Sura ya 31

Tabia ya Mungu hujumuishwa katika matamko yote ya Mungu, lakini wazo kuu la maneno Yake ni kufichua uasi wa wanadamu wote na kufunua mambo kama kutotii, kuasi, utovu wa haki, udhalimu, na kutoweza kumpenda Mungu kweli. Ni kiasi kwamba, maneno ya Mungu yamefikia kiwango ambacho Yeye husema kwamba kila kinyweleo katika miili ya watu kina upingaji kwa Mungu, kwamba hata kapilari zao zina ukinzani kwa Mungu. Ikiwa watu hawatajaribu kuchunguza hili, wao daima watakuwa wasioweza kuyajua, na hawataweza kamwe kuyaweka kando. Ambayo ni kusema, virusi vya upingaji wa Mungu vitaenea ndani yao na hatimaye, itakuwa kana kwamba seli zao nyeupe za damu zimezila seli zao nyekundu za damu, zikiacha mwili wao wote bila seli nyekundu za damu; mwishowe, watakufa kutokana na lukemia. Hii ndiyo hali halisi ya mtu, na hakuna yeyote anayeweza kuikana. Kwa kuzaliwa kwenye eneo ambamo joka kuu jekundu hulala likiwa limejikunja, kuna angalau kitu kimoja ndani yaa kila mtu kinachoonyesha na ni mfano wa sumu ya joka kuu jekundu. Hivyo, katika hatua hii ya kazi, wazo kuu katika maneno yote ya Mungu limekuwa ni kujijua mwenyewe, kujikana mwenyewe, kujiacha mwenyewe, na kujiua mwenyewe. Yaweza kusemwa kuwa hii ni kazi ya msingi ya Mungu katika siku za mwisho, na kuwa duru hii ya kazi ndiyo pana zaidi na kamilifu kupita zote—ambayo inaonyesha kuwa Mungu anapanga kuhitimisha hii. Hakuna yeyote aliyetarajia hili, lakini pia ni kitu ambacho wamekitarajia katika hisi zao. Ijapokuwa Mungu hakusema hivyo kwa wazi sana, hisi za watu ni kali sana—wao daima huhisi muda ni mfupi. Naweza kusema kuwa kadri mtu anavyohisi hivi, ndivyo anavyokuwa na ufahamu wazi zaidi wa enzi. Si kwa kuona ulimwengu kama kawaida na hivyo kuyapinga maneno ya Mungu; bali, ni kujua maudhui ya kazi ya Mungu kupitia kwa njia ambayo kwayo Mungu hufanya kazi. Hii inaamuliwa na sauti ya matamshi ya Mungu. Kuna siri kutokana na sauti na matamshi ya Mungu ambayo hakuna yeyote amegundua na pia hasa ni iliyo ngumu sana kwa watu kuingia ndani yake. Kiini cha kwa nini watu hawawezi kuelewa maneno ya Mungu ni kuwa bado hawajui sauti ambayo Mungu huzungumzia—na kama wataimudu siri hii, wataweza kuwa na ujuzi fulani wa maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu daima yamefuata kanuni moja: kuwafanya watu kujua kuwa maneno ya Mungu ni kila kitu, na kutatua matatizo yote ya mwanadamu kupitia kwa maneno ya Mungu. Kwa mtazamo wa Roho, Mungu huweka wazi matendo Yake, kwa mtazamo wa mwanadamu, Anafunua dhana za watu, kwa mtazamo wa Roho, Anasema mwanadamu si mzingatifu wa mapenzi Yake, na kwa mtazamo wa mwanadamu, Anasema Ameonja ladha tamu, chachu, chungu, na mbaya ya uzoefu wa binadamu, na Anakuja katika upepo na kuenda na mvua, kwamba Amepitia mateso ya jamii, na Amepitia milima na mabonde ya maisha. Haya ni maneno yanayosemwa kutoka kwa mitazamo tofauti. Anaponena kwa watu wa Mungu, ni kama msimamizi wa nyumba akiwakaripia watumwa, au kama kichekesho kifupi; maneno Yake huwaacha watu wameaibika, bila mahali pa kujificha kutokana na aibu, ni kana kwamba wamezuiliwa na mamlaka ya kikabaila ili kukiri chini ya mateso makali. Wakati Anapozungumza na watu wa Mungu, Mungu hazuiliki kama wanafunzi wa chuo kikuu wanaolalamika wakifichua kashfa ndani ya serikali kuu. Iwapo maneno yote ya Mungu yangekuwa yanadhihaki, yangekuwa magumu zaidi kwa watu kuyakubali; hivyo, maneno ambayo hunenwa na Mungu ni halisi, hayana maandishi ya kimafumbo kwa mtu, lakini yanaonyesha hali halisi ya mtu moja kwa moja—ambayo inaonyesha kwamba upendo wa Mungu kwa mwanadamu sio maneno tu, bali ni kweli. Ingawa watu huthamini uhalisi, hakuna kitu chochote halisi kuhusu upendo wao kwa Mungu. Hii ndiyo inayokosekana kwa mwanadamu. Ikiwa upendo wa watu kwa Mungu si wa kweli, basi ukamilifu wa kila kitu utakuwa mtupu na wa uongo, kana kwamba wote ungetoweka kwa ajili ya hili. Ikiwa upendo wao kwa Mungu unazidi ulimwengu wote, basi pia hali yao na utambulisho, na hata maneno haya, yatakuwa halisi, na sio tupu—unaona hili? Je, umeona matakwa ya Mungu kwa mwanadamu? Mtu hapaswi tu kufurahia baraka za cheo, lakini kuishi kwa kudhihirisha ukweli wa cheo. Hili ndilo Mungu anataka kutoka kwa watu wa Mungu, na kwa binadamu wote, na sio nadharia kubwa iliyo tupu.

Kwa nini Mungu anasema maneno ya aina hii: “kana kwamba yote Nifanyayo ni jaribio la kuwafurahisha, kutokana na hilo wao daima huchukizwa na matendo Yangu”? Je, unaweza kuzungumza juu ya maonyesho halisi ya mwanadamu kumchukia sana Mungu? Katika dhana za watu, mwanadamu na Mungu “wanapendana kwa shauku,” na leo, hamu ya watu kwa maneno ya Mungu imefikia kiwango cha kuwa wao hutamani kwa hamu kummeza Mungu kwa funda moja—lakini Mungu anasema aina ya maneno yafuatayo: “Mtu hunidharau Mimi. Kwa nini upendo wangu umelipwa na chuki ya mwanadamu?” Je, hii sio amana ya madini ndani ya watu? Je, hii sio inayopasa kuchimbuliwa? Hii ndiyo kasoro ya ukimbizaji wa watu, ni suala kubwa ambalo linapaswa kutatuliwa, na ni simba ambaye husimama kwa njia ya ujuzi wa mwanadamu juu ya Mungu na ambayo inapaswa kuondolewa kwa mwanadamu—je, hili sio linalopaswa kufanyika? Kwa sababu, kama nguruwe, mtu hana kumbukumbu, na daima hutamani raha, Mungu humpa mtu dawa ya usahaulifu—Anazungumza zaidi, anasema zaidi, na Anawakamata watu kwa masikio na kuwafanya wasikize kwa makini, na kuwavisha vifaa vya kusikizia. Kuhusu baadhi ya maneno Yake, kusema mara moja tu hakuwezi kutatua tatizo; yanapaswa kusemwa tena na tena, kwa maana “watu daima husumbuliwa na usahaulifu katika maisha yao, na siku za maisha ya wanadamu wote ziko katika mchafukoge.” Kwa njia hii, watu wanaweza kuokolewa kutoka kwa hali ambayo kwayo “wanasoma wakati wanapokuwa na wakati, wanasikiliza wakiwa hawana kazi, na kuyaacha wakati hawana muda; ikiwa maneno yanasemwa leo, wanayazingatia, lakini watayapuuza, ikiwa hayatasemwa kesho.” Kadri asili ya watu inavyohusika, kama leo Mungu angezungumza juu ya hali yao ya kweli na wapate ujuzi wake kamili, basi wangejawa na majuto—lakini baadaye, wangerejelea njia zao za zamani, wakitahadhari maneno ya Mungu na kurudia yale hapo juu wakati wanapokumbushwa. Hivyo, wakati unapofanya kazi au kuzungumza, usisahau kiini hiki cha mwanadamu; ingekuwa ni kosa kutelekeza kiini hiki wakati wa kufanya kazi. Katika kufanya kazi yote, hasa ni muhimu kuzungumza kwa kuzingatia dhana za watu. Hasa, unapaswa kuongeza ufahamu wako mwenyewe kwa maneno ya Mungu na kuyawasilisha Hii ndiyo njia ya kuwapa watu na kuwaruhusu wajijue wenyewe. Katika kutoa kwa watu kwa kutegemea maudhui ya maneno ya Mungu, kwa hakika itawezekana kuelewa hali yao halisi. Katika maneno ya Mungu, inatosha kuelewa hali halisi ya mwanadamu na hivyo kuwapa—na kwa hivyo, Sitasema zaidi juu ya maneno ya Mungu kuonyesha kuwa “Mungu alikubali mwaliko wa kukaa katika meza ya karamu duniani.”

Iliyotangulia: Sura ya 30

Inayofuata: Sura ya 32

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp