita tu kunatosha, na wao daima hufanyia utani maisha yao. Watoto wajinga! Sio mapema, sio muda wa kucheza tu. Mnapaswa kuyafungwa macho yenu na kutazama wakati. Jua li karibu kuvuka upeo wa macho na kuangaza dunia. Fungua macho yenu na muangalie kwa uangalifu, msiwe wazembe.

Mnachukua jambo kubwa kama hili kwa wepesi na kulichukulia hivi! Moyo Wangu una wasiwasi, lakini kunao wachache ambao hufikiria kuhusu moyo Wangu na wana uwezo wa kusikia shawishi Zangu nzuri na kusikiliza ushauri Wangu! Huu ujumbe ni mgumu, lakini kunao wachache kati yenu nyinyi ambao wanaweza kushiriki sehemu ya mzigo kwa ajili Yangu, bado mna msimamo huu. Ingawa mmeendelea kiasi ikilinganishwa na hapo zamani, hampaswi kubaki katika hali hii! Nyayo Zangu zinasonga mbele kwa kasi, lakini bado mko kwa aina hii ya mwendo. Mnawezaje kwenda kwa mwendo sawa na nuru ya leo na kwenda kwa mwendo sawa na hatua Zangu? Msisite tena. Nimewasisitizia nyinyi tena na tena, siku Yangu haitacheleweshwa tena!

Nuru ya leo hata hivyo ni ya leo. Haiwezi kulinganishwa na nuru ya jana na haiwezi kulinganishwa na nuru ya kesho. Ufunuo mpya, nuru mpya inazidi nguvu kila siku na inang’aa zaidi kila siku. Jiondoeni kutoka kwa kutunduwaa kwenu, msiwe wajinga tena, msiwe wenye kushikilia ukale tena, msicheleweshe wakati Wangu tena wala msipoteze muda Wangu bure.

Tazama! Tazama! Niombeni Mimi zaidi, tumia muda zaidi mbele Yangu, na bila shaka mtapata kila kitu! Amini kwamba kwa njia hii bila shaka mtapata kila kitu!

Iliyotangulia: Sura ya 36

Inayofuata: Sura ya 38

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp