Mbona Huna Hiari ya Kuwa Foili?
Wale ambao wanashindwa ni foili[a], na ni baada tu ya kukamilishwa ndipo watu huwa vielelezo na mifano ya kazi ya siku za mwisho. Kabla ya kukamilishwa wao ni foili, vifaa, pamoja na vyombo vya huduma. Wale ambao wameshindwa kabisa na Mungu ndio dhihirisho la kazi Yake ya usimamizi, na vile vile mifano na vielelezo. Maneno haya ambayo nimetumia kuwaeleza watu kama hawa yanaweza kutokuwa ya kifahari, lakini yanafichua hadithi nyingi zenye kuvutia. Ninyi wenye imani ndogo mtabishana daima juu ya jina lisilokuwa lakifahari mpaka nyuso zenu zibadilike na kuwa nyekundu, na wakati mwingine hata mahusiano yanaharibika kama matokeo. Ingawa ni jina dogo tu, katika fikira zenu na katika imani yenu, hili si jina ambalo ni la umuhimu kabisa, bali ni jambo muhimu linalohusu majaliwa yenu. Basi, wale ambao hawana busara mara nyingi watapata hasara kubwa juu ya jambo dogo kama hili—huku ni kuokoa kidogo tu, na kisha kupoteza kingi. Kwa sababu tu ya jina lisilo na maana, mtatoroka na kamwe hamtarudi. Hii ni kwa sababu mnaona maisha kama hayana maana na mnaweka thamani kubwa sana juu ya majina mnayoitwa. Hivyo katika maisha yenu ya kiroho, na hata katika maisha yenu ya vitendo, mara nyingi mtakuza hadithi nyingi zilizo ngumu kueleweka na ambazo ni za ajabu kwa sababu ya dhana zenu kuhusu hadhi. Labda hamtakubali jambo hili, lakini Nitawaambia kwamba watu kama hawa kweli wapo katika maisha halisi, ingawa bado hamjafunuliwa mmoja mmoja. Mambo ya aina hii yamefanyika katika maisha ya kila mmoja wenu. Kama huamini hilo, tazama tu nakshi iliyo chini kutoka kwa maisha ya dada (au ya kaka). Inawezekana kwamba mtu huyo kwa kweli ni wewe, au pengine ni mtu mnayefahamiana katika maisha yako. Kama Sikosei, nakshi hii inaelezea uzoefu ambao umekuwa nao. Hakuna kitu kinachokosa katika maelezo, hakuna fikira au wazo hata moja limeachwa nje, lakini yote yamerekodiwa kwa ukamilifu katika hadithi hii. Kama huamini jambo hilo, hebu isome tu kwanza.
Huu ni uzoefu mmoja mdogo kutoka kwa “mtu wa kiroho.”
Alihisi wasiwasi alipoona kwamba mambo mengi ambayo ndugu kanisani walifanya hayakuwa sambamba na mapenzi ya Mungu, hivyo alianza kuwakaripia, akisema: “Ninyi vitu viovu! Je, hamna dhamiri hata kidogo? Mbona mnafanya vitu visivyo vya busara? Mbona msiutafute ukweli badala ya kufanya chochote mpendacho? … Ni ni nyinyi ndio ninaowaambia mambo haya, lakini wakati huo huo ni mimi mwenyewe ninayejichukia. Ninaona kwamba Mungu hawezi kuvumilia kabisa na ninahisi moto ndani yangu. Kweli niko tayari kutekeleza kazi ambayo Mungu ameaminia kwangu kwa ukamilifu na kweli ninataka niwatumikie. Ni kwamba tu sasa hivi mimi ni mnyonge sana. Mungu ametumia muda mwingi sana kwetu na Amenena maneno mengi sana, lakini bado tuko vivyo hivyo. Moyoni mwangu, daima nahisi kwamba bado nina deni kubwa sana….” (Alianza kulia, asiweze kuendelea kuzungumza.) Kisha, akaanza kuomba: “Ee Mungu! Nakuomba unipe nguvu na uniguse zaidi ya vile ambavyo Umefanya awali, na Roho Wako aweze kufanya kazi ndani yangu. Niko tayari kushirikiana na Wewe. Mradi hatimaye Upate utukufu, niko tayari sasa kujitolea Kwako kabisa, hata kama inamaanisha ni lazima nife. Tunataka kutoa sifa kubwa, ili ndugu zetu waweze kuimba na kucheza kwa furaha kulisifu jina Lako takatifu, kukutukuza, kukudhihirisha, kubaini kwamba kazi Yako ni ya kweli na kukujali Wewe kabisa kwa ajili ya mizigo Unayobeba….” Kwa ari aliomba kwa namna hii, na kweli Roho Mtakatifu alimpa mzigo. Kwa kipindi hiki, alibebeshwa mzigo sana, na alitumia siku nzima kusoma, kuandika, na kusikiliza. Alijishughulisha iwezekanavyo. Hali yake ya kiroho ilikuwa bora sana, na daima moyoni, alikuwa mwenye nguvu na wa kusumbuka. Mara kwa mara alidhoofika na kushindwa kuendelea, lakini kabla ya muda mrefu alirejesha tena hali yake ya kawaida. Baada ya kipindi cha muda kama huu, kuendelea kwake kulikuwa kwa kasi, aliweza kupata uelewa kiasi wa maneno mengi ya Mungu, naye pia alijifunza kwa wepesi nyimbo za kidini—kwa jumla, hali yake ya kiroho ilikuwa bora sana. Alipoona kwamba mambo mengi kanisani hayakukubaliana na mapenzi ya Mungu, alipata wasiwasi na kuwashutumu ndugu zake, akisema: “Je, huu ni upendo kwa jukumu lenu? Mbona hamwezi hata kulipa gharama ndogo kama hii? Kama hamtaki kulifanya, nitafanya….”
Alipokuwa akibeba mzigo, alihisi thabiti zaidi katika imani yake Roho Mtakatifu alivyofanya kazi zaidi. Mara kwa mara angekabiliwa na matatizo kiasi na kuwa hasi, lakini aliweza kuyashinda haya. Yaani, alipopitia kazi ya Roho Mtakatifu, hata wakati hali yake ilikuwa nzuri sana, hangeweza kuepuka kukumbana na matatizo fulani au kudhoofika kwa namna fulani. Vitu kama hivyo hufanyika bila kuepukika, lakini kabla ya muda mrefu aliweza kutoka kwa hali hizo. Alipopitia udhaifu, angeomba na angehisi kwamba kimo chake mwenyewe kweli kilikuwa na upungufu, lakini alikuwa tayari kushirikiana na Mungu. Haidhuru kile Mungu alichofanya, alikuwa tayari kuridhisha mapenzi Yake na kutii mipango Yake yote. Kulikuwa na baadhi ya watu ambao walikuwa na maoni fulani na chuki bila sababu kwake, lakini aliweza kujiweka kando upande mmoja na kwa vitendo kushiriki katika ushirika nao. Hivi ndivyo hali za watu ziko wakati ambapo Roho Mtakatifu anatekeleza kazi Yake ya kawaida. Baada ya muda fulani, kazi ya Mungu ilianza kubadilika, na watu wote waliingia katika hatua nyingine ya kazi ambapo Mungu alikuwa na mahitaji tofauti kwao. Hivyo kulikuwa na maneno mapya yaliyonenwa yaliyoleta mahitaji mapya kwa watu: “… Nina chuki kwenu tu, kamwe si baraka. Sijawahi kuwa na fikira ya kuwabariki kamwe, wala Sijawahi kuwa na fikira ya kuwafanya kamili kwani ninyi ni waasi sana. Kwa sababu nyinyi si waaminifu na ni wadanganyifu, na kwa sababu mnakosa ubora wa tabia na nyinyi ni wa hadhi ya chini, kamwe hamjawahi kuwa karibu na macho Yangu au katika moyo Wangu. Kazi Yangu inafanywa kwa kusudi la kuwahukumu tu; mkono Wangu kamwe haujawahi kuwa mbali nanyi, wala kuadibu Kwangu. Nimeendelea kuwahukumu na kuwalaani. Kwa sababu hamna ufahamu Wangu, ghadhabu Yangu daima imekuwa juu yenu. Ingawa daima Nimefanya kazi miongoni mwenu, mnapaswa kujua mtazamo Wangu kuwaelekea. Si chochote ila maudhi—hakuna mtazamo au maoni mengine. Ninataka tu mtende kama foili kwa ajili ya hekima Yangu na uwezo Wangu mkubwa. Nyinyi si kitu zaidi ya foili Wangu kwa sababu haki Yangu inafichuliwa kupitia uasi wenu. Ninawataka mtende kama foili kwa ajili ya kazi Yangu, kuwa viambatisho vya kazi Yangu….” Mara tu alipoona maneno, “viambatisho” na “foili,” alianza kufikiri: “Napaswa kufuataje kwa mujibu wa maneno haya? Baada ya kulipa gharama kama hiyo, mimi bado ni foili. Je, foili si mtendaji-huduma tu? Hapo zamani ilisemekana kwamba hatungekuwa watendaji huduma, kwamba tungekuwa watu wa Mungu, ilhali si bado sisi tuko hap oleo katika wajiby wa watendaji huduma? Je, si watendaji huduma hawana uzima? Haijalishi navumilia mateso kiasi gani, Mungu hatanisifu kwa ajili ya jambo hili! Baada ya mimi kumaliza kuwa foili, mambo hayatakuwa yamekamilika? …” Alipofikiri zaidi kuhusu jambo hilo, ndivyo alivyokuwa mwenye huzuni zaidi. Alihisi hata vibaya zaidi alipokuja kanisani na kuona hali za ndugu zake: “Nyinyi hamko sawa! Mimi siko sawa! Nimekuwa hasi. Wai! Ni kipi kinaweza kufanywa? Mungu bado hatutaki. Katika kufanya kazi ya aina hii, hakuna namna hatatufanya hasi. Sijui ni nini kibaya na mimi. Sitaki hata kuomba. Hata hivyo, siko sawa sasa hivi na kweli sina nguvu ndani yangu. Nimeomba mara nyingi lakini bado siwezi, na siko tayari kuendelea. Hivi ndivyo ninavyoona jambo hili. Mungu anasema kwamba sisi ni foili, hivyo, je, si foili ni watendaji huduma tu? Mungu anasema kwamba sisi ni foili, si wana Wake, na sisi si watu Wake, pia. Sisi si wana Wake, sembuse wana Wake wazaliwa wa kwanza. Sisi si chochote, bali ni foili tu. Kama hilo ndilo tulilo nalo, je, tunaweza kuwa na matokeo yenye kufaa? Foili hawana matumaini kwa sababu hawana maisha. Kama tungekuwa wana Wake, watu Wake, basi kungekuwa na matumaini katika jambo hilo—tungefanywa kamili. Je, foili wanaweza kuwa na uzima wa Mungu? Je, Mungu anaweza kuweka uhai ndani ya wale ambao hufanya huduma kwa ajili Yake? Wale Anaowapenda ni wale ambao wana uzima Wake, na wale tu walio na uzima Wake ni wana Wake, watu Wake. Ingawa mimi ni hasi na dhaifu, natumaini kwamba nyinyi nyote si hasi. Ninajua kwamba kuwa mwenye kusalia nyuma na kuwa hasi namna hii hakuwezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, lakini siko tayari kuwa foili. Ninahofia kuwa foili. Vyovyote vile, nina nguvu kiasi fulani tu, na siwezi kuendelea sasa. Ninatumaini kwamba hakuna yeyote kati yenu atakayefanya jinsi nilivyofanya, lakini atapata kiasi fulani cha msukumo kutoka kwangu. Nahisi kwamba ni heri niende nife! Nitawaacha na maneno fulani ya mwisho kabla nikutane na mauti yangu—ninatumaini kwamba mnaweza kutenda kama foili hadi mwisho; labda hatimaye Mungu atawasifu foili….” Ndugu walipoona hili, walishangaa: “Ni jinsi gani anaweza kuwa hasi hivyo? Je, hajakuwa sawa kabisa katika siku kadhaa zilizopita? Mbona amepoteza ari yake ghafla? Je, mbona yeye si wa kawaida?” Alisema: “Usiseme mimi siwi kawaida. Kwa kweli, nina uhakika kuhusu kila kitu moyoni mwangu. Ninajua kwamba sijayaridhisha mapenzi ya Mungu, lakini, je, si hilo ni kwa sababu tu siko tayari kutenda kama foili Yake? Mimi sijafanya jambo lolote baya. Labda siku moja Mungu atabadili jina la ‘foili’ liwe ‘viumbe,’ na si hivyo tu, ila viumbe Wake ambao wanatumika naye kwa njia muhimu. Je, si kunayo matumaini kiasi katika jambo hili? Ninatumaini kwamba hamtakuwa hasi ama kuvunjika moyo, na mnaweza kuendelea kumfuata Mungu na kufanya kila muwezalo kutumika kama foili. Hata hivyo, siwezi kuendelea. Msiache matendo yangu yawawekee mipaka.” Watu wengine walisikia hayo, na wakasema, “Hata ukiacha kumfuata Yeye, tutaendelea, kwani Mungu hajawahi kututendea bila haki. Hatutazuiwa na uhasi wako.”
Baada ya kupitia tukio hili kwa kipindi cha muda, yeye bado alikuwa katika hali hasi juu ya kuwa foili, hivyo Nilimwambia: “Wewe huna ufahamu wa kazi Yangu. Huna ufahamu wa ukweli wa ndani, asili, au matokeo yaliyokusudiwa ya maneno Yangu. Hujui malengo ya kazi Yangu, wala hekima yake. Huna ufahamu wa mapenzi Yangu. Unajua tu kurudi nyuma kwa sababu wewe ni foili—unajishughulisha sana na hadhi! Wewe ni mpumbavu uliyeje! Hapo zamani Nimesema mengi sana kwako. Nimesema kuwa Nitakufanya mkamilifu; jje, umesahau? Je, sikuzungumza kuhusu kukamilishwa kabla ya kuzungumza kuhusu foili?” “Subiri, hebu nifikirie kulihusu. Ndiyo, hiyo ni sahihi! Ulisema mambo hayo kabla uliwahi kuzungumza kuhusu foili!” “Nilipozungumza kuhusu kukamilishwa, je, Sikusema kwamba ni baada tu ya watu kushindwa ndiyo wangekamilishwa?” “Ndiyo!” “Je, maneno Yangu hayakuwa ya kweli? Je, hayakusemwa kwa nia njema?” “Ndiyo! Wewe ni Mungu ambaye hajawahi kusema kitu chochote cha udanganyifu—hakuna yeyote anayeweza kuthubutu kukana jambo hili. Lakini mnazungumza kwa njia nyingi sana tofauti.” “Je, njia Zangu za kuzungumza hazibadiliki kulingana na hatua tofauti za kazi? Je, maneno Ninayoyasema hayafanywi na kusemwa kulingana na mahitaji yako?” “Wewe hufanya kazi kulingana na mahitaji ya watu na Wewe huwapa kile wanachohitaji. Jambo hili si la uwongo!” “Je, basi mambo ambayo Nimekwambia hayajakuwa yenye manufaa? Je, kuadibu Kwangu hakujatekelezwa kwa ajili yako?” “Je, bado unawezaje kusema kwamba ni kwa ajili yangu mwenyewe! Umeniadibu hadi karibu nife—sitaki kuishi zaidi. Leo Unasema hili, kesho Unasema lile. Ninajua kwamba Wewe kunikamilisha ni kwa ajili yangu mwenyewe, lakini hujanikamilisha—Wewe unanifanya foili na bado unaniadibu. Unanichukia, sivyo? Hakuna yeyote anayethubutu kuamini maneno Yako, na ni sasa tu Nimeona dhahiri kwamba kuadibu Kwako ni ili kutatua tu chuki iliyo katika moyo Wako, si ili kuniokoa. Awali ulinificha ukweli; Ulisema ungenikamilisha na kwamba kuadibu kulikuwa kwa ajili ya kunikamilisha. Hivyo daima nimetii kuadibu Kwako; sikuwahi kufikiri kwamba leo ningebeba jina la foili. Mungu, je, haingekuwa bora zaidi kama Ungenitaka nitende kama kitu kingine chochote? Ni lazima unishurutishe kufanya wajibu wa foili? Hata ninaweza kukubali kuwa bawabu katika ufalme. Nimekuwa nikikimbia huku na kule nikijitumia, lakini mwishowe mikono yangu ni mitupu—sina chochote kabisa. Ilhali hata sasa Unaniambia Utanifanya nitende kama foili Yako. Ninawezaje hata kuonyesha uso wangu?” “Ulikuwa unazungumza kuhusu nini? Nimefanya kazi nyingi mno ya kuadibu zamani, na wewe huielewi? Je, wewe unajifahamu mwenyewe kwa kweli? Je, jina la ‘foili’ pia si hukumu ya maneno? Je, unafikiri kwamba kuzungumza Kwangu kuhusu foili pia ni njia, namna ya kukuhukumu? Basi utanifuataje?” “Bado sijapanga jinsi ya kukufuata Wewe. Kwanza ninataka kujua: Je, mimi ni foili au la? Je, foili pia wanaweza kukamilishwa? Je, jina la ‘foili’ linaweza kubadilishwa? Ninaweza kutoa ushuhuda mkubwa sana kupitia kuwa foili, na kisha kuwa mtu ambaye amekamilishwa, ambaye ni mfano wa kumpenda Mungu, na mwandani wa Mungu? Ninaweza kukamilishwa? Niambie ukweli!” “Je, huna habari kwamba daima vitu vinakua, daima vinabadilika? Mradi sasa hivi uko tayari kuwa mtiifu katika kazi yako kama foili basi utaweza kubadilika. Kama wewe ni foili au la haina uhusiano wowote na hatima yako. Cha muhimu ni kama unaweza kuwa mtu ambaye ana badiliko katika tabia ya maisha yake au la.” “je, unaweza kuniambia iwapo unaweza kunikamilisha au la?” “Mradi ufuate na kutii mpaka mwisho, Ninakuhakikishia kwamba Ninaweza kukufanya kamili.” “Na itanibidi nipitie mateso ya aina gani?” “Utapitia shida, na vile vile hukumu na kuadibu kwa maneno, hasa kuadibu kwa maneno, ambako ni sawa na kuadibiwa kwa kuwa foili!” “Kuadibu sawa na ya foili pia? Hivyo, kama ninaweza kukamilishwa na Wewe kwa kupitia shida, kama kuna matumaini, basi hiyo ni sawa. Hata kama ni chembe ya matumaini tu, ni bora zaidi kuliko kuwa foili. Jina hilo, ‘foili,’ husikika kuwa baya sana. Siko tayari kuwa foili!” “Ni nini kibaya sana kuhusu foili? Je, si foili ni wazuri kikamilifu kwa njia yao wenyewe? Je, foili hawastahili kufurahia baraka? Nikisema kwamba foili wanaweza kufurahia baraka, basi utaweza kufurahia baraka. Si ukweli kwamba majina ya watu hubadilika kwa sababu ya kazi Yangu? Na ilhali jina tu linakusumbua kiasi hiki? Ukweli kwamba wewe ni foili wa aina hii kunastahili kabisa. Je, uko tayari kufuata au la?” “Kwa hivyo, unaweza kunifanya kamili au la? Je, Unaweza kuniruhusu nifurahie baraka Zako?” “Je, uko tayari kufuata mpaka mwisho au la? Je, uko tayari kujitoa?” “Acha nilifikirie. Foili pia anaweza kufurahia baraka Zako, na anaweza kukamilishwa. Baada ya kufanywa mkamilifu nitakuwa mwandani Wako na kufahamu mapenzi Yako kwa ukamilifu, na nitamiliki Unachomiliki. Nitaweza kufurahia kile Unachofurahia, na nitajua kile Unachojua. … Baada ya kupitia shida na kukamilishwa, nitaweza kufurahia baraka. Hivyo ni baraka zipi Nitakazofurahia kwa kweli?” “Usiwe na wasiwasi juu ya baraka utakazofurahia. Hata Ningekwambia, mambo haya yanazidi mawazo yako. Baada ya kuwa foili mzuri, utashindwa, na utakuwa foili mwenye mafanikio. Huu ni mfano na kielelezo cha mtu ambaye ameshindwa, lakini bila shaka unaweza tu kuwa mfano na kielelezo baada ya kushindwa.” “Mfano na kielelezo ni nini?” “Ni mfano na kielelezo kwa wote wasio Wayahudi, yaani, wale ambao hawajashindwa.” “Hilo linawajumuisha watu wangapi?” “Ni watu wengi sana. Si tu watu wale elfu nne au tano kati yenu—wale wote ambao wanalikubali jina hili katika dunia nzima lazima washindwe.” “Hivyo si miji mitano au kumi tu!” “Usiwe na wasiwasi kuhusu hili sasa, na usijishughulishe kupita kiasi. Lenga tu jinsi unavyopaswa kupata kuingia sasa hivi! Ninakuahidi kwamba unaweza kukamilishwa.” “Hadi kiwango kipi? Na ni baraka zipi ninazoweza kufurahia?” “Kwa nini una wasiwasi sana? Nimeahidi kwamba unaweza kufanywa mkamilifu. Je, umesahau kwamba Mimi ni mwaminifu?” “Ni kweli kwamba Wewe ni mwaminifu, lakini baadhi ya mbinu Zako za kuzungumza daima zinabadilika. Leo Unasema Unaahidi kwamba ninaweza kukamilishwa, lakini kesho unaweza kusema hakuna uhakika. Na kwa watu wengine unasema ‘Ninaahidi kwamba mtu kama wewe hawezi kukamilishwa.’ Sijui kile kinachoendelea na maneno Yako. Hasa sithubutu kuliamini kwa urahisi.” “Hivyo unaweza kujitoa au la?” “Kutoa nini?” “Kutoa maisha yako ya baadaye na matumaini yako.” “Ni rahisi kuyaachilia mambo hayo! Jambo kuu ni jina la ‘foili’—kwa kweli silitaki. Ukiondoa jina hilo kutoka kutoka kwangu basi nitakaribisha chochote, nitaweza kufanya chochote. Je, haya si mambo madogo tu? Je, Unaweza kuondoa jina hilo?” “Hilo litakuwa jambo rahisi tu, sivyo? Kama Ninaweza kukupa jina hilo, bila shaka pia Ninaweza kuliondoa. Lakini sasa si wakati wa hilo. Lazima kwanza ukamilishe uzoefu wako wa hatua hii ya kazi, na ni hapo tu ndipo unaweza kupata jina jipya. Zaidi mtu alivyo kama wewe, ndivyo anahitaji zaidi kuwa foili. Unavyoogopa zaidi juu ya kuwa foili, ndivyo Nitakavyokupachika jina hilo zaidi. Mtu kama wewe lazima apewe nidhamu kali na kushughulikiwa. Kadiri mtu alivyo muasi, ndivyo atakavyokuwa mtendaji huduma zaidi, na mwishowe, hatapata chochote.” “Kuona kwamba natafuta kwa bidii sana, kwa nini nisiweze kulitupilia mbali jina la ‘foili’? Tumekufuata hii miaka yote na kuteseka sana. Tumekufanyia mambo mengi. Tumepita katika upepo na mvua; tunakaribia mwisho wa ujana wetu. Hatujaoa wala kuanzisha familia, na wale kati yetu ambao wamefanya hivyo bado wamejitokeza wazi. Nilikuwa shuleni wakati wote hadi katika shule ya upili, lakini mara tu niliposikia kwamba ulikuwa Umekuja, niliacha nafasi yangu ya kwenda chuo kikuu. Na Unasema kwamba sisi ni foili! Tumepoteza mengi mno! Tunafanya mambo haya yote, lakini sasa inatokea kwamba sisi ni foili Zako tu. Je, jambo hili linawafanya wenzangu tuliosoma nao darasani na marika wangu kunifikiria mimi nini? Wanaponiona na kuuliza juu ya cheo changu na hadhi yangu, ninakosaje kuwa na aibu kuwaambia? Mwanzoni, nililipa gharama yoyote kwa sababu ya imani yangu Kwako na wengine wote walinidhihaki kama mpumbavu. Lakini bado nilifuata na nilikuwa na hamu ya wakati ambapo siku yangu ingekuja, na ambapo ningewaonyesha wale wote ambao hawakuamini. Lakini badala yake, leo Unaniambia kwamba mimi ni foili. Kama Ungenipa jina la chini kabisa, kama Ungeniruhusu niwe mmoja wa watu wa ufalme, hilo lingekuwa sawa! Hata kama singekuwa mwanafunzi Wako au msiri Wako, ningekuwa sawa tu kuwa mfuasi Wako! Tumekufuata miaka hii yote, tumeziacha familia zetu, na imekuwa vigumu sana kuendelea kutafuta muda huo wote mpaka sasa, na kile tulicho nacho ni jina la ‘foili’ tu! Nimeacha kila kitu kwa ajili Yako; Nimeacha utajiri wote wa dunia hii. Kabla, mtu fulani alinitambulisha kwa mtu ambaye angeweza kuwa mwenzi. Kwa kweli alikuwa mwenye sura nzuri na alivalia vizuri, alikuwa mwana wa kiongozi wa serikali wa ngazi ya juu. Wakati huo nilivutiwa naye. Lakini mara tu niliposikia kwamba Mungu alikuwa ameonekana na alikuwa akitekeleza kazi Yake, kwamba Ulikuwa Utuongoze kuingia katika ufalme na kutukamilisha, na kwamba Ulikuwa umetuomba tuwe na uamuzi wa kutosita katika kuwacha kila kitu nyuma, niliposikia hayo, niliona kwamba sikuwa na uamuzi wowote hata kidogo. Kisha nilijikaza kisabuni na kukataa fursa hiyo. Baada ya hapo, alituma zawadi kwa familia yangu mara kadhaa, lakini hata sikuziangalia. Je, Unafikiri kwamba nilikuwa nimekasirika wakati huo? Kilikuwa kitu kuziri sana lakinihakikufanikiwa. Ningekosaje kufadhaika? Nilifadhaika kukihusu kwa siku kadhaa hivi kwamba singeweza kulala usiku, lakini hatimaye bado nilikiacha. Kila wakati nilipoomba, nilisisimuliwa na Roho Mtakatifu, ambaye Alisema: ‘Je, uko tayari kutoa kila kitu kwa ajili Yangu? Je, uko tayari kujitumia kwa ajili Yangu?’ Kila Nilipofikiri juu ya maneno hayo Yako ningelia. Niliguswa na nikalia kwa huzuni mara nyingi zaidi ya ninavyojua. Mwaka mmoja baadaye nilisikia kwamba mtu huyo alikuwa ameoa. Ni wazi kwamba, nilikuwa mwenye taabu sana, lakini bado niliacha jambo hilo kwa ajili Yako. Haya yote licha ya kutaja kuwa chakula changu na mavazi ni duni—niliacha ndoa hiyo, niliyaacha haya yote, kwa hivyo Hupaswi kunitaka nitende kama foili! Niliiacha ndoa yangu, tukio muhimu zaidi maishanimwangu, kwa ajili tu ya kujidhabihu Kwako. Maisha yote ya mtu si kitu chochote zaidi ya kupata mwenzi mzuri na kuwa na familia yenye furaha. Niliacha hili, hili bora kati ya mambo yote, na sasa sina chochote na mimi niko mpweke. Ni wapi Ungenitaka niende? Nimeteseka tangu nilipoanza kukufuata. Sijakuwa na maisha mazuri. Nimeiacha familia yangu na amali yangu pamoja na furaha za mwili, na dhabihu hii ambayo sote tumetoa bado haitoshi kufurahia baraka Zako? Hivyo sasa ni suala hili la ‘foili’. Mungu, kwa kweli Wewe umezidi! Tuangalie—hatuna kitu chochote cha kutegemea katika dunia hii. Wengine wetu tumewaacha watoto wetu, wengine tumeacha kazi zetu, wenzi wetu,[b] na kadhalika; tumeacha furaha zote za mwili. Kuna tumaini lipi lingine kwetu? Tunawezaje kuendelea kuishi katika ulimwengu? Je, kujitoa huku ambako tumejitoa hakuna thamani ya peni moja? Huwezi kuona hilo kabisa? Hadhi yetu ni duni na ubora wetu wa tabia ni pungufu—tunakubali jambo hili, lakini wakati upi hatujawahi kutii kile Ulichotaka tufanye? Sasa unatuacha bila huruma na ‘kutulipa’ kwa jina ‘foili’? Je, kujitolea kwetu kumetuletea hili tu? Hatimaye, watu wakiniuliza ni nini nimepata kutokana na kumwamini Mungu, je, kweli naweza kuwaruhusu waone neno hili ‘foili’? Ninawezaje kufungua mdomo wangu kusema kwamba mimi ni foili? Siwezi kueleza hilo kwa wazazi wangu, na siwezi kulieleza kwa yule angeweza kuwa mwenzi wangu wa zamani. Nimelipa gharama kubwa sana, na kile ninachopata kama malipo ni kuwa foili! Aa! Nahisi huzuni sana!” (Alianza kuyapiga mapaja yake na kulia.) “Ningesema kwamba sasa kwa kuwa sasa Sikuwa nikupe jina la foili lakini badala yake Ningekufanya mmoja wa watu Wangu na Nikuamuru uende na ukaeneze injili, kama Ningekupa hadhi ya wewe kufanya kazi, je, ungeweza kuifanya? Kwa kweli ni kipi ambacho umepata kutokana na hatua baada ya hatua ya kazi hii? Ilhali uko hapa ukiniburudisha Mimi na hadithi yako—huna aibu! Unasema kwamba umelipa gharama lakini hujapata chochote. Inawezekana kwamba Nimepuuza kukwambia masharti Yangu ni gani ya kumpata mtu? Kazi Yangu ni kwa ajili ya nani? Je, unajua? Uko hapa ukirudisha manung’uniko ya zamani! Je, hata unahesabika kama mwanadamu tena? Je, huchukui kuteseka kokote kwamba ulipitia kwa hiari yako mwenyewe? Na, je, kuteseka kwako hakukuwa ili kupata baraka? Je, umetosheleza mahitaji Yangu? Yote unayotaka ni kupata baraka. Huna aibu! Ni lini mahitaji Yangu kwako yaliwahi kuwa ya lazima? Ikiwa uko tayari kunifuata ni lazima unitii katika mambo yote. Usijaribu kujadili juu ya masharti. Hata hivyo, Nilikuambia awali kuwa njia hii ni njia ya kuteseka. Imejawa na uwezekano wa kutia hofu, na msaada kidogo. Je, umesahau? Nimesema jambo hili mara nyingi. Ikiwa uko tayari kuteseka basi Nifuate. Kama huko tayari kuteseka, basi acha. Sikulazimishi—uko huru kuja au kwenda! Hata hivyo, hivi ndivyo kazi Yangu inavyofanywa, na Siwezi kuchelewesha kazi Yangu yote kwa sababu ya uasi wako binafsi. Unaweza kuwa huko tayari kutii, lakini kunao wengine ambao wako tayari. Nyinyi nyote ni watu walio tayari kufanya lolote! Huogopi chochote! Unajadili nami juu ya masharti—unataka kuendelea kuishi au la? Unajipangia mwenyewe na kupigania umaarufu na faida yako mwenyewe. Je, kazi Yangu yote si kwa ajili yenu? Je, wewe ni kipofu? Kabla Nipate mwili, hungeweza kuniona, na maneno haya ambayo umeongea yangesameheka wakati huo, lakini sasa Mimi Nimepata mwili na Ninafanya kazi kati yenu, lakini bado huwezi kuona? Ni nini usichoelewa? Unasema umepata hasara; hivyo Nimekuwa mwili ili kuwaokoa nyinyi watu waliokata tamaa na Nimefanya kazi kubwa sana, na hata sasa bado mnalalamika—hamwezi kusema kwamba Nimepata hasara? Je, si kile ambacho Nimefanya ni kwa ajili yenu kabisa? Ninawapa watu jina hili kulingana na kimo chao cha wakati uliopo. Nikiwaita ‘foili,’ basi unakuwa foili mara moja. Vivyo hivyo, Nikikuita ‘mmoja wa watu wa Mungu,’ basi hilo ndilo unalokuwa mara moja. Chochote Nikuitacho, hicho ndicho ulicho. Je, si yote yanatimizwa kwa maneno machache kutoka kwa kinywa Changu? Na haya maneno Yangu machache yanakughadhibisha sana? Sawa basi, Niwie radhi! Usipotii sasa, hatimaye utalaaniwa—utafurahi wakati huo? Huzingatii njia ya maisha lakini unalenga tu hadhi na jina lako; je, maisha yako yakoje? Sikani kwamba umelipa gharama kubwa, lakini angalia kimo na matendo yako mwenyewe—na hata sasa, bado unajaribu kujadili masharti. Je, hiki ni kimo ambacho umekipata kupitia katika uamuzi wako? Je, bado una uadilifu wowote? Je, una dhamiri? Je, ni Mimi niliyefanya kitu kibaya? Je, mahitaji Yangu kwako yalikuwa ya makosa? Haya, ni nini? Ningetaka utende kama foili kwa siku chache na bado huko tayari kufanya hivyo. Huo ni uamuzi wa aina gani? Nyinyi nyote ni wenye mioyo dhaifu, nyinyi ni waoga! Kuwaadhibu watu kama nyinyi sasa ni jambo la linalotarajiwa!” Mara tu Niliposema jambo hili, hakusema neno lolote.
Kupitia kazi ya aina hii sasa, lazima muwe na ufahamu fulani kuhusu hatua za kazi ya Mungu na mbinu Zake za kuwabadili watu. Kuwa na hili ndiyo njia ya pekee ya kutimiza matokeo katika mabadiliko. Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. Sababu ambayo vitu hivi vipo katika mioyo ya watu ni kwa sababu hasa sumu ya Shetani daima inaharibu fikira za watu, na daima watu hawawezi kuondoa vishawishi hivi vya Shetani. Wanaishi katikati ya dhambi ilhali hawaiamini kuwa dhambi, na bado wao huwaza: “Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima Atupe baraka na kupanga kila kitu kwa ajili yetu ipasavyo. Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima tuwe wa cheo cha juu kuliko wengine, na lazima tuwe na hadhi zaidi na maisha zaidi ya baadaye kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu.” Kwa miaka mingi, mawazo ambayo watu wametegemea kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao yamekuwa yakiharibu mioyo yao hadi kiwango ambapo wamekuwa wadanganyifu, waoga, na wenye kustahili dharau. Hawakosi tu ushupavu na uamuzi, lakini pia wamekuwa walafi, wenye kiburi, na wa kudhamiria. Kabisa wanakosa uamuzi wowote upitao sana ubinafsi, na hata zaidi, hawana ujasiri hata kidogo wa kuondoa shutuma za ushawishi huu wa giza. Fikira na maisha ya watu ni mabovu sana kiasi kwamba mitazamo yao juu ya kuamini katika Mungu bado ni miovu kwa namna isiyovumilika, na hata watu wanaponena kuhusu mitazamo yao juu ya imani katika Mungu haivumiliki kabisa kusikia. Watu wote ni waoga, wasiojimudu, wenye kustahili dharau, na dhaifu. Hawahisi maudhi kwa nguvu za giza, na hawahisi upendo kwa nuru na ukweli; badala yake, wanafanya kila wanaloweza kuvifukuza. Je, si fikira na mitazamo yenu ya sasa iko hivi tu? “Kwa kuwa ninaamini katika Mungu ninapaswa tu kumiminiwa baraka na inapaswa kuhakikishwa kwamba hadhi yangu kamwe haitelezi na kwamba inabaki kuwa juu kuliko ile ya wasioamini.” Hamjakuwa mkihodhi mtazamo wa aina hiyo ndani yenu kwa mwaka mmoja au miaka miwili tu, lakini kwa miaka mingi. Kufikiria kwenu kwa kibiashara kumekua sana. Ingawa mmewasili kwenye hatua hii leo, bado hamjaacha hadhi lakini mnapambana bila kukoma kuuliza kuihusu, na mnaichunguza kila siku, kwa hofu kubwa kwamba siku moja hadhi yenu itapotea na jina lenu litaharibiwa. Watu hawajawahi kuweka kando tamaa yao ya starehe. Hivyo, Ninapowahukumu hivi leo, mtakuwa na kiwango kipi cha ufahamu mwishowe? Mtasema kwamba ingawa hadhi yenu haiko juu, mmefurahia kuinuliwa na Mungu. Kwa sababu mmezaliwa katika tabaka la chini, hamna hadhi, lakini mnapata hadhi kwa sababu Mungu anawainua—hiki ni kitu ambacho Aliwapa. Leo mna uwezo wa kibinafsi wa kupokea mafunzo ya Mungu, kuadibu Kwake, na hukumu Yake. Huku, hata zaidi, ni kuinuliwa na Yeye. Mnaweza kupokea utakaso na kuchomwa Kwake binafsi. Huu ni upendo mkuu wa Mungu. Kupitia enzi hakujakuwa hata mtu mmoja ambaye amepokea utakaso na kuchomwa Kwake, na hakuna hata mtu mmoja ambaye ameweza kukamilishwa kwa maneno Yake. Mungu sasa Ananena nanyi ana kwa ana, Akiwatakasa, Akifichua uasi wenu wa ndani—huu kweli ni kuinuliwa na Yeye. Watu wana uwezo upi? Kama wao ni wana wa Daudi au ni uzao wa Moabu, kwa jumla, watu ni viumbe ambao hawana chochote chenye kustahili kujigamba kuhusu. Kwa kuwa nyinyi ni viumbe wa Mungu, lazima mtekeleze wajibu wa kiumbe. Hakuna mahitaji mengine kwenu. Hivi ndivyo mnavyopaswa kuomba: “Ee Mungu! Kama nina hadhi au la, sasa ninajielewa mwenyewe. Hadhi yangu ikiwa juu ni kwa sababu ya kuinuliwa na Wewe, na ikiwa iko chini ni kwa sababu ya mpango Wako. Kila kitu ki mikononi Mwako. Sina chaguzi zozote, wala malalamishi yoyote. Ulipanga kwamba ningezaliwa katika nchi hii na miongoni mwa watu hawa, na yote ninayopaswa kufanya ni kuwa mtiifu kabisa chini ya utawala Wako kwa sababu kila kitu ki ndani ya yale ambayo Umepanga. Sifikirii kuhusu hadhi; hata hivyo, mimi ni kiumbe tu. Ukiniweka kwenye shimo lisilo na mwisho, katika ziwa la moto wa jahanamu, mimi si chochote isipokuwa kiumbe. Ukinitumia, mimi ni kiumbe. Ukinikamilisha, mimi bado ni kiumbe. Usiponikamilisha, bado nitakupenda kwa sababu mimi si zaidi ya kiumbe. Mimi si chochote zaidi ya kiumbe mdogo sana aliyeumbwa na Bwana wa uumbaji, mmoja tu miongoni mwa wanadamu wote walioumbwa. Ni Wewe uliyeniumba, na sasa kwa mara nyingine tena Umeniweka katika mikono Yako ili unitumie Utakavyo. Niko tayari kuwa chombo Chako na foili Yako kwa sababu vyote ni vile Umepanga. Hakuna anayeweza kubadili jambo hilo. Vitu vyote na matukio yote yako katika mikono Yako.” Wakati utakapofika ambapo hutafikiria tena hadhi, basi utaondokana na hilo. Hapo tu ndipo utaweza kwa kujiamini na kutafuta kwa ujasiri, na ni hapo tu ndipo moyo wako unaweza kuwa huru dhidi ya vikwazo vyovyote. Mara tu watu watakapokuwa wamenasuliwa kutoka katika mambo haya, basi hawatakuwa na shaka tena. Ni nini kinawahangaisha wengi wenu sasa hivi? Mnazuiwa daima na hadhi na mnashughulishwa daima na matarajio yenu wenyewe. Kila wakati mnayaangalia matamshi ya Mungu, mkitaka kusoma misemo inayohusu hatima ya wanadamu na kutaka kujua matarajio yenu ni yapi na hatima yenu itakuwa ipi. Mnajiuliza, “Kweli nina matarajio yoyote? Je, Mungu ameyaondoa? Mungu anasema tu kwamba mimi ni foili; basi matarajio yangu ni yapi?” Ni vigumu kwa ninyi kuweka kando matarajio na kudura yenu. Sasa nyinyi ni wafuasi, na mmepata ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu. Kwa nini watu wengi hawawezi kujiondoa katika uhasi? Je, si jibu bila shaka ni kwa sababu ya matarajio ya kuvunja moyo? Mara tu matamshi ya Mungu yanapotolewa nyinyi huharakisha kuona hadhi na utambulisho wenu kweli vikoje. Mnaipa hadhi na utambulisho kipaumbele, na kuyaweka maono katika nafasi ya pili. Katika nafasi ya tatu ni kitu mnachopaswa kuingia katika, na katika nafasi ya nne ni mapenzi ya Mungu ya sasa. Nyinyi huangalia kwanza iwapo jina la Mungu kwenu kama “foili” limebadilika au la. Mnasoma na kusoma, na mnapoona kwamba jina la “foili” limeondolewa, mnafurahi sana na kumshukuru Mungu kwa nguvu sana na kuisifu nguvu Yake kuu. Lakini mnapoona kwamba nyinyi bado ni foili, mnafadhaika na msukumo ulio mioyoni mwenu unatoweka mara moja. Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii, ndivyo utakavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo watakavyozalimika kupitia usafishaji mkubwa. Watu kama hao hawana thamani kabisa! Lazima wshughulikiwe na wahukumiwe vya kutosha ili waachane na mambo haya kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii uzima hawawezi kubadilishwa, na wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na uingiaji, lakini badala yake unalenga tamaa badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kumkaribia Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme? Ikiwa kusudi la kufuatilia kwako si kutafuta ukweli, basi afadhali utumie fursa hii na kurudi duniani ili kufanikiwa. Kupoteza muda wako hivi kwa kweli hakuna thamani—kwa nini ujitese? Je, si kweli kwamba unaweza kufurahia mambo ya aina yote katika dunia hii nzuri? Pesa, wanawake warembo, hadhi, majivuno, familia, watoto, na kadhalika—je, matokeo haya ya dunia siyo mambo mazuri zaidi ambayo ungeweza kufurahia? Kuna faida gani kuzurura zurura hapa ukitafuta mahali ambapo unaweza kuwa na furaha? Mwana wa Adamu hana pahali pa kulaza kichwa Chake, hivyo ungekuwaje na pahali pa utulivu? Angewezaje kukuumbia pahali pazuri pa utulivu? Hilo lawezekana? Kando na hukumu Yangu, leo unaweza kupokea tu mafundisho ya ukweli. Huwezi kupata faraja kutoka Kwangu na huwezi kupata kitanda cha starehe unachotamani sana usiku na mchana. Sitakupa utajiri wa duniani. Ukifuatilia kwa kweli, basi Niko tayari kukupa njia ya uzima yote, kukutaka uwe kama samaki aliyerudi majini. Usipofuatilia kwa kweli, Nitayafuta yote. Siko tayari kutoa maneno kutoka kwa kinywa Changu kwa wale ambao ni wenye tamaa ya faraja, ambao ni kama nguruwe na mbwa tu!
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
b. Nakala ya asili inasema “wake.”