Sura ya 75

Yote yatatimizwa punde tu maneno Yangu yanapozungumzwa, bila kupotoka hata kidogo. Kuanzia sasa kwendelea, mafumbo yote yaliyofichwa hayatazuiwa au kufunikwa hata kidogo, na yatafichuliwa kwenu—wanangu wapendwa. Nitakufanya uone hata ishara na maajabu kubwa zaidi ndani Yangu, na kuona hata mafumbo makubwa zaidi. Mambo haya hakika yatawashangaza na kuwapa ufahamu bora zaidi wa Mimi, mwenyezi Mungu, na kuwaruhusu kufahamu hekima Yangu humo. Leo ninyi mnaletwa uso kwa uso na Mungu mmoja wa kweli ambaye wanadamu hawajawahi kumwona tangu uumbaji, na hakuna kitu maalum kunihusu Mimi. Ninakula, kuishi, kuzungumza na kucheka na nyinyi, na daima Ninaishi ndani yenu, wakati huo huo pia Nikisonga miongoni mwenu. Kwa wale ambao hawaamini au ambao wana mawazo yao wenyewe ya kusikitisha, hiki ni kizuizi. Hii ni hekima Yangu. Nitawafichulia pia watu wengine juu ya vitu ambavyo ubinadamu Wangu wa kawaida haujui, lakini hili halimaanishi kwamba Mimi si Mungu Mwenyewe. Kinyume chake, hoja hii inatosha kuthibitisha kwamba Mimi ni mwenyezi Mungu. Kwa watu wanaoamini, hoja hii ina athari ya maamuzi, na kwa sababu ya hoja hii tu, wao wana uhakika wa asilimia mia moja Kwangu. Msiwe na hamu kupita kiasi; Nitawafichulia vitu kimoja baada ya kingine.

Kwa ajili yenu, Mimi ni wazi na Sijajificha. Hata hivyo, kwa ajili ya wasioamini—wale walio wadanganyifu, ambao wamepotoshwa na Shetani kwa kiwango fulani—Nitabaki Nimejificha. Hata hivyo, Nilipozungumzia awali kuhusu kujifichua kwa watu wote, Nilikuwa nikirejelea haki Yangu, hukumu Yangu, na utukufu Wangu, ili kuwa wangejua kutokana na matokeo wanayopokea kwamba Mimi ni msimamizi wa ulimwengu na vitu vyote. Tendeni kwa ujasiri! Kuweni watulivu tu! Usiogope: Mimi—Baba yenu—niko hapa kuwasaidia na hamtateseka. Alimradi muombe na kusali zaidi mbele Yangu mara kwa mara, Nitawapa imani yote. Kutoka kwa nje, wale walio na mamlaka wanaweza kuonekana kuwa waovu, lakini msiogope, kwa kuwa hii ni kwa sababu mna imani kidogo. Almuradi imani yenu ikue, hakuna kitu kitakachokuwa kigumu mno. Rukeni kwa furaha hadi mridhike sana! Kila kitu ki chini ya miguu yenu, na ndani ya mshiko Wangu. Je, si mafanikio au maangamizo hayaamuliwi na neno Langu moja tu?

Wale wote ambao Ninawatumia sasa Niliwakubali zamani, mmoja baada ya mwingine. Yaani, wale watu katika kikundi cha wazaliwa wa kwanza wameshaamuliwa, na wameamuliwa tangu Nilipoumba ulimwengu huu. Hakuna anayeweza kubadilisha hili, na vyote lazima viamrishwe na Mimi. Hakuna binadamu anayeweza kufanya hivyo; hii yote ni mipangilio Yangu. Nikiwepo, kila kitu kitakuwa thabiti na salama; Nikiwepo, vyote vitafanywa kwa usahihi na vizuri, bila kutumia jitihada hata kidogo. Ninasema na yanatendeka; Ninazungumza na yanafanywa. Hali ya kimataifa ikiwa katika msukosuko, kwa nini hamjakimbia kuanza mafunzo yenu? Mtangoja hadi lini? Je, mtasubiri mpaka ile siku ambayo wageni watafurika nchini China kukutana na nyinyi? Huenda mlikuwa goigoi kidogo hapo awali, lakini hamwezi kuendelea kujifurahisha! Wanangu! Kuweni wenye kufikiria nia Zangu za bidii! Wale ambao wananikaribia mara nyingi zaidi watapata kila kitu. Je, hamniamini?

Kasi ya kazi Yangu ni mwali wa umeme, lakini hakika si sauti ingurumayo ya radi. Je, mnaelewa maana halisi ya maneno haya? Lazima muwe na uwezo wa kuratibu vyema zaidi na Mimi na kuwa wenye kufikiria nia Zangu. Mnataka kupokea baraka, lakini pia mnaogopa mateso; hii si hisia yenu kinzani? Hebu Nikwambie! Kama mtu anatamani kupokea baraka leo lakini hajitolei kila kitu kuhusiana na hilo, basi yote atakayopokea ni adhabu na hukumu Yangu. Hata hivyo, wale wanaojitolea kila kitu watapata amani katika kila kitu na kuwa na kila kitu kwa wingi, na kila kitu wanachopokea kitakuwa baraka Zangu. Kinachohitajika kwa dharura leo ni imani yenu, na kwenu kulipa gharama. Msitafsiri visivyo nia Zangu. Kila kitu kitakuja kutimia, na mtakiona kwa macho yenu wenyewe na kukipitia ninyi wenyewe. Nikiwepo, hakuna neno hata moja lisilo kweli au la uongo; kila kitu Ninachosema ni ukweli kabisa, na hakikosi hekima. Msiamini nusu na kushuku nusu. Mimi ndimi Ninayekamilisha kila kitu miongoni mwenu, na Mimi pia ndimi Ninayehukumu na kuwashughulikia wale wanaofanya maovu. Ninawapenda, na ninawafanya muwe wakamilifu. Kwao, hata hivyo, Mimi ni kinyume kabisa: chuki na uharibifu, bila ya uhuru wa kuwa na fikira tofauti na bila kuacha alama. Wingi Wangu ni wa asili katika kila kitu Ninachosema na kufanya. Je, mmevichunguza kidogo kidogo? Maneno mengine Nimeyasema mara nyingi, basi kwa nini hamwelewi kile Ninachomaanisha? Baada ya ninyi kusoma Maneno Yangu, je, kila kitu kitakuwa kama vile kinavyopaswa kuwa? Je, kila kitu basi kinafanikishwa? Hamna nia yoyote ya kufikiria moyo Wangu. Kwa nini Nasema kuwa Mimi ni Mungu mmoja wa kweli mwenye mamlaka kamili, mwenye kudura ambaye anaangalia ndani sana ya mioyo ya watu? Je, bado hamwelewi maana ya maneno haya? Je, umekariri kila neno Niliyosisitiza Je, yamekuwa kwa kweli kanuni za jinsi unavyotenda?

Ninasimama juu ya kila kitu, Nikiutazama ulimwengu wote. Nitaonyesha nguvu Zangu kuu na hekima Yangu yote kwa kila taifa na watu. Msifanye tu kila mnachoweza kufuatilia raha hivi sasa. Wakati mataifa yote ya ulimwengu yanaungana, ni kitu gani ambacho hakitakuwa chenu? Hata hivyo, Sitawaacha mpungukiwe sasa, wala Sitawaacha mteseke. Amini kwamba Mimi ni mwenyezi Mungu! Kila kitu kitafanikishwa na kuwa bora zaidi na zaidi! Wazaliwa Wangu wa kwanza! Baraka zote zitawajia! Ninyi mtazifurahia bila kukoma, zisizopungua katika ugavi, zilizojaa na za wingi, na zilizojaa kikamilisho!

Iliyotangulia: Sura ya 74

Inayofuata: Sura ya 76

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp