Sura ya 55

Ule unaodaiwa kuwa ubinadamu wa kawaida si wa kimwujiza sana kama watu wanavyofikiria, lakini unaweza kuvuka mipaka ya pingu za watu wote, matukio, na vitu, na mateso yatokanayo na mazingira ya mtu. Unaweza kunikaribia Mimi na kuwasiliana kwa karibu na Mimi mahali popote au katika hali yoyote. Ninyi daima hutafsiri vibaya nia Zangu. Ninaposema mnapaswa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, mnajizuia na kudhibiti miili yenu. Lakini huzingatii kutafuta kwa makini ndani ya roho, ila kwa kile mnachovaa kwa nje pekee, ukipuuza ufunuo Wangu ndani yako, na kusisimua Kwangu ndani yako. Jinsi ulivyo mzembe! Mzembe sana! Inaweza kuwa kwamba kumaliza kile ambacho Nimekuaminia ni ufanisi mkubwa? Wewe ni mpumbavu! Huzingatii kukita mizizi kwa kina! “Usiwe jani kwa mti, ila uwe mzizi wa mti huo”—huo kweli ni wito wako? Hujali! Mzembe! Unaridhika punde unapofikiria kuwa umepata faida kidogo. Jinsi unavyojali mapenzi Yangu kidogo sana! Kuanzia sasa, sikiliza, usiwe baridi na usiwe hasi! Unapohudumu, Nikaribie mara kwa mara na kuwasiliana kwa karibu na Mimi. Hii ndiyo njia yako ya pekee ya kujiokoa. Najua kwamba tayari umejikana mwenyewe, unajua upungufu wako mwenyewe, unajua udhaifu wako mwenyewe. Lakini kujua tu hakutoshi. Unahitaji kushirikiana na Mimi na punde unapoelewa nia Zangu ziweke katika vitendo mara moja. Hii ndiyo njia bora kabisa ya kuonyesha kujali mzigo Wangu, njia bora kabisa ya kutii.

Bila kujali jinsi unavyonitendea, Ninataka kutekeleza mapenzi Yangu kwako na watakatifu wote, na Ninataka mapenzi Yangu yatekelezwe bila kuzuiwa katika nchi nzima. Tambua hili kikamilifu! Hili linahusu amri Zangu za utawala! Huogopi hata kidogo? Hutetemeki kwa hofu kwa sababu ya vitendo vyako na mienendo yako? Miongoni mwa watakatifu wote karibu wote hawahisi nia Yangu. Je, wewe hutaki kuwa wa kipekee kama mtu anayefikiria mapenzi Yangu kabisa? Je, wajua? Nia yangu ya dharura kwa sasa ni kutafuta kundi la watu wanaoweza kufikiria mapenzi Yangu kabisa. Hutaki kuwa mmoja wao? Hutaki kujitumia kwa ajili Yangu, kujitolea kwa ajili Yangu? Hutaki kulipa gharama hata kidogo, kutoa juhudi hata kidogo! Mambo yakiendelea kuwa hivyo, juhudi Yangu ya bidii itakuwa bure kwenu. Baada ya Mimi kukuonyesha hilo, bado hujaelewa uzito wa suala hili?

“Kwa wale wanaojitumia kwa dhati kwa ajili Yangu, hakika Nitakubariki sana.” Unaona! Nimekuambia hili mara kadhaa, lakini bado una mashaka mengi, ukiogopa mazingira ya familia, ukiogopa mazingira ya nje. Kweli hujui kinachokufaa! Ninawatumia tu watu waaminifu, wa kawaida, na wazi. Umekuwa na furaha na radhi kwa Mimi kukutumia, lakini kwa nini bado una wasiwasi sana? Inaweza kuwa kwamba maneno Yangu hayana athari hata kidogo kwako? Nimesema kuwa Nakutumia wewe, ilhali huwezi kuamini hilo kwa uthabiti. Kila mara unashuku, ukiogopa kwamba Nitakuacha. Dhana zako zimefungwa sana! Ninaposema kwamba Nakutumia hilo linamaanisha Nakutumia. Kwa nini una shaka sana kila mara? Je, ni kwamba Sijaongea kwa uwazi vya kutosha? Kila neno ambalo Nimesema ni kweli. Hakuna tamko hata moja ambalo si la kweli. Mwanangu! Niamini. Jitolee kwa niaba Yangu, na hakika Nitajitolea kwako!

Iliyotangulia: Sura ya 54

Inayofuata: Sura ya 56

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp