Sura ya 7

Kuinuka kwa mazingira pande zetu zote huharakisha kurudi nyuma kwetu katika roho. Usitende kwa moyo mgumu, usipuuze kwa vyovyote vile kama Roho Mtakatifu Ana wasiwasi, usijaribu kuwa mjanja na usiwe na ridhaa kupita kiasi na kuridhika kibinafsi au kuzingatia sana matatizo yako mwenyewe; kitu pekee cha kufanya ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Huwezi kuyaacha maneno ya Mungu nyuma au kuyapa kisogo; lazima uyaelewe kwa makini, rudia kuomba-kusoma kwako, na uelewe maisha ndani ya maneno hayo. Usishiriki katika yale yasiyokuwa na maana kwa kuyabugia pasipo kujipa mwenyewe wakati wa kuyawaza. Je, unategemea maneno ya Mungu kwa kila kitu unachofanya? Usizungumze makubwa kama mtoto na kisha ukuwe katika mvurugo wakati wowote kitu chochote kinazuka. Lazima utumie roho yako kila saa ya kila siku, usipumzike hata kwa muda. Lazima uwe na roho yenye makali. Haijalishi ni mtu, tukio au kitu gani unachoweza kukumbana nacho, ukija mbele ya Mungu utakuwa na njia ya kufuata. Lazima ule na kunywa maneno ya Mungu kila siku, uelewe maneno Yake bila kuwa na uzembe, ufanye juhudi zaidi, upate kabisa kila maelezo na kujiandaa mwenyewe na ukweli kamili ili kuepukana na kutoelewa mapenzi ya Mungu. Ni lazima upanue safu zako za uzoefu na ulenge kupitia maneno ya Mungu. Kupitia uzoefu utakuwa na uwezo wa kuwa yakini zaidi kuhusu Mungu; bila uzoefu, kusema u yakini juu Yake ni maneno tu tupu. Ni lazima tuwe wenye kuelewa haraka! Amka! Usiwe mlegevu tena; ukikabiliana na mambo kwa njia paruparu na wala hautajitahidi kwa maendeleo basi kwa kweli wewe ni kipofu. Ni lazima ulenge kazi ya Roho Mtakatifu, sikiza kwa makini sauti ya Roho Mtakatifu, fungua masikio yako kwa maneno ya Mungu, tunza muda uliobaki na ulipe gharama, hata iwe ni gani. Ukiwa na chuma cha pua, kitumie pahali kinapofaa zaidi—kutengeneza upanga thabiti; shikilia kwa uthabiti kile kilicho muhimu na ulenge kuweka maneno ya Mungu katika vitendo. Ukiwa umeyaacha maneno ya Mungu, basi haijalishi unavyoweza kufanya vizuri kwa nje, yote itakuwa ni bure. Kutenda kwa maneno matupu tu haikubaliki kwa Mungu; mabadiliko lazima yaje kwa njia ya mwenendo wako, tabia, imani, ujasiri na utambuzi.

Wakati u karibu sana! Haidhuru mambo ya dunia ni mazuri kiasi kipi, ni lazima yote yaachwe kando. Matatizo mengi na hatari hayawezi kutuogofya sisi, wala anga kuanguka hakutatushinda kabisa. Bila aina hii ya azimio itakuwa ngumu tu sana kwako wewe kuwa mtu yeyote wa umuhimu. Wale ambao ni wadhaifu na ambao kwa uoga hushikilia maisha hawastahili kusimama mbele ya Mungu.

Mwenyezi Mungu ni Mungu wa vitendo. Haidhuru jinsi tu wapumbavu, Yeye bado Atatuonea huruma, mikono Yake hakika itatuokoa sisi na bado Atatufanya kamili. Mradi tuna moyo ambao kwa kweli unamtaka Mungu, mradi tumfuate karibu na wala tusikatishwe tamaa, na tutafute kwa hisia ya haraka, basi kwa hakika Hatachukulia yeyote kati yetu bila haki, kwa hakika Atatufidia sisi kile ambacho tuna ukosefu nacho na Yeye Ataturidhisha—yote hii ni wema wa Mwenyezi Mungu.

Kama mtu ni mlafi na mvivu, anaongoza maisha shibe, legevu na hajali chochote, yeye atapata kuwa ni vigumu kuepuka kupata hasara. Mwenyezi Mungu Hutawala mambo yote na matukio yote! Mradi tunamtegemea mioyoni mwetu kila wakati na tuingie rohoni na kufanya ushirika na Yeye, basi Atatuonyesha mambo yote tunayotafuta na mapenzi Yake kwa hakika yatafichuliwa kwetu; mioyo yetu kisha yatakuwa katika furaha na amani, thabiti kwa uwazi kamili. Ni muhimu kuwa na uwezo wa kutenda kulingana na maneno Yake; kuwa na uwezo wa kuelewa mapenzi Yake na kuishi katika utegemezi wa maneno Yake—hii tu ndiyo kupitia kwa kweli.

Ni kwa kuelewa tu maneno ya Mungu ndipo ukweli wa maneno Yake utaweza kuingia ndani yetu na kuwa maisha yetu. Bila kupitia kwa vitendo vyovyote, unawezaje kuingia kwa uhalisi wa maneno ya Mungu? Kama huwezi kupata maneno ya Mungu kama maisha yako basi tabia yako haitaweza kubadilika.

Kazi ya Roho Mtakatifu sasa inaendelea kwa upesi sana! Kama haufuati kwa karibu na kupokea mafunzo, itakuwa vigumu kuwa sawa na kuendelea kwa kasi kwa Roho Mtakatifu. Harakisha na usababishe mabadiliko ya kimsingi usije ukakanyagwa chini ya miguu na Shetani na kuingia katika ziwa la moto wa jahanamu ambako hakuna kutoroka. Nenda tafuta kadri unavyoweza sasa ili usitelekezwe.

Iliyotangulia: Sura ya 6

Inayofuata: Sura ya 8

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp