Sura ya 8

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu.

Lugha za mataifa mbalimbali ni tofauti na kila nyingine lakini kuna Roho mmoja tu. Huyu Roho huunganisha makanisa kote ulimwenguni na ni mmoja na Mungu, bila tofauti hata kidogo, na hili ni jambo ambalo halina shaka kabisa. Roho Mtakatifu sasa anawapaazia sauti na sauti Yake yawaamsha. Hii ni sauti ya huruma ya Mungu. Wanaliita kwa sauti jina takatifu la Mwenyezi Mungu! Wao pia wanatoa sifa na kuimba. Hakuwezi kuwa na mkengeuko wowote katika kazi ya Roho Mtakatifu, na watu hawa hufanya linalowezekana ili kuendelea kwenye njia sahihi, huwa hawajitoi na maajabu yake hulundikana juu ya maajabu. Ni kitu ambacho watu huona ugumu kufikiria na kisichowezekana kukikisia.

Mwenyezi Mungu ndiye Mfalme wa maisha katika ulimwengu! Yeye huketi juu ya kiti kitukufu cha enzi na huihukumu dunia, huwatawala wote, huyaongoza mataifa yote; watu wote hupiga magoti Kwake, humwomba, huja karibu naye na kuwasiliana na Yeye. Bila kujali muda gani mmemwamini Mungu, jinsi hadhi yenu ilivyo ya juu au jinsi ukubwa wenu wa vyeo ulivyo, kama nyinyi humpinga Mungu katika mioyo yenu basi ni lazima mhukumiwe na lazima msujudu mbele Yake, mkitoa sauti chungu ya kusihi kwenu; huku kweli ni kuvuna matunda ya matendo yenu wenyewe. Sauti hii ya kupiga mayowe ni sauti ya kuteswa katika ziwa la moto na kiberiti, na ni kilio cha kuadibiwa na fimbo ya chuma ya Mungu; hii ndiyo hukumu mbele ya kiti cha Kristo.

Baadhi ya watu huogopa, baadhi huficha dhamiri zenye hatia, baadhi wako macho, baadhi huwa waangalifu kusikiza kwa makini, baadhi hutubu na kuanza upya, wakihisi majuto makubwa sana, baadhi hulia kwa uchungu na maumivu, baadhi huachilia kila kitu na kutafuta bila tumaini, baadhi ya watu hujichunguza wenyewe na hawathubutu kutenda bila mpango tena, baadhi hujaribu kwa haraka kuwa karibu na Mungu, baadhi huchunguza dhamiri zao wenyewe, wakijiuliza kwa nini maisha yao hayawezi kuendelea. Baadhi hubaki katika mkanganyiko, baadhi hujifungua pingu za miguu yao na kusonga mbele kwa ushujaa, wakishika ufunguo na kutopoteza wakati kuzingatia maisha yao. Baadhi bado husita na hawako wazi juu ya maono—mzigo walio nao na wanaoubeba katika mioyo yao ni mzito kweli kweli.

Kama mawazo yako si wazi basi Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi ndani yako. Yote unayoyazingatia, njia unayoitembea na yote ambayo moyo wako unatamania sana yamejawa na dhana zako na wazo lako la uadilifu wa kibinafsi! Mimi nawashwa na ukosefu wa subira—jinsi Mimi natamani kuwa Ningewafanya nyote wakamilifu moja kwa moja hivi karibuni ili muwe wa faida Kwangu na mzigo Wangu mzito unaweza kufanywa mwepesi. Lakini kwa kuwaangalia nyinyi, Mimi naona ni muhali kuwa na shauku juu ya matokeo. Naweza tu kusubiri kwa ustahimilivu, nitembee polepole na kuwasaidia polepole na kuwaongoza. Ah, lazima mviweke vichwa vyenu wazi! Ni kipi kinachopaswa kutelekezwa, hazina zako ni zipi, udhaifu wako ni upi, vikwazo vyako ni vipi, zielewe zaidi katika roho yako na ufanye ushirika na Mimi zaidi. Kile Ninachotaka ni kwa nyoyo zenu zinitegemee Mimi kwa unyamavu, si kuniunga mkono kinafiki. Wale ambao kwa kweli hutafuta mbele Yangu, Nitayafichua yote kwako. Kasi Yangu huongezeka mwendo; bora moyo wako hunitegemea Mimi na wewe hufuata wakati wote basi mapenzi Yangu unaweza kupewa wewe kwa msukumo na kufichuliwa kwako wakati wowote. Wale wanaotahadhari kusubiri watapata chakula na watakuwa na njia ya kwenda mbele. Wale wasiojali wataona ugumu wa kuuelewa moyo Wangu, na watafikia mwisho kabisa.

Mimi natamani nyinyi muinuke haraka na kushirikiana na Mimi, na muwe karibu na Mimi wakati wote, siyo tu kwa siku moja na usiku mmoja. Mkono Wangu ni lazima daima uwavute na kuwachochea, kuwaendeleza kwa nguvu, kuwashawishi kuendelea na kuwasihi ili mwendelee! Nyinyi hamuelewi kabisa mapenzi Yangu. Vizuizi vya fikira zenu wenyewe na vizuizi vya matatizo ya dunia ni makali mno, na hamna uwezo kuwa karibu zaidi na Mimi. Kusema kweli, nyinyi huja Kwangu wakati mna hoja, lakini wakati hamna hoja yoyote mawazo yenu huwa na mahangaiko. Yanakuwa kama soko huru na yamejawa na tabia ya kishetani, nyoyo zenu zinamilikiwa na mambo ya kidunia na hamjui jinsi ya kufanya ushirika na Mimi. Ningekosaje Mimi kuwahangaikia? Lakini haitasaidia kuhangaika. Muda umeyoyoma sana na kazi hii inahitaji nguvu nyingi. Hatua Zangu zaruka kuelekea mbele; lazima mshikilie imara yote mliyo nayo, nitumainieni Mimi kila wakati, fanyeni ushirika wa ndani na Mimi na mapenzi Yangu kwa hakika yatafichuliwa kwako wakati wowote. Mnapouelewa moyo Wangu basi mna njia ya kwenda mbele. Lazima msisite tena. Shikilia ushirika wa kweli na Mimi, na usiishie kudanganya au kujaribu kuwa mwerevu sana; huko kutakuwa ni kujidanganya wenyewe tu na kutafichuliwa wakati wowote mbele ya kiti cha Kristo. Dhahabu halisi haiogopi kujaribiwa na moto—huu ndio ukweli! Usione haya, usivunjike moyo au kuwa dhaifu. Fanya ushirika na Mimi moja kwa moja katika roho yako, subiri kwa ustahimilivu na Mimi kwa hakika Nitakufichulia kulingana na wakati Wangu. Wewe kweli, lazima kabisa utahadhari na usiache juhudi Zangu zipotelee bure kwako, na usipoteze wakati. Wakati moyo wako una ushirika na Mimi daima, wakati moyo wako huishi daima mbele Yangu, basi hakuna mtu, hakuna tukio hakuna kitu, hakuna mume, hakuna mwana au binti anayeweza kuvuruga ushirika wako na Mimi ndani ya moyo wako. Wakati moyo wako unawekewa mipaka daima na Roho Mtakatifu na wakati unafanya ushirika na Mimi kila wakati, mapenzi Yangu kwa hakika yatafichuliwa kwako. Wakati unapojongea karibu na Mimi daima kwa njia hii, bila kujali mazingira yako au upo kwa wakati upi maalum, basi huwezi kuvurugika bila kujali ni nani au ni nini unachokabili, na wewe utakuwa na njia ya kwenda mbele.

Kama kwa kawaida huachi chochote kiteleze katika mambo makubwa au madogo, kama moyo wako na mawazo yako yametakaswa, na kama wewe ni mtulivu katika roho yako, basi wakati unapokutana na suala fulani maneno Yangu mara moja yatakuwa na msukumo ndani yako, kama kioo chenye kung'aa kwako kujiangalia mwenyewe kwacho, na wewe ndipo utakapokuwa na njia ya kwenda mbele. Hii inaitwa kuwa na dawa sahihi kwa hali sahihi! Na hali yoyote kwa hakika itatibiwa—Mungu ni mwenyezi hivi. Kwa hakika Mimi nitawaangazia na kuwapa nuru wale wote wenye njaa na kiu ya haki na ambao hutafuta kwa uaminifu. Mimi nitawaonyesha ninyi nyote siri za ulimwengu wa kiroho na kuonyesha njia ya kwenda mbele, Niwafanye mtupilie mbali tabia zenu mbovu za zamani haraka iwezekanavyo na mfikie ukomavu wa maisha ili kwamba muweze kuwa na manufaa Kwangu, na kwamba kazi ya injili hivi karibuni itaendelea bila kizuizi. Ni hapo tu mapenzi Yangu yatakaporidhishwa, ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita utatimizwa haraka iwezekanavyo. Mungu ataupata ufalme na atakuja chini duniani, na kwa pamoja tutaingia katika utukufu!

Iliyotangulia: Sura ya 7

Inayofuata: Sura ya 9

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp