Sura ya 17
Sauti yangu inasikika kama radi, ikiangaza pande zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, ubinadamu unapigwa chini. Hakuna mwanadamu ambaye amewahi kukaa imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa nuru Yangu na hawajui la kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao. Lakini, hakuna aliyewahi kutambua kwamba siku imewadia mwangaza Wangu unaposhuka duniani. Wanadamu wengi wanashtuliwa na ujio wa ghafla wa mwangaza; baadhi yao, kwa macho ya kuvutiwa ya dadisi, wanaangalia mwendo wa mwangaza na kutoka upande upi unasongea; ama wengine wanasimama tayari wakitazama mwangaza, ili waweze kuelewa wazi zaidi palipotoka mwangaza. Iwe ilivyo, kuna yeyote aliyewahi kugundua thamani ya mwangaza wa leo? Kuna yeyote aliyewahi kufahamu ajabu ya mwangaza huu? Wanadamu wengi wamechanganyikiwa tu; wamejeruhiwa machoni na kutupwa chini matopeni na mwangaza. Mtu anaweza kusema kwamba, chini ya mwangaza huu usiokuwa na ufasili, dunia imefunikwa na vurugu, ikifanya mtazamo wa kusikitisha usiovumilika ambao, ukichunguzwa kwa kina, unamtesa mtu na huzuni nyingi. Kutoka hapa, mtu anaelewa kwamba, wakati mwangaza una nguvu kabisa, hali ya dunia itakuwa na uwezo mdogo zaidi wa kumruhusu mwanadamu kusimama mbele Yangu. Ubinadamu upo katika mng’ao wa mwangaza; tena, ubinadamu uko katika wokovu wa mwangaza lakini wakati huo huo pia chini ya majeraha yaliyoletwa na mwangaza: Kuna yeyote asiye chini ya mapigo yanayoua ya mwangaza? Kuna yeyote anayeweza kutoroka kuchoma kwa mwangaza? Nimetembea kote duniani, kutawanya mbegu za Roho Wangu, ili binadamu wote duniani kwa sababu hii wataguswa nami. Kutoka kwa urefu wa juu wa mbingu, Naangalia chini kwa dunia yote, Nikitazama matukio ya ajabu na yasiyo ya kawaida ya viumbe wa dunia. Sehemu ya juu ya bahari inaonekana kuteswa na mshtuko wa tetemeko la ardhi: Ndege wa baharini huruka huku na kule, wakitafuta samaki wa kuwameza. Wakati huo huo, jambo hili halijulikani kabisa chini ya bahari, ambayo hali ya uso haiwezi kabisa kuamsha fahamu, kwa sababu chini ya bahari ni tulivu kama mbingu ya tatu: Hapa vitu vilivyo hai vikubwa na vidogo vinaishi pamoja kwa upatano, bila kushirki hata mara moja katika “migogoro ya kinywa na ulimi.” Miongoni mwa maelfu ya matukio ya ajabu na ya kichekesho, ubinadamu ndio unaona ugumu zaidi kuniridhisha Mimi. Nafasi ambayo Nimempa mwanadamu ni ya juu sana, na tamaa yake ni kubwa sana, na machoni pake, daima kuna kiwango cha kutotii. Katika kuadibu Kwangu kwa mwanadamu, ndani ya hukumu Yangu kwake, kumekuwa na mengi ambayo ni ya uchungu, mengi ambayo ni ya wema, lakini kati ya mambo haya mwanadamu hana habari hata kidogo. Sijawahi kumtendea mwanadamu yeyote kwa ukali: Nimekuwa tu, wakati wanadamu wamekuwa wakaidi, Nimefanya masahihisho yafaayo, na tu, wakati mwanadamu amekuwa dhaifu, Nimetoa msaada unaofaa. Lakini, wakati ubinadamu utajiweka mbali na Mimi na zaidi ya hayo kutumia mbinu za udanganyifu za Shetani ili kuasi dhidi Yangu, Mara moja Nitawaangamiza wanadamu, Nikiwaacha wanadamu bila nafasi ya kuonyesha ustadi wao mbele Yangu, ili wasije tena kuwa na uwezo wa kuzunguka-zunguka kwa fahari na hali, kuwaonea wengine, juu ya uso wa dunia.
Natumia mamlaka Yangu duniani, Nikidhihirisha kazi Yangu yote. Yote yaliyo katika kazi Yangu yanajitokeza duniani; mwanadamu hajawahi, duniani, kuweza kuufahamu mwendo Wangu mbinguni, wala kutafakari kabisa mizunguko na njia za Roho Wangu. Wanadamu wengi wanaelewa tu maelezo madogo yaliyo nje ya roho, bila kuweza kuelewa hali halisi ya roho. Matakwa Yangu kwa binadamu hayatoki kwa Mimi wa mbinguni Nisiye dhahiri, ama kwa Mimi wa dunia Nisiyekadiriwa: Natoa matakwa ya kufaa kulingana na kimo cha mwanadamu. Sijawahi kumweka yeyote kwa matatizo, wala Sijawahi “kukamua damu ya mtu yeyote” ili kujiridhisha—matakwa Yangu yanaweza kuwekewa mipaka tu kwa hali kama hizo? Kwa viumbe lukuki duniani, ni yupi asiyetii tabia za maneno yaliyo mdomoni Mwangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa, wanaokuja mbele Yangu, hajachomwa kabisa kupitia maneno Yangu na moto Wangu unaochoma? Ni yupi kati ya viumbe hawa anayethubutu kujigamba mbele Yangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa hainami mbele Yangu? Mimi ni Mungu anayelazimisha tu ukimya kwa viumbe? Kwa mambo lukuki katika uumbaji, Nachagua yale yanaoridhisha nia Yangu; kwa wanadamu lukuki, Nawachagua wale wanaotunza roho Yangu. Nachagua bora zaidi kwa nyota zote, hivyo Naongeza mwangaza hafifu kwa ufalme Wangu. Natembea duniani, Nikitawanya harufu Yangu nzuri kila mahali, nami Naacha umbo Langu kila mahali. Kila pahali panatingika kwa mvumo wa sauti Yangu. Watu kila mahali wanadumu kwa hamu ya mambo waliyozea ya urembo wa mandhari ya jana, kwani binadamu wote wanakumbuka siku za nyuma …
Ubinadamu wote hutamani kuuona uso Wangu, lakini Ninaposhuka kibinafsi duniani, wote wanachukia kuja Kwangu, wote wanafukuza nuru isije, kana kwamba Mimi ni adui wa mwanadamu mbinguni. Mwanadamu ananisalimia kwa mwanga wa kujihami machoni pake, na kubaki macho kila mara, akiogopa sana kwamba Ninaweza kuwa na mipango mingine kwake. Kwa sababu binadamu wananiona kama rafiki asiyejulikana, wanahisi kwamba Nina nia ya kuwaua bila kujali. Katika macho ya mwanadamu, Mimi ni adui wa mauti. Baada ya kuonja joto Langu katikati ya msiba, mwanadamu hata hivyo bado hafahamu pendo Langu, na bado ameamua kunifukuza na kunikaidi. Mbali na kujinufaisha na yeye kuwa katika hali hii ili kuchukua hatua dhidi yake, Namfunika mwanadamu na joto la kumbatio, Najaza mdomo wake na utamu, na kuweka chakula anachohitaji tumboni mwake. Lakini, hasira Yangu ya ghadhabu itakapotikisa milima na mito, Sitampa tena, kwa sababu ya woga wa mwanadamu, aina hizi tofauti za usaidizi. Wakati huu, Nitakuwa na ghadhabu, Nikiwanyima viumbe hai fursa ya kutubu na, kuachana na matumaini Yangu yote kwa mwanadamu, Nitatoa adhabu anayostahili sana. Wakati huu, radi na umeme vinang’aa ghafla na kunguruma, kama mawimbi ya bahari yakisonga kwa hasira, kama milima makumi ya maelfu ikigonga chini. Kwa ajili ya uasi wake, mwanadamu anaangushwa na radi na umeme, viumbe wengine wanafutwa katika milipuko ya radi na umeme, ulimwengu mzima unazorota ghafla katika machafuko, na uumbaji huwezi kupata pumzi muhimu ya uhai. Majeshi lukuki ya binadamu hayawezi kutoroka kishindo cha radi, katikati ya nuru ya ghafla ya umeme, wanadamu, makundi mengi sana, wanaanguka ndani ya mto unaobubujika haraka, kutokomezwa na mafuriko yanayotiririka chini kutoka milimani. Kwa ghafula, kunakutana ulimwengu wa “watu” badala ya “hatima” ya mwanadamu. Maiti huelea juu ya uso wa bahari. Wanadamu wote huenda mbali na Mimi kwa sababu ya ghadhabu Yangu, kwani mwanadamu amefanya dhambi dhidi ya kiini cha Roho Wangu, uasi wake umeniudhi. Lakini, katika sehemu zisizo na maji, wanadamu wengine bado wanafurahia, katikati ya kicheko na wimbo, ahadi ambazo Nimewapa.
Binadamu wote wanapotulia, Natoa kimulimuli cha mwangaza mbele ya macho yao. Hapo, wanadamu wanakuwa na uwazi wa akili na uangavu wa jicho, na wanakoma kuwa na nia ya kukimya; hivyo, hisia ya kiroho inakusanywa ndani ya mioyo yao mara moja. Wakati huu, binadamu wote wanafufuka. Wakiweka kando malalamiko yao, wanadamu wote wanakuja mbele Yangu, baada ya kushinda nafasi nyingine ya kusalimika kupitia maneno Ninayotangaza. Hii ni kwa sababu wanadamu wote wanataka kuishi duniani. Lakini nani miongoni mwao amewahi kuwa na nia ya kuishi kwa ajili Yangu? Nani miongoni mwao amewahi kufichua mambo mazuri ndani yake kunipa furaha? Nani miongoni mwao amewahi kugundua harufu ya kuvutia Kwangu? Wanadamu wote ni vitu hafifu na visivyotakaswa: Nje, wanaonekana kuangaza macho, lakini kwa nafsi zao muhimu hawanipendi kwa dhati, kwa sababu ndani ya nafasi ya kina cha moyo wa binadamu hakujawahi kuwa hata na kiasi kidogo cha Mimi. Mwanadamu anakosa sana: Kumlinganisha nami Mwenyewe, ingeonekana kwamba tuko mbali sana kama dunia kutoka kwa mbingu. Lakini, hata hivyo, Simshambulii mwanadamu katika sehemu zake dhaifu na zenye kasoro, wala Simcheki kudharau upungufu wake. Mikono Yangu imekuwa kazini duniani kwa maelfu ya miaka, na muda huo wote, macho Yangu yamelinda binadamu wote. Bado, Sijawahi kuchukulia mzaha maisha ya binadamu hata mmoja kana kwamba ni kitu cha kuchezea. Nachunguza machungu mwanadamu amechukua na kuelewa bei ambayo amelipa. Anaposimama mbele Yangu, Sitamani kumpata mwanadamu kwa kumshtua kwa nia ya kumwadibu, wala kumtakia na kutawaza kwake vitu visivyohitajika. Badala yake, wakati huu wote, Nimemruzuku mwanadamu tu na kumpa. Hivyo basi, yote anayofurahia mwanadamu ni neema Yangu, yote ni fadhila inayotoka kwa mkono Wangu. Kwa sababu Niko duniani, mwanadamu hajawahi lazimika kuteseka mateso ya njaa. Badala yake, Namruhusu mwanadamu kupokea kutoka mikono Yangu mambo ambayo anaweza kufurahia, na kumruhusu mwanadamu kuishi ndani ya baraka Zangu. Je, wanadamu wote hawaishi chini ya kuadibu Kwangu? Kama tu jinsi kuna mengi ndani ya vina vya milima, na vitu vingi vya kufurahia ndani ya maji, je, watu wanaoishi ndani ya maneno Yangu leo wanavyo, hata zaidi, chakula wanachopenda na kuonja? Niko duniani, na mwanadamu anafurahia baraka Zangu duniani. Niachapo dunia nyuma, ambapo ndipo pia kazi Yangu itafika ukamilishaji wake, wakati huo, wanadamu hawatapata tena hisani yoyote kutoka Kwangu kwa sababu ya udhaifu wao.
Machi 16, 1992