Sura ya 9

Nataka kukukumbusha kwamba huwezi kuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya neno Langu na kutokujali kwa aina yoyote hakukubaliki. Unapaswa kulisikiliza na kulitii na kutenda mambo kulingana na nia Zangu. Daima lazima uwe macho na kamwe usiwe na tabia ambayo ni ya kiburi na ya kujidai, na lazima kila wakati unitegemee Mimi ili kutupilia mbali tabia ya zamani ya asili ambayo hukaa ndani yako. Unapaswa daima kuwa na uwezo wa kudumisha hali ya kawaida mbele Yangu, na uwe na tabia thabiti. Kuwaza kwako lazima kuwe kwa busara na wazi na hakupaswi kuyumbishwa au kudhibitiwa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Unapaswa kuwa mtulivu daima katika uwepo wangu na daima udumishe ukaribu wa kuendelea na kushiriki na Mimi. Ni sharti uonyeshe nguvu na ukakamavu na usimame imara katika ushahidi wako Kwangu. Simama na kuzungumza kwa ajili Yangu na usiogope kile ambacho watu wengine wanasema. Zingatia kukidhi nia Zangu na usidhibitiwe na wengine. Kile Ninachokufichulia lazima kifanywe kwa mujibu wa nia Zangu na hakiwezi kucheleweshwa. Je, unajihisi vipi ndani yako? Je! una wasiwasi? Utaelewa. Kwa nini huwezi kusimama kuzungumza kwa ajili yangu na kufikiria juu ya mzigo Wangu? Unaendelea kujihusisha na hila ndogo, lakini ninayaona yote kwa uwazi. Mimi ni msaada wako na kinga yako, na vyote viko mikononi Mwangu, hivyo unaogopa nini? Je, huko sio kuwa na mhemuko sana? Lazima utupilie kando hisia haraka sana; Sitendi kwa kufuata muhemko, bali Ninatenda haki badala yake. Wazazi wako wakifanya chochote kisicho na faida kwa kanisa, hawawezi kuepuka. Nia Zangu zimefichuliwa kwako na hupaswi kuzipuuzia. Badala yake, lazima uweke uangalifu wako wote katika hayo na kutupa kila kitu kando ili kufuata kwa moyo wako wote. Mimi nitakuweka mikononi Mwangu siku zote. Usiwe mwoga na kudhibitiwa na mume au mke wako; utaruhusu mapenzi Yangu kufanywa.

Kuwa na imani! Kuwa na imani! Mimi ni mwenyezi wako. Hiki ni kitu ambacho unaweza ukakitambua kiasi, lakini bado unapaswa kutahadhari. Kwa ajili ya kanisa, mapenzi Yangu, na usimamizi Wangu, lazima ujitoe kikamilifu, na siri zote na miisho yote itaonyeshwa kwako. Hakutakuwa na uchelewaji zaidi na siku zitafikia mwisho. Kwa hiyo utafanya nini? Unawezaje kutafuta kuyafanya maisha yako yakomae kwa kasi zaidi? Je! Utafanyika mwenye manufaa Kwangu haraka kiasi gani? Utafanyaje ili mapenzi Yangu yatekelezwe? Ili kufanya hivyo kunahitaji kutafakari kikamili na ushirika wa kina zaidi na Mimi. Nitegemee Mimi, niamini Mimi, usiwe mzembe kamwe, na uweze kufanya mambo kulingana na mwongozo Wangu. Ukweli lazima utayarishwe vizuri na unapaswa kuula na kuunywa mara kwa mara zaidi. Kila ukweli lazima utekelezwe kabla ya kueleweka vizuri.

Je, sasa unahisi hakuna muda wa kutosha? Je, wewe pia unahisi kuwa u tofauti ndani ukilinganishwa na kabla na kwamba mzigo wako unaonekana kuwa mzito sana? Nia zangu ni juu yako; lazima uelewe waziwazi, usiende mbali nazo, na daima uunganike na Mimi. Kaeni karibu na Mimi daima, wasilianeni na Mimi, muwe wenye kufikiria moyo Wangu, na kuwa na uwezo wa kuhudumu katika ushirikiano, ili nia Zangu zifichuliwe kwenu. Daima zingatia kwa karibu! Uangalifu wa karibu! Usizembee hata kidogo; huo ni wajibu wako na kazi Yangu hukaa ndani yake.

Unaweza kuwa na ufahamu mdogo katika hatua hii na ukajihisi kuwa hii ni ajabu sana. Huenda ulikuwa na mashaka katika siku za nyuma na ukahisi kuwa ilikuwa tofauti kabisa na dhana, mawazo, na fikra za mwanadamu, lakini wewe unaelewa kimsingi kwa sasa. Hii ni kazi Yangu ya ajabu na ni kazi ya ajabu ya Mungu pia. Lazima uwe macho kabisa na usubiri na kutembea ndani yake. Muda uko mikononi Mwangu; usiupoteze, na kamwe usizembee hata kwa muda mchache; kupoteza muda kunachelewesha kazi Yangu na kunasababisha mapenzi Yangu yazuiwe ndani yako. Lazima ufikirie na uwasiliane na Mimi mara kwa mara. Lazima ulete matendo yote, harakati, fikra, mawazo, familia, mume, wana na mabinti mbele Yangu. Usijitegemee mwenyewe katika matendo yako, vinginevyo Nitakuwa na hasira na hasara zako zitakuwa ghali.

Zizuie hatua zako mwenyewe wakati wote na uwe na uwezo wa kutembea ndani ya maneno Yangu daima. Itawezekana tu ikiwa una hekima Yangu. Njoo mbele Yangu ikiwa unakabiliwa na shida na nitakupa mwongozo. Usifanye fujo na kuwasiliana bila kujali. Ikiwa maisha yako hayapati faida ni kwa sababu hauna ujuzi na hauwezi kutofautisha kati ya maneno mazuri na mabaya. Hutambui hili mpaka udhuriwe na hali zenu ni duni, na huna uwepo wa Roho Mtakatifu. Kwa wakati huo, unakuwa umechelewa sana. Muda unasonga sana sasa, hivyo hupaswi kusalia nyuma hata kidogo katika mbio za maisha yako; lazima ufuate hatua Zangu kwa karibu. Wakati shida zozote zinapotokea, fikiria mara kwa mara kupitia kukaa karibu na Mimi na kuwasiliana Nami moja kwa moja. Ikiwa unaelewa njia hii, kuingia kwako kutakuwa rahisi wakati unavyoendelea kusonga mbele.

Maneno Yangu hayaelekezwi kwako tu; kila mtu kanisani amepungukiwa katika vipengele tofauti tofauti. Lazima muwasiliane zaidi, muweze kula na kunywa kwa kujitegemea wakati wa ibada zenu za kiroho, na muweze kuelewa ukweli muhimu wa kutia katika vitendo mara moja. Lazima uweze kuhisi uhalisi wa neno Langu. Elewa kiini chake na kanuni zake kabisa; usizembee. Litafakari neno Langu daima na uwasiliane nami daima, na hatua kwa hatua litafichuliwa. Huwezi kuja karibu na Mungu kwa wakati kidogo na kisha kabla moyo wako unaweza kuwa na utulivu mbele ya Mungu, usumbuliwe pale vitu vingine vitakapokutokea. Wewe daima unachanganyikiwa na hauna uhakika juu ya mambo na hauwezi kuuona uso Wangu, hivyo hauwezi kuuelewa vizuri Moyo wangu. Hata kama unaweza kuelewa kidogo huna uhakika na bado una shaka. Mpaka pale nitakapomiliki moyo wako kwa ukamilifu na akili zako hazisumbuliwi tena na mambo yote ya kidunia, na unaposubiria kwa akili zilizo wazi na zenye utulivu—ndipo wakati ambao, nitawafichulia, kidogo kidogo, kwa mujibu wa nia Zangu. Mnapaswa kuielewa njia hii ya kuwa karibu na Mimi. Yeyote anayekupiga au kukulaani, au jinsi gani vitu wanavyokupa watu vilivyo vizuri, havikubaliki ikiwa vinakufanya kutokuwa karibu na Mungu. Acha moyo wako uwe ndani ya mshiko Wangu na usiniache kamwe. Kwa aina hii ya ukaribu na ushirika, bila kujali kama ni wazazi wako, mume, watoto, mahusiano mengine ya kifamilia, au vifungo vya kidunia, vyote vitaondoka. Utafurahia utamu ambao ni karibu na usioelezeka ndani ya moyo wako na utapitia ladha ya harufu nzuri na utamu mzuri, na hakika hutatengeka kutoka Kwangu. Ikiwa daima ni kama hivi, mtaelewa yaliyo ndani ya moyo Wangu. Kamwe hamtapoteza njia yenu mtakavyokuwa mnaendelea mbele, kwa maana Mimi ni njia yenu, na kila kitu kipo kwa sababu Yangu. Jinsi maisha yako yamekomaa, lini utaweza kuwa huru dhidi ya ulimwengu huu, lini utaweza kutupilia mbali hisia zako, lini utaweza kuwaacha nyuma mume wako na watoto, maisha yako yatakomaa lini … mambo haya yote yatafanyika kulingana na wakati Wangu. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.

Lazima uingie kutokea upande mzuri. Ikiwa unasubiri kwa kukaa tu, bado ni hasi. Lazima uwe wa vitendo katika kushirikiana na Mimi; kuwa na bidii na usiwe mvivu kamwe. Daima uwe katika ushirika na Mimi na uwe na urafiki wa kina sana na Mimi. Ikiwa huelewi, usikose subira kwa ajili ya matokeo ya haraka. Sio kwamba sitakuambia, Ninataka kuona ikiwa unanitegemea Mimi wakati unapokuwa katika uwepo Wangu na ikiwa unanitegemea Mimi kwa ujasiri. Lazima ubaki karibu na Mimi daima na kuweka mambo yote katika mikono Yangu. Usirudi nyuma. Baada ya kuwa karibu na Mimi kwa kipindi cha muda bila kujua, nia Zangu zitafichuliwa kwako. Ikiwa utazielewa, basi kweli utakuwa uso kwa uso na Mimi, na utakuwa umeupata uso wangu kweli. Utakuwa dhahiri na imara ndani na utakuwa na kitu cha kutegemea, na utakuwa na nguvu na ujasiri pia. Pia utakuwa na njia ya kusonga mbele na kila kitu kitakuja kwako kwa urahisi.

Iliyotangulia: Sura ya 8

Inayofuata: Sura ya 10

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp